Taarifa kwa vyombo vya Habari ya zamani
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Kikwete aanza ziara rasmi Vietnam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Hanoi asubuhi ya jana, Jumatatu, Oktoba 27, 2014 kuanza ziara rasmi ya siku mbili ya Kiserikali nchini Vietnam.
Rais Kikwete amewasili mjini Hanoi akitokea nchi jirani ya Jamhuri ya Watu wa China ambako Jumapili, Oktoba 26, 2014 alimaliza ziara rasmi ya Kiserikali yeye mafaniko makubwa ya siku sita nchini humo.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Noi Bai mjini Hanoi, Rais Kikwete amepokelewa na viongozi wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam na baada ya mapumziko mafupi, Rais Kikwete amekwenda Kasri ya Kirais kukutana na Rais Truong Tan Sang kwa mazungumzo ya faragha na baadaye kwa mazungumzo ya Serikali kati ya Tanzania na Vietnam.
Mara baada ya kuwasili kwenye Kasri hiyo, Rais alipokelewa na Rais Sang na akakagua gwaride la heshima ambalo liliundwa na Jeshi la nchi hiyo lililokuwa na vikosi vya anga, maji na nchi kavu.
Baada ya mazungumzo hayo, Marais hao wawili wameshuhudia utiaji saini wa Makubaliano katika Usafiri wa Majini (Marine Transport) ambao umetiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe kwa niaba ya Tanzania na Waziri wa Usafirishaji wa Vietnam, Mheshimiwa Dinh Li Thang kwa niaba ya nchi yake.
\
Mbali na kukutana na Rais Sang, Rais Kikwete baadaye amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, Mheshimiwa Nguyen Phu Trong, ambaye pia ndiye kiongozi mkuu wa nchi hiyo. Viongozi hao wawili wamekutana kwenye Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho cha Kikomunisti, yanayoangaliana na Kasri ya Rais.
Rais Kikwete pia amefanya ziara kwenye Makao Makuu ya Kampuni ya Simu ya Viettel ambayo inajiandaa kuingia katika soko la vijijini katika Tanzania. Wakati wa mazungumzo kati ya Rais Kikwete na viongozi wa Kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki ameukabidhi uongozi wa Kampuni hiyo hati ya kuanzishwa kwa Kituo hicho.
Baadaye usiku, Rais Kikwete amehudhuria Hafla ya Chakula cha Jioni iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rais Sang kwenye Kituo cha Kimataifa cha International Convention Centre mjini Hanoi. Rais Kikwete ataendelea na ziara yake ya Vietnam leo kwa kutembelea sehemu mbali mbali na kukutana na Spika wa Bunge la Vietnam, Mheshimiwa Nguyen Sinh Hung.
Hiyo ni ziara ya kwanza kufanywa na Mheshimiwa Kikwete akiwa Rais wa Tanzania, lakini hiyo ni mara ya pili kwake kutembelea Vietnam. Alitembelea Vietnam mwaka 2004, akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
28 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kila Mtanzania kupata simu ya kisasa bure
Kila Mtanzania nchini atakuwa na uwezo wa kupata simu ya kisasa na yenye uwezo mkubwa (smart phone) kwa bei ya chini kabisa katika miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2020 kwa mujibu wa mipango ya kampuni mpya ya simu inayojiandaa kuingia katika soko la simu la Tanzania.
Aidha, Kampuni ya Viettel ya Vietnam imemwambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Oktoba 27, mwaka huu, 2014 kuwa itateremsha kwa kiasi kikubwa bei ya simu za kawaida na smart phone, ili kuwezesha kila Mtanzania kuwa na simu.
Kampuni hiyo pia imemwambia Rais Kikwete kuwa itasambaza mawasiliano ya internet kwa kila kijiji nchini na kuwa kwa taasisi za umma kama vile shule, hospitali, vituo vya polisi zitapatiwa huduma hiyo bila malipo yoyote.
Rais Kikwete ameambiwa habari hiyo njema kwa Watanzania na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu ya Viettel wakati alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo mjini Hanoi kwenye siku yake ya kwanza ya ziara yake rasmi ya Kiserikali katika Vietnam.
Mwenyekiti wa Kampuni hiyo ya umma ambayo inamilikiwa na Jeshi la Vietnam, Bwana Nguyen Manh Hung amemwambia Rais Kikwete kuwa Viettel inakusudia kumwezesha kila Mtanzania kumiliki smart phone kwa kupunguza bei ya simu hiyo na pia kupunguza bei ya huduma muhimu kama vile ile ya internet.
Bwana Hung amesema kuwa Kampuni yake inapanga kupunguza bei ya simu za kawaida hadi kufikia dola za Marekani 15, sawa na shilingi 25,000 na punguza ile bei ya smart phone hadi kufikia dola za Marekani 40, sawa na shilingi 65,000. S asa hivi, bei ya simu hizo ni kubwa mara nyingi ya kisai hicho kinachokusudiwa.
“Tunataka kuifanya bei ya kununua smart phone kuwa mara 10 chini ya bei ya kununua kompyuta. Tunasukudia pia kupunguza bei ya matumizi ya simu kuwa dola moja tu ya Marekani, sawa na shilingi 1,600, kwa watu wa kawaida kwa mwezi na kwa wale ambao wanatumia simu kwa huduma nyingi zaidi watalipa dola za Merakani 50, sawa na shilingi 78,000, kwa mwezi,” amesema Bwana Hung.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa Kampuni yake itawekeza kiasi cha dola za Marekani bilioni moja katika huduma za simu na huduma nyingine katika Tanzania na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili nyuma ya Peru kupata mfumo wa simu wa kisasa zaidi miongoni mwa nchi ambako Kampuni hiyo ina shughuli zake.
Amesema kuwa ndani ya miaka mitatu tokea Kampuni hiyo kuanza shughuli zake katika Tanzania, kiasi cha vijiji 4,000 ambavyo kwa sasa havina mawasiliano vitapatiwa huduma hiyo katika awamu ya kwanza.
“Katika awamu ya pili, kiasi chavituo 150 vya polisi, hospitali za umma 150, ofisi za Shirika la Posta kiasi cha 65 nchini vitapatiwa huduma ya mawasiliamo yakiwemo ya internet bure katika mwaka wa kwanza wa Kampuni hiyo kuanza shughuli zake. Tutatoa pia huduma ya internet na mfumo wa teknolojia ya mawasiliano bure kwa shule 450 za umma katika wilaya 150 ambazo tayari zina umeme, huduma ambazo pia zitatolewa katika mwaka wa kwanza wa Kampuni hiyo kuanza kazi,” amesema.
Bwana Hung amesema kuwa Kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1989 iliingia katika shughuli za simu mwaka 2000 na kuanza shughuli za simu za mkononi mwaka 2004.
Mwaka jana, mapato ya kampuni hiyo yalikuwa ni dola za Marekani bilioni 9.1 na kati ya hizo kampuni hiyo ilikuwa imepata faida ya karibu dola za Marekani bilioni moja.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
28 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya habari
Hati ya ujenzi wa Bagamoyo yatiwa saini China
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taasisi mbili kubwa za kimataifa jana, Jumapili, Oktoba 26, 2014, zilitiliana saini Hati ya Makubaliano (MOU) ya kuendeleza kwa pamoja Eneo la Kiuchumi la Bagamoyo ambako pia itajengwa bandari kubwa ya Bagamoyo ambayo inatarajiwa kutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania.
Pande hizo tatu ambazo ni pamoja na Kampuni ya Uendeshaji Bandari ya China Merchant Holding International (CMHI) ya Jamhuri ya Watu wa China na Mfuko wa Uwekezaji wa Oman wa State General Reserve Fund of Oman ya Oman zimetilia saini Hati hiyo kwenye sherehe iliyofanyika katika Hoteli ya Hilton Shenzhen Shekou Nahai ya mjini Shenzhen, Kusini mwa China.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ametembelea Jimbo la Guang Dong ambako liko Eneo la Uwekezaji wa Kiuchumi la Shenzhen alishuhudia utiaji saini huo ambao kwa upande wa Tanzania saini ilitiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servicus Likwelile.
Chini ya Hati hiyo ya uendelezaji wa Eneo la Uwekezaji la Bagamoyo litaanza kujengwa Julai Mosi mwakani, 2015.
Kabla ya sherehe hiyo ya kutiliana saini Hati ya Makubaliano, Rais Kikwete ametembelea Eneo la Kontena la Bandari ya Shenzhen ambako alionyeshwa vifaa vya kisasa kabisa vya kupakia na kupakulia kontena kazi inayofanywa na CMHI ambayo ina uzoefu wa miaka 140 wa uendeshaji wa bandari.
Akizungumza katika sherehe hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake imedhamiria kuhakikisha kuwa mradi huo wa mamilioni ya fedha wa Bangamoyo unaanza. “Tutafanya lolote linalowezekana kuhakikisha kuwa mradi huu unaanza kwa sababu utaleta neema kubwa ya kiuchumi kwa nchi nzima.”
Naye Mwenyekiti wa CMHI, Bwana Li Jianhong ameitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kumaliza vikwazo vyote ambavyo vimechelewesha kuanzishwa kwa mradi huo ili uweze kuanza Julai Mosi, mwakani, kama ilivyokubaliwa.
Mapema leo akiwa Shenzhen, Rais Kikwete ametembelea makao makuu ya Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Hauwei Technologies inayoajiri maelfu ya watu duniani, ikiwemo Tanzania, na kutengeneza mamilioni ya faida.
Aidha, Rais Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Manispaa ya Shenzhen ambayo yalifanyika kwenye hoteli ambako alifikia Rais Kikwete katika ziara yake ya Shenzhen ya Shenzhen Wazhou Guest Hotel ambayo ni mali ya Serikali ya China.
Rais pia ametembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya ZTE iliyoko mjini Shenzhen ambayo inaendesha shughuli zake Tanzania na inaajiri wafanyakazi 60,000 dunia nzima.
Rais Kikwete amemaliza ziara ya China jana, naleo, Jumatatu, Oktoba 27, anaanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika Vietnam.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya habari
JK Rais wa kwanza kupokelewa kwa pikipiki China kwa miaka 10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesababisha mageuzi makubwa kwa namna Jamhuri ya Watu wa China inavyowapokea viongozi wageni kutoka nje kwa kuwa kiongozi wa kwanza duniani kupokewa rasmi na pikipiki za polisi na kuongozwa na pikipiki hizo kwa muda wote wa ziara katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Rais Kikwete ambaye aliwasili nchini China Jumanne iliyopita, Oktoba 21, 2014, kuanza ziara rasmi ya siku sita nchini humo, amekuwa kiongozi wa kwanza wa nje kupokelewa na msafara wa pikipiki tokea Januari Mosi, mwaka 2004, miaka 10 iliyopita wakati China ilipofuta utaratibu wa misafara ya viongozi kusindikizwa na pikipiki za polisi.
