Taarifa kwa vyombo vya Habari ya zamani
Taarifa kwa vyombo vya habari
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mtumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama cha TANU na Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika kwa miaka mingi, Brigedia Hashim Mbita. Mzee Mbita ambaye amekuwa anauguza afya yake kwa muda sasa amefariki asubuhi ya leo, Jumapili, Aprili 26, 2015 mjini Dar Es Salaam. Kufuatia taarifa za msiba huo, Rais Kikwete ameelekeza Serikali na Jeshi kushirikiana na familia kusimamia msiba huo na kuandaa mazishi ya Mzee huyo. (N.B. Salamu Kamili za Rambirambi za Mhe. Rais zinafuatia baada ya muda) Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 26 April, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mtumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama cha TANU na Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika kwa miaka mingi, Brigedia Hashim Mbita.
Mzee Mbita ambaye amekuwa anauguza afya yake kwa muda sasa amefariki asubuhi ya leo, Jumapili, Aprili 26, 2015 mjini Dar Es Salaam.
Kufuatia taarifa za msiba huo, Rais Kikwete ameelekeza Serikali na Jeshi kushirikiana na familia kusimamia msiba huo na kuandaa mazishi ya Mzee huyo.
(N.B. Salamu Kamili za Rambirambi za Mhe. Rais zinafuatia baada ya muda)
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 April, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili, Aprili 12, 2015 aliungana na maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Shinyanga, kuhudhuria Ibada rasmi ya kumweka wakfu na kumsimika Askofu mpya wa Jimbo hilo, Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu.
Rais Kikwete aliwasili kwenye Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga kiasi cha saa sita unusu mchana kwa ajili ya Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wasaidizi 38, akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Rais wa Mabaraza ya Kipapa na Katibu Mwambata wa Uenezaji Injili Ulimwenguni Askofu Mkuu Protase Rugambwa kutoka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.
Askofu Sangu ambaye amewekwa wakfu na kusimikwa kwenye Siku ya Huruma ya Mungu Duniani anakuwa Askofu wa nne wa Jimbo la Shinyanga na anachukua nafasi iliyoachwa wazi tokea Novemba 6, 2012, wakati aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo, Baba Askofu Aloysius Balina alipofariki dunia.
Kwa miaka karibu mitatu, jimbo hilo limekuwa chini ya Usimamizi wa Kitume wa Askofu Mkuu Yuda Tadei R’uaichii wa Jimbo Kuu la Mwanza.
Askofu Sangu mwenye umri wa miaka 52 baada ya kuwa amezaliwa Februari 19, Mwaka 1963, katika Kijiji cha Mwazye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, alipata daraja la upadrisho Julai 3, Mwaka 1994. Wakati anateuliwa na Baba Mtakatifu Francesco kuwa Askofu Februari 2, mwaka huu wa 2015, alikuwa na daraja la Mosinyori.
Akikabidhi Jimbo hilo kwa Askofu mpya, Askofu Mkuu R’uaichii amesema kuwa Jimbo la Shinyanga ni moja ya majimbo makubwa zaidi ya Kanisa Katoliki nchini, likiwa na kilomita za mraba karibu 30,000 na waumini Wakatoliki wanaokaridiwa kufikia 300,000 katika Mkoa ambao idadi kiasi ya wakazi wake bado wanaamini imani za jadi.
Amesema kuwa Jimbo hilo lina parokia 29, mapadre wa Jimbo 52, mapadre wa Kitawa 18 na hivyo kulifanya jimbo hilo kuwa na jumla ya mapadre 70 na “jeshi kubwa” la watawa 70.
Kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na viongozi wengi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Lufunga, Askofu Sangu amepewa zawadi ya sh. milioni 18, fimbo ya kiuchungaji na ng’ombe 10 wa maziwa na Wakatoliki wa Jimbo hilo.
Rais Kikwete alirejea Dar es Salaam jana jioni baada ya kumalizika kwa Ibada hiyo.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
13 Aprili, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Aprili 10, 2015 amepokea Ripoti ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza katika halfa fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Mara baada ya kupokea Ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru Tume kwa kazi nzuri na kuongeza kuwa amefurahi kuwa suala zima la Operesheni Tokomeza sasa limefika mwisho wake.
Aidha, Rais amesema kuwa Serikali itaisoma Ripoti hiyo na katika wiki mbili itatoa maelezo ya jinsi Ripoti hiyo itakavyoshughulikiwa.
Rais Kikwete amepokea Ripoti hiyo kutoka kwa Balozi Jaji (mstaafu) Hamisi Amiri Msumi, Mwenyekiti wa Tume ambayo Rais Kikwete aliiteua Mei Mosi, mwaka jana, 2014, na kuitaka ichunguze tuhuma mbali mbali za uvunjifu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea za Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.
Aidha, Rais Kikwete aliipa Tume hiyo jukumu la kupendekeza hatua stahiki za kisheria za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuhusika na uvunjifu huo. Vile vile, Rais aliiagiza Tume hiyo ishauri namna bora ya utekelezaji wa Operesheni kama hiyo hapo baadaye.
Rais Kikwete pia aliipa Tume hiyo Hadidu za Rejea sita ambazo pia ziliainishwa katika Taarifa ya Serikali Nambari 131 ya 2014. Hadidu za Rejea hizo ni kama zifuatazo:
(a) Kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa;
(b) Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tomokeza walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea walizopewa;
(c) Kuchunguza iwapo maofisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa.
(d) Kuchunguza iwapo kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na iwapo hatua zilizochukuliwa na maofisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya wakosaji hao na mali zao zilikuwa sahihi;
(e) Kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea za Operesheno Tokomeza; na
(f) Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kupanga na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii, ili kuepuka malalamiko mengine yasitokee.
Jaji Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa katika kutelekeza majukumu yake, Tume ilitembelea mikoa 20 na wilaya 38 na kupokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa wafuatao:
(a) Viongozi wa Serikali ikiwa ni pamoja na mawaziri wanne waliojiuzulu kutokana na sakata hilo;
(b) Watekelezaji wa Operesheni; na
(c) Walalamikaji/wahanga wa Operesheni.
Jaji Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa Ripoti ya Tume ina Juzuu kumi, Juzuu ya kwanza ikiwa ni Muhtasari wa Taarifa ya Tume, Juzuu ya pili ikiwa ni Taarifa yenyewe ya Tume, Juzuu ya tatu hadi ya tisa ikiwa ni Mwenendo wa Ushahidi (Proceedings) na Juzuu ya kumi ikiwa ni vielelezo vilivyotolewa na mashahidi.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Aprili, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Dkt. Rajabu Rutengwe kuomboleza vifo vya watu 18 na wengine 11 kujeruhiwa katika ajali ya basi na lori iliyotokea mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Msimba kwenye Barabara Kuu ya Morogoro – Mbeya kilometa chache kutoka Ruaha Mbuyuni na kusababisha miili ya abiria hao 18 kuungua vibaya.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 18 kutokana na ajali mbaya ya barabarani iliyosababisha miili yao kuungua vibaya. Huu ni msiba mkubwa kwa Taifa, hivyo nakutumia salamu zangu za rambirambi, na kupitia kwako naomba salamu zangu za rambirambi na pole nyingi ziwafikie pia wanafamilia, ndugu na jamaa waliopotelewa na wapendwa wao katika ajali hiyo.
