Hotuba
- Feb 06, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA, UKUMBI WA MIKUTANO WA KIMATA...
Soma zaidiHotuba
Ndugu Peter Mziray, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Ndugu Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa;
Ndugu Wenyeviti wa Vyama vya Siasa;
Ndugu Wajumbe wa Baraza la Vyama Siasa;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Utangulizi
Nakushukuru ndugu Peter Mziray, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na viongozi wenzako kwa kunishirikisha kwenye kikao hiki maalum cha Baraza na kwa maelezo mazuri ya utangulizi. Tutayatafakari ya kufanyika yafanyike. Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa busara wa kuzungumzia nafasi ya vyama vya siasa katika Bunge Maalum la kutunga Katiba. Jambo hili ni muhimu kwa uhai, maendeleo na ustawi wa nchi yetu na watu wake. Mmeonesha moyo wa uzalendo na ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu
Tangu Baraza hili la vyama vya siasa lizinduliwe mwezi Mei, 2010, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu shughuli zake na jinsi linavyofanya kazi. Kwa kweli nimeridhishwa na hatua mliyopiga. Ndiyo maana mliponiita sikusita kuja. Nawaahidi kuwa nitaendelea kufanya hivyo katika siku zijazo ili mradi tu nafasi iwepo.
Serikali Kuimarisha Uwanja wa Siasa
Ndugu Wajumbe;
Mtakubaliana nami kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kujenga na kuendeleza demokrasia ya vyama vingi na ushindani wa kisiasa. Kuwepo kwa vyama 21 vyenye usajili wa kudumu vilivyo huru kuendesha shughuli zao na Baraza la Vyama vya Siasa ni kielelezo tosha cha ukweli huu. Wazo la kuwa na Baraza hili liliibuka wakati wa mchakato wa kutatua mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar uliozuka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000. Kamati ya Pamoja ya Mwafaka iliyokuwa na wajumbe kutoka CCM na CUF iliundwa ili kutafuta suluhu ya mgogoro ule. Mojawapo ya mambo ambayo Kamati hiyo ilipendekeza ni kuundwa kwa chombo kitachowezesha viongozi wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadili masuala ya kisiasa ili kuepusha migogoro ya kisiasa.
Baada ya Baraza kuundwa, mwaka 2009, Serikali ikaona haja ya kupanua wigo wa ushiriki na kukifanya chombo hiki kuendesha kazi zake kwa mujibu wa Sheria. Matokeo yake Wenyeviti wa vyama vyote vya siasa wakajumuishwa kufuatia marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa yaliyofanyika mwaka 2009. Baraza la Vyama vya Siasa likatambulika kisheria na majukumu yake kuorodheshwa katika Sheria husika. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikapewa jukumu la kuratibu na kugharimia shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa.
Mabibi na Mabwana;
Nimeamua kueleza chimbuko la Baraza la Vyama vya Siasa, ili Wajumbe wa Baraza na watu wote wanaonisikiliza wajue kwamba Baraza hili limetokeaje kuwepo na lina nafasi gani katika jamii na siasa za Tanzania. Ni chombo kilichotokana na mafunzo tuliyopata katika migogoro ya kisiasa huko nyuma. Baraza hili ndicho chombo ambacho kikitumiwa vizuri na vyama vya siasa matatizo na malalamiko yao na masuala mengine ya kisiasa yana mahali pa kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi. Aidha, ni jukwaa linalotoa fursa kwa vyama vya siasa kuzungumzia masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa na kukubaliana kuhusu nini vyama vyenyewe vifanye au vishauri yafanyike na mamlaka husika. Ushauri unaotolewa unawasilishwa Serikalini kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo ndio Sekretarieti ya Baraza hili.
Hakuna chombo kingine zaidi ya Baraza hili kinachowakutanisha viongozi wote wa kitaifa wa vyama vya siasa kujadili masuala ya kisiasa yenye maslahi ya kitaifa. Kwa kuzingatia nafasi yake na majukumu ya Baraza hili, nawasihi viongozi wenzangu hususan Wenyeviti wa vyama vya siasa tulipe uzito na tulitumie ipasavyo. Nawaomba tuwe tunashiriki kwa ukamilifu katika vikao na shughuli za Baraza. Natambua kwamba kwa vile Baraza linajumuisha vyama vyote hata Mwenyekiti wa Chama kidogo anaweza kuongoza Baraza inaweza kutokupendeza kwa vyama vikubwa. Si jambo la ajabu wala si jambo baya ndiyo maana na faida ya demokrasia. Wale wanaotoka vyama vikubwa wasichukie, wakifanya hivyo wanakiuka kanuni moja ya msingi ya uongozi nayo ni “kiongozi mzuri pia huwa ni mfuasi mzuri”. Hata mdogo analo la maana la kuwanufaisha wote wadogo na wakubwa. Naamini Baraza likitumika vizuri litatunufaisha wote: vyama vyote, nchi yetu na wananchi wote.
Mimi na Mheshimiwa Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa nafasi zetu hatushiriki moja kwa moja katika mikutano ya Baraza hili. Pamoja na hilo bado tunalitambua, tunalithamini na tunayachukulia maamuzi ya Baraza hili kwa uzito unaostahili. Ndiyo maana Chama changu kimemteua kiongozi mzito anayenifuata kwa madaraka yaani Makamu Mwenyekiti, ndugu Philip Mangula kuwa Mjumbe wa Baraza. Kutoka Zanzibar tumemteua Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Vuai Ali Vuai.
Kwa kweli ingependeza sana kama viongozi wa vyama vingine nao wangetoa uzito unaostahili kwa Baraza hili. Natoa rai kwa viongozi wakuu wa vyama vya siasa, hususan wenyeviti kwa wao wenyewe kuwa Wajumbe wa Baraza hili adhimu ili kulipa uzito na hadhi stahiki. Baraza hili lilianzishwa kwa ajili yetu, kujadili masuala ya kuimarisha na kuboresha uwanja wa siasa nchini na kuweka mazingira na uwanja ulio huru na sawa. Kusudi la kutaka wenyeviti wote wa kitaifa wa vyama vya siasa wawe wajumbe wa Baraza ni kuhakikisha kuwa Baraza linakuwa na uwakilishi wa watu wenye mamlaka kamili kufanya maamuzi kwa niaba ya vyama vyao. Ni muhimu sote tuone hoja hiyo na kuitumia fursa inayotolewa na Baraza. Napenda kuwahakikishia ndugu wajumbe kuwa Serikali itaendelea kusikiliza na kuheshimu ushauri wa Baraza hili kwani ni chombo muhimu sana kwa mustakabali wa ustawi wa siasa na maendeleo ya nchi yetu.
Ndugu Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Jambo lingine muhimu tunaloendelea kufanya ni kuimarisha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili iweze kumudu vyema majukumu yake. Mwaka jana (2013) niliidhinisha muundo mpya wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wenye vitengo vingi kuliko ilivyokuwa kabla ya hapo. Muundo mpya unaoongozwa na watumishi wenye taaluma nyingine mbalimbali badala ya kutegemea wanasheria peke yake. Changamoto zinaongezeka na mazingira ya kufanya kazi yanabadilika, hivyo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itafaidika na kuwa na watumishi wa kada nyingine kama vile wa sosholojia, sayansi ya siasa na kadhalika.
Ili kuhakikisha ufanisi zaidi, Serikali imedhamiria kuongeza bajeti ya ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika mwaka ujao wa fedha. Bila ya kufanya hivyo tutakuwa hatukufanya kitu cha maana. Ofisi haitaweza kutimiza wajibu wake. Kwa kweli itakuwa ni kuwaonea kuwadai wafanye zaidi.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Nimeelezwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa, jambo moja linaloikwaza ofisi yake ili waweze kutimiza ipasavyo jukumu lao la kuwa mlezi wa vyama vya siasa nchini ni mfumo wa Sheria ya Vyama vya Siasa. Nimeelezwa kuwa Sheria hii imeweka adhabu moja tu ambayo ni kukifuta Chama kinachofanya makosa yaliyoainishwa katika Sheria badala ya kutafuta taratibu za kurekebisha. Kwa maoni yake Sheria haitoi nafasi ya kutosha ya kuvilea vyama vikue, vikomae na vijiepushe na migogoro ya kisiasa ndani ya vyama na ndani ya jamii. Kwa sababu hiyo, inamfanya Msajili aonekane kuwa ni mtu wa kutoa vitisho vya kufungia vyama. Kwa maoni yake hatuna budi kuangalia sheria hiyo upya ili iweze kushughulikia changamoto hizo.
Naiona hoja ya Msajili na nampongeza sana kwa kuliona jambo hilo. Leteni mapendekezo yenu tuyatazame ili hatua zipasazo zichukuliwe. Pamoja na hayo usisubiri sheria. Mlezi hutoa ushauri na kusaidia kupata ufumbuzi wa mambo mbalimbali yanayowatatiza viongozi na wanachama wa vyama vya siasa. Usisite kututembelea mara kwa mara kuzungumza nasi na kutushauri unavyoona inafaa. Itasaidia sana wakati tunasubiri Sheria kufanyiwa marekebisho. Nafurahi kwamba kazi hiyo unaifanya. Tafadhali endelea. Pia usisite kutuita wote au mmoja mmoja unapoona inafaa kufanya hivyo.
Nimeambiwa mchakato wa kupitia upya Sheria hiyo na ile ya Gharama za Uchaguzi umeanzishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Bila ya shaka marekebisho ya Sheria ya Vyama yatasaidia kuboresha uratibu wa shughuli za kisiasa hapa nchini bila kuingilia uhuru wa vyama vya siasa. Vilevile marekebisho ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi yatasaidia kuhakikisha wananchi wetu wanachagua viongozi kwa kuzingatia uwezo wao, mwenendo na ubora wa sera za vyama vyao na si uwezo wao wa kifedha. Nimefurahi na nimefarijika sana na hatua hiyo. Ongezeni kasi ya kukamilisha zoezi hilo.
Ndugu Washiriki;
Naomba kurudia tena kusema kuwa tunafanya hayo yote ili kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na ushindani wa kisiasa nchini. Kwetu sisi Serikalini, vyama vya siasa ni wadau muhimu wa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Kwa maana hiyo tunapenda vyama viwe na uwezo wa kutekeleza wajibu huo. Kinyume chake, yaani vyama vinaweza kugeuka na kuwa wakala wa kurudisha nyuma maendeleo. Hii haikubaliki, itashangaza na kusikitisha.
Mada ya Kikao
Ndugu Mwenyekiti;
Kama wote mnavyofahamu, nchi yetu ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Hatua inayofuatia sasa ni Bunge Maalum la Katiba kukutana na kujadili Rasimu ya Pili na kuamua ipasavyo. Kazi ya uteuzi wa Wajumbe 201 wa kuungana na Wabunge na Wawakilishi katika Bunge hilo imekamilika na kesho watatangazwa. Ilikuwa kazi ngumu sana. Watu wengi wazuri walipendekezwa hivyo hujui umchague nani na umuache nani. Kwa vile hatuwezi kuwapeleka wote basi tumewateua hao 201 na kuwaacha maelfu ya watu wazuri. Kama wote wanaofaa wangechukuliwa nchi ingenufaika sana. Lakini hatuwezi kuwa na Bunge la watu 5,000 hata China haifanyi hivyo. Ilikuwa hapana budi kuchagua baadhi yao tu. Kwa ajili hiyo nawasihi wale wote wasioteuliwa wasisononeke. Hawajapungukiwa sifa ila nafasi hazitoshi.
Ndugu Wajumbe;
Wiki iliyopita nilitembelea ukumbi wa Bunge Dodoma na kujionea mwenyewe maandalizi ya Ukumbi na vifaa unavyoendelea. Mambo yanakwenda vizuri. Nimeelezwa kuwa ifikapo tarehe 10 Februari, 2014 kila kitu kitakuwa tayari na majaribio kufanywa ya vifaa vilivyofungwa. Nimeona tujipe wiki moja baada ya hapo ili tuweze kurekebisha panapostahili. Kwa ajili hiyo nimekubaliana na Rais wa Zanzibar niangalie uwezekano wa kuliitisha Bunge Maalum tarehe 18 Februari, 2014. Tutaitangaza rasmi siku hiyo kupitia gazeti la Serikali.
Bunge la Katiba ndilo lenye mamlaka ya kutunga Katiba mpya ya nchi yetu. Hatua zote zilizopita ni za kutoa mapendekezo jukumu ambalo Tume ya Mabadiliko ya Katiba imelikamilisha vyema. Ipo Rasimu ya Katiba itakayofikishwa kwenye Bunge Maalum kujadiliwa na kufanyiwa uamuzi. Ingekuwa Bunge la kawaida au Baraza la Wawakilishi, Rasimu ya Katiba ndiyo Muswada wa Sheria utakaofikishwa Bungeni na kwenye Baraza.
Wajumbe wa Bunge hilo watambue kuwa wana dhamana isiyokuwa na mfano wake kwa nchi yetu na Watanzania wenzao kwa jumla. Wanalo jukumu la kuwapatia Katiba nzuri itakayodumu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo. Katiba itakayoimarisha Muungano badala ya kuudhoofisha. Katiba itakayodumisha umoja, amani na utulivu nchini badala ya kuvuruga. Vilevile Katiba itakayoweka mazingira mazuri ya kisiasa, kijamii na kiuchumi na kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi yetu na ustawi wa watu wake kwa miaka mingi ijayo. Ili haya yafanyike ni vyema Wajumbe wajue vyema kinachopendekezwa, wapambanue kinachofaa na kisichofaa, na kubwa zaidi, watangulize maslahi ya taifa mbele kuliko maslahi yao binafsi au ya makundi yao.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Mabibi na Mabwana;
Vyama vya siasa vina nafasi ya pekee katika majadiliano ya Bunge Maalum la Katiba na katika mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya. Mafanikio ya mchakato huu yatategemea sana kauli, mwenendo na matendo ya vyama vya siasa. Ukweli ni kwamba vitendo na kauli za viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa ndivyo vitakavyojenga au kubomoa, na ndivyo vitakavyowezesha au kukwamisha mchakato huu.
Mimi nataka vyama vijenge na kuwezesha mchakato ufanikiwe na Katiba mpya ipatikane kwa wakati tunaoutarajia sote. Yaani tufanye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2015 tukiwa na Katiba Mpya. Mimi naamini kwa dhati ya moyo wangu kuwa vyama vya siasa vikiamua Katiba ipatikane, itapatikana. Hivyo basi, kama vyama vya siasa vitaamua kishirikiana kwa dhati, na kwa nia njema tutapata Katiba mpya bila kelele wala mikwaruzo. Kama vyama vya siasa vitatambua kuwa tunatengeneza jambo la kutunufaisha wote, yaani nchi yetu na watu wake na siyo maslahi binafsi ya vyama vyao itakuwa hatua kubwa ya mwanzo ya kufanya kazi ya Bunge kuwa rahisi. Pia kama vyama vitakubali kuongozwa kwa nguvu ya hoja alizotoa Mjumbe na siyo Mjumbe anatokea Chama gani au kundi gani, tutapata Katiba yenye maslahi kwa taifa letu. Tutapata Katiba itakayoridhiwa na wananchi bila ya taabu.
Ninaposema hayo sina maana kuwa vyama vya siasa au Wajumbe wanaotokana na vyama wasiende Bungeni na maoni yao au na misimamo ya vyama vyao. La hasha! Nikifiria hivyo sitakuwa mkweli kwangu mwenyewe. Nitakuwa najidanganya. Ninachosema ni kwamba, pamoja na kuwa na maoni, mwongozo na misimamo ya vyama vyenu, lazima muwe na unyumbufu wa mawazo kwa kiasi fulani ili mpate nafasi ya kusikiliza hoja za wengine zinazotofautiana na zenu, kuzivumilia na kuzikubali pale ambapo kuna mantiki. Kwa lugha ya Kiingereza natoa wito wa “flexibility”. Muungwana hukubali mawazo bora na yenye ukweli ya watu wengine. Hata wengine nao wanaweza kuwa na mawazo bora kuliko yako. Muungwana ni yule anaekiri ukweli huo na yuko tayari kupokea mawazo bora ya watu wengine hata kama watu hao hawapendi. Kama tutakwenda kwenye Bunge na azimio la kupinga kila wazo litakalosemwa na mtu fulani, hatutafikia kupata Katiba mpya. Haitawezekana.
Ndugu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Ndugu Wajumbe;
Mtakubaliana nami kuwa Baraza hili na hasa ninyi viongozi mliokusanyika hapa leo mnayo dhamana na jukumu la kipekee la kuipatia nchi yetu Katiba nzuri yenye maslahi kwa nchi yetu na inayojali maslahi ya watu na kukubalika na watu wote. Katiba ambayo itakapotangazwa watu waseme naam, hii ni Katiba inayojali maslahi ya nchi zetu mbili zilizoungana na kuwa nchi moja miaka 50 iliyopita. Katiba inayojali maslahi ya raia wa Tanzania ndani ya Muungano na ule upande wa Muungano anakoishi au unakotoka kwa asili yake au historia yake.
Ni kwa kutambua umuhimu huu wa vyama vya siasa ndiyo maana nilitoa wito kwa vyama vya siasa kukutana na kuzungumza miongoni mwenu. Ningependa mzungumze kuhusu namna bora ya kujadili rasimu ili mwishowe tupate Katiba nzuri. Ningependa mzungumze jinsi vyama vya siasa vitakavyoshirikiana hasa kutafuta ufumbuzi wakati majadiliano yanapokuwa magumu kwa baadhi ya mambo.
Si vyema mkadhani jawabu ni kushindana mpaka mwenye nguvu ashinde. Mnaweza kushindwa wote. Na mkishindwa, mjue sote tumeshindwa na nchi imekwama. Msikubali kuifikisha nchi hapo. Tuzidi kumuomba Mola atusaidie tusifike hapo. Lakini, Mwenyezi Mungu husaidia wanaojisaidia. Na sisi tutengeneze namna bora ya kujisaidia ili Mungu akitia mkono wake mambo yanajipa. Lililoonekana kuwa zito linakuwa jepesi kama kanda la usufi.
Ndugu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa;
Nawaamini nyote mliopo hapa mnaweza kutengeneza mfumo huo na taratibu hizo. Sina majibu wala maelekezo ya mfumo huo ni upi. Nimekuja kutoa rai. Nimekuja kutoa maombi. Majibu mnayo ninyi. Mimi nasubiri jibu jema kama wanavyosubiri Watanzania wengine. Nawaomba myatafakari ninayosema na myape uzito unaostahili.