Rais Kikwete na msafara wake alipokewa na msafara wa pikipiki wa polisi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Beijing hadi kwenye Nyumba ya Kufikia Wageni wa Serikali ya Diaoyutai, katikati ya Jiji la Beijing na utaratibu huo kuendelea kuongoza msafara wake kwa siku zote alipokuwa China.
Taarifa ya habari iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China na kukaririwa na Shirika la Habari la nchi hiyo la Xinhua haikutoa sababu zozote za mabadiliko ya sera hiyo.
Katika nchi karibu zote duniani, utaratibu wa viongozi wa nchi mbali mbali kupokelewa kwa misafara ya pikipiki ni protokali ya juu kabisa ambayo pia huongeza usalama wa kiongozi na ni utaratibu wa kawaida katika nchi nyingi duniani.
Tokea kuasisiwa kwake mwaka 1949, Jamhuri ya Watu wa China ilikuwa na utaratibu wa pikipiki za polisi kuongoza misafara ya viongozi lakini utaratibu huo ulisimamishwa Januari Mosi, mwaka 2004, kwa sababu ambazo hazijapata kuelezwa.
Baada ya kuweka historia hiyo ya kuwa kiongozi wa kwanza wa nchi ya kigeni kupokelewa na msafara wake kuongozwa na msururu wa pikipiki nane, Rais Kikwete anatarajiwa kuondoka China leo, Jumatatu, Oktoba 27, 2014, baada ya kuwa amemaliza ziara yake rasmi.
Rais Kikwete anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika Vietnam kwa mwaliko wa Mheshimiwa Truong Tan Sang, Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam ambako miogoni mwa mambo mengine nchi hizo mbili zitaadhmisha miaka 50 tokea kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.
Miongoni mwa shughuli zake kubwa, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, Mheshimiwa Nguyen Phu Trong na Mwenyekiti wa Bunge la Vietnam, Mheshimiwa Nguyen Sinh Hung.
Aidha, Mheshimiwa Rais atatembelea taasisi mbalimbali zenye uhusiano wa kiuchumi na Tanzania ikiwemo Kampuni ya Viettel inayotaka kuwekeza katika mawasiliano ya simu za maeneo ya vijijini katika Tanzania kwa bei nafuu zaidi.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzania yaomba madaktari zaidi kutoka China
- Imekuwa inapokea madaktari kutoka China kwa miaka 46
- Yashukuru kwa kujengewa Hospitali ya magonjwa ya moyo Muhimbili
Tanzania imeiomba Jamhuri ya Watu wa China kuongeza idadi ya madaktari wake inaowatuma Tanzania kama msaada kutoa huduma ya tiba kama njia ya kuzidi kusaidia kukabiliana na upungufu wa madaktari nchini.
Aidha, Tanzania imeishukuru China kwa kujenga hospitali kubwa inayoweza kulaza wagonjwa 100 kwa wakati mmoja wa magonjwa ya moyo na yenye uwezo wa kuwafanyia wagonjwa wa moyo operesheni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa ombi hilo na shukurani hizo leo, Jumamosi, Oktoba 25, 2014 wakati alipokutana na kuzungumza na Mheshimiwa Jiang Yikang, Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) cha Jimbo la Shandong, jimbo ambalo tokea mwaka 1968 limekuwa linatuma madaktari kutoka jimbo hilo kuja nchini kusaidia kutoa huduma ya tiba.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara rasmi ya Kiserikali katika China amesimama kwa siku nzima katika mji mkuu wa Jimbo la Shandong wa Jinan akiwa njiani kutoka Beijing kwenda Jimbo la Shenzhen ambako atafanya ziara kesho, Jumapili,Oktoba 26.
Rais Kikwete na ujumbe wake ambaye amesafiri kwa treni iendayo kasi kutoka Beijing, amewasili kwenye Kituo cha Treni cha Jinan Magharibi kiasi cha saa 5:53 na kupokelewa na viongozi wa Serikali na wa CPC wa Jimbo hilo, siyo mbali na nchi jirani ya Korea kusini.
Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Yikang: “Tunalishukuru sana Jimbo la Shandong ambalo kwa miaka 46 tokea mwaka 1968 limekuwa linatuma madaktari wake kuja Tanzania kutoa huduma ya tiba kwa msaada. Tumepokea makundi 23 ya madaktari zaidi ya 1,000 ambao huja kila baada ya miaka miwili. Tunalishukuru sana Jimbo hilo kwa msaada huu mkubwa.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Lakini bado tunazidi kuwaomba muendelee kutusaidia. Tunahitaji madaktari wengi zaidi kwa sababu uwiano kati ya daktari na wagonjwa nchini kwetu bado ni mkubwa. Katika mazungumzo yangu na Rais Xi Jinping jana nilitoa ombi hili, lakini nalitoa tena hapa kwa sababu madaktari wanatoka Jimbo hili.”
Rais Kikwete pia amelishukuru Jimbo hilo kwa msaada uliowezesha kujengwa kwa Hospitali ya Moyo kwenye Hospitali Kuu ya Taifa ya Muhimbili, Dar Es Salaam. “Hospitali hii ya kisasa kabisa sasa imeanza kufanya kazi. Imeiweka nchi yetu kwenye ngazi tofauti kabisa. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuuunga mkono.”
Jimbo la Shandong ni la tatu kwa utajiri na uchumi imara katika China ambalo pato lake mwaka jana lilikuwa ni dola za Marekani bilioni 882.9 kiasi kikubwa kuliko nchi nyingi za Afrika zikiwekwa kwa pamoja. Thamani ya biashara kati ya Jimbo hilo na Tanzania kwa mwaka jana ilikuwa dola za Marekani milioni 470.
Baadaye jioni, Rais Kikwete alikutana na baadhi ya madakati waliopata kufanya kazi katika Tanzania na akawashukuru kwa mchango wao katika maendeleo ya huduma ya tiba nchini.
Amewaambia madaktari hao kwenye Hospitali Kuu ya Jimbo la Shandong: “Nimeomba niwaone ili niwashukuru sana kwa kuokoa maisha ya watu wetu. Mnashikilia nafasi ya pekee katika mioyo ya Watanzania. Kama mnavyojua fika, madaktari wa Shandong wamekuwa wanatusaidia katika Tanzania tokea 1968 na mpaka sasa kiasi cha madaktari 1223 wametusaidia. Kuna wakati lilikuja hapa kundi kubwa la madaktari 84 kwa wakati mmoja. Nyie mnajua Kiswahili – Nasema asanteni sana.”
Hospitali hiyo ni moja ya hospitali za Jimbo hilo ambazo zimekuwa zinapeleka madaktari wake Tanzania tokea mwaka 1968. Mwaka huo, hospitali hiyo iliweka katika kundi la madaktari waliokwenda Tanzania madaktari wake wanne.
Katika miaka yote 46, Hospitali hiyo imepeleka Tanzania madaktari 70 na kwa sababu ya kazi hiyo nzuri Mei mwaka 2004, Rais Benjamin William Mkapa aliitembelea Hospitali hiyo, akakutana na kuwashukuru madaktari waliokuwa wametoa ujuzi wao kuokoa maisha ya Watanzania. Hospitali hiyo iliyoanzishwa mwaka 1897, ina historia ya miaka 117 ya kutoa huduma za tiba.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ametembelea Kampuni ya Kompyuta ya Inspur iliyoko mjini Jinan na baada ya kutembelea Kampuni hiyo ameondoka mjini Jinan kwenda mji wa Shenzhen ambako atafanya ziara ya siku mbili kuanzia baadaye leo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Oktoba, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
China yatangaza mamilioni zaidi kubabiliana na Ebola
Jamhuri ya Watu wa China Ijumaa, Oktoba 24, 2014 imetangaza kuwa kwa mara ya nne katika kipindi kifupi inapeleka msaada wa dawa, vifaa na mahitaji mengine ya tiba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 85 kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zinapambana na ugonjwa huo ambao mpaka sasa umeua zaidi ya watu 4,000.
Aidha, China imetangaza kuwa itajenga kituo kikubwa cha afya na tiba katika nchi ya Liberia kama sehemu ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Msaada huo mwingine wa China umetangazwa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa XI Jinping katika mazungumzo yake rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye The Great Hall of the People mjini Beijing ikiwa ni sehemu ya ziara rasmi ya Rais Kikwete, Rais Jinping amesema: “Hali katika Afrika sasa ni ya utulivu lakini yapo matishio ya mara kwa mara mengine ya ndani ya Afrika na mengine ya nje na mojawapo ya matishio hayo ni ugonjwa wa Ebola.”
Ameongeza Rais Jinping: “Mpaka sasa, Jamhuri ya Watu wa China imetuma misaada ya dawa na raslimali nyingine mara tatu kwa nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zinakabiliana na ugonjwa wa Ebola. Napenda kutangaza leo kuwa China, kwa mara nyingine, imeamua kupeleka msaada mwingine wenye thamani ya RMB 500 ikiwa ni fedha taslim, wataalam wa afya,wataalam wengine na raslimali nyingine.”
Ameongeza Rais Jinping: “China pia itajenga kituo kikubwa cha afya na tiba ili kiweze kusaidia nchi zote tatu ambazo zinakumbwa na ugonjwa huo wa Ebola Liberia, Guinea na Sierra Leone. Tunaungana na wananchi wa nchi hizo tatu katika kubaliana na tishio hili kubwa ambalo kwa hakika linahitaji ushirikiano wa dunia nzima.”
Rais Kikwete ambaye anaendelea na ziara yake katika China mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la China la National People's Congress, Mheshimiwa Zhang Deajing.
Aidha, Rais Kikwete amekutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa China, Mheshimiwa Li Keqiang.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
24 Oktoba, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
China yamwaga neema kubwa kwa Tanzania
Jamhuri ya Watu wa China leo, Ijumaa, Oktoba 24, 2014, imetangaza neema kubwa kwa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa dola za Marekani milioni 85 kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuisaidia Tanzania kufanya mageuzi ya viwanda.
Neema hiyo ya China kwa Tanzania imetangazwa na Rais Xi Jinping wa nchi hiyo katika mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati yake na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye yuko katika ziara rasmi ya siku sita katika China.
Mazungumzo hayo kwenye Jumba la The Great Hall of the People yamefanyika baada ya Rais Kikwete kukaribishwa rasmi katika Jamhuri ya Watu wa China kwa kupokelewa na Rais Xi Jinping katika eneo la East Plaza ya Jumba hilo.