Namuomba Mola awape moyo wa uvumilivu na subira watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao katika ajali hiyo mbaya. Vilevile namuomba Mola awawezeshe majeruhi wote wa ajali hiyo kupona haraka, ili warejee katika hali yao ya kawaida na kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao, ameongeza kusema Rais Kikwete.
Aidha, namuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza mahala pema peponi Roho za Marehemu wote, Amina.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu - Dar es Salaam.
14 Aprili, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Aprili 10, 2015 amepokea Ripoti ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza katika halfa fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Mara baada ya kupokea Ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru Tume kwa kazi nzuri na kuongeza kuwa amefurahi kuwa suala zima la Operesheni Tokomeza sasa limefika mwisho wake.
Aidha, Rais amesema kuwa Serikali itaisoma Ripoti hiyo na katika wiki mbili itatoa maelezo ya jinsi Ripoti hiyo itakavyoshughulikiwa.
Rais Kikwete amepokea Ripoti hiyo kutoka kwa Balozi Jaji (mstaafu) Hamisi Amiri Msumi, Mwenyekiti wa Tume ambayo Rais Kikwete aliiteua Mei Mosi, mwaka jana, 2014, na kuitaka ichunguze tuhuma mbali mbali za uvunjifu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea za Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.
Aidha, Rais Kikwete aliipa Tume hiyo jukumu la kupendekeza hatua stahiki za kisheria za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuhusika na uvunjifu huo. Vile vile, Rais aliiagiza Tume hiyo ishauri namna bora ya utekelezaji wa Operesheni kama hiyo hapo baadaye.
Rais Kikwete pia aliipa Tume hiyo Hadidu za Rejea sita ambazo pia ziliainishwa katika Taarifa ya Serikali Nambari 131 ya 2014. Hadidu za Rejea hizo ni kama zifuatazo:
(a) Kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa;
(b) Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tomokeza walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea walizopewa;
(c) Kuchunguza iwapo maofisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa.
(d) Kuchunguza iwapo kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na iwapo hatua zilizochukuliwa na maofisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya wakosaji hao na mali zao zilikuwa sahihi;
(e) Kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea za Operesheno Tokomeza; na
(f) Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kupanga na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii, ili kuepuka malalamiko mengine yasitokee.
Jaji Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa katika kutelekeza majukumu yake, Tume ilitembelea mikoa 20 na wilaya 38 na kupokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa wafuatao:
(a) Viongozi wa Serikali ikiwa ni pamoja na mawaziri wanne waliojiuzulu kutokana na sakata hilo;
(b) Watekelezaji wa Operesheni; na
(c) Walalamikaji/wahanga wa Operesheni.
Jaji Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa Ripoti ya Tume ina Juzuu kumi, Juzuu ya kwanza ikiwa ni Muhtasari wa Taarifa ya Tume, Juzuu ya pili ikiwa ni Taarifa yenyewe ya Tume, Juzuu ya tatu hadi ya tisa ikiwa ni Mwenendo wa Ushahidi (Proceedings) na Juzuu ya kumi ikiwa ni vielelezo vilivyotolewa na mashahidi.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Aprili, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Kissiok Ole Mbille Lukumay kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.
Aidha, Rais Kikwete amemteua Bwana Onesmo Hamis Makombe kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu.
Taarifa iliyotolewa usiku wa jana, Alhamisi, mjini Dar es Salaan na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa maofisa hao wawili ulianza Ijumaa ya Machi 27, 2015.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Lukumay ambaye ana diploma in Materials Management na ni Certified Supplies Professional na pia ana MBA (Procurement and Logistics) alikuwa Ofisa Ugavi Mkuu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.
Naye Bwana Makombe kabla ya uteuzi wake alikuwa Kaimu Kamishna, Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu. Kielimu, Bwana Makombe ana shahada za B.Com, CPA na MBA (Finance and Human Resources Management).
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Aprili,2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Serikali ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani Mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka 2025 (Tanzania Development Vision 2025) ambao unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International Centre.
"Naamini mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza kutoka pale tutakapoachia" Rais amesema na kuongeza kuwa pia anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia Gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo Mwaka 2020. Katika mhadhara huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Mabalozi, wasomi na viongozi wa taasisi hiyo, Rais Kikwete ameelezea mafanikio na changamoto katika uongozi wake wa miaka 10 katika elimu, siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.
"Najivunia kuweza kuendelea kuliweka Taifa katika hali ya Umoja pamoja na changamoto zote, tumepambana na vitisho pale vilipojitokeza na pia tumetoa mchango mkubwa katika harakati za kisiasa zilizopelekea vyama viwili kutiliana saini maridhiano na kupata muafaka Mwaka 2010".
Rais ameelezea na kuongeza kuwa makubaliano hayo yalipelekea Zanzibar kufanya uchaguzi kwa amani na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina ya vyama vya CCM na CUF.
"Natumaini tutafanya uchaguzi huru, haki na amani ili niweze kumkabidhi Urais mrithi wangu katika hali ya utulivu" Rais ameongeza.
............Mwisho............
Imetolewa na;
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Washington DC - Marekani
4 Aprili, 2015.
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa furaha na unyenyekevu uteuzi iliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Ban Ki Moon kuwa Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya (High - Level Panel on Global Responses to Health Crises) .
"Ni majukumu makubwa na yenye changamoto nyingi lakini dunia inahitaji tuwe na mikakati katika masula haya ambayo ni muhimu kwa maisha ya binadamu, hivyo hatuna budi kufanya kazi hii Kama mchango wetu kwa ajili ya maisha ya wanadamu na dunia kwa ujumla". Rais amesema mara baada ya kutolewa kwa Tangazo hilo tarehe 2 April, 2015.
Wengine walioteuliwa katika Jopo hili ni Bw. Delos Luiz Nunes Amorim wa Brazil, Bi. Micheline Calmy-Rey wa Switzerland , Bw. Marty Natalegawa wa Indonesia, Bi. Joy Phumaphi wa Botswana na Bw. Rajiv Shah wa Marekani.
Jopo linatarajiwa kufanya kikao chake cha kwanza mapema Mwezi Mei, 2015 na linatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu wa UN mwishoni mwa Mwezi Disemba, 2015.
.........Mwisho……….
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Seattle - Marekani
3 Aprili, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Marekani ni mshirika mkubwa wa Maendeleo Tanzania kwa kuunga mkono shughuli mbalimbali za maendeleo na kijamii , ambazo zimeleta mafanikio na mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jana tarehe 2 April, 2015 jijini Seattle, katika mhadhara uliondaliwa na taasisi ya World Affairs Council na kuhudhuriwa na wafanyabiashara , wafanyakazi wa taasisi mbalimbali walimu na wanafunzi wa shule na vyuo kutoka Seattle.
