Taarifa kwa vyombo vya Habari ya zamani
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzania yaunga mkono Malengo Endelevu ya Maendeleo duniani
- Yasema kuwa ni silaha tosha kufuta umasikini duniani katika sura zake zote
- Ni ya miaka 15, yachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia
Tanzania imeunga mkono rasmi Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals – SDG’s), ikisisitiza kuwa, kwa hakika, malengo hayo ni silaha ya kutosha ya kufuta umasikini duniani katika sura zake zote ifikapo mwaka 2030.
Tanzania pia imesema kuwa endapo dunia itafanikiwa kutekeleza SDG’s katika miaka 15 ijayo kama ilivyopangwa ni dhahiri kuwa ifikapo mwaka 2030 dunia itakuwa mahali pazuri zaidi pa kuishi kwa ajili ya “watoto wetu na watoto wa watoto wetu.”
Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa Jumamosi, Septemba 26, 2013 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linalojadili kwa nia ya kupitisha SDG’s chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Denmark, Mheshimiwa Lars Lokke Rusmussen.
Rais Kikwete ameliambia Baraza Kuu hilo kuwa ni vyema vile vile nchi zilizoendelea kuelewa fika kuwa pamoja na kwamba nchi zinazoendelea zitalenga kutimiza wajibu wake wa msingi wa kuzalisha fedha za ndani kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizo, bado juhudi pekee za nchi zinazoendelea hazitatosha kuhakikisha utekelezaji kamili wa agenda hiyo ya maendeleo endelevu inayojulikana rasmi kama, “Transforming our World: The 2030 Agenda for Sustainable Development.”
“Juhudi za nchi zilizoendelea zitaongeza nguvu katika juhudi zetu wenyewe ambazo nazo zina ukomo. Ni ushirikiano huu kati ya walioendelea na sisi tunaoendelea ambao utatuhakikishia utelekezaji kamili wa malengo mapya ya maendeleo endelevu. Tafadhalini endeleeni kutushika mkono. Hili ndilo jambo la maana zaidi, bora zaidi na la ukweli zaidi kwa ajili ya faida yetu sote.”
Rais Kikwete amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni mwendelezo wa shughuli zake mjini New York, Marekani, ambako anahudhuria mikutano mbali mbali ya Baraza Kuu la UN mwaka huu ambayo kimsingi yote inalenga katika kujenga msingi mzuri wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu mapya katika mambo mbali mbali.
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) yanachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia – Millennium Development Goals (MDG’s) ambayo utekelezaji wake wa miaka 15 umefikia mwisho mwaka huu. Wakati MDG’s ulikuwa na malengo manane, SDG’s una malengo 17 na shahaba za kukamilishwa 169.
Rais Kikwete pia amegusia baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa ni kikwazo kwa nchi nyingi zinazoendelea duniani kilichozifanya nchi huzo kushindwa kufikia malengo yote ama baadhi yake ikiwamo changamoto ya upatikanaji wa fedha za kutosha na kwa wakati kwa ajili ya utekelezaji wa MDG’s.
“Ni muhimu kulitaja jambo hilo, kama jambo muhimu na jambo kuu, kwa sababu ilikuwa ni hali ya ukosefu wa uhakika wa upatikanaji wa raslimali fedha ambao ulikuwa kikwazo kikubwa kuliko vyote katika utekelezaji wa MDG’s,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Ni jambo linalonipa faraja, hata hivyo, kuwa katika mpango wa malengo mapya ya maendeleo endelevu, jambo hilo limefafanuliwa na kupewa umuhimu pekee. Upatikanaji wa raslimali fedha wenyewe ni lengo linalojitegemea, lengo nambari 17, ambalo linaelezea jinsi gani ya utekelezaji wa kila mojawapo ya malengo hayo.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za Rambirambi Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda, kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mheshimiwa Celine Ompeshi Kombani.
“Pokea rambirambi zangu za dhati, sote kwa pamoja tumepoteza mama mchapakazi, hodari na aliyependa kushirikiana na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote” Rais Amesema.
Rais Pia amemtumia salamu za pole mume wa marehemu Kombani, Bwana Swaleh Ahmad Pongolani, watoto, ndugu na jamaa wa Mama Kombani.
“Nimepokea taarifa za kifo cha mama Kombani kwa huzuni kubwa, najua machungu na maumivu mliyonayo kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika familia yenu, poleni sana, mama ni nguzo ya familia, niko nanyi katika msiba huu mzito kwenu” Rais ametuma salamu hizo kwa Mume wa Marehemu Celine, Bwana Pongolani, watoto, wajukuu na ndugu wa Marehemu mama Kombani.
Rais amesema pamoja na kwamba kifo hakiepukiki, bado ni kitu ambacho kinashtua, kuhuzunisha na kuleta unyonge mkubwa kwa wafiwa katika jamii.
Marehemu Kombani pia alikua ni mgombea ubunge wa jimbo la Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, ambapo amekwisha kulitumikia jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.
“Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu kumuombea Mama Kombani ili mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema ya Milele” Rais amesema na kuwaombea wana familia na ndugu wa Marehemu “Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape uvumilivu na subira katika kipindi hiki”.
“Niko nanyi katika kipindi hiki kigumu kwa hali na mali, nawaomba msijisikie wapweke” Rais amesema na kuwatakia utulivu na amani katika kipindi hiki cha msiba mkubwa kwa familia ya mama Kombani
Marehemu Mama Kombani amefariki jana tarehe 24 Septemba, 2015 nchini India ambapo alikua anapatiwa matibabu baada ya kugundulika kuwa na kansa.
Marehemu Kombani alizaliwa Juni 19, 1959 ameacha Mume, watoto watano na wajukuu wane.
Mwili wa marehemu unatarajia kuwasili nchini kesho mchana na anatarajiwa kuzikwa Mkoani Morogoro katika shamba lake.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Celine Kombani mahali Pema Peponi, Amina.
…………………………Mwisho………………………
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM.
25 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Kikwete afafanua changamoto za utaalii wa Afrika
- Asema habari hasi kuhusu Afrika zinavuruga utalii wa Afrika
- Asisitiza Tanzania itaendelea kupambana na ujangili
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea changamoto kubwa zinazozuia kukua haraka zaidi kwa sekta ya utalii katika Afrika na hivyo kuliwezesha Bara hilo kuchuma matunda makubwa zaidi kutokana na sekta hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii, Bara la Afrika, bado linabakia nyuma kwa kiasi kikubwa katika kuvutia watalii wa kimataifa na katika mapato yanayotokana na utalii.
Rais Kikwete vile vile amesema kuwa Tanzania itaendelea kutenga eneo kubwa la ardhi yake kwa ajili ya hifadhi na pia itaendelea kukabiliana na ujangili dhidi ya tembo, ambao hata hivyo amesema kuwa umepungua katika mwaka uliopita.
Rais Kikwete ameyasema hayo, Alhamisi, Septemba 24 wakati alipotoa hotuba ya ufunguzi wa shughuli za Miaka 10 ya Chama cha Usafiri cha Afrika – Africa Travel Association (ATA) na Miaka 10 ya Jukwaa la Rais Kuhusu Utalii – Presidential Forum on Tourism kwenye Kituo cha Kimmel cha Chuo Kikuu cha New York (New York University Kimmel Center) Africa House, mjini New York.
Rais Kikwete yuko New York, Marekani kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) baada ya kumaliza kuendesha vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani ambao wanatafuta jinsi gani dunia inavyoweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambavyo pia vilifanyika New York.
Rais Kikwete ametambulishwa na kukaribishwa kutoa hotuba yake na Dkt. Yaw Nyarko, Raia wa Ghana na Mkurugenzi wa Africa House ambaye pia ni Profesa wa Uchumi kwenye Chuo Kikuu cha New York na Bwana Edward Bergman, Mkurugenzi Mtendaji Mwanzilishi wa ATA.
Alikuwa ni Rais Kikwete na familia ya Bergman ya New York ambao walianzisha na kujadili wazo la kuanzishwa kwa chama hicho miaka 10 iliyopita.
Kabla ya kutoa hotuba yake, washiriki wa Kumbukumbu hiyo ya miaka 10 wamesikia maelezo ya kina kutoka kwa mawaziri wa nchi tano za Afrika kuhusu hali ya utalii katika nchi hizo na katika Bara la Afrika kwa jumla.
Mawaziri waliozungumza kwenye shughuli hiyo iliyoendeshwa na Bwana Peter Greenberg, Mhariri wa Usafiri wa Televisheni ya CBS ni Mheshimiwa Lazaro Nyalandu wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Maria Mutagamba, Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Nyaraka wa Uganda ambaye pia ni Rais wa ATA na Mheshimiwa N’Diaye Ramatoulaye Diallo, Waziri wa Utamaduni, Utalii na Usanii wa Vinyango wa Mali.
Mawaziri wengine ambazo wamezungumza katika shughuli hiyo ni Mheshimiwa Phylis Kandie ambaye ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya na Mheshimiwa Pohamba Shifeta, Waziri wa Mazingira na Utalii wa Jamhuri ya Namibia.