Katika mapokezi hayo ya kuvutia na kusisimua, Rais Kikwete amepigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la ukakamavu la Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China la People’s Liberation Army.
Katika mazungumzo hayo, Rais Xi Jinping alitangaza kuwa China itaipatia Tanzania kiasi cha dola milioni 85 ikiwa ni mchanganyiko wa msaada na mkopo usiokuwa na riba, fedha ambazo Tanzania itaamua yenyewe jinsi gani ya kuzitumia.
“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kuboresha maisha ya wananchi wake, napenda kutangaza kuwa Jamhuri ya Watu wa China itatoa kiasi cha RMB milioni 200 ikiwa ni msaada na RMB 200 milioni nyingine zikiwa ni mkopo usiokuwa na riba kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiasi cha RMB 100 milioni za msaada kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zitatumika kwa kadri Serikali hizo mbili zitakavyoamua,” amesema Rais Jinping.
Rais huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi hiyo itaisaidia Tanzania katika uendelezaji wa maeneo ya uwekezaji ya EPZ, uendelezaji wa miundombinu, itaharakisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na itaingia katika shughuli za kutafuta gesi na mafuta katika ukanda wa Bahari ya Hindi katika eneo la Tanzania.
Rais Jinping pia ametangaza kuwa Serikali ya China imefanya uamuzi wa kuikarabati Reli ya Uhuru ya TAZARA inayounganisha Tanzania na Zambia na yenye urefu wa kilomita 1,860 na kusaidia uendeshaji wa reli hiyo. “Ili kutekeleza uamuzi huu kwa haraka, napendekeza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya wataalam kuandaa ramani ya namna ya kuitoa reli hiyo katika matatizo yake ya sasa.”
TAZARA ndiyo reli ya kwanza duniani kujengwa na Jamhuri ya Watu wa China ambao utaalamu wake sasa unasakwa na nchi nyingine nyingi duniani.
Rais Jinping pia ametangaza kuwa Serikali yake itatoa nafasi 100 za masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi kutoka Tanzania katika miaka mitano ijayo, itaongeza idadi ya madaktari ambao China inapeleka Tanzania, itahimiza makampuni zaidi ya China kuwekeza katika Uchumi wa Tanzania na kuzishawishi taasisi za kifedha za China kuanzisha shughuli zake katika Tanzania.
Kiongozi huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi yake itajenga chuo kikubwa cha mafunzo ya ufundi katika Tanzania na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika eneo la uimarishaji wa ulinzi na usalama.
Rais Jinping amesema kuwa urafiki na uhusiano kati ya China na Tanzania ni mfano unaong’ara wa uhusiano mzuri na mwema duniani na kuwa China iko tayari kutoa uzoefu wake wa maendeleo kwa Tanzania bila wasiwasi wowote.
Rais Kikwete amemshukuru sana Rais Jinping na Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada yake ambayo baadhi yake haikutarajiwa
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Oktoba, 2014.
taarifa kwa Vyombo vya habari
Makubaliano ya mabilioni ya fedha yatiwa saini kati ya Tanzania na China
Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China leo, Alhamisi, Oktoba 23, 2014, zimetiliana saini Hati za Makubaliano (Memorandum of Undestanding) ambako taasisi za China zitawekeza mabilioni ya dola za Marekani katika uchumi wa Tanzania.
Shughuli hiyo ya utiaji saini imekuwa sehemu ya Mkutano wa Tatu wa Uwekezaji Kati ya Tanzania na China uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Nyumba ya Kufikia Wageni wa Serikali ya Diaoyutai mjini Beijing, China.
Aidha, utiaji saini huo ambao utaziwezesha taasisi kadhaa za Tanzania kunufaika na mitaji na uwekezaji kutoka China ulikuwa sehemu ya ziara rasmi ya Kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping. Rais Kikwete ameshuhudia shughuli hiyo ya utiaji saini.
Miongoni mwa Makubaliano yaliyotiwa saini ni pamoja na Makubaliano ya Ushirikiano wa Kimkakati kati ya Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) na Kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE) ambako kiasi cha dola bilioni moja unusu zitawekezwa katika uchumi wa Tanzania.
Kiasi cha dola bilioni moja zitawekezwa katika ujenzi wa mji mpya wa Salama Creek Satellite, eneo la Uvumba, Wilaya yaTemeke, Dar es Salaam na kiasi cha dola milioni 500 zitawekezwa katika ujenzi wa Financial Square, eneo la Upanga.
Aidha, NHC itapata kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kutoka Kampuni ya Poly Technologies kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Valhalla, eneo la Masaki, Dar es Salaam.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pia limetiliana saini Makubaliano na Kampuni ya Hengyang Transformer ambako Kampuni hiyo ya Tanzania itapata mamilioni ya dola za Marekani kwa ajili ta mradi wa kusambaza umeme vijijini.
Aidha, Shirika hilo la TANESCO limetiliana saini Makubaliano ya ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Kinyerezi IV.
Halmashauri ya Manispaaa ya Temeke, Dar es Salaam imetiliana saini Makubaliano na Kampuni ya Jiangyin Tianhe Gasses Group ya ujenzi wa barabara ya lami ya Kikwete Friendship Highway katika Wilaya ya Temeke. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Saidi Mecky Sadiq na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Sofia Mjema wameshuhudia utiaji saini Makubaliano hayo.
Vile vile, Mkoa wa Pwani, umetiliana saini Makubaliano na Kampuni ya Jiansu Shenli Plastics Gropu Limited ya China kwa ajili ya kugharimia na kuendeleza Mradi wa Viwanda na Uchumi katika eneo la Mlandizi. Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mama Mwantumu Bakari Mahiza ametia saini kwa niaba ya Mkoa wake.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya habari
Kiwango cha uwekezaji wa China kinavutia – Rais Kikwete
- Miradi ya makampuni kutoka nchini humo yafikia 522
- Ina thamani ya dola za Marekani bilioni mbili unusu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anafurahishwa na kiwango cha uwekezaji wa makampuni ya Jamhuri ya Watu wa China katika uchumi wa Tanzania ambao hadi mwishoni mwa mwaka jana ulikuwa umefikia miradi 522 yenye thamani ya dola za Marekani 2,490.21 milioni (dola bilioni 2.5).
Rais Kikwete amesema kuwa kiwango hicho kinaufanya uwekezaji wa China katika Tanzania kushika nafasi ya tano, kwa thamani ya fedha, na kuwa uwekezaji huo utaiwezesha Tanzania kupata ajira 77,335 baada ya kukamilika kwa miradi yote kukamilika ambayo ujenzi wake unaendelea.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa uzuri wa uwekezaji huo kutoka China ni kwamba miradi mingi, 354 kati ya miradi hiyo yote 522 ya wafanyabiashara kutoka China ni kwenye sekta ya uzalishaji.
Rais Kikwete amesema hayo leo, Alhamisi, Oktoba 23, 2014, wakati alipofungua Mkutano wa Tatu wa Uwekezaji wa Tanzania na China (Third Tanzania-China Investment Forum) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Nyumba ya Kulala Wageni ya Serikali ya Diaoyutai mjini Beijing, China ambako Rais anafanya ziara ya Kiserikali.
Akizungumza na mamia kwa mamia ya wafanyabiashara ambao walijaa kwenye ukumbi huo, Rais Kikwete amesema kuwa uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China umekua mno kiasi cha kwamba kati ya Julai na Septemba mwaka huu, 2014, thamani ya miradi imefikia dola za Marekani milioni 533.9 kulinganisha na miradi yenye thamani ya dola za Marekani 124.14 kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka jana.
Rais Kikwete amesema kuwa ongezeko hilo lilifuatia kufanyika kwa Mkutano wa Pili wa Uwekezaji Kati ya Tanzania na China uliofanyika Dar Es Salaam Juni 23 hadi 25, mwaka huu, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa China katika Tanzania, Mheshimiwa Li Yuanchao ambaye aliambatana na wafanyabiashara 100.
Rais Kikwete amesema pia kuwa biashara kati ya Tanzania na China imeongezeka lakini kwa kutilia maanani ukubwa wa uchumi wa China ambao ni wa pili duniani kwa ukubwa, bado biashara hiyo inaweza kukua zaidi.
“Kwa mwaka 2012/2013, kwa mfano, biashara kati ya nchi hizo ilikuwa na thamani ya dola za Marekani 1,595.16. Kati ya hizo, mauzo ya bidhaa za China kwa Tanzania zilikuwa sawa na dola 1,099.42 wakati China ilinunua kutoka Tanzania bidhaa zenye thamani ya dola milioni 495.74. Lakini ni dhahiri kuwa tunaweza kufanya vizuri,” alisema Rais Kikwete.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa katika enzi za sasa za Utawala Bora bado baadhi ya Serikali na viongozi wa Afrika bado wanaua na kutesa raia wao kwa kisingizio kuwa Utawala Bora siyo mfumo wa Kiafrika.
Rais Kikwete pia amesema kuwa Mpango wa Nchi za Afrika Kujithamini Kuhusu Utawala Bora (APRM) ni mfumo mzuri sana ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha udikteta katika Bara la Afrika.
Rais Kikwete alikuwa anazungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China kwenye siku yake ya pili ya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku sita katika China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping.
Katika mkutano huo uliofanyika jana, Jumatano, Oktoba 22, 2014, kwenye Nyumba ya Kufikia Wageni wa Serikali ya Diaoyutai mjini Beijing, ambako Mheshimiwa amefikia wakati wa ziara hiyo, Rais Kikwete aliulizwa kuhusu manufaa ya APRM na kama mfumo huo umekuwa wa manufaa kwa nchi za Afrika.
Akijibu swali hilo ambalo liliulizwa na Mheshimiwa Balozi SolaOnadipe, Naibu Balozi wa Nigeria katika China, Rais Kikwete amesema kuwa mfumo wa APRM umekuwa wa manufaa makubwa kwa Bara la Afrika na hasa kwenye mifumo ya Utawala Bora wa nchi za Afrika.
“APRM ni chombo murua sana. Kimesaidia sana kuboresha mifumo yetu ya Utawala Bora, hata kama bado wapo watu wanaosema kuwa APRM na falsafa yake ni jambo la Wazungu jambo ambalo siyo la kweli kwa kutilia maanani faida za mfumo huu wa kujithamini wenyewe” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Hivi tunahitaji Wazungu kuja kutufundisha kuwa ni jambo baya kuua raia wako? Unahitaji Mzungu aje kukuambia kuwa ni jambo baya kufanya ukatili na unyama wananchi wako? Je sisi Waafrika tunahitaji Wazungu watuambie kuwa ni jambo baya kuwaswaga wananchi wako kwa udikteta? Je tunahitaji watu wa nje kutuhubiria faida za Utawala Bora?”