Rais ametoa mifano ya kazi na michango inayofanywa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kuchangia katika misaada ya kiuchumi na kijamii, misaada ya dharura ya kupunguza makali ya Ukimwi (PEPFER), misaada ya Milenia inayolenga kuondoa umaskini (MCC), Mpango wa Usalama wa Chakula na Kupambana na Njaa maarufu kama Feed the Future na Mpango wa Kusambaza umeme kwa watu wengi zaidi barani Afrika maarufu kama Power Africa.
"Mipango na programu zote hizi zina mchango mkubwa kwa Maendeleo ya Tanzania na Watu wake“. Rais amesema na kuonyesha jinsi mahusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ulivyo imara na wa manufaa makubwa.
Katika hotuba yake, Rais Kikwete amesema anatumaini kuwa ziara yake jijini Seattle itakuza mahusiano baina ya watu wa nchi hizi mbili na kuyafanya kukua na kuimarika kwa kupitia uwekezaji na shughuli mbalimbali za pamoja katika sekta za binafsi na biashara.
Rais Kikwete yuko jijini Seattle kwa shughuli za kikazi kwa siku moja ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea Makao Makuu ya Taasisi ya Bill and Melinda Gates na kufanya mazungumzo na Bw. Bill Gates.Katika mazungumzo yao, Bw. Gates ameahidi kuendeleza juhudi zake na misaada kwa Tanzania katika sekta za Afya na Kilimo.
"Tunatakiwa kuendeleza ushirikiano wetu nawe kwani sauti kama yako katika masuala ya Afya na Kilimo ni chache, hivyo tunataka kuendelea kushirikiana nawe". Bw. Bill Gates amemwambia Rais Kikwete.
Rais pia amefanya ziara katika Makao Makuu ya Shirika la kutengeneza ndege la Boeing ambapo amepata maelezo na kutembelea kiwandani na kuona utengenezaji wa ndege unaofanywa na shirika hilo.
Rais Kikwete anaendelea na ziara katika jiji la Washington DC.
...............Mwisho...............
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Seattle –Marekani.
2 April, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Vijana wa Afrika wamemtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete moja ya matuzo makubwa zaidi yanayotolewa na vijana wa Afrika kwa kutambua uongozi wake bora na mchango wake katika kuendeleza vijana.
Tuzo hiyo iitwayo The African Youth Peace Award hutolewa na Umoja wa Vijana wa Africa wa Pan Africa Youth Union kwa wakuu wan chi na viongozi wa Afrika ambao wamethibitika kuchangia sana kwa ustawi wa Waafrika.
Rais Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo na Rais wa Pan African Youth Union, Bi. Francine Furaha Muyumba wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wakati Rais aliposimama kwa dakika chache kuwasalimia vijana wanaohudhuria Mkutano wa Tatu waViongozi Vijana wa Afrika na China (3rd Africa-China Young Leaders Forum) ulioanza jana, Jumamosi, Machi 28, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ngurdoto, Arusha.
Katika salamu zake za utangulizi, Bi. Muyumba alimweleza Rais Kikwete kama kiongozi mfano wa kuigwa kwa mchango wake katika kuwatambua na kuwaendeleza vijana katika nafasi za uongozi.
Kabla ya kuwasalimia vijana hao, Rais Kikwete ambaye alitembelea Arusha kwa saa chache kabla ya kurejea Dar es Salaam, alikutana kwa mazungumzo na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Zimbabwe, Mheshimiwa Robert Gabriel Mugabe, ambaye alikuwa Arusha kufungua Mkutano huo wa Africa-China Young Leaders Forum jioni ya jana hiyo hiyo.
Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete alimshukuru Rais Mugabe ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa Jumuia ya Mandeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kukubali mwaliko wake wa kutembelea Tanzania, ili kufungua Mkutano huo wa siku mbili. Mkutano huo unaandaliwa kwa pamoja na Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wa Chama cha Kikomunisti cha China.
Mkutano huo wa Africa-China Young Leaders Forum ni wa tatu lakini unafanyika nchini kwa mara ya kwanza. Mikutano miwili ya kwanza ilifanyika Windhoek, Namibia na Beijing, China.
Mbali na Tanzania na China, nchi nyingine za Afrika zinazohudhuria Mkutano huo ni Angola, Kenya, Uganda, Sudan, Shelisheli, Afrika Kusini, DRC, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Eritrea, Burundi, Namibia na Niger.
Rais Kikwete pia alikutana kwa mazungumzo na Mheshimiwa Wang Jiariu, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye ndiye kiongozi wa msafara wa vijana kutoka China kwa ajili ya Mkutano huo.
Rais Kikwete amemshukuru Mheshimiwa Jiariu kwa heshima ambayo vijana wa Afrika na China wameipa Tanzania na Chama cha Mapinduzi kwa uamuzi wao wa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumamosi, Machi 28, 2015 kwenda Marekani kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa.
Miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete amealikwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC - UN).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais apokea Ripoti ya CAG na kuagiza hatua kali zichukuliwe kwa wabadhirifu wa fedha za Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameviagiza vyombo vya Serikali kubaini maofisa wote wa Serikali wanaohusishwa na matumizi mabaya ya fedha za Serikali, ikiwa ni pamoja na kutoa malipo bila nyaraka zozote, kutumia fedha nje ya Bajeti na kutoa malipo bila idhini ya ofisa masuhuli, ili wachukuliwe hatua kali za kisheria na hatua nyingine.
Aidha, Rais Kikwete ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa maofisa wote wa Serikali ambao wanahusika katika kulipa mishahara hewa kwa watumishi ambao wameacha kazi, wamefariki, wamestaafu lakini ambao wanaendelea kulipwa mishahara kupitia akaunti zao za benki.
Rais pia ameiomba Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuisaidia Serikali katika kuboresha mfumo wa zabuni ambako Serikali inapoteza fedha nyingi kwa kupitia mchakato mrefu mno wa kupatikana kwa wazabuni wa kutoa vifaa na huduma kwa Serikali.
“Naagiza kuwa tutume ujumbe wenye nguvu za kutosha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Serikali,” Rais Kikwete ameviagiza vyombo vya Serikali baada ya kupokea Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Mwaka wa Fedha Unaoishia Juni 30, 2014 katika shughuli iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, leo, Ijumaa, Machi 27, 2015.
Rais Kikwete ametoa maagizo hayo baada ya kujulishwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad kuhusu nini ukaguzi wake umegundua kuhusu Usimamizi na Matumizi ya Fedha za Serikali.
Miongoni mwa mambo mengine, ukaguzi huo umebaini mapungufu mbali mbali katika usimamizi wa matumizi ya fedha za Serikali kama vile malipo yasiyokuwa na nyaraka, hati za malipo ambazo hazikuwasilishwa kwa ukaguzi, fedha iliyotumika nje ya Bajeti, matumizi yasiyokuwa na manufaa (nugatory expenditure) na malipo ambayo hayakuidhinishwa na maafisa masuuuli.
