Taarifa kwa vyombo vya Habari ya zamani
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuombeleza kifo cha mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Mafia, Mkoa wa Pwani, Kanali (mst) Ayubu Shomari Mohamed Kimbau, ambaye aliaga dunia asubuhi ya leo, Jumapili, Agosti 30, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Katika salamu za rambirambi alizomtumia Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo, Rais Kikwete ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa za kifo cha Mzee Kimbau ambaye kwa miaka mingi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mafia kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Amesema Rais Kikwete katika salamu zake: “Nimesikitishwa na taarifa za kuaga dunia kwa Mzee Ayubu Kimbau ambaye nimejulishwa kuwa amefariki asubuhi ya leo katika Hospitali ya Muhimbili. Mzee Kimbau atakumbukwa sana kwa utumishi wake wa umma na uzalendo wake kwa taifa lake kuanzia alipokuwa katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambako alipanda nafasi hadi kufikia cheo cha Kanali na baadaye katika uwakilishi wa wananchi wa Mafia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
“Kupitia kwako, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, naungana na wananchi wote wa Mafia na wa mkoa wa Pwani kuomboleza kifo cha mmoja wa magwiji wa siasa na wauwakilishi wa wananchi katika nchi yetu. Nawaombeni mpokee salamu zangu za dhati ya moyo wangu katika kuomboleza kifo hiki,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Aidha, kupitia kwako naitumia familia ya Kanali Kimbau salamu zangu nyingi za pole. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa na kuwa msiba wao ni msiba wangu. Naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kuwapa nguvu, uvumilivu na subira. Naungana nao pia kumwomba Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Kanali Ayubu Shomari Mohamed Kimbau. Amen.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
30 Agosti, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Jumamosi, Agosti 29, 2015, ameungana na mapadre na waumini wa Kanisa Katoliki na wananchi wa mji mdogo wa Lugoba, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, kusherehekea miaka 50 ya utawa wa Sista Perpetua Mlamwaza.
Rais Kikwete amewasili kwenye Ukumbi wa Mkulima,Lugoba kiasi cha saa saba unusu mchana kuungana na wananchi hao katika sherehe ambako pia alikuwa anapongezwa Sista Ponsiana wa Paroko hiyo hiyo yaLugoba kwa kufikisha miaka 25 yanadhiri ya usista.
Miongoni mwa waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na baba mzazi wa Sista Perpetua, Mzee Ariseni, pamoja na dada yake mkubwa na wadogo zake.
Masista hao wawili wanatoka Parokia ya Lugoba, eneo ambako shughuli za Kanisa Katoliki ziliingia kiasi cha miaka 100 iliyopita na Sista Perpetua alikuwa msichana wa kwanza wa Parokia ya Lugoba kujiunga na utawa wa Kanisa Katoliki alipoweka nadhiri ya kwanza mwaka 1965 kuwa Mtawa wa Shirika la Moyo Safi wa Maria Mgolole na kuweka nadhiri ya kudumu,miaka tisa baadaye, mwaka 1974.
Katika risala yao kwa Sr. Perpetua, wananchi wa Lugoba wamempongeza Sista huyo kwa “safari ndefu ya maisha ya kumtumikia Mungu kwa sababu safari hiyo siyo ya mchezo…ina mabonde na milima, furaha na machungu na yote wewe Sr umeyashinda yote hayo katika miaka 50 iliyopita. Tunakupongeza sana kwa kututoa kimasomaso”
Sista Perpetua mwenye umri wa miaka 72, alizaliwa katika Kijiji cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani baba yake akiwa Mzee Arisenina mama yake akiitwa Maria Nyau (Mama wa Mungu) ambao kwa pamoja walimpa binti yao jina la Marystella.
Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Kikwete amempongeza sana Sr. Perpetua kwa ujasiri wake wa kuingia katika utawa katika kipindi na nyakati ambako uelewa wa watu wa eneo hilo ulikuwa tofauti sana na sasa. “Wakati huo, uamuzi wa namna hiyo haukuwa uamuzi rahisi hata kidogo. Ulikuwa uamuzi mgumu lakini dada yangu Perpetua aliufanya uamuzi huo.”
Aidha Rais Kikwete ameongeza: “Nakupongeza pia kwa kuchagua maisha ya kujinyima na kuwatumikia watu. Ungeweza kabisa kuchagua maisha ya kubadili magauni kila siku na kwenda saluni, lakini hukuyataka maisha ya namna hiyo. Umetuletea heshima sana kwa uamuzi wako huu. Tunakushukuru na kukupongeza.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
30 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Said Meck Sadik kufuatia vifo vya watu tisa wa familia moja ya Bwana Masoud Matal vilivyotokea alfajiri ya tarehe 27 Agosti, 2015 kwa ajali ya moto.
Wanafamilia hao wakiwemo watoto watano walipoteza maisha baada ya nyumba yao iliyoko katika Mtaa wa Gulam, eneo la Buguruni Malapa katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kuungua na kuteketea kabisa kwa moto. Baba wa familia, Bwana Masoud Matal alisalimika kwa vile hakuwamo katika nyumba hiyo wakati ikiungua.
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na nimesikitishwa mno kutokana na taarifa za kupoteza maisha kwa watu tisa wa familia moja ya Bwana Masoud Matal baada ya nyumba yao kuunguzwa na kuteketezwa kabisa na moto alfajiri ya tarehe 27 Agosti, 2015”, amesema kwa huzuni Rais Kikwete akiomboleza vifo vya wanafamilia hao.
“Kwa hakika hili ni pigo kubwa kwa Bwana Masoud Matal, lakini namuomba awe mvumilivu kwa machungu yote ya kupotelewa ghafla na familia nzima, lakini yote amwachie Mwenyezi Mungu muweza wa yote”, ameongeza kusema Rais Kikwete.
Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amemwomba Mheshimiwa Sadik kumfikishia Salamu zake za rambirambi na pole nyingi kwa Bwana Masoud Matal kutokana na msiba huo mkubwa uliompata, na amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Mahala Pema Peponi Roho za Marehemu wote, Amina.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
28 Agosti,2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
RaiswaJamhuriyaMuunganowa Tanzania, MheshimiwaJakayaMrishoKikweteamesemakuwaniwajibuwaMikoanaSerikalizaMitaakusimamiachangamotonamapungufukatikausimamiziwaujenziwabarabaranchinikamavile kuwepokwatuhumazarushwakatikautoajiwakazizabarabaranaucheleweshajiwautekelezajiwakazizaujenziwabarabarakwavisingiziovinavyotokananamipangiliomibovu.
Aidha, RaisKikweteamesemakuwaniwajibuwangazihizozauongozikuhakikishakuwakazizabarabarahazifanyikikwaviwangoduninakukomeshauwepowaupendeleokatikauteuziwawakandarasiwakazizaujenziwabarabarakinyume cha SheriayaManunuzi.
RaisKikwetealikuwaanafunguaMkutanowaNnewaMwakawaMaofisawaOfisiyaWaziriMkuu – Tamisemi, BodiyaMfukowaBarabaranaWadauwaBarabarazaMamlakayaSerikalizaMitaaunaohudhuriwanaWakuuwaMikoayotenchininawilayazotekwenyeUkumbiwaMikutanowaHoteliyaNgurdoto, Arusha, Jumatatu, Agosti 24, 2015.
RaisKikweteamewaambiaviongozihaokuwakuondoamigonganoyamaslahikwabaadhiyawataalamnaviongoziwahalmashaurikatikausimamiziwabarabaranakukomeshausimamizidunikatikakazizaujenzinamatengenezoyabarabara.
Amewaambiawashirikiwamkutanohuo: “ZipochangamotozausimamizizitokanazonamapungufukatikangaziyaMkoanaSerikalizaMitaaukiwemoucheleweshajiwautekelezajiwakazizaujenziwabarabarakwavisingiziombalimbalivitokanavyonamipangiliomibovunaujenziwabarabarakwaviwangoduniikilinganishwanaviwangovilivyomokatikamikatabayaujenziwabarabarahizo.”
MkutanohuounajadilibarabarazinazosimamiwanaSerikalizaMitaazikiwemobarabarazamijininavijijiniambazoRaisKikweteamesemakuwanimuhimusanailikazikubwayaujenziwabarabarakuuiliyofanywanauongoziwaSerikaliyasasayaAwamuyaNneionekaneyamaana.
“IpopiachangamotoyakuteuamakandarasiwakazizabarabarakwaupendeleokinyumenaSheriayaManunuzinahivyokupatawakandarasiwasiokuwanauwezonatuhumakubwazarushwakatikautoajiwakazizaujenziwabarabara,”amesemaRaisKikwetenakuongeza:
“Changamotonyingineambazonyiekamaviongozimnawajibuwakukabiliananazonipamojanatuhumazakuwepokwamgonganowamaslahikwabaadhiyawataalamnaviongoziwahalmashaurimbalimbalinchinikatikausimamiziwakaziyabarabaranausimamiziduniwaujenzinamatengenezoyabarabarazenyewe, wenginekwauzembenawenginekwamakusudi.”
AmesisitizaRaisKikwete: “Majawabuyachangamotohizoyakondaniyamamlakanauwezowenukuyatatua, maanayanatendekambeleyamachonipenunakatikataasisimnazozisimamia. Ninawakumbushanakuwasisitiziaviongozinawatendajiwotewahalmashaurikutimizawajibuwenu. Wajibuhuondiosababuyaninyikuwemokatikanafasizauongozinautendajimlizonazo.”
RaisKikweteataondokaArushaleo, Jumanne, Agosti 25, 2015 kwendaMwanzanabaadayeTangakablayakurejea Dar es salaam jioni.
Imetolewana:
KurugenziyaMawasilianoyaRais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamilioni ya Watanzania sasa wanufaika na huduma za kifedha –BOT
BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imetaja mafanikio makubwa manane ya maendeleo ya huduma za kifedha na za kibenki katika Tanzania katika miaka 10 iliyopita, ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa katika idadi ya Watanzania wanaofikiwa na huduma rasmi za kifedha za kibenki na zisizokuwa za kibenki ambayo limepaa kutoka asilimia tisa mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 57.6 mwaka juzi, 2013.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imesema kuwa imeamua kujenga tawi kubwa la benki hiyo katika Mkoa wa Mtwara kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya kiuchumi ambayo yanayotokea katika mkoa huo na mkoa jirani wa Lindi, mikoa ambayo kwa miaka mingi ilikuwa inafikiriwa kuwa nyuma zaidi katika maendeleo katika Tanzania.
Hayo yamesemwa , Jumapili, Agosti 9, 2015 na Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndullu, wakati akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tawi la BOT katika mji wa Mtwara. Rais Kikwete ameweka jiwe hilo ikiwa ni sehemu ya shughuli zake nyingi wakati wa ziara yake ya siku moja ya kikazi mkoani Mtwara.
Ujenzi wa jengo la tawi la BOT mjini Mtwara ulianza Oktoba mwaka juzi, 2013 na unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu, 2015 kabla ya shughuli rasmi kuanza kwenye tawi hilo Juni mwakani, 2016 kwa watumishi 60 wa awali. Tawi hilo litakuwa tawi la sita la BOT kufuatia matawi ya Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar.