Mwisho
Narudia kuwashukuru Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kunialika kuja kuongea na viongozi wa vyama vya siasa kupitia Baraza hili. Ni matumaini yangu kuwa, miaka ishirini na mbili tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe tena hapa nchini kwetu mwaka 1992, vyama vya siasa vimekomaa na vinaelewa nafasi na umuhimu wake katika jamii. Hivyo basi, tutegemee matokeo mema katika mkutano wenu huu wa kihistoria na mchakato utakaozaa matunda mema katika Bunge Maalum la Katiba.
Kabla ya kumaliza napenda kurudia kuwahakikishia kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza tutaendeleza ushirikiano wetu na Baraza. Tuko tayari kuitikia wito wa kuja kuongea nanyi wakati wowote. Baada ya kuyasema maneno yangu mengi, nawatakia kila heri katika Mkutano wenu.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
- Feb 03, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA SHEREHE YA KUADHIMISHA SIKU YA SHERIA NCHINI TAREHE 3 FEBRUARI, 20...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania;
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania;
Waheshimiwa Majaji Wakuu Wastaafu;
Mheshimiwa Dkt. Asha-Rose Migiro, Waziri wa Katiba
na Sheria;
Mheshimiwa Angella Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria;
Waheshimiwa Majaji wa Rufani;
Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Kiongozi na Majaji
wa Mahakama Kuu;
Waheshimiwa Mabalozi mliopo;
Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania;
Mahakimu na Watumishi wa Mahakama;
Wageni Waalikwa Mabibi na Mabwana;
Utangulizi
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Nakushukuru sana Mheshimiwa Jaji Mkuu kwa kunialika kwa mara nyingine tena kuja kujumuika nanyi kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini na ya Mahakama kuanza kazi mwaka huu. Ni jambo la busara kuwa siku hii inaadhimishwa kila mwaka. Inatupa fursa nzuri sisi tusio wanasheria kujifunza masuala mengi yahusuyo sheria na utoaji haki nchini.
Naomba na mimi niungane na wenzangu walionitangulia kukupongeza na kukushukuru Mheshimiwa Jaji Mkuu, Waheshimiwa Majaji, Mahakimu na watumishi wote wa Mahakama kwa kazi nzuri mliyofanya mwaka jana. Nami nawatakia mafanikio mema na utendaji mzuri zaidi katika mwaka huu wa 2014.
Kaulimbiu ya Mwaka Huu
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Kama ilivyo kawaida yenu, kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inayosema “Utendaji haki kwa wakati: Umuhimu wa Ushiriki wa Wadau” imebeba ujumbe mzito na muhimu kwa wadau wa utoaji haki nchini. Kwa jumla inatukumbusha kuwa ili haki iwe na maana, ni lazima ipatikane kwa wakati. Msemo wenu maarufu wa “Justice delayed is justice denied” unaelezea kwa ufasaha dhana hii. Ni ukweli usiopingika kwamba ili haki ipatikane kwa wakati, ushiriki kwa ukamilifu wa wadau wote ni jambo la lazima. Wadau hao ni pamoja na Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Polisi, TAKUKURU, Mawakili, Serikali na wengineo.
Endapo mmoja wa wadau hao atashindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo, haki ya mtu au watu itachelewa kupatikana au itadhulumiwa. Hali hii inatokana na ule ukweli kwamba kila mdau anao wajibu maalum ambao hana budi kuutimiza. Ufanisi wa mmoja unategemea sana utendaji wa mwingine. Ni kama mwili wa binadamu ulivyo, kila kiungo kina nafasi yake, kimoja kisipofanya kazi vizuri siha ya mwili hodhoofika. Ndiyo hivyo ilivyo pia kwa mfumo wa utoaji haki. Mahakama ambapo ni kilele katika mtandao au mfumo wa utoaji haki haikamati wahalifu, haipelelezi mazingira ya utendaji kosa, haitayarishi wala haiendeshi mashtaka. Hivyo basi, kazi ya Polisi, TAKUKURU na Mkurugenzi wa Mashtaka husaidia sana kuharakisha utoaji haki, Mahakama ina uharaka wa kusikiliza kesi hasa pale ambapo upelelezi umekamilika mapema na waendesha mashtaka wako tayari, na pia, uharaka wa upatikanaji wa nakala ya hukumu ili mtu aweze kukata rufaa kwa wakati.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Masuala mengi kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu umeyaeleza vizuri pamoja na wazungumzaji waliotangulia. Jambo kubwa na muhimu ambalo limejitokeza ni kuwa ushiriki na ushirikiano wa wadau ni muhimu sana katika utoaji haki kwa wakati. Mahakama ni kilele katika mfumo wa utoaji haki nchini. Lakini, Mahakama haipelelezi, haifikishi wahalifu mahakamani, haiendeshi mashtaka. Hasikilizi mashauri na hutoa kutoa uamuzi kuhusu upande upi una haki. Hivyo, wale wapelelezi na waendesha mashtaka na wanaotetea wasipofanya kazi yao ipasavyo haki huchelewa. Hii ina maana kuwa Polisi wahakikishe wahalifu wanakamatwa, upelelezi unafanyika kwa makini na kesi zao zinapelekwa kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ili zipelekwe Mahakamani.
Hivyo kwa TAKUKURU nao wahakikishe kuwa upelelezi unafanywa vizuri ili shauri linapofikishwa Mahakamani halichelewi kwa sababu ya upelelezi kutokukamilika. Mkurugenzi wa Mashtaka nae ahakikishe shauri analolipeleka limeandaliwa vizuri ili lichukue muda mfupi kusikilizwa na kuamuliwa. Weledi na uadilifu wa Polisi, TAKUKURU na DPP ni mambo ya msingi sana. Hivyo hivyo, Mawakili nao wana nafasi yao. Naambiwa kuna wakati shauri huaihirishwa kwa sababu ya wakili wa utetezi kushindwa kufika Mahakamani. Ukiacha sababu ya kuumwa lakini wakati mwingine ni kwa sababu ya kuwa na kesi mahali pengine.
Nafasi ya Mahakama
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Ni ukweli usiopingika kuwa Mahakama inayo nafasi ya pekee katika mfumo wa kutoa haki nchini. Nakubaliana na wale wanaouita Mhimili huu wa dola kuwa ni “The temple of Justice” kutokana na ukweli kwamba watu wanapokuja Mahakamani wanategemea kutendewa haki. Hakuna mahali pengine pa kukimbilia kutafuta haki zaidi ya Mahakamani. Wanaweza wasijue sheria za vitabuni, lakini wakajua haki yao. Hivyo, Waheshimiwa Majaji, Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama mnayo dhamana na wajibu mkubwa wa kusimamia sheria kwa haki. Ili haki itolewe bila upendeleo wa aina yoyote ile.
Matarajio ya wananchi ni kuwa kesi zisicheleweshwe kusikilizwa na kuamuliwa. Pale ambapo upelelezi umekamilika na mashtaka yametayarishwa vizuri kuahirishwa kusikilizwa kwa kesi huzaa manung’uniko. Pale shauri linapoamuliwa kutolewa kwa nakala ya hukumu ili anayetaka kukata rufaa afanye hivyo ni jambo la muhimu. Kinyume chake watu wanakata tamaa na kuamua kuchukua njia za mkato ambazo madhara yake ni makubwa. Wanakuwa hawana mahali pengine pa kupeleka mashtaka yao. Ndiyo maana nakubaliana na kauli yako Mheshimiwa Jaji Mkuu kwamba tusiiache misingi ya haki ikamomonyoka katika jamii yetu mpaka ukafika wakati watu wakaamini kwamba bila kutumia jambia hakuna haki. Naomba muendelee na kazi nzuri muifanyayo ili muwe kimbilio la uhakika kwa yeyote ambaye anajiona haki yake inadhulumiwa.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Nimefarijika sana kusikia kwamba mmejiwekea utaratibu mzuri na misingi ya ushirikiano wa mawasiliano baina yenu na wadau wengine kwa ajili ya kuboresha utendaji wenu. Utaratibu huo utasaidia sana kuhakikisha upelelezi wa mashauri unakamilika haraka na haki inapatikana kwa wakati. Vilevile nawapongeza kwa kuelewa umuhimu wa kuhuisha sheria, kanuni na taratibu mara kwa mara ili kukidhi mahitaji ya wakati. Bila shaka hatua zote hizi zitasaidia sana kutatua changamoto ya siku nyingi ya ucheleweshwaji wa kesi.
Wajibu wa Serikali
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Napenda kukuhakikisha kuwa sisi Serikalini tutaendelea kutimiza wajibu wetu ili Mahakama na wadau wengine wa utoaji haki wafanye kazi ipasavyo. Kwanza tumechukua na tunaendelea kuchukua hatua kadhaa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali kufuatia tafiti na mapendekezo ya Tume zilizoundwa kuangalia mifumo yetu ya kutoa haki kwa lengo la kuiboresha. Kazi hiyo tunaendelea nayo. Tumeanza na kurekebisha sheria na mifumo ya utoaji haki na kuweza kutenganisha upelelezi na uendeshaji wa mashtaka.
Pili, tumeanza kuchukua hatua thabiti kuongeza bajeti ya Mahakama ili muweze kutimiza kwa ufanisi zaidi wajibu wenu. Mwaka huu wa fedha kwa mfano, tumetenga shilingi bilioni 86 kwenye Mfuko wa Mahakama na shilingi bilioni 42.7 kwa ajili ya maendeleo. Kiasi hiki ni kikubwa maradufu ukilinganisha na mwaka wa fedha uliopita ambapo zilitengwa shilingi bilioni 57 kwa shughuli zote. Pamoja na hatua hii muhimu tumejitahidi sana kuwezesha Mahakama kuongeza rasilimali watu, yaani Majaji Mahakimu na watumishi wengine. Idadi ya Majaji wa Rufani sasa imefikia 16 kutoka 9 waliokuwepo mwaka 2005, na wa Mahakama Kuu ni 69 kutoka 35 waliokuwepo mwaka 2005. Nilishakubali Majaji 20 wapya waajiriwe. Nileteeni mapendekezo niteue. Vilevile idadi ya Mahakimu imeongezeka zaidi na kufikia 672 na tayari kibali cha kuajiri wengine 300 kimeshapatikana. Hivi sasa mchakato wa ajira ya wahitimu wa sheria katika Mahakama za Mwanzo unaendelea.
Kufuatia mapendekezo ya Kamati za Jaji Mrosso na ya Jaji Lubuva, tumekamilisha mchakato wa kutenganisha shughuli za kutenda haki na utawala kwa kuanzisha nafasi ya Mtendaji Mkuu. Sasa hivi naambiwa pamekuwa na nafuu sana kwani mzigo waliokuwa nao Majaji kwenye masuala ya utawala haupo tena. Nasikitika kuwa idhini ya Muundo wa Mahakama umechelewa kuliko kawaida. Naahidi kuwa litakamilika wiki hii. Tumeendelea kuziongezea uwezo wa rasilimali fedha, vitendea kazi na nguvu kazi Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na TAKUKURU.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali nayo pia imefanyiwa marekebisho makubwa. Shughuli za Wizara zilizokuwa zimechanganyika na zile za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali sasa hivi zimetenganishwa. Wizara imebaki na jukumu lake la kusimamia sera na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inafanya shughuli za kisheria. Hatukuishia hapo. Tumefikia hatua nzuri ya kutenganisha shughuli za upelelezi na za kuendesha mashtaka. Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka imebaki na majukumu yake ya kusimamia mashtaka na Polisi, TAKUKURU na wengineo wanabaki na majukumu yao ya ukamataji wa wahalifu na upelelezi. Tunafanya yote haya kuboresha mifumo ya kutoa haki nchini.
Mwisho
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Mabadiliko yaliyofanyika yana lengo zuri la kuboresha taratibu zetu za kutoa haki nchini. Jambo kubwa ni mabadiliko kwa jamii na watendaji wenyewe. Watoaji haki ni lazima wajipime kwa matakwa na mahitaji yao. Endeleeni kutekeleza majukumu yenu mkielewa kwamba wananchi na jamii wanawategemea katika kuhakikisha kwamba haki inatolewa kwa wakati. Wadau wa utoaji haki muendelee kutimiza wajibu wenu wa kutatua migogoro, kuwapatanisha wananchi na kuwaadhibu wahalifu ili amani na utulivu nchini mwetu idumu. Watu wawe na maelewano na waishi bila wasiwasi.
Naomba kila mmoja wetu ashiriki kikamilifu kuhakikisha lengo letu linafikiwa. Kila mmoja wetu anayo nafasi yake, hili siyo jukumu la polisi peke yao, Mwanasheria Mkuu au Jaji Mkuu. Ni jukumu la wote. Basi mwaka huu tujitahidi kufanya vizuri zaidi, kila mtu afanye hivyo mahali alipo. Bila shaka haki itapatikana kwa wakati.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
- Jan 22, 2014
Hotuba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati ufunguzi wa kongamano la viongozi wa dini kuhusu matumizi ya rasilim...
Soma zaidiHotuba
Waheshimiwa Viongozi wa Dini;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa;
Ndugu Makatibu Wakuu;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo kujadili matumizi ya rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya nchi yetu. Kwa namna ya pekee nawashukuru viongozi wa dini kwa kunishirikisha kwenye Kongamano hili muhimu na la aina yake. Mmenipa heshima kubwa ambayo sikuitegemea. Asanteni sana.
Nawapongeza sana kwa uamuzi wenu wa busara wa kuandaa Kongamano hili. Mmedhihirisha kwa vitendo uhodari wenu wa kutekeleza jukumu lenu la msingi la kulea taifa letu kiroho na kushiriki kikamilifu katika masuala mengine muhimu yahusuyo maendeleo na ustawi wa Tanzania na watu wake. Ninyi ni wazalendo wa kweli. Ni matumaini yangu na ya Serikali ninayoingoza kuwa ubia wa aina hii utaimarishwa na kudumishwa kwa faida ya nchi yetu.
Najua mlianza kwa kukereketwa na athari za matumizi makubwa ya miti kwa matumizi ya nishati jambo ambalo linachangia sana kuharibika kwa mazingira duniani. Mmeishia kwenye Kongamano hili. Lina uwiano kabisa kwani tunakata miti kwa ajili ya kuni na mkaa. Tukitumia gesi itatoa huko. Ni dhamira yetu hiyo.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Kongamano hili linafanyika katika kipindi mwafaka kabisa, kipindi ambacho ugunduzi mkubwa wa gesi tayari umefanyika na dalili za kugunduliwa zaidi zipo. Kipindi ambacho hazina ya madini mbalimbali inazidi kugunduliwa na makampuni ya utafiti yanatupa moyo kuwa mambo huenda yakawa mazuri zaidi. Pia, ni kipindi ambacho rasilimali zetu za wanyamapori na misitu zinatishiwa kutoweka. Ni kipindi ambacho wakulima na wafugaji na wafugaji na wahifadhi wa misitu na wanyamapori wanashindania ardhi ya kufanyia shughuli zao. Sasa hivi ni kipindi mwafaka kabisa kukaa chini na kutafakari jinsi gani rasilimali hizi zinaweza kulindwa na kutumika kwa manufaa ya nchi yetu na watu wake wote zikiwanufaisha kule ambako rasilimali hizo zipo na hata kule ambako hazipo.
Ni ukweli usiopingika kuwa Mwenyezi Mungu ameijalia nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za asili. Ametujaalia ardhi kubwa yenye rutuba, madini ya aina mbalimbali, misitu na mbuga za wanyama wa kila aina, hali ya hewa nzuri, bahari, maziwa makubwa, mito mingi, watu wengi na kadhalika. Rasilimali hizi, kwa tabia yake, inatakiwa zitumiwe vizuri ili kuboresha hali na maisha ya Watanzania wote sawia na kwa miaka mingi na hata milele. Vinginevyo rasilimali hizi zinaweza kugeuka kuwa chanzo cha mifarakano, magomvi na mauaji. Zinaweza kuwa balaa na kuleta maangamizi nchini badala ya kuwa baraka na neema.
Mifano ipo ya nchi mbalimbali duniani zilizojikuta zina migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na kugombania utajiri wao wa rasilimali za asili. Watu wa nchi hizo wanajuta kuwa na rasilimali ambazo zimekuwa chanzo cha kuhatarisha amani, utulivu, usalama na hata uhai wao. Kwa hapa Tanzania tunashukuru Mungu rasilimali hazijageuka kuwa balaa na tunaomba hilo lisitokee. Tangu Tanganyika ipate uhuru na Zanzibar kufanya Mapinduzi Matukufu na hatimaye nchi zetu mbili kuungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali za awamu zote zimesimamia kwa makini rasilimali za nchi yetu ili ziwanufaishe Watanzania wote. Tumetunga sheria na sera mbalimbali kuhakikisha kuwa lengo letu hilo linatimia.
Hata hivyo, usimamizi wa sheria hizo na utekelezaji wa sera zetu nzuri umekuwa unakabiliwa na changamoto mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Mpaka hapa tulipofika ni umahiri wa viongozi wetu ndiyo uliotuwezesha kuzuia mambo yasiharibike na kugeuka kuwa matatizo makubwa. Tumefanikiwa kiasi chake ingawaje hatujaweza kuzuia kabisa matatizo yasitokee hapa na pale. Taarifa za kugombea rasilimali zimekuwa zinasikika na nyingine zikiwa zimesababisha watu kupoteza maisha, kujeruhiwa na mali kuharibiwa. Tutafanya nini kukomesha hali hiyo isijitokeze, ni jambo ambalo sisi kama taifa, yaani Serikali, wananchi na wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini hatuna, budi kulizungumza na kulipatia ufumbuzi.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Nimefarijika sana na uamuzi wenu wa kufanya mkutano huu kuzungumzia rasilimali ya mafuta na gesi. Juhudi za kutafuta mafuta na gesi imeanza tangu ukoloni, zikaendelea katika awamu zote baada ya Uhuru. Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) lilianzishwa mwaka 1969 kuongoza juhudi hizo na kusimamia sekta ya mafuta nchini kwa manufaa ya Watanzania wote. Hatujajaaliwa kupata mafuta mpaka sasa lakini tumefanikiwa kupata gesi. Ugunduzi wa kwanza wa gesi asilia ulifanyika Songosongo mwaka 1971 na baadae Msimbati, Mtwara mwaka 1982. Utafutaji na ugunduzi huo uligharimiwa na Serikali yetu na hivyo gesi hiyo ni mali ya Serikali. Baada ya ugunduzi huo makampuni binafsi yalipata shauku ya kutafuta mafuta na gesi nchini.
