Taarifa kwa vyombo vya Habari ya zamani
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, uteulzi huu umaanza tarehe 06 Mei, 2014. Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14 Desemba,2013.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.
Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato kama ifuatavyo:-
- Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
- Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
- Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.
- Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).
- Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
- Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank Plc Emerging Markets.
- Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance Company.
Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).
Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.
“Mwisho”
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
08 Mei, 2014
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Jumatano, Mei 7, 2014 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Li Keqiang.
Katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Transcorp Hilton ya mjini Abuja nchini Nigeria ambako wote wawili wamefikia wakati wanashiriki katika Kongamano la Uchumi Duniani Afrika (World Economic Forum -Africa), viongozi hao wawili wamezungumzia, kimsingi, mambo yanayohusu uhusiano wa Tanzania na China.
Katika mkutano huo, Rais Kikwete amemwomba Mheshimiwa Li Keqiang kuisaidia Tanzania kuboresha mfumo wake wa kutunza na kuhifadhi nafaka kutokana na ongezeko kubwa za uzalishaji wa nafaka, ambao unatokana na kukua kwa kilimo cha Tanzania.
Waziri Mkuu Li Keqiang amekubali ombi hilo la Tanzania kwa kumweleza Rais Kikwete Waziri wa Serikali ya China ambaye atasimamia kutekelezwa kwa mradi huo mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la nafaka katika kilimo cha Tanzania.
Rais Kikwete pia amemwomba Waziri Mkuu huyo wa China kusaidia kuhakikisha kuwa kazi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo inaanza mapema iwezekanavyo, ombi ambalo Waziri Mkuu Li Keqiang amelikubali.
Rais Kikwete pia ameipongeza China kwa dhana yake iliyotangazwa karibuni ya 4-6-1 ambako kuna misingi minne, maeneo sita ya kipaumbele na eneo moja la mwelekeo kama msingi mkuu wa Siasa za Nje za Jamhuri ya Watu wa China.
Rais Kikwete pia ameisifu China kwa kusaidia maendeleo ya Afrika kwa kutoa misaada ya maendeleo, kuwekeza na kufanya biashara na Bara la Afrika na pia kuiwezesha Afrika kupata teknolojia ya kisasa kutoka China.
Aidha, Rais Kikwete ameishukuru China kuwekeza katika uchumi wa Tanzania, akisema kuwa China ni moja ya wawekezaji wakuu katika uchumi wa Tanzania kwa kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.5.
“Tunashukuru sana kwa uwekezaji wa kila aina, wa mwisho mkubwa ikiwa ni kutupatia mkopo wa kiasi cha dola milioni 1.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar Es Salaam,” amesema Rais Kikwete na kuongeza kumshukuru Waziri Mkuu kwa misaada ya kijeshi ambayo Tanzania inaipata kwa China. “Nchi yetu inalindika vizuri zaidi kwa sababu ya misaada yenu.”
Naye Waziri Mkuu Li Keqiang ameipongeza Tanzania kwa kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na pia ameonyesha furaha yake kuona maendeleo ya kiuchumi ambayo Tanzania inaendelea kuyapata.
Amesema kuwa urafiki wa China na Tanzania siku zote umekuwa msingi mkuu wa mahusiano ya China na Afrika na hali hiyo itaendelea kuwa ukweli wa mahusiano baina ya China, Afrika na Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Mei, 2014
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu ya Kimataifa – UN Special Envoy for Global Education - na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Mheshimiwa Gordon Brown amesema kuwa Tanzania imefanya vizuri zaidi kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika katika uandikishaji wa watoto kuanza shule.
Aidha, Mheshimiwa Brown amesema kuwa hana uhakika kama Watanzania wanajua fika kuwa nchi yao imefikia mafanikio makubwa mno ya elimu ambayo bado ni ndoto tu kwa nyingine nyingi za Afrika.
Kwa sababu hiyo na kwa sababu ya mafaniko hayo, Mheshimiwa Brown amesema kuwa Umoja wa Mataifa na taasisi zake na nyingine za kimataifa ziko tayari kuisaidia Tanzania kufikia lengo la kusajili watoto wote kwa asilimia 100 ya watoto wote wanaotakiwa kuingia shule katika muda wa uongozi wa Rais Kikwete na kabla hajaondoka madarakani mwishoni mwa mwaka ujao.
“Mheshimiwa Rais, tunapenda kukupongeza kwa kufanya vizuri sana katika nyanja ya elimu. Haya ni mafanikio ya uongozi wako. Umewezesha asilimia 98 ya watoto wanaotakiwa kuanza shule kuingia shule. Hakuna nchi nyingine ya Afrika ambayo imefikia mafanikio kiasi hiki. Tunapenda kukusaidia na kufanya kazi na wewe ili tufikie asilimia 100, “ amesema Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Uingereza katika mkutano na Rais Kikwete.
Rais Kikwete na Mheshimiwa Brown wamekutana kwenye Hoteli ya Hilton mjini Abuja ambako wote wawili wanakaa wakati wanahudhuria Kongamano la Uchumi Duniani – kwa Bara la Afrika lilioanza leo, Jumatano, Mei 7, 2014 katika mji mkuu wa Nigeria.
Ameongeza Mheshimiwa Brown, “Mheshimiwa Rais, sasa tunataka kusaidia kuwapeleka shule kiasi cha watoto 100,000 ambao ni asilimia mbili ambao kwa sasa hawaendi shule. Tunajua hawa ni watoto wa makabila ya wafugaji ambao wanahamahama kila siku na mifugo yao na watoto wao vile vile. Lakini Serikali yako imepiga hatua kubwa, kubwa kuliko inavyofikiriwa na mataifa mengine ya Afrika katika kukabiliana na hali hiyo.”
Mheshimiwa Gordon Brown pia amesema kuwa Umoja wa Mataifa na taasisi zake ziko tayari kuisaidia Tanzania katika kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi ambayo hayana walimu wa kutosha katika Tanzania na duniani pote kwa kutumia njia za ufundishaji za kutumia teknolojia ya habari, mawasiliano na teknolojia.
Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Bwana Mark Suzman, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani. Aidha, Rais amekutana na kufanya mazunguzo na Bwana Sunnil Bharti Mittal, Mwenyekiti wa Kampuni ya kimataifa ya simu ya Airtel duniani.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
07 Mei,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili kwenye mji mkuu wa Nigeria wa Abuja usiku wa jana, Jumanne, Mei 6, 2014 kuhudhuria Kongamano Uchumi Duniani (WEF) kwa Bara la Afrika – World Economic Forum Africa - linaloanza leo.
Rais Kikwete amewasili kujiunga na marais 13 na wajumbe zaidi ya 1,000 ambao watahudhuria Kongamano hilo la siku tatu ikiwa ni mara ya tatu kwa Kongamano hilo kufanyika nje ya mji wa Cape Town wa Afrika Kusini. Nchi ya kwanza nje ya Afrika Kusini kuandaa Kongamano hili ilikuwa Tanzania, ikifuatiwa na Ethiopia na sasa Nigeria.
Rais Kikwete ambaye amehudhuria karibu kila Kongamano la WEF tokea kuingia madarakani mwaka 2005, amepangiwa kushiriki katika mikutano mitano mikuu hata kama awali wenyewe walikuwa wamemwomba kushiriki katika mikutano 12 ya Kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni “Kujenga ukuaji unaomshirikisha kila mtu pamoja na kutengeneza nafasi za ajira.”
Baadaye mchana wa leo (Jumatano), Rais Kikwete atashiriki na kuzungumza katika mkutano wa Baraza la Uongozi (Leadeship Council Meeting) ambao umeandaliwa chini ya Visheni Mpya Kilimo ya WEF na unafanyika kwa WEF kushirikiana na Umoja wa Afrika na NEPAD na ambao utahudhuriwa na Wakuu wa nchi na Serikali, Mawaziri wa Maendeleo wa Kundi la Nchi Tajiri zenye viwanda za G8 na viongozi wa AU na NEPAD.
Rais Kikwete pia atashiriki katika mkutano wa Uwekezaji katika Kilimo wa Grow Africa Investment Forum na baadaye jioni atahudhuria hafla ambako Rais wa Nigeria, Mheshimiwa Goodluck Jonathan atawakaribisha wakuu wa nchi na Serikali wanaoshiriki katika Kongamano la WEF-A.
Kesho (Alhamisi), Rais Kikwete atashiriki katika mkutano utakaozungumzia jinsi ya kuboresha miundombinu katika Afrika ambao ni muhimu kwa Tanzania kwa sababu Njia ya Kati ya Tanzania (Central Corridor) imeteuliwa kuendelezwa miongoni mwa njia 51 za Afrika ambazo zilijadiliwa katika Kongamano la WEF la mwanzoni mwa mwaka huu mjini Davos, Uswisi. Rais pia atashiriki katika mikutano mingine miwili.
