Taarifa kwa vyombo vya Habari ya zamani
MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIHUTUBIA BUNGE LA KENYA
TAAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi, 2021 amepokea taarifa za mwaka za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Hafla ya kupokea taarifa hizo imefanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu Wakuu na viongozi wakuu wa taasisi na idara za Serikali.
Mhe. Rais Samia ameipongeza ofisi ya CAG na TAKUKURU kwa kazi za ukaguzi na uchunguzi zilizofanywa katika mwaka 2019/20.
Ameiagiza ofisi ya CAG kuongeza wataalamu wa ukaguzi ili waweze kukagua mashirika mengi zaidi na miradi mingi zaidi hususani iliyopo mikoani ambayo maendeleo yake hayaridhishi.
Kutokana na taarifa ya CAG kuonesha kuwa kuna kusuasua kwa utekelezaji wa mapendekezo juu ya usimamizi wa hesabu za Serikali na hali isiyoridhisha ya mashirika na taasisi za Serikali, Mhe. Rais Samia ameahidi kuongeza msukumo katika utekelezaji wa mapendekezo hayo na kuchukua hatua za haraka dhidi ya mashirika na taasisi ambazo zimetajwa kufanya vibaya kutokana na wizi na upotevu wa fedha za umma.
Ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko kufuatia taarifa za kuwepo upotevu wa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 3.6 na ameiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi katika mamlaka hiyo.
Mhe. Rais Samia amemuagiza CAG Charles Kichere kufanya ukaguzi wa fedha zote zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kati ya mwezi Januari na Machi, 2021. Ameitaka Ofisi ya CAG na TAKUKURU kushirikiana kuweka sawa mifumo ya fedha inayotumiwa na hazina ili kuondokana na changamoto na athari za kuwepo mifumo mingi tena isiyowasiliana na ambayo inasababisha upotevu mkubwa wa fedha. Kuhusu mashirika yasiyofanya vizuri amemtaka CAG kutomung’unya maneno akisema “mashirika yasiyofanya vizuri, naomba sana CAG ulimi wako usiwe na utata, kama kuna shirika halifanyi vizuri tuambie hili halifanyi vizuri, kama bodi haisimami vizuri tuambie bodi hii haisimami vizuri, kwa sababu tutakaposema mapungufu ndipo tutakapoweza kurekebisha na kufanya vizuri zaidi, tukinyamaziana na kuficha sura hatutarekebisha na tutawaumiza wananchi, naomba sana ripoti yako iwe wazi zaidi, utakaponiletea ukaguzi wa mashirika naomba uwe wazi zaidi ili tujue tunachukua hatua gani”.
Kwa upande wa TAKUKURU, Mhe. Rais Samia ameitaka taasisi hiyo kuongeza juhudi zaidi kwa kuharakisha kufikisha Mahakamani kesi za rushwa na ufisadi, kuachana na kesi ambazo hazina msingi wa kushinda na ameitaka taasisi hiyo kujielekeza zaidi katika masuala yanayohusiana na rushwa na yale yanayopaswa kufanywa na vyombo vingine viachiwe vyombo husika.
Amehimiza uadilifu kwa watumishi wa TAKUKURU ambao wamekuwa wakiwafichua mashahidi na watoa taarifa na pia ametaka taasisi hiyo ipanue uwigo wa kufuatilia vitendo vya rushwa ikiwemo uvujaji wa mitihani, kuboresha mifumo yake ya kukabiliana na rushwa na ufisadi na ishirikiane na taasisi nyingine katika kufanikisha vita dhidi ya rushwa.
Mhe. Rais Samia amewahakikishia Watanzania kuwa atasimama imara kulinda makusanyo na matumizi ya fedha za Serikali pamoja na vita dhidi ya rushwa.
Katika taarifa yake CAG Charles Kichere amesema katika mwaka 2019/20 ofisi yake imetoa jumla ya hati 900 za ukaguzi (zikiwemo 243 za Serikali Kuu, 185 Serikali za Mitaa, 165 za Mashirika ya Umma, 290 za miradi na 17 vyama vya siasa) ambapo 800 (89%) zinaridhisha, 81 zina mashaka (9%), 10 mbaya (1%) na hati 9 alishindwa kutoa maoni.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo amesema katika mwaka 2019/20 taasisi hiyo ilifanikiwa kutekeleza majukumu yake kwa asilimia 89.8 ikilinganishwa na mwaka uliopita ilipotekeleza majukumu yake kwa asilimia 88.1 ongezeko ambalo limetokana na kukamilisha uchunguzi kwa majalada 1,079 ikilinganishwa na majalada 911 ya mwaka uliopita.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam Bw. Aron Titus Kagurumjuli.
Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 16 Februari, 2021.
Uteuzi wa Mkurugenzi mwingine wa Manispaa hiyo utafanywa baadaye.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza Majaji, Mahakimu na watumishi wa Mahakama hapa nchini kwa kuboresha huduma za Mahakama ikiwemo kuongeza kasi ya kupunguza mrundikano wa kesi Mahakamani ambao umekuwa ukisababisha usumbufu na gharama kubwa kwa wananchi.
Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 01 Februari, 2021 katika sherehe maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Sheria, Siku ya Sheria nchini na maadhimisho ya miaka 100 ya Mahakama Kuu zilizofanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma chini ya kauli mbiu isemayo “Miaka 100 ya Mahakama Kuu: Mchango wa Mahakama katika kujenga nchi inayozingatia uhuru, haki, udugu, amani na ustawi wa wananchi”.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na hatua kubwa za kuboresha Mahakama zilizopigwa katika miaka 5 iliyopita ambapo shilingi Bilioni 135 zilizotolewa na Serikali zimewezesha kuboreshwa kwa miundombinu ya Mahakama ikiwemo kujenga Mahakama Kuu za Kanda 3, Mahakama za Hakimu Mkazi 5, Mahakama za Wilaya 15, Mahakama za Mwanzo 18, Mahakama inayotembea (Mobile Court) ambayo imesikiliza Mashauri 778 na kuimarisha mifumo ya TEHAMA.
Mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi, kuteua Majaji wa Mahakama ya Rufani 17, kuteua Majaji wa Mahakama Kuu 52 (ambao wanafanya jumla ya Majaji kufikia 88) na kuajiri Mahakimu 396 (ambao wanafanya idadi ya Mahakimu kufikia 1,287).