Mwaka 1980 ikatungwa Sheria ya Utafutaji wa Uzalishaji wa Mafuta kwa nia ya kuweka masharti na utaratibu wa makampuni kushiriki katika utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi nchini. Pia unatoa mwongozo wa mgawanyo wa mapato baina ya makampuni na Serikali. Sheria hiyo imeendelea kufanyiwa maboresho kwa nyakati mbalimbali kulingana na mahitaji ya wakati husika. Kuanzia mwaka 2007 shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia ziliongezeka kwa nguvu na kasi kubwa. Juhudi hizo zilizaa matunda mwaka 2010 kwa uvumbuzi wa kwanza wa gesi katika Bahari Kuu uliofanywa na Kampuni za Orphir na British Gas. Baada ya hapo ugunduzi umeendelea hadi kufikia futi za ujazo trilioni 46.5 za rasilimali ya gesi nchini mpaka sasa. Utafiti unaendelea na matumaini ya kupata gesi zaidi yapo. Kufuatia ugunduzi huo, Tanzania sasa ni moja ya nchi zimazohesabiwa kuwa na gesi nyingi duniani na ni nchi inayovutia wawekezaji wengi katika sekta ya gesi. Kwa sababu hiyo, tukaamua kuifanyia mapitio Sheria ya Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi. Mwaka 2013 tumetunga Sera ya Gesi na kurekebisha masharti ya Mkataba wa Kugawana Mapato yatokanayo na gesi (Production Sharing Agreement) na kuongeza mgao wa Serikali.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Sera ya Gesi Asilia iliyopitishwa mwezi Oktoba, mwaka jana (2013) imeeleza wazi, tena kwa lugha nyepesi, kuwa gesi ya Tanzania ni mali ya Watanzania wote na itatumika kwa manufaa ya Watanzania wote – wa kizazi hiki na kijacho. Katika matumizi ya gesi, kipaumbele kitakuwa matumizi ya ndani. Msingi wa hoja yetu ni ule ukweli kwamba ukiuza nje gesi yote, unapata mapato peke yake lakini unakosa faida nyinginezo. Ukiitumia ndani unapata mapato na faida nyingine nyingi, kwa mfano, uzalishaji wa umeme, matumizi ya majumbani, kwenye magari na viwandani kuzalisha bidhaa mbalimbali. Hivyo basi mnapoitumia ndani gesi inakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu.
Vilevile tupo katika mchakato wa kuandaa sera ya kuwashirikisha zaidi Watanzania (Local Content Policy) ili wanufaike zaidi na rasilimali yao ya gesi. Kwa sasa nimewaagiza TPDC wajiandae kushiriki katika utafutaji wa gesi, uzalishaji wake mpaka inapofika sokoni. Wasiwe wagawaji vitalu tu pekee. Katika sera hiyo mpya pia tunaangalia shughuli zinazoweza kufanywa na Watanzania ili tuone njia bora ya kuwawezesha kushiriki. Kwa sasa tunadhani wanaweza kushiriki kwa urahisi katika utoaji wa huduma kwa kampuni zinazofanya utafiti na uzalishaji wa gesi na mafuta. Wapo walioanza na wanafaidika. Nia yetu ni kuona idadi yao inaongezeka.
Mabibi na Mabwana;
Tumeanza pia mchakato wa kuiboresha TPDC ishiriki katika uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi kwa niaba ya Watanzania. Katika utaratibu huo, baadaye TPDC itauza hisa zake kwenye Soko la Mitaji ili Watanzania washiriki moja ka moja katika kumiliki rasilimali hii muhimu.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Mambo yote hayo yanafanyika ili kuhakikisha masilahi ya taifa yanalindwa na Watanzania wote wananufaika na rasilimali zao kwa usawa. Changamoto kubwa tunayoiona kuhusu ushiriki wa Watanzania kwenye utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi ni uwezo mdogo wa fedha, utaalamu na teknolojia tulionao. Fedha zinazohitajika kwenye shughuli ya utafutaji mafuta na gesi, kwa mfano, ni nyingi mno na Watanzania wenzetu hawanazo na hakuna uhakika wa benki iliyo tayari kumkopesha mtu asiyekuwa nacho.
Namna nyingine ni kuwapa maeneo ili wao watafute wabia wawekeze. Lakini, mnapokuwa mnasheria inayoshirikisha ubia baina ya Serikali na mwekezaji, kuamua kuacha Serikali ili badala yake apewe Mtanzania binafsi si uamuzi rahisi sana kuufanya. Mtu binafsi ananufaika mwenyewe wakati Serikali inanufaisha wengi. Ninachokiona nafuu kufanya ni kutumia mwanya wa ushiriki wa TPDC ili tuone baadhi ya hisa ziuzwe kwa Watanzania. Hapa kunakuwa na ubia wa TPDC na wananchi upande mmoja na Serikali upande mwingine.
Jambo lingine tunalolifanya ni kuhakikisha kuwa rasilimali ya gesi inatumika vizuri, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazo vijavyo. Tutaanzisha mfuko maalum wa kuhifadhi mapato ya gesi na kuwekewa masharti ya matumizi yake. Tutatunga sheria maalum kwa ajili hiyo na tutafanya hivyo kwaka huu.
Mabibi na Mabwaba;
Kwa upande wa rasilimali ya madini mabadiliko makubwa ya kiuchumi yaliyoanza miaka 1980 katikati, Serikali ilijitoa katika uwekezaji na ikabaki kuwa mhamasishaji na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji. Kufuatia hali hiyo wawekezaji wengi walianza kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali pamoja na utafutaji na uchimbaji wa madini. Serikali ikaweka Sera (1997) na Sheria (1998) ya madini kusimamia sekta hiyo. Ni kweli mapato ya Serikali na fedha za kigeni ziliongezeka kutokana na uzalishaji wa madini. Lakini palikuwa na manung’uniko mengi kutoka kwa wananchi kuwa hawafaidiki sana na rasilimali zao.
Kamati mbalimbali ziliundwa kuangalia tatizo lipo wapi ili jawabu lake litafutwe. Nilipochaguliwa kuwa Rais wa nchi yetu mwaka 2005 niliyakuta manung’uniko hayo na kuamua tuyatafutie jawabu. Mwaka 2006 nikaunda Kamati ya Jaji Bomani ili ichambuwe mapungufu yaliyopo na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua. Matokeo ya taarifa ya Kamati ile ni Sera Mpya ya Madini (2009) na Sheria Mpya ya Madini (2010). Sera na Sheria hii inalenga kuongeza faida zaidi kwa Serikali na jamii, bila kuwasahau wale wanaozunguka migodi.
Faida hizo ni pamoja na kuhimiza kampuni za uchimbaji wa madini kufungamanisha uchumi kati ya sekta ya madini na nyingine. Vilevile tumewataka waongeze nafasi ya ajira kwa Watanzania na ununuzi wa huduma na bidhaa nchini. Aidha, tumeamua Serikali iwe inapata hisa katika migodi mikubwa itakayoanzishwa siku za usoni. Ndiyo maana tunaendelea kufanya mazungumzo na kampuni zitazochimba uranium na nickel. Hatujamaliza lakini tunakwenda vizuri.
Halikadhalika, Sheria na Sera vimeweka mkazo wa kuendeleza wachimbaji wadogo ambao ni Watanzania tu. Katika kutekeleza hilo, tumeanza kutenga maeneo kwa ajili yao. Changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa mitaji, vifaa na utaalamu. Kuhusu fedha, tumeanzisha mfuko wa kuwasaidia na mwaka huu wa fedha tumewatengea jumla ya shilingi bilioni 2.5. Vile vile tunakamilisha taratibu za kuanza kuwakodisha vifaa kupitia ofisi zetu za madini za Kanda.
Jambo lingine kubwa ambalo tunajiandaa kulifanya ili kunufaisha wananchi na nchi yetu ni kutunga Sheria itakayohakikisha kuwa madini mengi yanayochimbwa nchini yanaongezewa thamani hapahapa nchini. Hatua hii itachangia sana kuongeza mapato na fursa ya ajira kwa watu wetu.
Nduvu Viongozi wa Dini;
Nimeyasema haya yote kuwaonesha kuwa Serikali haina mchezo katika usimamizi wa rasilimali zetu za asili. Tunafanya hayo kwa vile tunafahamu kuwa zinaweza kutuletea maendeleo ya haraka. Lakini pia zinaweza kusababisha nchi yetu kuingia kwenye dimbwi la migogoro inayotokana na rasilimali. Yote mawili yanaweza kutokea kutegemea tutasimamiaje na kuzitumiaje rasilimali zetu.
Jambo la muhimu ni kusaidiana kuelimisha jamii ya Watanzania namna tulivyojipanga kusimamia rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini. Waelewe kuwa utajiri huu ni mali yao na hivyo ni haki yao kunufaika nao. Wafahamu kuwa ni wajibu wao kulinda na kuzitunza rasilimali hizo ili zisipotee. Ninyi mnayo dhamana ya kuelimisha jamii waelewe nia hiyo njema ya Serikali. Pia napenda kusema kuwa siyo kweli kwamba Serikali haijali rasilimali za nchi au haitaki Watanzania wafaidike nazo; siyo kweli eti Serikali inapendelea wawekezaji wageni kuliko wazawa na hakuna mkoa au eneo linapuuzwa au kubaguliwa. Mimi na Serikali ninayoiongoza tutakua watu wa mwisho kupuuza wazawa na kupendelea wageni au kupuuza watu wa maeneo ambako rasilimali zinapatikana au hazijapatikana.
Ndugu Viongozi wa Dini;
Naomba muendelee kutekeleza jukumu lenu la msingi la kulea taifa kiroho. Mhimize waumini wenu wawe waadilifu na wazalendo. Waache kujihusisha na vitendo viovu vya wizi, ubadhilifu, matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Mkifanikiwa hilo, rasilimali zetu zitakuwa salama. Vile vile muendelee kuhubiri upendo miongoni mwenu, miongoni mwa waumini wenu na miongoni mwa watu wote. Watu wakumbushwe kuwa sisi wote ni viumbe wa Mungu na mbele yake sisi wote ni ndugu na inabidi kuheshimiana na kuvumiliana kwa tofauti zetu. Tukifaulu kwenye hili nchi yetu itabaki salama daima milele.
Nafahamu kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanafanya vitendo vya kuhujumu rasilimali zetu. Wapo wanaoingia mikataba isiyozingatia maslahi ya taifa katika uvunaji wa rasilimali zetu. Wapo wengine wanaokula njama na wawekezaji ili Serikali ipunjwe mapato yake. Watu wa aina hiyo wapo katika jamii ye yote ile na sisi kuwa nao si ajabu. Napenda mfahamu kuwa Serikali inapinga vitendo vya aina yoyote vya kuhujumu rasilimali zetu. Ndiyo maana watu wa aina hiyo wanapobainika, wanachukuliwa hatua na vyombo vinavyohusika. Ninyi pia msichoke kuwafichua, wapo miongoni mwa waumini wenu.
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza, napenda kumshukuru Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo na timu yake Wizarani kwa kushirikiana na viongozi wa dini katika jambo hili muhimu. Naamini hatua hii ya kuwapa taarifa sahihi viongozi wa dini kuhusu matumizi ya rasilimali zetu hususan gesi na madini itasaidia kuongeza uelewa wa waumini wenu na wananchi kwa jumla. Watafahamu fursa zilizopo na jinsi ya kuzitumia ili wafaidike nazo. Nakushukuru pia kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali katika sekta ya nishati na madini. Kazi yenu nzuri inaonekana na sisi wote ni mashahidi.
Mwisho, nawashukuru viongozi wa dini kwa kunishirikisha kwenye Kongamano lenu. Naamini mkitoka hapa mtakuwa mabalozi wazuri wa kueneza ujumbe kuwa rasilimali za Watanzania zipo kwenye mikono salama. Baada ya kusema hayo, napenda kutamka kuwa Kongamano la Viongozi wa Dini kujadili matumizi ya rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya nchi yetu limefunguliwa rasmi. Nawatakia kila la heri na mafanikio katika mwaka huu wa 2014.
Asanteni sana kwa kunisikiliza
- Jan 05, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI AKIPOKEA MAANDAMANO YA VIJANA WA CCM WALIOTEMBEA KUADHIMISHA MIAK...
Soma zaidiHotuba
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Mama Mwanamwema Shein;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Bi Asha;
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM;
Ndugu Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar;
Ndugu Sadifa Juma Khamis; Mwenyekiti wa UVCCM Taifa;
Bi Mboni Mhita, Makamu Mwenyekiti Taifa;
Ndugu Sixtus Mapunda, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa;
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC);
Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wabunge, Wawakilishi na Viongozi wa Ngazi Mbalimbali wa Chama na Serikali;
Mabibi na Mabwana;
Ndugu Wananchi;
Nawapongeza sana viongozi wa Umoja wa Vijana kwa uamuzi wenu wa kuandaa matembezi haya ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Nawashukuru kwa heshima kubwa mliyonipa ya kuja kujumuika nanyi kwenye kuhitimisha matembezi haya.
Lazima nikiri kuwa nimefurahi na kupata faraja kubwa kuona vijana wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika matembezi haya. Tumeelezwa hapa kuwa mlianza 600 mnamaliza 1,800. Wengine wamejiunga njiani. Huu ni uthibitisho tosha kuwa UVCCM iko hai na CCM inapendwa na itadumu tofauti na dhana ya wale wasioitakia mema. Katu dua zao hazitafanikiwa. Maandamano haya ni kielelezo thabiti kuwa Jumuiya yetu na vijana wetu wanatambua wajibu wao wa kuenzi na kusimamia mambo ya msingi yahusuyo taifa letu. Miongoni mwa mambo hayo ni Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 na Muungano wa Zanzibar na Tanganyika wa Aprili, 1964. Naomba muendelee na moyo huo wa kuhamasishana na kuelimishana kuhusu tunu za taifa ambazo zimeachwa kama urithi na viongozi na waasisi wa nchi zetu tatu za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao pia ndiyo waasisi wa vyama vya ASP, TANU na CCM.
Nimefurahishwa na kuunga mkono kaulimbiu ya matembezi haya inayosema “Vijana Tusirudi Nyuma Katika Kuyalinda na Kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964”. Kaulimbiu hii ni mwafaka kabisa. Hakika msirudi nyuma na wala hakuna sababu ya kufanya hivyo. Daima mbele, nyuma mwiko. Ni usaliti. Kaulimbiu hii inawakumbusha vijana jukumu lenu la msingi la kutetea malengo na madhumuni ya Mapinduzi. Pili inawafundisha kuwa umoja na mshikamano ni jambo la msingi kwani hiyo ndiyo siri ya ushindi waliopata mashujaa wetu waliokuwa na mapanga na marungu. Umoja na nguvu. Umoja ni Ushindi. Na, nguvu ya mnyonge ni umoja. Ishikilieni kamba ya umoja.
Nilipendezwa sana na taarifa kuwa wakati wa matembezi yenu watu mbalimbali wakiwemo wazee walipata nafasi ya kuzungumza nanyi kuwaelimisha kuhusu historia ya Zanzibar kabla, wakati na baada ya Mapinduzi. Bila ya shaka mmepata kuifahamu vizuri historia ya Zanzibar kabla ya mapinduzi na kwa nini waasisi walilazimika kufanya uamuzi wa kuchukua silaha kupambana na utawala uliokuwapo.
Hatuna budi kuwapongeza na kuwashukuru kwa dhati mashujaa wetu hao walioongozwa na kiongozi mkuu wa Mapinduzi Sheikh Abeid Amani Karume kwa moyo wao wa ujasiri, utayari wa kujitolea muhanga kwa faida ya wengine na upendo wao kwa nchi yao na watu wake. Walikubali kwa hiari yao wenyewe kuweka maisha yao rehani kwa ajili ya kuwatetea wanyonge waliokuwa wanadhulumiwa na kunyanyaswa katika nchi yao. Jukumu lenu vijana, ni kuiga moyo huo wa kujitolea. Mnatakiwa wakati wote muwe tayari kujitolea kwa ajili ya taifa na wananchi wake. Muwe tayari kujitolea kwa ajili ya Chama cha Mapinduzi. Muwe tayari kuenzi na kulinda ukombozi huo uliopatikana kwa jasho jingi na damu za wana Mapinduzi.
Kwenye Mapinduzi mnaenzi na kutetea malengo na madhumuni yake ya msingi ambayo ni kuwapatia wananchi wa Zanzibar uhuru wa kweli. Ule wa Desemba 10, 1963 ulikuwa wa bandia. Ulikuwa “feki”. Waingereza walifanya kiini macho. Walifanya danganya toto ambayo Mapinduzi iliiondoa ghiliba ile. Kuwakomboa watu waliokuwa wanabaguliwa na kukandamizwa pamoja na kuwaondoa wale waliokuwa wanabagua na kuwakandamiza wenzao. Ndiyo maana baada ya Mapinduzi ASP iliunda Serikali na kujenga nchi isyokuwa na ubaguzi wa rangi, kabila, dini wala eneo. Waasisi wa Mapinduzi walipinga ubaguzi wa aina zote. Naomba vijana hili mlifahamu vizuri na kulizingatia ipasavyo. Mapinduzi hayakufanywa kwa ajili ya kundi fulani teule. Jasho na damu ya mashujaa iliyomwagika ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wote wa Zanzibar. Kudumisha msingi huo ni jambo ambalo vijana mnao wajibu wa kuutambua vizuri na kuutekeleza. Hamtegemewi kufanya kinyume chake, si sera ya ASP na wala siyo sera ya TANU na CCM iliyobeba ya TANU na ASP.
Jambo la tatu ni Umoja na mshikamano miongoni mwa Waafrika na watu wanaoonewa na kudhulumiwa kote duniani ilikuwa sera ya msingi ya Afro Shirazi Party. Sera hiyo ilitekelezwa kwa vitendo na waasisi wa ASP na Mapinduzi kwa maana kwamba Chama cha ya Afro Shirazi Party ni Chama kilichotokana na kuungana kwa vyama vya African Association na Shirazi Association. Waasisi wetu ni watu waliotambua nguvu ya umoja. Walikuwa mstari wa mbele kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao na vyama rafiki na nchi rafiki. Kwa ajili hiyo kulikuwa na uhusiano wa karibu baina ya African Association ya Zanzibar na African Association ya Tanganyika ambayo mwaka 1954 ikawa TANU. Aidha, kulikuwa na uhusiano wa karibu kati ya ASP na TANU kabla, wakati na baada ya Mapinduzi. Hivyo haikushangaza walipounganisha nchi zao huru na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 1964.