Rais Kikwete amesema kuwa mageuzi na mabadiliko ya kidemokrasia katika nchi za Afrika ni jambo zuri na ni jambo la lazima na kuwa viongozi wa Bara hilo lazima waendelee kukumbatia, kulea na kuendelea kujenga demokrasia.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Afrika ni salama pamoja na ugonjwa wa Ebola – Rais Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa changamoto kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Afrika katika Jamhuri ya Watu wa China kuendelea kutangaza habari njema kuwa bado ni salama kutembelea Bara la Afrika pamoja na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola ambao umeua maelfu ya watu hasa katika nchi tatu za Afrika Magharibi.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania imetuma madaktari watano kwenda Afrika Magharibi kusaidia kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ambao unaendelea kuua maelfu ya watu katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone. Mpaka sasa watu zaidi ya 4,000 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huo katika nchi hizo.
Rais Kikwete pia amesema kuwa ni muhimu zaidi kwa nchi za Afrika kuongeza mshikamano na kusaidiana, ili kuongeza nguvu za pamoja za kukabiliana na ugonjwa huo ambao umeanza kuwa tishio kwa dunia nzima.
Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Jumatano, Oktoba 22, 2014, kwenye Nyumba ya Kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai mjini Benjing, wakati alipokutana na kuzungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini China ikiwa ni shughuli yake ya kwanza ya ziara yake rasmi ya Kiserikali nchini humo.
Rais Kikwete akifuatana na Mama Salma Kikwete aliwasili mjini Beijing, usiku wa jana, Jumanne, Oktoba 21, 2014, kuanza ziara rasmi ya siku sita katika China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping.
Katika mkutano wake na mabalozi hao wa Afrika, Rais Kikwete amepata nafasi ya kuwaeleza hali ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama Barani Afrika hasa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Libya, Sudan Kusini na Somalia na tishio la ugaidi wa makundi mbali mbali katika nchi za Afrika.
“Lakini habari kubwa katika Afrika kwa sasa ni ugonjwa wa Ebola. Bara la Afrika linabaguliwa sasa kwa sababu ya ugonjwa huo. Watu wanafuta mipango yao kutembelea Bara letu, watalii wanapungua. Kwetu sisi ugonjwa huu ni tishio kubwa kwa maisha ya watu wetu lakini ni tishio kubwa kiuchumi,” Rais Kikwete amewaambia mabalozi hao na kuongeza:
“Sasa kwa sababu ugonjwa wa Ebola unaongeza kubaguliwa kwa Bara la Afrika, ni wajibu wenu nyie wawakilishi wetu, mabalozi wetu kutusemea. Elezeni habari njema na nzuri za Afrika. Waambie hawa wakubwa kuwa Bara la Afrika ni Bara salama kutembelea pamoja na kushambuliwa na ugonjwa wa Ebola. Aidha, kwa sababu kuna majaribio ya dawa nyingi za ugonjwa huo yanafanyika katika nchi mbali mbali ikiwemo China, waombe wakubwa hawa watusaidiE kupatikana kwa dawa hizo.”
Kuhusu mchango wa Tanzania katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania imetuma madaktari wake watano katika nchi zinazokabiliwa na ugonjwa huo kwa sasa kuongeza nguvu za kukabiliana na Ebola. “Nchi za Afrika zinahitaji sana mshikamano na ushirikiano kwa sasa kukabiliana na ugonjwa huo hatari sana.”
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
22 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
JK: Mfumo wa Rais kung’atuka madarakani ni mzuri
. Unatoa nafasi kwa nchi kupata mawazo na fikra mpya
.Anaamini Tanzania itapata Rais bora zaidi wa kumrithi yeye
. Atamani muda wake umalizike akalee wajukuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mfumo wa Tanzania ambako Rais anatumikia nafasi ya uongozi kwa muhula wa miaka mitano na siyo zaidi ya miaka 10 ni mfumo mzuri na unaovutia kwa sababu unaiwezesha nchi kupata fikra na mawazo mapya.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa anaamini kuwa Tanzania itapata Rais bora zaidi kuliko yeye, Rais ambaye ataiwezesha Tanzania kusonga mbele kwa kasi kubwa zaidi.
Rais Kikwete pia amesema kuwa anayo hamu kubwa ya kumaliza muda wake wa uongozi, ili arudi kijijini kushughulika na wajuu wake na mifugo yake.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Oktoba 22, 2014, mjini Beijing, China, wakati akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao katika China.
Mkutano huo uliofanyika kwenye Nyumba ya Kufikia Wageni wa Serikali ya China ya Diaoyutai, ulikuwa shughuli ya kwanza ya Rais Kikwete katika ziara yake rasmi ya siku sita ya Jamhuri ya Watu wa China ambako amealikwa na Rais Xi Jinping.
Wakati wa maswali na majibu, Mheshimiwa Balozi Sola Onadipe, Naibu Balozi wa Nigeria katika China, alishangazwa na kauli ya Rais Kikwete kuwa anatamani amalize muda wake wa uongozi, ili astaafu na kusema kuwa lingekuwa jambo la maana kwa Afrika kama viongozi wengine wangekuwa na mawazo ya namna hiyo ya kuheshimu Katiba za nchi zao na kung’atuka kwenye uongozi muda wao unapowadia.
Rais Kikwete amemwambia Balozi huyo: ” Ni kweli naona kama muda hauendi kwa kasi ya kutosha, ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga ng’ombe na mbuzi wangu na nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha. Lakini Mheshimiwa Balozi usishangazwe na utayari wangu kuondoka katika uongozi.”
“Kwanza utaratibu huu wa miaka mitano ama miaka 10 ni utaratibu wa Kikatiba, ni jambo lililoko katika Katiba yetu na hatuna kishawishi cha kulibadilisha. Pili, kazi hii ya Urais ni kazi ngumu sana. Kwa hakika, binafsi nawaonea gele sana wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye kazi hii kwa miaka mingi. Pengine wana nguvu zaidi kuliko mimi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“ Lakini pia kuna uzuri katika mfumo huu wa kwetu kwa sababu kila baada ya miaka mitano na hata kama ni baada ya kila miaka kumi, anaingia mtu mwingine madarakani akiwa na fikra mpya na mawazo mapya.”
“ Mfumo huu ni mfumo unaoniridhisha sana na wala hakuna kinachonishawishi nibakie katika madaraka zaidi ya muda wangu kikatiba. Nina hakika, nchi yetu itapata kiongozi mwingine, bora kuliko hata mimi, kuongoza vizuri nchi yetu.”
Rais Kikwete pia amesema kuwa siyo busara pia kwa kiongozi kuwasikiliza wale wanaoshauri wakisema kuwa akiondoka madarakani nchi itavurugika.
“Kwa hakika, hawa wanatetea maslahi yao tu wakisema kuwa ukiondoka wewe madarakani, wao hawatakuwa tena mabalozi ama mawaziri ama nafasi nyingine yoyote.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Oktoba, 2014
taarifa kwa Vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi na pole nyingi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange kuomboleza kifo cha Meja Jenerali Herman Cornel Lupogo ambaye aliaga dunia Jumapili, Oktoba 19, 2014, akiwa na umri wa miaka 76 katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam, ambako alikuwa anapata matibabu.
Katika salamu zake, Mheshimiwa Kikwete amemweleza Meja Jenerali Lupogo kama mzalendo halisi, ofisa mtiifu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyeitumikia nchi yake kwa moyo wote na wakati wote na ambaye ataendelea kuvikumbusha vizazi vingi vya Watanzania maana halisi ya mapenzi kwa nchi yao.
Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo za rambirambi: “Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa za kifo cha Meja Jenerali Herman Cornel Lupogo ambaye nimejulishwa kuwa alipoteza maisha juzi katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Lugalo. Kwa hakika, taifa letu limempoteza Mtanzania halisi, ofisa mtiifu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambaye ataendelea kuvikumbusha vizavi vingi vya Watanzania maana halisi ya mapenzi kwa nchi yao.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Tokea alipojiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Julai 23, mwaka 1965 hadi alipostaafu utumishi wake Septemba 11, 1992 baada ya kulitumikia Jeshi kwa miaka 28, miezi minne na siku 13, Meja Jenerali Lupogo alionyesha weledi mkubwa wa kazi ya Jeshi na mapenzi makubwa ya kutumikia nchi yake. Alikuwa Ofisa wa mfano.”
“Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu zangu za rambirambi kuomboleza kifo hiki. Najiunga nawe, maofisa wote wakuu, maofisa wadogo na wapiganaji wote kumlilia Meja Jenerali Lupogo. Napenda mjue kuwa niko nanyi katika msiba huu mkubwa,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Aidha, kupitia kwako, napenda kufikisha salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kwa wanafamilia wote wa Meja Jenerali Lupogo kwa kuondokewa na mhimili wa familia yao. Niko nao katika majonzi ya msiba huu mkubwa. Niko nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema roho ya Marehemu Meja Jenerali Herman Cornel Lupogo. Amina.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya habari
Rais Kikwete aanza ziara rasmi ya China
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Oktoba 21, 2014, anaanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping, ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Baada ya China, Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Vietnam kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.
Wakati wa ziara yake nchini China, Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Oktoba 20, 2014, atatembelea majimbo matatu ya nchi hiyo, atafanya mazungumzo na viongozi wakuu wa China, atashuhudia utiaji saini mikataba muhimu ya shughuli za maendeleo, atatunukiwa shahada za heshima na atashiriki katika sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China.
Rais Kikwete amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping; Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Zhang Dejiang.
Rais Kikwete pia atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya miradi ya maendeleo ya Tanzania ambayo inasaidiwa ama inagharimiwa na fedha kutoka China na pia atakutana kwa mazungumzo na wakuu wa taasisi muhimu zinazogharimia baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo katika Tanzania zikiwamo China-Africa Development Fund (CADB) na China Development Bank (CDB).
Akiwa Beijing, Rais Kikwete atakutana na Mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao katika China, atafungua Mkutano wa Tatu wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China na atazindua rasmi Kijiji cha Kiafrika.
Aidha, Rais Kikwete atatunukiwa uprofesa wa heshima na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China cha China Agricultural University na Chuo Kikuu cha East China Normal University na pia atakuwa mwenyeji wa hafla maalum ya kusherehekea miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China. Uhusiano huo ulitimiza miaka 50, Aprili 26, mwaka huu, siku ambako Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia ilitimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake.