Mbali na mikutano hiyo, Rais Kikwete amepangiwa kukutana na viongozi maarufu duniani akiwamo Waziri Mkuu wa China Mheshimiwa Li Keqiang, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Mheshimiwa Gordon Brown, Mtawala Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID) Dr. Rajiv Shah, Waziri wa Biashara wa Marekani Balozi Michael Froman na Rais wa Sera za Kimataifa, Uhamasishaji na Mipango ya Maendeleo ya nchi mbali mbali ya Taasisi ya Gates Foundation Bwana Mark Suzman.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Mei, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
UTEUZI WA MTENDAJI MKUU WA MAMLAKA YA UDHIBITI NA
UNUNUZI WA UMMA (PPRA)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Laurent M. Shirima kuwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA).
Dkt. Shirima ni Mkurugenzi wa kujenga Uwezo wa Huduma za Ushauri (Capacity Building and Advisory Service-PPRA) na pia ndiye anaye kaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa PPRA.
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2014.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-Dodoma
Tanzania.
6 Mei, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais atoa changamoto sekta binafsi kujihusisha zaidi na mapambano dhidi ya Ukimwi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka sekta binafsi kujihusisha zaidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa sababu ugonjwa huo unaathiri uchumi na biashara na kuongeza mzigo wa gharama za uzalishaji wa makampuni hayo.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kwamba Tanzania imekuwa inapata michango mikubwa kupambana na UKIMWI kutoka kwa washirika wake wa maendeleo, bado jukumu la msingi la kupambana na ugonjwa huo nchini ni la Watanzania wenyewe.
Pia, Rais Kikwete amewakumbusha Watanzania kuwa UKIMWI hauna tiba ya kisayansi ama tiba mbadala ya waganga wa jadi ama wapiga ramli kama baadhi ya Watanzania wanavyopenda kujiaminisha.
Rais Kikwete alikuwa anazungumza hayo usiku wa kuamkia, Jumamosi, Mei 3, 2014, wakati alipokuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa uchagishaji fedha za kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya mapambano ya UKIMWI kwa mwaka huu wa 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency mjini Dar es Salaam.
Rais Kikwete amewaambia washiriki wa hafla hiyo: “Tumefanikiwa sana kuhamasisha Serikali na wananchi kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI. Hata hivyo, hamasa hii haijaingia sawa sawa miongoni mwa ndugu zetu wa sekta binafsi, ambao ndio waajiri wakubwa kuliko hata Serikali. Upo ushahdi wa kutosha kuwa wao wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na UKIMWI kwa sababu ugonjwa huo huathiri uchumi na biashara kwa kuongeza mzigo wa gharama za uzalishaji wa makampuni.”
Ameongeza Rais Kikwete: “ Uzoefu kwingineko Barani Afrika na haswa Afrika Kusini, unaonyesha kuwa uwekezaji wa sekta binafsi katika mapambano dhidi ya UKIMWI ni muhimi sana kwao na kwa uchumi wa nchi. Ni gharama ndogo zaidi kwao kupambana na UKIMWI kuliko gharama za kuupuzia, ambazo huishia kuwa kubwa zaidi kwa mwajiri.”
Rais amesema kuwa wajibu wa msingi wa kupambana na UKIMWI nchini ni wa Watanzania na hivyo Watanzania hawana budi kuendeleza mapambano hayo hata pasipo na ufadhili.
“Wajibu wa msingi wa kusimamia mapambano dhidi ya UKIMWI na kuwahudumia wale walioathirika ni jukumu letu sisi Watanzania wenyewe. Hivyo, hatuna budi kuendeleza mapambano hata pale pasipo na ufadhili. Njia pekee ni kuongeza jitihada za ndani kwa kuunganisha nguvu zetu kwenye utafutaji wa raslimali fedha.”
Uchangishaji huo chini ya Kili Challenge 2014 huendeshwa kwa pamoja na Kampuni ya Anglo Gold Ashanti kupitia kampuni tanzu yake ya uchimbaji dhahabu ya Geita Gold Mine (GGM) ya Mkoa wa Geita na mwaka huu ni mara ya 12 tokea kuanzishwa uchangishaji wa fedha za kuunga mkono mapambano ya UKIMWI.
Kiasi cha shilingi bilioni 12 zimechangwa katika miaka hiyo 12 na kiasi cha makampuni 30 yasiyokuwa ya kiserikali na yanayojihushisha na mapambano dhidi ya UKIMWI yamenufaika. Aidha, katika miaka hiyo 12 kiasi cha watu 500 wameshiriki kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhamasisha mapambani dhidi ya UKIMWI.
Mwaka huu, kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zinatarajiwa kukusanywa na hadi jana kiasi cha wachangiaji 50 walikwishajiandikisha.
Katika shughuli ya usiku huo, Rais Kikwete alitoa hundi za kiasi cha shilingi milioni 700 kwa taasisi mbali mbali kutokana na fedha zilizokusanywa mwaka jana chini ya mpango huo wa Kili Challenge.
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
03 Mei,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais aunda Tume kuchunguza mwenendo wa Operesheni Tokomeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry) Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jioni ya leo, Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa uteuzi huu ulianza jana, Alhamisi, Mei Mosi 2014.
Taarifa ya Balozi Sefue iliyataja majukumu ya Tume hiyo yatakuwa yafuatayo:
- Kuchunguza na kubaini Operesheni Tokomeza ilivyoendeshwa.
- Kuchunguza na kubaini iwapo Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea zilifuatwa na watu waliotekeleza Operesheni Tokomeza.
- Kuchunguza na kubaini iwapo yupo mtu yeyote aliyekiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea wakati wa Operesheni Tokomeza.
- Kuchunguza na kubaini kama wapo watu wowote waliokiuka Sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na kupima kama hatua zilizochukuliwa dhidi yao au mali zao zilikuwa stahiki.
- Kupendekeza hatua zozote zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea za Operesheni Tokomeza.
- Kupendekeza mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza operesheni nyingine siku zijazo ili kuepuka kasoro.
Uteuzi huo wa Tume hiyo unatekeleza ahadi ya Rais Kikwete ambayo aliitoa wakati anahutubia Bunge Novemba 18, mwaka jana, 2013 mjini Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
2 Mei, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais aunda Tume kuchunguza mwenendo wa Operesheni Tokomeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry) Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jioni ya leo, Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa uteuzi huu ulianza jana, Alhamisi, Mei Mosi 2014.
Taarifa ya Balozi Sefue iliyataja majukumu ya Tume hiyo yatakuwa yafuatayo:
- Kuchunguza na kubaini Operesheni Tokomeza ilivyoendeshwa.
- Kuchunguza na kubaini iwapo Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea zilifuatwa na watu waliotekeleza Operesheni Tokomeza.
- Kuchunguza na kubaini iwapo yupo mtu yeyote aliyekiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea wakati wa Operesheni Tokomeza.
- Kuchunguza na kubaini kama wapo watu wowote waliokiuka Sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na kupima kama hatua zilizochukuliwa dhidi yao au mali zao zilikuwa stahiki.
- Kupendekeza hatua zozote zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea za Operesheni Tokomeza.
- Kupendekeza mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza operesheni nyingine siku zijazo ili kuepuka kasoro.
Uteuzi huo wa Tume hiyo unatekeleza ahadi ya Rais Kikwete ambayo aliitoa wakati anahutubia Bunge Novemba 18, mwaka jana, 2013 mjini Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
2 Mei, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais aunda Tume kuchunguza mwenendo wa Operesheni Tokomeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameunda Tume ya Uchunguzi (Commission Inquiry) Kuhusu Vitendo vilivyotokana na Uendeshaji wa Operesheni Tokomeza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam jioni ya leo, Ijumaa, Mei 2, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Rais ameunda Tume hiyo kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32.
Kutokana na hatua yake ya kuunda Tume hiyo, Rais Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji na Balozi Mstaafu Hamisi Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Stephen Ernest Mtashiwa Ihema na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Vincent Kitubio Damian Lyimo kuwa Makamishna. Rais pia amemteua Ndugu Frederick Manyanda, Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Katibu wa Tume hiyo.
Taarifa ya Balozi Sefue inasema kuwa uteuzi huu ulianza jana, Alhamisi, Mei Mosi 2014.
Taarifa ya Balozi Sefue iliyataja majukumu ya Tume hiyo yatakuwa yafuatayo:
- Kuchunguza na kubaini Operesheni Tokomeza ilivyoendeshwa.