Mhe. Rais Magufuli amesema juhudi hizo zimewezesha kuongezeka kwa kasi ya usikilizaji wa mashauri ambapo katika mwaka 2020 Mahakama za Mwanzo zilisikiliza mashauri 164,758 na kubakiwa na mrundikano wa mashauri 29 tu, Mahakama za Wilaya zilisikiliza mashauri 43,149 na kubakiwa na mrundikano wa mashauri 12 tu, Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi ilisikiliza mashauri 9 kati ya 11 na Mahakama ya Rufani ilisikiliza mashauri 1,216 na kubakiza mashauri 155 tu.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa kueleza historia ya Mahakama tangu ilipoanzishwa hapa nchini miaka 100 iliyopita ambapo amesema wakati Tanganyika ikipata Uhuru mwaka 1961 Mhimili huo wa Dola ulikuwa umeshikiliwa na wakoloni kutokana na kutokuwepo kwa Majaji, Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama wa Kitanzania, na kwamba sura ya Mahakama inayoonekana leo imetokana na juhudi kubwa zilizofanyika baada ya Uhuru chini ya Marais wa Tanzania, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin William Mkapa, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa sasa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa vijana kujifunza historia ili kuelewa vizuri Taifa lilikotoka na juhudi kubwa zilizofanyika badala ya kuwasikiliza wanaosema Tanzania haijapiga hatua zozote tangu Uhuru, na kwamba hiyo ndio sababu ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kulifanya somo la historia kuwa la lazima kwa wanafunzi.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameeleza kutoridhishwa kwake na kucheleweshwa kwa kesi za kodi zinazowahusu wafanyabiashara ambapo takwimu zinaonesha benki 4 kati takribani benki 50 zilizopo hapa nchini zimerekodi kesi 378 za kodi na mikopo zenye thamani ya shilingi Bilioni 738.99, hivyo ametoa wito kwa Mahakama kuharakisha maamuzi ya kesi hizo kwa kuwa zinaathiri uchumi na maendeleo.
Ametoa wito kwa Jaji Mkuu kuendelea kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya rushwa ambavyo bado vinafanywa na baadhi ya watumishi wa Mahakama kama ambavyo amechukua hatua dhidi ya watumishi 19 mwaka jana (2020), na amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ambao ni wenyeviti wa Kamati za Mahakama za Mikoa na Wilaya kuitisha vikao vya kamati hizo mara moja.
Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Majaji na Mahakimu wa Mahakama kutumia lugha ya Kiswahili katika uendeshaji wa mashauri yao ili kuiendeleza lugha hiyo na kuwarahisishia wananchi kuelewa, na kutokana na hilo amempongeza na kumpandisha cheo Mhe. Zepharine Nyalugenda Galeba kutoka Jaji wa Mahakama Kuu na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani baada ya kutumia lugha ya Kiswahili kutoa hukumu kwenye kesi ya Mgodi wa North Mara dhidi ya Gerald Nzumbi.
Kwa upande wake, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa Serikali kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli za Mahakama ikiwemo kuboresha miundombinu, na kwamba juhudi hizo zinaendelea ambapo hivi sasa ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu katika Mikoa 6 (Mwanza, Arusha, Dodoma, Morogoro, Temeke na Kinondoni) unaendelea na pia ujenzi wa majengo 25 ya Mahakama za Wilaya unaendelea.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Februari, 2021 amemuapisha Mhe. Zephrine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Hafla ya kuapishwa kwa Mhe. Jaji Galeba imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu na viongozi wa taasisi ambazo ni wadau wa karibu wa Mahakama.
Mhe. Galeba (aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu) ameapishwa baada ya kupandishwa cheo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni kutambua mchango wake wa kuthamini lugha ya Kiswahili ambapo alitumia lugha hiyo kutoa hukumu ya kesi ya mapitio namba 23/2020 kati mgodi wa dhahabu wa North Mara na mwananchi Gerald Nzumbi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Galeba kwa kupandishwa cheo na amemtaka kwenda kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na taratibu za Mahakama, na kwa kumtanguliza Mungu.
Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria kufanya mabadiliko ya sheria na mifumo ya Mahakama iliyorithiwa kutoka kwa wakoloni na ambayo imesababisha hukumu za Mahakama kutolewa kwa lugha ya Kiingereza ambayo haifahamiki kwa Watanzania wengi, ili hukumu hizo zitolewe kwa lugha ya Kiswahili.
Amesema hoja za kuwa Kiswahili hakina misamiati ya kutosha hazina mashiko kwa kuwa mwaka 1999 timu ya Wanasheria iliandika kamusi ya sheria na pia lugha hiyo inatumiwa na watu wengi, Mataifa na taasisi mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari vya kimataifa.
Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutofurahishwa na ucheleweshaji wa mambo unaofanywa na Wizara ya Katiba na Sheria na amemuagiza Waziri Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kufuatilia na kuhakikisha mchakato wa kuwaajiri watumishi 200 wa Mahakama ambao kibali cha kuajiriwa kwao kilishatoka wanaajiriwa.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchini na viongozi wa Wilaya ya Manyoni kutatua mara moja mgogoro wa ardhi wa eneo la Majengo lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ambao umesababishwa na Idara ya Ardhi ya halmashauri hiyo.
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 31 Januari, 2021 aliposimama kuwasalimu wananchi wa Manyoni wakati akiwa safarini kutoka Tabora kwenda Dodoma.
Baada ya kuwasalimu na kuwashukuru kwa kumpigia kura nyingi zilizomwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili, Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero ya ardhi inayowakabili wananchi hao ambapo wamelalamikia kitendo cha Idara ya Ardhi kuchukua maeneo yao bila kuwalipa fidia na wengine kuamriwa kuondoka katika eneo hilo baada ya kupewa nyaraka za kupatiwa radhi (Offer) hali iliyozua mgogoro kati ya wamiliki wa asili wa eneo hilo na Idara ya Ardhi.
Mhe. Rais Magufuli ameagiza wananchi wenye Offer waruhusiwe kuendeleza maeneo waliyopatiwa, na wamiliki wa asili wa eneo hilo kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria.
Ameagiza eneo lililokuwa mali ya Mama mmoja aitwaye Elizabeth Msalali (90) ambalo lilichukuliwa na Afisa Ardhi mmoja aitwaye Msafiri na kisha kupangishwa kwa kampuni ya simu za mkononi ambayo imeweka mnara wa mawasiliano, lirejeshwe mara moja kwa Mama huyo ambaye ndiye ataingia mkataba wa upangaji na kampuni hiyo.