Vilevile, watu wa nchi zetu mbili ni ndugu wa damu hivyo kuziunganisha nchi zao ni sawa na kuziunganisha familia zilizojikuta zinatenganishwa na mazingira maalum ya kihistoria hasa kutawaliwa na watu wawili mbalimbali. Waliamua kuyasahihisha mambo hayo kwa kuunganisha nchi zao. Vilevile inatupasa tukumbuke kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ndiyo yalikuwa chachu ya Muungano wa nchi zetu mbili. Huwezi kuzungumzia Muungano bila Mapinduzi. Kama Mapinduzi yasingefanyika Muungano usingekuwepo. Muungano ni mtoto wa Mapinduzi.
Ndugu Wananchi;
Ili kuimarisha umoja, udugu na mshikamamo ulioanzishwa Aprili 26, 1964, vyama tawala vya ASP na TANU viliungana tarehe 5 Februari, 1977. Hatua hiyo iliimarisha Muungano wetu na kuupandisha hadhi kufikia daraja la juu zaidi la utangamano. Ni vyema vijana mkajua ukweli huu ili mtambue wajibu wa kuulinda Muungano wetu udumu. Pia mtambue wajibu wenu wa kuimarisha Chama cha Mapinduzi kama kiungo cha kudumisha na kuendeleza Muungano wetu. Kuna watu hawaupendi Muungano na hawaiombei mema CCM. Ni wajibu wenu kuhakikisha kuwa Muungano unadumu na CCM inazidi kuimarika na inaendelea kuongoza nchi yetu.
Ndugu Mwenyekiti wa Vijana;
Ndugu Vijana;
Ni jukumu la msingi la vijana kuhakikisha kuwa sera ya Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 yanatekelezwa, kuenziwa na kulindwa kwa hali na mali, mchana na usiku iwe jua iwe mvua. Pia vijana mnao wajibu wa kuhakikisha Muungano wa Zanzibar na Tanganyika wa Aprili, 1964 unadumu na kustawi pamoja na uhuru wa taifa letu, umoja wa watu wake na mshikamano wa kitaifa. Mkifanya hayo vijana mtakuwa mnawaenzi kwa vitendo waasisi wa taifa letu na viongozi waliofuatia. Mtaonesha kweli mmekomaa na mko tayari kurithi uongozi wa nchi yetu na kusimamia tunu za taifa letu. Tutaondoka madarakani na hata duniani nyoyo zetu zikiwa baridi na raha tukisema hakika nchi iko kwenye mikono salama. Hayo ndiyo matamanio yetu sisi wazazi wenu na viongozi tuliopo kwenye uongozi hivi sasa.
Ndugu Vijana;
Jambo lingine muhimu kwa vijana kutambua na kufanya ni wajibu wao kushiriki kwa ukamilifu katika maendeleo yao wenyewe, kisiasa, kiuchumi na jamii yao wenyewe wanayoishi na nchi yao. Kuinua hali za maisha ya watu wa Zanzibar ni shabaha kuu ya Mapinduzi ambayo tarehe 12 Januari 2014 tutadhimisha miaka 50 ya uhai wake. Ni jambo la kusikitisha kama kijana atashindwa kutimiza wajibu wake huo. Ni jambo linalofadhaisha kwa kijana kuwa mvivu, mlevi na mhalifu. Ni hasara kwake, kwa jamii yake na nchi yetu. Vijana ndiyo nguvu kazi ya leo na kesho ya kuliletea taifa maendeleo na ndiyo urithi wa familia, jamii na taifa. Tunapenda muwe wachapakazi hodari na warithi wema ili mlihakikishie taifa maendeleo endelevu na ustawi. Vijana mlinde Mapinduzi, Muungano na mafanikio ya Zanzibar na Tanzania.
Ndugu Mwenyekiti;
Ndugu Viongozi na Ndugu Vijana;
Mwaka huu pia tunasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Katika uhai wa Muungano wetu ambao hauna mfano wake Afrika tumepata mafanikio mengi. Pia kumekuwepo na changamoto kadhaa ambazo kwa nyakati tofauti hatua zimechukuliwa kuzipatia ufumbuzi. Hata hivyo, kumekuwapo changamoto zilizohusishwa na Katiba ambazo marekebisho yaliyokuwa yanafanywa yalionekana kutokuyamaliza. Kwa kutambua hayo niliamua kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya sasa kwa nia ya kuihuisha. Tupate Katiba itakayosaidia kuondoa changamoto zilizopo za Muungano wetu ili mambo yaende vizuri na Muungano wetu ustawi na kudumu kwa miaka 50 ijayo na kuendelea bila vikwazo.
Kama mjuavyo, kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar niliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tume hiyo imekamilisha kazi yake na kutoa mapendekezo yake. Kazi iliyo mbele yetu sasa Watanzania ni kuisoma Rasimu hiyo na kutoa mawazo yetu ya kuwasaidia Wajumbe wa Bunge Maalum katika kujadili na kuamua kuhusu vipengele mbalimbali vya Rasimu ya Katiba. Ni matumaini yangu kuwa vijana mtachangamkia fursa hiyo na kutoa maoni yenu.
Napenda kulisisitiza hili la watu kutoa maoni kwa sababu baadhi ya watu wanadhani kuwa kazi ya Katiba imekamilika baada ya Rasimu ya pili. La hasha! Tume imetoa mapendekezo ambayo yanatakiwa kujadiliwa na kuamuliwa ipasavyo na Bunge la Katiba. Bunge hilo lina mamlaka ya kuamua inavyoona inafaa kwa kifungu cho chote. Itumieni vizuri fursa hii kutoa maoni yenu ili tupate Katiba itakayotupatia Muungano imara na nchi ya kidemokrasia inayozingatia na kuheshimu haki za binadamu. Katiba itupatie nchi iliyo salama, tulivu na yenye kupata maendeleo shirikishi na kunufaisha watu wote. Vijana toeni maoni bila ya hofu. Nguvu mnazo, akili mnazo na sababu mnazo. Sisi tutaendelea kuwashirikisha na kuwajengea uwezo ili mtoe mchango wenu.
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kurudia kuwapongeza tena vijana wote walioshiriki kwenye matembezi ya kilometa 340 kuenzi Mapinduzi Matukufu yaliyotokea miaka 50 iliyopita. Kwa namna ya pekee nawashukuru wote waliochangia kwa hali na mali kufanikisha matembezi haya. Wapo wenzetu wengi waliotoa misaada mbalimbali kwa vijana wetu. Sina neno zuri la kuwashukuru zaidi ya kusema asanteni sana.
Nawatakia nyote heri ya mwaka mpya. Asanteni sana kwa kunisikiliza.
- Dec 06, 2013
Closing remarks by his excellency Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania, at the Africa-France conference on new economic mod...
Soma zaidiHotuba
Your Excellency President Hollande;
Excellencies Fellow Leaders From Africa;
Mr. Pierre Moscovici, French Minister of Economy and Finance;
Ladies and Gentlemen:
I thank you Mr. President and your esteemed government for conceiving the idea of holding this meeting on a New Economic Model between Africa and France. I congratulate Minister Moscovici, heartily for organizing this meeting so well. I also thank you for affording us the opportunity to speak at this landmark event.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
Africa has got all what it takes to become a prosperous continent. The prevalent poverty is a contradiction in terms. It can be made history and the continent can become the new economic powerhouse of this planet.
Africa is well endowed with natural resources such as land, minerals, oil and gas, forest and marine based resources. These are critical resources for growth and development to happen. Fortunately, most of these resources are yet to be fully utilized which means the future prospects for Africa are good.
Africa has 60 percent of the world’s uncultivated arable land. On the average many countries of Sub-Saharan Africa get good rainfall despite the stresses and strains being caused by climate change from time to time. Moreover, there are sizeable surface and ground water resources for irrigation. And, with the permissive climate for agriculture, the potential for Africa to become a dependable grain basket of this world is huge.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
Eleven African countries, rank among the top ten sources for at least one major mineral in the world. Africa has 10 percent of the world’s reserves of oil. The ongoing exploration activities across Africa are bound to increase more oil and gas resources which together with wind and solar sources of energy can produce a lot of electricity for own use and export. My country Tanzania has been added on to the map as discoveries of gas have been made and several companies are continuing with exploration.
Ladies and Gentlemen;
People are another important resource that Africa has in abundance. Africa’s population is estimated to be 1.033 billion roughly 15 percent of the world’s population. There are two things worth noting about Africa’s population. First, is that Africa has a very young population, two-third of which is below the age of 25. This means there is a huge reservoir of energetic workforce and there are prospects for further growth of Africa’s population. Second, with expansion of education at all levels, the size of the educated workforce is increasing and the middle class is growing. Therefore, Africa is a dynamic source of skilled and semi skilled labor force and a growing market. On the other hand, through regional integration the African markets are being consolidated and better defined.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
Fortunately, also, in most African countries economic fundamentals are right because of pursuing sound economic policies. As a result, most countries have strong macro-economic performance, making Africa’s future economic prospects to be very promising indeed. The economies of many African countries are growing at rates of around 5 percent and above. IMF forecast shows that 7 African countries will be among 10 fastest growing economies in the world during 2011 - 2015. Because of improved macro-economic environment as well as business and investment climate, foreign direct investment flows to Africa have registered significant increase in the last decade. For example, between the year 2000 and 2010 FDIs to Africa increased from US$ 27 billion to US$ 126 billion. But this is far too small. Africa needs and can absolve much more than this amount. Africa can absolve 10 times this amount and still leave a lot of potential untapped.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
Democracy is taking roots as the multiparty system has become the norm rather than the exception for over two decade now. There are regular periodic elections being held in all countries. The good thing is the elections are now better organized and the people get the opportunity to elect leaders of their choice. Governance has improved tremendously. There is greater awareness and strong commitment to observe human rights and deal with corruption and other social vices.
The security situation on the continent, has improved significantly. There are by far, fewer conflicts raging in Africa, now than they were two decades or a decade ago. And, what is even more encouraging is the fact that most conflicts are managed and resolved by Africans themselves through mechanisms and initiatives of the African Union and Regional Economic Groupings. Africa’s political and governance landscape has changed for the better and things look more promising in future.
Excellencies,
Ladies and Gentlemen;
Africa needs partnership with France and other countries both in the developed and developing nations to exploit its potential. Africa needs partners with capital, technology, know-how and market to transform Africa’s potential into goods and services to increase the wealth of our nations and our people. That is why we find this meeting to be quite opportune indeed. The 800 captains of industry gathered here are the very people we are looking for. They are the appropriate answer to the longstanding question about a new model for addressing poverty and development challenges facing Africa. A model which underscores the fact that Official Development Assistance alone is not enough. Indeed, ODA has been useful in helping our nations build capacity to deal with the teething challenges impeding growth and development. We still need ODA for capacity building in areas such as education, infrastructure, social and economic services etc. We appreciate the fact that, ODA needs to be combined with investments in the productive and service sectors to make the comprehensive difference we all desire.
In this context therefore, the New Economic Model being proposed should hinge on increased investment and trade without undermining the role of ODA, where necessary. This way African nations will build own capacity and become less dependent on ODA. In other words, under the envisaged model, investment and trade have to be viewed as sustainable ways of generating needed investment resources which can make poor countries achieve growth in a more sustainable manner than being predominantly dependent on ODA.
In this regard, Africa invites FDI in the form of private investment, joint venture, or public-private partnership in infrastructure, agriculture and agro-processing, manufacturing, ICT, petrochemical industries and other potential areas deemed as potential. Africa has a huge market, a growing middle class and a rising human capital base.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
France and Africa relationship has to fit in the emerging global trend marked by increasing global investment and trade inter-linkages. This calls for the need to focus more on economic and trade relationship while a certain levels of financial and technical support is maintained.
The benefits, however, are not automatic given different levels of economic and technological development. We need to take deliberate policy and administrative measures that would create conducive environment for mutual benefit. Indeed issues of market access and preferential treatment of products from Africa is essential.
Furthermore, Excellencies, our governments must encourage and support private sector to invest in each other’s country. Fortunately, this is already happening in all African nations. Besides that there are policies and frameworks in place to promote and protect private investment throughout the African continent, Tanzania included. There is no doubt that there is a lot of business potential in Africa and African governments are committed to work with the France to utilize that potentials for our mutual benefit.
Ladies and Gentlemen;
In the envisaged economic model between Africa and France, we expect France to play an important role in supporting infrastructure and human resource development in Africa, which is key to unlocking supply constraints. Africa has not been able to utilize various preferential trade opportunities offered by European Union such as “Everything But Arms” partly because of weak supply side capacity. We expect France to also support human development efforts and regional integration, both of which are key in increasing Africa’s capacity to manage the economy and expand trade and output. Let me reiterate that we in Africa are ready to work with government of France and French private sector in a win-win arrangement for mutual benefit.
Ladies and Gentlemen;
Let me conclude by once again thanking President Hollande and the Government of France for organizing this important conference which has afforded us the opportunity to exchange views on how best we can improve our economic relations in a win-win- manner. I would like to reiterate that, Africa has all that is required to make her an economic power house of the 21st Century. There are abundant resources that are yet to be exploited and the political – economic environment is permissive. Our governments and people are ready to work in partnership with France, other developed countries and international private sector like the captains of industry and business that are part of this audience. Africa is ready to do business with you to develop Africa’s potential for our mutual benefit. In the process Africa will cease to be a poor and basket case and become not only a prosperous continent but the new emerging economic power house of this century.
Thank you
- Nov 08, 2013
Hotuba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyotoa Bungeni kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, 7 Novemba, 2013, Dodo...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu;
Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri;
Mheshimiwa Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni;
Waheshimiwa Wabunge;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kukubali ombi langu na kutenga muda wenu ili niweze kuzungumza na Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuhusu masuala muhimu kwa uhai, ustawi na maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Mheshimiwa Spika;
Nimeambiwa kuwa taarifa ilipotolewa kuwa ninaomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge, kumekuwepo na dhana mbalimbali. Wapo waliodhani kuwa nakuja kuzungumzia mchakato wa kuunda Katiba mpya na hasa matukio ya wiki chache zilizopita. Wapo waliodhani nakuja kuzungumzia “Operesheni Tokomeza”. Tena wapo waliokwenda mbali na kufikiria kuwa nakuja kuwakaripia Waheshimiwa Wabunge waliotoa maoni yao kuelezea kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni hii muhimu. Na wapo pia waliodhani ninakuja kuzungumzia ushiriki wa majeshi yetu ya Tanzania katika Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa nchini Kongo.
Mheshimiwa Spika;
Hayo si makusudio yangu. Kinachonileta mbele ya Bunge lako Tukufu ni kuzungumzia Jumuiya ya Afrika Mashariki na mustakabali wa Tanzania katika Jumuiya hiyo. Lakini, kwa sababu ya umuhimu wa masuala hayo niliyoyataja na rai niliyopewa kuwa niyasemee japo kidogo. Nimeona ni vyema nifanye hivyo.
Mheshimiwa Spika;
Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, napenda kusema kuwa tumefikia hatua nzuri katika utekelezaji wake. Kama mjuavyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekamilisha, kwa mafanikio, hatua ya mwanzo ya kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu Katiba wanayoitaka. Pia walishatoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba na kukamilisha mchakato wa Mabaraza ya Katiba. Kinachosubiriwa kwa hamu na sisi wote, ni Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 15 Desemba 2013 au kabla ya hapo.
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa Bunge lako Tukufu, tunategemea kupata mambo mawili kutoka kwenu yatakayowezesha mchakato kutekelezwa vizuri katika hatua zinazofuata. Jambo la kwanza ni kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni na pili kufanyika kwa marekebisho ya nyongeza ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu Bunge Maalum ili kuboresha utekelezaji wake. Baada ya Bunge kukamilisha kazi yake hiyo itafuatia uteuzi wa Wajumbe wa Bunge Maalum ili kazi ya kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba ifanyike na kutupatia Rasimu ya Mwisho. Rasimu ambayo ikikubaliwa na wananchi katika Kura ya Maoni itakayofanyika wakati wo wote mwakani, tutakuwa tumepata Katiba Mpya. Hivi sasa katika Serikali tunaendelea kufanya tafakuri na tunachukua hatua za kuwezesha Bunge Maalum na Kura ya Maoni kufanyika kwa mafanikio.
Operesheni Tokomeza
Mheshimiwa Spika;
Napenda kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuwa sikukasirishwa na maoni yao kuhusu madai ya kuwepo kasoro katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Shabaha ya Operesheni hii ni kuokoa maliasili za misitu na wanyamapori dhidi ya uvunaji haramu ambao umefikia kiwango kinachotishia kutoweka kwa raslimali hizo. Kwa kweli hali inatisha. Miti inakwisha na ndovu na faru wanaangamia.
Mheshimiwa Spika;
Wakati, tunapata Uhuru Tanzania ilikuwa na ndovu waliokadiriwa kuwa takribani 350,000. Lakini, kwa sababu ya ujangili uliokithiri katika miaka ya 1970 na 1980 ilipofika mwaka1989 kulikuwa na ndovu wapatao 55,000 tu. Ilipofikia hali hiyo Serikali ikaanzisha Operesheni Uhai iliyohusisha Jeshi la Ulinzi na kuongozwa na Meja Jenerali John Walden (ambaye sasa ni marehemu) kuendesha mapambano dhidi ya majangili. Kutokana na hatua hiyo na uamuzi wa Shirika linalosimamia biashara ya wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka (CITES) kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu duniani, idadi ya ndovu nchini iliongezeka na kufikia 110,000 mwaka 2009.
Tumewaomba Fankfurt Zoological Society ambao ni wabia wetu katika uhifadhi wa wanyama pori kwa miaka mingi wafanye sensa maalum ya ndovu katika Hifadhi ya Selous na kote nchini ili tujue hali halisi ikoje. Kazi hiyo inaendelea hivi sasa.