- Kuchunguza na kubaini iwapo Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea zilifuatwa na watu waliotekeleza Operesheni Tokomeza.
- Kuchunguza na kubaini iwapo yupo mtu yeyote aliyekiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea wakati wa Operesheni Tokomeza.
- Kuchunguza na kubaini kama wapo watu wowote waliokiuka Sheria yoyote wakati wa utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na kupima kama hatua zilizochukuliwa dhidi yao au mali zao zilikuwa stahiki.
- Kupendekeza hatua zozote zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukiuka Sheria, Taratibu na Hadidu za Rejea za Operesheni Tokomeza.
- Kupendekeza mambo ya kuzingatiwa wakati wa kuandaa na kutekeleza operesheni nyingine siku zijazo ili kuepuka kasoro.
Uteuzi huo wa Tume hiyo unatekeleza ahadi ya Rais Kikwete ambayo aliitoa wakati anahutubia Bunge Novemba 18, mwaka jana, 2013 mjini Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
2 Mei, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone kufuatia vifo vya watu 19 wakiwemo Askari Polisi wanne (4) na Viongozi watatu wa Kijiji kufuatia ajali ya barabarani iliyosababishwa na basi lililokuwa likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam katika Barabara kuu ya Singida - Dodoma.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa tarehe 27 Aprili, 2014 katika Kijiji cha Utaho, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida baada ya basi la Kampuni ya Sumry lenye Nambari ya Usajili T. 799 BTE aina ya Nissan kuwagonga watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo ambapo ajali nyingine ilikuwa imetokea wakiwa pamoja na Askari Polisi kutoa msaada katika ajali nyingine iliyokuwa imetokea katika eneo hilo ambapo mwendesha baiskeli aligongwa na lori na kufariki papo hapo.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 19 wakiwemo Askari Polisi wanne na Viongozi watatu wa Kijiji cha Utaho katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida. Vifo hivi vimetupotezea kama Taifa nguvu kazi muhimu kwa ujenzi wa nchi yetu na hakika vimeacha simanzi na huzuni kubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Perseko Kone kumfikishia Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa watu wote waliopotelewa na ndugu na jamaa zao kutokana na ajali hiyo, na amewahakikishia wafiwa kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huo mkubwa.
“Ninamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awawezeshe kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida watu wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo ili waweze kupona haraka na kuungana tena na ndugu na jamaa zao”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
30 Aprili,2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA
WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA
UTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap
83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo
na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa
Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na
(2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali
anapotoka mjumbe husika.
2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama
ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali
10 yanayohusika. 2
3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
4. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika
Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba,
2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili
kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya
majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha,
Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali
yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la
Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe
02/01/2014.
5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu
Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 3
upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo
yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
6. Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178
kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo
yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa
upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo
basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina
3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza
wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.
7. Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi
mbalimbali ni kama ifuatavyo: 4
Na. Kundi/Taasisi Taasisi zilizoleta
mapendekezo
Idadi ya Watu
Waliopendekezwa
Idadi ya
Wajumbe
Wanaotakiwa
Idadi ya
Walioteuliwa
Tanzania
Bara
Zanzibar Tanzania
Bara
Zanzibar Tanzania
Bara
Zanzibar
1. Taasisi zisizokuwa
za Kiserikali
246 98 1,203 444 20 13 7
2. Taasisi za Kidini 55 17 344 85 20 13 7
3. Vyama vya Siasa
vyenye Usajili wa
Kudumu
21 14 129 69 42 28 14
4. Taasisi za Elimu 9 9 84 46 20 13 7
5. Makundi ya
Walemavu
24 6 97 43 20 13 7
6. Vyama vya
Wafanyakazi
20 1 89 13 19 13 6
7. Vyama
Vinavyowakilisha
Wafugaji
8 1 43 4 10 7 3
8. Vyama
vinavyowakilisha
Wavuvi
7 3 45 12 10 7 3 5
Na. Kundi/Taasisi Taasisi zilizoleta
mapendekezo
Idadi ya Watu
Waliopendekezwa
Idadi ya
Wajumbe
Wanaotakiwa
Idadi ya
Walioteuliwa
Tanzania
Bara
Zanzibar Tanzania
Bara
Zanzibar Tanzania
Bara
Zanzibar
9. Vyama vya
Wakulima
22 8 115 44 20 13 7
10. Makundi yenye
Malengo
Yanayofanana
142 21 613 114 20 14 6
Mapendekezo
Binafsi
- - 118
-
Jumla 672 178 2,880 874 201 134 67
Jumla Kuu 850 3,754 1
8. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa
katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba.
Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja
wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania
Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka
Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo
wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa
nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi
wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo
wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201
halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa
sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9. Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara
yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa
Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na
idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya
maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua
taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara
walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa
kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za
kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na
nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
2
WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar
wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya
wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a) Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana,
watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani
wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe
wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe
wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b) Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake
na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika
orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa
vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya
wajumbe wanaume ni 101.
(c) Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama
chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili
umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili
wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa
maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika
kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya
wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:
3
TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Magdalena Rwebangira 2. Kingunge Ngombale Mwiru
3. Asha D. Mtwangi 4. Maria Sarungi Tsehai
5. Paul Kimiti 6. Valerie N. Msoka
7. Fortunate Moses Kabeja 8. Sixtus Raphael Mapunda
9. Elizabeth Maro Minde 10. Happiness Samson Sengi
11. Evod Herman Mmanda 12. Godfrey Simbeye
13. Mary Paul Daffa
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Idrissa Kitwana Mustafa 2. Siti Abbas Ali
3. Abdalla Abass Omar 4. Salama Aboud Talib
5. Juma Bakari Alawi 6. Salma Hamoud Said
7. Adila Hilali Vuai
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Tamrina Manzi 2. Olive Damian Luwena
3. Shamim Khan 4. Mchg. Ernest Kadiva
5. Sheikh Hamid Masoud Jongo 6. Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald
Leo Mtetemela
7. Magdalena Songora 8. Hamisi Ally Togwa
9. Askofu Amos J. Muhagachi 10. Easter Msambazi
11. Mussa Yusuf Kundecha 12. Respa Adam Miguma
13. Prof. Costa Ricky Mahalu
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Sheikh Thabit Nouman Jongo 2. Suzana Peter Kunambi
3. Sheikh Nassoro Mohammed
Ibrahimu
4. Fatma Mohammed Hassan
5. Louis Majaliwa 6. Yasmin Yusufali E. H alloo
7. Thuwein Issa Thuwein
4
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)
TANZANIA BARA (28)
1. Hashim Rungwe Spunda 2. Thomas Magnus Mgoli