Mhe. Rais Magufuli ameeleza kutofurahishwa na uelewa mdogo wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mhe. Jumanne Mlagaza kuhusu masuala mbalimbali ya halmashauri ikiwemo masuala ya kibajeti, miradi na kero za wananchi, na amewataka Madiwani kote nchini kuwa makini na kufuatilia kwa ukaribu masuala yahusuyo halmashauri zao badala ya kuwaachia watendaji wafanye wanavyotaka.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Seif Sharif Hamad leo tarehe 14 Januari, 2021 wamemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nyumbani kwake Chato Mkoani Geita na kufanya nae mazungumzo.
Wakizungumza na vyombo vya habari baada ya mazungumzo hayo, Mhe. Rais Mwinyi na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwakaribisha nyumbani kwake Chato na wameelezea kufurahishwa kwao na mazungumzo mazuri yaliyofanyika, yenye maslahi makubwa kwa Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla.
Mhe. Rais Mwinyi ambaye ameongozana na Mkewe Mama Mariam Mwinyi amesema mazungumzo baina yao yalilenga kujenga nchi, kuwaunganisha zaidi Wazanzibar na amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa dhamira yake ya kuendelea kuisaidia Zanzibar ikiwemo ombi aliloliwasilisha hivi karibu kwa Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje ya China Mhe. Wang Yi la kuomba fedha kiasi cha Dola za Marekani Milioni 75 kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 148 za barabara za Zanzibar.
“Kwa hivyo kwanza nianze kukushukuru wewe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utayari wako, wa kufanya kazi na sisi viongozi wa Zanzibar. Leo tupo hapa mimi na Maalim Seif Sharif Hamad tukiwa wamoja, tukiwa tunaongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa kule Zanzibar, na nataka niseme haya yasingewezekana kama tusingeungwa mkono nawe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu mara zote umekuwa mstari wa mbele kutaka Zanzibar iwe na umoja. Ukiwa kama Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, mara zote umekuwa ukiniunga mkono katika juhudi zetu za kuleta umoja kule Zanzibar. Leo tupo hapa tukiwa wamoja, tukiwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na nataka nikuhakikishie kwamba sio sisi tu kama viongozi ndio tumeungana bali Wazanzibar wote wana muelekeo wa kuungana. Zile tofauti zetu za kisiasa tumeziweka pembeni, sasa hivi sote tunashirikiana katika kuijenga nchi yetu” amesema Mhe. Rais Mwinyi.
Kwa upande wake, Mhe. Seif Sharif Hamad amesema wamekuwa na mazungumzo mazuri ya namna ya kuwaunganisha Watanzania wote na kwamba amepata matumaini makubwa kuona Mhe. Rais Magufuli yupo pamoja na nao na ana dhamira ya kuwaunganisha Waunguja na Wapemba.
“Tulikuwa na mazungumzo mazuri, mazungumzo ya kidugu, na mazungumzo ambayo mimi yamenipa matumaini kwamba kiongozi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo pamoja na sisi, hasa katika suala zima la kuimarisha umoja, upendo na maelewano katika visiwa vya Unguja na Pemba, nimefarijika sana kumsikia yeye mwenyewe Mheshimiwa Rais akituhakikishia kwamba yupo pamoja na sisi na anatuunga mkono kwa hali na mali, kwa hiyo Mhe. Rais nakushukuru sana. Lakini vile vile nimshukuru Rais wangu Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, nae vilevile tumekuwepo pamoja na kwa pamoja tumeweza kuchangia mawazo na nadhani kumsikia Mhe. Rais Magufuli kumetupa uzaidi sisi wa kuzidi kuwaunganisha Wazanzibari” amesema Mhe. Seif Sharif Hamad.
Aidha, Mhe. Seif Sharif Hamad ambaye wakati akitoka Mwanza kwenda Chato ameshuhudia ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi Mkoani Mwanza, amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo amesema litakuwa ukombozi na manufaa makubwa ya kijamii na kiuchumi sio tu kwa Watanzania bali pia nchi jirani.
Katika salamu zake, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru viongozi hao wa Zanzibar kwa kumtembelea nyumbani kwake Chato na pia amewapongeza wao na Wazanzibari wote kwa kuadhimisha miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Seif Sharif Hamad kwa kukubali kwake kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kwamba kitendo hicho kimeonesha ukomavu wake katika uongozi na jinsi alivyoweka mbele maslahi ya Wazanzibari badala ya maslahi yake binafsi.
Mhe. Rais Magufuli amesema ana matumaini makubwa kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar itafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii na amempongeza Mhe. Rais Mwinyi kwa kuanza vizuri uongozi wake ikiwemo kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuwashughulikia mafisadi.
Amewahakikishia viongozi hao kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuiunga mkono Zanzibar na amesisitiza kuwa Watanzania wana kila sababu ya kuwa wamoja badala ya kuruhusu watu wenye maslahi yao binafsi kuwavuruga.
“Sitawaacha kamwe, na hasa kwa sababu wote kwa umoja wao wanahubiri amani, Rais wa Zanzibar Mhe. Mwinyi anahubiri amani, Maalim Seif anahubiri amani, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar anahubiri amani, Wazanzibari wote tuhubiri amani” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Viongozi wengine waliokuwepo ni Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wa Mkoa wa Geita.

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi leo tarehe 11 Januari, 2021 amefanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini ambapo amekutana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato, Mhe. Rais Nyusi amepokewa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli na kisha viongozi hao wakaelekea katika eneo la Kitela ambako wameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Rufaa ya Kanda – Chato.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewaeleza Waheshimiwa Marais kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali hiyo imefikia asilimia 90 kwa gharama ya shilingi Bilioni 16 na kwamba hospitali nyingine kama hiyo inajengwa katika Kanda ya Kusini huko Mkoani Mtwara.
Dkt.Gwajima ameeleza kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuimarisha huduma za matibabu yakiwemo matibabu ya kibingwa na kwamba pamoja na kujengwa kwa hospitali za kanda, Serikali imejenga Hospitali mpya 5 za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Wilaya 99, Vituo vya Afya 487 na Zahanati 1,198 nchi nzima.
Hospitali hiyo inatarajiwa kuhudumia wananchi takribani milioni 14 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria na Mikoa ya Kanda ya Magharibi.