Akizungumza katika shughuli hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa “changamoto kuu zinazokabili maendeleo ya utalii katika Afrika ni miundombinu ya kitalii, utangazaji wa masoko ya utalii na matatizo ya usafiri wa anga kuingia na kutoka Afrika.”
“Lakini pia kuna jambo kubwa la mtazamo hasi kuhusu Afrika. Kwa kawaida, vyombo vya habari vya nje vinalielezea Bara la Afrika kama Bara hatari ambalo sifa zake kuu ni migogoro, magonjwa na matatizo yanayotokana na umasikini. Haya yote siyo ya kweli ni upotoshaji wa makusudi.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Ukweli kuhusu Afrika lazima uelezwe kwa usahihi na sisi wenyewe. Picha inayojengwa kuwa tatizo katika nchi moja ni tatizo la Bara zima siyo ya kweli na lazima itafutwe namna ya kulisahihisha jambo hilo. Afrika ni Bara la nchi 54 na siyo nchi moja ya majimbo 54.”
Ameongeza: “Ni upotoshaji huu ambao ulisababisha watu kufuta safari za kitalii kwenda Afrika wakati ugonjwa wa Ebola ulipolipuka katika Guinea, Liberia na Sierra Leone. Lakini Zanzibar katika Tanzania ni safari ya saa tisa za ndege kutoka nchi hizo tatu za Afrika Magharibi. Kwa hakika nchi hizo tatu ziko karibu zaidi na Bara la Ulaya kuliko ilivyo Kenya. Hili ni tatizo kubwa ambalo lazima lisahihishwe haraka iwezekanavyo.”
Kuhusu mapato ya utalii, Rais Kikwete amesema: “Mwaka jana, Afrika ilipokea watalii wa kimataifa milioni 56 ambalo ni ongezeko la asilimia mbili tu ya watalii wote wa kimataifa waliotembelea maeneo mbali mbali ya dunia na asilimia tano ya watalii wote waliotembelea dunia mwaka jana.”
Kuhusu Tanzania, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania inaendelea kutenga asilimia 36 ya eneo lake lote kwa ajili ya shughuli za hifadhi.
“Tumefanya hivyo tokea uhuru wetu. Tutaendelea kufanya hivyo. Kama mnavyojua pia tumekuwa tunakabiliana na changamoto ya ujangili ambao ulitishia kumaliza idadi ya tembo wetu. Tumechukua hatua na kuendesha kampeni dhidi ya janga hili. Sasa tunaanza kuona matunda ya juhudi zetu. Mwaka 2012 walikuwa wanauawa tembo sita kwa mwezi. Katika mwaka mmoja uliopita, hajauawa tembo yoyote.”
Rais Kikwete pia ameshangiliwa sana wakati alipowaambia washiriki wa shughuli ya leo: “Napenda kuchukua nafasi hii, vile vile, kuwaageni marafiki zangu wote wa ATA kwa sababu hotuba hii ni ya mwisho kwangu nikiwa Rais wa nchi yangu. Nitaondoka madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, 2015 baada ya kuwa nimekamilisha vipindi viwili vya uongozi wangu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marais Kikwete, Museveni wakutana New York
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya Alhamisi, Septemba 24, 2015 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni mjini New York, Marekani, ambako viongozi hao wawili wapo kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Matifa (UNGA).
Viongozi hao wawili wamekutana kwenye Hoteli ya Trump International Hotel na Tower, ambako Rais Museveni amefikia, na wamezungumzia masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Uganda, yanayohusu Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) ambako Tanzania na Uganda ni wanachama na masuala mengine.
Miongoni mwa mambo ambayo viongozi hao wamezungumzia ni maendeleo ya uchimbaji mafuta katika Uganda na faida za mafuta hayo kwa Tanzania na kwa nchi zote wanachama wa EAC wakati ukifika mafuta hayo yakaanza kutumika.
Marais hao pia wamejadili hali ya kisiasa katika nchi jirani ya Burundi ambayo pia ni mwanachama wa EAC. Rais Museveni ndiye amepewa jukumu na viongozi wenzake wa EAC kusimamia mazungumzo ya kuleta maelewano na maridhiano ndani ya Burundi wakati Rais Kikwete ndiye Mwenyekiti wa sasa wa EAC.
Viongozi hao pia wamejadili hali ya kisiasa na kiusalama ilivyo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na jinsi gani juhudi zinavyoweza kufanyika kusaidia kuboresha hali hiyo hasa kwa kutilia maanani kuwa Tanzania inayo majeshi ya kulinda amani nchini humo.
Rais Kikwete na Rais Museveni pia wamepata nafasi ya kujadiliana kuhusu hali ya jumla ya kisiasa katika Afrika na jinsi gani hali hiyo inavyoweza kuimarishwa katika baadhi ya nchi.
Miongoni mwa viongozi ambao wamehudhuria mazungumzo hayo ni Mheshimiwa Sam Kutesa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda ambaye pia anamaliza muda wake kama Rais wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na Mheshimiwa Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Kikwete amesema kuwa Serikali mpya haitabadilisha uhusiano
wa Tanzania na Marekani
- Aiomba Serikali ya Marekani kuendelea kuiunga mkono Serikali mpya kama ilivyofanya kwake
- Aishukuru kwa misaada iliyobadilisha maisha ya Watanzania katika miaka 10 ya uongozi wake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameihakikishia Serikali ya Marekani kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili hautabadilika na kuwa utaendelea kuboreshwa zaidi hata baada ya kuingia madarakani kwa Serikali mpya Novemba mwaka huu, 2015.
Aidha, Rais Kikwete ameiomba Serikali ya Marekani kuunga mkono utawala mpya wa Tanzania unaoingia madarakani Novemba mwaka huu kwa kiwango kile kile ambacho Serikali hiyo imeipatia Serikali yake kwa miaka 10 iliyopita.
Vile vile, Rais Kikwete ameishukuru Serikali na wananchi wa Marekani kwa misaada mingi ambayo imechangia sana kuboreka kwa maisha ya Watanzania na kuinua kiwango cha maendeleo nchini katika miaka 10 ya uongozi wake wa Tanzania.
Rais Kikwete ameyasema hayo , Jumanne, Septemba 22, 2015 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani, Mheshimiwa Anthony Blinken kwenye Hoteli ya Ritz-Carlton mjini Washington ambako Rais Kikwete amefikia katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili kwenye mji huo mkuu wa Marekani.
Rais Kikwete amemwambia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani: “Sioni uwezekano wowote wa msimamo wa Serikali mpya ya Tanzania kuhusu uhusiano wake na Marekani kuwa tofauti na ule ambao umekuwepo katika miaka 10 iliyopita. Dhahiri uhusiano huo hautabadilika kama Rais mpya atatoka katika chama chetu, lakini hata Rais akitokea chama kingine, sioni kama yanaweze kuwepo mabadiliko yoyote ya msingi ya sera au uhusiano kati ya Tanzania na Marekani.”
Kuhusu ombi lake ya Serikali ya Marekani kuendelea kuunga mkono Serikali ijayo ya Tanzania, Rais Kikwete amesema: “Naiomba Serikali ya Marekani iendelee kuunga mkono Serikali yetu ijayo na wananchi wa Tanzania.”
Ameongeza: “ Nawaombeni muendelee kuunga mkono maendeleo ya Tanzania. Matunda ya misaada yenu sasa yameanza kuonekana. Kwa mfano katika miaka 10 iliyopita Pato la Taifa limepanda mara tatu kutoka dola za Marekani bilioni 14.4 hadi kufikia dola za Marekani bilioni 50 kwa sasa.”
Kuhusu misaada ambayo Serikali ya Marekani imeitoa kwa Tanzania katika miaka 10 ya uongozi unaomaliza muda wake, Rais Kikwete amesema: “Naishukuru sana Serikali na wananchi wa Marekani kwa misaada mingi na kila aina ambayo mmeitoa kwa nchi yetu na Serikali yangu. Mmeacha nyanyo katika maendeleo ya nchi yetu. Tumepata ustawi usiokuwa wa kawaida katika miaka 10 iliyopita.”
Rais Kikwete amesema kuwa Marekani kupitia mpango wake wa Pepfar, imechangia kupunguza sana makali ya magonjwa ya malaria na ukimwi. “Kwa upande wa malaria, mmesaidia kuokoa mamilioni ya maisha ya watu na vifo kutokana na ugonjwa huo sasa vimepungua kwa kiwango cha asilimia 70. Maambukizo ya ugonjwa wa ukimwi yamepungua sana. Matokeo yake ni kwamba wastani wa Watanzania kuishi umepanda kutoka miaka 55 hadi kufikia miaka 62 katika kipindi kifupi sana cha miaka 10 tu.”
Baada ya hapo, Rais Kikwete ameingia katika undani wa misaada ya Marekani katika maeneo mbali mbali kuanzia kwenye kilimo na mipango inayoungwa mkono na Marekani ya Feed The Future na Alliance for Food and Nutrition Sufficiency.