3. Rashid Hashim Mtuta 4. Shamsa Mwangunga
5. Yusuf S. Manyanga 6. Christopher Mtikila
7. Bertha Ng’angompata 8. Suzan Marwa
9. Dominick Abraham
Lyamchai
10. Mbwana Salum Kibanda
11. Peter Kuga Mziray 12. Isaac Manjoba Cheyo
13. Dr. Emmanuel John Makaidi 14. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
15. Modesta Kizito Ponera 16. Prof. Abdallah Safari
17. Salumu Seleman Ally 18. James Kabalo Mapalala
19. Mary Oswald Mpangala 20. Mwaka Lameck Mgimwa
21. Nancy S. Mrikaria 22. Nakazael Lukio Tenga
23. Fahmi Nasoro Dovutwa 24. Costantine Benjamini Akitanda
25. Mary Moses Daudi 26. Magdalena Likwina
27. John Dustan Lifa Chipaka 28. Rashid Mohamed Ligania Rai
TANZANIA ZANZIBAR (14)
1. Ally Omar Juma 2. Vuai Ali Vuai
3. Mwanaidi Othman Twahir 4. Jamila Abeid Saleh
5. Mwanamrisho Juma Ahmed 6. Juma Hamis Faki
7. Tatu Mabrouk Haji 8. Fat –Hiya Zahran Salum
9. Hussein Juma 10. Zeudi Mvano Abdullahi
11. Juma Ally Khatibu 12. Haji Ambar Khamis
13. Khadija Abdallah Ahmed 14. Rashid Yussuf Mchenga 5
TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA
1. Dr. Suzan Kolimba 2. Prof. Esther Daniel Mwaikambo
3. Dr. Natujwa Mvungi 4. Prof. Romuald Haule
5. Dr. Domitila A.R. Bashemera 6. Dr. Jasmine Bendantunguka
Tiisekwa
7. Prof. Bernadeta Kilian 8. Teddy Ladislaus Patrick
9. Dr. Francis Michael 10. Prof. Remmy J. Assey
11. Dr. Tulia Ackson 12. Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
13. Hamza Mustafa Njozi
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Makame Omar Makame 2. Fatma Hamid Saleh
3. Dr. Aley Soud Nassor 4. Layla Ali Salum
5. Dkt. Mwinyi Talib Haji 6. Zeyana Mohamed Haji
7. Ali Ahmed Uki
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Zuhura Musa Lusonge 2. Frederick Msigala
3. Amon Anastaz Mpanju 4. Bure Zahran
5. Edith Aron Dosha 6. Vincent Venance Mzena
7. Shida Salum Mohamed 8. Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
9. Elias Msiba Masamaki 10. Faustina Jonathan Urassa
11. Doroth Stephano Malelela 12. John Josephat Ndumbaro
13. Ernest Njama Kimaya
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Haidar Hashim Madeweyya 2. Alli Omar Makame
3. Adil Mohammed Ali 4. Mwandawa Khamis Mohammed
5. Salim Abdalla Salim 6. Salma Haji Saadat
7. Mwantatu Mbarak Khamis
6
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
TANZANIA BARA (13)
1. Honorata Chitanda 2. Dr. Angelika Semike
3. Ezekiah Tom Oluoch 4. Adelgunda Michael Mgaya
5. Dotto M. Biteko 6. Mary Gaspar Makondo
7. Halfani Shabani Muhogo 8. Yusufu Omari Singo
9. Joyce Mwasha 10. Amina Mweta
11. Mbaraka Hussein Igangula 12. Aina Shadrack Massawe
13. Lucas Charles Malunde
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1. Khamis Mwinyi Mohamed 2. Jina Hassan Silima
3. Makame Launi Makame 4. Asmahany Juma Ali
5. Mwatoum Khamis Othman 6. Rihi Haji Ali
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1. William Tate Olenasha 2. Makeresia Pawa
3. Mabagda Gesura Mwataghu 4. Doreen Maro
5. Magret Nyaga 6. Hamis Mnondwa
7. Ester Milimba Juma
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1. Said Abdalla Bakari 2. Mashavu Yahya
3. Zubeir Sufiani Mkanga
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1. Hawa A. Mchafu 2. Rebecca Masato
3. Thomas Juma Minyaro 4. Timtoza Bagambise
5. Tedy Malulu 6. Rebecca Bugingo
7. Omary S. Husseni
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1. Waziri Rajab 2. Issa Ameir Suleiman
3. Mohamed Abdallah Ahmed 7
VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Agatha Harun Senyagwa 2. Veronica Sophu
3. Shaban Suleman Muyombo 4. Catherine Gabriel Sisuti
5. Hamisi Hassani Dambaya 6. Suzy Samson Laizer
7. Dr. Maselle Zingura Maziku 8. Abdallah Mashausi
9. Hadijah Milawo Kondo 10. Rehema Madusa
11. Reuben R. Matango 12. Happy Suma
13. Zainab Bakari Dihenga
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Saleh Moh’d Saleh 2. Biubwa Yahya Othman
3. Khamis Mohammed Salum 4. Khadija Nassor Abdi
5. Fatma Haji Khamis 6. Asha Makungu Othman
7. Asya Filfil Thani
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (14)
1. Dr. Christina Mnzava 2. Paulo Christian Makonda
3. Jesca Msambatavangu 4. Julius Mtatiro
5. Katherin Saruni 6. Abdallah Majura Bulembo
7. Hemedi Abdallah Panzi 8. Dr. Zainab Amir Gama
9. Hassan Mohamed Wakasuvi 10. Paulynus Raymond Mtendah
11. Almasi Athuman Maige 12. Pamela Simon Massay
13. Kajubi Diocres Mukajangwa 14. Kadari Singo
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1. Yussuf Omar Chunda 2. Fatma Mussa Juma
3. Prof. Abdul Sheriff 4. Amina Abdulkadir Ali
5. Shaka Hamdu Shaka 6. Rehema Said Shamte
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Februari, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma.
Rais amekabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo Cha Kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha.
Library hiyo ilianzishwa na Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita.
"Lazima mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi nitaendelea kutafuta vitabu niwaletee ili kuijengea uwezo Library yetu ya Monduli”.
Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Mwamunyange amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.
“Juhudi zako za kuliendeleza Jeshi letu imetuongezea uwezo na kujiamini zaidi. Bila juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia sana mafanikio haya” amesema Jenerali Mwamunyange .
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
28 Aprili,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameiamuru Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake kuchukua hatua za mara moja kukomesha aibu ya viwanja vya ndege vya Tanzania kutumika katika uchochoro wa kupitisha na kusafirisha madawa ya kulevya.
Aidha, Rais Kikwete amesema ukweli kuwa madawa ya kulevya yanazidi kupita katika viwanja vya ndege za Julius Nyerere International Airport (JNIA) na ule wa Kilimanjaro International Airport (KIA) unazidi kuchafua heshima na jina la Tanzania.
Rais Kikwete alikuwa anazungumza leo, Alhamisi, Aprili 24, 2014, kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Awamu ya Tatu ya Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam kwenye eneo la Uwanja huo.
Rais ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Uwanja huo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Ujenzi wa Hospitali ya Kisasa ya Kufundishia na Kutoa Huduma katika eneo la Mlongazila, eneo la Kibamba, Dar Es Salaam. Shughuli zote mbili ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano.
“Siridhishwi na hali ya usalama katika viwanja hivi viwili na matukio ya kusikia madawa yametokea Tanzania kupitia viwanja vyake na yamekamatwa huko Australia yanachafua sana jina la nchi yetu. Badala ya kuchukua hatua kukomesha jambo hili tunakwenda mbele, tunakwenda nyuma…mbele, nyuma. Hili haliwezi kuruhusiwa kuendelea. Ni jambo la kutia simanzi sana,” amesema Rais Kikwete na kuendelea:
“Mmeyasema wenyewe…leo kiwanja hiki kinapitisha abiria milioni 2.5 kwa mwaka, mkifikisha abiria milioni sita si mtakuwa soko huria kabisa…..mara leo mwanamuziki huyu kakamatwa Afrika Kusini…mara kesho yule….limalizeni hili haraka. Nataka tuongeze usalama sana katika viwanja hivi viwili…. vimekuwa kama uchochoro.”
Rais Kikwete amemtaka Waziri wa Uchukuzi kumjulisha ni maofisa gani wa Idara za Serikali wanahusika kupitisha madawa hayo kwenye viwanja hivyo: “Kama kuna maofisa wa ushuru, ama maofisa wa uhamiaji, ama maofisa wa polisi ama maofisa wa uwanja wa ndege ambao wanashiriki katika mchezo huu wa kupitisha madawa haya nipeni orodha yao, nitawaondoa kazini. Tusifanye masihara na hili, linatuaibisha sote. Tusiwaonee aibu watu katika jambo hili.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
24 Aprili, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ya Dodoma yasikuvunje moyo – Mzee Msuya amwambia Rais
Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Mstaafu, Mheshimiwa Cleopa David Msuya amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya na amemshauri kutokuvunjwa moyo na kile ambacho amekielezea kama “mambo madogo madogo” yanayoendelea ndani ya Bunge Maalum la Katiba.
Aidha, Mzee Msuya amesema kuwa Rais Kikwete hatasahauliwa kwa kipindi chake cha uongozi kutokana na upanuzi mkubwa wa shughuli za maendeleo.
Mzee Msuya ameyasema hayo leo, Jumatano, Aprili 23, 2014 wakati alipozungumza kuwashukuru na kuwaaga wananchi wa Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia hatua yake ya kunga’atuka katika uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, shughuli ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete iliyofanyika ofisi za CCM Wilaya ya Mwanga.
Katika hotuba yake ndefu, Mheshimiwa Msuya ambaye ameshikilia nyadhifa nyingi za uongozi nchini ikiwamo ile ya kuwa Mbunge wa Mwanga kwa miaka 20 mfululizo amemwambia Rais Kikwete:
“Tunakupongeza kwa kuanzisha uandaaji wa Katiba mpya itakayoongoza Taifa letu la Tanzania kwa miaka 100 na zaidi ijayo. Zoezi hili likikamilika kama ulivyoliweka itatuwezesha kusonga mbele na maendeleo ya umma kwa kasi zaidi chini ya utawala bora unaotabirika. Hii ni shughuli kubwa na muhimu sana kwa wananchi wetu, na Mheshimiwa Rais wala usivunjwe moyo na mambo madogo madogo ambayo yanatokea Dodoma,”amesema Mzee Msuya.