Akizungumza na wananchi waliohudhuri sherehe za uwekaji jiwe la msingi la hospitali hiyo, Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Nyusi kwa kukubali kuweka jiwe hilo la msingi na ameiagiza Wizara ya Afya kuhakikisha awamu zilizobaki za ujenzi wa hospitali hiyo zinaunganishwa na kufanya kwa pamoja ili ikamilike haraka na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa kujengwa kwa hospitali hiyo ni muendelezo wa kazi nzuri ya ujenzi wa Wilaya ya Chato iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye alitembelea Chato tarehe 09 Januari, 1967 ambapo alifungua kiwanda cha kuchambua pamba cha Chato (Chato Ginnery) chenye uwezo wa kuchambua marobota 20,000 ya pamba kwa mwaka na akaanzisha mchango wa ujenzi wa Bandari ya Nyamirembe iliyopo Chato kwa ajili ya kusafirisha pamba kwenda Mwanza na kwingineko. Yeye mwenyewe Hayati Mwl. Nyerere alichangia paundi 1,000 sawa na shilingi 20,000 (kwa wakati huo).
Ameongeza kuwa kitendo cha Hayati Mwl. Nyerere kuanzisha mchango wa kujenga Bandari ya Nyamirembe, kiliitikiwa na wananchi na hatimaye kukamilisha bandari hiyo kwa gharama ya paundi 10,000 na kwamba ujenzi huo ulifanikiwa kutokana na kuhimiza dhana ya kujitegemea. Siku chache baadaye yaani tarehe 05 Februari, 1967 Hayati Mwl. Nyerere alikwenda Arusha ambako alitangaza Azimio la Arusha ambalo pia lilikuwa linahimiza kujitegemea.
Ameongeza kuwa juhudi hizo ziliendelezwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi aliyeitembelea Chato wakati wa kipindi chake, Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamini William Mkapa aliyeitangaza Chato kuwa Wilaya mpya ikitokea Wilaya ya Biharamulo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeizindua Wilaya ya Chato.
Kwa upande wake, Mhe. Rais Nyusi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumpa heshima ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Rufaa ya Kanda – Chato na amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa za kuwajali watu kwa kujenga sehemu za huduma za matibabu na kujenga miundombinu mingine mbalimbali ambayo inawahudumia wananchi na kukuza uchumi.
Mhe. Rais Nyusi ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mhe. Rais Magufuli kwa kuchapa kazi, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewajalia nchi yenye rasilimali na utajiri mkubwa.
Baada ya kuweka jiwe la msingi la hospitali hiyo, Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Nyusi wamefanya mazungumzo na baadaye kuzungumza na Vyombo vya Habari ambapo wamesema ziara hii imefanyika kwa lengo la kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania na Msumbiji ni ndugu, marafiki na majirani wa kweli.
Mhe. Rais Nyusi amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 1 na amerejea nchini Msumbiji.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi 3 kama ifuatavyo;
Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Dkt. Shein anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas A. Samatta ambaye anamaliza muda wake.
Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Dkt. Mwakyembe anachukua nafasi ya Bi. Mariam Joy Mwaffisi ambaye amemaliza muda wake.
Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudentia Mugosi Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Bi. Gaudensia Mugosi Kabaka anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 24 Novemba, 2020.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2020 amewaongoza Watanzania katika mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa aliyezikwa kijijini kwake Lupaso, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Mazishi ya Mhe. Benjamin William Mkapa yamefanyika kwa taratibu za kidini na heshima zote za kijeshi ambapo Ibada ya Mazishi imeongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga (Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limefanya gwaride la mazishi likiambatana na kupiga mizinga 21 kwa heshima ya Rais Mstaafu na Amiri Jeshi Mkuu wa Awamu ya Tatu.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria mazishi hayo wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi wengine ni Maspika, Majaji Wakuu, Makamu wa Rais Wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Maspika Wastaafu, Majaji Wakuu Wastaafu, Mawaziri na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi.
Pamoja na kuongoza Ibada ya mazishi, Askofu Mkuu Nyaisonga amesoma salamu za rambirambi za Baba Mtakatifu (Papa Francis) aliyewapa pole Watanzania wote na kuwataka kuwa wavumilivu na wenye matumaini na salamu za Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi na Rais Mstaafu wa Nchi hiyo Mhe. Joaquim Chissano zimesomwa na Balozi wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Mónica Patrício Clemente.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amesema wananchi wa Zanzibar wanaungana na Watanzania wenzao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na kiongozi shupavu na hodari aliyetoa mchango mkubwa kwa Taifa na katika kuuhifadhi na kuutunza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kwamba Wazanzibar daima watamkumbuka na kuuenzi mchango huo.
Marais Wastaafu Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wamemuelezea Hayati Benjamin William Mkapa kuwa alikuwa kiongozi hodari, mbunifu, aliyechukia umasikini na aliyeelekeza nguvu zake kujenga uchumi wa Tanzania.
Wamempa pole Mhe. Rais Magufuli na familia ya Hayati Benjamin William Mkapa ikiongozwa na Mjane wake Mama Anna Mkapa kwa kuguswa zaidi na msiba huu mkubwa na wamewataka Watanzania wote waendelee kumuombea.
Katika salamu zake, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Watanzania kwa uvumilivu wao katika kipindi chote cha maombolezo, ameishukuru kamati ya maombolezo iliyoongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na amewashukuru viongozi wote wa Dini ambao walimlea tangu alipobatizwa na hata alipofariki dunia wamemuombea na kufanyia Ibada ya maziko.
Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kujifunza kutoka kwa Hayati Benjamin William Mkapa aliyewapenda Watanzania kwa dhati na aliyewapenda wanakijiji wenzake wa Lupaso kwani wakati wa uhai wake alipoulizwa azikwe wapi atakapofariki dunia alisema anataka azikwe kijiji cha Lupaso na sio Dodoma ambako kulikuwa na mapendekezo ya viongozi wakuu wa kitaifa kuzikwa makao makuu ya nchi.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa masikitiko makubwa ametangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 24 Julai, 2020.
Mhe. Rais Magufuli amesema Mhe. Benjamin William Mkapa amefariki dunia hospitalini Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuwa watulivu na wastahimilivu baada ya kupokea taarifa za kuondokewa na mpendwa wao Mhe. Benjamin William Mkapa.
“Kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa, Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu amefariki dunia, amefariki dunia katika hospitali Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa, niwaombe Watanzania tulipokee hili, tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele za haki, taarifa zingine zitaendelea kutolewa lakini Mzee Mkapa hatuanaye tena” amesema Mhe. Rais Magufuli katika taarifa yake kwa Taifa.
Taarifa zingine kuhusiana na msiba huu mkubwa zitatolewa baadaye.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Juni, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) kwa sehemu
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Juni, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) kwa sehemu ya kwanza ya Dar es Salaam – Morogoro na kuelezea kuridhishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa.