“Kutokana na misaada yenu, sasa tunajitegemea kwa chakula na hata kubakiza kiasi cha kuwauzia majirani zetu. Na hii yote ni kwa kutilia maanani kuwa wakati tunaingia madarakani tulilazimika kuwalisha kiasi cha watu 3.7 milioni kwa sababu ya ukame na ukosefu wa chakula.”
Kwa upande wa misaada iliyotolewa chini ya Mpango wa Millenium Challenge Corporation (MCC - 1), Rais amesema kuwa misaada hiyo katika ujenzi wa barabara, usambazaji umeme na kuanzishwa kwa miradi ya kusambaza maji imechangia mno kuboresha kiwango cha maisha ya Watanzania.
“Chini ya MCC, tumejenga kwa kiwango cha lami barabara zote za Pemba, tumejenga barabara kubwa kama ile ya Tanga-Horohoro, Tunduma-Sumbawanga, Songea-Namtumbo, tumepanua huduma za maji katika miji ya Dar es Salaam na Morogoro na tumesambaza umeme katika mamia ya vijiji katika mikoa 10 ya Tanzania Bara. Mwaka 2015, ni asilimia 10 ya vijiji vyetu vilikuwa na umeme. Sasa kwa msaada wetu, kiwango hicho kimefikia asilimia 46.”
Katika sekta ya elimu, Marekani imesaidia upatikanaji wa vitabu vya kufundishia masomo ya hisabati na sayansi katika shule za sekondari nchini. “Msaada wetu katika eneo hili, umeanza kuboresha elimu yetu. Ubora wa elimu umepanda na viwango vinapanda.”
Rais Kikwete pia ameishukuru Serikali ya Marekani kwa misaada yake katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na katika masuala ya usalama na vita dhidi ya ugaidi akisisitiza: “kwa sababu ya misaada yenu katika eneo hili, tuko imara zaidi hata kama matishio bado yapo.”
Rais pia ameishukuru Serikali ya Tanzania katika ujenzi wa utawala bora yakiwemo mapambano dhidi ya rushwa. “Demokrasia yetu inaendelea kuwa bora zaidi. Tunaendelea kupambana na rushwa, hata kama mapambano yenyewe ni magumu. Kama mnavyojua, hata mawaziri wenzangu wawili sasa wako jela baada ya kupatikana na hatia za matumizi mabaya ya madaraka.”
Rais Kikwete pia ameishukuru Serikali ya Marekani kwa mchakato wa kuanzishwa kwa Mpango wa MCC -2, akisisitiza kuwa changamoto ambazo zimejitokeza katika maandalizi ya mpango huo zitashughulikiwa ipasavyo na kwa haraka na Serikali yake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
24 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
JK: Mwenye tatizo na Muswada wa Habari alete maoni Serikalini
badala ya kukaa na kulalamika
- Aunga mkono asilimia 100 staili ya Kampeni ya Magufuli
- Asema Tanzania inahitaji mawazo mapya ili iweze kusonga mbele
- Atamani muda wake wa kuongoza Tanzania kumalizika haraka zaidi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kama wapo watu binafsi ama taasisi yoyote mahali popote wenye matatizo na Sheria ya Takwimu mpya ama Muswada wa Habari nchini basi wawasilishe mapendekezo yake Serikalini ili yafanyiwe kazi badala ya kukaa na kulalamika pembeni ama kwenye vyombo vya habari.
Rais Kikwete pia amesema kuwa ni jambo zuri na jema kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM anaelezea fikra na matumaini ya kuleta mabadiliko makubwa zaidi katika uendeshaji wa Tanzania tofauti na uendeshaji huo ulivyo chini ya uongozi wake.
Vile vile, Rais Kikwete amesema kuwa anatamani muda uende kwa kasi zaidi ili aweze kukabidhi madaraka ya kuongoza Tanzania kwa Rais wa Tano, ili yeye apate muda wa kumpumzika baada ya kazi ngumu ya miaka 10 ambayo ameilezea kama mzigo mkubwa.
Rais Kikwete ameyasema hayo, Jumanne, Septemba 22, 2015 wakati alipozungumza na wafanyakazi wa taasisi nne za Marekani ambazo kwa namna moja ama nyingine zimefanya kazi na Serikali yake katika miaka 10 ya uongozi wake mjini Washington, D.C., ambako Rais amefanya ziara ya siku mbili ya kikazi.
Rais Kikwete amezungumza na wafanyakazi wa taasisi za National Democratic Institute (NDI) yenye uhusiano na chama cha siasa cha Democratic, International Republican Institute (IRI) yenye uhusiano na chama cha siasa cha Republican, International Foundation for Electoral Systems (IFES) na United States Institute of Peace (USIP) kwenye makao makuu ya NDI.
Wakati wa kipindi cha maswali na majibu na wafanyakazi wa taasisi hizo, Rais Kikwete ameulizwa swali kuhusu madai kuwa Sheria ya Takwimu na Muswada wa Habari inavuruga sifa za kidemokrasia za Tanzania chini ya uongozi wa Rais Kikwete.
Akijibu swali hilo, Rais Kikwete amesema: “Nimelizungumza hilo huko nyuma na napenda kurudia. Sheria ya Takwimu inahusu tu takwimu rasmi za Serikali na wala si takwimu zote. Pili Sheria hii inatokana na matakwa na taratibu za Umoja wa Mataifa na Sheria yetu imetungwa kwa kutilia maanani matakwa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa. Kwa nini hili linakuwa tatizo kwa Tanzania pekee ni jambo gumu kueleza.”
Kuhusu Muswada wa Sheria ya Habari, Rais Kikwete amesema: “Nimelisema hili huko nyuma lakini inaelekea halijaeleweka. Nilipata kusema pale Dar es Salaam na hata wakati nazungumza na wabunge wa Sweden mjini Stockholm kuwa kama mtu ana tatizo ama maoni na maudhui ya Muswada ule basi ayafikishe Serikali. Tutafanyia kazi. Hakuna tatizo na jambo hili. Ajabu ni kwamba tunachosikia ni malalamiko tu na hakuna yoyote ambaye amefikisha maoni yake kwetu.”
Hata hivyo, Rais Kikwete ameongeza: “Jambo muhimu ambalo lazima sote tuelewane hapa ni kwamba Muswada wowote, uwe wa habari ama wa jambo jingine, ni lazima ulinde maslahi ya nchi yetu, yalinde umoja wetu, yalinde utulivu wa nchi yetu na yalinde usalama wa nchi yetu. Haya ni mambo ambayo hatuna haja ya kujadiliana na yoyote kwa sababu nchi zote duniani zinalinda kwa namna hii na zinaendeshwa namna hii.”
Rais Kikwete pia ameunga mkono mwenendo wa mgombea urais wa CCM wakati wa kampeni ya Uchaguzi mkuu inayoendelea nchini, Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli, akisema: “Wamepata kuja watu kwangu… wakaniambia kuwa Mgombea wetu wa CCM anashutumu na kusahihisha Serikali yangu na utendaji wake kwenye mikutano ya kampeni. Niliwaambia hivi…..analofanya Mgombea wetu ni jambo sahihi na barabara kabisa na lazima afanye hivyo.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Niliwaambia nchi yetu inahitaji mawazo mapya na mwelekeo mpya ulio tofauti na uongozi wangu. Niliwambia kuwa tuliporuhusu jambo hilo kufanyika, nchi yetu itabakia pale pale ambako nimeifikisha mimi. Haya yatakuwa na makosa makubwa kwa sababu nchi yetu lazima isonge mbele kwa mawazo mapya, kwa uongozi mpya na kwa staili mpya ya uongozi. Na haya ndiyo anayasema Mgombea wetu. Vinginevyo ni jambo lisilokuwa na maana kubadilisha uongozi kama hatuko tayari kukubali kuwa kila kiongozi lazima awe na staili yake ya uongozi na namna yake ya kuongoza na kuendesha nchi yetu.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
24 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzania kunufaika na uwekezaji wa mabilioni ya Marekani katika umeme
. Ni moja ya nchi tatutuza Afrika zitakazonufaika kwa sasa
. India nayo italengwa na mpango huo wasekta binafsi
. Walioubuni wasema umasikini haufutiki bila umeme wa kutosha
Tanzania nimojayanchitatutuzaAfrikaambazozitanufaikanauwekezajiwamabilioniyafedhakatikasektayaumemekutokananampangomaalumwakuwekezakwakiwangokikubwakatikahudumazaumemekatikaAfrikakwaniayakuongezakasiyamaendeleonakupunguzakiwango cha umasikini.
RaiswaJamhuriyaMuunganowa Tanzania, MheshimiwaJakayaMrishoKikweteameambiwaJumanne, Septemba 22, 2015, mjiniWashington D.C. Marekanikuwa, Tanzania itakuwamiongonimwanchiambazozitanufaikanauwekezajiambaoutafikiakiasi cha bilionitanozadolazaMarekani.