Profesa Assad amemweleza Rais Kikwete pia kuwa Ofisi yake inapendekeza kuwa taasisi zote za Serikali zisiendelee kununua vifaa na huduma kutoka kwa wafanyabiashara wasiotumia mashine za stakabadhi za kielektroniki (EDF), stakabadhi ya kukiri kupokea fedha.
Rais Kikwete ameagiza: “Kwa wale ambao wanatumia fedha za Serikali vibaya wachukuliwe hatua. Wenye ushahidi wa waziwazi wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Kwa wale ambao hakuna ushahidi wa kuweza kuwafikisha mahakamani lakini wamekula fedha za Serikali wachukuliwe hatua nyingine kama vile kuachishwa kazi kwa manufaa ya umma ama kushushwa vyeo ama kuchukuwa hatua nyingine za kiutawala.”
Kuhusu usimamizi wa rasilimali watu, Profesa Assad amemwambia Rais Kikwete: “Ukaguzi wangu pia umebaini kuwa mishahara ya watumishi waliocha kazi, waliofariki, waliostaafu wameendelea kulipwa mishahara kupitia akaunti zao. Vile vile, fedha za makato ya mishahara ya wafanyakazi hao zimeendelea kupelekwa kwenye taasisi husika kama vile Bima ya Taifa ya Afya, Mamlaka ya Mapato na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.”
Profesa Assad anasema kuwa tatizo hili linaendelea kuwepo hata kama linapungua kwa sababu ya mfumo wa udhibiti ambao Serikali imeanzisha na kuwa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, mwaka jana, 2014, kiasi cha Sh. Bilioni 141.4 zilitumika kulipa watumishi hao hewa.
CAG amewasilisha Ripoti yake kwa mujibu wa Ibara ya 143 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na pia kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008.
Profesa Assad amewasilisha Ripoti tano ambazo ni Ripoti ya Serikali Kuu, Ripoti ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Ripoti ya Mashirika ya Umma, Ripoti ya Miradi ya Maendeleo na Ripoti ya Ufanisi (Value for Money Audit).
Rais Kikwete amemshukuru Mkaguzi Mkuu na watumishi wengine wa CAG kwa kuwasilisha ripoti yenye ubora wa kiwango cha juu na ameahidi kuwa ataiwasilisha Ripoti hiyo Bungeni Jumatatu ya Machi 31 ili ipate kujadiliwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Machi,2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake, Rais Paul Kagame wa Rwanda, leo, Alhamisi, Machi 26, 2015, wametembelea Bandari ya Dar es Salaam na baadaye Rais Kagame ameanzisha safari ya treni maalum za kusafirisha mizigo ya Rwanda kutoka Tanzania.
Rais Kagame amewasili nchini asubuhi ya leo na kufungua Mkutano wa Wawekezaji katikaUjenzi wa Miundombinu Ukanda wa Kati (High Level Investors Forum – Central Corridor Development Acceleration Programme) uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.
Mara baada ya hotuba ya ufunguzi na kipindi cha maswali kutoka kwa washiriki na majibu kutoka kwa viongozi wa nchi tano zinazounda Shirika la Uwezeshaji wa Usafiri wa Ukanda wa Kati (The Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA), viongozi hao wawili wamekwenda Bandari ya Dar es Salaam.
CCTTFA lilianzishwa Septemba 2, mwaka 2006, na Makubaliano yaliyotiwa saini na nchi tano ambazo zinanufaika na usafiri wa Ukanda wa Kati – Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Rwanda na Uganda.
Katika Bandari ya Dar es Salaam, Rais Kagame na mwenyeji wake wameanza kwa kutembelea ofisi mpya za Mpango wa Ukusanyaji Ushuru kwa Pamoja (Single Customs Territory) miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mpango ulioanza kutumika Julai mwaka jana, 2014. Chini ya Mpango huo, kila nchi inashughulikia mizigo yake yenyewe, ikiwa ni pamoja na kukusanya kodi yake.
Rais Kagame na mwenyeji wake wametembelea ofisi za Mamlaka ya Kodi ya Rwanda (RRA) na Mamlaka ya Kodi ya DRC ambako walipewa maelezo kuhusu faida za mpango huo.
Miongoni mwa mambo mengine, marais hao walielezwa kuwa chini ya Mpango huo, waagizaji wa mizigo ya Rwanda, kupitia Bandari ya Dar es Salaam, sasa wanajaza fomu moja tu badala ya tatu na sasa mizigo ya Rwanda inachukua siku mbili tu kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Kigali, badala ya siku kati ya tano na 10 kabla ya kuanzishwa Mpango huo.
Nchi ambazo tayari zimefungua ofisi zao katika Bandari hiyo kutekeleza Mpango huo ni Tanzania yenyewe, Burundi, DRC na Rwanda. Uganda inakamilisha maandalizi ya utekelezaji na Zambia imeonyesha nia ya kujiunga na Mpango huo, kwa sababu inapitishia mizigo yake katika Bandari ya Dar es Salaam, hata kama siyo mwanachama wa EAC.
Kutoka kwa ofisi za Single Customs Territory, viongozi hao wamekwenda kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambako wamepatiwa maelezo kuhusu jinsi utendaji wa Bandari hiyo ulivyoboreka katika miaka miwili iliyopita.
Aidha, viongozi hao wameelezwa jinsi gani pia utendaji wa kampuni binafsi ya upakiaji na upakuaji mizigo ya TICTS inavyofanya kazi na ilivyoboresha utendaji wake katika sehemu nne za meli kutia nanga (berths) ambako inafanyia kazi yake katika Bandari hiyo yenye sehemu 11 za kupakia na kupakulia mizigo.
Katika Bandari hiyo, marais hao wameelezwa kuwa katika miaka mitano iliyopita, kiwango cha mizigo inayopitia katika Bandari hiyo kimekuwa kinaongezeka kwa wastani wa asilimia 12.8 kila mwaka.
Wameelezwa pia kuwa mwaka jana, kiasi cha tani milioni 14.6 ya mizigo kilipitia katika Bandari hiyo zikiwemo kontena 621,000 na kuwa kati ya mizigo hiyo kiasi cha asilimia 34, sawa na mizigo tani milioni 5.020 ilikuwa mizigo kwa ajili ya nchi za jirani.
Aidha, viongozi hao wameelezwa kuwa muda wa kontena kukaa Bandarini hapo sasa ni siku tisa tu badala ya siku 21 Februari mwaka 2008, muda wa meli kukaa nje ya Bandari ikisubiri kuingia Bandarini ili ipakuliwe, sasa ni siku moja unusu badala ya siku tatu unusu za mwaka 2013.
Marais Kagame na Kikwete pia wameelezwa kuwa usalama wa mizigo ya waagizaji sasa umeongezeka mno, kiasi cha kwamba halijakuwepo tukio hata moja la wizi wa mizigo ya wateja yakiwemo magari na spea zake kwa miaka mitatu mfululizo sasa.