Mhe. Rais Magufuli amesafiri kwa gari kandokando ya reli hiyo kuanzia Kisarawe hado Soga Mkoani Pwani na kisha akapanda kiberenge kilichopita katika reli hiyo mpya kuanzia Soga hadi Kikongo kabla ya kuendelea na safari yake kwa gari kuelekea Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kazi ya ujenzi wa sehemu ya kwanza ya reli hiyo imefikia asilimia 82 ambapo Watanzania 13,000 wamenufaika na ajira na inatarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu (2020).
Akizungumza na wananchi wa Soga na Kikongo, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza kwa kupata mradi huo na ametaka waendelee kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa ili waweze kunufaika zaidi na mradi huo.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero za wananchi hao ambapo ameendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa Shule ya Msingi Soga na kufanikiwa kukusanya shilingi 68,535,000/- zikiwemo shilingi Milioni 5 alizochangia yeye mwenyewe, na amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kufika Kijijini hapo ili kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mmiliki wa shamba kubwa lililopo kijijini hapo ambalo halilimwi.
Mhe. Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa kuhakikisha anatatua tatizo la maji linalokikabili kijiji cha Soga.
Ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imechukua hatua madhubuti za kutekeleza mradi huo ambao utagharimu shilingi Trilioni 7.02 kwa sehemu ya kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora Mkoani Dodoma, pamoja na kutekeleza mradi mkubwa wa uzalishaji wa megawati 2,115 za umeme katika Bwawa la Nyerere ili kukuza uchumi wa Watanzania na kuinua kipato cha wananchi na hivyo amewataka Watanzania wote kuunga mkono juhudi hizo.
Akiwa Mlandizi, Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero za wananchi na kumuagiza Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso kuhakikisha Wizara ya Maji inatatua tatizo la maji la Mitaa ya Mbwawa Shule na Mbwawa Mkoleni na pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe kuanza mchakato wa ujenzi wa barabara ya lami ya Mafia – Mzenga – Vikumbulu ili kuunganisha Mlandizi na reli.
Mhe. Rais Magufuli amewasili Mjini Morogoro na kesho ataendelea na ziara yake Mkoani hapa ambapo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa mahandaki ya reli ya kisasa (standard gauge) sehemu ya Morogoro – Makutupora, kuzindua barabara ya lami ya Rudewa – Kilosa na atafanya mkutano wa hadhara katika eneo Mkadage Wilayani Kilosa.
Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu (2020) huku wakikumbuka kudumisha amani, umoja na mshikamano pamoja na kuwachagua viongozi watakaowafaa.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Chamwino.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya India, Mhe. Narendra Modi leo tarehe 12 Juni, 2020 amempigia simu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo viongozi hao wamezungumzia masuala yahusuyo uhusiano na ushirikiano mzuri, wa kirafiki na kihistoria uliopo kati ya Tanzania na India.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Modi amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake wa Awamu ya Tano na amemtakia heri yeye na Watanzania wote katika juhudi kubwa za kuijenga nchi zinazoendelea na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Pamoja na kumhakikishia kuwa India itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano wake na Tanzania katika nyanja mbalimbali hasa kiuchumi, Mhe. Modi amempa mrejesho wa yaliyojiri katika mkutano wa nchi 20 tajiri duniani (G20) uliofanyika hivi karibuni (India ikiwa ni mojawapo) ambapo nchi hizo zimekubaliana kuwa taasisi za fedha za kimataifa zitoe msamaha wa madeni kwa nchi masikini na zinazoendelea, zilizopata madhara kutokana ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).
Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Modi kwa kumpigia simu, kumtakia heri na kumpa mrejesho wa yaliyojiri katika mkutano wa G20, na ameomba taasisi za fedha za kimataifa zitakapotoa msamaha wa madeni ziitupie macho Tanzania ambayo pia imepatwa na madhara ya ugonjwa wa Corona ili iweze kuimarisha uchumi wake.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza India kwa juhudi za kutafuta chanjo ya virusi ya Corona ambazo anaamini zitafanikiwa na kwamba Tanzania ikiwa moja ya nchi zilizokubwa na ugonjwa huo itanufaika, japo ugonjwa wenyewe unapungua kwa kasi kubwa hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Modi kwa uhusiano na ushirikiano mzuri wa Tanzania na India ambayo ni miongoni mwa nchi 5 zinazoongoza kwa uwekezaji hapa nchini na pia ameshukuru kwa mikopo nafuu inayotolewa na India kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa hapa nchini.
Ameitaja baadhi yake kuwa ni mkopo wa ujenzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Nelson Mandela, mikopo ya miradi ya maji na ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa Tanzania wanaokwenda kusomea masuala ya afya, uhandisi na TEHAMA nchini India.
Mikopo ya miradi ya maji ni pamoja na shilingi Bilioni 225.9 (Ruvu- Dar es Salaam, ambao umekamilika), shilingi Bilioni 611.5 (Maji ya Ziwa Victoria kwenda Tabora, Nzega na Igunga ambao unakaribia kukamilika), shilingi Trilioni 1.2 (miradi ya maji ya Miji 28, ambayo utekelezaji wake unaendelea) na shilingi Bilioni 209.9 (miundombinu ya maji ya Zanzibar, ambayo inaendelea kujengwa).
Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia Mhe. Modi kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na India, na amewaalika wafanyabiashara na wawekezaji wa India kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, kilimo, ufugaji, madini na nyingine kwani Tanzania imejenga mazingira mazuri ya uwekezaji.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Juni, 2020 amefungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kuwahakikishia Walimu wote nchini kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inathamini kazi kubwa wanayoifanya na itaendelea kuboresha maslahi yao na mazingira yao ya kazi.
Ufunguzi wa mkutano huo umefanyika katika uwanja wa CCM Jamhuri Jijini Dodoma na umehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa pamoja na viongozi na wanachama wa CWT 1,138 waliowakilisha mikoa 26 na wilaya 151 hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Rais wa CWT Mwl. Leah Ulaya na viongozi wenzake kwa kumkaribisha kufungua mkutano huo na amebainisha kuwa yeye pamoja na viongozi wengine wakiwemo Waziri Mkuu na Spika, hawakusita kukubali mwaliko huo kutokana na uongozi wa sasa wa CWT kujenga uhusiano mzuri na Serikali hali iliyowezesha kujenga daraja zuri la kushauriana na kushughulikia masuala mbalimbali yanayowahusu Walimu.
Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kuwepo uhusiano huo mzuri, Serikali imechukua hatua madhubuti za kuimarisha na kuboresha elimu zikiwemo kutoa elimu bila malipo ambapo kati ya Desemba 2015 na Februari 2020 imetoa shilingi Trilioni 1.01 kugharamia mpango huo, kuongeza shule za msingi kutoka 16,899 hadi kufikia 17,804, kuongeza shule za sekondari kutoka 4,708 hadi 5,330, kukarabati shule kongwe 73 kati ya 89 zilizopo, kujenga mabweni 253 na vyumba vya maabara 227, kutoa vifaa kwa maabara 2,956 pamoja na kuongeza madawati kutoka 3,024,311 hadi 8,095,207.