Mheshimiwa Spika;
Baada ya mwaka 2009 kumezuka wimbi jipya, tena la nguvu kubwa, la kuua ndovu na faru nchini na kwingineko katika Bara la Afrika ambako wanyama hao wapo. Idadi kubwa ya meno ya ndovu yaliyokamatwa na yanaoendelea kukamatwa nchini na kwingineko duniani inathibitisha ukweli huo. Kwa mfano, kati ya mwaka 2010 na Septemba, 2013, hapa nchini, kwa jitihada zetu vipande 3,899 vya pembe za ndovu vyenye uzito wa kilo 11,212 na vipande 22 vya pembe za ndovu zilizochakatwa zenye uzito wa kilo 3,978vilikamatwa. Aidha, katika kipindi hicho vipande 4,692 vya pembe za ndovu vilivyotokea Tanzania vyenye uzito wa kilo 17,797vilikamatwa nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika;
Kama nilivyokwisha sema hapo awali matatizo ya kuuawa kwa wingi kwa ndovu na faru lipo pia katika nchi nyingine Afrika zenye wanyama hao. Nchi za Gabon, Kenya, Afrika ya Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uganda, Zimbabwe, Zambia na nyinginezo nazo zinakabiliwa na matatizo kama yetu. Tatizo limekuwa kubwa kiasi cha kuifanya Jumuiya ya Kimataifa kushtuka na kuamua kuingilia kati kwa namna mbili. Kwanza kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa ndovu na faru katika nchi zenye wanyama hao. Na, pili, kuchukua hatua thabiti kudhibiti biashara ya meno ya ndovu duniani. Ni ukweli ulio wazi kuwa kama hakutakuwepo na wanunuzi wa meno ya ndovu na faru hakuna ndovu au faru atakayeuawa.
Mheshimiwa Spika;
Kutokana na ukweli ulivyo uamuzi wetu wa kuendesha Operesheni Tokomeza ni sahihi kabisa. Manufaa yaliyopatikana baada ya Operesheni Uhai ya mwaka 1989 yanatupa imani kuwa na safari hii pia tutafanikiwa. Tusipochukua hatua kama hii sasa ni sawa na kuwapa kibali majangili waendelee kumaliza ndovu na faru nchini. Hakika wanyama hao watakwisha. Itakuwa ni aibu kubwa kwetu na historia itatuhukumu vibaya.
Mheshimiwa Spika;
Tumeyasikia maelezo ya Wabunge kuhusu kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Nawaahidi kuwa tutayafanyia kazi. Serikali imeahirisha kwa muda Operesheni hii ili kujipa muda wa kurekebisha kasoro hizo na kujipanga upya. Watendaji wasiokuwa waadilifu na wale wasiokuwa waaminifu wataondolewa. Halikadhalika, kasoro za kimfumo nazo zitasahihishwa ili tutakapoanza upya Operesheni itekelezwe kwa mafanikio yaliyokusudiwa.
Mheshimiwa Spika;
Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa kwa uchungu ni ukamataji wa mifugo iliyokutwa kwenye mapori ya hifadhi za wanyama na vitendo vibaya walivyofanyiwa wenye mifugo na mifugo yenyewe. Narudia kusisitiza kuwa taarifa zote hizo zitafanyiwa kazi na waliohusika watachukuliwa hatua zipasazo. Pamoja na hayo, napenda kuwakumbusha ninyi watunga sheria wetu kuwa sheria ya hifadhi za wanyamapori hairuhusu mifugo kuchungwa katika maeneo ya hifadhi.
Naomba tuwakumbushe wananchi tunaowaongoza wajiepushe na kufanya hivyo. Ni uvunjifu wa Sheria za nchi. Naomba pia, wananchi waelimishwe ili wajue kuwa wakifanya hivyo na kukutwa katika maeneo hayo na mifugo yao kuna adhabu iliyotamkwa kwenye sheria. Hivyo tusiwalaumu wala kuwaona maafisa wanyamapori kuwa ni watu wabaya. Wanatekeleza Sheria iliyotungwa na Bunge hili. Pale wanapotenda visivyo tuseme, watawajibishwa ipasavyo.
Jeshi la Umoja wa Mataifa Kongo
Mheshimiwa Spika;
Mapema mwaka huu (2013) Umoja wa Mataifa uliomba nchi yetu ichangie kikosi kimoja cha wanajeshi katika Brigedi Maalum iliyoundwa na Umoja huo kuongeza nguvu ya kudhibiti waasi Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lengo la msingi ni kuiwezesha nchi hiyo kupata amani ya kudumu ambayo imekosekana kwa muda mrefu kutokana na kuibuka kwa uasi mara kwa mara.
Mheshimiwa Spika;
Tulikubali, kwani hata kabla ya kuombwa na Umoja wa Mataifa tulishakubali maombi kama hayo yaliyotolewa kwenye Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu. Ni miezi saba (tangu Aprili) sasa tangu wanajeshi wetu waende Kongo na wamekuwa wanatekeleza majukumu yao vizuri tena kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Sifa hiyo kwa wanajeshi wetu imekuwa inatolewa na viongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa juu wa Jeshi la Umoja wa Mataifa Kongo (MONUSCO) na viongozi wa juu wa Serikali ya Kongo.
Mheshimiwa Spika;
Majeshi ya Umoja wa Mataifa hupewa majukumu na mamlaka ya namna mbili. Yapo yanayopewa jukumu la kulinda amani tu. Wanajeshi wake huwa hawapewi majukumu ya kimapigano na hata pale wanaposhambuliwa wanatakiwa kujihami tu. Kwa kawaida majeshi yenye jukumu hili hupelekwa mahali ambapo kumekuwepo na makubaliano ya kuacha mapigano. Wanapelekwa kusaidia kuona Mkataba unatekelezwa ipasavyo.
Aina ya pili ni ile ya majeshi yanayopelekwa mahali ambapo hakuna amani hivyo wanapewa jukumu la kuchukua hatua za kufanya amani ipatikane. Majeshi haya hupewa mamlaka ya kutumia nguvu ya kijeshi dhidi ya wanaosababisha amani ikosekane kama ni lazima kufanya hivyo. Maana yake ni kwamba wanayo ruhusa kuingia katika mapigano dhidi ya watu au vikundi vinavyovuruga amani. Tofauti na wenzao wa kundi la kwanza, wanajeshi wa kundi la pili wako kwenye hatari zaidi ya kupoteza maisha au kujeruhiwa kuliko wenzao ingawaje wapo wengi nao wameuawa na kujeruhiwa.
Mheshimiwa Spika;
Wanajeshi wetu wamekwenda Kongo chini ya utaratibu huu wa pili ambao unahusu kuingia kwenye mapigano dhidi ya waasi kama hapana budi kufanya hivyo. Wametekeleza majukumu yao vyema na kwa ujasiri mkubwa na weledi wa hali ya juu. Bahati mbaya tumepoteza vijana wetu watatu shupavu. Daima tutawakumbuka na tutawaenzi ipasavyo mashujaa wetu hawa. Tuzidi kuwaombea kwa Mola awape mapumziko mema. Ameen.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Spika, napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mafanikio ya kihistoria waliyoyapata hivi majuzi dhidi ya waasi wa M23. Tunamtakia yeye na wananchi wa Kongo kila la heri katika kazi ngumu iliyo mbele yao ya kujenga upya eneo hilo na kujenga mahusiano mapya miongoni mwa watu wa Kongo. Pia nawapongeza sana wanajeshi wa Brigedi Maalum ya Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri waliyoifanya iliyowezesha mafanikio kupatikana. Wanajeshi hao ni kutoka Afrika Kusini, Tanzania na Malawi wanaoongozwa na Brigedia Jenerali James Aloisi Mwakibolwa wa JWTZ.
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mheshimiwa Spika;
Kama nilivyosema awali, haya mambo matatu siyo hasa makusudio yangu nilipoomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge wetu. Nimeyachomekea tu kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii kwa wakati tulio nao. Jambo lililonileta hapa leo ni kuzungumzia hali ilivyo sasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na nafasi ya Tanzania katika Jumuiya hiyo. Nimeona nifanye hivyo kutokana na maswali mengi ambayo Watanzania wanajiuliza kufuatia matukio ya hivi karibuni ya viongozi wa nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani Uganda, Rwanda na Kenya kukutana bila ya ushiriki wa viongozi wa Tanzania na Burundi. Viongozi wenzangu hao wamefanya mikutano mitatu yaani: tarehe 24-25 Juni, 2013 mjini Entebbe, Uganda; tarehe 28 Agosti, 2013 mjini Mombasa, Kenya; na tarehe 28 Oktoba, 2013 mjini Kigali, Rwanda.
Mheshimiwa Spika;
Naomba kwanza niweke wazi jambo moja, kwamba nchi mbili wanachama au zaidi hazikatazwi kuwa na makubaliano ya ushirikiano katika kufanya mambo mbalimbali. Hata sisi Tanzania tunao ushirikiano wa namna hiyo na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Lakini, nchi wanachama zinatakiwa kufanya hivyo kwa yale mambo ambayo hayako kwenye shughuli za Jumuiya kwa maana kwamba hayamo katika Mkataba au Itifaki au hakuna uamuzi wa msingi uliofanywa na vikao au taasisi za Jumuiya kuyashughulikia. Pia, tunaweza kufanya hivyo kwa mambo ambayo yalishaamuliwa na Jumuiya yatekelezwe na ruhusa imetolewa kwa nchi yo yote iliyokuwa tayari kutekeleza ama peke yake au kwa kushirikiana na nchi nyingine.
Mheshimiwa Spika;
Kwa mujibu wa matamko ya pamoja (Communique) yaliyotolewa baada ya mikutano hiyo, kuna mambo yapatayomanane ya msingi yaliyoamuliwa kufanywa na nchi hizo kwa lengo la kuendeleza utengamano wa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
(1) Kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Kampala, Kigali na Bujumbura.
(2) Ujenzi wa Bomba la Mafuta la kutoka Kenya hadi Uganda na Sudani ya Kusini.
(3) Kujenga Kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda.
(4) Kuanzisha Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutekeleza vipengele vyote;
(5) Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki na kwamba itaundwa Kamati ya kuandaa rasimu ya Katiba ya Shirikisho.
(6) Kuharakisha uanzishwaji wa Visa ya pamoja ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Single East African Community Tourist Visa);
(7) Kuandaa utaratibu wa kutumia vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria katika nchi zao; na
(8) Kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme.
Mheshimiwa Spika;
Ni dhahiri kwamba orodha hiyo imechanganya mambo yale ambayo ni ya Jumuiya na yale yasiyo ya Jumuiya. Kwa mfano, mambo manne kati ya hayo manane hayamo kwenye masharti ya kutokufanyika bila ya kuihusisha au kupata ridhaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jambo la kwanza ni uzalishaji na usambazaji wa umeme. Ni kweli kwamba tunao mkakati wa kuwa na akiba ya pamoja ya nguvu ya umeme (East African Power Pool). Hata hivyo, bado jukumu la kuzalisha na kusambaza umeme huo limeachiwa nchi wanachama zenyewe kuamua. Lakini, hivi ndugu zetu hawa wanao muhali kuishirikisha Tanzania katika mpango ambao kimsingi umebuniwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo sote ni wanachama?
Jambo la pili, ni ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda. Hili si suala la Jumuiya bali la nchi ya Uganda kuamua yenyewe peke yake au kwa kushirikiana na wadau wengine. Rais Yoweri Museveni alituarifu mpango huo na sote tuliupokea kwa furaha kwamba sasa tutapata mafuta karibu na nyumbani. Alitualika kushiriki katika ujenzi wake sijui sasa amebadili mawazo kwamba Tanzania siyo muhimu.
Mheshimiwa Spika;
Jambo la tatu ni ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Kenya hadi Sudani ya Kusini na Uganda. Hili si jambo linalobanwa na masharti ya Jumuiya. Ni juu ya nchi hizi tatu kuamua kufanya ili kuwezesha mafuta yao kufika kwenye masoko. Hata hivyo, nimeambiwa kuwa Jumuiya imeshazungumzia bomba la mafuta kutoka Eldoret hadi Uganda, Rwanda na Burundi kuwa nalo lifike Tanzania kupitia upande wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania. Inaelekea mpango huo sasa haupo maana hatujausikia kutajwa katika ujenzi wa bomba hilo.
Mheshimiwa Spika;
Jambo la nne ni ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mombasa – Kampala – Kigali – Bujumbura. Hili nalo hatuna tatizo nalo. Si mradi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni jambo lililo chini ya mamlaka ya nchi wanachama husika. Hata hivyo, ni vyema kutambua ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara na usafiri wa anga na majini kuunganisha nchi za Afrika Mashariki ni miongoni mwa mambo ya kipaumbele cha juu yanayoshughulikiwa na Jumuiya yetu. Jumuiya hutengeneza mikakati ya pamoja na ndiyo maana tuna East African Railway Masterplan, tuna East African Road Network, na tuna Lake Victoria Development Programme kwa ziwa Victoria.
Kwa ajili hiyo, nilitegemea kuwa reli ya kutoka Mombasa hadi Kigali na Juba ingekuwa na tawi linalounganisha reli hiyo na reli ya Tanzania kama ilivyo reli ya Moshi – Voi – Taveta aliyotuachia mkoloni. Tulitegemea hivyo kwa minajili ya kuunganisha soko la Afrika Mashariki ambapo naamini Tanzania ni mdau muhimu. Lakini inaelekea kwa maoni ya wenzetu hivyo sivyo.
Mheshimiwa Spika;
Lazima nikiri kuwa inashangaza na tunayo kila sababu ya kuuliza kwa nini wenzetu wameamua kufanya hivi. Kumetokea nini toka tukutane pale Arusha Aprili 28, 2013 na Juni 24, 2013 walipokutana kuamua kufanya mambo ya kujenga na kuimarisha utengamano wa Afrika Mashariki kwa kubaguana, Haijawahi kuwa hivi kabla.
Mheshimiwa Spika;
Katika mambo manne yaliyosalia ambayo yaliamuliwa na kuwekewa utaratibu wake wa utekelezaji na Jumuiya ya Afrika Mashariki mawili hatuna maneno nayo. Mambo hayo ni matumizi ya vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria na Visa ya Pamoja ya Utalii kwani tuliamua kwa pamoja kuwa nchi wanachama zilizokuwa tayari waanze. Lakini, kwa upande wa kuanzishwa kwa Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha (Single Customs Territory) na Shirikisho la Afrika Mashariki tunadhani wenzetu wamekiuka uamuzi wetu wa pamoja.
Mheshimiwa Spika;
Katika Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu wa Nchi wanachama uliofanyika tarehe 28 Aprili, 2012 Jijini Arusha, tulipokea na kuridhia mapendekezo ya kuanzisha Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha (Single Customs Territory). Kwa mujibu wa mapendekezo hayo kila nchi mwanachama itasimamia shughuli zake za kiforodha na kukusanya mapato yake kama ilivyo sasa. Hata hivyo, kwa bidhaa zinazopitia nchi moja kwenda nchi nyingine mwanachama, ukaguzi na ukusanyaji wa mapato utafanyika katika kituo cha kwanza bidhaa hizo zinapoingilia. Mapato hayo yatawasilishwa kwa nchi husika baada ya kuthibitisha kuwa bidhaa zilivuka mpaka.
Mheshimiwa Spika;
Kutokana na uamuzi huo, Wakuu wa Nchi waliagiza Baraza la Mawaziri kuunda Kikosi Kazi cha kujadiliana na kuandaa utaratibu wa utekelezaji wa mfumo huo. Taarifa ya kikosi kazi inatakiwa kutolewa katika Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Nchi utakaofanyika Kampala, Uganda tarehe 30 Novemba, 2013. Iweje leo nchi tatu wanachama ziamue peke yao kuanza kutekeleza? Wanatekeleza nini na kwa nini wafanye hivyo?
Mheshimiwa Spika;
Kuhusu Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki hadithi yake inafanana na hii ya Himaya ya Forodha. Katika Mkutano wa 14 wa Wakuu wa Nchi wanachama uliofanyika tarehe 30 Novemba, 2012, Nairobi, tulipokea taarifa ya hatua iliyofikiwa kuhusu mchakato wa kutaka kuanzishwa kwa Shirikisho. Mkutano huo uliagiza nchi wanachama kujadiliana zaidi kuhusu mpango kazi wa kufikia Shirikisho la Kisiasa na mpango wa kutekeleza mapendekezo mengine yaliyotolewa na Timu ya Wataalamu. Inategemewa kuwa Baraza la Mawaziri litawasilisha mapendekezo ya majadiliano hayo katika Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Nchi mwezi Novemba, 2013. Iweje leo wenzetu hawa waamue kuanzisha mchakato wao wa kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika;
Kwa kweli huwa najiuliza maswali mengi na kukosa majibu kuhusu nini kinachoendelea kufanywa na viongozi wenzangu watatu na kwa nini! Nakosa majibu ya uhakika. Je wenzetu wamekosa imani na Jumuiya ya Afrika Mashariki na je wanataka kuunda yao? Je wanaichukia nchi yetu na hivyo wameamua kutufanyia vitimbi tutoke! Au sijui wanachuki na mimi! Napenda kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kuwa hatuna mpango wa kutoka (kama vijana wasemavyo hatoki mtu hapa). Tupo na tutaendelea kuwepo!
Mheshimiwa Spika;
Tanzania haijafanya jambo lo lote baya dhidi ya Jumuiya au nchi yo yote mwanachama. Na ukweli ni kwamba ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu kwa Jumuiya. Tunatimiza ipasavyo wajibu wetu kwa Jumuiya na kushiriki kwa ukamilifu katika ujenzi wake na utengamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Sabahu ya wenzetu watatu kuamua kufanya mambo yahusuyo Jumuiya yetu peke yao kwa kweli haieleweki.
Mheshimiwa Spika;
Tunasikia eti kuwa baadhi yao walipoulizwa kwa nini wengine hatupo wakasema kuwa wao wametangulia na sisi tutakapokuwa tayari tutajiunga. Yaani wana Umoja wa Waliokuwa Tayari (Coalition of the Willing). Hivi ni nani hayuko tayari (who is not willing?) Haiwezekani watu waitane wenyewe bila ya kutualika halafu wadai kuwa wao ndiyo wako tayari na kujenga dhana kuwa sisi wasiotualika ndiyo ambao hatuko tayari. Madai hayo hayana ukweli. Ni vyema waseme ukweli. Kama walitualika tukakataa ndiyo wanaweza kusema hayo.
Mheshimiwa Spika;
Kumekuwepo na madai kutoka kwa baadhi ya wenzetu, eti kwamba Tanzania haina moyo wala dhamira ya dhati ya kuendeleza utengamano wa Afrika Mashariki. Kwa sababu hiyo inasemekana eti nchi yetu imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba Tanzania tunawachelewesha wengine kupiga hatua za haraka. Wanadai kama siyo hivyo Jumuiya ya Afrika Mashariki ingekuwa mbali kwa maendeleo. Maneno hayo yamekuwa yanarudiwa au kujirudia mara nyingi kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu wa Afrika Mashariki na hata kwingineko duniani waamini hivyo.