Mheshimiwa Msuya ambaye alishikilia ubunge kwa jumla ya miaka 39, ikiwamo 20 ya Ubunge wa Mwanga na anajulikana kama “Baba wa Mwanga” amemwambia Rais Kikwete:
“Tunakupongeza kwa maamuzi makubwa na mazito ya msingi uliyoyafanya kuonyesha njia ya maendeleo kwa Taifa letu la Tanzania ikijumuisha Mwanga”.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
24 Aprili, 2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais Kikwete: Acheni kuwatumia wananchi kama chambo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi nchini kuacha kuwatumia wananchi kama chambo cha kufanikisha malengo yao ya kisiasa na kusababisha migororo na uvunjifu wa amani.
Aidha, Rais Kikwete amewataka wananchi wa Wilaya ya Karatu wasiige mfano wa Arusha ambako fujo zinazoongozwa na baadhi ya viongozi zimezorotesha sana uchumi wa mji huo kwa sababu usalama ni kigezo kikuu cha maendeleo ya uchumi.
Akizungumza wakati anazindua Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, mjini Karatu asubuhi ya leo, Jumanne, Aprili 22, 2014, Rais Kikwete amesema:
“Usalama ni jambo muhimu sana na kwa maana hiyo, nawaombeni msiige kabisa mfano wa Arusha, sote tunajua kimetokea nini kule kwa sababu ya fujo za kisiasa ambazo zinachochewa na viongozi na hasa Mbunge wa Arusha mjini Bwana Lema,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mbunge anayo nafasi kubwa kujenga hoja zake ndani ya Bunge na ndani ya mikutano ya halmashauri. Lakini kwa mbunge kuwachochea wananchi na kuwachukua na kuwatembeza barabarani ambako wanakumbana na virugu vya polisi siyo uongozi wa busara hata kidogo.”
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mheshimiwa Lazaro Titus Massey amewaambia wananchi kuwa moja ya mwelekeo mkuu wa CHADEMA wilayani Karatu ni kushirikiana na Serikali na polisi katika kudumisha amani.
Tunawakaribisha Arusha waje kujifunza kwetu namna ya kudumisha amani. Tunamkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Bwana John Mongella kuja kujifunza namna ya kurejesha na kudumisha amani mjini humo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
22 Aprili,2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
CHADEMA yamshukuru Rais Kikwete kwa maendeleo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wilaya ya Karatu katika Mkoa wa Arusha.
Aidha, chama hicho kimempongeza Rais Kikwete kwa kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali msimamo wao wa kisiasa na hata katika maeneo yanayounga mkono upinzani.
Shukurani na pongezi hizo zimetolewa mchana wa leo, Jumanne, Aprili 22, 2014 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Mheshimiwa Lazaro Titus Massey wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini Karatu. Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na CHADEMA.
“Ni lazima tutoe shukurani nyingi kwako Mheshimiwa Rais kwa sababu bila wewe kuwa Rais wa Tanzania sisi Karatu tusingepata jengo hili. Pamoja na kwamba Halmashauri yetu ni CHADEMA bado umeamua kuchangia sana maendeleo ya Wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo hili. Sisi hata robo ya fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” amesema Mheshimiwa Massey huko akishangiliwa na wananchi.
Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.412 na kati ya hizo, Serikali imetoa shilingi bilioni 1.394 na Halmashauri imechangia shilingi milioni 18 tu.
Akizungumza baada ya kumsikiliza Mheshimiwa Massey, Rais Kikwete amesema kuwa ni sera ya Serikali yake kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa kila Mtanzania anataka na anayo haki ya kupata maendeleo.
“Sisi hatuna wasiwasi, wananchi wa Karatu wamechagua CHADEMA lakini chama hiki hakina Serikali. Wananchi wamechagua chama bila Serikali. Halmashauri mnayo lakini Serikali tunayo sisi. Katika kusambaza maendeleo, sisi hatuwezi kubagua. Hiyo ndiyo demokrasia na Serikali yetu inaheshimu sana demokrasia na misingi ya utawala bora,” amesema Rais Kikwete.
Wakizungumza baadaye kwenye mkutano wa hadhara wabunge wote wawili wa CHADEMA, waheshimiwa Cecilia Paleso na Israel Nanse wamerudia tena kumpogeza Rais Kikwete kwa kusambaza maendeleo katika maeneo yote ya Tanzania yakiwemo yaliyoko chini ya wapinzani.
“Chini ya uongozi wako, maendeleo yamesambazwa na sisi Karatu tumenufaika sana. Ni matumaini yetu kuwa chini yako, tutaendelea kunufaika na sera zako sahihi,”amesema Mheshimiwa Paleso.
Naye Mheshimiwa Nanse amesema: “Mheshimiwa Rais sisi kwetu hapa hatuna ugomvi kati ya vyama vya siasa. Siye CHADEMA tunajua kuwa CCM ni chama tawala Tanzania na CHADEMA ni chama kiongozi hapa kwetu Karatu. Ni uhusiano huu uliowezesha Karatu kuendelea kupata maendeleo.”
“Tunakushukuru na kukupongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuifungua nchi yetu kwa barabara kila mahali. Aidha, sisi wana-Karatu tunakushukuru sana kwa mradi wa maji ambao umeuzindua leo”. Tunakushukuru sana.
Rais Kikwete alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha na kesho atafanya ziara ya Wilaya ya Mwanga katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu- Dar es Salaam.
22 Aprili,2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
Tunawatakia kazi njema.
Taarifa kwa vyombo vya habari
Kifo cha DC: Rais Kikwete amtumia salamu Waziri Mkuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuomboleza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa, Ndugu Moshi Chang’a.
“Ni kifo cha kusikitisha kwa sababu kimepunguza safu ya uongozi wetu na kimelinyang’anya taifa letu mhamasishaji hodari na mtetezi wa kuaminika wa maendeleo ya wananchi,” Rais Kikwete amesema katika salamu hizo.
Amesema Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi: “Nilimjua Ndugu Chang’a kwa miaka mingi tokea mwaka 1979 alipojiunga na utumishi wa Chama cha Mapinduzi ambacho pia alikitumia kwa uaminifu mkubwa hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya mwaka 2003. Alikuwa kiongozi wa kweli kweli wa maendeleo na kifo chake kimetuachia pengo la uongozi.”
“Nakutumia salamu zangu za dhati kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako, naitumia familia wa Ndugu Chang’a pole za dhati ya moyo wangu kwa kuondokewa na mzazi na mhimili wa familia. Nakuomba uwajulishe kuwa naelewa machungu yao katika kipindi hiki na nawaombea subira na uvumilivu kwa sababu yote ni mapenzi ya Mungu. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya marehemu. Amen,” amesema Rais katika salamu hizo.
Ndugu Moshi Chang’a ambaye aliaga dunia jioni ya jana, Jumapili, Aprili 20, 2014 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar Es Salaam amekuwa mkuu wa wilaya katika Mikoa ya Mbeya, Tabora na Rukwa.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Aprili,2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Paschal Mabiti,kuomboleza vifo vya watu 11 ambao wamepoteza maisha yao katika ajali ya basi iliyotokea mkoani humo leo, Jumatatu, Aprili 21, 2014.
Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa ajali zabarabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu wasiokuwa na hatia.
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya ajali hiyo ambayo nimejulishwa kuwa imetokea katika Kijiji cha Itwimila katika Wilaya ya Busega katika Mkoa wako wa Simiyu wakati basi lililokuwa linasafiri kutoka Tarime, Mkoa wa Mara kwenda Mwanza kupitia Simiyu lilipoacha njia na kugonga nyumba kabla ya kupinduka.”
Amesema Rais Kikwete: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi na najiunga nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu. Aidha, kupitia kwako, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia zote ambazo zimepoteza wapendwa wao katika ajali hiyo. Naungana nao katika kuomboleza wapendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aziweke peponi roho za marehemu.”
Rais Kikwete vile vile ametoa pole kwa wote ambao wameumia katika ajali hiyo, akiwaombea wapone haraka na kurejea kwenye shughuli zao za kujiletea maendeleo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Aprili,2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
Rais Kikwete, TUCTA wajadili jinsi ya kuboresha maslahi na
ustawi wa wafanyakazi
Aagiza kukamilishwa kwa uundwaji wa mabaraza ya wafanyakazi katika utumishi wa umma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, Alhamisi, Aprili 17, 2014, alifanya mazungumzo na majadiliano ya kina na viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi nchini yenye nia ya kutafuta njia za kuboresha maslahi na ustawi wa wafanyakazi nchini.
Mazungumzo hayo ya muda mrefu yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam yalihudhuriwa pia na Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudensia M. Kabaka, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi) Mheshimiwa Celina Kombani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) Mheshimiwa Hawa Ghasia, Waziri wa Fedha Mheshimiwa Saada Mkuya na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue.