Profesa Ndullu amemwambia Rais Kikwete kuwa yamekuwepo mafanikio makubwa manane dhahiri katika maendeleo ya kibenki na kifedha katika miaka 10 iliyopita chini ya uongozi wa Rais Kikwete, ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la Watanzania ambao wanafikiwa na huduma za kifedha za kibenki ama zisizokuwa za kibenki ambazo sasa zinawafikia Watanzania asilimia 57.3 kulinganisha na asilimia tisa mwaka 2006.
“Kati ya mwaka 2009 na 2013, kwa mfano, idadi ya Watanzania wasiopata huduma yoyote ya kifedha ilipungua kwa kasi sana kutoka asilimia 55.4 ya watu wazima hadi kubakia asilimia 26.8. Yote haya yamepatikana kutokana na matumizi ya teknolojia ya kidigitali yaliyowezesha kupungua kwa gharama za huduma za kifedha kwa kiwango kikubwa sana,” Gavana Ndullu amemwambia Rais Kikwete.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa katika kipindi hicho, huduma za kibenki zimepanuka sana akisema kuwa mwaka 2006 idadi ya Watanzania waliokuwa wanatumia huduma za kibenki walikuwa milioni 1.5 idadi ambayo ilipanda na kufikia watu milioni 3.3 mwishoni mwa mwaka juzi 2013.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa kumekuwepo na uimarikaji wa usimamizi wa sekta ya fedha ambako kumewezesha kuanzishwa na kuwepo kwa taasisi nyingi za kutoa mikopo midogo midogo kwa wananchi, mkopo ambayo inatilia maanani hali halisi na kwa ajili ya wajasiriamali na inayochangia kwa kiwango kikubwa kupunguza umasikini.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa kuwa idadi ya mabenki na taasisi nyingine za fedha imeongezeka mno nchini kufikia mabenki na taasisi 57, zikiwemo benki mbili za maendeleo za Tanzania Investment Bank (TIB) na Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) ambayo Rais Kikwete aliizundua rasmi wakati wa sherehe za Siku ya Nanenane mkoani Lindi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa limekuwepo ongezeko kubwa la huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambayo alisema kuwa hadi Machi, mwaka huu, 2015, idadi ya akaunti zake ilifikia milioni 40.7.
“Watanzania milioni 26.8 ama asilimia 95 ya Watanzania watu wazima walikuwa na akaunti kwenye simu zao hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka huu. Kati ya hizo akaunti milioni 15, sawa na asilimia 55 zilikuwa zinatumika mara kwa mara (active accounts),” amesema Gavana Ndullu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
10 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali imenunua vivuko vingi zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuliko vivuko ambavyo vilipata kununuliwa katika miaka 45 kabla ya mwaka 2005 wakati Rais alipoingia madarakani.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemwambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa katika miaka 10 iliyopita wakati Tanzania ikiwa chini ya uongozi wa Rais Kikwete, Wizara ya Ujenzi imejenga vivuko 15 vipya kulinganisha na 13 tu vilivyokuwepo mwaka 2005 wakati Serikali ya Rais Kikwete inaingia madarakani na hivyo kuifanya Tanzania kuwa na vivuko 28 vya uhakika na salama kwa matumizi ya wananchi.
Aidha, Waziri Magufuli amewaambia wananchi wa Mtwara kuwa katika kipindi hicho cha miaka 10, Serikali imefanya ukarabati mkubwa wa vivuko saba na kuwa ukarabati huo umegharimiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Rais Kikwete.
Waziri Magufuli ametoa maelezo hayo Jumapili, Agosti 9, 2015 wakati alipomkabidhi Rais Kikwete kivuko kipya cha MV Mafanikio kinachotoa huduma kati ya Mji wa Mtwara na eneo la Msangamkuu, mkoani humo katika mkutano uliofanyika Msangamkuu na kuhudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi.
Rais Kikwete amefanya uzinduzi wa MV Mafanikio katika sherehe iliyofanyika mjini Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kazi katika Mkoa huo ambako amewasili asubuhi akitokea Mkoa wa Lindi, ambako alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili. Mara baada ya uzinduzi huo, Rais Kikwete akiambatana na Mama Salma Kikwete, Waziri Magufuli, mawaziri kadhaaa na viongozi wa Mkoa wa Mtwara wamepanda kivuko hicho kwenda Msangamkuu ambako wamefanya mkutano wa hadhara wa wananchi.
Kivuko cha MV Mafanikio ni matokeo ya ahadi ya Rais Kikwete wakati wa kampeni ya urais mwaka 2010, na kina uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita na kimegharimu kiasi cha sh bilioni 3.3.
Kivuko hicho ambacho kimejengwa na Kampeni ya Songoro Marine Transport Ltd Boatyard ya Mwanza, baada ya wajenzi wake wa kwanza kutoka Uholanzi kushindwa na kukimbia nchi, kinasafiri kwa dakika saba tu kati ya Mtwara Mjini na Msangamkuu.
Kivuko hicho ambacho Waziri Magufuli amekielezea kama ukombozi mkubwa kwa wananchi, kinaondoa adha na kero ya wananchi wa Msangamkuu ambao walikuwa wanalazimika kuweka maisha yao hatarini kwa kuvuka eneo hilo la Bahari ya Hindi kwa boti ndogo ndogo ama kufanya safari ya mzunguko wa kilimota 21 ili kwenda mjini Mtwara kupata huduma zao. Kata ya Msangamkuu ina wakazi wanaokadiriwa kufikia 12,000.
“Nawapeni pole sana kwa sababu najua wako ndugu zetu wengi ambao wamepoteza maisha yao katika eneo hili kwa sababu ya usafiri uliokuwa unatumika hapa kwa miaka mingi,” Waziri Magufuli amewaambia wananchi hao wa Msangamkuu mbele ya Rais Kikwete.
Waziri Magufuli pia amemwambia Rais Kikwete na wananchi wa Mtwara kuwa Serikali imeamua kuwa wanafunzi wote wenye sare pamoja na wananchi wenye ulemavu watakuwa wanavuka bure kwa kutumia kivuko hicho chenye urefu wa mita 33.
Aidha, Waziri Magufuli amemwambia Rais Kikwete na wananchi wa Msangamkuu kuwa sambamba na kivuko hicho, Serikali pia imenunua na kuweka kivuko kipya cha MV Kilambo kwenye mpaka wa Tanzania na Mozambique katika Mto Ruvuma katika Mkoa wa Mtwara.
Waziri Magufuli amesema kuwa vivuko vilivyojengwa katika miaka 10 iliyopita ni MV Kilombero kinachoa huduma kwenye Mto Kilombero, Mkoa wa Morogoro, chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita kwa wakati mmoja; MV Ruhuhu kinachotoa huduma kwenye Mto Ruhuhu, Mkoa wa Ruvuma, chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Misungwi kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi, Mkoa wa Mwanza, chenye uwezo wa kubeba tani 250, abiria 1,000 na magari 36 na MV Magogoni kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni, Dar es Salaam chenye uwezo wa kubeba tani 500, abiria 2000 na magari 60.
Waziri Magufuli ametaja vivuko vingine kuwa ni MV Kome 11 kinachotoa huduma kati ya Nyakalilo na Kome, Mwanza na chenye uwezo wa kubeba tani 40, abiria 100 na magari manne; MV Pangani kinachotoa huduma kati ya Pangani na Mbweni, Tanga, chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Utete 11 kinachotoa huduma kwenye Mto Rufiji, Pwani na chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Kisorya na Rugezi, Wilaya ya Ukerewe, Mwanza chenye uwezo wa tani 85, abiria 330 na magari manane.
Vivuko vingine vilivyotanjwa na Waziri Magufuli ni MV Musoma kinachotoa huduma kati ya Kinesi na Musoma, Mkoa wa Mara na chenye uwezo wa tani 85, abiria 330 na magari manane; MV Ruvuvu kinachotoa huduma kati ya Rusumo na Nyakiziba, Ngara, Kagera na chenye uwezo wa kubeba tani 35, abiria 80 na magari manne; MV Kilambo kinachotoa huduma kati ya Kilambo (Tanzania) na Namoto (Mozambique) mkoani Mtwara chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita.
Waziri Magufuli ametaja vivuko vingine kuwa ni MV Malagarasi kinachotoa huduma kati ya Ilagala na Kajeje, Kigoma, na chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Tegemeo kinachotoa huduma kati ya Maisome, Kahunda na Nkome, wilayani Sengerema, Mwanza na chenye uwezo wa kubeba tani 85, abiria 200 na magari 10, MV Dar es Salaam kinachotoa huduma kati ya Dar es salaam na Bagamoyo kwenye mwamboa wa Bahari ya Hindi chenye uwezo wa kubeba abiria 300 na MV Mafanikio kinachotoa huduma kati ya Mtwara Mjini na Msangamkuu.
Waziri Magufuli amesema kuwa vivuko vilivyofanyiwa ukarabati mkubwa ni MV Kigamboni (Dar Es Salaam) chenye uwezo wa kubeba tani 160, yaani abiria 800 na magari 22, MV Sengerema (Mwanza) chenye uwezo wa kubeba tani 179, yaani abiria 490 na magari 18,MV Chato (Geita) chenye uwezo wa kubeba tani 75, yaani abiria 200 na magari sita.
Vingine ni MV Ukara, chenye uwezo wa kubeba abiria 70, MV Sabasaba (Mwanza) chenye uwezo wa kubeba tani 85, abiria 300 na magari manane, MV Temesa (Mwanza) zamani kikiitwa MV Geita chenye uwezo wa tani 65, yaani abiria 120 na magari sita na MV Mara (Mara) zamani kikiitwa Kone 1, chenye uwezo wa tani 35, yaani abiria 60 na magari matatu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
10 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
UTEUZI NA UHAMISHO WA MABALOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:
(i) Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico
(iii) Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
11 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Benki hii ni mkombozi wa kweli wa mkulima – Rais Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete , Ijumaa, Agosti 7, 2015 amezindua rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), akiielezea Benki hiyo kama Mkombozi wa Kweli wa Mkulima na yenye nia ya kumaliza changamoto na kero ambazo kwa muda mrefu zimekwamisha maendeleo ya haraka katika sekta ya kilimo.
Rais Kikwete amesema kuwa uamuzi wake wa kuanzisha Benki ya Kilimo Tanzania unalenga kimsingi kumwezesha mkulima wa kawaida wa Tanzania kuweza kupata mikopo ya kuendeleza kilimo chake wakati wowote na mahali popote nchini.
Aidha, Rais Kikwete ametangaza kuwa Serikali yake tayari imewekeza mtaji wa sh. bilioni 60 katika Benki hiyo na kuwa katika miaka minane ijayo, Serikali itawekeza kiasi cha sh. bilioni 800, ikiwa ni uwekezaji wa mtaji wa kiasi cha sh.bilioni 100 kila mwaka, ili kuwawezesha mkulima wa Tanzania kunufaika na juhudi za jasho lao.
Vile vile, Rais Kikwete amesema kuwa imekuwa lazima kwa Serikali kuanzisha TADB kwa sababu kilimo ni biashara na biashara yoyote inahitaji mitaji ya kuweza kuiendeleza.
Rais Kikwete alitoa ufafanuzi huo alipozindua rasmi TADB katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) mjini Dar es Salaam siku ya Ijumaa, baada ya kuridhika kuwa uleaji wa shughuli za mikopo ya kilimo zilizokuwa zinafanywa na Benki ya Raslimali Tanzania (TIB) zimekomaa kiasi cha kuanzisha benki kamili ya kilimo.