MtendajiMkuunaMtawalaMkuuwazamaniwaShirika la MaendeleoyaMisaadayaKimataifa la Marekani (USAID), Bwana Raj Shah, amemwambiaRaisKikwetekuhusumpangohuowakatiwalipokutanakatikaHoteliya Ritz-Carlton, Washington, D.C. MarekaniwakatiwaziarafupiyasikumbiliyaRaisKikwetekatikamjimkuuhuowaMarekaniakitokeakatikajiji la New York.
Bw. Shah ambayepianimjumbekatikaJopo la WatuMashuhuriDunianilinaloongozwanaRaisKikwetekuangaliajinsiduniainavyowezakukabilianavizurizaidinamagonjwayamilipukokatikasikuzijazoamemwambiaRaisKikwetekuwaunaanzishwampangomkubwawamabilioniyafedhawakuzalishaumemekatika Bara la Afrikana India kwaniayakuharakishamaendeleoyamaeneohayomawili.
“ChiniyampangomaalumunaosimamiwanaLatitude Capital, tunaanzishajuhudibinafsiambazouwekezaji wake utafikiadolazaMarekanibilionitanokuzalisha, kusafirishanakuzambazaumemehasakatika Tanzania, Ghana na Kenya nabaadayenchinyinginezinazotawaliwavizurizaidikatikaAfrika,”amesemaBw. Shah nakuongeza:
“Mpangohuuunatokananampangokabambewa Power Africa uliotangazwanaRais Barack Obama wakatiwaziarayakekatika Tanzania Julai 1-2, mwaka 2013 nataasisizaBenkiyaDunia, IFC, BenkiyaMaendeleoyaAfrika (AfDB) zikotayarikuwekezamabilioniyafedhakatikakuzalishaumemekatikaAfrikana India.”
Bw. Shah amemwambiaRaisKikwetekuwauamuziwakuanzishampangohuoumetokananaukwelikuwawaanzilishiwake wamefikiaazmakuwanivigumukumalizaumasikinikatikaAfrikana India bilakupatikanaumemewakutosha.
“UzalishajinautumiajiwaumemekatikaAfrikana India nikidogosana. Tunatakakuwakatikamiaka 15 ijayo, Afrikana India, ziwenaumemewakiasi cha sasa cha umemeunaotumikakatikaMarekani. Tunatakakuwanampangowenyekufanyakazikwaufanisisanakatika Tanzania.”
Bw. Shah piaamesemakuwa“chiniyampangohuo, uwekezajiutakuwakatikamiradimikubwayaserikaliyaumemeambayohainamtajiwakutosha, kuanzishamiradimipyanakuanzishamiradiyapamojayaSerikalinasektabinafsi.”
MpangohuounaongozwanaMtendajiMkuu Bwana Frank Perez ambayeamepatakuwaMtendajiMkuuwakampuniyataifayakuzalishaumemeyaAbudhabiyaAbudhabi National Power CompanyambayeameandamananaBw. ShahkujakumwonaRaisKikwete.
Imetolewana:
KurugenziyaMawasilianoyaRais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani yamwagia sifa Rais Kikwete kwa kuheshimu Katiba na kukabidhi madaraka
Viongozi wa Marekani wamemwagia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete sifa kubwa za ujenzi na ulezi wa demokrasia, heshima kwa haki za binadamu na zaidi ya yote uheshimu wa Katiba ambao unamwezesha kuondoka madarakani kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na kukabidhi madaraka kwa Rais ajaye kwa hiari na kwa amani.
Rais Kikwete amemwagiwa sifa hizo, Jumanne, Septemba 22, 2015 katika mikutano yake mbali mbali na viongozi wa Serikali ya Marekani na wa taasisi kubwa na muhimu zisizokuwa za Kiserikali nchini humo katika ziara yake ya siku mbili katika mji mkuu wa Marekani wa Washington, D.C.
Rais Kikwete ametembelea Washington kutoka mjini New York ambako amemaliza kuendesha vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani wanaotafuta jinsi gani dunia inaweza kujikinga vizuri zaidi dhidi ya magonjwa ya milipuko kufuatia madhara makubwa ya ugonjwa wa Ebola.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mheshimiwa Anthony J. Blinken amemwambia Rais Kikwete kuwa uamuzi wake wa kuheshimu Katiba ya Tanzania kwa kukabidhi madaraka ya uongozi wa nchi baada ya kumaliza vipindi viwili vya uongozi wake, unatuma ujumbe mzito, dhahiri na unaosikika sana katika Bara zima la Afrika na Kanda ambako Tanzania ipo.
“Mafanikio yako ya uongozi yamekuwa ya kifani kabisa. Hayana mfano katika Afrika ya leo. Umeacha historia kubwa na ya kudumu (legacy) ya kuheshimu demokrasia na Katiba ya nchi yako. Umeacha na kutuma ujumbe wa wazi kabisa kwa Bara zima la Afrika na katika ukanda ambako nchi yako ya Tanzania ipo,” amesema Mheshimiwa Blinken katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Ritz-Carlton, Georgetown, ambako Rais Kikwete alikuwa amefikia.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani mwishoni mwa mwaka jana, Mheshimiwa Blinken alikuwa Msaidizi wa Rais Barack Obama na Msaidizi Mkuu wa Baraza la Ushauri wa Usalama la Marekani. Pia amepata kuwa msaidizi wa ushauri wa usalama wa Makamu wa Rais wa Marekani na pia amepata kuwa ujumbe kwenye Baraza la Ushauri wa Taifa la Rais Bill Clinton.
Naye Mheshimiwa Ken Wallack, Rais wa Taasisi ya National Democratic Institute (NDI) ya chama cha siasa cha Democratic amemwambia Rais Kikwete:
“Tuseme hivi…kwa kutilia maanani yanayotokea katika dunia ambako unaishi na unatokea, sote tunakushukuru na kukupongeza kwa msimamo wako wa kuheshimu Katiba ya nchi yako. Unajiunga na kundi la viongozi wa kuheshimiwa sana katika Bara la Afrika ambao hawakuamini kuwa wao tu ndio wenye uwezo wa kuongoza.”
Mheshimiwa Balozi Mark Green, Rais wa Taasisi ya International Republican Institute (IRI) ya chama cha siasa cha Republican amemwambia Rais Kikwete, ”unaacha mfano kwetu sisi sote katika kupigania na kulea demokrasia duniani na hasa katika Bara la Afrika.”
Balozi Green amepata kuwa Balozi wa Marekani katika Tanzania wakati wa kipindi cha uongozi wa Rais Kikwete na alichangia kwa kiasi kikubwa jitihada za Serikali ya Rais Kikwete katika nyanja nyingi za maendeleo.
Aliyekuwa waziri mdogo wa Mambo ya Nje Marekani aliyeshughulikia masuala ya Afrika, Mheshimiwa Johnnie Carson amemwambia Rais Kikwete: “Kuna kiwango kikubwa cha heshima kwako katika Marekani kwa jinsi ulivyoongoza nchi yako na Serikali yako katika miaka 10 iliyopita. Chini ya uongozi wako, Tanzania imeendelea kuonyesha mfano usiokuwa na kifani katika ujenzi wa demokrasia na umeheshimu sana Katiba ya nchi yako. Sisi katika Marekani, tunakupongeza sana.”
Balozi Carson ambaye sasa ni Rais wa Taasisi ya Amani katika Marekani ya United States Institute of Peace amesema kuwa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Kikwete imeendelea kuwa rafiki mkubwa zaidi wa Marekani katika Afrika.
Waheshimiwa Wallack, Balozi Green na Balozi Carson wamezungumza wakati Rais Kikwete alipokutana kwa mazungumzo na viongozi wa taasisi za NDI, IRI, Peace Institute na IFES katika makao makuu ya NDI mjini Washington. Mwenyekiti wa NDI, Balozi Madeline Albright, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani za zamani hakuweza kuhudhuria mazungumzo hayo hata kama alituma salamu zake kwa Rais Kikwete.
Akizungumza baada ya kutolewa sifa zake za kuheshimu demokrasia na Katiba ya Tanzania, Rais Kikwete amewaambia viongozi wa taasisi hizo maarufu duniani: “Nawaheshimu sana wale ambao wanataka kuendelea na madaraka ya kuongoza nchi zao. Kazi ya urais ni kazi ngumu na mzigo mkubwa, ukiifanya miaka kumi inatosha.”
Ameongeza: “Isitoshe katika Tanzania tuna jadi sasa ya kuheshimu Katiba. Unachaguliwa kwa miaka mitano na ukichaguliwa tena unaongeza mingine mitano. Baada ya hapo unawapisha watu wengine. Isitoshe ni jambo zuri kupata kiongozi mpya baada ya muda ambaye atakuja na mawazo mapya na aina mpya ya uongozi.”
Rais Kikwete amerejea mjini New York usiku wa leo tayari kuhudhuria shughuli za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (General Assembly) mwaka huu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa tuzo nyingine, zamu hii ikiwa imetolewa na wananchi wa Afrika Mashariki ambao wanaishi katika nje ya Afrika Mashariki na hasa Marekani (East African Diaspora) kutambua utawala bora wa uongozi wake katika nchi za Afrika Mashariki.