Aidha, mazungumzo hayo yalihudhuriwa na maofisa waandamizi wa Serikali wakiwemo Makatibu Wakuu wa Wizara ambazo zinahusika moja kwa moja na maslahi na ustawi wa wafanyakazi na uongozi wa vyama vya wafanyakazi uliongozwa na uongozi wa juu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania - TUCTA.
Rais Kikwete na viongozi hao wa vyama vya wafanyakazi nchini kwa zaidi ya saa 10 walijadili hali ya utekelezaji wa masuala na mambo yaliyokubaliwa katika kikao chao cha namna hiyo kilichofanyika Februari 27, Mwaka jana wa 2013.
Vile vile, Rais Kikwete na viongozi hao wakiwemo wale wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) walichambua kwa kina hoja za wafanyakazi zilizowasilishwa kwa Rais Kikwete na vyama hivyo.
Hoja hizo zilijadiliwa katika kikao hicho. Miongoni mwa hoja hizo ni ajira kwa wageni na athari zake kwa ajira ya Watanzania, athari za kuzuka kwa mawakala wa ajira nchini, watumishi waandamizi wa Serikali kushikilia nafasi za uongozi katika vyama vya wafanyakazi na athari zake, ushirikishwaji wa wafanyakazi katika bodi za taasisi za umma na Serikali na uhamisho wa maofisa kazi ambao Rais Kikwete aliuagiza miaka mitatu iliyopita.
Hoja nyingine zilizojadiliwa ni hali ya afya ya wafanyakazi katika migodi mbali mbali nchini, bei ya umeme majumbani na athari yake kwa wafanyakazi, uwezekano wa kupunguza tena kodi kwenye mishahara ya wafanyakazi jambo ambalo Serikali ililifanya Mwaka 2013, madai ya malimbikizo ya mapato ya wafanyakazi, madeni ya walimu na uwezekano wa nyongeza ya mishahara kwa walimu.
Katika kikao hicho, Rais Kikwete ameagiza wizara, idara na taasisi zote za Serikali na umma ambazo hazijatekeleza hitaji la kisheria ya kuundwa kwa mabaraza ya wafanyakazi katika utumishi wa umma kufanya hivyo mara moja bila kuchelewa.
Rais Kikwete ametoa muda hadi Mei Mosi, mwaka huu, kwa wizara, idara na taasisi hizo kuwa tayari zimeunda mabaraza hayo na amemwagiza Balozi Sefue kutuma barua za maagizi hayo ya Rais kwa wizara, idara na taasisi husika.
Aidha, Rais amesema kuwa mwishoni mwa mwaka huu atapenda kupata taarifa kuhusu hali ya uanzishwaji na utendaji wa mabaraza hayo ambayo ni muhimu kwa uwakilishi wa wafanyakazi katika uendeshaji wa taasisi za umma ambazo wanazifanyia kazi.
Rais Kikwete amekiambia kikao hicho: “Wafanyakazi lazima washirikishwe kikamilifu katika uendeshaji wa taasisi wanazozifanyika kazi na hasa katika vikao vyote vya bajeti za wizara, idara na taasisi za umma ambako wameajiriwa.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
19 Aprili,2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
JK: Tuzo hii ni ya Watanzania wote
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa Tuzo la Kiongozi Bora wa Maendeleo Afrika – “Africa’s Most Impactful Leader of The Year Award” kwa Watanzania wote, kama heshima kwao, kwa sababu wao ndio waliochangia maendeleo yaliyomwezesha kutunukiwa Tuzo hiyo.
“Napokea Tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Aidha, naitoa Tuzo hiyo kwa Watanzania kwa sababu, hata kama nimekuwa kiongozi, ukweli ni kwamba mafanikio na maendeleo yote yaliyopatikana na kupelekea kutunukiwa Tuzo hii, yametokana na juhudi zetu za pamoja,” amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alikuwa anapokea Tuzo ya Kiongozi Bora wa Maendeleo Afrika mwaka 2013 kwa kuwa kiongozi bora wa utumishi bora wa umma katika Afrika na aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Benard Membe katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, asubuhi ya leo, Aprili 17, 2014.
Mheshimiwa Membe ndiye alipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Kikwete katika sherehe kubwa iliyofanyika kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, Marekani, usiku wa Aprili 9, mwaka 2014.
Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine kwa kiongozi wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi wa maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wake na Rais Kikwete anakuwa Rais wa tatu wa Afrika kupokea tuzo hiyo. Kabla ya Rais Kikwete Tuzo hiyo ilikwishakutolewa kwa marais wa Sierra leone na Liberia.
Akipokea Tuzo hiyo mbele ya waandishi wa habari, Rais Kikwete amesema kuwa Tuzo hiyo ina maana kuwa dunia “inaona, inatambua na inathamini” kazi kubwa ambayo inafanywa na Watanzania katika jitihada zao za kujiletea maendeleo. Hivyo, hii ni Tuzo yetu sote na naikabidhi kwa Watanzania wote kwa heshima ya jitihada kubwa wanazozifanya kuboresha maisha yao.”
Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Membe na Balozi wa Nigeria katika Marekani, Mheshimiwa Profesa Ade Adefuye kwa niaba ya Rais Goodluck Jonathan ambaye awali alipangwa kukabidhi Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Tuzo hiyo, Profesa Adefuye alielezea kwa undani jinsi anavyomfahamu Rais Kikwete akisisitiza kuwa Kiongozi wa Tanzania ni kilelezo halisi cha rika la viongozi wapya wa Afrika ambao dira na visheni yao ni maendeleo ya Bara la Afrika na watu wake.
Alisema Profesa Adefuye: “Kwa niaba ya Nigeria na kwa niaba ya Bara la Afrika nawasilisha kwenu Mwafrika wa wakati huu, mtoto maarufu wa Tanzania na mtoto maarufu wa Afrika – Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Aprili, 2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
Ni ukosefu wa adabu kuwatukana waasisi wa Tanzania - JK
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu kuwa baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli Waanzilishi wa Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa viongozi hao wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi, mambo makubwa na mambo ya kihistoria kiasi cha kwamba Watanzania wanao wajibu wa kudumisha na kuenzi heshima yao kwa namna ya kudumu.
Akizungumza na Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari usiku wa jana, Jumatano, Aprili 16 katika mahojiano maalum ya kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano, Rais Kikwete amesema: “Ni kukosa adabu na ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mtanzania yoyote kuwatukana, kuwadhihaki ama kuwakejeli waasisi wa Taifa letu. Hawa ni watu ambao waliifanyia nchi yetu mambo makubwa,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mzee Karume yule aliongoza Mapinduzi yaliyoondoa dhuluma na uonevu pale Visiwani. Waafrika walio wengi walikuwa wanaonewa sana pale Tanzania Visiwani, pengine watu wamesahau, lakini hata pale walipokuwa wanashinda uchaguzi bado walikuwa hawapewi nafasi ya kuongoza maisha yao wenyewe.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Ni ukosefu wa adabu kwa yoyote kumshutumu mtu aliyejitolea kiasi hicho ili kubadilisha mfumo dhalimu na kujenga maisha na mazingira ya maisha bora kwa wengi.”
“Mzee Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye umoja, lenye amani na mshikamano. Misingi ambayo aliijenga yeye ndiyo imeendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka yote hii. Viongozi wengine wote ambao wamemfuata yeye – Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa mimi mwenyewe, tumefuata na kuongozwa na misingi hii. Na siku nchi yetu inaamua kuipuuza misingi hiyo, tutaingia katika matatizo makubwa.”
Rais Kikwete ametoa msimamo huo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu matusi, kejeli, dhihaki ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache wa Bunge Maalum la Katiba juu ya waasisi hao wa Tanzania na Wabunifu Wakuu wa Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
17 Aprili, 2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Dkt. Jacob Chimeledya, Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, kuomboleza kifo cha Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Dayosisi ya Kati, Dodoma kilichotokea tarehe 27 Machi, 2014 katika Hospitali ya Mil Park nchini Afrika Kusini alikokuwa amepelekwa kwa matibabu.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu, Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo aliyelitumikia Kanisa lake la Anglikana kwa uaminifu na uadilifu mkubwa, na ambaye mchango wake kwa maisha ya kiroho ya Waumini wake unajulikana kwa wengi miongoni mwetu”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
Rais Kikwete amesema kuondoka kwa Askofu Mhogolo kumeacha pengo kubwa siyo tu kwa Waumini wa Kanisa la Anglikana katika Dayosisi yake, Dayosisi ya Kati,Dodomabali pia kwa Waumini wote wengine wa Madhehebu hayo kote nchini, na kwa kweli wapenda amani wote popote walipo.