Baada ya kumaliza ziara yake Beijing, Rais Kikwete atatembelea Jimbo la Jinan ambako atashuhudia maonyesho rasmi ya kijeshi ya Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China la Chinese People’s Liberation Army (PLA) lililoandaliwa rasmi kwa heshima yake. Hiyo itakuwa mara ya kwanza katika historia kwa heshima ya namna hiyo kutolewa kwa kiongozi wa nchi yoyote duniani, nje ya China.
Akiwa Jimbo la Jinan, Rais Kikwete pia atakutana na viongozi wa Jimbo hilo na pia atakutana kwa mazungumzo na madaktari wa Kichina ambao wamefanya kazi katika Tanzania katika miaka 50 iliyopita.
Baada ya Jimbo la Jinan, Rais Kikwete atakwenda Jimbo la Shenzhen ambako atatembelea makao makuu ya taasisi na makampuni makubwa ya China ya Shenzhen Economic Zones Authority, China Merchants Holdings International (CMHI), Huawei na ZTE. Shenzhen ndiko Watanzania wengi wanaonunua bidhaa kutoka China hufanyia biashara zao.
Mara ya mwisho, Rais Kikwete alitembelea China mwaka 2008 wakati alipoliwakilisha Bara la Afrika katika Mkutano wa Kwanza wa China-Afrika katika nafasi yake wakati huo kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Rowland Mhaka Makunda kilichotokea tarehe 16 Oktoba, 2014 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Meja Jenerali Mstaafu, Rowland Mhaka Makunda ambaye, pamoja na kwamba alikuwa amestaafu, ushauri wake kuhusu masuala mbalimbali ya Jeshi ulikuwa bado unahitajika sana kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu.
Meja Jenerali Makunda alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Mwaka 1961 na kulitumikia Jeshi hilo kwa muda wa zaidi ya miaka 32 baada ya kupata mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi, na kutunukiwa Nishani kadhaa zikiwemo za Utumishi wa Muda Mrefu na Uliotukuka.
Rais Kikwete amesema enzi za uhai wa Meja Jenerali Rowland Mhaka Makunda, yeye binafsi alimfahamu Marehemu kama Askari Hodari na wa kupigiwa mfano kutokana na uchapakazi, utiifu na uaminifu wake kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, hivyo kuchangia katika kuliletea Taifa heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
“Ni kwa kutambua sifa zake hizo na mchango wake mkubwa kwa Taifa, nadiriki kusema kwamba kifo cha Meja Jenerali Rowland Mhaka Makunda kimetuhuzunisha sana sote kama Taifa. Kutokana na msiba huu mkubwa, nakutumia Salamu za Rambirambi kwa kumpoteza Mpiganaji Hodari wa Jeshi letu la Ulinzi la Wananchi wa Tanzani. Kupitia kwako naomba Salamu zangu pia ziwafikie Askari na Wapiganaji wote wa JWTZ kwa kumpoteza mwenzao”.
Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange kumfikishia Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa familia ya Marehemu, Meja Jenerali Rowland Mhaka Makunda kwa kupoteza mhimili madhubuti na kiongozi mahiri wa familia.
Amewaomba wanafamilia wawe na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza kifo cha mpendwa wao. Amewahakikishia kuwa yuko pamoja nao katika kipindi chote cha maombolezo.
Mwisho.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
18 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais atoa Hati ya Uraia kwa waliokuwa wakimbizi wa Burundi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya jana, Jumanne, Oktoba 14, 2014, alitoa Hati za Uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 162 ambao walikuwa wakimbizi kutoka Burundi na ambao wameishi nchini kwa miaka 42, tokea Mwaka 1972.
Rais Kikwete ametoa Hati hizo katika shughuli fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ikiwa sehemu ya shughuli za Rais Kikwete katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. Kwa niaba ya wenzao, Rais Kikwete ametoa Hati hizo kwa wakimbizi hao 19 wa zamani kwa niaba ya wenzao.
Shughuli hiyo ya utoaji Hati za Uraia ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Mathias Chikawe, Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi nchini na mabalozi wa Uingereza, Canada, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Ireland,Ubelgiji na mwakilishi wa Ubalozi wa Japan pamoja na Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Tabora.
Shughuli ya leo inakamilisha mchakato mbao ulianzishwa na Rais Kikwete Mwaka 2007 wakati alipoamua kuwapa wakimbizi hao wa Burundi uraia wa Tanzania baada ya kuwa wameishi nchini kama wakimbizi tokea walipoingia kwa mara ya kwanza Mwaka 1972 kufuatia machafuko katika Burundi. Wameishi katika kambi za ukimbizi katika Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora.
Akizungumza katika shughuli hiyo, Mwakilishi wa UNHCR katika Tanzania, Bi. Joyce Mends-Cole amesema kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza katika historia ya dunia kwa kutoa uraia kwa watu wengi kiasi hicho na kwa wakati mmoja.
Naye Balozi wa Ireland nchini Mheshimiwa Fionnula Gilsenan, akizungumza kwa niaba ya mabalozi wenzake ameisifu sana Tanzania na kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wa kutoa Uraia na Hati za Uraia kuwa ”kitendo kikubwa na kitendo kizuri sana.”
“Mheshimiwa Rais umefanya kitu kikubwa mno. Hili ni jambo kubwa na wewe mwenyewe umeshuhudia furaha ya watu hawa. Umesikia nyimbo zao za shukurani kwako na kwa Serikali.”
Akizungumza na raia hao wapya wa Tanzania, Rais Kikwete amesema kuwa matarajio yake na yale ya Watanzania ni kuwaomba raia wapya ni kuwaona wakitimiza ahadi yao kwa nchi yao kwa kuwa raia wapya.
“Shughuli ya leo ni kutimiza tu mchakato kwa sababu hili la uraia wenu tulilimaliza siku nyingi. Matarajio yangu na yale ya Watanzania wenzenu ni nyie kutimiza ahadi ya kiapo chenu cha kuwa raia wema wa nchi yenu. Heshimuni kiapo chenu.”
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
15 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzania kusuluhisha mgororo wa Sudan Kusini
- Ni kweli ngazi ya vyama tawala na mikutano ya upatanishi
kufanyika Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s Liberation Movement (SPLM), mgogoro ambao umesababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa usuluhishi huo utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Kikwete amesema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Rais Kikwete ametangaza jitihada hizo za upatanishi za Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Rais Kikwete amewaambia wananchi kuwa Tanzania imekubali kuwasaidia ndugu zao wa Sudan Kusini kwa nia ya kutimiza wajibu wake wa kimataifa na kwa kuongozwa na kaulimbiu ya Oktoba Mwaka 1959 ambayo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliitoa wakati nchi ya Tanganyika bado ikidai uhuru wake kutoka kwa Wakoloni wa Kiingereza.
Rais Kikwete ameikariri kaulimbiu hiyo maarufu: “Sisi Watu wa Tanganyika tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambako hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau.”
Rais Kikwete amesema kuwa Mwenge wa Uhuru unabeba falsafa kubwa ndani yake kuhusu “nchi yetu na uhusiano wake na watu wengine duniani hasa wanyonge, wenye dhiki na wasiokuwa na amani. Dhamira hii ya Mwalimu na nchi yetu ilitimizwa Desemba 9, 1961, siku Tanganyika ilipopata Uhuru ambako Bendera ya Taifa huru la Tanganyika na Mwenge wa Uhuru vilipandishwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro na Mwenge kuwashwa.”
“Toka wakati huo mpaka sasa, Mwenge wa Uhuru umeendelea kumulika nchi nzima ukipita katika mitaa, vijiji, shehia na majimbo, wilaya na mikoa ukieneza ujumbe wa udugu, umoja, upendo, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Kwa kuzingatia ujumbe uliobebwa na Mwenge wa Uhuru, nchi yetu na sisi Watanzania tumejitolea kwa hali na mali kusaidia ndugu zetu Barani Afrika waliokuwa wanatawaliwa kujikomboa kutoka kwenye makucha ya wakoloni na wabaguzi wa rangi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu. Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
15 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali Tatu zingekuwa kejeli kwa Mwalimu Nyerere – Rais
. Maisha yake yote alipigania Muungano wa muundo wa Serikali mbili
. Katiba Inayopendekezwa ndiyo hasa Katiba ya Wananchi
. Siyo tu kwamba ni nzuri bali ni Katiba bora
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa sherehe za leo za Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, zingekuwa zinamkejeli moja kwa moja Mwalimu kama Katiba Inayopendekezwa ingekubali pendekezo la Serikali Tatu.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hajui Watanzania wangesema nini katika sherehe za mwaka huu wa Kumbukumbu hiyo kama Tanzania ingekuwa na Katiba Inayopendekezwa ingekuwa imesisitiza Muungano wa muundo wa Serikali tatu.
Vile vile, Rais Kikwete amesema kuwa Muungano wa Serikali Mbili ndiyo hasa urithi mkuu ambao Mwalimu Nyerere aliwaachia Watanzania na wana budi kuendelea kuulinda na kuuthamini urithi huo.
Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Taifa leo, Jumanne, Oktoba 14, 2014, kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbumbuku za Mwalimu Nyerere na Kumalizika kwa Wiki ya Vijana iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambao ulijaa maelfu kwa maelfu ya wananchi kuasdhimisha matukio hayo.
Rais Kikwete amewaambia wananchi kuwa ni jambo mwafaka na faraja kabisa kuwa Katiba Inayopendekezwa imesisitiza ubora wa kuendelea na Muungano wa Serikali mbili alizoziasisi Mwalimu Julius Nyerere akiwa na Mzee Abeid Amani Karume.
Amesema Rais Kikwete: “Bila shaka mtakumbuka jinsi Mwalimu alivyoupigania muundo huu kwa nguvu zake zote wakati wa uhai wake. Hatuna budi kulipongeza Bunge Maalum la Katiba kwa kumuenzi kwa dhati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kudumisha urithi wake mkuu.”
Ameongeza Rais Kikwete: “ Sijui tungesema nini katika Sherehe za mwaka huu kama ndiyo tungekuwa na Katiba Inayopendekezwa yenye Muungano wa muundo wa Serikali Tatu?”