Miaka michache iliyopita, Rais Kikwete aliagiza kuwa fedha zote zilizokuwa zimerudishwa Serikalini kutokana na sakata la Akaunti ya EPA katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT) zitumike kama raslimali ya kufungulia dirisha la mikopo ya kilimo katika TIB na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Benki ambayo Rais ameifungua ijumaa.
Katika maandalizi ya Benki hiyo, Rais Kikwete aliunda Bodi ya TADB Aprili mwaka juzi 2013 chini ya uenyekiti wa Ndugu Rosebud Violet Kurwijila na Agosti mwaka jana, 2014, Benki hiyo ikapata menejimenti ya awali kabla ya TADB kupewa leseni kamili ya kuendesha shughuli zake na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) , Alhamisi, Agosti 6, 2015.
Rais Kikwete amesema kuwa kwa kuanzia TADB itatoa mikopo katika minyoyoro 10 ya thamani (value chain) katika maeneo ya kilimo cha mahindi, mchele, miwa, mbegu za mafuta, kilimo cha matunda, maua na mbogamboga, ng’ombe wa maziwa na nyama, ufugaji wa kuku wa kienyeji, ufungaji wa samaki na ufugaji wa nyuki. “Lakini huo ni mwanzo tu,” Rais Kikwete alisema kwenye ufunguzi huo.
Rais Kikwete pia amekumbusha kuwa kilimo bado ni sekta kubwa na uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania kwa sababu asilimia 75 ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo kwa maisha yao, na kuwa kilimo kinachangia asilimia 25 ya pato la taifa na asilimia 34 ya mauzo ya Tanzania nje ya nchi.
Lakini Rais Kikwete amesema kuwa takwimu hizo zingekuwa kubwa zaidi kama changamoto zinazokabili kilimo zingelitatuliwa ikiwa ni pamoja na kuinua kiwango cha tija katika sekta hiyo.
Akitoa mifano, Rais Kikwete amesema kuwa uzalishaji wa mahindi ni tani 1.5 kwa hekta nchini kulinganisha na wastani wa tani 1.9 katika Afrika na tani 5.7 katika China. Uzalishaji wa mpunga ni tani mbili kwa hekta hapa nchini kulinganisha na wastani wa tani 5.5 katika Vietnam. Uzalishaji wa pamba nchini ni tani 300 kwa hekta wakati katika Afrika wastani ni tani 700 na Marekani ni tani 3,000.
Ameongeza kusema kuwa uzalishaji wa maziwa ya ng’ombe katika Afrika kwa wastani ni lita tatu kwa siku wakati New Zealand ni lita 20 kwa siku. N’gombe wa Tanzania wanazalisha wastani wa kilo 180 za nyama, wastani wa Afrika ni kilo 240 na katika New Zealand ni kilo 540 kwa ng’ombe mmoja.
Rais Kikwete amesema kuwa changamoto zinazolengwa kutatuliwa na kuanzishwa kwa benki hiyo ni matumizi ya zana duni za kilimo. “Katika Tanzania bado jembe la mkono linategemewa kwa asilimia 62, plau asilimia 24 na matrekta asilimia 14 tu. Kilimo cha Tanzania bado kinategemea mvua ya Mungu na umwagiliaji ni mdogo sana. Eneo linalomwagiliwa ni hekta 461,326 na ukilinganisha na hekta milioni 29 zinazoweza kumwagiliwa.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Wakuliwa wanatumia mbegu duni za asili. Matumizi ya mbolea ni kilo 13 tu kwa hekta wakati katika Uholanzi ni kilo 577 kwa hekta. Mazao mengi hupotea kwa mimea kuathiriwa na maradhi na wadudu na wakulima wetu wana maarifa na ujuzi mdogo wa kilimo na ufugaji wa kisasa.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
8 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ni aibu kwa Serikali kuwakopa wakulima masikini kwa ujanjaujanja –
Rais Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka maofisa wa Serikali kuacha kabisa tabia ya kuwakopa wakulima masikini nchini kwa ujanjaujanja kwa kusingizia kuwa hawana fedha ya fidia mali zao ili kupisha ujenzi wa miradi mbali mbali ya Serikali.
“Nimepata kulisema hili lakini nataka kulirudia tena, Serikali haiwezi kuendelea kuwakopa wakulima masikini kwa visingizio kuwa haina wala haijapata fedha za kufidia mali za wananchi kupisha miradi ya Serikali. Ni jambo la aibu kabisa kwa Serikali kuwakopa wakulima masikini,” amesema Rais Kikwete
“ Serikali hii haiwezi kufidiwa na masikini. Mnavunja nyumba za watu, mnaangusha minazi yao, mnakata miembe yao kwa kuwaambia kuwa hamna fedha za kuwalipa fidia ili kupisha miradi ya maendeleo ama kuwa fedha hizo zimechelewa. Ni aibu kwa Serikali kuwakopa masikini. Hata mimi ningejua kuwa mnataka kupitisha mradi bila kunifidia ningekataa kuwaruhusu kupitisha mabomba ya mradi shambani kwangu,” amesema Rais Kikwete.
Rais alikuwa anazungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mradi mkubwa wa maji katika eneo la Ng’apa, nje kidogo ya mji wa Lindi, ambako Rais amelalamikiwa na maofisa wa Serikali kuwa mradi huo ulichelewa kuanza kwa sababu baadhi ya watu waligoma mabomba ya mradi yasipitishwe kwenye maeneo na mashamba yao kwa sababu walikuwa hawajalipwa fidia.
“Haya ni mawazo ya ovyo ovyo sana kwa maofisa wa Serikali kwamba mnaweza kuharibu mali za watu bila kuwalipa fidia. Ni aibu kubwa. Achaneni na mawazo haya. Badala ya kuwasaidia wakulima na wananchi masikini tunawalazimisha kupitisha nguzo za umeme ama mabomba ya maji kwenye mashamba yao bila kuwalipa fidia,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Hakuna mradi unaoandaliwa bila kutilia maanani fidia ya watu. Pangeni mambo yenu vizuri siyo kudhulumu watu. Watu hawa ni masikini . Hata kama nyumba zao ni za makuti, hata kama ana mnazi mmoja ama mwembe mmoja bado ni mali yake anayo haki ya kunufaika nayo. Hatuwezi kuikata bila kumlipa fidia. Hili naomba lisirudiwe, popote nchini. Ni marufuku kwa Serikali kusaidiwa na masikini. Serikali haiwezi kufanya hivyo. Hii ni changamoto ya aibu.”
Mradi wa maji wa Ng’apa unalenga kuchimba visima 10 kwa ajili ya kuwaongezea huduma ya maji safi na salama wakazi wa mji wa Lindi na baadhi ya vitongoji vyake ambao kwa sasa wanapata kiasi cha lita milioni 2,466 kwa siku. Mradi huo utaongeza kiasi cha lita milioni 7,500 za maji kwa ajili ya wakazi 82,000 wa maeneo hayo.
Mradi huo ulioanza kujengwa Machi 18, mwaka juzi, 2013 lakini kwa sababu mbali mbali mradi huo umekuwa unacheleweshwa kumalizika. Mradi huo ulikuwa ujengwe kwa miezi 24 na umalizike Machi mwaka huu lakini inakadiriwa kuwa sasa utamalizika mwezi ujao.
Mradi huo wa Ng’apa unaojengwa kilomita 12 kutoka mjini Lindi unajengwa kwa kiasi cha Euro milioni 11.6 na unagharimiwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya (EU) na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika lake la misaada ya maendeleo ya kimataifa la KFW chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Milenia. EU unagharimia mradi huo kwa asilimia 85 na Serikali ya Ujerumani kwa asilimia 15.
Mradi huo wa maji wa Ng’apa ni moja ya miradi mitano inayogharimiwa kwa pamoja na EU na Serikali ya Ujerumani katika Tanzania. Miradi mingine iko katika miji ya Babati, Kigoma, Sumbawanga na Mtwara.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
8 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali yamaliza kero ya Barabara ya Kusini
HATIMAYE Serikali imekalimisha ujenzi wa Barabara ya Kusini yenye urefu wa kilomita 504, ambayo kwa miaka na miaka imekuwa kero kubwa kwa wananchi wa mikoa minne, kufuatia kuzinduliwa kwa kipande cha kilomita 60 cha kati ya Ndundu na Somanga katika sherehe iliyofanyika , Ijumaa, Agosti 7, 2015.
Aidha, kuzinduliwa kwa kipande hicho cha barabara kumeiwezesha Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kukamilisha ujenzi wa miradi 13 mikubwa katika Ukanda wa Maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor).
Vile vile, kwa kukamilisha kipande hicho cha barabara ambayo ni sehemu ya Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Kibiti-Lindi hadi Mingoyo, kunaifanya Serikali ya Awamu ya Nne kutumia kiasi cha shilingi trilioni tisa katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Kikwete.
Kilomita 60 za Ndundu-Somanga ni sehemu pekee iliyokuwa imebakia katika kukamilisha ujenzi, kwa kiwango cha lami, barabara kuu iendayo mikoa ya kusini ambayo kabla na baada ya uhuru imekuwa kero kwa wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara.
Sherehe ya uzinduzi wa kipande hicho cha barabara umefanywa na Rais Kikwete katika eneo la Marendego, Wilaya ya Kilwa, mpakani kwa mikoa ya Pwani na Kilwa na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wakiwemo mawaziri na Naibu Mawaziri sita akiwemo Waziri wa Ujenzi John Pombe Joseph Magufuli.
Akizungumza katika sherehe hiyo kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete kuzindua barabara hiyo, Waziri Magufuli amesema kuwa chini ya uongozi wa Rais Kikwete,miradi 13 mikubwa ya barabara imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika Ukanda wa Maendeleo wa Mtwara ambao unaunganisha nchi za Tanzania, Malawi na Mozambique.
Waziri Magufuli ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Daraja la Umoja ambao umekamilika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Songea-Namtumbo yenye kilomita 72 ambao umekamilika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Peramiho Junction-Mbinga yenye kilomita 78 ambao umekamilika na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi yenye urefu wa kilomita 200 ambao umekamilika na ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Masasi-Mangaka yenye kilomita 54 ambao umekamilika.
Miradi mingine ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala yenye kilomita 65.5 ambao unaendelea, ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Mangaka-Nakapanya wenye kilomita 70.5 ambao unaendelea, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Nakapanya-Tunduru wenye urefu wa kilomita 66.5 ambao unaendelea, ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Tunduru-Matemanga yenye kilomita 58.7 ambao unaendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Matemanga-Kilimasera yenye urefu wa kilomita 68.2 ambao unaendelea.
Waziri Magufuli ameitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Kilimasera-Namtumbo wenye kilomita 60.7 ambao unaendelea, upembuzi yakinifu wa barabara ya Mtwara-Newala-Masasi yenye kilomita 221 ambao umekamilika na tenda tayari imetangazwa kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami cha sehemu ya Mtwara-Mnivata yenye kilomita 50, maandalizi ya nyaraka ya zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay wenye kilomita 66 ambao unagharimiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Waziri Magufuli amesema kuwa miradi hiyo na mingine mingi ya ujenzi ambayo imejengwa na inaendelea kujengwa wakati wa uongozi wa Rais Kikwete imegharimu kiasi cha sh. trilioni tisa, ambacho ni kiwango kikubwa kuliko vyote vilivyopata kutumika kwa miradi ya ujenzi katika muongo mmoja katika historia ya Tanzania.