Mheshimiwa Spika;
Napenda kusema kwa dhati ya moyo wangu kwamba madai hayo hayana ukweli wo wote. Isitoshe hata sababu zinazotolewa kuthibitisha ukweli wake hazina mashiko. Hazifanani na ukweli kuhusu Tanzania na Watanzania walivyo. Tanzania ni muumini wa dhati wa umoja na utengamano wa nchi za Afrika Mashariki na Afrika. Tumethibitisha hivyo kwa vitendo kwa kuunganisha nchi zetu mbili huru yaani Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika na kuwa taifa moja liitwalo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano wa nchi zetu mbili ndio pekee uliodumu kwa muda mrefu kuliko yote Afrika.
Mheshimiwa Spika;
Tanzania ni mwanachama mwaminifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa maana ya kutekeleza Mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo, kwa Itifaki zake na maamuzi halali ya vikao na taasisi za Jumuiya. Kama lipo jambo ambalo hatujalifanya ilivyotakiwa itakuwa ni kwa sababu za msingi na siyo kwa sababu ya kupuuza Jumuiya. Tunaithamini sana Jumuiya na tumeipa kipaumbele cha juu. Hatuwezi kuhangaika kwa gharama kubwa ya muda wetu, fedha zetu na kutoa mchango wa hali na mali kuianzisha, kujenga na kuifikisha Jumuiya hapa ilipo halafu tuwe ni watu tunaoongoza kutokuipenda na kudhoofisha maendeleo na ustawi wake. Ni maneno ya kushangaza na wala hayaingii akilini. Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.
Mheshimiwa Spika;
Nionavyo mimi msimamo wetu kuhusu kuharakisha Shirikisho na masuala ya ardhi, ajira, uhamiaji, pengine ndiyo yanayotuletea hisia zisizokuwa sahihi juu yetu. Mimi siamini kama kuna mengine. Hata hivyo, napata taabu kuamini kwamba kutofautiana kwa mawazo katika mambo hayo kutapelekea baadhi ya wenzetu wasipende hata kushirikiana nasi kwa mambo ambayo hayana matatizo na tumekuwa tunashirikiana vizuri.
Mheshimiwa Spika;
Tanzania imekuwa inawasihi wanachama wenzetu kuwa tujenge Jumuiya yetu hatua moja baada ya nyingine kama ilivyo kwenye Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hatuna tatizo la kuongeza kasi ya ujenzi wa Jumuiya lakini tusivuke hatua yo yote. Tusiende kasi ya kupindukia. Mkataba unaelekeza tunaanza na Umoja wa Forodha, inafuatia Soko la Pamoja kisha Umoja wa Kifedha na hatimaye Shirikisho la Kisiasa.
Mheshimiwa Spika;
Ni kweli kabisa hatukuunga mkono kuharakisha Shirikisho la Kisasa kabla ya kukamilisha baadhi ya hatua. Na, tulifanya hivyo kwa nia njema ya kutaka Shirikisho lijengwe juu ya msingi imara. Na, msingi huo si mwingine bali utengamano wa kiuchumi kwa maana ya Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja na Umoja wa Kifedha zilizojengeka vizuri na kufanya kazi ipasavyo na kunufaisha wanachama wote sawia.
Mheshimiwa Spika;
Lazima tutambue ukweli kuwa kunufaika kiuchumi ndicho kichocheo kikubwa cha nchi kujiunga na kuendelea kuwa mwanachama wa Jumuiya yetu. Kama mambo ya kiuchumi yakipangika vizuri na kila nchi ikanufaika sawia, unajenga msingi imara kwa Shirikisho la Kisiasa kustawi na kudumu. Kama ngazi hizi tatu za awali hazitashughulikiwa vizuri na nchi wanachama zikahisi hazinufaiki ipasavyo, Shirikisho litayumba au kuyumbishwa hivyo kudumu kwake kutakuwa kwa mashaka.
Mheshimiwa Spika;
Tanzania ni kati ya zile nchi zinazotaka ngazi zote za mchakato wa utengamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka hata moja. Kwa msimamo na mtazamo wetu, Shirikisho iwe ndiyo hatua ya mwisho. Na huo siyo msimamo wangu au wa Serikali peke yake, ndiyo msimamo wa Watanzania walio wengi.
Bila ya shaka sote tutakumbuka kuwa mwaka 2006 Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya waliunda Kamati Maalum katika kila nchi kukusanya maoni ya wananchi kuhusu kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki. Kwa hapa nchini Kamati hiyo iliongozwa na Profesa Samwel Wangwe na katika taarifa yake, Kamati ilieleza kuwaasilimia 74.4 ya Watanzania wanaunga mkono kuwepo kwa Shirikisho lakini ni asilimia 25.4 tu ndiyo waliunga mkono kuharakishwa kwake.
Mheshimiwa Spika;
Takwimu hizi zinaelezea ukweli kuhusu hisia za Watanzania, kuhusu kuwepo kwa Shirikisho na kasi ya utekelezaji wake. Watanzania wengi sana wanaunga mkono kuwepo kwa Shirikisho la Afrika Mashariki lakini wanataka jambo hilo lisifanywe haraka haraka. Wanataka lifanywe kwa umakini mkubwa na tuende hatua kwa hatua kama ilivyoainishwa katika Mkataba uliounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika;
Sera na msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakwenda sambamba na ile ya wananchi wa Tanzania. Ndiyo maana tumeafiki mapendekezo ya Kamati ile ya mwaka 2004iliyoongozwa na Mheshimiwa Amos Wako wakati ule akiwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya. Kamati hiyo iliundwa kupendekeza namna ya kuharakisha utekelezaji wa mchakato wa utengamano wa Afrika Mashariki.
Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umetamka muda wa kutekeleza ngazi ya Umoja wa Forodha lakini uko kimya kuhusu ngazi zilizofuata. Ili kuondoa kasoro hiyo na kwa nia ya kuharakisha Shirikisho Kamati ilipewa jukumu la kutoa maoni na mapendekezo juu ya namna ya kufanya hivyo. Kamati ilifanya kazi nzuri ya kupata maoni na hisia za watu wa makundi mbalimbali katika nchi wanachama kuhusu ujenzi wa Jumuiya na utengamano.
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa Tanzania kwa mfano, Kamati ya Mheshimiwa Amos Wako ilitambua hisia za Watanzania kuhusu ardhi na ajira na kupendekezwa kuwa masuala hayo yabaki kwenye mamlaka ya nchi wanachama kuamua. Kuhusu mchakato wa utengamano Kamati ilipendekeza kwanza kwamba mchakato wa ujenzi wa Umoja wa Forodha uachwe mpaka ufike ukomo wake wa miaka mitano. Baada ya hapo muda wa kutekelezwa ngazi zinazofuata unaweza kupunguzwa. Kwa mfano walipendekeza kuwa matayarisho ya kuunda Soko la Pamoja yaanze hata kabla ya mchakato wa Umoja wa Forodha kufika mwisho ili mara wakati huo ukifikiwa Soko la Pamoja linaanze. Hivyo hivyo mara baada ya ngazi hiyo kuanza matayarisho ya kuanza ngazi ya Umoja wa Kifedha yanaanza. Ngazi hiyo nayo ikianza matayarisho ya kuunda Shirikisho yanaanza. Kamati pia imetoa mapendekezo ya namna ya kufikia uamuzi kuhusu Shirikisho kwamba wananchi wa nchi wanachama wataamua kwa kura. Tukifuata mapendekezo ya Kamati ya Mheshimiwa Amos Wako na wenzake kama tufanyavyo sasa Tanzania haina matatizo nayo.
Mheshimiwa Spika;
Baada ya kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na wana-Afrika Mashariki kuhusu ujenzi wa Jumuiya yao inasikitisha kuona vinafanyika vitendo vinavyoanzisha mivutano kuhusu mambo yaliyokwisha fanyiwa kazi na kuamuliwa. Tunapata taabu zaidi pale watu wanapobagua wenzao na wanapofanya mambo yanayopingana na Mkataba wa Jumuiya na Itifaki zake. Kwa kweli kama mwenendo huu hautabadilika sijui mambo yatakuwaje mbele ya safari.
Mheshimiwa Spika;
Nchi yetu inapenda kuona kuwa tunakuwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyo imara na iliyo endelevu. Jumuiya ambayo inaendeshwa vizuri, mambo yake ni mazuri na nchi zote wanachama na watu wake wananufaika nayo, na hivyo wanaifurahia. Tanzania haina tatizo na kuharakisha mchakato wa utengamano, lakini tunapata taabu kuruka baadhi ya hatua kabla hazijakamilika. Tunawaomba wenzetu kuwa makini katika kila hatua tunayochukua. Bila ya kufanya hivyo, Jumuiya yetu itakuwa imejengeka katika msingi dhaifu hivyo ustawi na uhai wake utakuwa na changamoto nyingi. Hatupendi ya mwaka 1977 yatokee tena.
Mheshimiwa Spika;
Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushiriki katika shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuimarisha utengamano wa Afrika Mashariki kwa kuzingatia matakwa ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Itifaki zake. Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa Jumuiya haidhoofiki wala kufa. Na iwapo itadhoofika au kufa kamwe hatutaki Tanzania inyooshewe kidole kuwa chanzo wala kichocheo chake. Ndiyo maana, hatutachoka kuzungumza na wenzetu kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki inaendelea kustawi.
Tutaendelea kukumbushana umuhimu wa kufanya mambo yanayojenga na kuepuka yale yanayoweza kubomoa. Tutakumbushana umuhimu wa kuheshimu matakwa na masharti ya Mkataba ulioanzisha Jumuiya, Itifaki zake na maamuzi halali ya vikao rasmi na asasi za Jumuiya. Tukifanya hivyo Jumuiya ya Afrika ya Mashariki itadumu, itazidi kustawi na kunufaisha nchi wanachama na watu wake kama yalivyo malengo na madhumuni ya kuundwa kwake.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Idumu Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mheshimiwa Spika na
Waheshimiwa Wabunge;
- Oct 29, 2013
Hotuba ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Kanisa Katoliki, Parokia ya Lugoba, tarehe 27 O...
Soma zaidiHotuba
Mhashamu Baba Askofu, Telesphor Mkude, Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro;
Mhashamu Baba Askofu Anthony Banzi wa Jimbo Katoliki Tanga;
Wahashamu Maaskofu,
Viongozi wa Dini mliopo hapa;
Baba Paroko, Padri Constantine Luhimbo;
Mapadri, Mashemasi na Watawa;
Ndugu waumini;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Shukrani kwa Mwaliko
Niruhusuni niungane na wasemaji walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uzima na kutukutanisha hapa katika Kanisa la Msalaba Mtukuka kusherehekea Jubilei ya miaka mia moja ya Kanisa Katoliki la Lugoba. Nakushukuru sana Baba Askofu Mkude pamoja na Baba Paroko na waumini wa Parokia ya Lugoba kwa kunishirikisha katika maadhimisho haya ya kihistoria.
Nawapongeza sana waumini wa Parokia ya Lugoba kutimiza karne moja tangu ianzishwe. Hayo ni mafanikio makubwa, hivyo mnastahili kusherehekea kwa nderemo na vinubi. Nawapongeza sana kwa kuwakumbuka, kuwaenzi na kuwashukuru Padri Cornel na Padri Herman ambao ndiyo waanzilishi wa Parokia hii miaka 100 iliyopita. Hakika leo ni siku yao wao zaidi pengine kuliko sisi. Bila ya juhudi zao, moyo wao wa ujasiri, uvumilivu na kujituma huenda leo tusingekuwa hapa kufanya maadhimisho haya. Sote tumesikia kuwa mwanzoni mambo hayakuwa rahisi sana. Lakini, ni ushirikiano wa Wamisionari hao na baadhi ya wenyeji kama vile Mzee Kinogile, aliyekuwa Mtawala, Mzee Matei, Mzee Lui na wengineo ndiyo weliowezesha mambo kwenda vizuri na Parokia ikaanzishwa. Nafurahi nao pia mmewatambua na kuwaenzi.
Kwa ujumla nimefarijika sana kuona kwamba katika kusherehekea siku ya leo mnawatambua na kuwaenzi watumishi wa Mungu tangu wakati ule mpaka sasa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kujenga na kuimarisha kanisa kwenye Parokia hii. Kutokana na kazi yao nzuri waumini wameongezeka, huduma za kiroho zimeimarika na kwamba Kanisa limetoa mchango muhimu kwa maendeleo ya jamii katika eneo letu hili.
Ndugu waumini;
Ninyi na mimi ni shuhuda wa jinsi Kanisa Katoliki la Lugoba lilivyochangia na linavyoendelea kuchangia katika upatikanaji wa huduma za jamii kama vile elimu na afya bila ya kuwabagua watu kwa imani zao za kumuabudu Mungu. Kwa upande wa afya tumesikia zahanati zilizojengwa na Kanisa na mipango iliyopo ya kuboresha zaidi huduma zinazotolewa. Vile vile, tumesikia shule zilizojengwa na kuanzishwa na Kanisa la Lugoba. Hata mimi ni mmoja wa watu walionufaika kwani nilipata elimu ya darasa la tano hadi la nane mwaka 1962 mpaka 1965 katika shule iliyokuwa inaitwa St. John Bosco’s Lugoba Middle School iliyomilikiwa na Kanisa Katoliki Lugoba.
Kunako mwaka 1965, Serikali iliamua kuwa elimu za msingi hazitakuwa na madaraja mawili yaani ya darasa la kwanza hadi la nne (Primary School) na darasa la tano hadi la nane (Middle School) badala yake elimu ya msingi ikawa kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Kufuatia uamuzi huo Lugoba Middle School na Lugoba Primary School ziliunganishwa na kuwa shule ya Msingi Lugoba. Wakati madarasa tuliyosomea yanaunganishwa na shule hiyo mpya, iliyokuwa ofisi ya Walimu ikawa zahanati ya Kanisa na yaliyokuwa mabweni sasa yamekuwa madarasa ya Sekondari ya Lugoba.
Kwa kweli hatuna maneno mazuri ya kuelezea shukrani zetu kwa Kanisa Katoliki Parokia ya Lugoba kwa mchango muhimu iliyotoa kwa maendeleo ya watu wa eneo hili, Wilaya ya Bagamoyo na kwingineko nchini. Watu wengi wamefaidika na wanaendelea kunufaika. Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki ili muendelee kuwahudumia watu katika Parokia yetu ya Lugoba na taifa kwa ujumla. Tunapenda miaka mia moja ijayo, kwa watakaokuwepo kipindi hicho, wakiri utume huo usiokifani. Na waseme “hakika wenzetu waliotangulia walikuja kufanya kazi, walikuwa watu wa kazi”.
Serikali Inathamini Mchango wa Kanisa
Mhashamu Baba Askofu Mkude;
Mabibi na Mabwana;
Napenda kuwahakikishia kuwa serikali inatambua vyema na kuthamini mambo yote mazuri yanayofanywa na Kanisa Katoliki. Kabla na hata baada ya uhuru, Kanisa limekuwa mdau muhimu na mshirika muhimu wa Serikali katika kuhudumia wananchi. Wakati mwingine unakuta huduma za jamii kama zahanati ipo mahali ambapo hata Serikali bado haijafika. Kutuunga mkono kwa namna hiyo ndiko kumechangia sana nchi yetu kupiga hatua kubwa kwenye kufikisha huduma kwa jamii nchini.
Ahadi yangu kwenu ni kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa Katoliki pamoja na madhehebu mengine ya dini kuboresha maisha ya Watanzania. Tutaendelea kupokea ushauri wenu na kuwashirikisha katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Naomba muendelee kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma kwa wananchi. Muendelee kutumia mtandao wenu mpana uliopo nchi nzima kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu. Lengo letu libaki kuwa moja daima na milele. Tufanye kazi pamoja ili tufanikiwe zaidi.
Maombi kwa Viongozi wa Dini
Mhashamu Baba Askofu Mkude, Baba Paroko na viongozi wa dini mliopo;
Naomba muongeze juhudi za kuhubiri umoja na kutoa mafundisho ya kuhimiza udugu na mshikamano miungoni mwa Watanzania. Sote tunafahamu kuwa kuna baadhi ya watu wanaofanya juhudi usiku na mchana kuuvuruga upendo, umoja na mshikamano wa wananchi wa Tanzania. Kwa sasa watu hawa hawajafanikiwa lakini tuelewe kuwa hawajachoka na wala hawajaaacha. Wana sifa ya ushetani, maana shetani hachoki wala hakati tamaa katika kuwashawishi wanaadamu kutenda maovu. Na, hawa si ajabu wakathubutu tena na tena. Inatupasa na sisi pia tuwe macho. Naomba msilegeze uzi katika kuwaelimisha waumini wenu waelewe nia mbaya za watu wasioitakia mema nchi yetu, wawaepuke wala wasiwasikilize. Tudumishe upendo, umoja na mshikamano wetu. Sisi sote Mungu wetu ni mmoja kwa nini tuchukiane, tubaguane na hata tuuane kwa sababu ya kutofautiana katika kumuabudu Mungu? Wengine ni ndugu wa damu kwa nini tufarakane kwa namna ya kumsujudia Muumba wetu? Kila mtu aachwe kufuata dini anayoipenda na udugu wetu na umoja wetu kama wanadamu ubaki pale pale. Ipo hatari hata ndugu wa damu tukafarakana kwa sababu ya kuwa dini mbalimbali. Siyo sawa.
Niliwahi kusema siku za nyuma na leo narudia tena kuwa viongozi wa dini wanayo nafasi ya pekee katika kufikisha ujumbe huo kwa watu wote. Hii inatokana na ule ukweli kwamba wanasikilizwa na kuaminiwa sana na waumini wao na watu wengine pia. Wanasikilizwa na watu wengi. Waumini wakielezwa, wakaelewa na wote wakazingatia kuishi kama mafundisho ya viongozi wao, nchi yetu itabaki salama. Hakuna mtu atakayefanikiwa kutufarakanisha na kuichezea amani yetu. Hata kama ni muumini wa dini ya shetani.
Pili, naomba tuendelee kusaidiana kulea nchi yetu kimaadili. Hakuna siri kwamba kuna mmonyoko mkubwa wa maadili mema. Vitendo viovu na mambo yasiyoipendeza jamii na yasiyompendeza Mwenye Mungu yanazidi kuongezeka kwenye jamii. Mambo ambayo siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikika sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekana ati ndiyo usasa. Matumizi makubwa ya dawa za kulevya, ngono, ubakaji, watoto kutokuheshimu wakubwa, wazee kutokujiheshimu, ulevi wa kupindukia, vitendo vya rushwa, uvivu, wizi na idadi kubwa ya ndoa kuvunjika ni vielelezo dhahiri vya hali mbaya ya kimaadili inayokabili jamii zetu nchini.