“Ni kutokana na msiba huu mkubwa, ninakutumia wewe Dkt. Jocob Chimeledya, Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, na Waumini wote wa Kanisa hilo Salamu zangu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa kuondokewa na Mtumishi huyu wa Mungu aliyejitoa kikamilifu kuwatumikia Waumini wa Kanisa lake”, ameongeza kusema Rais Kikwete na kuongeza,
“Kupitia kwako naomba pia Salamu zangu za Rambirambi na Pole nyingi ziifikie familia ya Marehemu Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo kwa kuondokewa na Kiongozi na mhimili wa familia yao”.
Rais Kikwete ameiomba familia ya Marehemu kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola.
“Ninaihakikishia familia ya Marehemu kuwa binafsi niko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa kutambua kuwa msiba wao ni wetu sote. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi, Roho ya Marehemu Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo, Amina”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika Salamu zake.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
28 Machi,2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
TAMKO LA KATIBU MKUU KIONGOZI KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
IKULU, DAR ES SALAAM, TAREHE 14 APRILI, 2014
__________________________________________________
Siku 12 zijazo tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wamezaliwa watu ndani ya Muungano huu na wengine wana wajukuu.
Inasikitisha sana kuwa leo, miaka 50 baadaye ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna Hati ya Muungano (Articles of the Union).
Waasisi wa Taifa letu ambao tarehe 22 Aprili, 1964 kule Zanzibar walitia saini Hati hiyo, mbele ya mashuhuda, nao wameonekana kama walichokifanya kilikuwa kiini macho, na kwa hiyo kwamba waliongoza Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msingi wa kiini macho hicho kwa miaka yote hadi Mwenyezi Mungu alipowaita.
Mambo yote mawili yametusononesha sana sisi Serikalini, na bila shaka yamewasononesha wananchi wanaoipenda nchi yao, wanaowapenda Waasisi wa Taifa letu na kuuenzi Muungano wao.
Madai ya kuonyeshwa Hati ya Muungano yalianza siku nyingi lakini hatukuweza kuamini hali itafikiwa ilipofikia, ambapo wapo watu wanathubutu kudai na kuapa kuwa Hati hiyo haipo.
Ukweli ni kuwa hati hiyo ipo, ilikuwepo siku zote. Hata hivyo, lazima tukubaliane kuwa zipo Hati fulani ambazo ni kiini cha uwepo wetu kama Taifa huru, Jamhuri huru na Muungano huru, ambazo tunazihifadhi kama mboni ya jicho. Hati hizo ni pamoja na Hati ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961, Hati ya Tanganyika kuwa Jamhuri mwaka 1962, na Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964. Hati za aina hii zinahifadhiwa maeneo maalum ambayo ni salama ili zisipotee wala kuharibika. Kwa kawaida hatuzitoi, tunazifungua ili kuzihifadhi kwa namna yoyote ile.
Lakini sasa maneno yanakua mengi, tuhuma zimekuwa nyingi, dhihaka zimekuwa nyingi, kiasi cha wananchi kuanza kutiwa mashaka iwapo kweli Hati ya Muungano ipo au la.
Hivyo, kwa maagizo na ridhaa ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaleta mbele yenu Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyotiwa saini Zanzibar na waasisi wetu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume, ili muione na kuwahakikishia Watanzania kuwa yanayosemwa kuwa hakuna Hati hiyo si kweli. Hati hiyo ipo tangu wakati huo, imetunzwa vizuri na waliotutangulia, tumeirithi, na tutaendelea kuihifadhi.
Na, tukiombwa kufanya hivyo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum nina uhakika Rais ataridhia ipelekwe huko ili kuondoa mjadala wa kama Hati ipo au la.
Isitoshe, tufanye utaratibu wa kuweka nakala kwenye Makumbusho ya Taifa ili kila atakayetaka kuiona katika miaka mingine 50 ijayo na kuzidi aione.
Mwisho, narejea kusema kuwa kwa upande wa Serikali tunasikitishwa na kufadhaishwa sana na tuhuma nzito kwamba labda waasisi wetu hawakuwa makini au walitufanyia kiini macho. Hatukutarajia wawepo Watanzania wenzetu, wafikie hapo.
Ni jambo zito. Vile vile hatukutarajia kuwa Serikali itatuhumiwa kuwa haikuwa makini kuhifadhi waliosaini waasisi wetu.
Matumaini yetu ni kuwa baada ya leo tutaendelea na mambo ya msingi kwa mustakabali, umoja na uimara wa Taifa letu badala ya kuchochea hisia kuwa Muungano wetu hauna msingi imara wa kisheria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Aprili, 2014
Taarifa kwa vyombo vya habari
KWA WAHARIRI WOTE
LEO SAA 10:00 JIONI KATIKA OFISI ZA MAWASILIANO YA RAIS – IKULU, KUTAKUWA NA PRESS CONFERENCE YA KATIBU MKUU KIONGOZI AMBAYO ITAFAFANUA MAMBO KADHAA YA KITAIFA.
KWA SABABU YA UMUHIMU WA UFAFANUZI HUU, TUNAOMBA PRESS CONFERENCE HII IRUSHWE MOJA KWA MOJA (LIVE).
TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU.
ASANTENI NA KARIBUNI SANA.
IMETOLEWA NA;
PREMI KIBANGA,
MWANDISHI WA HABARI WA RAIS MSAIDIZI,
IKULU – DAR ES SALAAM.
14 APRILI,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kwa kutwaa Kombe la Dunia huko Rio de Janeiro – Brazil.
“Mmetuwakilisha vyema, ninawapongeza sana, pia mmewapa moyo watoto wengine wote wenye vipaji maalum lakini hawakubahatika kuwa na makazi rasmi, hongereni sana” Rais amesema.
Timu hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 (under 16) ilipangwa kundi la 2 ambapo wamekuwemo na Nchi za Argentina, Nicaragua,Philippines na Burundi na kulikuwa na makundi matatu.
Tanzania iliingia nusu fainali kwa kuwa mshindi wa pili na pia kuminyana na Marekani na kuichapa mabao 6-1 na baadae kuitoa Burundi kwa mabao 3-1.
“Hongereni kwa kujituma na kucheza kwa ustadi”. Rais amesema na kuwaasa watoto “ongezeni bidii, nidhamu na mazoezi ya kutosha na hakika mtafanikiwa zaidi na kulibeba jina la Tanzania mbali zaidi ya hapa katika ulimwengu wa soka duniani, kwani hakuna kisichowezekana kama mtazingatia maelekezo, mafunzo, bidii na nidhamu ya yote mnayofanya” Ameongeza .
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Aprili,2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tuzo la Rais Kikwete lakadhibiwa Washington
Apokea Waziri Bernard Membe kwa niaba katika sherehe ya kuvutia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa leo, Jumatano, Aprili 9, 2014, ametunukiwa Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika katika sherehe kubwa iliyofanyika kwenye Hoteli ya St. Regis kwenye mji mkuu wa Marekani wa Washington.
Tuzo hiyo ambayo imepokelewa, kwa niaba ya Rais Kikwete, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine kwa Rais Kikwete kwa kuwa “Kiongozi wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kwa mwaka 2013.”
Pamoja na Rais Kikwete, Waafrika wengine ambao wamepewa heshima kwenye sherehe hiyo ni Dkt. Kingsley Moghalu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria na Bwana John Kennedy Opara, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mahujaji Wakristo wa Nigeria ambaye pia ni mshauri wa Rais Gooluck Jonathan wa nchi hiyo kuhusu mahusiano ya kidini nchini Nigeria.
Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Membe, kwa niaba ya Rais Kikwete, na Balozi wa Nigeria katika Marekani, Profesa Ade Adefuye ambaye naye ametoa Tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Jonathan ambaye, kama alivyo Rais Kikwete, hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo ya kuvutia.
Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington, lilimchagua Rais Kikwete kushinda Tuzo hiyo kwa mwaka 2013 baada ya wasomaji na wadau wake wengine wa Jarida hilo kuwa wamemchagua kwa njia ya kura ya maoni Rais Kikwete kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika. Rais Kikwete anamfuatia Rais wa Sierra, Mheshimiwa Ernest Bai Koroma, ambaye alishinda Tuzo hiyo mwaka 2012.