Juhudi zingine ni kukarabati vyuo vya walimu 18 na kujenga vyuo vipya 2, kupeleka kompyuta 1,550 katika vyuo 35 kwa lengo la kuimarisha ufundishaji wa masomo ya TEHAMA, kuongeza Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) kutoka 672 hadi 712, kukarabati na kuongeza vifaa katika vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) na kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka shilingi Bilioni 341 hadi kufikia shilingi Bilioni 450.
Mhe. Rais Magufuli amesema juhudi hizo zimezaa matunda yenye manufaa makubwa kwa Watanzania kwani idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kuanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka Milioni 1 hadi Milioni 1.6 hivi sasa, idadi ya wanafunzi wa kidato cha 1 hadi cha 4 imeongezeka kutoka 1,648,359 hadi kufikia 2,185,037 na ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Kuhusu maslahi ya Walimu, Mhe. Rais Magufuli amesema katika mwaka 2014/15 Watumishi wa Umma 306,917 walipandishwa vyeo ambapo kati yake 160,367 ni Walimu na kwamba katika mwaka huu Serikali itawapandisha vyeo Watumishi wa Umma 290,625 ambapo kati yake 166,548 ni Walimu.
Kuhusu malimbikizo ya madeni, Mhe. Rais Magufuli amesema tangu Novemba 2015 Serikali imelipa malimbikizo ya mishahara ya jumla ya shilingi Bilioni 115.3 ambapo kati yake shilingi Bilioni 38.3 wamelipwa Walimu wapatao 35,805. Serikali pia imelipa madeni yasiyo ya mishahara (likizo na uhamisho) ya shilingi Bilioni 358.1 na kwamba itaendelea kulipa madeni hayo kadiri uhakiki unavyofanyika.
Mhe. Rais Magufuli amezungumzia malipo ya mafao ya Walimu ambapo amesema kati ya Agosti 2018 na Juni 2020, Walimu 15,029 wamelipwa kiasi cha shilingi Trilioni 1.2 kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF na kwamba Walimu 2,631 waliobaki ambao wanadai shilingi Bilioni 215, watakuwa wamelipwa ifikapo Agosti 2020.
Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inatambua kuwa kati ya Watumishi wa Umma wote 524,295, Watumishi 266,905 ni Walimu (sawa na asilimi 51) na kwamba pamoja na kuwaajiri walimu 22,342 katika kipindi hiki cha miaka mitano walimu wengine 13,526 wataajiriwa katika mwaka huu wa fedha.
Amewataka viongozi wa CWT watakaochaguliwa leo kuendeleza uhusiano mzuri na Serikali na kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya Walimu badala ya maslahi yao wenyewe, pamoja na kusimamia vizuri mali na miradi ya chama hicho.
Rais wa CWT Mwl. Leah Ulaya na Katibu Mkuu wake Mw. Deus Seif wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ushirikiano mkubwa ambao CWT inaupata kutoka Serikalini ikiwa ni pamoja na kuwapandisha vyeo Walimu, kutopunguza mishahara yao baada ya shule kufungwa kutokana na ugonjwa wa Corona, kulipa madeni ya Walimu na kuboresha mazingira ya kazi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
05 Juni, 2020
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 30 Mei, 2020 wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi Kuu za Ikulu, Mkoani Dodoma.
Majengo 6 ya Ofisi za Ikulu yaliyounganishwa yanajengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika eneo la Vikonje Jijini Dodoma kwa usanifu na muonekano sawa na majengo ya Ofisi za Ikulu Jijini Dar es Salaam, na yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 5 ijayo.
Ujenzi wa majengo ya ofisi hizo ni sehemu ya ujenzi mkubwa wa Ikulu Mkoani Dodoma, na tayari majengo mengine mbalimbali ikiwemo nyumba ya makazi ya Rais, Ofisi mbalimbali na uwigo wa ukuta (Fence) wenye urefu wa kilometa 27 yamekamilika na yanatumika.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kazi nzuri ya ujenzi wa ofisi hizo pamoja na majukumu mengine ya ujenzi na uzalishaji mali wanayoyatekeleza, na ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada hizo.
Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambayo ni mkandarasi mshauri wa mradi huo na amemuagiza Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango kutoa shilingi Bilioni 2 zitakazoungana na shilingi Bilioni 1 zilizotolewa awali ili JKT kupitia shirika lake la SUMA-JKT wakamilishe ujenzi katika kipindi cha miezi 5 walioahidi.
Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Mama Maria Nyerere na Marais Wastaafu kwa kuhudhuria sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo na kutembelea maeneo ya Ikulu ya Chamwino ambapo wamejionea kazi iliyofanyika kujenga miundombinu na majengo ikiwemo makazi ya Rais.
Mhe. Rais Magufuli ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kuchukua hatua madhubuti za kutekeleza azimio la Serikali kuhamia Dodoma kama alivyoahidi mwezi Julai 2016 ambapo tayari Wizara zote, watumishi, viongozi wakuu akiwemo yeye mwenyewe wamehamia Dodoma, na kwamba kutokana na mafanikio hayo ameona ni vema jengo kuu la Ofisi za Ikulu lijengwe kwa mfano uleule wa Ikulu ya Dar es Salaam ili kutunza historia.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere alipotangaza uamuzi wa kuhamia Dodoma na kujenga Ikulu ya Chamwino, alichukua eneo la ekari 61 ambalo lilikuwa ni kubwa zaidi ya ekari 41 za Ikulu ya Dar es Salaam, lakini baada ya yeye kuamua kutekeleza uamuzi huo ameongeza eneo hadi kufikia ekari 8,473, amejenga kilometa 27 za ukuta wa kuzunguka eneo lote, amejenga barabara za lami na ameweka wanyama mbalimbali wakiwemo pundamilia, twiga, swala, sungura pori, kudu, batamaji na aina mbalimbali za ndege.
Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa ukubwa wa Ikulu ya Chamwino (ekari 8,473) ni zaidi ya mara 15 ya ukubwa Hifadhi ya Taifa ya Saanane yenye ukubwa ekari 533 na kwamba kutokana na uwepo wa wanyamapori na mandhari ya kuvutia, Ikulu ya Chamwino inaweza kutumika kama kivutio cha utalii
Katika salamu zao, Waheshimiwa Marais wastaafu na familia ya Baba wa Taifa (salamu zimewasilishwa na Ndg. Makongoro Nyerere) wamempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuhamisha Serikali yote kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma pamoja na kujenga majengo na miundombinu mbalimbali ya Ikulu, Chamwino ikiwemo Ofisi Kuu ya Ikulu.