Waziri Magufuli amesema kuwa miradi hiyo ni pamoja na madaraja makubwa 12 ambao yamejengwa na kukamilika katika kipindi hicho ambayo ni Rusumo (Kagera), Umoja (Mtwara), Mwanhuzi (Simiyu), Kikwete (Kigoma), Nangoo(Mtwara), Ruhekei (Ruvuma), Mbutu (Tabora), Mwatisi (Morogoro), Ruvu (Pwani),(Nanganga (Mtwara), Maligisu (Mwanza) na daraja la waendao kwa miguu la Mabatini (Mwanza).
Waziri Magufuli pia amesema kuwa jumla ya madaraja mengine madogo zaidi ya 7,200 yamejengwa na kukamilika na madaraja mengine makubwa saba yapo katika hatua mbali mbali za ujenzi ambayo ni Kigamboni (Dar es Salaam), Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi), Sibiti (Singida), Ruvu Chini (Pwani), Lukuledi 11 (Mtwara) na Kolo (Dodoma).
Amesema kuwa madaraja mengine makubwa ambayo yako katika maandalizi ya kujengwa ni Momba, Mwiti, Simiyu, Wami, Ruhuhu, Daraja jipya la Salendar, Daraja jipya la Wami Chini, Pangani,na daraja la wandeao kwa miguu la Furahisha.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
8 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamilioni ya Watanzania sasa wanufaika na huduma za kifedha –BOT
BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imetaja mafanikio makubwa manane ya maendeleo ya huduma za kifedha na za kibenki katika Tanzania katika miaka 10 iliyopita, ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa katika idadi ya Watanzania wanaofikiwa na huduma rasmi za kifedha za kibenki na zisizokuwa za kibenki ambayo limepaa kutoka asilimia tisa mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 57.6 mwaka juzi, 2013.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imesema kuwa imeamua kujenga tawi kubwa la benki hiyo katika Mkoa wa Mtwara kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya kiuchumi ambayo yanayotokea katika mkoa huo na mkoa jirani wa Lindi, mikoa ambayo kwa miaka mingi ilikuwa inafikiriwa kuwa nyuma zaidi katika maendeleo katika Tanzania.
Hayo yamesemwa , Jumapili, Agosti 9, 2015 na Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndullu, wakati akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tawi la BOT katika mji wa Mtwara. Rais Kikwete ameweka jiwe hilo ikiwa ni sehemu ya shughuli zake nyingi wakati wa ziara yake ya siku moja ya kikazi mkoani Mtwara.
Ujenzi wa jengo la tawi la BOT mjini Mtwara ulianza Oktoba mwaka juzi, 2013 na unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu, 2015 kabla ya shughuli rasmi kuanza kwenye tawi hilo Juni mwakani, 2016 kwa watumishi 60 wa awali. Tawi hilo litakuwa tawi la sita la BOT kufuatia matawi ya Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar.
Profesa Ndullu amemwambia Rais Kikwete kuwa yamekuwepo mafanikio makubwa manane dhahiri katika maendeleo ya kibenki na kifedha katika miaka 10 iliyopita chini ya uongozi wa Rais Kikwete, ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la Watanzania ambao wanafikiwa na huduma za kifedha za kibenki ama zisizokuwa za kibenki ambazo sasa zinawafikia Watanzania asilimia 57.3 kulinganisha na asilimia tisa mwaka 2006.
“Kati ya mwaka 2009 na 2013, kwa mfano, idadi ya Watanzania wasiopata huduma yoyote ya kifedha ilipungua kwa kasi sana kutoka asilimia 55.4 ya watu wazima hadi kubakia asilimia 26.8. Yote haya yamepatikana kutokana na matumizi ya teknolojia ya kidigitali yaliyowezesha kupungua kwa gharama za huduma za kifedha kwa kiwango kikubwa sana,” Gavana Ndullu amemwambia Rais Kikwete.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa katika kipindi hicho, huduma za kibenki zimepanuka sana akisema kuwa mwaka 2006 idadi ya Watanzania waliokuwa wanatumia huduma za kibenki walikuwa milioni 1.5 idadi ambayo ilipanda na kufikia watu milioni 3.3 mwishoni mwa mwaka juzi 2013.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa kumekuwepo na uimarikaji wa usimamizi wa sekta ya fedha ambako kumewezesha kuanzishwa na kuwepo kwa taasisi nyingi za kutoa mikopo midogo midogo kwa wananchi, mkopo ambayo inatilia maanani hali halisi na kwa ajili ya wajasiriamali na inayochangia kwa kiwango kikubwa kupunguza umasikini.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa kuwa idadi ya mabenki na taasisi nyingine za fedha imeongezeka mno nchini kufikia mabenki na taasisi 57, zikiwemo benki mbili za maendeleo za Tanzania Investment Bank (TIB) na Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) ambayo Rais Kikwete aliizundua rasmi wakati wa sherehe za Siku ya Nanenane mkoani Lindi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Gavana Ndullu pia amesema kuwa limekuwepo ongezeko kubwa la huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambayo alisema kuwa hadi Machi, mwaka huu, 2015, idadi ya akaunti zake ilifikia milioni 40.7.
“Watanzania milioni 26.8 ama asilimia 95 ya Watanzania watu wazima walikuwa na akaunti kwenye simu zao hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka huu. Kati ya hizo akaunti milioni 15, sawa na asilimia 55 zilikuwa zinatumika mara kwa mara (active accounts),” amesema Gavana Ndullu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
10 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali imenunua vivuko vingi zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuliko vivuko ambavyo vilipata kununuliwa katika miaka 45 kabla ya mwaka 2005 wakati Rais alipoingia madarakani.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemwambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa katika miaka 10 iliyopita wakati Tanzania ikiwa chini ya uongozi wa Rais Kikwete, Wizara ya Ujenzi imejenga vivuko 15 vipya kulinganisha na 13 tu vilivyokuwepo mwaka 2005 wakati Serikali ya Rais Kikwete inaingia madarakani na hivyo kuifanya Tanzania kuwa na vivuko 28 vya uhakika na salama kwa matumizi ya wananchi.
Aidha, Waziri Magufuli amewaambia wananchi wa Mtwara kuwa katika kipindi hicho cha miaka 10, Serikali imefanya ukarabati mkubwa wa vivuko saba na kuwa ukarabati huo umegharimiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Rais Kikwete.
Waziri Magufuli ametoa maelezo hayo Jumapili, Agosti 9, 2015 wakati alipomkabidhi Rais Kikwete kivuko kipya cha MV Mafanikio kinachotoa huduma kati ya Mji wa Mtwara na eneo la Msangamkuu, mkoani humo katika mkutano uliofanyika Msangamkuu na kuhudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi.
Rais Kikwete amefanya uzinduzi wa MV Mafanikio katika sherehe iliyofanyika mjini Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kazi katika Mkoa huo ambako amewasili asubuhi akitokea Mkoa wa Lindi, ambako alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili. Mara baada ya uzinduzi huo, Rais Kikwete akiambatana na Mama Salma Kikwete, Waziri Magufuli, mawaziri kadhaaa na viongozi wa Mkoa wa Mtwara wamepanda kivuko hicho kwenda Msangamkuu ambako wamefanya mkutano wa hadhara wa wananchi.
Kivuko cha MV Mafanikio ni matokeo ya ahadi ya Rais Kikwete wakati wa kampeni ya urais mwaka 2010, na kina uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita na kimegharimu kiasi cha sh bilioni 3.3.
Kivuko hicho ambacho kimejengwa na Kampeni ya Songoro Marine Transport Ltd Boatyard ya Mwanza, baada ya wajenzi wake wa kwanza kutoka Uholanzi kushindwa na kukimbia nchi, kinasafiri kwa dakika saba tu kati ya Mtwara Mjini na Msangamkuu.
Kivuko hicho ambacho Waziri Magufuli amekielezea kama ukombozi mkubwa kwa wananchi, kinaondoa adha na kero ya wananchi wa Msangamkuu ambao walikuwa wanalazimika kuweka maisha yao hatarini kwa kuvuka eneo hilo la Bahari ya Hindi kwa boti ndogo ndogo ama kufanya safari ya mzunguko wa kilimota 21 ili kwenda mjini Mtwara kupata huduma zao. Kata ya Msangamkuu ina wakazi wanaokadiriwa kufikia 12,000.
“Nawapeni pole sana kwa sababu najua wako ndugu zetu wengi ambao wamepoteza maisha yao katika eneo hili kwa sababu ya usafiri uliokuwa unatumika hapa kwa miaka mingi,” Waziri Magufuli amewaambia wananchi hao wa Msangamkuu mbele ya Rais Kikwete.
Waziri Magufuli pia amemwambia Rais Kikwete na wananchi wa Mtwara kuwa Serikali imeamua kuwa wanafunzi wote wenye sare pamoja na wananchi wenye ulemavu watakuwa wanavuka bure kwa kutumia kivuko hicho chenye urefu wa mita 33.
Aidha, Waziri Magufuli amemwambia Rais Kikwete na wananchi wa Msangamkuu kuwa sambamba na kivuko hicho, Serikali pia imenunua na kuweka kivuko kipya cha MV Kilambo kwenye mpaka wa Tanzania na Mozambique katika Mto Ruvuma katika Mkoa wa Mtwara.
Waziri Magufuli amesema kuwa vivuko vilivyojengwa katika miaka 10 iliyopita ni MV Kilombero kinachoa huduma kwenye Mto Kilombero, Mkoa wa Morogoro, chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita kwa wakati mmoja; MV Ruhuhu kinachotoa huduma kwenye Mto Ruhuhu, Mkoa wa Ruvuma, chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Misungwi kinachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi, Mkoa wa Mwanza, chenye uwezo wa kubeba tani 250, abiria 1,000 na magari 36 na MV Magogoni kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni, Dar es Salaam chenye uwezo wa kubeba tani 500, abiria 2000 na magari 60.
Waziri Magufuli ametaja vivuko vingine kuwa ni MV Kome 11 kinachotoa huduma kati ya Nyakalilo na Kome, Mwanza na chenye uwezo wa kubeba tani 40, abiria 100 na magari manne; MV Pangani kinachotoa huduma kati ya Pangani na Mbweni, Tanga, chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Utete 11 kinachotoa huduma kwenye Mto Rufiji, Pwani na chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Ujenzi kinachotoa huduma kati ya Kisorya na Rugezi, Wilaya ya Ukerewe, Mwanza chenye uwezo wa tani 85, abiria 330 na magari manane.
Vivuko vingine vilivyotanjwa na Waziri Magufuli ni MV Musoma kinachotoa huduma kati ya Kinesi na Musoma, Mkoa wa Mara na chenye uwezo wa tani 85, abiria 330 na magari manane; MV Ruvuvu kinachotoa huduma kati ya Rusumo na Nyakiziba, Ngara, Kagera na chenye uwezo wa kubeba tani 35, abiria 80 na magari manne; MV Kilambo kinachotoa huduma kati ya Kilambo (Tanzania) na Namoto (Mozambique) mkoani Mtwara chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita.