“Sherehe za mwaka huu ni spesheli kweli kweli kwani zinafanyika siku chache baada ya Bunge Maalum la Katiba kukamilisha kazi na kukabidhi Katiba Inayopendekezwa, Katiba ambayo siyo tu ni nzuri lakini ni Katiba bora. Nimebahatika kuisoma Katiba Inayopendekezwa na naendelea kuisoma kwa sababu ina mambo mengi mazuri. Kwa kweli ni Katiba bora kuliko hii tuliyonayo sasa yaani Katika ya Mwaka 1977.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Hii ndiyo yenyewe hasa. Hii ndiyo Katiba ya Wananchi. Ni Katiba inayotambua na kuimarisha tunu za taifa letu na mambo mazuri ya huko tulikotoka na hapa tulipo. Ni katiba inayorekebisha upungufu uliopo sasa na kuweka mifumo mizuri inayoendana na wakati tulionao sasa na huko mbele tuendako. Kwa lugha nyepesi ni Katiba inayojibu changamoto zetu za leo na kesho.”
Amewaambia wananchi Rais Kikwete: “Katiba Inayopendekezwa inatokana na ushirikishwaji mpana wa wananchi wa Tanzania walioko ndani na nje ya nchi. Hata Watanzania waishio nje ya nchi walikuwa na uwakilishi ndani ya Bunge Maalum la Katiba. Ndiyo maana haki na maslahi ya makundi yote yametambuliwa na kupewa nafasi yake stahiki.”
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
14 Oktoba, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumamosi, Oktoba 11, 2014 alijiunga na mamia kwa mamia ya wananchi kumzika Meja Jenerali Muhidin Mfaume Kimario kwenye Makaburi ya Mjini Moshi yaliyoko Kata ya Bondeni.
Rais Kikwete aliwasili mjini Moshi kiasi cha saa 11 kamili jioni akitokea Mkoani Mwanza ambako alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu.
Alikwenda moja kwa moja makaburini kujiunga na mamia kwa mamia ya waombolezaji kwa ajili ya mazishi ya Meja Jenerali huyo mstaafu ambaye mwili wake ulifikishwa makaburini kiasi cha saa 11:25 jioni na kuteremshwa kaburini saa 11:40.
Meja Jenerali Mstaafu Kimario amezikwa kwa heshima zote za kidini na kijeshi ambazo zilikuwa ni pamoja na kupigiwa mizinga tisa na kuagwa kwa gwaride kamili la kijeshi.
Meja Jenerali Kimario ambaye aliaga dunia wiki hii, Jumatatu, Oktoba 6, mwaka huu, katika Hospitali ya Apollo, nchini India ambako alikuwa anapata matibabu, mbali na kuwa Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) pia alipata kuwa Waziri Mwandamizi wa Serikali. Alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na pia mara mbili alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Aidha, alipata kuwa Mkuu wa Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza na pia alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu, Dodoma – CDA. Vile vile, alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo kati ya 1975 na 1990.
Muhidin Mfaume Kimario alizaliwa Moshi mjini na kupata elimu katika Shule ya Msingi ya Majengo na Shule ya Kati ya Marangu za Mkoa wa Kilimanjaro, kabla ya kujiunga na Chuo cha Ualimu cha Butimba, Mwanza.
Marehemu alijiunga na TPDF Januari 10, Mwaka 1963 na alistaafu utumishi wa Jeshi Desemba 28, 1992, baada ya kulitumikia TPDF kwa miaka 29, miezi 11 na siku 17.
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Kikwete amwaga Dkt. Shija
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Oktoba 12, 2014, ameungana na waombolezaji kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Katibu Mkuu wa Kwanza Mwafrika wa Chama cha Mabunge ya Jumuia ya Madola (CPA) Dkt. William Ferdinand Shija, ambaye pia alipata kuwa Waziri Mwandamizi wa Serikali, katika shughuli iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amewasili kwenye Viwanja vya Karimjee kiasi cha saa 4:10 asubuhi kujiunga na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mwenyekiti wa CPA-Kanda ya Afrika Mheshimiwa Anne Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho.
Baada ya kuaga mwili, Rais Kikwete ametia saini Kitabu cha Maombolezo ya Dkt. Shija ambaye alifariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita, Oktoba 4, 2014 kwenye Hospitali ya Charing Cross mjini London, Uingereza ambako alikuwa anapata matibabu ya ugonjwa wa Saratani. Makazi yake ya kazi yalikuwa huko huko Uingereza.
Miongoni mwa waombolezaji wengi kwenye shughuli hiyo ya leo ulikuwa ni ujumbe mzito wa CPA ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Lindiwe Maseko wa Afrika Kusini. Pia shughuli hiyo imehudhuriwa na Bwana Joe Omoldin ambaye sasa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho.
Dkt. Shija ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Nyalukomba, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Aprili 28, Mwaka 1947, alipata elimu ya awali maeneo ya kwako kabla ya kujiunga na Sekondari ya Chopra mjini Mwanza kwa elimu ya sekondari na kuhitimu ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Chan’gombe cha Dar es Salaam Mwaka 1968.
Baadaye, Dkt. Shija alipata Shahada ya kwanza ya Uzamili ya Uandishi wa Habari nchini India kabla ya kupata Shahada ya Uzamivu ya fani hiyo hiyo ya Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Howard cha mjini Washington, D.C., Marekani. Wakati wote wa masomo yake alikuwa Mhadhiri wa Uandishi kwenye Chuo cha Nyegezi, Mwanza.
Dkt. Shija aligombea na kushinda Ubunge wa Jimbo la Sengerema Mwaka 1990 na kuingia Serikali ambako alishikilia nafasi tofauti kwa vipindi tofauti kama Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Habari na Utangazaji, Waziri wa Nishati na Madini na Waziri wa Biashara na Viwanda. Dkt. Shija pia amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Katika Mkutano Mkuu wake wa 52, Desemba, Mwaka 2006 mjini Abuja, Nigeria, Dkt. Shija alichaguliwa, baada ya mchuano mkali sana, kuwa Katibu Mkuu wa Kwanza Mwafrika wa CPA, taasisi ambayo tokea kuanzishwa kwake Mwaka 1911 ilikuwa haijapata kumchagua Mwafrika kuwa Mtendaji Mkuu wake.
Alichaguliwa kwa kipindi cha pili Mwaka 2012 baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Alikuwa anamaliza muda wake Desemba 2016.
Mpaka anaaga dunia, Dkt. Shija alikuwa ameshikilia nafasi ya Ukatibu Mkuu wa CPA kwa mafanikio makubwa sana kwa miezi saba na miezi tisa. Atazikwa kesho, Jumatatu, Oktoba 13, 2014 katika kijiji cha kwao cha Nyalukomba, Sengerema, Mwanza.
……Mwisho……
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Kikwete amwaga Dkt. Shija
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Oktoba 12, 2014, ameungana na waombolezaji kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Katibu Mkuu wa Kwanza Mwafrika wa Chama cha Mabunge ya Jumuia ya Madola (CPA) Dkt. William Ferdinand Shija, ambaye pia alipata kuwa Waziri Mwandamizi wa Serikali, katika shughuli iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amewasili kwenye Viwanja vya Karimjee kiasi cha saa 4:10 asubuhi kujiunga na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mwenyekiti wa CPA-Kanda ya Afrika Mheshimiwa Anne Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho.
Baada ya kuaga mwili, Rais Kikwete ametia saini Kitabu cha Maombolezo ya Dkt. Shija ambaye alifariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita, Oktoba 4, 2014 kwenye Hospitali ya Charing Cross mjini London, Uingereza ambako alikuwa anapata matibabu ya ugonjwa wa Saratani. Makazi yake ya kazi yalikuwa huko huko Uingereza.
Miongoni mwa waombolezaji wengi kwenye shughuli hiyo ya leo ulikuwa ni ujumbe mzito wa CPA ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Lindiwe Maseko wa Afrika Kusini. Pia shughuli hiyo imehudhuriwa na Bwana Joe Omoldin ambaye sasa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho.
Dkt. Shija ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Nyalukomba, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Aprili 28, Mwaka 1947, alipata elimu ya awali maeneo ya kwako kabla ya kujiunga na Sekondari ya Chopra mjini Mwanza kwa elimu ya sekondari na kuhitimu ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Chan’gombe cha Dar es Salaam Mwaka 1968.
Baadaye, Dkt. Shija alipata Shahada ya kwanza ya Uzamili ya Uandishi wa Habari nchini India kabla ya kupata Shahada ya Uzamivu ya fani hiyo hiyo ya Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Howard cha mjini Washington, D.C., Marekani. Wakati wote wa masomo yake alikuwa Mhadhiri wa Uandishi kwenye Chuo cha Nyegezi, Mwanza.
Dkt. Shija aligombea na kushinda Ubunge wa Jimbo la Sengerema Mwaka 1990 na kuingia Serikali ambako alishikilia nafasi tofauti kwa vipindi tofauti kama Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Habari na Utangazaji, Waziri wa Nishati na Madini na Waziri wa Biashara na Viwanda. Dkt. Shija pia amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Katika Mkutano Mkuu wake wa 52, Desemba, Mwaka 2006 mjini Abuja, Nigeria, Dkt. Shija alichaguliwa, baada ya mchuano mkali sana, kuwa Katibu Mkuu wa Kwanza Mwafrika wa CPA, taasisi ambayo tokea kuanzishwa kwake Mwaka 1911 ilikuwa haijapata kumchagua Mwafrika kuwa Mtendaji Mkuu wake.
Alichaguliwa kwa kipindi cha pili Mwaka 2012 baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Alikuwa anamaliza muda wake Desemba 2016.
Mpaka anaaga dunia, Dkt. Shija alikuwa ameshikilia nafasi ya Ukatibu Mkuu wa CPA kwa mafanikio makubwa sana kwa miezi saba na miezi tisa. Atazikwa kesho, Jumatatu, Oktoba 13, 2014 katika kijiji cha kwao cha Nyalukomba, Sengerema, Mwanza.
……Mwisho……
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais: Msitumie fedha za maendeleo kulipia posho za vikao vya madiwani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezitaka halmashauri nchini kuepukana na vishawishi vya kutumia fedha za maendeleo ya wananchi kulipia posho za vikao vya madiwani.
Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Ijumaa, Oktoba 10, 2014, wakati alipozungumza na wananchi na viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakati anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Usagara-Kisesa kwa kiwango cha lami katika sherehe ya kufana iliyofanyika Kisesa, kilomita 16 kutoka mjini Mwanza.
Rais amelazimika kutoa maelekezo hayo baada ya kujulishwa na Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuwa kwa mwaka huu wa fedha, Mkoa wa Mwanza utapewa kiasi cha Sh.bilioni 7.2 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara za Mkoa huo ambao ziko chini ya Halmashauri za Mkoa huo nyingi zikiwa za vijijini.
Fedha hizo kutoka Mfuko wa Barabara ni kiwango kikubwa zaidi cha fedha ambazo zimepata kutolewa kwa Mkoa huo kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara za halmashauri ambazo haziko chini ya Wakala wa Barabara wa Tanroads.