Tuzo hiyo imetolewa kwa niaba ya Wana-Afrika Mashariki hao na Baraza la Biashara la Wana-Afrika Mashariki Waishio Nje ya Afrika Mashariki – East African Diaspora Business Council (EADBC) ambalo linaunganisha wafanya biashara wa nchi za Afrika Mashariki wanaoishi nje ya eneo la Afrika Mashariki.
Tuzo hiyo kwa Rais Kikwete lilitolewa usiku wa Jumapili, Septemba 20, 2015, katika sherehe iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency ya Dallas Kaskazini, Jimbo la Texas na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania katika Marekani, Mheshimiwa Wilson Masilingi ambaye alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Kikwete.
Awali, Rais Kikwete ambaye anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Marekani alikuwa apokee tuzo hiyo mwenyewe lakini kwa sababu ya kutingwa na shughuli nyingi za kikazi katika miji ya New York na Washington, D.C alimwomba Balozi Masilingi kumwakilisha.
Rais Kikwete aliwasili nchini Marekani wiki iliyopita kuongoza vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani ambalo limepewa jukumu la kupendekeza njia bora zaidi za jinsi dunia inavyoweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko katika siku zijazo kufuatia balaa la ugonjwa wa Ebola ambao uliua zaidi ya watu 11,000 katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone katika muda mfupi.
Jopo hilo lenye wajumbe sita, wakiongozwa na Rais Kikwete, liliteuliwa Aprili mwaka huu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Ban Ki Moon ambaye ametaka wana-jopo hao kuwasilisha ripoti yao kwake Desemba mwaka huu. Wajumbe wengine wanatoka Botswana, Brazil, Indonesia, Marekani na Uswisi.
Katika sherehe za usiku wa jana mjini Dallas, Balozi Masilingi alipokea tuzo hiyo ya utawala bora katika Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais Kikwete kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Bwana David Mureeba, raia wa Uganda, ambaye amemweleza Rais Kikwete kuwa ni kiongozi wa mfano katika eneo la Afrika Mashariki na Bara zima la Afrika.
Tuzo hiyo ni ya tatu kutolewa kwa Rais Kikwete katika siku za karibuni. Taasisi ya East African Records karibu ilimtunukia Rais Kikwete tuzo kwa kutambua mchango wake katika kudumisha amani katika Tanzania na eneo zima la Afrika Mashariki. Rais Kikwete alipokea tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Kabla ya hapo, Rais Kikwete alitunukiwa tuzo ya uongozi bora iliyotolewa na Taasisi ya African Achievers Awards ya Afrika Kusini na kupokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na kupokelewa kwa niaba yake na Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Asha Rose Migiro ambayo hatimaye alikabidhi tuzo hiyo kwa Rais Kikwete.
Rais Kikwete amewasili mjini Washington Jumatatu, Septemba 21, 2015, ambako kesho anatarajiwa kukutana na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Marekani kujadiliana nao kuhusu masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Marekani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Septemba, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais Kikwete akutana na wawakilishi wa kudumu wa UN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete , Ijumaa, Septemba 18 amekutana na kueleza wawakilishi wa kudumu wa mataifa mbali mbali kwenye Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani kuhusu maendeleo ya kazi ya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani linalongalia jinsi gani dunia inavyoweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika siku zijazo.
Rais Kikwete akiongozana na wajumbe wote watano ambao pamoja naye wanaunda Jopo lililoundwa na Katibu Mkuu wa UN Mheshimiwa Ban Ki Moon kupendekeza jinsi gani dunia inavyoweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kufuatia majanga ya ugonjwa wa Ebola amezungumza na wawakilishi hao ikiwa ni hatua ya mwisho ya raundi ya tatu ya mazungumzo na kazi ya Jopo hilo kwenye makao makuu ya UN, New York.
Rais Kikwete amewaambia wawakilishi hao wa mataifa mbali mbali katika UN kuwa Jopo linaendelea vizuri na kazi yake na kuwa sasa limeingia katika hatua ya kuandaa mapendekezo ya ripoti ambayo itawasilishwa kwa Mheshimiwa Ban Ki Moon ambaye aliteua Jopo hilo Aprili mwaka huu.
Bila kuingia katika undani wa nini kitapendekezwa katika ripoti hiyo, Rais Kikwete amewaambia wawakilishi hao: “Hatujafikia mahali pa kuwaambia nini kitapendekezwa. Tayari tunayo maoni yetu lakini maoni siyo mapendekezo. Ninaloweza kuthibitisha ni kwamba tutawasilisha ripoti Desemba kama tulivyoangizwa na Katibu Mkuu wa UN.”
Alipoulizwa na Balozi wa Guinea kwenye UN kama tayari Jopo limekutana na wanachama wa Umoja wa Afrika kuwalezea kuhusu kazi ya jopo hilo, Rais Kikwete amesema: “Tunajiandaa kukutana na Umoja wa Afrika kwa sababu kama unavyojua Umoja huo ulifanya kazi kubwa na nzuri sana ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.”
Ugonjwa huo wa Ebola ulizusha hofu kubwa duniani baada ya kuua watu 11,000 katika muda wa miezi mitatu tu katika nchi tatu za Afrika Magharibi za Guinea, Liberia na Sierra Leone kati ya mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu. Liberia sasa imetangazwa kuwa imefanikiwa kuthibiti maambukizi ya ugonjwa huo hatari lakini wagonjwa bado wanaendelea kujitokeza katika nchi za Guinea na Sierra Leone.
Katika mkutano wa leo, wawakilishi wa kudumu wa mataifa mbali mbali kwenye UN wamezungumzia kuunga mkono shughuli na kazi za Jopo hilo ambayo lilianza mikutano yake ya raundi ya tatu tokea mwanzoni mwa wiki hii.
Nchi ambazo wawakilishi wake wa kudumu wamezungumza katika mkutano na Jopo ni Ujerumani, Uswisi, Ufaransa, Vietnam, Brazil, Sierra Leone, Indonesia, Guinea na Liberia.
Mwakilishi wa Kudumu wa Ujerumani amesema kuwa nchi yake tayari imechangia kiasi cha Euro milioni 195 kusaidia kazi za Jopo hilo na kuwa tayari imetoa kiasi cha Euro milioni 205 kusaidia nchi tatu zinazokabiliwa na majanga ya Ebola na kuwa kati ya sasa na mwaka 2019 nchi hiyo itatoa kiasi cha Euro milioni 445 kwa ajili ya kukabiliana na Ebola.
Mwakilishi huyo pia amesema kuwa nchi yake inaunga mkono kufanyika kwa mageuzi makubwa katika Shirika la Afya Duniani (WHO) na jinsi shirika hilo linavyofanya kazi yake ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko duniani.
Mkutano uliomalizika leo ulikuwa wa raundi ya tatu ya Jopo hilo ambalo lina wajumbe kutoka Tanzania (mwenyekiti), Botswana, Brazil, Indonesia, Marekani na Uswisi.
Mara ya kwanza Jopo hilo lilikutana Makao Makuu ya UN mjini New York Mei, mwaka huu, 2015, baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Ban Ki Moon. Mkutano huo ulifuatiwa na raundi ya pili ya mikutano iliyofanyika mjini Geneva, Uswisi, Julai mwaka huu.
Mwezi uliopita, baadhi ya wajumbe wa Jopo hilo walitembelea nchi tatu zinazokabiliana na majanga ya Ebola kwa nia ya kupata uzoefu wa papo kwa papo na moja kwa moja kutoka kwa watu ambao wamekuwa wanapigana kumaliza majanga ya ugonjwa huo.
Leo imekuwa mwisho wa raundi ya tatu ya mikutano ya Jopo hilo ambalo sasa limefikia hatua ya kuanza kuandika ripoti ya mapendekezo ambayo yatawasilishwa kwa Mheshimiwa Ban Ki Moon mwezi Desemba.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Septemba, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Casmir Kyuki kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Kabla ya uteuzi huu, ndugu Kyuki alikuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria.
Kufuatia uteuzi huu, Rais amemteua Bibi Sarah Barahomoka kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na ndugu Kyuki.
Kabla ya uteuzi huu, Bibi Barahomoka alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya uandishi wa Sheria.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Wateule hawa wataapishwa Tarehe 16 Septemba, 2015, Ikulu Dar-es-Salaam saa 3 asubuhi.
.................Mwisho........
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari, Msaidizi,
Ikulu-DSM
15 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Awamu ya nne inayomaliza muda wake mwezi Octoba mwaka huu, imeyashughulikia matatizo yaliyokuwepo kwa kiasi kikubwa na yale ambayo bado kukamilika, utekelezaji wake unaendelea na mengine mipango imekwisha anza.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jana mjini Kigoma katika uwanja wa Tanganyika, kwenye mkutano wa hadhara kwa madhumuni ya kuagana na wananchi wa Kigoma.