Bandari ya Dar es Salaam ambayo huhudumia mizigo ya nchi saba – ya Tanzania yenyewe, Malawi, Zambia, DRC, Burundi, Rwanda na Uganda pia huendesha Bandari kwenye maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Jana, Jumatano, Machi 25, 2015, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi pamoja na wawakilishi wa nchi za DRC na Uganda pia walianzisha safari za treni za namna hiyo kwenda katika nchi zao.
Rais Kagame ameondoka nchini kurejea kwao leo baada ya kuanzisha safari hizo na mkutano wenyewe kuhusu Ukanda wa Kati, ambao pia ulihudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, umemalizika jioni ya leo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
26 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.
Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.
Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.
Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
- Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
- Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
- Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
- Mhe. Janet Zebedayo Mbene
- Mhe. Saada Salum Mkuya
- Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
- Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
- Mhe. James Fransis Mbatia
Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.
……………………………MWISHO……………………………….
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
26 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo wana wajibu wa kupunguza tofauti za usawa na kuongeza ushirikishaji wa maendeleo miongoni mwa nchi wanachama wa nchi hizo kama njia ya kuendeleza Jumuiya hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali ya baadaye ya Jumuiya hiyo itategemea jinsi gani wananchi wa nchi wanachama wanavyohisi wananufaika na kuwepo kwa Jumuiya hiyo na uanachama wao katika Jumuiya hiyo.
Rais Kikwete pia amewataka Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kushughulika na yale mambo ya Afrika Mashariki badala ya kila mbunge kushughulikia mambo ya nchi yake.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana, Alhamisi, Machi 19, 2015 wakati alipohutubia Bunge la Afrika Mashariki mwanzoni mwa kikao cha Bunge hilo katika Bunge la Burundi mjini Bujumbura ambako Rais Kikwete alizungumzia Hali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The State of EAC Address).
Katika hotuba iliyopokelewa kwa makofi ya mara kwa mara, Rais Kikwete amewaambia Wabunge hao kuwa hali ya baadaye ya Jumuiya itategemea mno ni jinsi gani nchi wanachama zinapunguza tofauti za usawa miongoni mwao na jinsi gani zinawashirikisha wananchi katika maendeleo ya pamoja.
“Sisi kama viongozi tusipolifanya hili, tutajikuta mahali ambako Jumuiya yetu inakufa tena, na kamwe hatutaki kuona Jumuiya hii inakufa kama ile ya zamani,” alisema Rais Kikwete.
Kuhusu jinsi gani wananchi wa EAC wanaikubali Jumuiya hiyo na ushirikishwaji wao katika masuala ya Jumuiya Rais Kikwete alisema: “Hali ya baadaye ya Jumuiya itategemea sana jinsi sisi viongozi tunavyofanikiwa kuwafanya wananchi hao kujiona na kujisikia kama wananufaika na Jumuiya yetu. Na hili haliweza kufanikiwa kwa sisi viongozi kusema kuwa Jumuiya imefanikiwa. Ni lazima wananchi wayaone na wayahisi mafanikio hayo.”
Rais Kikwete pia aliwamwagia sifa nyingi za utendaji Wabunge wa Afrika Mashariki lakini akaongeza: “Lazima muonekane mnatumia muda wenu mwingi kujadili na kufanya maamuzi kuhusu mambo yanayowahusu wananchi wa Afrika Mashariki na siyo vinginevyo. Lazima mtoe kipaumbele kwa mambo ambayo yanasura ya Afrika Mashariki kuliko mambo madogo madogo ya manufaa ya nchi zenu. Lazima tuone moyo wa uafrika mashariki ndani yenu na katika maamuzi yenu.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
20 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Serikali yaongeza kasi ya upatikanaji maji
- Miji ya Tabora, Nzega na Igunga kupatiwa maji ya Ziwa Victoria
- Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani nayo kuongezewa wingi wa maji
- Mipango imeanza kwa ajili ya miji ya Magu, Bariadi, Maswa, Kishapu na Mwanuhuzi kupata maji ya Ziwa Victoria pia
Serikali imekamilisha mipango ya kuvuta maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya wakazi wa mjini ya Tabora, Nzega na Igunga katika Mkoa wa Tabora.
Aidha, Serikali ya India imekubali kuipatia Tanzania dola za Marekani milioni 100 kwa ajili ya kuongeza maji katika Jiji la Dar Es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani, ambako kwa sasa unakamilishwa mradi mkubwa wa kuwaongezea maji wakazi wa jiji hilo.
Katika awamu nyingine ya uvutaji maji kutoka Ziwa Victoria, Serikali vile vile inakusudia kuanza mazungumzo na Serikali ya India kwa ajili ya kupatiwa mkopo ambao utapeleka maji katika miji ya Magu, Bariadi, Maswa, Kishapu na Mwanuhuzi katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu.
Mipango hiyo mikubwa mitatu ya kuongeza upatikana wa maji kwa wananchi ilielezwa wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kuzungumza na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umma la India ambalo linashughulikia miradi ya maji na umeme la WAPCOS.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa WAPCOS, Bwana R.K. Gupta amemweleza Rais Kikwete kuwa India imekubali kugharimia mradi huo na iko tayari kusaini mkataba na Tanzania ambako Serikali hiyo itatoa mkopo wa dola za Marekani zinazokaribia milioni 280 kwa ajili ya kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria kwenda mjini ya Tabora, Nzega na Igunga katika Mkoa wa Tabora.
Pamoja na kumshukuru binafsi Gupta na Serikali ya India kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali yake katika sekta ya maji, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania iko tayari wakati wowote kutia saini makubaliano ya kuwezesha kupatikana kwa fedha za kusambaza maji katika miji hiyo mitatu.
Uvutaji maji huo utakuwa ni awamu ya pili, baada ya Serikali kukamilisha uvutaji maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya wakazi wa mjini ya Shinyanga na Kahama ambao sasa wanapata maji safi na salama na kwa kiasi cha kutosheleza kutoka Ziwa hilo.
Rais Kikwete amemweleza Bwana Gupta kuwa pamoja na kwamba Serikali inakamilisha mradi mkubwa wa kuongeza upatikanaji maji katika mikoa wa Dar Es Salaam na Pwani, bado zinahitaji juhudi zaidi ili kuhakikisha kuwa wakazi wote wa Mikoa hiyo miwili wanaongezewa maji safi na salama.
Bwana Gupta amesema kuwa Serikali ya India iko tayari kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 100 ili kufanikisha ongezeko la maji katika maeneo hayo ya Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
Kuhusu miji ya Magu, Bariadi, Maswa, Kishapu na Mwanuhuzi, Gupta pia ameelezea utayari wa Serikali yake kutoa fedha za kujenga miundombinu ya kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika miji hiyo iliyoko Kanda ya Ziwa Victoria.
