Taarifa kwa vyombo vya Habari ya zamani
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku 7 za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Zambia, Dkt. Kenneth David Kaunda, kilichotokea jana tarehe 17 Juni, 2021 mjini Lusaka Zambia. Katika kipindi hicho cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti. Aidha, Mhe. Rais Samia ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Chagwa Lungu, familia ya marehemu na wananchi wote wa Zambia kwa kumpoteza kiongozi wao. Mhe. Rais Samia amemtaja Hayati Dkt. Kaunda kuwa miongoni mwa viongozi mahiri na jasiri kuwahi kutokea barani Afrika, ambapo wakati wa uhai wake alitoa mchango mkubwa kwenye harakati za ukombozi wa Bara la Afrika kwa kushirikiana na viongozi wengine, akiwemo Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vilevile, Hayati Dkt. Kaunda alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Tanzania itamkumbuka Hayati Dkt. Kaunda kwa mchango wake katika kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa yetu mawili, ambao uliwezesha kutekelezwa kwa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Mamlaka ya Reli kati ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Bomba la Kusafirisha Mafuta (TAZAMA). Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema Peponi.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Adesina Akinumwi amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa benki hiyo itaendelea kufadhili miradi ya maendeleo hapa nchini na ipo tayari kufadhili miradi mipya kwa kuwa Tanzania ina sifa za kuendelea kupata ufadhili. Dkt. Adesina aliyepo Jijini Abidjan nchini Ivory Coast amesema hayo tarehe 11 Juni, 2021 wakati akizungumza kwa njia simu na Mhe. Rais Samia aliyepo Jijini Dar es Salaam kuhusu uhusiano wa Tanzania na benki hiyo ambayo imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali ya maendeleo. Katika mazungumzo hayo Dkt. Adesina ambaye ameanza kwa kutoa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kutoa pongezi kwa Mhe. Rais Samia kwa kupokea kijiti cha Urais amesema Tanzania inafanya vizuri katika uchumi na ana matumaini makubwa kuwa Mhe. Rais Samia ataendeleza jitihada zilizokuwa zikifanywa na mtangulizi wake. Ameahidi kuwa AfDB itatoa ufadhili kwa Tanzania ili kuanzisha benki za wajasiriamali zitakazowakopesha vijana wanaohitimu mafunzo ya ufundi stadi pamoja na kujihusisha na kilimo, jambo litakalosaidia kupungua kwa tatizo la ajira kwa vijana na kuwaongezea kipato. Aidha, Dkt. Adesina amemualika Mhe. Rais Samia kuhudhuria mkutano wa uwekezaji utakaowaleta wawekezaji wakubwa pamoja ambao unatarajiwa kuvutia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuwekeza katika nchi mbalimbali. Pia, Dkt. Adesina amesema AfDB imetenga dola za Marekani Bilioni 5 kwa ajili ya kusaidia wanawake na ameomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo Mhe. Rais Samia amekubali ombi hilo. 2 Dkt. Adesina ameahidi kuleta wataalamu wa benki hiyo hapa nchini ili wakutane na wataalamu wa Tanzania kwa ajili ya kupitia miradi ambayo tayari inafadhiliwa na benki hiyo na kujadili fursa za kuanzisha miradi mipya. Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Dkt. Adesina kwa salamu zake za pole na pongezi na amemshukuru kwa benki hiyo kufadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwemo inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa awamu ya pili na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na benki hiyo. Ameelezea kufurahishwa kwake na mradi wa AfDB wa kufadhili vijana wanaojihusisha na kilimo na wanaomaliza mafunzo katika vyuo vya ufundi stadi kwa kuwa ufadhili huo utawawezesha vijana wengi wa Tanzania kuzalisha mali. Pamoja na kumpongeza Dkt. Adesina kwa ushindi wake wa kuchaguliwa kuwa Rais wa AfDB kwa kipindi cha pili, Mhe. Rais Samia amemuomba kuongeza nafasi za Watanzania wanaoajiriwa katika benki hiyo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo: Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhandisi. Robert Gabriel Luhumbi anahamia Mkoa wa Mwanza ambapo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Albert Chalamila uteuzi wake umetenguliwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bwana Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara. Mhe. Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora Aidha Ndugu Zuwena Omari Jiri ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Simanjiro ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani. Tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wanawake kote nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazowasaidia kusukuma mbele maendeleo yao na ya Taifa kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayo dhamira ya dhati ya kuwaunga mkono. Mhe. Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 08 Juni, 2021 alipokuwa akizungumza na wanawake wa Tanzania kupitia wanawake wa Mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma uliohudhuriwa na zaidi ya Wanawake 8,000. Mhe. Rais Samia amesema kutokana na takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuonesha kuwa hadi mwaka jana Tanzania ilikuwa na wanawake zaidi ya Milioni 29.4 ambao ni asilimia 51.04 ya watu wote, wanawake ni jeshi kubwa ambalo linategemewa katika uchumi na ustawi wa jamii hivyo hawapaswi kubaki nyuma na badala yake watumie fursa mbalimbali zilizopo kufanya mageuzi yatakayolisaidia Taifa kusonga mbele. Amebainisha kuwa Serikali itaendelea kujenga miundombinu na kuimarisha huduma zitakazowawezesha wanawake kufanya shughuli zao kwa manufaa na tija ikiwemo kujenga miundombinu ya usafiri, elimu, afya, maji na kuwaunganisha na taasisi zinazotoa ujuzi na fedha za kuendeshea biashara Mhe. Rais Samia ametaja baadhi ya maeneo ambayo Serikali imewawezesha wanawake kiuchumi kuwa ni kuanzisha mifuko 61 ambayo imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Trilioni 2.22 kwa wanawake Milioni 5.3 na mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 63.489 iliyowafikia wanawake 938,802. Kuhusu majukwaa ya kuwawezesha wanawake ambayo yeye mwenyewe ameyaanzisha katika ngazi za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji, na ambayo yamewasaidia wanawake wengi kuanzisha vyama vya akiba na mikopo, Mhe. Rais Samia ametaka viongozi wa ngazi husika wahakikishe majukwaa hayo yanakuwa na uhai na kwamba yeye mwenyewe atayatupia macho. Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa wanawake wote nchini, kukaa na kutafakari maeneo ambayo wanafanya vizuri na maeneo ambayo hawafanyi vizuri ili kuchukua hatua za kurekebisha dosari na amewata Mawaziri wenye dhamana za afya, elimu na Serikali za Mitaa kushughulikia changamoto za Wanawake ili kurahisisha shughuli zao. Amewahakikishia Watanzania wote kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha inatekeleza ipasavyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ikiwemo kuhakikisha usambazaji wa maji Mijini unafikia asilimia 95 na Vijijini asilimia 85, kujenga miundombinu ya usafiri na usafirishaji ikiwemo ujenzi wa reli na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato Mkoani Dodoma. Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka wanawake kote nchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira ambayo ni muhimu katika utatuzi wa changamoto ya maji, kuhamasika kutumia mifumo ya kidijitali na amezialika taasisi na mashirika mbalimbali ya binafsi na Serikali kujitokeza kuwawezesha wanawake wa Tanzania. Katika risala ya wanawake, iliyosomwa na Bi. Joyce Kashozi wanawake hao wamemshukuru Mhe. Rais Samia kwa namna anavyowaamini wanawake na kuwapa nafasi nyingi za uongozi na wamemuahidi kutomuangusha.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RIPOTI YA KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA WA COVID-19 NCHINI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS SAMIA SULUHU AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA NA KUWAHAMISHA WENGINE.
TAAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMKABIDHI NYUMBA RAIS MSTAAFU JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 09 Mei, 2021 amemkabidhi nyumba ya kuishi Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete iliyojengwa katika Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam.
Nyumba hiyo imejengwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ikiwa ni utekelezaji wa kifungu namba 12 cha Sheria ya mafao ya hitimisho la kazi kwa viongozi wa siasa, sura ya 225 na marejeo ya mwaka 2020 ambayo pamoja na stahili zingine za matunzo ya viongozi wakuu wastaafu inaelekeza kuwa Rais anayestaafu anastahili kujengewa nyumba ya kuishi yenye hadhi ya Rais.
Akizungumza baada ya kukabidhi nyumba hiyo, Mhe. Rais Samia amempongeza Mhe. Rais Mstaafu Kikwete kwa kupata makazi hayo na amemhakikishia kuwa Serikali itaendelea kumtunza yeye na viongozi wengine wastaafu kama inavyoelekezwa katika sheria.
Amebainisha kuwa Serikali itafanyia kazi uboreshaji wa sheria hiyo pamoja na kuhakikisha wajane/wagane wa viongozi wanatunzwa.
Mhe. Rais Samia amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa kuanza maandalizi ya kutimiza haki zote anazostahili aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Kwa upande wake, Mhe. Waziri Mchengerwa amesema nyumba hiyo ni ya 3 kukabidhiwa ikitanguliwa na nyumba ya Mhe. Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa na Mhe. Rais Mstaafu Dkt. Ali Hassan Mwinyi na kwamba nyumba ya Baba wa Taifa Hayati Mw. Julius Kambarage Nyerere ilijengwa na kukabidhiwa kwake na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Katika shukrani zake, Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeongozana na Mkewe Mhe. Mama Salma Kikwete ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutekeleza takwa hilo la kisheria, ameishukuru TBA kwa kukamilisha ujenzi tangu ulipoanza mwaka 2018 na amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kumkabidhi nyumba hiyo.
Mhe. Rais Mstaafu Kikwete amempongeza Mhe. Rais Samia kwa uongozi wake tangu alipopokea kijiti kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwani nchi imetulia, mambo yanakwenda na watu wana matumaini makubwa nae.