"Mlinichagua, mlinipa imani yenu, sikusahau kwa sababu nilikua naifahamu Kigoma, kilio chenu nilikuwa nakifahamu". Rais amewaambia wananchi waliofurika uwanjani hapo.
Matatizo yaliyokuwepo Mkoani Kigoma wakati Rais Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 ni pamoja na tatizo la umeme ambapo serikali ilinunua jenereta na kulifunga Mkoani Kigoma.
Jenereta hilo lilitatua matatizo ya umeme katika miji ya Kasulu, Kibondo na Kigoma Ujiji.
Awamu ya pili ya utatuaji wa matatizo ya Umeme, yanatatuliwa chini ya Mradi wa Umeme Vijijini, maarufu kama Rural Electrification Agency (REA), ambao umekua na lengo la kuunganisha vijiji vilivyobakia.
Tayari vijiji 92 vimeunganishwa na hatimaye vijiji 306 vya Mkoa mzima vitaunganishwa. Awamu hii itahusisha Ujenzi wa kituo cha kuongeza nguvu ya umeme na hatimaye umeme kufika Wilaya zingine za Uvinza, Buhigwe na Kakonko.
Tatizo lingine lilokuwepo ni Maji ambapo Rais Kikwete amesema Mradi mkubwa unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya unatarajia kukamilika mapema mwakani
Mkoa wa Kigoma pia umekua na tatizo la Mawasiliano ambapo, mwaka 2005 wakati Rais Kikwete anaingia madarakani, Mkoa ulikua na barabara moja ya lami yenye urefu wa kilomita 7.36, Hivi sasa kuna barabara za lami zenye kilomita 28.7 Kigoma mjini, Kasulu kilomita 1.5 na Kibondo kilomita 2.7.
Mbali na barabara za mjini, serikali ya awamu ya nne imeunganisha Mkoa wa Kigoma na Mikoa jirani kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami. Barabara hizo ni za Kigoma-Kidahwe km 28.2, Mwadiga-Manyovu km 60 na Kidahwe Uvinza km 76.6 na ujenzi ukiwa bado unaendelea kwa barabara za Kidahwe-Kasulu km 50, Nyakanazi- Kakonko-Kabingo km 75.
Leo tarehe 15 Septemba, Rais Kikwete anatarajia kuzindua daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi lenye urefu mita 275 na barabara zake unganishi zenye urefu wa km 48. Rais pia atazindua barabara ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa km 76.6 ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami.
.................................Mwisho...........................
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-Kigoma
15 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Victoria Richard Mwakasege kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mwakasege alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi.
Aidha, Rais Kikwete amemteua Msaidizi wa Rais wa Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete ameteua Ndugu Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) kujaza nafasi iliyoachwa na Ndugu Shelukindo. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Bundala alikuwa Mkurugenzi Msaidizi na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Afrika.
Taarifa hiyo iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015, imesema vile vile kuwa Rais Kikwete amewateua wakurugenzi wengine wanne wa Wizara hiyo ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimatiafa na kuwapandisha cheo kuwa mabalozi.
Walioteuliwa ni Ndugu Abdallah Kilima ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kilima alikuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman.
Ndugu Baraka H. Luvanda ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Luvanda alikuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu.
Ndugu Innocent E. Shiyo ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Shiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Idara hiyo hiyo.
Bibi Anisa K. Mbega ambaye ameteuliwa kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mbega alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda.
Uteuzi huo wote umeanza leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Mlingi Elisha Mkucha kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC). Uteuzi huo ulianza Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 12, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa Ndugu Mlingi Elisha Mkucha ni mwanasheria kwa taaluma na mwajiriwa wa NDC kwa miaka 14 iliyopita ambako ametumikia katika nafasi mbali mbali mpaka akawa Kaimu Mtendaji Mkuu.
Ndugu Mkucha anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Gideon Nassari aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Tulia Ackson ni Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Makamishna wawili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Uteuzi wa Makamishna hao Mhe. Mary Longway na Bi. Asina A. Omari umeanza leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015.
Mhe. Mary Longway ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Bi. Asina A. Omari ni Wakili wa Kujitegemea.
Wataapishwa, Ikulu, Dar es Salaam kesho kutwa, Jumatano, Septemba 16, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Muhammed Bakari Kambi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Jumatano, Septemba 9, 2015.
Kabla ya uteuzi wake, Profesa Muhammed Bakari Kambi alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Shirikishi cha Muhimbili, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Aidha, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa – Ndugu Mwantumu Bakari Mahiza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ndugu Saidi Magalula ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitokea Mkoa wa Tanga.
Ndugu Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma pia.
Ndugu Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Morogoro na Naibu Waziri wa Maji anachuku anafasi iliyoachwa wazi na ndugu Leonidas Gama ambaye anawania ubunge mkoani Ruvuma.
Ndugu Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Mahiza.
Uteuzi na uhamisho huo ulianza Jumamosi, Septemba 12, mwaka huu, 2015 na wakuu wapya wa mikoa wataapishwa kesho kutwa Jumatano, Septemba 16, 2015, Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Victoria Richard Mwakasege kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mwakasege alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi.
Aidha, Rais Kikwete amemteua Msaidizi wa Rais wa Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete ameteua Ndugu Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) kujaza nafasi iliyoachwa na Ndugu Shelukindo. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Bundala alikuwa Mkurugenzi Msaidizi na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Afrika.
Taarifa hiyo iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015, imesema vile vile kuwa Rais Kikwete amewateua wakurugenzi wengine wanne wa Wizara hiyo ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimatiafa na kuwapandisha cheo kuwa mabalozi.
Walioteuliwa ni Ndugu Abdallah Kilima ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kilima alikuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman.
Ndugu Baraka H. Luvanda ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Luvanda alikuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu.
Ndugu Innocent E. Shiyo ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Shiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Idara hiyo hiyo.
Bibi Anisa K. Mbega ambaye ameteuliwa kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mbega alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda.
Uteuzi huo wote umeanza leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 10, 2015 amepokea tuzo nyingine ya kimataifa, siku mbili tu baada ya kupokea tuzo ya kutambua mchango wake katika kudumisha amani na utulivu katika Tanzania.
Rais amekabidhiwa tuzo hiyo ya Uongozi na Utawala Bora na Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa AshaRose Migiro ambaye aliipokea kwa niaba ya Rais Kikwete katika sherehe iliyofanyika Julai 25, mwaka huu, 2015, Afrika Kusini.
Rais Kikwete ametunukiwa tuzo hiyo na Bodi ya Uongozi ya Africa Archiever’s Award kwa kutambua mchango wake katika maeneo ya uongozi na utawala bora wakati wa uongozi wake wa miaka 10 wa Tanzania.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, miongoni mwa viongozi waliohudhuria, ni Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju, Kaimu Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Susan Mlawi na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ndugu Tom Bahame Nyanduga.
Akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo,Waziri Migiro amesema kuwa kwa kupata tunuku hiyo sasa Rais Kikwete anajiunga na waafrika wengine mashuhuri ambao wamepata tuzo hiyo ambao ni Rais wa zamani wa Ghana, Hayati John Atta Mills, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mama Nkozana Dlamini Zuma na aliyekuwa kiongozi wa Kanisa la Anglikana na Duniani na mwanaharakati mashuhuri waAfrika, Askofu Mkuu Desmond Tutu.
Waziri Migiro amesema kuwa Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa Waafrika mashuhuri 1,202 ambao majina yao yalipendekezwa kwa ajili ya kutunukiwa tuzo hiyo kwa mwaka huu lakini Bodi iliyomtunukia Rais Kikwete tuzo hiyo imeridhishwa zaidi na mchango wake mkubwa katika kujenga na kuleta utawala bora katika miaka yake 10 ya uongozi wa Tanzania.
Amesema kuwa miongoni mwa vigezo vikuu vya tunuku hiyo ni jinsi Rais Kikwete alivyosimamia utawala wa sheria, alivyochangia kujenga demokrasia nchini, uongozi wake ulivyopambana na rushwa, ulivyoheshimu haki za binadamu, ulivyokuwa stahimilivu na ulivyoinua uhuru wa kila aina nchini.
Waziri Migiro pia amezungumzia maudhui ya mada ambayo Rais Kikwete aliitoa baada ya kutunukiwa tuzo hiyo ambayo kichwa chake cha habari kilikuwa African Unity: Prospects and Challenges (Umoja wa Afrika: Fursa na Changamoto) ambako miongoni mwa mambo mengine Rais alithibitisha uhusiano kati ya ustawi ama umasikini na utulivu katika Bara la Afrika.
Rais pia alizungumzia kuhusu hamu yake ya kustaafu baada ya kumaliza ngwe ya uongozi wake, akisisitiza kuwa hiyo ni sehemu ya utamaduni na ustawi wa demokrasia ya Tanzania na kuwa kwa sababu ya uvumilivu wa uongozi hakuna Rais yoyote wa Tanzania amepata kulazimika kukimbia nchi kwenda kuishi uhamishoni.
Naye Rais Kikwete amesema kuwa hakuweza kwenda mwenyewe kupokea tuzo hiyo kwa sababu wakati huo alikuwa katika ziara rasmi ya Kiserikali katika Australia lakini akaongeza kuwa amefurahi kutunukiwa tuzo hiyo.