Bwana Gupta ameishauri Serikali ya Tanzania kuwasilisha ombi rasmi kwa Serikali ya India ambayo ameonyesha mwelekeo mkubwa kuwa inaweza kutoa fedha za kujenga miundombinu hiyo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
17 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
JK: Wasakeni na kuwarudisha shule watoto hawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kuwasaka na kuwarudisha shule kiasi cha wanafunzi 6,000 ambao wamefaulu kwenda sekondari mwaka huu, lakini hawako shule, na hawajulikani walipo.
Rais Kikwete alitoa maagizo hayo, jana, Machi 12, 2015 mjini Kahama alipopatiwa ripoti ya maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara yake maalum ya siku mbili kuwapa pole wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha usiku wa Machi 3, mwaka huu, na kusababisha vifo vya watu 47 na uharibifu mkubwa wa nyumba, mali na mazao katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Lufunga, alimwambia Rais Kikwete kuwa mwaka jana watoto 13,349 mkoani humo walishinda mtihani wa kuingia kidato cha kwanza lakini hadi Februari 29, mwaka huu, ni asilimia 56 ya watoto waliokuwa wamejiunga sekondari wakati asilimia 44, sawa na watoto 5,913, hawajaripoti shuleni na hawajulikani walipo pamoja na ukweli kuwa kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo Mkoa huo umefanya vizuri kitaaluma.
Rais Kikwete ameuagiza Mkoa huo kutumia sheria kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu wote, wakiwemo wazazi na walezi, ambao wanahusika na utoro wa watoto hao.
“Hawa ni watoto wengi sana na siyo jambo gumu kujua waliko. Hatuhitaji kujua sayansi ya kutengeneza roketi ama undani wa sayansi ya nyuklia kuwasaka na kuwapata watoto hawa. Shule walizosoma zinajulikana, walimu wakuu wa shule hizo wanajulikana, wenyeviti wa vijiji wanakoishi wanajulikana, wazazi wao wanajulikana …hawa wote watatoa habari walipo watoto hawa, tena katika muda mfupi tu wa wiki moja.”
Rais Kikwete ameongeza kuutaka uongozi wa Mkoa kutokutoa visingizio vya kuhalalisha kushindwa kupatikana kwa watoto hao: “Katika muda wa wiki moja, pateni taarifa za kila mtoto. Kama kuna wazazi wameoza watoto wa kike wabanwe na kurudisha ng’ombe wa mahari, kama kuna waliooa watoto hawa wa shule wakamatwe na kushitakiwa, kama watoto hawa wamekwenda kwenye machimbo wasakwe huko huko…watafuteni watarudi tu.”
Katika Mkoa wa Shinyanga, kama ilivyo katika mikoa karibu yote nchini, watoto wote ambao wanashinda mtihani wa kumaliza darasa la saba, wanapata nafasi ya kuingia sekondari kwa sababu ya upanuzi mkubwa wa elimu ya sekondari nchini na kuwepo kwa nafasi za kutosha kwa watoto wote wanaoshinda mtihani.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
13 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea tarehe 11 Machi, 2015 Mafinga katika Mkoa wa Iringa katika eneo lijulikanalo kwa jina la Changarawe, ambayo imepoteza uhai wa watu zaidi ya 40 waliokuwa wakisafiri kwa basi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi la Kampuni ya Majinja Express walilokuwa wakisafiria watu hao kutoka Mbeya kwendaDar es Salaamkugongana na lori lililokuwa likitokeaDar es Salaamkwenda Mbeya, hivyo kusababisha kontena lililokuwa limebebwa na lorihilokuliangukia basi.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kufuatia taarifa za vifo vya watu zaidi ya 40 huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika ajali hii mbaya ambayo imesababisha simanzi na majonzi makubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huu.
“Huu ni msiba mkubwa, na Taifa kwa ujumla limepata pigo kubwa, hivyo naomba upokee salamu zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hii iliyotokea Mkoani kwako. Naomba, kupitia kwako, rambirambi zangu na pole nyingi ziwafikie watu wote waliopotelewa ghafla na wapendwa wao. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho za Marehemu wote mahala pema peponi, Amina”, ameongeza kusema Rais Kikwete.
Katika Salamu zake hizo, Rais Kikwete amewahakikishia wafiwa wote kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa ndugu na jamaa zao, lakini amesema, pamoja na machungu yote ya kupotelewa na ndugu na jamaa zao, anawaomba wafiwa wawe na moyo wa uvumilivu na subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya wapendwa wao.
Aidha, Rais Kikwete amehitimisha rambirambi zake kwa kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema watu wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo wapone haraka, ili waweze kuungana tena na ndugu na jamaa zao.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi ya leo, Jumamosi, Machi 7, 2015, kwenda Kigali, Rwanda kwa ziara ya siku moja nchini humo kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame.
Wakati akiwa Kigali, miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini - Northern Corridor Integration Projects unaofanyika leo katika Hoteli ya Serena mjini Kigali.
Mkutano wa leo unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zimealikwa kuhudhuria mkutano huo.
Lengo la mkutano huo ni kujadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.
Rais Kikwete atarejea nchini jioni ya leo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
7 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali Nasoro Rufunga kuomboleza vifo vya watu 38 huku wengine 82 wakijeruhiwa usiku wa kuamkia tarehe 4 Machi, 2015.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika Kata ya Mwakata iliyoko katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali, hivyo kuathiri watu 3,500. katika Kata Mwakata iliyoathiriwa zaidi, kaya 350 zimeathiriwa katika Kijiji cha Makata wakati katika Kijiji cha Ngumbi, kaya 100 zimeathirika. Katika Kijiji cha Magung’hwa, kaya 50 zimeathiriwa..
“Nimepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 38 waliopoteza maisha na wengine 82 waliojeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa matibabu baada ya nyumba zao kusombwa kabisa na maji kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huo.
Rais Kikwete amesema msiba huo siyo wa Wana-Shinyanga pekee bali ni wa Taifa zima ambalo limepoteza nguvukazi muhimu kwa maendeleo yake na ustawi wa jamii ya Watanzania kwa ujumla.
“Naomba upokee Salamu zangu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kupotelewa ghafla na wananchi 38 kwa mara moja katika Mkoa wako. Kupitia kwako naomba Rambirambi zangu na Pole nyingi ziwafikie wafiwa wote kwa kuondokewa na wapendwa, ndugu na jamaa zao. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho za Marehemu wote Mahala Pema Peponi, Amina”, amezidi kuomboleza Rais Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete amewaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na subira wakati huu wa majonzi makubwa kwao wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao, lakini amewataka wasisahau ukweli kwamba kazi ya Mungu haina makosa. Aidha amewahakikishia wafiwa wote kuwa binafsi yuko pamoja nao katika kipindi chote cha kuomboleza msiba huu mkubwa kwao na kwa Taifa.