“Fedha hizi ni nyingi. Kwa kweli kwa sasa, tatizo siyo upatikanaji wa fedha. Tatizo ni mchwa unaotafuna fedha hizi za umma. Kwa hiyo fedha hizo nyingi ambazo mnapewa msizitumie kulipia posho za madiwani. Jipangeni vizuri, zitumieni vizuri fedha hizo,” amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo ya Usagara-Kisesa yenye urefu wa kilomita 16.95 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu ya kikazi katika Mkoa wa Mwanza.
Rais Kikwete aliwasili Mwanza jioni ya jana, Alhamisi, Oktoba 9, 2014 akitokea Kampala, Uganda ambako alikuwa Mgeni Maalum katika Sherehe za Miaka 52 ya Uhuru wa Uganda zilizofanyika kwenye Viwanja vya Sherehe vya Kololo mjini humo.
Barabara ya Usagara-Kisesa ambayo ni pamoja na ujenzi wa daraja kubwa la Nyanshishi inagharimu kiasi cha Sh.17.895 bilioni mbali na kiasi cha Sh. milioni 122 ambacho kimetolewa na Serikali kufidia wananchi ambao mali zao zitaharibiwa kupisha ujenzi wa barabara hiyo.
Barabara hiyo inalenga kurahisisha usafiri kati ya Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara na Kagera ambako sasa wasafiri hawatakuwa tena na ulazima wa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza ili kuendelea na safari zao.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia C. Ako amemwambia Rais Kikwete kuwa ujenzi wa barabara hiyo unafanywa na kampuni ya kizalendo ya Nyanza Road Works Limited na imepangwa kumalizika katika kipindi cha miezi 15.
Baadaye, Rais Kikwete amefungua Daraja la Wavukaji Barabara kwa miguu katika eneo la Mabatini mjini Mwanza ambalo limepunguza kwa kiasi kikubwa madhara ya watu kugongwa na magari na pia limepunguza msongamano wa magari katika eneo hilo la barabara ya Mwanza-Musoma.
Barabara hiyo inapitisha magari 30,000 kila siku na takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa watu wanane walikuwa wanagongwa na magari katika eneo hilo la Mabatini na kati ya hao wawili walikuwa wanapoteza maisha
Rais Kikwete jioni ya leo, amezindua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la PPF lililoko katikati ya Jiji la Mwanza, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mkoa wa Mwanza.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kama Katiba Inayopendekezwa ni mbaya, hiyo nzuri ikoje?
auliza Rais Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewashangaa watu wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya, akiuliza kuwa kama Katiba hiyo ni mbaya basi hiyo nzuri ikoje?
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Katiba inayojali makundi yote ndani ya jamii, kama ilivyo Katiba Inayopendekezwa, kamwe haiwezi kuwa Katiba mbaya.
Rais Kikwete ameyasema hayo nyakati tofauti leo, Ijumaa, Oktoba 10, 2014, wakati alipozungumza na wananchi katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mwanza, ambako anafanya ziara ya siku tatu ya kikazi kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.
Akizungumza na mamia kwa mamia ya wananchi mjini Kisesa ambako ameweka jiwe la msingi la ujenzi kwa kiwango cha lami na Barabara ya Usagara-Kisesa, Rais Kikwete amewataka wananchi kuwapuuza watu wachache wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya na badala yake wajiandae kuipigia kura ya kuikubali wakati ukiwadia.
“Sijui katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani ya jamii kama hii Katiba Inayopendekezwa. Hakuna aliyeachwa – wavuvi wamo, wajane wamo, wafanyabiashara ndogo ndogo wamo, akinamama lishe wamo, wakulima wamo, wafungaji wamo….kila mtu yumo. Akinamama ndio usiseme kabisa wao wamepata hata asimilia 50 kwa 50 ndani ya Bunge.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Hivi katiba mbaya inakuwa kama inayopendekezwa na kama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa hivi nzuri ikoje?”
Rais Kikwete amewambia wananchi: “Watakuja watu kuwashawishi kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya, wasikilizeni lakini tumieni akili yenu, kama ile hadithi ya mbayuwayu. Jiandaeni tu kupiga kura na kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa kwa sababu hii ni Katiba nzuri sana.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumamosi, Oktoba 11, 2014 alijiunga na mamia kwa mamia ya wananchi kumzika Meja Jenerali Muhidin Mfaume Kimario kwenye Makaburi ya Mjini Moshi yaliyoko Kata ya Bondeni.
Rais Kikwete aliwasili mjini Moshi kiasi cha saa 11 kamili jioni akitokea Mkoani Mwanza ambako alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu.
Alikwenda moja kwa moja makaburini kujiunga na mamia kwa mamia ya waombolezaji kwa ajili ya mazishi ya Meja Jenerali huyo mstaafu ambaye mwili wake ulifikishwa makaburini kiasi cha saa 11:25 jioni na kuteremshwa kaburini saa 11:40.
Meja Jenerali Mstaafu Kimario amezikwa kwa heshima zote za kidini na kijeshi ambazo zilikuwa ni pamoja na kupigiwa mizinga tisa na kuagwa kwa gwaride kamili la kijeshi.
Meja Jenerali Kimario ambaye aliaga dunia wiki hii, Jumatatu, Oktoba 6, mwaka huu, katika Hospitali ya Apollo, nchini India ambako alikuwa anapata matibabu, mbali na kuwa Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) pia alipata kuwa Waziri Mwandamizi wa Serikali. Alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na pia mara mbili alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Aidha, alipata kuwa Mkuu wa Mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza na pia alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu, Dodoma – CDA. Vile vile, alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo kati ya 1975 na 1990.
Muhidin Mfaume Kimario alizaliwa Moshi mjini na kupata elimu katika Shule ya Msingi ya Majengo na Shule ya Kati ya Marangu za Mkoa wa Kilimanjaro, kabla ya kujiunga na Chuo cha Ualimu cha Butimba, Mwanza.
Marehemu alijiunga na TPDF Januari 10, Mwaka 1963 na alistaafu utumishi wa Jeshi Desemba 28, 1992, baada ya kulitumikia TPDF kwa miaka 29, miezi 11 na siku 17.
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Oktoba,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Alhamisi, Oktoba 9, 2014, amekuwa Mgeni Maalum katika Sherehe za Kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Uganda zilizofanyika kwenye Viwanja vya Sherehe vya Kololo mjini Kampala.
Kwa nafasi yake ya kuwa Mgeni Maalum, Rais Kikwete amekuwa kiongozi pekee mwalikwa kupata nafasi ya kutoa salamu kwa wananchi wa Uganda ambayo Oktoba 9, mwaka 1962, ilipata Uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza.
Viongozi wengine ambao wameshiriki katika sherehe hizo za kufana na zilizohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi ni Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Makamu wa Rais wa Burundi na wawakilishi wa nchi za Kenya na Ethiopia.
Rais Kikwete ambaye aliwasili Uganda mapema jana asubuhi akitokea Dodoma, ambako juzi alipokea Katiba Inayopendekezwa katika sherehe kubwa na ya kufana sana iliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, amekwenda moja kwa moja Uwanja wa Kololo, ambako aliingia dakika mbili kabla ya kuingia kwa mwenyeji wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Akimtambulisha Rais Kikwete kwa wananchi waliofurika kwenye Uwanja huo wa Kololo, Rais Museveni aliwaambia wananchi hao: “Hapa mbele yenu mnaona Jeshi imara kabisa la UPDF (Uganda People’s Defence Army) na Jeshi la Polisi lililo imara pia. Nguvu na uwezo huu wa Jeshi na Polisi wetu umejengwa na pande mbili kubwa.”
Ameongeza Rais Museveni: “Upande wa kwanza ni sisi wenyewe wananchi wa Uganda na hili mnalijua vizuri sana. Upande wa pili alikuwa ni Mwalimu Julius Nyerere, Mwanzilishi na Baba wa Taifa la Tanzania. Yeye hatunaye tena, yeye sasa amekuwa Omugenzi, yaani ametangulia, kama sisi sote tutakavyokwenda. Hata hivyo, leo tunaye mmoja wa viongozi wa Tanzania ambao wamemfuatia Mwalimu Nyerere katika uongozi wa nchi hiyo, naye ni Rais Kikwete. Karibu Rais Kikwete uzungumze na wananchi wa Uganda.”
Akizungumza kwa ufupi tu na wananchi hao, Rais Kikwete amewaambia wananchi hao: “Ndugu zangu wananchi wa Uganda, nawaleteeni salamu nyingi za kindugu na kirafiki kutoka kwa ndugu zenu wa Tanzania. Wamenituma niwaletee salamu nyingi za pongezi katika kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa nchi yenu.”
Rais Kikwete aliwapongeza wananchi wa Uganda kwa mafanikio makubwa ambayo yamepatikana tokea Uhuru na hasa katika miaka 28 ya uongozi wa Rais Museveni.
“Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikia. Kama kuna mtu haoni maendeleo dhahiri kabisa ambayo yamepatikana chini ya uongozi wa Rais Museveni basi ana lake jambo ama hataki tu kuambiwa, kutambua na kukubali ukweli.”
“Chini ya uongozi imara wa Rais Museveni, Uganda imefanikiwa kurejesha amani na utulivu, jambo ambalo kuna wakati lilipotea kabisa katika nchi hii madhubuti. Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, napenda kukupongeza wewe Mheshimiwa Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa mafanikio haya,” amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete ambaye amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, ameondoka Uganda mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo kwenda Mwanza, ambako atafanya ziara ya siku mbili kukagua shughuli za maendeleo katika mkoa huo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Gazeti la Raia Mwema la wiki hii ya Oktoba 8-14 ambalo limetolewa jana, Jumatano, Oktoba 8, 2014, limeandika kwenye ukurasa wake wa kwanza habari yenye kichwa cha habari, “Mwekezaji aliyemzawadia saa Kikwete aibua utata”.
Kichwa cha habari hicho kinafuatiwa na habari yenyewe ambayo kwenye moja ya aya zake inadai kuwa “tayari Rais Kikwete amekutana na mwekezaji huyo wa Marekani, Bwana Roberk Shumake na kumpa zawadi ya saa aina ya Rolex katika mojawapo ya ziara za Rais nchini Marekani”.
Hii ni habari ya uongo na haiwezi kuwa ya uongo zaidi kuliko ilivyochapishwa. Ni habari ya uzushi na upuuzi. Ni habari inayolenga kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwamba amepokea zawadi kutoka kwa mtu ambaye anajaribu kupewa kandarasi ya kujenga usafiri wa treni jijini DSM na ambaye pia anahusishwa kwenye shughuli nyingine za kibiashara zenye utata huko kwao Marekani.