Amesema kuwa tunuku hiyo ni ya Watanzania na yeye ameipokea tu kwa niaba yao na kwa niaba ya Serikali yake ambayo ndiyo imechangia kuboresha utawala bora chini ya uongozi wake.
“Mimi naipokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania. Wao ndio washindi wa kwelikweli wakiongozwa na Serikali yao ambayo imefanikisha kudumisha utawala bora katika miaka 10 iliyopita.Wenzetu wametupima kwa kutulinganisha na wengine na tukaonekana bora. Nawashukuru sana kwa imani yao kwetu.”
Tuzo hiyo ya Uongozi na Utawala Bora imekuja siku mbili baada ya Rais kupokea Nishani ya Amani na Utulivu iliyotolewa kwake na Taasisi ya East Africa Book Records yenye makao makuu yake Uganda na kukabidhiwa kwa Rais Kikwete na mtendaji wake mkuu, Dkt. Paul Bamutize.
Akitunuku nishani hiyo juzi, Jumanne, Septemba 8, 2015 katika hafla nyingine iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Dkt. Bamutize alisema kuwa amani na utulivu ambao Rais Kikwete na Serikali wamejenga katika Tanzania imeleta matumaini kwa wawekezaji na majirani wa Tanzania na kuwa mfano dhahiri wa kuigwa.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na mabalozi wa Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
10 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzania itafanya uchaguzi Mkuu ujao kwa Amani na Utulivu ambapo watanzania watapata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka ifikapo Oktoba mwaka huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza mabalozi wanne wapya waliofika Ikulu kuwasilisha Hati zao za utambulisho Ikulu leo.
“Kampeni zinakwenda vizuri na tunategemea uchaguzi mkuu utakua wa amani na Watanzania watapata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka” Rais Kikwete amewaeleza mabalozi hao katika nyakati tofauti mara baada ya kupokea hati zao na kufanya nao mazungumzo.
Rais Kikwete ametumia nafasi hiyo kuwaeleza mabalozi kuhusu hali ya kisiasa , kiuchumi na kijamii.
Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu ambapo wananchi watachagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Rais Kikwete pia amewaeleza mabalozi hao furaha yake na hamasa aliyonayo ya kumaliza uongozi wa Tanzania kwa Amani na kukabidhi .
Mabalozi waliowasilisha hati zao leo ni Balozi Florence Tinguely Mattli wa Uswizi, Balozi Yesmin Eralp wa Uturuki, Balozi Pekka Juhani Hukka wa Finland na Balozi Katarina Rangnitt wa Sweden.
Rais Kikwete pia amewahakikishia mabalozi hao kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mwema baina yake na nchi hizi ambazo ni rafiki na washirika wake wa maendeleo kwa miaka mingi.
……………………………Mwisho……………………………
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-Dsm
9 Septemba, 2015
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Amani na utulivu ulioko nchini , umechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wote wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo Ikulu wakati akipokea nishani ya Amani kutoka kwa Dr. Paul Bamutize, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya East Africa Book Records yenye makao yake makuu nchini Uganda.
Rais amepokea nishani mbili leo ambazo ni kwa ajili ya nchi na ingine kwa ajili yake kama Kiongozi wa Tanzania.
Dr. Bamutize amesema Tanzania imekua mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki ambapo pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi kama chama ambacho kimesimamia Amani hiyo hapa nchini.
“Amani hii tuliyonayo hapa nchini imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania ambao napenda kupokea nishani hii kwa niaba yao kwa sababu wao ndiyo watunzaji na walinzi wakubwa wa Amani hii” Rais Kikwete amesema.
Dr. Bamutize amempongeza Rais Kikwete na kuelezea kuwa amani hiyo imeleta matumaini kwa wawekezaji na majirani wa Tanzania na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na majirani zake wote katika ukanda huu na Afrika kwa ujumla.
Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na mabalozi wa Burundi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Congo na Uganda.
Wakati huo huo Rais Kikwete amepokea Ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi.
Ujumbe huo umeletwa Ikulu na Mheshimiwa Rajiv Pratap Rudy Waziri wa Nchi anaeshughulikia Maendeleo ya Ujasiriamali ambaye pia amefanya mazungumzo na Rais Kikwete kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na ushirikiano katika biashara na ujasiriamali.
……………………………Mwisho……………………………
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-Dsm
8 Septemba, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Thadeo Marko Mwenempazi kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Sheria.
Uteuzi wa Ndugu Mwenempazi umeanza tokea Jumatatu ya Agosti 24, mwaka huu, 2015.
Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 4, 2015 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mwenempazi alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkoa wa Dar es Salaam.
Ndugu Mwenempazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Sirilius Matupa ambaye karibuni aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
04 Septemba, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika.
Mkutano huo utakaofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete utafanyika tarehe 4 – 5 Septemba, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kauli Mbiu ni “Tumia Takwimu Huria Kuendeleza Afrika” (Developing Africa Through Open Data).
Washiriki takriban 400 kutoka Serikalini, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu na Washirika wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya Nchi wanatarajiwa kushiriki. Miongoni mwa washiriki kutoka Serikalini ni pamoja na Wakurugenzi kutoka Idara za Sera na Mipango, Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA na Maofisa Takwimu Waandamizi wa Wizara zote.
Mkutano wa Takwimu Huria kwa Kanda ya Afrika ni wa kwanza wa aina yake Barani Afrika Tanzania ikiwa nchi ya kwanza kuwa mwenyeji. Heshima hiyo imetokana na Tanzania kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership – OGP) unaolenga kuifanya Serikali kuwa wazi zaidi na hivyo kuleta uadilifu na uwajibikaji katika kuwahudumia Wananchi. Katika utekelezaji wa Mpango wa OGP, Tanzania iliweka kipaumbele katika kuanzisha Tovuti ya Takwimu Huria itakayoweka wazi takwimu mbalimbali za Serikali na Taasisi zake.
Madhumuni ya Mkutano ni kujadiliana kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na jinsi utakavyoleta maendeleo hususan kwa nchi za Afrika.
Mkutano utawawezesha wadau kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na kuona jinsi gani Sera za nchi zenye mfumo huo zinavyofanya kazi na kusimamia viwango vya upatikanaji wa Takwimu Huria.
Aidha, Mkutano huo utaihusisha sekta binafsi na wadau wengine katika matumizi ya Takwimu Huria katika kuleta maendeleo ya kasi zaidi Barani Afrika.
Washiriki watajadili jinsi ya kukuza na kuimarisha matumizi ya Mfumo wa Takwimu Huria katika kutoa huduma kwa wananchi hasa katika sekta ya Huduma za Jamii za elimu, afya, maji na kilimo.
Tunaomba ushirikiano wenu ili Mkutano huu ufanyike na kukamilika kwa ufanisi.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu –Dar es Salaam.
03 Septemba, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu ameyaelekeza majeshi ya ulinzi na usalama nchini kulinda mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu na kulinda mchakato mzima wa uchaguzi huo,ili kushamirisha zaidi demokrasia ya Tanzania.
Akizungumza na maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Usalama wa Taifa na Idara ya Uhamiaji usiku wa jana, Jumanne, Septemba Mosi, 2015, Rais Kikwete amesema kuwa majeshi ya ulinzi na usalama ya Tanzania yana wajibu wa pekee wa kulinda ustawi wa demokrasia ya Tanzania katika kipindi cha sasa cha kampeni na uchaguzi mkuu.
Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu alikuwa anazunguza na maofisa hao katika halfa ya kumwaga kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu iliyoandaliwa na majeshi hayo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Dar es Salaam.
“Sasa tuko katika kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu na ni kipindi chenye changamoto nyingi iwe ni wakati wa kampeni zenyewe, wakati wa upigaji kura na baada ya kupiga kura. Lindeni mikutano ya kampeni ya vyama vyote ili mikutano hiyo ifanyike kwa salama na amani,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza: “Lindeni usalama wa kati na siku ya kupigakura, linden usalama baada ya kumalizika uchaguzi mkuu kwa nia ya kuhakikisha kuwa demokrasia yetu change inazidi kukua na kushamiri na nchi yetu inabakia tulivu na yenye amani.”
Halfa hiyo ya kumwaga Rais Kikwete ilikuwa tukio la mwisho katika siku ambako majeshi ya Tanzania yalimwaga Amiri Jeshi Mkuu wao kwa shughuli mbalimbali.
Mapema asubuhi, majeshi yalimwandalia Rais Kikwete gwaride rasmi la kumwaga katikaUwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Baadaye, Rais Kikwete alitunuku nishani za Utumishi Uliotukuka Tanzania, Utumishi Mrefu Tanzania na Utumishi MrefunaTabiaNjema katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Nishani hizo walitunukiwa maofisa walio bado kwenye utumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
2 Septemba,2015
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kwa kadri uchumi wa Tanzania unavyozidi kukua ni lazima majeshi ya ulinzi nayo yaboreshwe kwa sababu uchumi imara ni lazima ulindwe na jeshi imara.