“Namwomba Mola awawezeshe majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao na kuendelea na maisha yao kama kawaida”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
04 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Serikali ya Tanzania inasikitishwa na kufedheheshwa sana na mauaji ya watu wenye Albino nchini na itafanya kila linalowezekana kukomesha mauaji haya.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo Ikulu Dar es Salaam alipokutana na viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Albino Tanzania, wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bwana Ernest Kimaya.
“Mauaji haya yanaisikitisha Serikali na kuifedhehesha sana, msidhani hatufanyi lolote, tunafanya juhudi kubwa na mbalimbali lakini imefikia wakati tuongeze juhudi hizo” Rais amesema
Katika kikao hicho viongozi wa watu wenye Albino nchini wamesoma risala ambayo imetoa kilio chao na mapendekezo yao kwa serikali na hatimaye ikaafikiwa kuwa na haja ya kuunda kamati ya pamoja ambayo itajumuisha Serikali, viongozi wa watu wenye Albino, viongozi wa waganga wa jadi na wadau wote wakuu katika suala hili ili kupata mapendekezo na mkakati wa pamoja ambao hatimaye mauaji haya kukomeshwa kabisa nchini Tanzania.
Rais Kikwete amesema mauaji ya watu wenye Albino hayafanywi na Serikali bali watu ambao wako katika jamii zetu kwa kushirikiana na waganga wa jadi na watu wengine wenye tamaa mbalimbali katika jamii hivyo ni lazima yakomeshwe.
“Kwenye familia, jamii na hatimaye vyombo vya ulinzi na usalama na hilo ndiyo jukumu kubwa ambalo Serikali inapaswa kulisimamia na tutalisimamia kwa ushirikiano wa pamoja”. Rais amesisitiza na kuongeza kuwa kamati hiyo ya pamoja itaweka mikakati ya kuwabaini wale wote wanaohusika kuanzia wakala, waganga na hatimaye wale wanaonufaika na viungo vya watu wenye Albino.
Rais Kikwete pia amesema Serikali itasaidia familia na wahanga wa vitendo vya mauaji kwa hali na mali ili waweze kujimudu na pia kuwapa ushauri nasaha ili kuondokana na majonzi yanayosababishwa na vitendo hivyo kwani vinawaletea waathirika na watu wanaoishi na Albino mfadhaiko na msongo wa mawazo katika jamii na hivyo kushindwa kuendelea na maisha yao ama kufanya shughuli zao za kila siku.
Katika kikao cha leo, viongozi wametoa kilio chao kwa serikali kuziangalia na kuzimulika taasisi zisizo za kiserikali ambazo pamoja na kujipambanua kuwa zinatetea haki za watu wenye Albino nchini bado hazina mkakati wa pamoja na hazipo wazi kwa walengwa hapa nchini.
Mapema leo asubuhi mara baada ya kufika Ikulu, kulitokea sintofahamu baina ya viongozi wa Chama cha Watu Wenye Albino na watu wasio wanachama kwa kile kilichoelezwa kuwa uongozi huo sio halali kwa vile muda wake umeshakwisha wa kukaa madarakani.
Hata hivyo Bw. Ernest Kimaya ameelezea masikitiko kwake kwa Rais na kuelezea kuwa uchaguzi haukuweza kufanyika kutokana na ukosefu wa fedha na wamemuomba Rais awasaidie kutimiza azma yao ya kuitisha mkutano na kuchagua viongozi wa Chama chao.
Kulingana na Bw. Kimaya wamepanga kufanya mkutano huo wa kuchagua viongozi katikati ya mwaka huu ambapo pia dunia itakua inaazimisha siku ya watu wenye Albino duniani.
Rais amekubali ombi hilo na hiyo itazungumzwa kwa urefu katika kamati ya pamoja ambayo inatarajiwa kuwa imekamilika wiki ijayo.
……………………MWISHO………………………………
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu –Dar es Salaam
5 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
RAIS KIKWETE AUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUMZIKA KEPTENI JOHN DAMIANO KOMBA KIJIJINI LITUHI LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Machi 3, 2015, ameungana na mamia ya waombolezaji kumzika Mbunge wa Jimbo la Nyasa na msanii mahiri wa muziki nchini, Mheshimiwa Kepteni John Damiano Komba, kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, akitokea Dar es Salaam, kiasi cha saa tano na robo asubuhi, Rais Kikwete amekwenda moja kwa moja Lituhi, karibu kiasi cha kilomita 140 kutoka mjini Songea, kwa ajili ya mazishi ya Mheshimiwa Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete amejiunga na waombolezaji akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kiasi cha saa tisa mchana kwa ajili ya mazishi ya mmoja wa wasanii ambao walijijengea heshima kubwa kwa nyimbo zake za uhamasishaji.
Wakati wa shughuli za mazishi ambazo kidini zimeongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga, waombolezaji walisomewa salamu za rambirambi ambazo zimetumwa na Rais wa Pili wa Malawi, Mheshimiwa Bakili Muluzi ambaye sasa amestaafu.
Katika salamu hizo, Mheshimiwa Muluzi amesema: “Nilimjua Komba kama rafiki na taarifa za kifo chake cha ghafla zimenistua sana.”
Mwili wa Marehemu Komba uliteremshwa kaburini saa 9:30 mchana huku ukishuhudiwa na mjane wa marehemu Salome Komba na watoto wake 11.
Rais Kikwete ameondoka Lituhi mara baada ya mazishi kurejea mjini Songea kumalizia ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Ruvuma.
Ends
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
3 Machi, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais Kikwete ateta na Watanzania waishio Zambia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa jana, Jumatano, Februari 25, 2015, amekutana na kuzungumza na mamia ya Watanzania waishio nchini Zambia, ikiwa sehemu ya ziara yake rasmi ya siku mbili ya Kiserikali katika nchi hiyo.
Rais Kikwete akifuatana na Mama Salma Kikwete alikutana na Watanzania hao usiku kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, ambako alipata nafasi ya kujibu maswali yao na kuelezea kwa undani mafanikio ya maendeleo ambayo yanaendelea kupatikana nchini.
Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa kwanza wa nje kualikwa kutembelea rasmi Zambia tokea Rais mpya wa nchi hiyo, Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu kushika madaraka ya dola mwezi uliopita, hatua inayoonyesha hali ya uhusiano mzuri katika ya nchi hizo mbili jirani na marafiki.
“Ukisoma magazeti yetu nchini na kufuatilia mijadala kwenye mitandao ya kijamii utadhani kuwa hakuna kinachofanyika na kuwa nchi nzima inaongelea katika siasa tu. Lakini tunaendelea kufanya mambo mengi iwe katika elimu, katika afya, kukabiliana na malaria na magonjwa wengine makubwa, kupambana na ukimwi, kusambaza umeme vijijini, mapambano dhidi ya ujambazi na majambazi, shughuli za miundombinu na ujenzi wa barabara pote tunafanya vizuri sana,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Wakati Serikali yangu inaingia madaraka ni asilimia 10 tu ya vijiji vyetu vilikuwa na umeme, sasa tunazungumzia asilimia 45 ya vijiji vya Tanzania vina umeme. Hapa tunazungumzia kiasi cha vijiji 5,000 kati ya vijiji 12,000 vya nchi yetu. Kwa ujumla, asilimia ya usambazaji umeme katika nchi yetu imepanda kutoka asilimia 10 ya mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 36 kwa sasa. Siyo mafanikio madogo hata kidogo.”