Waziri Magufuli ametaja vivuko vingine kuwa ni MV Malagarasi kinachotoa huduma kati ya Ilagala na Kajeje, Kigoma, na chenye uwezo wa kubeba tani 50, abiria 100 na magari sita; MV Tegemeo kinachotoa huduma kati ya Maisome, Kahunda na Nkome, wilayani Sengerema, Mwanza na chenye uwezo wa kubeba tani 85, abiria 200 na magari 10, MV Dar es Salaam kinachotoa huduma kati ya Dar es salaam na Bagamoyo kwenye mwamboa wa Bahari ya Hindi chenye uwezo wa kubeba abiria 300 na MV Mafanikio kinachotoa huduma kati ya Mtwara Mjini na Msangamkuu.
Waziri Magufuli amesema kuwa vivuko vilivyofanyiwa ukarabati mkubwa ni MV Kigamboni (Dar Es Salaam) chenye uwezo wa kubeba tani 160, yaani abiria 800 na magari 22, MV Sengerema (Mwanza) chenye uwezo wa kubeba tani 179, yaani abiria 490 na magari 18,MV Chato (Geita) chenye uwezo wa kubeba tani 75, yaani abiria 200 na magari sita.
Vingine ni MV Ukara, chenye uwezo wa kubeba abiria 70, MV Sabasaba (Mwanza) chenye uwezo wa kubeba tani 85, abiria 300 na magari manane, MV Temesa (Mwanza) zamani kikiitwa MV Geita chenye uwezo wa tani 65, yaani abiria 120 na magari sita na MV Mara (Mara) zamani kikiitwa Kone 1, chenye uwezo wa tani 35, yaani abiria 60 na magari matatu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
10 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Agosti 5, 2015, amewaapisha Majaji 14 akiwamo Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani Tanzania katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliwateua majaji hao hivi karibuni katika mwendelezo wake wa kuhakikisha kuwa Muhimili wa Mahakama unakuwa na raslimali watu ya kutosha ili kuendelea kutoa haki kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi.
Walioapishwa leo katika sherehe iliyohudhuriwa pia na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman ni pamoja na Jaji Richard Mziray ambaye anakuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Majaji wengine ambao wote ni Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Mheshimiwa Ignas Pius Kitusi, Mheshimiwa Lameck Michael Mlacha, Mheshimiwa Wilfred Peter Dyansobera, Mheshimiwa Salima Mussa Chikoyo, Mheshimiwa Issa Kweka Arufani, Mheshimiwa Sirilius Betran Matupa na Mheshimiwa Julius Benedicto Malaba.
Wengine ni Mheshimiwa Victoria Lyimo Makani, Mheshimiwa Lucia Gamuya Kairo, Mheshimiwa Rehema Joseph Kirefu, Mheshimiwa Benhaji Shaaban Masoud, Mheshimiwa Issa John Maige na Mheshimiwa Adam Juma Mwambi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
5 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Agosti 4, 2015, ametia saini Miswada ya Sheria mitano hadharani ikiwa ni hatua yake ya mwisho kabisa kuridhia Miswada ya Sheria akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika sherehe iliyofanyika katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam,Rais Kikwete ameridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na mamia ya wageni waalikwa, mawaziri wanaohusika na sekta hizo, Mheshimiwa George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wametoa maelezo ya miswada hiyo mitano kabla haijaridhiwa na Rais Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue pia wamehudhuria sherehe hizo ambazo vile vile zimehudhuriwa na mawaziri wa Serikali, mabalozi, wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s) na wadau wengine wa sekta ambazo Miswada yake imeridhiwa.
Hiyo ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria hadharani. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 wakati Rais Kikwete aliporidhia hadharani Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi.
Aidha, hiio ni mara ya mwisho kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria nchini kabla ya kuondoka madarakani mwanzoni mwa Novemba, 2015. Rais tayari amelivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
RaiswaJamhuriyaMuunganowa Tanzania, MheshimiwaJakayaMrishoKikweteamesikitishwanakuhuzunishwamnonakifo cha mmojawawanasiasawakongwenchini, Mzee Peter KIsumoambayealipatakuwaMzeewa Chama cha TANU, Muasisinamdhaminiwa Chama cha CCM naaliyeshikilianafasinyingizauongozindaniyaSerikalinautumishiwaummaukiwemouwaziri.
“Nimepokeakwamasikitikomakubwanahuzuninyingitaarifayakifo cha Mzee Peter Kisumoambayenimejulishwaaliagaduniajana, Jumatatu, Agosti 3, 2015, katikaHospitaliyaTaifaMuhimbili, Dar es Salaam, ambakoalikuwaanapatiwamatibabuyafigo,”amesemaRaisKikwetekatikasalamuzakezarambirambikwafamiliayaMzeeKisumo.
AmesemaRaisKikwete: “Kwahakika, kamataifaletulimeondokewanakiongoziwakupigiwamfanokatikautumishiuliotukukawaummana Chama chetu cha Mapinduzi, nakablayahapo Chama cha TANU,niMzeePeter Kisumo. Alikuwamzalendowakweli. AlikuwaMtanzaniahalisiambayehakusitakuteteamaslahiyataifa lake.Katikanafasizotezauongoziwataifaletualizozishikilia – Ubunge, UkuuwaMkoa, Uwaziri, Udhaminiwa Chama Chetu – daimaalionyeshauongoziwakiwango cha juu. Alikuwamwadilifunamwaminifunawalahakusitakuyasemeakwanguvuzakezotenakuyateteayalealiyoyaamininayaleyaliyohusuustawiwanchiyetu.”
AmeongezaRaisKikwete: “MzeeKisumoametuachawakiwa. TumeondokewanaMzeehodariambayebusarazakenaulezi wake vilikuwabadovinahitajikasanakatikataifaletukwanyakatizasasa. Tutamkumbukadaima.”
Katikasalamuhizokwafamilia, RaisKikweteamesema: “Nawatumienisalamuzadhatiyamoyowangukuombolezakifo cha Mzeewetu. HuyualikuwaMzeewenukamaalivyokuwaMzeewangunaMzeewataifaletunahivyomsibahuuniwakwetusote. Naunganananyikatikamajonzinamaombolezo. KwapamojatunamwombaMwenyeziMungu, MwingiwaRehema, atupesubiranauvumilivukatikakipindihikikigumu. Aidha, tunamwombaaiwekapeponirohoyaMarehemuMzeePeter Kisumo. Amen”
Imetolewana:
KurugenziyaMawasilianoyaRais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Jakaya Kikwete amesihi watanzania kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha vyanzo vya ajali vinakomeshwa ili kunusuru maisha ya watu ambayo hupotea kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika.
Ameyasema wakati akifungua sherehe za ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani zilizofanyika katika uwanja Tangamano Mjini.
Rais Kikwete amesema asilimia 56 ya ajali zote zinazotokea zinasababishwa na ukosefu wa umakini wa madereva na kwamba endapo madereva watatekeleza wajibu wao wa kuwa makini ajali hizo zinaweza kuepukika
Halikadhalika amesema endapo kila mwananchi atatimiza wajibu wake wa kukemea na kutoa taarifa katika vyombo husika dhidi ya vitendo vya uvunjaji wa sheria na taratibu za usalama barabarani ajali hizo zitapungua.
Amebainisha kuwa kati ya mwaka 2010 na mwaka 2014 watu 19,264 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani na watu 96, 708 walijeruhiwa, idadi ambayo inakaribia idadi ya watoto wanaokufa kutokana na ugonjwa wa Malaria na kusisitiza kuwa idadi hiyo inaweza kuepukika.
"Hivi sasa idadi ya majeruhi wa pikipiki pekee ni kubwa kiasi kwamba wakati wagonjwa wa malaria wanapungua mawodini, majeruhi wa pikipiki wanaongezeka"
Rais Kikwete amewataka watumiaji wa barabara hususani madereva kuepuka uendeshaji wa mwendo kasi na kutoyapita magari mengine bila tahadhari kwa kuwa hivyo ndivyo vimekua vyanzo vikubwa vya ajali.
Ameagiza kuweka matuta ya kudhibiti mwendo kasi katika maeneo yote yenye makazi ya watu ili kukabiliana na vifo vinavyosababishwa na madereva wanaoendesha mwendo mkali katika maeneo ya makazi ya watu.
Aidha Rais Kikwete amelitaka jeshi la polisi kuweka kamera za kurekodi mwendo kasi wa magari barabarani badala ya kutumia askari.
"Mkitumia kamera kila atakayezidisha mwendo mtamkamata, lakini kwa kutumia askari mnatoa mianya ya baadhi ya watu kuendesha mwendo mkali na wanapokamatwa hawachukuliwi hatua"
Pamoja na kutaka polisi wafikirie kutumia kamera katika kukabiliana na ukikwaji wa sheria za usalama barabarani Rais Kikwete pia ametaka leseni za madereva wanaokamatwa kutokana na kuvunja sheria za usalama barabarani zianze kuwekwa alama ambazo ambazo hatimaye zitamwondolea dereva sifa ya kuendelea kuendesha gari.
"Mkifanya hayo ndio mtakua mnakwenda na wakati" Alisema Rais Kikwete.
Mapema akitoa taarifa ya Baraza la Usalama barabarani Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa iliyofanywa na serikali yake katika ujenzi wa barabara hali iliyosaidia kupungua kwa ajali za barabarani ambazo zimekua zikisababisha vifo, majeruhi na watu kupata ulemavu.
Pamoja na kutoa pongezi hizo Kamanda Mpinga pia amemuhakikishia Rais Kikwete kuwa Baraza hilo litaongeza juhudi za kukabiliana na vyanzo vya ajali vikiwemo uendeshaji wa mwendo kasi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said Magalula amesema mkoa huo umefanikiwa kupunguza madhara yatokanayo na ajali za barabarani ambapo vifo vimepungu kutoka 219 mwaka 2013 hadi kufikia vifo 144 mwaka 2014 na vifo 68 mwaka huu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Pereira Ame Silima amesema baraza hilo linaendelea kushauriana na serikali ili kuifanyia marekebisho sheria inayounda baraza hilo ili liweze kupata bajeti ya kuendesha shughuli zake
………………….Mwisho………………………
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru wananchi wa Tanga kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha uongozi wake hali iliyomwezesha kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo
Rais Kikwete amesema hayo katika Uwanja wa Mkwakwani Mjini TANGA tarehe 3 Augusti, 2015 wakati akiwaaga rasmi wananchi wa Tanga.
“Naungana nanyi kujipongeza kwa hatua za maendeleo tulizopiga katika kipindi cha miaka 10. Sote tunaona na kukiri kwa vinywa vyetu kuwa Tanga ya leo si ile ya miaka 10 iliyopita" Amesema Rais Kikwete
Ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika mkoa wa Tanga katika kipindi chake cha uongozi wa miaka 10 kuwa ni ongezeko maradufu la pato la mtu kutoka shilingi 537,277/= mwaka 2005 hadi kufikia shilingi 1,187,044 mwaka 2013.