Sherehe hizo, zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Mawaziri Wakuu Wastaafu (Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda), Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa.
Mapema, Mama Maria Nyerere (kwa niaba ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere), Rais Mstaafu Mwinyi, Rais Mstaafu Mkapa na Rais Mstaafu Kikwete walikabidhiwa ndege aina ya Tausi 25 na kilo 100 za chakula cha Tausi kwa kila mmoja kwa ajili ya kwenda kuwafuga katika bustani zao. Viongozi hao waandamizi wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwapa ndege hao.
Ndege aina ya Tausi ambao waliletwa nchini na Baba wa Taifa hayati Mwl. Nyerere wameongezeka kwa idadi kubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kutoka 403 hadi 2,260 na hivi sasa wanawekwa katika Ikulu ndogo za hapa nchini.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
-
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
-
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Mei, 2020 ameungana na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato Mkoani Geita kusali Ibada ya Jumapili iliyoongozwa na Mchungaji Thomas Paschal Kangeizi.
Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amewashukuru Waumini wa KKKT Usharika wa Chato kwa kumkaribisha kusali Ibada ya Jumapili pamoja nao, na pia amemshukuru Askofu Mkuu wa KKKT Dkt. Fredrick Shoo na Askofu wa Jimbo la Kusini C (Biharamulo) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Askofu Abednego Keshomshahara kwa kuwaruhusu Waumini kuendelea na Ibada huku wakichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru viongozi wote wa Dini hapa nchini ambao wamemtanguliza Mwenyezi Mungu na kuwaongoza Waumini kumuomba Mungu aepushe janga la ugonjwa wa Corona na pia kwa kumuombea na kumtia moyo katika kipindi hiki kigumu ambapo dunia inapita katika janga la ugonjwa huo.
Mhe. Rais Magufuli amesema hakutoa amri ya kuwafungia ndani wananchi (lockdown) wala kufunga mipaka kwa sababu ingeleta madhara makubwa katika shughuli za uzalishaji mali, utekelezaji wa miradi, ajira za watu na pia upatikanaji wa mahitaji muhimu ikiwemo chakula hali ambayo ingesababisha madhara makubwa zaidi.
Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa anamuamini Mungu aliyehai na ndio maana aliamua kumtanguliza Mungu katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwa maombi ya siku 3 na sasa amewasihi viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa ujumla kutumia siku 3 za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ijayo kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa hivi sasa maambukizi ya ugonjwa Corona yameanza kupungua.
Ametoa takwimu za mpaka leo tarehe 17 Mei, 2020 kuwa Hospitali ya Amana (Dar es Salaam) iliyokuwa na wagonjwa 198 imebakiwa na mgonjwa 12, Hospitali ya Mloganzila iliyokuwa na wagonjwa 30 imebakiwa na wagonjwa 6, Kituo cha Lulanzi (Kibaha) kulikuwa na wagonjwa zaidi ya 50 wamebaki 22, Agha Khan wamebaki wagonjwa 31, Hindu Mandal 16, Regency wamebaki 17, TMJ 7, Rabinisia 14, Moshono (Arusha) 11, Longido 0, Karatu 0, Buswelu 2, Misungwi 2, Ukerewe 0, Magu 0, Mkuyuni 0, Nyahunge 0, Sengerema 0, Kwimba 0, Bugando na Sekou Toure 2, Dodoma 2 (kutoka zaidi ya 40), Kongwa 0, Kondoa 0 nakadhalika. Na kwamba wagonjwa wengi wana hali nzuri.
“Mimi namwamini Mungu na Mungu amejibu maombi yetu, tumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutusikiliza na tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu wa Corona” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amesema endapo hali ya ugonjwa wa Corona itaendelea hivi Serikali inafikiria kufungua vyuo ili wanafunzi warudi vyuoni kuendelea na masomo na pia michezo itaruhusiwa kuendelea kufanyika hapa nchini.
Amebainisha kuwa kuna idadi kubwa ya watalii wanaotaka kuja hapa nchini na ambao tayari wameonyesha nia ya kukata tiketi za kuja, hivyo ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na mamlaka zingine zinazohusika kutowazuia watalii na ndege zinazotaka kuleta wageni hapa nchini.
Amesisitiza kuwa viongozi na Watanzania wote wasiwe na hofu kubwa dhidi ya ugonjwa wa Corona kiasi cha kusababisha matatizo mengine ikiwemo kutowahudumia ipasavyo wagonjwa mbalimbali ambao baadhi wanaambiwa wana Corona ilihali hawajaambukizwa ugonjwa huo, ama kuwazuia watoa huduma wakiwemo Madaktari na Wauguzi wanaoshukiwa kuwa wameambukizwa Corona.
Amesema “wapo watu ambao wanaambiwa wana Corona lakini wakipimwa tena wanakutwa hawana” na amewataka viongozi waache kuwazuia watu kuzika kwa heshima marehemu wao kama ambavyo wanawazika watu waliokufa kwa magonjwa mengine yakiwemo ukimwi, kifua kikuu na surua.
“Hata mimi mtoto wangu alipata Corona lakini amepona, alikuwa anakula limau, tangawizi, anajifukiza mpaka amepona, kwa hiyo ugonjwa huu utasambaa na utakwisha, hatuwezi kufunga mipaka, sisi Tanzania tukifunga mipaka nchi zinazotuzunguka watapata shida, hata sasa tulipata tatizo la upungufu wa sukari, nimezungumza na Rais wa Uganda Mhe. Museveni na zimekuja tani 26,000 kwa meli hadi Mwanza, na tani nyingine 10,000 zimekuja kupitia bandari ya Dar es Salaam, tungefunga mipaka ingekuwaje?” amesema Mhe. Rais Magufuli
Amesisitiza kuwa Watanzania waendelee kuchapa kazi hasa kuzalisha chakula kwa wingi kwa kuwa majirani ambao wamefunga mipaka na wamewafungia watu wao (lockdown), pindi watakapofungua watahitaji chakula na watakuja Tanzania.