Kuporomoka kwa maadili ni jambo lenye athari mbaya kwa jamii na taifa kwa ujumla. Kunachangia sana kurudisha nyuma juhudi za kujiletea maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Kunaifanya kazi ya kuondoa umaskini kuwa ngumu na kuongeza watoto wa mitaani. Kunachangia kuenea kwa maambukizi ya UKIMWI. Kunaongeza uhalifu wa aina mbalimbali nchini pamoja na mauaji.
Mimi naamini kwa dhati kuwa watu wakishika mafundisho ya dini, wakamuogopa Mwenyezi Mungu, maovu mengi yatapungua. Hayawezi kuisha kabisa lakini yatapungua sana. Ndiyo maana narejea ombi langu ninalolitoa mara kwa mara kwa viongozi wa dini zote. Tusaidiane kulea taifa letu kimaadili. Tuweke mkazo zaidi kwa vijana kwa sababu, kwanza wao ndio walengwa wakuu wa maovu yanayotendeka. Lakini pili, wao ndio taifa la leo na kesho, ndio warithi wa taifa letu. Tukiwaandaa vyema, mustakabali wa taifa letu na watu wake utakuwa kwenye mikono salama. Tukishindwa leo, tutalia na kusaga meno kesho. Taifa letu litakuwa mashakani.
Mwisho
Kwa kumalizia nawapongeza wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kuandaa sherehe hizi. Kwa kweli zimefana sana na watu wote hapa ni mashahidi. Nakushukuru kwa mara nyingine tena Mhashamu Baba Askofu na Baba Paroko kwa uongozi wenu uliotukuka. Nimefurahi sana kujumuika nanyi katika maadhimisho haya. Naomba tuendelee kushirikiana kuleta maendeleo zaidi kwenye Parokia yetu na nchi yetu kwa ujumla. Tukiunganisha nguvu zetu, daima ushindi utapatikana. Naomba tuamue kuwa washindi. Tumsifu Yesu Kristu.
Asante kwa kunisikiliza.
- Oct 28, 2013
Hotuba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwia Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kufunga semina ya makatibu wa...
Soma zaidiHotuba
Ndugu Phillip Mangula, Makamu Mwenyakiti wa CCM;
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM;
Ndugu Manaibu wa Katibu Mkuu;
Ndugu Makatibu wa Sekretariat Mliopo;
Ndugu Wanasemina;
Ndugu Watoa Mada;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru na kukupongeza sana Katibu Mkuu kwa uamuzi wa busara wa kuwa na mafunzo haya kwa Wenyeviti wa Wilaya, Makatibu wa Wilaya na Makatibu wa Mikoa wa Chama chetu. Nafurahi kwamba mafunzo haya yamefanyika wakati muhimu katika safari yetu ya kuelekea mwaka 2015. Hivi sasa tupo takriban katikati ya safari hiyo. Naamini mafunzo haya yatasaidia kujiweka sawa katika ngwe ya pili ya kipindi cha pili cha uongozi wa Awamu ya Nne ya uongozi wa CCM katika nchi yetu. Awamu ambayo mimi ndiye kiongozi wake kwa niaba ya Chama chetu.
Ni mategemeo yangu kuwa baada ya mafunzo haya, mijadala iliyofuatia na mapendekezo mliyoyatoa mnaondoka hapa mkiwa manahodha bora zaidi wa kuongoza vyema Chama cha Mapinduzi kwenda na kufika salama katika safari yetu ya kuelekea 2015. Mnatoka kwenye mafunzo haya mkiwa na kauli mbiu moja tu kwamba “Ushindi ni Hakika mwaka 2014 na 2015”.
Lengo Kuu la Chama cha Siasa
Ndugu viongozi wenzangu;
Sote tunafahamu kwamba lengo kuu la Chama cha Mapinduzi kama ilivyo kwa vyama vyote vya siasa nchini na duniani ni kushika dola. Hivyo ndivyo Katiba ya CCM inavyotamka wazi katika Ibara ya 5 kwamba malengo na madhumuni ya CCM ni; Nanukuu “Kushinda katika uchaguzi wa Serikali Kuu na Mitaa, Tanzania Bara
na Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu na Mitaa katika Jamhuri ya Muungano kwa upande mmoja na Zanzibar kwa upande wa pili”. Katika mazingira ya nchi yetu ni kushinda uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi, Madiwani na ule wa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Hivyo pamoja na majukumu mengine mengi mliyonayo lazima mtambue kwamba hatimaye shabaha yetu kuu ni kuhakikisha kuwa wagombea wa Chama chetu wanashinda katika chaguzi hizo.
Nyie kama viongozi na watendaji wakuu wa maeneo yenu lazima mtambue kuwa chombo cha kutuongoza, kutuimarisha na kutufikisha kwenye ushindi ni Chama cha Mapinduzi. Hivyo basi, lazima Chama kiwe na nguvu ya kutosha ya kutufikisha kwenye lengo letu kuu. Hamna budi kila mnapofanya jambo mpime kama jambo hilo linakisaidia Chama chetu kuwa na nguvu za kushinda uchaguzi au la. Msifanye mambo yatakayoipunguzia CCM nguvu na yanayojenga mazingira yatakayosababisha wagombea wa CCM kushindwa na hivyo Chama chetu kushindwa. Mkifanya hivyo mtakuwa hamkisaidii Chama chetu. Wakati wote kila mmoja wetu ajiulize je hili nilifanyalo linasaidia CCM kushinda? Au kwa lugha nyingine tujiulize ni kitu gani nikifanya kinasaidia Chama cha Mapinduzi kushinda.
Uhai na Uimara wa Chama
Ndugu viongozi wenzangu;
Kwa maoni yangu kuna mambo matatu muhimu ambayo yakifanyika yatasaidia Chama cha Mapinduzi kushinda:-
(1) Uimara wa Chama;
(2) Tabia na mwenendo wa viongozi na wanachama wa CCM; na,
(3) Utendaji wa Serikali ya CCM.
Inatupasa kuhakikisha kuwa Chama chetu kinashiriki katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kikiwa na nguvu kubwa, hai na imara kwa kila hali toka ngazi ya shina, tawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hadi taifa. Siku za nyuma nilishasema kuwa Chama ni kama ulivyo mwili wa mwanadamu, uimara wake unategemea sana ukamilifu na uzima wa viungo vyake. Kikipungua kiungo kimojawapo Chama kina ulemavu na kikidhoofika chochote kinakuwa na afya mbaya. Kwa ajili hiyo basi uimara wa Chama cha Mapinduzi unategemea kuwepo kwa wanachama, viongozi, watendaji, vikao, rasilimali na jumuiya za Chama na vyote vikiwa vinafanya kazi zake ipasavyo.
Ninyi mliopo hapa yaani Wenyeviti wa Wilaya, Makatibu wa Wilaya na Makatibu wa Mikoa ndiyo mnaotegemewa zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kuhakikisha kuwa viungo vya Chama vinakamilika na kwamba viko hai kwa maana ya kufanya kazi kama inavyotarajiwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Mapinduzi, sera na maamuzi mbalimbali.
Ndugu viongozi;
Ni matumaini yangu na nimehakikishiwa hivyo kwamba katika mafunzo haya mmepewa maarifa ya kuhakikisha kuwa Chama cha Mapinduzi kinakuwa hivyo. Mmejifunza juu ya nini mnachowajibika kufanya ili Chama chetu kiwe imara, hai na chenye nguvu. Nimeambiwa pia kuwa katika majadiliano mlipata nafasi ya kubadilishana uzoefu kutoka kwa wale waliofanikiwa na hata wale walioshindwa. Ndugu zangu mpate nini zaidi ya hayo. Mfanyiwe nini tena lililo bora zaidi kuliko hilo. Ndiyo maana sipati kigugumizi kusema kuwa sasa ninyi mmekuwa wapiganaji bora zaidi. Haya nendeni mkaoneshe umahiri wenu kwenye medani ya kujenga Chama. Nendeni mkaoneshe mtindo bora wa uongozi na utendaji. Nendeni mkakipe Chama chetu sura mpya, uhai mpya na kasi mpya ya maendeleo.
Kuingiza Wanachama
Ndugu Viongozi;
Hatuna budi kwanza kabisa kuhakikisha kwamba Chama chetu kinapata wanachama wapya wengi na kuwaimarisha waliopo. Wanachama ndiyo kielelezo cha awali cha kuwepo kwa Chama. Wingi wa wanachama ndio nguvu ya kufanya kazi ya Chama na mtaji wa uhakika wa kuanzia katika kutafuta ushindi. Hivyo basi, lazima wakati wote Chama chetu kiendelee kuingiza wanachama wapya. Tusisubiri mpaka karibu au wakati wa uchaguzi ndipo tuongeze nguvu ya kusajili wanachama wapya. Twende tukafanye kazi ndani ya umma kuwashawishi na kuwahamasisha wananchi, hususan vijana, kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Mnapaswa kuwa na mikakati madhubuti ya kupata wanachama wapya katika maeneo yenu. Kupata wanachama wapya ni kazi ya kudumu ya Chama.
Ndugu viongozi;
Kimsingi uimara wa Chama chetu unategemea uhai wa wanachama wake. Mwanachama hai wa CCM ni yule anayelipa ada na kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli za Chama, mojawapo ikiwa kuwashawishi watu wasiokuwa wanachama kuunga mkono CCM. Ili wanachama wawe hivyo ni wajibu wa viongozi kuwa na mikakati maalum ya kuwawezesha kufanya hivyo. Kuwatembelea mara kwa mara kuzungumza nao na kuwaelimisha mambo mbalimbali yanayohusu Chama na nchi kwa ujumla ni mbinu muhimu sana kwa ajili hiyo. Tukifanya hivyo Chama chetu kitakuwa na wanachama wengi wanaojua mambo na wenye moyo wa kukitumikia. CCM itakuwa na uwezo mkubwa wa kujiendesha na kufanya mambo yake. Kitakuwa kimeimarika zaidi. Viongozi wa Chama lazima tujenge mazoea ya kuwatembelea wanachama na kuzungumza nao. Hili ndilo jukumu la msingi na asiyefanya hivyo ameshindwa kutimiza wajibu wake.
Ndugu zangu;
Ni ukweli ulio wazi kuwa si viongozi na watendaji wengi wanaofanya hivyo. Lazima mjisahihishe. Zamani mlidai hamna magari sasa mnayo. Kwa kweli kutowatembelea wanachama ni jambo lisilokuwa na maelezo. Nilishaagiza siku za nyuma na narudia kusisitiza tena leo kuwa katika Taarifa ya kazi za Chama ya kila mwezi kila Wilaya itoe taarifa ya kuhusu viongozi kutembelea matawi na kuzungumza na wanachama. Hivyo hivyo kwa Mikoa, nao watoe taarifa ya kutembelea Wilaya zao na kuzungumza na viongozi wa Wilaya, Kata, Matawi na Mashina pamoja na kuzungumza na wanachama. Ndugu Katibu Mkuu naomba hili lazima tulidai lifanyike kwani manufaa yake kwa uhai wa Chama cha Mapinduzi hayana mfano wake.
Ndugu viongozi;
Jambo la pili muhimu kwa uhai na maendeleo ya Chama chetu ni kuwatembelea wananchi na kuzungumza nao. Ni vyema mkatambua kuwa tunapotaka kuongoza dola kwa mfumo wa vyama vingi kazi yetu kubwa ni ile ya kuwavutia watu upande wetu. Tushinde mioyo na akili zao. Tuwafanye watu waelewe sera na siasa ya Chama cha Mapinduzi, wazikubali na kutuunga mkono. Tufute maneno hasi na uongo wa wapinzani dhidi ya CCM na serikali yake. Lazima viongozi mtoke muwatembelee wananchi, mzungumze nao kuhusu Chama chetu na taifa kwa ujumla. Tumekuwa wazito sana kufanya hivyo, lazima tujirekebishe.
Utendaji wa Serikali
Ndugu viongozi na Watendaji;
Kwa vile hivi sasa CCM ndicho Chama tawala, viongozi wa Chama wanaowajibu wa namna mbili. Kwanza, kuhakikisha kuwa serikali yao inatekeleza Ilani ya Uchaguzi na pili, kuwaelezea wananchi masuala mbalimbali ya utendaji wa serikali. Viongozi wa Chama mmepewa dhamana ya kuyasimamia hayo katika maeneo yenu. Lazima mfuatilie utekelezaji wa Ilani kupitia vikao vyenu hususan Kamati za Siasa na Halmashauri Kuu za Wilaya na Mikoa. Ndiyo maana Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni wajumbe wa vikao hivyo na hutoa taarifa ya kazi nyakati mbalimbali.
Ili muweze kufanya hivyo, lazima ninyi wenyewe mfahamu vizuri Ilani ya CCM inasema nini kuhusu Mikoa na Wilaya zenu. Pili, lazima mfahamu ahadi za wagombea wa Chama chetu na za viongozi wa Chama katika ngazi mbalimbali. Lengo ni kujua na kufuatilia utekelezaji wa ahadi hizo ili zisije zikageuka kuwa tatizo katika uchaguzi ujao. Tujue zipi zimetekelezwa, zipi hazijatekelezwa na zilizotekelezwa zimetekelezwa kwa kiwango gani. Tujue mipango iliyopo na nini kinapaswa kufanyika ili kutekeleza au kukamilisha ahadi hizo. Tukumbushane mambo ambayo hayajatekelezwa. Wakumbusheni Marais, Mawaziri, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Madiwani na viongozi wa Serikali za Mitaa juu ya ahadi zao walizozitoa ambazo hazijatekelezwa ili wazitekeleze au wawe na mipango thabiti ya kutekeleza.
Pia, ziambieni serikai katika ngazi zote husika kuhusu masuala mapya yaliyojitokeza ambayo wananchi wanataka tuyatekeleze. Tukiweza kuyafanya na hayo pia yatatuongezea kuaminika, kupendwa na kutuongezea uhakika wa kuchaguliwa tena. Naomba mshirikiane na viongozi wa Serikali katika maeneo yenu kutengeneza utaratibu mzuri ili masuala hayo yajulikane na kutengenezwa mkakati maalum wa kuyatekeleza.
Ndugu viongozi;
Tumieni vikao vyenu au njia nyingine za mawasiliano kuyafikisha masuala hayo na mengine. Katika vikao hivyo pia, Wakuu wa Wilaya na Mikoa wanao wajibu wa kuelezea na kufafanua masuala mbalimbali yahusuyo Serikali au Mkoa au Wilaya husika. Wajumbe waulize ili wapate maelezo ya kusaidia kujibu hoja za wananchi au wapotoshaji kwa kazi nzuri za serikali ya CCM.
Vikao
Ndugu Viongozi;
Hatuna budi kuhakikisha kuwa vikao vya Chama vinafanyika na vinaendeshwa vizuri ili viweze kutekeleza ipasavyo jukumu lake la kufuatilia utendaji wa serikali ya CCM na uendeshaji wa Chama. Lazima vikao vya Kikatiba vifanyike bila kukosa na pawepo na kalenda maalum kwa ajili hiyo. Kuwa na kalenda inayojulikana ni muhimu kwa wajumbe kwani wanashughuli zao zinazowapatia riziki hivyo wakijua mapema vikao vya Chama watajua namna bora ya kujipanga. Si vizuri taarifa ya vikao vya Kikatiba ikatolewa kwa muda mfupi kana kwamba ni vikao vya dharura.
Jambo lingine muhimu kuhusu vikao ni kuwa na agenda za maana na zilizoandaliwa vizuri. Kwa mfano, mnaweza mkaamua kila kikao kiwe na agenda ipi kuu katika Wilaya na Mkoa wenu. Mathalani mnaweza kupanga kuwa kikao cha mwezi fulani kiwe cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, cha mwezi fulani kupokea taarifa ya uhai wa Chama na kadhalika. Mkifanya hivyo mnajipa muda wa kushughulikia masuala muhimu. Hata hivyo haizuiliwi kuzungumzia au kushughulikia masuala mengine muhimu. Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa vikao vinaendeshwa vizuri na wajumbe wanapata nafasi ya kutoa maoni yao kwa uhuru. Kumbukumbu za vikao ziandikwe vizuri na kuhifadhiwa vizuri.
Ndugu Katibu Mkuu;
Chama lazima kiwe na utaratibu wa kuwafundisha Makatibu Tawi, Makatibu Kata, Makatibu Wasaidizi, Makatibu wa Wilaya na Mikoa kuhusu uandishi wa kumbukumbu na namna ya kuzihifadhi na kuzifanyia kazi. Lazima pia kiwe na utaratibu wa mafunzo kwa watumishi na watendaji wake wa kada mbalimbali katika ngazi zote za utumishi na utendaji. Chama kina mifumo yake na taratibu zake za kuendesha shughuli ambazo lazima zifuatwe. Ni lazima watu wafundishwe ili wazielewe na kuzifuata. Vile vile ni muhimu Chama kuwekeza katika kuwaendeleza watumishi na watendaji wake kielimu na kitaaluma. Aidha, tuwalipe maslahi mazuri.
Mali za Chama
Ndugu Viongozi na Watendaji;
Jambo lingine muhimu sana katika kuimarisha Chama ambalo naamini mmelizungumzia kwa undani ni rasilimali za Chama kwa Chama kuwa na fedha, majengo, vyombo vya usafiri na vifaa vingine vya kuendeshea shughuli zake ni jambo la kufa na kupona. Lazima tuwe na fedha za kutosha, majego mazuri ya kufanyia kazi, magari na vyombo vingine vya usafiri na vifaa mbalimbali. Lazima tuwe na mipango na mikakati dhabiti ya kuwa na rasilimali hizo na hasa fedha. Katika historia ya Chama chetu vyanzo vikuu vya fedha ni ada za wanachama, uuzaji wa vitabu na mali nyingine za Chama na michango ya hiari. Hali ilivyo sasa ni kwamba wanachama wamekuwa wazito kulipa ada, vitabu na mali za kuuza hazipo za kutosha. Na michango ya hiari haibuniwi. Kwa kweli, Chama siku hizi kinaendeshwa kwa taabu. Wilaya na Mikoa hutegemea Makao Makuu tofauti na ilivyokuwa zamani. Pale ambapo kuna wafadhili ambao ni wabunge wajumbe wa NEC wenye uwezo na wapenzi wa Chama mambo huwa mazuri. Pale ambapo hawapo kuna shida. Aghalabu baadhi ya wafadhili au wapenzi wa Chama ni watu wenye agenda zao. Ama wana tamaa za kugombea uongozi fulani hivyo wananunua kuungwa mkono au wanatafuta msaada fulani.