Katika sekta ya Elimu Rais Kikwete amesema idadi ya vyumba vya madarasa ya awali vimeongezeka kutoka 127 hadi 418, shule za msingi zimeongezeka kutoka 3,943 hadi kufikia 8,821 na sekondari zimeongezeka kutoka 671 hadi kufikia 3,171.
Mafanikio mengine katika sekta ya elimu mkoani Tanga ni pamoja na kuongezeka kwa nyumba za walimu wa shule za msingi kutoka 597 hadi 1,883 na nyumba za walimu wa sekondari zimeongezeka kutoka 154 hadi kufikia 610 hivi sasa.
Idadi ya walimu wa shule za msingi pia imeongezeka kutoka 1,807 hadi kufikia 7,256 wakati shule za sekondari zimeongezeka kutoka 772 hadi kufikia 5,193.
Katika sekta ya afya Rais Kikwete amesema pamoja na kuiboresha na kuipandisha hadhi hospitali ya mkoa ya Bombo ambayo sasa ni hospitali ya Rufaa, zahanati zimeongezwa kutoka 146 hadi kufikia 263, vituo vya afya vimeongezeka kutoka 18 hadi kufikia 43.
Aidha amezungumzia mafanikio katika uboreshaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa vijijini Mkoani Tanga ambapo sasa wanavijiji 926,345 wanapata maji safi na salama kati ya 1,650,873 sawa na asilimia 56.3 ilihali Tanga Mjini asilimia 96 wanapata maji safi na salama na wanayapata jirani na makazi yao.
Kwa upande wa Umeme, Rais Kikwete amesema serikali imeongeza upatikanaji wa umeme kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa kilometa 430.1 za umeme wa msongo mkubwa na kilometa 393 za umeme wa msongo mdogo na kuweka transfoma 126 kwenye wilaya za Korogwe, Lushoto na Handeni.
Rais Kikwete ameongeza kuwa Serikali bado inaendelea na juhudi za kuboresha upatikanaji wa umeme.
“Tunafanya hivyo pia katika awamu ya pili kwa kujenga km 246.5 za umeme wa msongo mkubwa na km 177.5 za umeme wa msongo mdogo na uwekaji wa transfoma 86 katika wilaya za Muheza, Mkinga, Tanga na Pangani" Rais ameeleza na kuongeza kuwa
"Kutokana na juhudi hizo, tumepata mafanikio makubwa katika usambazaji umeme vijijini. Sasa vijiji 469 vimefikiwa na huduma ya umeme ikilinganishwa na vijiji 118 mwaka 2005 na hivyo kuongeza idadi ya watu wanaopata huduma ya umeme kutoka asilimia 11.04 mwaka 2005 hadi asilimia 60.54 mwaka 2011".
Rais pia amezungumzia sekta ya barabara mkoani Tanga kwa kueleza kuwa Mkoa umejengewa barabara muhimu kwa kiwango cha lami zikiwemo barabara ya Mkata - Korogwe kupitia Handeni yenye kilometa 125 na Tanga - Hororo yenye kilometa 65.
Hata hivyo amesema serikali inaendelea na matayarisho ya ujenzi wa barabara nyingine za lami zikiwemo za Kibrashi- Songea, Soni - Bwembera - Dindira - Kwashemshi na barabara ya Handeni - Turiani - Kibirashi - Kondoa yenye urefu wa kilometa 460
"Tunaendelea na matayarisho ya ujenzi wa barabara za lami za Kibrashi hadi Makao Makuu ya Wilaya ya Songe, Soni-Bwembera-Dindira-Kwashemshi kule Wilayani Lushoto, na ile barabara ya Handeni-Turiani-Kibirashi-Kondoa (km 460)" Rais amefafanua na kuwaeleza wananchi kuwa
"Mipango ya barabara hizi imeiva tayari kwa kujengwa. Tunaendelea pia kutafuta fedha kwa ajili ya barabara ya lami ya Tanga-Pangani-Bagamoyo na ujenzi wa daraja la Mligazi linalounganisha Wilaya ya Handeni (Tanga) na Miono (Pwani)”.
Kuhusu bandari ya Tanga na Reli, Rais Kikwete amesema juhudi zinafanyika kuirejesha Tanga katika umaarufu wake.
“Katika kuirejesha Tanga katika umaarufu wake wa zamani, tunafanya jitihada za kuimarisha bandari ya Tanga na reli ya kaskazini ya Tanga-Arusha-Musoma. Kwa kufanya haya viwanda vitarudi Tanga" amesema.
Rais amesema serikali imeamua kuifanya bandari ya Tanga kuwa bandari ya pili ya kupakulia mafuta yanayonunuliwa kwa pamoja yaani Bulk Procument System kuanzia Julai 2015 uamuzi ambao utafuatiwa na kujenga na kupanua bandari ya Tanga ili iweze kupokea meli kubwa zaidi.
Rais Kikwete pia amezungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu kuwa yanakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na zoezi la uandikishaji wapiga kura lakini akawasihi watanzania kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mapema akizungumza kabla ya Rais Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Magalula Said Magalula amesema wananchi wa Tanga wanamshukuru Rais kwa maendeleo makubwa waliyoyapata katika kipindi cha uongozi wake.
Hata hivyo Magalula amemuomba Rais Kikwete amsisitizie Rais ajae kuendeleza juhudi kubwa zilizofanywa katika kipindi chake ikiwemo kuendeleza bandari ya Tanga, upanuzi wa barabara za lami na Reli pamoja na huduma nyingine za kijamii.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Tanga Sheikh Mzee Makalo, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuuwezesha mkoa wa Tanga kupata mabadiliko makubwa ya kimaendeleo na akasisitiza kuwa sio sahihi kwa mtu yeyote kudai hakuna maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
...................Mwisho...........
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Agosti 4, 2015, ametia saini Miswada ya Sheria mitano hadharani ikiwa ni hatua yake ya mwisho kabisa kuridhia Miswada ya Sheria akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika sherehe iliyofanyika katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam,Rais Kikwete ameridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na mamia ya wageni waalikwa, mawaziri wanaohusika na sekta hizo, Mheshimiwa George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wametoa maelezo ya miswada hiyo mitano kabla haijaridhiwa na Rais Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue pia wamehudhuria sherehe hizo ambazo vile vile zimehudhuriwa na mawaziri wa Serikali, mabalozi, wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s) na wadau wengine wa sekta ambazo Miswada yake imeridhiwa.
Hiyo ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria hadharani. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009 wakati Rais Kikwete aliporidhia hadharani Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi.
Aidha, hiio ni mara ya mwisho kwa Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria nchini kabla ya kuondoka madarakani mwanzoni mwa Novemba, 2015. Rais tayari amelivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia.
Sherehe za kumtunuku Rais shahada hiyo zimefanyika leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Newcastle.
Akisoma maelezo ya utangulizi katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans amesema Rais Kikwete ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.
Mkuu huyo wa Chuo amesema Rais Kikwete ametunukiwa shahada hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya duniani si kwa Tanzania tu bali kwa Dunia nzima kwani mchango wake umetambulika na mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Benki ya Dunia kwa ujumla.
“Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete amechangia katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu , uchumi na Afya" amesema Bw. Jean na kuongeza kuwa “utawala wake umethibitishia sio Chuo cha Newcastle pekee bali pia kuonesha kanuni ya Msingi kuwa Elimu ni muhimu katika kukuza uchumi, uvumbuzi na katika maendeleo ya jamii" amesisitiza.
Tanzania imekua ikipokea misaada ya elimu kutoka Australia katika nyanja mbalimbali zikiwemo za madini, fedha, habari na tafiti mbalimbali ambazo zimeleta mabadiliko chanya katika jamii na duniani kwa ujumla.
Kwa sasa Watanzania wanne wanachukua masomo ya uzamifu katika masuala ya elimu na siasa.Tayari Watanzania 45 wamemaliza digrii na pia wapo watafiti kutoka Newcastle wanaofanya tafiti zao nchini Tanzania katika masuala ya elimu, afya na uhandisi.
Rais Kikwete ameshukuru na kuelezea jinsi alivyoguswa na tukio hilo ambapo ameushukuru uongozi wa Chuo hicho kwa kutambua mchango wake ambao ameelezea kuwa ameufanya wakati wa kipindi cha uongozi wake kwa moyo, upendo na nia njema kwa wananchi wote wa Tanzania na Dunia kwa ujumla.
"Ilikua nia yangu na wajibu wangu mkubwa kutumia ahadi nilizo waahidi wa Tanzania na hata zaidi ya kile nilicho ahidi na kuelezea kuwa mafanikio haya yote yamechangiwa pia kwa kiasi kikubwa na misingi imara iliyowekwa na viongozi walionitangulia upande wa Tanzania bara na Tanzania Visiwani kwa ujumla"
Katika utawala wake Rais Kikwete ametunukiwa shahada za heshima kutoka vyuo mbalimbali vya Marekani, Canada, China, Uturuki na Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.
Rais Kikwete pia ametunukiwa tuzo za heshima mbalimbali katika masuala ya Kijamii (United Nations Social Good Award), Afya, Technolojia na Maendeleo (South-South Award for Global Health, Technology and Development) pamoja na Demokrasia (Icon of Democracy Award (Nertherlands)
Rais pia amepata kutunukiwa na kutambuliwa kwa Mchango wake ambapo alitunukiwa nishani kadhaa zikiwemo;
1. (Most Excellent Order of the Peral of Africa) ambayo ni nishani ya juu nchini Uganda.
2. The order of the Green Crescent of the Comoros (Comoros)
3. Order of Abdulazizi Al Saud (Saudi Arabia)
4.Order of excellence (Jamaica)
5. Order of Oman (Oman)
6. AAI African National Achievement Award
7. U.S. Doctors for Africa Award
8. Good Governance in Africa 2015
Sherehe hiyo imehudhuriwa na Mstahiki Meya wa mji wa Newcastle, Mama Nuatali Nelmes, walimu na wakufunzi wa Chuo cha Newcastle, wanafunzi wa Kitanzania na familia zao pamoja na Watanzania kadhaa wanaoishi na kufanya kazi katika mji wa Newcastle.
Rais Kikwete amekamilisha ziara yake ya Kiserikali ya siku nne nchini Australia na anatarajia kuelekea Dar-es Salaam tarehe 30 Julai, 2015
...........Mwisho..........
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Newcastle-Australia
29 Julai, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot amempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba nchini Tanzania.
"Nakupongeza sana kwa uamuzi wako wa kukabidhi madaraka kwa amani nchini kwako , ni jambo la nadra sana Barani Afrika, kuwa na utaratibu mzuri na wa Amani namna hii" Bw. Abbot amemuambia Rais Kikwete na kumueleza awe na uhakika kuwa " Australia itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kukuza uchumi" ameongeza.
Rais Kikwete na Waziri Mkuu Abbot pia wamezungumzia jinsi nchi zao zinaweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii.
Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.
Rais Kikwete amepokelewa leo asubuhi tarehe 28 katika makao Makuu ya kiongozi wa Australia kwa heshima zote kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula rasmi cha mchana na baadae kupanda mti kuashiria kuimarisha mashirikiano baina ya nchi hizi mbili kwa kipindi kirefu kijacho.
Tanzania na Australia zimedumu katika ushirikiano baina ya nchi zao tangu miaka ya sitini na sasa nchi mbili hizi zimeazimia kuimarisha mahusiano haya zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo za uwekezaji na biashara kati yao.