“Tutumie mvua hizi za mwisho zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwetu, kuzalisha mazao yanayokomaa haraka ili baadaye wenzetu watakapofunguliwa tuwauzie chakula, endeleeni kuchapa kazi” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Kuhusu uchunguzi uliofanyika katika Maabara ya Taifa, Mhe. Rais Magufuli amesema tume iliyoundwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu imefanya kazi nzuri na matokeo ya uchunguzi wake yatatangazwa na Waziri mwenyewe.
Mchungaji wa KKKT Usharika wa Chato Thomas Paschal Kangeizi amemshukuru Mhe. Rais Magufulu kwa kuungana nao katika Ibada, kuruhusu Makanisa kufanya Ibada na amemuahidi kuwa Wataendelea kumuombea ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ulinzi wa Mwenyezi Mungu.
Katika Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamechangia shilingi Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jipya la KKKT Chato na amechangia shilingi Milioni 1 kwa ajili ya kwaya 3 zilizoimba katika Ibada hiyo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
17 Mei, 2020
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 03 Mei, 2020 amemuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Chato Mkoani Geita.
Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mhe. Nchemba kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na mtangulizi wake Marehemu Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga aliyefariki dunia tarehe 01 Mei, 2020 na pia kushirikiana na viongozi wenzake katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali.
“Nimekuteua kwa mara ya pili kwa sababu naamini unaweza kutekeleza jukumu hili vizuri, na bahati nzuri vijana wengi niliowateua hawajaniangusha, kwa hiyo nakutakia heri katika kazi zako na Mungu akutangulie” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amerejea kauli yake ya kuwataka Watanzania kutokuwa na hofu kubwa dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) na badala yake waendelee kuchukua tahadhari kama zinavyoelekezwa na wataalamu.
Amefafanua kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa ambao unasambazwa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi, hali ambayo haisadii kupunguza tatizo bali kuliongeza na kutengeneza sintofahamu kubwa.
Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia Walimu ambao ni asilimia 49 ya wafanyakazi wote hapa nchini pamoja na wafanyakazi wengine kuwa licha ya changamoto za kiuchumi zinazosababishwa na ugonjwa wa Corona, Serikali imejipanga kuhakikisha wanalipwa mishahara yao kama kawaida na ametoa wito kwa taasisi za kifedha za kimataifa zilizoonesha nia ya kusaidia uchumi wa nchi zinazoendelea, kusamehe mikopo badala ya kutaka kuzikopesha mikopo mipya.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe (aliyeteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni) kwa kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi wa vifaa vya uchunguzi wa ugonjwa wa Corona na ameagiza maabara kuu ya Taifa inayofanya uchunguzi wa ugonjwa huo ichunguzwe vizuri ili kujiridhisha juu ya usahihi wa majibu ya sampuli zinazopelekwa kuchunguzwa.
Amewataka Watanzania wote hasa wanasiasa pamoja vyombo vya habari kuacha kueneza taarifa zinazowajaza watu hofu ama kutumia ugonjwa huu kwa manufaa ya kisiasa na badala yake waungane kutoa elimu sahihi na kuhimizana kuchukua tahadhari za kutoambukizwa.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Madaktari, Wauguzi, Wafanyakazi wa Afya na wadau mbalimbai walio mstari wa mbele katika kuwahudumia watu wanaopatwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona na amewahakikishia kuwa Serikali inachukua hatua madhubuti za kukabiliana nao ikiwemo kupata dawa kutoka mahali popote itakapopatikana.
Ameelezea kushangazwa kwake na viongozi ambao wanazuia watu wanaofariki dunia kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao, na Viongozi wa Dini walioonesha kutetereka kiimani, hivyo ametoa wito kwa viongozi wote kusimama imara, kuonesha uongozi wa kweli na kuwapa matumaini wananchi badala ya kuwajaza hofu.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeiry bin Ally na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga pamoja na viongozi wengine wa Dini waliosimama katika imani na kuwataka Waumini waendelee kusali, kufunga na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe ugonjwa huu.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
03 Mei, 2020
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Brig. Jen Dkt. Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (Medical Stores Department - MSD).
Uteuzi wa Brig. Jen Dkt. Mhidize unaanza mara moja, leo tarehe 03 Mei, 2020.
Kabla ya uteuzi huo, Brig. Jen Dkt. Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Brig. Jen Dkt. Mhidize anachukua nafasi ya Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
03 Mei, 2020
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Delphine Diocles Magere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.
Dkt. Magere anachukua nafasi ya Bi. Theresia Mmbando ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Magere alikuwa Ofisi ya Rais akishughulikia masuala ya uchumi.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Dunstan Kyobya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mkoani Mtwara.
Bw. Kyobya anachukua nafasi ya Bw. Evod Mmanda aliyefariki Dunia tarehe 27 Aprili, 2020.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kyobya alikuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 06 Mei, 2020.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
06 Mei, 2020
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za kifo cha ghafla cha mtangazaji maarufu na mahiri Ndg. Marine Hassan kilichotokea leo asubuhi Jijini Dar es Salaam. Marine Hassan aliipenda kazi yake ya uandishi wa habari, aliifanya kwa weledi wa hali ya juu, alikuwa mzalendo wa kweli na alidhamiria kuitumikia nchi yake kupitia chombo cha habari cha Taifa (TBC) kwa nguvu na juhudi zake zote”.
Hii ni sehemu ya salamu za rambirambi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alizozitoa kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari Mwandamizi na mtangazaji maarufu wa Shirika la Utangazji Tanzania (TBC) Bw. Marine Hassan Marine kilichotokea leo asubuhi tarehe 01 Aprili, 2020 katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Katika salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli ametoa pole kwa familia ya Marine Hassan, Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba, Wafanyakazi wote wa TBC, Waandishi wa Habari wote na wote walioguswa na kifo cha mwanahabari huyo nguli hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli amesema alimfahamu Marine Hassan kama mtu aliyetoa mchango mkubwa katika ustawi wa Uandishi wa Habari nchini Tanzania na kwa juhudi zake kubwa ndani ya TBC ambapo aliliripoti habari kwa ubunifu na mvuto wa hali ya juu, alibuni na kufanya vipindi vilivyopendwa na Watanzania ikiwemo vipindi vya Uchaguzi Mkuu, Safari ya Dodoma na mabadiliko makubwa yaliyoanza juzi ambapo TBC inatangaza habari zake kupitia ARIDHIO.
“Marine Hassan ameondoka wakati ambapo tunamhitaji zaidi, Marine Hassan ni shujaa wa habari Tanzania, aliipenda sana TBC na nchi yake Tanzania. Naungana na familia yake, TBC na Waandishi wa Habari wote kumuombea apumzike mahali pema peponi, Amina” amesema Mhe. Rais Magufuli. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
01 Aprili, 2020