Rais Kikwete hakuwahi kupewa wala kupokea saa ya aina ya Rolex kutoka kwa Bwana Shumake ama kutoka kwa mfanyabiashara mwingine yoyote. Alichopewa Mhe. Rais na Balozi huyo wa Heshima anayewakilisha Tanzania katika jimbo la Illinois ni saa ya kumbukumbu ya mji wa Detroit ambako ndiko nyumbani kwa Bw. Shumake (Souvenir watch), sio saa ya aina ya Rolex kwa matumizi binafsi ya Mhe. Rais. Saa hiyo ya kumbukumbu ni mali ya Tanzania.
Na wala siyo hulka wala tabia yake ya kupokea zawadi kutoka kwa watu wanaotafuta fursa za kuwekeza katika Tanzania. Isitoshe kwa nafasi yake kama Rais hahitaji kupewa saa na watu wa nje kwa sababu mahitaji yake yote ya mavazi na mengine hutolewa kwake na Taifa analoliongoza.
Ni jambo la kusikitisha sana kuwa gazeti la hapa nyumbani linaweza, bila ushahidi wowote na kwa kukariri habari kutoka kwenye mitandao ya kijamii, kuamua kuchapisha habari yenye kulenga kumdhalilisha kiongozi wa Taifa letu, tena kwa kumhusisha na zawadi ya kipuuzi kama saa aina ya Rolex.
Ni matarajio yetu kuwa Gazeti hilo litaombwa kutoa ushahidi wa habari hiyo, ili kuondoa utata ambao dhahiri utajitokeza kutokana na kuchapishwa kwa habari hiyo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Gazeti la Raia Mwema la wiki hii ya Oktoba 8-14 ambalo limetolewa jana, Jumatano, Oktoba 8, 2014, limeandika kwenye ukurasa wake wa kwanza habari yenye kichwa cha habari, “Mwekezaji aliyemzawadia saa Kikwete aibua utata”.
Kichwa cha habari hicho kinafuatiwa na habari yenyewe ambayo kwenye moja ya aya zake inadai kuwa “tayari Rais Kikwete amekutana na mwekezaji huyo wa Marekani, Bwana Roberk Shumake na kumpa zawadi ya saa aina ya Rolex katika mojawapo ya ziara za Rais nchini Marekani”.
Hii ni habari ya uongo na haiwezi kuwa ya uongo zaidi kuliko ilivyochapishwa. Ni habari ya uzushi na upuuzi. Ni habari inayolenga kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwamba amepokea zawadi kutoka kwa mtu ambaye anajaribu kupewa kandarasi kujenga usafiri wa treni jijini DSM na ambaye pia anahusishwa kwenye shughuli nyingine za kibiashara zenye utata huko kwao Marekani.
Rais Kikwete hakuwahi kupewa wala kupokea saa ya aina ya Rolex kutoka kwa Bwana Shumake ama kutoka kwa mfanyabiashara mwingine yoyote. Alichopewa Mhe. Rais na Balozi huyo wa Heshima anayewakilisha Tanzania katika jimbo la Michigan ni saa ya kumbukumbu ya mji wa Detroit ambako ndiko nyumbani kwa Bw. Shumake (Souvenir watch), sio saa ya aina ya Rolex kwa matumizi binafsi ya Mhe. Rais. Saa hiyo ya kumbukumbu ni mali ya Tanzania.
Na wala siyo hulka wala tabia yake ya kupokea zawadi kutoka kwa watu wanaotafuta fursa za kuwekeza katika Tanzania. Isitoshe kwa nafasi yake kama Rais hahitaji kupewa saa na watu wa nje kwa sababu mahitaji yake yote ya mavazi na mengine hutolewa kwake na Taifa analoliongoza.
Ni jambo la kusikitisha sana kuwa gazeti la hapa nyumbani linaweza, bila ushahidi wowote na kwa kukariri habari kutoka kwenye mitandao ya kijamii, kuamua kuchapisha habari yenye kulenga kumdhalilisha kiongozi wa Taifa letu, tena kwa kumhusisha na zawadi ya kipuuzi kama saa aina ya Rolex.
Ni matarajio yetu kuwa Gazeti hilo litaombwa kutoa ushahidi wa habari hiyo, ili kuondoa utata ambao dhahiri utajitokeza kutokana na kuchapishwa kwa habari hiyo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais amwomboleza Meja Jenerali Muhidin Kimario
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, kuomboleza kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, Waziri Mwandamizi wa Zamani wa Serikali na Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF).
Aidha, Rais Kikwete amewatumia pole nyingi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange na familia ya Meja Jenerali Kimario kufuatia kifo hicho kilichotokea mchana wa leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, nchini India, ambako alikuwa anapata matibabu.
Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo kwa Waziri Mwinyi: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, ambaye alilitumikia Jeshi letu kwa heshima kubwa na weledi wa kuigwa na baadaye kulitumikia Taifa letu kwa uaminifu na uadilifu wa kujivunia katika nafasi ya uwaziri.”
Ameongeza Rais Kikwete katika rambirambi zake: “Uhodari na ujasiri ule ule ambao Meja Jenerali Kimario aliuonyesha akiwa askari na ofisa mkuu ndio ule ule uliomwongoza katika utumishi wa umma na kwa nafasi zote za waziri mwandamizi, ambazo alizishikilia katika maisha yake iwe ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mkuu wa Mkoa ama Mkurugenzi wa Ustawishaji wa Makao Makuu (CDA). Daima tutakosa uongozi na ushauri wake.”
“Nakutumia wewe Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo hiki. Aidha, kupitia kwako, namtumia pole nyingi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Jeshi letu lote kwa kuondokewa na ofisa mwenzao, kiongozi wao na mpiganaji mwenzao,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Aidha, kupitia kwako, natuma salamu zenye huzuni nyingi kwa familia ya Meja Jenerali Muhidin Kimario. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa wa kuondokewa na mhimili wa familia. Vile vile wajulishe kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Marehemu. Amin.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Msiingize dini katika siasa, Rais awaambia mabalozi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kuna ushahidi sasa unaothibitisha kuwa baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wamekuwa wanachaganya dini na ziasa wakitumia dini kuunga mkono baadhi ya vyama vya siasa na shughuli za kisiasa nchini.
Aidha, Rais Kikwete amewaomba mabalozi hao “kuiokoa” Tanzania katika majanga makubwa yanayoweza kuipata kwa kutumia dini kuendeleza siasa, hatua ambayo ameielezea kama “njia ya hatari kweli kweli.”
Rais Kikwete alikuwa anazungumza usiku wa jana, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, wakati wa chakula cha usiku ambacho alikula na viongozi wa dini nchini ambao wanaendelea na mkutano wao wa mwaka kwenye Hoteli ya White Sands ya Dar Es Salaam.
Mkutano huo wa siku nne ulioanza jana unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence ni mwendelezo wa mikutano ya viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini. Mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka juzi, 2012 kwenye Hoteli hiyo hiyo.
Aidha, Mkutano huo ambao moja ya wadhamini wake ni taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, unahudhuriwa na mabalozi 15 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na mashirika kadhaa ya kimataifa likiwemo lile la Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Mkutano huo ni wa Ujerumani, Iran, Marekani, Norway, Uturuki, Sweden, Canada, Denmark, Finland, Misri, Qatar, Uswisi, Palestina, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia na Umoja wa Ulaya (EU).
Viongozi wa dini wanaoshiriki katika Mkutano huo wanatoka Zanzibar, Dar Es Salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Lindi, Arusha, Geita na Mbeya.
Akizungumza kwenye chakula hicho cha usiku, Rais Kikwete aliungana na Mshauri Mkuu wa PROCMURA ambaye alionya kuhusu hatari za kweli zinazoendelea kuikabili dunia kwa sababu ya kuingiza dini katika siasa (Politicisation of Religion) na kuingiza siasa katika dini (Religinasation of Politics).
Rais Kikwete amewaambia viongozi hao: “Mwakilishi wa PROCMURA ametoa ujumbe mzito sana. Ametoa fumbo ambako amewaasa mabalozi wasiingize dini katika siasa na wasiingize siasa katika dini. Na mimi nataka kuungana naye na kuwaomba mabalozi waiokoe nchi yetu katika majanga makubwa yanayoweza kutokana na kutumia dini kuendeleza siasa. Ni njia ya hatari kweli kweli.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Kuna ushahidi sasa kuwa baadhi yetu, baada ya kushindwa kutumia ukabila katika kuendeleza siasa, sasa mmegeukia dini.Mnatumia dini katika kuunga mkono baadhi ya shughuli za kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
7 Oktoba, 2014.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea huzuni na masikitiko yake kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuia ya Madola (CPA), Mheshimiwa Dkt. William Shija.
Dkt. Shija aliyefariki dunia Jumamosi asubuhi mjini London, Uingereza, ambacho ndicho kilikuwa kituo chake cha kazi, alisomea na kuwa mhadhiri wa uandishi wa habari kabla ya kuwa mbunge wa Sengerema kwa miaka 15 mfululizo na Waziri Mwandamizi wa Serikali katika Wizara mbali mbali.
Katika salamu zake kwa Sekretarieti ya CPA, Kanda ya Afrika, Rais Kikwete amesema kuwa amestushwa sana na kifo cha Dkt. Shija ambacho kimeinyang’anya Afrika na dunia, na hasa Tanzania na Jumuia ya Madola, mtumishi mwadilifu na mwaminifu, ambaye alitoa maisha yake kwa utumishi wa umma.
“Alikuwa kiongozi mfano katika nafasi zote za umma alizozishikilia. Aliifanya kazi yake ya uhadhiri wa uandishi wa habari kwa ufanisi mkubwa na aliwapa utumishi uliotukuka wananchi wake wa Sengerema katika nafasi yake ya Ubunge. Dkt. Shija alitumainiwa sana katika nafasi zote nyingi na za uandamizi za Uwaziri wa serikali,” amesema rais Kikwete na kuongeza:
“Nawatumieni salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Dkt. Shija na naungana nanyi katika kumlilia. Kupitia kwenu, nawatumia wajumbe wote wa CPA na Sekretarieti ya Chama hicho pole nyingi sana kwa kuondokewa na kiongozi na mtendaji wao mkuu. Aidha, naomba pia mniwasilishie pole zangu kwa wana-Sengerema ambao Dkt. Shija aliwatumikia kwa uaminifu na kwa miaka mingi.”
“Wajulisheni wote kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa na naomboleza nao na niko nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweka peponi roho ya Marehemu William Shija. Amin.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Oktoba, 2014.