Baadae leo jioni Rais Kikwete atakutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inaweza kunufaika kutokana na kupata gesi.
Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na tafiti mbalimbali katika Kilimo.
Kesho tarehe 29 Julai, 2015 Rais Kikwete anatarajia kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.
Rais Kikwete anatarajia kuondoka Australia na kurejea Tanzania baada ya shughuli ya kupokea shahada yake na ratiba yake kwa ujumla.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Canberra-Australia
28 Julai, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatatu, Julai 27, 2015, kwenye
ukurasa wake wa 26 limechapisha habari yenye kichwa cha habari,
“Marais watano wanaotajwa kuongoza kwa mishahara minono
barani Afrika ni hawa hapa”.
Katika habari hiyo ambayo gazeti hilo linadai chanzo chake ni
“uchambuzi wa mtandao wa African Review” inadaiwa kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, anashilikia nafasi ya tano miongoni mwa viongozi 38 wa
nchi za Afrika wanaolipwa mshahara mnono zaidi.
Gazeti hilo linadai kuwa Rais Kikwete analipwa Dola za
Marekani 192,000 kwa mwaka, ikiwa ni malipo ya Dola za Marekani
16,000 kwa mwezi.
Habari hizi siyo za kweli. Ni uongo na uzandiki. Ni uzushi
mtupu na ni uzushi wa hatari.
Mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
mwezi ama kwa mwaka haufikii na hata wala kukaribia kabisa
kiwango kinachotajwa na Gazeti la Mwananchi.
Tangu Uhuru, mwaka 1961, Rais wa Tanganyika na baadaye
tangu mwaka 1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amekuwa miongoni mwa viongozi wanaolipwa mishahara ya chini
kabisa duniani.
Mshahara wa Rais wa Tanzania kwa mwezi ni wa chini kiasi
cha kwamba mshahara wake unazidiwa, tena kwa mbali, na
mishahara wanayolipwa baadhi ya watendaji wakuu wa baadhi ya
taasisi za umma nchini.
Aidha, ni jambo la kushangaza kwamba Gazeti la Mwananchi,
linalochapishwa hapa nchini, linaweza kupata kiasi cha uongo
anacholipwa Rais wa Tanzania katika mitandao ya nje badala ya
kuuliza rasmi na kupewa majibu sahihi.
Kwa kujiingiza katika uzushi wa kupindua kiasi hiki, Gazeti la
Mwananchi haliwezi kuwa na nia nyingine yoyote isipokuwa nia ya
kuwachochea wananchi na kuwajengea chuki dhidi ya Serikali yao na
Kiongozi wao Mkuu.
Ni matarajio yetu, kuwa Gazeti la Mwananchi litafanya jitihada
za makusudi, kama taaluma ya uandishi wa habari inavyoelekeza,
kutafuta usahihi wa jambo hili na kuwaambia Watanzania ukweli.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Julai, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko ya Utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kumteua Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Aidha, Rais Kikwete amemteua Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vile vile, Rais Kikwete amewateua majaji wapya 13 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumamosi, Julai 25, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa teuzi hizo zote zimeanza leo hii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Balozi Sefue, Ndugu Kombwey ambaye anaapishwa baadaye leo jioni, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu Julius Benedicto Mallaba.
Badala yake, Rais Kikwete amemteua Bwana Mallaba kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kombwey alikuwa Mkurugenzi wa Utawala, Tume ya Uchaguzi.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa Jaji Mziray ambaye anateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
Majaji wa Mahakama Kuu ambao wameteuliwa na Rais Kikwete, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ndugu Ignas Pius Kitusi ambaye ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Ndugu Wilfred Peter Dyansobera ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu; Ndugu Lameck Michael Mlacha ambaye ni Naibu Msajili na Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi; Ndugu Salima Mussa Chikoyo ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi; Ndugu Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Mkuu wa Tanzania na Ndugu Julius Benedicto Mallaba.
Wengine ni Ndugu Adam Juma Mambi ambaye ni Katibu Msaidizi, Tume ya Kurekebisha Sheria; Ndugu Sirilius Betran Matupa ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa Rais, Sheria, Ofisi ya Rais, Ikulu; Ndugu Issa Maige ambaye ni wakili wa kujitegemea, Ndugu Licia Gamunya Kairo ambaye ni wakili wa kujitegemea; Dkt. Masoud Shaaban Benhaji wakili wa kujitegemea na Mhadhiri Mwadamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam, Ndugu Victoria Makani ambaye ni wakili wa kujitegemea na Ndugu Rehema Joseph Kerefu ambaye ni mwanasheria wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imesema kuwa wakati Ndugu Kombwey anaapishwa leo, majaji wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Julai, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Julai 24, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia (WB) katika Tanzania, Bwana Philip Dongier ambaye amemaliza muda wake wa kazi nchini.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemshukuru Bwana Dongier kwa kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kukifikisha kwenye hatua za juu kabisa. Bw. Dongier alikuwa amekuja Ikulu kumuaga Rais Kikwete.
Bwana Dongier ambaye amemwambia Rais Kikwete kuwa anaondoka nchini mwanzoni mwa wiki ijayo, amekuwa nchini kwa miaka mitatu unusu ambako ameongoza jitihada kubwa za Benki ya dunia katika kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo ikiwamo ya ujenzi wa barabara.
“Tumefurahia sana kufanya kazi nawe, tumefurahishwa sana na ushauri wako. Kwa pamoja tumefanikisha mengi.Umefanikisha sana kusukuma mbele maendeleo yetu kwa namna ya kipekee na binafsi nimefurahi kufanya kazi nawe. Umekuwa mmoja wa wawakilishi bora wa Benki ya Dunia katika historia ya nchi yetu,” Rais Kikwete amemwambia Bwana Dongier.
Viongozi wamejadili mageuzi ambayo yamefanyika katika uchumi wa Tanzania tokea miaka ya shida kubwa kwa wananchi katika miaka ya mwanzoni mwa 1980 hadi sasa.
Aidha, viongozi hao wamejadili mchakato wa uchaguzi unaendelea katika Tanzania na kuelezea matumaini kuwa amani na utulivu vitaendelea kudumishwa katika kipindi cha kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu, 2015.
Rais Kikwete na Bw. Dongier pia wamezungumzia umuhimu wa Tanzania na Benki ya Dunia kuongeza kasi ya uwekezaji katika huduma ya maji safi na salama kwa nia ya kuhakikisha kuwa katika miaka michache ijayo kila Mtanzania anapata maji safi na salama.
Bw. Dongier ameelezea utayari wa Benki ya Dunia kuongeza kasi ya ushirikiano wake na Tanzania katika eneo hilo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Julai, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Kikwete atunukiwa Tuzo la Kudumisha Utawala Bora Barani Afrika
Jitihada za muongo mzima wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuimarisha na kudumisha Utawala Bora katika Tanzania zimetambuliwa kimataifa kwa Rais kutunukiwa Tuzo la Utawala Bora Barani Afrika mwaka 2015 (Good Governance in Africa.)
Rais Kikwete ametunukiwa Tuzo hiyo na Taasisi ya African Achievers Awards yenye makao yake makuu katika Afrika Kusini kutokana na kutambua mchango wake mkubwa katika kulea, kuimarisha, kuendeleza na kudumisha Utawala Bora katika Tanzania katika miaka yote 10 ya uongozi.
Rais Kikwete anajiunga na watu wachache ambao wamepata kupokea tuzo hiyo tokea lilipotolewa kwa mara ya kwanza kwa Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Afrika Kusini mwaka 2011 kwa kutambua mapambano yake katika kutetea haki za binadamu,usawa, haki na amani.
Rais Kikwete ameteuliwa kutoka miongoni mwa zaidi ya watu 1,202 ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye Jopo la Kimataifa Linalojitegemea na lenye wajumbe kutoka Uingereza na Afrika Kusini kwa ajili ya uteuzi.
Kutokana na tunuku hiyo, Rais Kikwete amealikwa kwenda Afrika Kusini kupokea tuzo hiyo katika sherehe kubwa inayofanyika jioni ya kesho, Jumamosi, Julai 25, 2015 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Sandton (Sandton Convention Centre) mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa sababu ya kukabiliwa na shughuli nyingi hapa nyumbani, Rais Kikwete amemwomba Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Asha Rose Migiro, kumwakilisha katika sherehe ya kupokea tuzo hiyo ambako pia atatoa mada kuhusu “Umoja wa Afrika: Fursa na Changamoto (Africa’s Unity: Prospects and Challenges) “ kwa niaba ya Rais Kikwete.
Tuzo za African Archievers Awards zinalenga kuwatambua watu binafsi na taasisi ambazo zimejitambulisha kwa michango yao kwa ustawi na maendeleo ya Bara la Afrika.
Katika barua ya kumjulisha Rais Kikwete kuhusu uteuzi wake, Mtendaji wa African Achievers Awards, Bwana Rex Indaminabo amesema: “Uongozi wa African Achievers Awards unayo furaha kukujulisha juu ya uteuzi wako wa kupokea Tuzo la 2015 African Achievers Awards katika kundi la Utawala Bora Barani Afrika.”
Ameongeza Mtendaji huyo: “Ni kwa furaha na heshima kubwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri na Taasisi ya Uongozi na Menejimenti wanakuandikia kukupongeza kwa kuteuliwa kwenye orodha ya mwisho na hatimaye kuwa mshindi wa Tuzo la African Achievers Awards katika kundi la Utawala Bora katika Afrika.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Julai, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amepokea Joho na Cheti cha Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sheria yaani Doctor of Laws, Honoris Causa kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM.
Tayari Rais Kikwete alishatunukiwa shahada hiyo katika mahafali ya 41 ya UDSM yaliyofanyika Octoba , mwaka 2011 na leo hii UDSM.
Rais Kikwete ametunukiwa shahada hiyo kwa sababu ya utumishi wake uliotukuka kwa Umma wa Watanzania na jamii nyingine zilizo nje ya mipaka ya Tanzania.
Akisoma maelezo mafupi kabla ya kumkabidhi cheti na kumvisha Joho, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Taaluma Prof. Florens Luoga amesema Shahada hii ya juu kabisa miongoni mwa tuzo zinazotolewa na UDSM , kulitokana na uamuzi uliofanywa na Seneta na kuridhiwa na Baraza la Chuo.
” Seneta ilizingatia busara, wema na Umakini uliodhihirika katika maisha yako yote ya uongozi, tangu ulipokuwa kijana hadi ulipofikia ngazi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu”ameeleza.
Rais Kikwete ameshukuru kwa Shahada hiyo na kueleza nia yake ya kuendelea kukisaidia Chuo Kikuu hicho ambacho ndiyo chuo Kikuu kikongwe hapa nchini.
“Nitaendelea kutoa mchango wangu katika Chuo chetu ambacho ndiyo Kikubwa hapa nchini kwa lolote ambalo naweza kulifanya kwa ajili ya Chuo sasa na hata baadaye” Rais ameahidi na kupata maelezo kutoka kwa Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Rwekaza Mukandala ya jinsi mchango wake umechangia katika kutengeneza dira ya UDSM.
Prof. Mukandala amesema baadhi ya mchango mkubwa wa Rais katika Chuo hicho ni kuanzishwa kwa shule ya Madaktari na masomo ya sayansi ya Kilimo ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi mwezi Octoba mwaka huu.