Kuhusu hali ya ujambazi nchini, Rais Kikwete amesema kuwa upo ujambazi katika Tanzania, kama ilivyo kwa nchi zote duniani. “Lakini, hawa tutapambana nao hawawezi kutushinda nguvu, tutazama nao na tutaibuka nao tu.”
Rais Kikwete pia ameelezea upanuzi mkubwa wa sekta ya elimu ikiwa ni elimu ya awali, ya sekondari na ya juu. “Katika elimu ya juu, kwa mfano, wakati tunaingia madarakani idadi ya wanafunzi katika vyuo vikuu vyote ilikuwa ni 40,000 tu lakini sasa tunazungumzia wanafunzi 200,000.”
Katika afya, Rais Kikwete ameelezea uboreshaji mkubwa wa hospitali za mikoa na ujenzi wa huduma nyingine za afya zikiwemo zahanati na vituo vya afya katika vijiji na kata nchini.
Aidha, Rais Kikwete amezungumzia hatua za kuongeza idadi ya madaktari nchini akisema kuwa kwa sasa idadi ya madaktari wapya kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili wameongezeka kutoka 200 hadi 400 kwa mwaka na kuwa idadi hiyo itakuwa kubwa zaidi wakati ujenzi wa Hospitali ya Mlongazila, nje tu ya Dar es Salaam, utakapokamilika.
Rais Kikwete pia alijibu maswali manane ya Watanzania hao ikiwa ni pamoja na lile kuhusu uraia pacha, misamaha ya kodi kwa Watanzania wanaorejea nyumbani, mikopo kwa wanafunzi wa kike wa Kitanzania ambao wanasomea masomo ya sayansi nje ya nchi, uwezekano wa Benki ya CRDB kufungua tawi katika Zambia, hatua za Serikali kupunguza idadi ya vizuizi vya barabarani, uwezekano wa Watanzania waishio nje kupata nafasi ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na jinsi gani Serikali ya Tanzania inaweza kuwasaidia Watanzania waishio Zambia kufanya shughuli zao kwa uhuru zaidi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Februari, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais Kikwete ameonyesha mfano wa mafanikio – Rais Lungu
Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu amesema kuwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika maendeleo ya Tanzania na amani ya Bara la Afrika ni mambo yasiyotiliwa shaka tena, akitamani naye apate mafanikio kama Rais Kikwete.
Aidha, Rais Lungu amesema kuwa Rais Kikwete ameonyesha kiwango kikubwa na cha juu cha uongozi, ambacho kinathibitishwa na aina ya mafanikio ambayo ameyaleta katika miaka yote ya uongozi wake.
Rais Lungu alifagilia na kusisitiza mafanikio hayo ya Rais Kikwete na uongozi wake kwa nyakati mbili tofauti jana, Jumatano, Februari 25, 2015, katika siku ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili ya Rais Kikwete nchini Zambia kwa mwaliko wa Rais Lungu.
“Nina mengi ya kujifunza kutoka kwa Mheshimiwa Kikwete ambaye kama mnavyojua anajiandaa kumaliza muda wake wa uongozi. Mimi bado mpya kabisa katika uongozi wa juu na hivyo nina mengi ya kujifunza kutoka kwake kwa sababu amefanikiwa sana katika uongozi wa nchi yake, “ Rais Lungu aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa na Rais Kikwete baada ya viongozi hao wawili kumaliza mazungumzo rasmi kati yao.
Akizungumza wakati wa dhifa ya taifa ambayo Rais Lungu alimwandalia Rais Kikwete kwenye Hoteli ya Taj Pamodzi mjini Lusaka, Rais Lungu alirudia kumpongeza na kumsifia Rais Kikwete kwa uongozi bora.
“Umeonyesha uongozi wa kutukuka sana ambao unathibitishwa na mafanikio makubwa katika miaka yote ya urais wako. Umeimarisha, umesimamia na kudumisha utawala bora, umepanua sana uhuru wa kila aina katika Tanzania ukiwemo uhuru wa vyombo vya habari. Tunakupongeza kwa mafanikio hayo na baadhi yetu tunaoanza uongozi tunatamani sana kufuata nyayo zao,” alisema Rais Lungu na kuongeza:
“Mchango wako katika kusaka amani katika Bara la Afrika ni jambo la kupongezwa sana na ni chimbuko la heshima kwetu sote na kwa Bara letu lote. Mchango wako katika maendeleo ya Tanzania na Bara la Afrika ni mambo yasiyotiliwa shaka na yoyote. Ni matumaini yangu na nataka kufuata nyayo za uongozi wako.”
Wakati wa dhifa hiyo, Baba wa Taifa la Zambia, Mzee Kenneth Kaunda alikunwa mno na muziki wa Malaika uliokuwa unatumbuizwa na bendi moja kiasi cha kuingia uwanjani na kumkaribisha Rais Kikwete pamoja na Rais Lungu uwanjani na kwa pamoja wakasakata rumba.
Rais Kikwete ambaye alikuwa Zambia kwa ziara rasmi kutokana na mwaliko wa Rais Lungu anakuwa kiongozi wa kwanza wa nje kutembelea Zambia rasmi tokea Rais Lungu ashike madaraka ya kuongoza Zambia mwezi uliopita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
Katika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe. DKT. STEPHEN JAMES BWANA, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na BWANA EDRISSA R. MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Mavura ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.
Sambamba na uteuzi huu, Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo, ambapo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ni:
(i) |
Bwana George D. YAMBESI, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. |
(ii) |
Alhaj Y. F. MBILA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.
|
(iii) |
Bwana Mgeni Mwalimu ALLY, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma iliyomaliza muda wake.
|
(iv) |
Bibi Adieu H. NYONDO, Mkurugenzi wa Maadili mstaafu.
|
(v) |
Bibi Salome S. MOLLEL, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu mstaafu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
|
(vi) |
Bibi Evelyne ITANISA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu. |
Aidha Makamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ni:
(i) |
Bwana Paul Herbert Kinemela, Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi na Ajira |
(ii) |
Bwana Mathias Bazi Kabunduguru, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
|
(iii) |
Bwana Njaa Ramadhani Kibwana, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU).
|
(iv) |
Bwana Jones Kyaruzi Majura, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Sekta ya Biashara na Viwanda – (TUICO).
|
(v) |
Bwana Jaffari Ally Omari, Mwanasheria Kiwanda cha Sukari – TPC, na Kamishna wa Tume iliyomaliza muda wake.
|
(vi) |
Bibi Suzane Charles Ndomba, Afisa Sheria wa ATE na Wakili wa Mahakama Kuu. |
Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2015.