Awali, Rais Kikwete alikuwa akabidhiwe Tuzo hiyo tokea Desemba mwaka jana, lakini kutokana na kuingiliana kwa shughuli za Rais, sherehe hiyo iliahirishwa hadi mwaka huu.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Membe, Balozi Adefuye wa Nigeria katika Marekani amemwelezea kwa undani anavyomfahamu Rais Kikwete akisisitiza kuwa kiongozi huyo wa Tanzania ni kielelezo cha rika jipya la viongozi wa Afrika ambao dira na visheni yao ni maendeleo ya Bara la Afrika na wananchi wake.
“Kwa niaba ya Nigeria, kwa niaba ya Bara la Afrika, nawasilisha kwenu Mwafrika wa wakati huu, mtoto maarufu wa Tanzania na mtoto maarufu wa Bara la Afrika – Rais Jakaya Mrisho Kikwete,” amesema Dkt. Adefuye katika sherehe iliyotangazwa na kuonyeshwa moja kwa moja na mitandao mbali mbali ya kijamii duniani.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na watu mbali mbali mashuhuri wakiwamo baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Marekani, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai ambaye yuko Washington kwa shughuli za kikazi, Mwakilishi katika Bunge la Wawakilishi wa Jimbo la Georgia katika Marekani, Bi. Dee Dawkins-Haigler ambaye pia ni mwenyekiti wa wabunge weusi katika Bunge hilo na Balozi wa Tanzania katika Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
Aidha, akizungumza katika hotuba yake ya utangulizi mwanzoni wa sherehe hiyo, Mchapishaji wa Jarida la African Leadership Magazine, Dkt. Ken Giami ameeleza jinsi Rais Kikwete alivyochaguliwa kwa kishindo na wasomaji na wadau wengine wa Jarida hiyo kutokana na mafanikio yake katika uendeshaji na utawala bora wa Tanzania pamoja na mafanikio yake katika ustawi wa kiuchumi wa wananchi wa Tanzania wakati wa kipindi chake cha uongozi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
9 Aprili, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Membe: Hakuna maendeleo bila kushirikiana na sekta binafsi
Tanzania itaendelea kufanya jitihada kubwa na kwa hakika itakufa ikijaribu kuimarisha ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kama njia bora zaidi ya kuleta na kudumisha maendeleo endelevu ya kiuchumi nchini.
Aidha, Tanzania imesisitiza kuwa nchi za Afrika ni lazima ziendelee kutafuta namna ya kumaliza migogoro na mizozo yake ya kisiasa na kijeshi, kama msingi mkuu wa kutafuta na kupata maendeleo endelevu na ya kudumu ya kiuchumi kwa watu wake.
Hayo yameelezwa usiku wa leo, Jumatano, Aprili 9, 2014 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, wakati alipopokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 ambalo ametunikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., Mheshimiwa Membe amesema kuwa uzoefu wa Tanzania unaonyesha kuwa ushirikiano na uhusiano wa karibu kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ni msingi mkuu wa maendeleo ya nchi yoyote, ikiwamo Tanzania.
Amesema kuwa ushirikiano kati ya sekta hizo mbili umeleta manufaa na faida kubwa katika maendeleo ya Tanzania katika sekta za huduma za jamii na katika huduma za kiuchumi.
Waziri Membe amesema kuwa mifano ya mafanikio ya ushirikiano kati ya sekta hizo mbili ni wazi katika sekta kama ya elimu ambako Tanzania imefanikiwa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika usajili wa watoto kuingia shule na katika kuleta usawa katika watoto wa kike na kiume wanaoandikishwa kuanza shule kwa sababu Sekta Binafsi inasaidiana na Sekta ya Umma katika kuwekeza katika elimu.
“Kwa sababu ya ushirikiano huo wa karibu, sisi katika Serikali, tumefanya uamuzi kwamba mikopo ya wanafunzi isitolewe kwa wananchi wanaosoma kwenye vyuo vya umma pekee bali kwa wanafunzi wote wakiwamo wale wanaosoma katika vyuo vikuu binafsi. Hivyo, uhusiano kati ya sekta hizo mbili umeleta mafanikio makubwa katika sekta hiyo ya elimu,” amesema Mheshimiwa Membe.
Waziri Membe pia ametaja mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maeneo mengine ya maendeleo kwa sababu ya ushirikiano huo yakiwemo ya utunzaji wa mazingira, usambazaji wa huduma ya maji safi na salama, uboreshaji wa huduma za afya, maendeleo ya miundombinu hasa ya barabara na uboreshaji wa huduma katika kilimo.
Aidha, Waziri Membe amezungumzia hatua zinazochukuliwa na Serikali kuleta uwazi na usimamizi mzuri katika sekta ya gesi hata kabla ya Tanzania haijaanza kuchimba gesi akisisitiza kuwa bila uwazi sekta hiyo itagubikwa na utawala duni, rushwa na usimamizi dhaifu.
Kuhusu umuhimu wa amani kama sharti la Maendeleo ya Afrika, Waziri Membe amesema kuwa uzoefu wa Afrika na dunia nzima unaonyesha kuwa hakuna maendeleo yoyote na hasa ya kiuchumi bila kuwepo na amani.
Wakati huo huo, Waziri Membe amekutana na kufanya mazungumzo na Gavana wa Jimbo la Maryland, Mheshimiwa Mark O’Malley katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, Marekani.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Membe amemwalika Gavana O’Malley kutembelea Tanzania na kutumia nafasi yake kuhakikisha kuwa Jimbo la Maryland linaanzisha ushirikiano na mkoa mmojawapo wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
9 Aprili, 2014
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wazee wa Baraza la Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wamempongeza na kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ufafanuzi na kuunga mkono hotuba yake kwa Bunge la Katiba aliyoitoa tarehe 21 Machi, Mjini Dodoma.
Wazee hao wamefika Ikulu ya Dar es Salaam leo jioni , tarehe 9 Aprili,2014 na kuelezea furaha yao kwa Rais Kikwete.
“Wazee wote tunakushukuru, tumefurahishwa sana na Hotuba ile kwani umetoa ufafanuzi wa mambo mengi, kwa hivyo tumefika hapa kukufahamisha kuwa tumefurahishwa sana, tuko pamoja nawe kwa hali ya aina yeyote “ wamesema na kumueleza Rais kuwa wanayo mabaraza katika Wilaya, Mikoa, Kata na hata Mashina.
“Tumefurahi sana , hotuba hii imetufungua na tumefunguka hivyo tunakuunga mkono na tuko nawe katika hoja ya Serikali mbili kama ilivyo katika Chama Chetu.” Wazee hao waliongozwa na Bi. Khadija Jabir Mohammed ambaye ndiye kiongozi wao na Bw. Waziri Mbwana Ali Katibu wa Wazee. Wazee wengine waliofika Ikulu ni Bw. Juma Ame Juma, Bw. Mohammed Khamis Haji, Bw. Juma Khamis Khamis na Bw. Tabib Omar Makungu. Wengine ni Alchui Khamis Alchui, Bw. Abdallah Rashid Abdalla na Bw. Haji Machano Haji.
Rais amewashukuru Wazee hao kwa kumtia moyo kwa kufika Ikulu kuelezea hisia zao ambapo Rais amewaeleza Wazee hao kuwa takwimu zote alizotumia katika Hotuba yake amezitoa kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Warioba na kwamba hata maswali aliyokuwa akiuliza, alikuwa akiyauliza kwa nia ya kuyatafutia majibu na majawabu ya misingi kama yalivyoandikwa kwenye rasimu ya Tume.
“Takwimu zote nimetoa kwenye taarifa ya Tume, Maswali niliyouliza nimeyatoa kwenye taarifa, pia kuna mambo ya uandishi ambayo hayakuwa yameandikwa sawasawa hivyo nina wajibu wa kutoa tahadhari kwa wajumbe wa tume ili kuwa na uhakika wa dhana na tafsiri zilizomo kwenye rasimu ya Tume” Rais Kikwete amefafanua zaidi.
Mwisho!
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 .
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo itatolewa jioni ya kesho, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, ambaye tayari amewasili mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya utawala bora.
Jarida hilo linasema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora chini ya uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sera na mifumo ya uchumi.
Jarida hilo linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la wasomaji wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za mawasiliano za jarida hilo.
Linasema Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila shaka yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake. Na ushahidi uko kila mahali – ameweza kusimamia uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asili mia saba kwa miaka yote ya uongozi wake.”
Sherehe za kesho, miongoni mwa mambo mengine, zitaliwezesha Jarida hilo kutangaza mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Kikwete kwa Jumuia ya Kimataifa, ikiwa ni pamoja na Jumuia ya Kimataifa ya Kibiashara, wanadiplomasia na taasisi nyingine zenye ushawishi mkubwa katika medani za kimataifa na zenye makao yake katika Jiji la Washington na maeneo ya jirani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
8 Aprili, 2014