Katika hatua ingine Rais Kikwete pia amepokea hundi yake ya Bima ya maisha (Flexi Provider) ambayo amekuwa nayo kwa kipindi cha miaka 9.
Akimkabidhi hundi hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Tanzania Limited (NIC) Bw. Sam Kamanga amesema uwepo wa Mheshimiwa Rais kama mteja wa NIC imesaidia kukuza uelewa na shughuli za shirika hilo.
“Kitendo cha Serikali kukatia Bima mali zake na taasisi zake, kumeongeza uwezo wa kifedha wa shirika na soko la Bima” amesema na kuwataka watu binafsi, taasisi mbalimbali na mashirika ya kiserikali kukata Bima kwa ajili ya maendeleo na akiba ya baadaye.
Rais Kikwete ameitaka NIC kuongeza juhudi katika kuhamasisha na kuelimisha watanzania umuhimu na manufaa makubwa yanayopatikana kutokana na Bima.
……………………………MWISHO……………………………
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
21 Julai , 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania wanaofanya kazi katika mashirika ya kimataifa nje ya nchi kuwasaidia Watanzania wenzao wenye sifa na uwezo kuweza kujiunga na mashirika hayo ya kimataifa.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali haiwadai chochote Watanzania wanaoishi nje na kufanya kazi nje ya nchi bali kuweza kuisaidia nchi yao na ndugu zao pale inapopatikana nafasi.
Rais Kikwete aliyasema hayo usiku wa Alhamisi, Julai 16, 2015, wakati alipokutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi katika Uswisi chini ya chama chao cha TAAS – Tanzania Association in Switzerland kwenye Hoteli ya Intercontinental, mjini Geneva.
“Saidieni ndugu zenu nyumbani, lakini pia saidieni wenzenu wenye sifa ya kuweza kupata kazi katika mashirika ya kimataifa. Wenzetu katika nchi nyingi za Afrika, hasa Afrika Magharibi wanafanya hivyo, ndio maana wamejaa katika mashirika hayo ya kimataifa. Sisi tuna haya na hatufanyi hivyo,” alisema Rais Kikwete.
Kuhusu matarajio ya Serikali kwa Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake haiwadai chochote.
“Sisi hatuwadai chochote. Nyie endeleeni kufanya kazi nje na kujenga maisha yenu, kazi ya maendeleo ya nchi mtuachie sisi, tunaiweza. Ushauri wangu ni wasaidieni ndugu zenu nyumbani. Dola 100 ya Marekani kila mwezi zina uwezo wa kusomesha mtoto shule.”
Baada ya mazungumzo na Watanzania hao, Rais Kikwete aliwafuturisha Watanzania hao ikiwa ni futari ya mwisho kwa Rais Kikwete na Watanzania, akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Julai, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jopo ya Watu Mashuhuri Duniani wanaotafuta njia za kuiwezesha dunia kujiandaa vizuri kwa majanga ya magonjwa ya kuambukiza , Ijumaa, Julai 17, 2015, amemaliza mikutano ya raundi ya pili ya Jopo hilo mjini Geneva, Uswisi.
Rais Kikwete na Wanajopo wenzake wamemaliza raundi ya pili ya mikutano ya Jopo hilo kwa kukutana na mabingwa magwiji ambao wengi wao wamo na wamekuwemo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Katika miezi mitatu ya mwaka jana, ugonjwa huo uliua watu 11,000 katika nchi za Afrika Magharibi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Mabingwa hao waliokutana na Jopo hilo kwenye Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ni kutoka Kamisheni ya Ulaya, Shirika la EPRUS la Ufaransa, Shirika la Kujihami la Nchi za Ulaya Magharibu la NATO, Shirika la GOAR la WHO, Shirika la Chakula Duniani (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la OCHA na wajumbe kutoka nchi za Marekani na Uingereza.
Kwa zaidi ya saa mbili, Rais Kikwete na wanajopo wenzake, wamesikiliza maelezo ya wataalam hao ambao kwa pamoja walihusika na mapambano dhidi ya Ebola, ugonjwa ambao umeanza kuibuka upya katika nchi hizo tatu za Afrika Magharibi.
Jopo la Rais Kikwete halichunguzi ugonjwa wa Ebola na madhara yake, lakini wajumbe hao waliombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon, wakati anawateua Aprili 2, mwaka huu, kutumia uzoefu wa dunia katika kukabiliana na ugonjwa huo kutoa mapendekezo yao.
Baada ya kuwasikiliza wataalam hao, wajumbe wa Jopo wamekubaliana kuwa vikao vyao vijavyo vitafanyika katika nchi zilizoathiriwa na Ebola za Guinea, Liberia na Sierra Leone mwanzoni mwa mwezi ujao.
Aidha, baada ya kumalizika kwa mkutanao wa Jopo, Rais Kikwete amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Bi. Margaret Chan kwenye makao makuu ya shirika hilo.
Rais Kikwete anaondoka mjini Geneva , Jumamosi, Julai 18, 2015 kurejea nyumbani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Julai, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Teteeni maslahi ya Bara letu, Rais Kikwete awaambia mabalozi wa Afrika Uswisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Mabalozi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kulitetea Bara hilo kwa sababu hamna mtu mwingine atakayetetea maslahi ya Afrika.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa kila nchi kuamua aina ya mfumo wa kisiasa ambao unaifaa nchi husika bila kulazimika kuwepo ukomo wa kiongozi kukaa madarakani.
Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo, Alhamisi, Julai 16, 2015, wakati alipozungumza na Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa na mashirika yake mjini Gevena, Uswisi.
Rais Kikwete yuko nchini Uswisi kuendesha vikao vya Jopo la Watu Washuhuri Duniani ambalo linatafuta njia bora zaidi za kuiwezesha dunia kukabiliana na majanga ya magonjwa ya milipuko katika siku zijazo.
Jopo hilo liliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Aprili 2, mwaka huu na Jopo lilifanya mikutano yake ya kwanza Mei mwaka huu mjini New York, Marekani.
Akijibu swali la Balozi wa Benin ambaye amelalamikia shutuma zisizokuwa halali zinazoendeshwa na nchi na mabalozi wake dhidi ya Afrika katika masuala mbali mbali zikiwemo haki za binadamu.
“Hii ni kazi na wajibu wenu. Afrika inaposhambuliwa isivyo halali na mataifa mbali mbali inakuwa ni kazi yetu kutetea. Nyie ndiyo mko hapa kwa ajili ya kutetea heshima ya Afrika na kulinda misimamo ya Bara letu. Na uwezo huo mnao wa kutosha kabisa.”
“ Ni lazima pia mkumbuke kuwa dunia hii ni katili sana. Msitegemee mtu yoyote wa kututeteeni na kutetea haki na matakwa yetu. Nyie mlioko hapa ndiyo wenye wajibu wa kututetea na kazi hiyo mnaiweza.”
Akijibu swali jingine ambalo mwuuliza amesema kuwa baadhi ya viongozi wa Afrika wamekuwa wanatumia visingizio mbali mbali ukiwemo ugaidi ili kuhalalisha kubakia madarakani, Rais Kikwete amesema kuwa ugaidi hauna uhusiano na uamuzi wa watu kubakia madarakani kwa muda mrefu.
“Nchi zinatofautiana. Kuna baadhi ya viongozi wana hamasa ya kubakia madarakani, wengine hawana. Ni uamuzi wao wenyewe kama wana hofu ya kutoka madarakani ama hawana uhakika kabisa kuwa maisha yao yataendelea kuwa ya kawaida kama wakitoka madarakani.”
Balozi wa Zimbabwe ameipongeza Tanzania na Rais Kikwete kwa mchango wake mkubwa katika jitihada za kukabiliana na malaria na kuonyesha uongozi katika Jumuia za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) .
Naye Balozi wa Rwanda amempogeza Rais Kikwete kwa uongozi wake katika EAC ambako Rais ni mwenyekiti.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Julai 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
UNHCR: Tanzania mlinzi mkuu wa wakimbizi duniani
ni kimbilio salama la wakimbizi
. Shirika hilo lasisitiza Tanzania ni kimbilio salama la wakimbizi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi Duniani (UNHCR) limesema kuwa Tanzania imekuwa kimbilio salama la wakimbizi kwa sababu ni nchi salama, ni nchi tulivu, ni nchi yenye mahusiano mazuri ya kijamii na yenye kuongozwa na sera nzuri na za kibinadamu.
Aidha, shirika hilo, limeiomba Tanzania kutoa ardhi ya kutosha ili kuliwezesha shirika hilo kujenga miundombinu na huduma kwa ajili ya wakimbizi 78,000 ambao wamekimbia Tanzania katika miezi ya karibuni kutoka Burundi.
UNHCR limetoa sifa hizo kwa Tanzania wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mheshimiwa Antonio Guterres alipomkaribisha Rais Kikwete kwenye makao makuu ya shirika hilo yaliyoko mjini Geneva. Kwenye makao makuu hayo, Rais Kikwete pia amelakiwa na watumishi wote wa shirika hilo ambao wametoka nje ya ofisi yao kumlaki kwa makofi na vifijo.
Mheshimiwa Guterres amemwambia Rais Kikwete: “Tunafurahi kuwa umefika kwenye makao makuu yetu na tunapenda kuishukuru Tanzania tokea wakati wa Mwalimu Nyerere mpaka wakati wako kwa yote ambayo mmetufanyia. Tanzania imekuwa ishara kuu ya matumaini na imekuwa mlinzi mkuu wa wakimbizi duniani.”amesema Mheshimiwa Guterres.
Viongozi hao wawili pia wamejadili hali ilivyo katika Burundi na Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Guterres kuwa watu wanaokimbia Burundi kuingi katika Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanakimbia kwa hofu tu lakini Burundi hakuna vita wala mapigano.
“Hakuna tishio la usalama kuhalalisha uzalishaji wa wakimbizi, lakini tumewapokea. Hakuna kubwa la kufanya kwa sababu unaamka asubuhi, unakuta wamekwishaingia nchini.”
Rais Kikwete pia amemwambia Mheshimi Guterres ambaye alipata kuwa Waziri Mkuu wa Ureno kwa miaka sita unusu: “Tutaendelea kuunga mkono wakimbizi. Tanzania siyo nchi tajiri na hivyo ni matarajio yetu kuwa Jumuia ya Kimataifa itatusaidia katika kuwatunza wakimbizi hao.”
Kuhusu ombi la UNHCR kupatiwa eneo kubwa la kujenga miundombinu na huduma kwa ajili ya wakimbizi hao 78,000, Rais Kikwete amesema kuwa ataangalia nini la kufanya kumaliza tatizo la msongamano wa wakimbizi hao.
Wakimbizi wa sasa ni mkumbo wa nne wa wakimbizi wa Burundi kuingia kwa wingi nchini tokea Uhuru mwaka 1961.
UNHCR ni moja ya mashirika 31 ya kimataifa yenye makao yake katika Jiji la Geneva ambalo pia ni mwenyeji wa mashirika ya kimataifa yasiyokuwa ya Serikali zaidi ya 250 na balozi za kudumu 250 za nchi 173. Balozi wa Kudumu wa Uswisi katika Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) Mheshimiwa Bruno Favel anasema kuwa mji huo ni mji mkuu wa shughuli za kibinadamu na masuala ya afya.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Julai 2015