Rais Kikwete pia amelisifia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuiletea Tanzania sifa na heshima kubwa katika kipindi cha uongozi wake na kulisifia Jeshi la Polisi kwa mchango wake mkubwa katika vikosi vya kulinda amani duniani.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa anaondoka madarakani kama Amiri Jeshi Mkuu akiwa mwenye furaha kwa sababu ya mchango wake katika ujenzi mkubwa wa majeshi ya ulinzi na usalama ya Tanzania katika kipindi cha miaka 10 iliyopita na kutangaza kuwa sasa JWTZ liko tayari na imara sasa kulinda nchi.
Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo, Jumatano, Septemba2, 2015 wakati alipozungumza na mamia ya maofisa wa JWTZ, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Usalama waTaifa na Idara ya Uhamiaji kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Dar es Salaam katika hafla ya kupendeza sana ya kumwaga kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu.
Katika hotuba yake ya kusisimua, Rais Kikwete amesema: “Tumewekeza sana katikakuboresha majeshi yetu katika miaka 10 iliyopita kwa ajili ya kulinda amani, utulivu, mipaka ya nchi yetu pamoja na chumi wetu. Uchumi wa nchi yoyote lazima ulindwe na uchumi imara kama wa kwetu lazima ulindwe na jeshi imara. Uchumi imara hauwezi kulindwa na jeshi dhaifu.”
Ameongeza: “Tumegundua gesi asilia nyingi sana sasa. Ni lazima tuilinde vinginevyo tutakuwa watu wa ajabu. Watu wanaiba samaki wetu katika bahari kuu na jambo hilo lazima lipatiwe ufumbuzi na ndiyo maana karibuni tulizindua meli mbili mpya kubwa za MV Butiamana MV Msogakwa ajili ya Kamandi yetu ya Maji.”
Rais Kikwete amemkariri Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Winston Churchill ambaye yeye alikuwa askari na alipata kusema,”uimara wa uchumi lazima ulindwe na uimara wa jeshi la nchi. Uchumi wa nchi lazima ulindwe kwa upanga.”
Rais amesema kuwa Tanzania lazima iendelee kuwekeza ipasavyo katika ujenzi na uimara wa majeshi yake kila wakati. “Hata katika mambo ya kiraia, msipowekeza katika usalama wa raia, wezi watawasumbua kila siku kwa kuvamia mabenki yetu na kuiba pesa za wananchi.”
Ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia, Rais amesema kuwa Serikali inakamilisha mpango wa kufunga kamera za ulinzi (CCTV) katika miji mikubwa ya Tanzania kwa kuanzia na Dar es salaam. “tutakomesha huu wizi wa jeuri wa watu kupora pesa za watu ama mali za watu kwa kutumia pikipiki kwa sababu kamera hizo zitakuwa zinaona sehemu zote za mji.”
Rais pia amesema utawala wake umefanya mambo mengi kuimarisha majeshi ya ulinzi na usalama “na yale ambayo hatukuweza kuyamalizia tumeyaacha katika hatua nzuri. Tumepanda mbegu kwa mambo mazuri zaidi kwa miaka ijayo.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Mwaka 2005, hatukuwa na ndege moja ya kijeshi iliyokuwa inaruka. Sasa tuna Jeshi la Anga lililo kamili bado dhana mojatu – na jeshi hilo litakuwa limekamilika kabisa na hata ile tayari tumeiagiza. Tumejenga kikosi cha mizinga, tumejenga kikosi cha vifaru, tuna uwezo wa kuaminika wa uhandisi, tunao uwezo mkubwa wa usafiri kwa sababu jeshi haliwezi kukabiliana na adui kwa kutembea kwa miguu tu. Kuna wakati jeshi letu lilikuwa na magari mengi zaidi kuliko madereva wa kuyaendesha. Tumekamilisha ujenzi wa nyumba 6,000 kati ya 10,000 ambazo tunawajengea wanajeshi. Mpango wa kupata magari kwa ajili yaJeshi la Polisi umekamilika. Ujenziwa nyumba 10,000 zaPolisi pia mpango wake umekamilika tayari kwa ujenzi.”
“Nimewaagiza wakuu wa Jeshi la Magereza kuniandalia Mpango wa Maendeleo ya Jeshi hilo kama ule wa JWTZ na Polisi na nataka kuuidhinisha kabla ya kuondoka madarakani. Wao wanajua nimekwishawaambia.”
Rais Kikwete pia amesema kuwa vyombo vya ulinzi vya Tanzania vimeipatia heshima kubwa nchi katika shughuli za ulinzi wa amani duniani. “Tuko Darfur, tuko Lebanon, tulikuwa Liberia, tuko Congo, tulikuwa Sierra Leone na tulipata kuwa katika mpaka wa Ethiopia na Eritriea na kila mahali askari wetu wa Jeshi na Polisi wamerejea na sifa nyingi. Kila mtu anawataka na kuwaomba sasa.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Ninaondoka mwenye furaha kuwa weledi wa jeshi letu sasa ni wa kiwango cha juu sana.Tumefanikiwa kuunda Kikosi Maalum (task Force) cha wakuu wa majeshi yetu ya JWTZ na Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa ambacho kimesaidiasana kwa ushauri na katika kuimarisha ulinzi na utulivu wa nchiyetu. Tuliongozavizuri kazi ya kuiunganisha tena Comoro baada ya kumwondoa muasi Kanali Bakari pale katika Kisiwa cha Anjuan.Sifa ni nyingi kila mahali. Nawashukuru sana kwa kunifanyia kazi nzuri kama Amiri Jeshi Mkuu wenu. Mmenifanyia kazi nzuri na yenye mafanikio makubwa. Asanteni.”
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi y Mawasiliano ya Rais,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Jumatatu, Agosti 31, 2015, ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (The National Defence Headquarters) eneo la Makongo Juu, Kambi ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.
Ujenzi huo wa Makao Makuu ya Ulinzi ambao dhana yake ni ya siku nyingi utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 55 na utachukua miaka miwili kukamilika. Gharama hizo ni pamoja na zile za upembuzi yakinifu na usanifu wa michoro, shughuli mbili ambazo zilifanywa na Kampuni ya Norinco ya China pamoja na gharama za ujenzi.
Kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo, Rais Kikwete ameambiwa kuwa Makao Makuu ya Ulinzi ya Taifa yatakuwa na Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Makao Makuu ya Ngome (Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania - JWTZ) na Makao Makuu ya Kamandi za Nchi Kavu, Maji na Anga za JWTZ.
Hiyo itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa taasisi hizo kuu za ulinzi wa Tanzania kuwa katika jengo moja na sherehe ya leo inaweka historia ya kutekelezwa kwa dhana ya miaka mingi ya kuwa na makao makuu ya ulinzi wa taifa. Baada ya kukamilika kwa ujenzi, makao makuu ya Wizara na yale ya Ngome yatahama kutoka eneo la sasa la Upanga, Dar es Salaam.
Akizungumza katika sherehe hizo, mwakilishi wa Kampuni ya Norinco amesema kuwa kampuni yake imeona fahari kubwa kushiriki katika mradi huo ambao utazalisha jengo la aina ya pekee katika ukanda huu na kuwa jengo hilo litakuwa ushahidi mwingine wa uhusiano wa karibu na wa miaka mingi kati ya Tanzania na China.
Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amewaambia waalikwa katika sherehe hiyo kuwa ujenzi wa makao makuu mapya umetokana na misingi miwili mikuu ambayo ni urekebishwaji wa muundo wa JWTZ ambao umekuwa unafanyika tokea miaka ya 1980 na hali ya mazingira ya sasa ya eneo la Upanga ambako yako makao makuu ya Ngome ambayo yamebadilika sana.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa, Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa ujenzi wa makao makuu hayo ni mradi mwingine mkubwa ulianzishwa na kutekelezwa katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Kikwete.
Ameitaja miradi mingine mikubwa kuwa ni kujengwa na kuanzishwa kwa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (The National Defence College), kujengwa na kuanzishwa kwa Chuo cha Ukamanda kilichoko Duluti, Mkoa wa Arusha na ujenzi mkubwa wa nyumba 10,000 za kuishi wanajeshi katika mikoa mbali mbali.
“Hii ni mbali na mambo mengine mengi yaliyofanyika wakati wa uongozi wako ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa dhana za kisasa za kufanyia kazi,” amesema Waziri Mwinyi.
Rais Kikwete amesema kuwa amefurahi kuona ndoto ya miaka mingi ya kuwepo kwa makao makuu ya ulinzi wa taifa sasa imetimia baada ya makao makuu ya jeshi kuhamahama kutoka makao makuu ya sasa ya DAWASCO, kabla ya kuhamia Army House na baadaye katika makao makuu ya sasa ya Upanga, ambayo awali ilikuwa shule ya msingi ya madhehebu ya Aga Khan. “Namaliza wajibu wangu wa Amiri Jeshi Mkuu nikiwa mtu mwenye furaha sana kwa sababu ya jambo hili.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Agosti,2015