Mtakubaliana nami kuwa jambo hili muhimu sana kwa uhai wa Chama lakini halijapata mwelekeo mzuri. Lazima tubadilike tena tubadilike haraka vinginevyo mbele ya safari hali itakuwa mbaya zaidi. Hatuna budi kuwa wabunifu na kuongeza jitihada za kukijengea Chama uwezo wa kifedha na rasilimali katika ngazi zote. Tulishatoa maagizo kwa kila ngazi kuwa na mfuko wa uchaguzi, sijui ni wangapi wanao na wana kiasi gani. Na watu hawashtuki. Hali hii haikubaliki lazima tujirekebishe, hatujachelewa. Mtakumbuka katika Mkutano Mkuu uliopita niliagiza majengo na viwanja vyote vya Chama vipatiwe hati. Je, limekalimika?
Maadili
Ndugu viongozi na Watendaji;
Tabia na mwenendo mwema ni sifa ya msingi ya kuwa kiongozi na mtendaji wa Chama cha Mapinduzi. Kwa namna ya pekee kiongozi hutoa taswira ya CCM kwa wananchi na wanachama. Mkiwa wachapa kazi hodari, watu wenye nidhamu na waadilifu ni sifa njema kwa Chama chetu. Mkiwa tofauti na hayo ni sifa mbaya kwa CCM. Naamini haya ninayoyasema yameelezwa vizuri na kusisitizwa sana katika mafunzo haya. Naomba muwayazingatie na kuyatekeleza.
Nendeni sasa mkadhihirishe kuwa ni mfano bora kwa wanachama na wananchi tunaowaongoza. Mkifanya hivyo mtakubalika na kuungwa mkono na wanachama na jamii kwa ujumla. Na hivyo basi chama chetu kitanufaika.
Ndugu viongozi;
Si jambo jema hata kidogo kwa viongozi au watendaji wa Chama kuwa na tabia na mwenendo mbaya wanakiumiza Chama. Jiepusheni kuwa waombaji na wapokeaji wa rushwa. Epukeni kuwa mawakala na wasambazaji wa fedha chafu za wagombea wanaotaka kununua uongozi. Tukifanya hivyo tutaiharibu sana sifa ya CCM. Mtashindwa kusimamia haki na mtakigawa Chama chetu. Ninyi mnategemewa kuwa wasimamizi wa michakato ya uchaguzi lazima mtende haki na muwe waadilifu. Mkikubali kuhongwa au kuwa wakala wa mgombea mtawanyima haki baadhi ya wagombea na itakuwa vigumu kwenu kutatua malalamiko yanayotokea kwa sababu ninyi wenyewe ni sehemu ya tatizo. Isitoshe wagombea watapoteza imani kwa viongozi na watendaji wa Chama chao, jambo ambalo ni la hatari. Linalofanya watu kupata hasira na wengine kufanya uamuzi usiotarajiwa na kukiathiri Chama. Katika maeneo mengi tuliyopoteza katika uchaguzi uliopita upendeleo wa viongozi kwa wagombea ulichangia sana. Hakikisheni kasoro za chaguzi zilizopita hazijirudii tena siku za usoni. Msije mkakiingiza Chama kwenye matatizo yanayoweza kuepukika.
Ndugu viongozi na Watendaji;
Kabla ya kumaliza, ningependa kuwakumbusha kuwa Chama chetu kupitia serikali yake kimefanya mambo mengi mazuri kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Sina shaka ifikapo 2015 tutakuwa tumefanya vizuri zaidi na hivyo hatutasutwa kwa kutokuwa wakweli. Kwa ajili hiyo sioni sababu kwa nini tusifanye vizuri katika chaguzi za 2014 na 2015. Lakini, tutaweza kutokufanya vizuri iwapo tutafanya makosa katika uteuzi wa wagombea. Tukiteua watu wasiokubaliwa na jamii kwa sababu ya urafiki, ujamaa au kwa kupewa chochote binafsi zetu, jamii itatuadhibu. Anayedhani kuwa kila aliyeteuliwa na CCM atachaguliwa anajidanganya. Wakati huo umepita. Tupate wagombea wazuri tusiendekeze rushwa. Tusiwaonee au kuwadhulumu watu na kuwafanya wajenge chuki dhidi ya Chama chetu na hata kususa au kufanya matendo ya kukidhuru Chama. Tusiwasukume watu ukutani bila ya sababu acheni mambo yawe wazi, ushindi uwe wa haki ili mtu akishindwa ajue kuwa haikuwa bahati yake. Mtu mwenye upungufu aambiwe kasoro zake kama ilivyo mila na desturi ya CCM. Si vizuri mtu ajione kaonewa au kadhulumiwa na viongozi wa Chama waliopokea rushwa kutoka kwa wagombea au wanaomchukia. Nalisema hili kwa sababu habari zimezagaa za watu wanaojipanga kugombea uongozi kuwa wanahonga sana viongozi na watendaji wa CCM. Mzee Mangula analishughulikia hilo. Nawasii mjiepushe nao msije mkakutwa kuhusika, mtapata matatizo makubwa. Lazima tulinde na kudumisha heshima ya Chama chetu.
Ndugu viongozi na watendaji;
Nimalizie kwa kuwapongeza watoa mada kwa kazi nzuri waliofanya ya kutoa mafunzo kwa viongozi wetu hawa. Viongozi wenzangu tusiwaangushe wakufunzi wetu kwa kutoonesha mabadiliko katika uongozi na utendaji wetu baada ya mafunzo hayo. Nawatakia safari njema na utendaji ulio bora zaidi.
Baada ya kusema haya, natamka rasmi kwamba, semina yenu imefungwa. Asanteni kwa kunisikiliza.
- Oct 28, 2013
Speech by his excellency Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania during launching of the 4th Tanzania deep offshore and north l...
Soma zaidiHotuba
Honourable Professor Sospeter Muhongo, Minister for Energy and Minerals;
Mr. Michael Peter Mwanda, Chairman of the Board of Directors of Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC);
Mr. Yona Killagane, Managing Director of Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC);
Mr. Brian Horn, Representative of ION-GXT;
Mr. Stewart Walter, Representative of WesternGeco;
Distinguished Representatives from Petroleum Industry;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen;
I thank you, Minister Muhongo, for inviting me to officiate at this auspicious and historic occasion of launching the 4th Licensing Round for Deep Offshore blocks and Lake Tanganyika North block. I am saying this occasion is auspicious and historic because it is important and it is the first time a Licensing Round is held in Tanzania. All the other rounds took place in Europe and America. In fact, it was on my advice that this Round is being held here. It was originally planned to be held in Houston Texas.
Oil and gas exploration in Tanzania has a long and interesting history. It started in 1952 when British Petroleum (BP) and Shell International Oil Company (SHELL) were jointly awarded a concession covering the onshore coastal basins and the islands of Zanzibar, Pemba and Mafia. Extensive geological and geophysical surveys were undertaken. Four deep exploration wells were drilled. These were Pemba-5 on Pemba Island, Zanzibar-1 on Zanzibar Island, Mafia-1 on Mafia Island and Mandawa-7 in Lindi Region. Unfortunately, the mission was not successful and the two companies relinquished the concession in 1964.
Ladies and Gentlemen;
In 1969, the government decided to establish a national oil company, hence the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC). It was tasked, among other functions, to spear head and coordinate all activities related to exploration of oil and gas in the country. Subsequently, the concession previously held by BP and SHELL was awarded to AGIP who were later joined by AMOCO. AGIP conducted the necessary surveys and drilled five deep exploration wells including Ras Machuisi-1, Songo Songo-1, Kisangire-1, Kisarawe-1 and Kizimbani-1. Luckily, these exploration efforts were not in vain. They revealed the presence of natural gas in Songo Songo-1 well. However, the evaluation indicated that the reserve, of around 4 Billion Standard Cubic Feet, was not of commercial quantity. In 1974, AGIP relinquished the Songo Songo licence.
Ladies and Gentlemen;
Our determination was not withered by the disappointment of previous two attempts. TPDC undertook further evaluation of the Songo Songo property by acquiring more seismic data and drilled three more wells. This extra effort and perseverance, was rewarded with the discovery of more natural gas and the new reserve estimates became 43 billion standard cubic feet.
Ladies and Gentlemen;
This new discovery then raised the interests of oil companies as a result exploration activities increased. New exploration licences were issued to SHELL in Ruvu, Selous, Mandawa and Mafia; International Energy Corporation (IEDC) in Tanga; ELF in Mafia and Nyuni; AMOCO in Lakes Tanganyika and Rukwa and TEXACO in the Ruvuma basin. These operators carried out geological and geophysical surveys and drilled a total of four exploration wells. This time round, AGIP was lucky as before. In 1982, they made another gas discovery at Mnazi Bay-1, in Mtwara. Once again, however, AGIP declared the discovery as non-commercial.
TPDC carried out seismic data acquisition onshore and offshore to promote open acreage and also drilled two exploration wells of Kimbiji-1 onshore and Tan-Can-1 offshore. Five gas appraisal wells were also drilled in the Songo Songo gas field. New reserve estimates became around 1 trillion Standard Cubic Feet (1Tcf), paving way for development. And the costs for appraising the Songo Songo gas field were around U.S. $ 100 million while costs for the two other wells were around U.S. $ 10 million.
Ladies and Gentlemen;
The exploration for oil and gas in the deep offshore Tanzania commenced in 1999. Players in the deep sea include Statoil and Exxon Mobil, BG and Ophir, Petrobras and Shell, and Dominion Oil and Gas. The first deep offshore well which became a discovery was completed in October 2010 in Block number 4. The wells drilled afterwards in the deep sea namely Jodari 1, Jodari North 1, Jodari South 1, Mzia 1, Mzia 2, Chaza 1, Pweza 1, Chewa 1, Ngisi 1, Papa 1, Zafarani 1, Zafarani 2, Lavani 1, Lavani 2 and Tangawizi 1 were all successful with the exception of Zeta 1. In this regard, we have been able to increase our natural gas reserves from 7.5 trillion standard cubic feet in 2003 to 43.1 trillion. Indeed these discoveries have transformed Tanzania into a hot spot for oil and gas exploration.
In view of the latest positive development in the oil and gas sector it became apparent that there was need to do a comprehensive review of the way we conduct the affairs of the sector. As a result of this we are in the process of putting in places a gas policy framework to ensure smooth operations of the industry. We have also reviewed the term of the Production Sharing Agreement (PSA) and we are taking concrete measures to improve investment climate in the country. As some foreign companies have confessed to me that our investment incentives are arguably among the best in the African Continent. This makes us feel good in the sense that we are as competitive as other players in the market. No wonder therefore, that we have 24 active PSA’s and 17 operators in the oil and gas industry in our dear country.
Ladies and Gentlemen;
The duty at hand for us is to ensure that there is a fair and a level playing field for operators and investors in the oil and gas industry and other sectors of the economy. This in our view will enhance further flow of foreign capital and technology in the country and intensify exploration and make more discoveries.
I wish to take this opportunity to assure all investors in the oil and gas industry and other sectors of the economy that Tanzania is ready and willing to do business with you. We are ready to facilitate your business and ensure that your investment is safe for our mutual benefits. We have the necessary institutional and regulatory frameworks in place. We will always endeavor to continue to improve the investment climate, provide efficient and effective regulatory framework and improve our infrastructure in order to reduce the costs of doing business. We intend to develop our human resource to match the requirements of the oil and gas industry. Our dream is to create a situation whereby the government, investors and the people of Tanzania will emerge as winners. There should be no loser in our envisaged set-up. In this regard, the spirit of partnership and cooperation is key.
Ladies and Gentlemen;
We all know that poorly planned petroleum operations may become an environmental hazard affecting people, land, water, plants and animals through pollution. Unfortunately, some of the negative effects of pollution are irreversible. It will be futile on our and an act of gross irresponsibility if we undertake poorly planned exploration activities that will have negative impacts to the environment. It will be adversely affect us and fortune generations. In this regard, it is important for oil and gas companies operating in Tanzania to abide by the operations guidelines and law. We want our resources to be a “blessing” not a “curse”.
While exploring and developing oil and gas resources, I urge you to seriously consider the emerging home and regional market which is growing fast. This market has a high demand of gas for power generation and industrialization. You must be aware that there is demand for gas here in Tanzania and in the region, therefore, plan to meet this demand first before considering to export to other markets elsewhere. Rest assured that the gas will not be sold at give away prices. Our ambition is to see to it that this important resource is playing an important role in promoting growth and development of our country. Let us work together towards realizing this dream.
After those many words, it is now my singular honour and pleasure to declare the historic 4th Licensing Round of the Deep Offshore and North Lake Tanganyika officially launched. I wish you all the best.
Thank you for kind attention.
- Oct 15, 2013
Hotuba ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye sherehe ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru, kumbukumbu ya ba...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge;
Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo;
Mheshimiwa Zainab Mohamed, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na watoto - Zanzibar;
Waheshimiwa Mawaziri na Nanaibu Mawaziri;
Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa Iringa;
Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi;
Makamu Mwenyekiti wa CCM (wa Mkoa) na Viongozi wa Vyama vya Siasa mliopo;Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Serikali wa Ngazi mbalimbali za Taifa na Mkoa;
Wageni Waalikwa;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana;
Shukrani
Niruhusuni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana tena mwaka huu kuadhimisha Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere na Wiki ya Vijana. Namshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Iringa, na viongozi wenzake pamoja na wananchi wa Iringa kwa kutupokea vizuri na ukarimu wenu. Pia nawapongeza kwa kukubali kuwa wenyeji wa maadhimisho haya. Kazi ya kuandaa sherehe kubwa kama hizi siyo jambo jepesi hata kidogo. Bahati nzuri mambo yamefana sana kama tunavyoshuhudia sote. Hongereni sana.
Pongezi Wizara
Ndugu wananchi;
Niruhusuni pia nitoe pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mheshimiwa Zainab Omary, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto wa Zanzibar kwa uongozi wao makini wa shughuli za Mbio za Mwenge. Kama tujuavyo shughuli za Mbio za Mwenge husimamiwa na Wizara zetu hizi mbili. Tunawapongeza kwa kazi nzuri waifanyayo. Ni ukweli ulio wazi kuwa kila mwaka tunashuhudia mambo yakiwa bora zaidi kuliko mwaka uliopita. Mcheza kwao hutunzwa. Hongereni sana.
Pamoja na Mawaziri napenda kuwatambua viongozi na wafanyakazi wote wa Wizara zetu mbili waliohusika na Mbio za Mwenge kwa kazi yao nzuri tunayojivunia sote. Aidha, nawapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, viongozi na watumishi wa Serikali zetu mbili na wajumbe wote wa kamati mbalimbali walioshiriki katika kuratibu Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu. Wamefanya kazi nzuri inayostahili kupongezwa na kila mmoja wetu.
Kwa namna ya pekee nawapongeza ndugu Juma Ali Sumai, kiongozi wa Mbio za Mwenge na Wakimbiza Mwenge wenzake kwa kutimiza kwa ufanisi wa hali ya juu jukumu kubwa na zito la kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchi nzima. Nawapa pole nyingi kwa changamoto mbalimbali walizokumbana nazo katika safari ya kilomita nyingi. Kazi hiyo wameimaliza salama na leo wameukabidhi Mwenge ukiwa salama. Nawapongeza sana kwa kuufikisha ujumbe wa Mwenge kwa uhodari mkubwa.
Waheshimiwa Mawaziri;
Ndugu wananchi;
Nafurahi kusikia kuwa kama ilivyokuwa miaka iliyopita, mwaka huu watu walijitokeza kwa wingi kila mahali Mwenge wa Uhuru ulipopita. Pia nimeambiwa ujumbe wa Mwenge ulifikishwa kwa ufasaha na kwamba umepokelewa vizuri. Miradi mingi ya maendeleo imezinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa wananchi wa Tanzania kwa ushiriki wao mzuri katika Mbio za Mwenge. Ushiriki wao ni kielelezo tosha cha kutambua umuhimu wa Mwenge wa Uhuru na cha moyo wa uzalendo kwa nchi yetu na kuwaenzi waasisi wa taifa letu. Kwa niaba ya Serikali nawahakikishia kuwa tutaendelea kuwahimiza viongozi wa ngazi mbalimbali kuhakikisha kuwa miradi yote iliyozinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru inaendelea kutekelezwa kama ilivyokusudiwa.
Kwa namna ya pekee nawapongeza waandishi na vyombo vya habari kwa kuwa nasi bega kwa bega kuhamasisha watu na kueneza ujumbe wa Mwenge. Mchango wao umesaidia sana kufanikisha malengo ya Mbio za Mwenge kwani siku zote wapotoshaji hawakosekani.
Kumbukumbu ya Baba wa Taifa
Ndugu Wananchi;
Kama mjuavyo siku ya kilele cha Mbio za Mwenge pia ni siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa letu la Tanzania kilichotokea miaka 14 iliyopita. Ni siku ambayo tunawajibika kukumbuka mema mengi aliyoifanyia nchi yetu, mafundisho yake na urithi aliotuachia. Nia yetu ni kutaka watu wasimsahau kiongozi wetu huyu maalum na muhimu sana katika historia ya nchi yetu.
Miongoni mwa mambo ya kukumbuka hasa wakati huu wa Mchakato wa Katiba Mpya ni (jambo la busara kutumia muda wetu) kujikumbusha mawazo ya Mwalimu kuhusu umoja wa nchi yetu pamoja na Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Hotuba zake na maandishi yake kuhusu mambo hayo yana mafundisho mengi mazuri ambayo tukiyaelewa vyema na kuyazingatia yatatusaidia sana katika mjadala na ukamilishaji wa mchakato wa Katiba mpya.
Mimi naamini fikra za Mwalimu na mtazamo wake kuhusu umoja wetu na Muungano bado vina maana hata leo. Tujiepushe na kuyapuuza tusije tukawa na Katiba itakayolibomoa taifa badala ya kulijenga. Ninaposema hivyo sipendi nieleweke kuwa sitaki mabadiliko ila napenda tuwe makini katika kufanya mabadiliko. Nataka tufanye mabadiliko yatakayotupeleka mbele na siyo kuturudisha nyuma.
Ndugu wananchi;
Pamoja na kuadhimisha siku ya kifo cha Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere), nadhani ni vyema pia tukawa tunaikumbuka siku ya kuzaliwa kwake yaani tarehe 13 Aprili (1922). Nisingependa kujiingiza katika mjadala wa siku ipi bora zaidi kwani zote ni siku muhimu katika historia ya maisha ya mwanadamu. Tofauti yake ni kuwa siku ya kuzaliwa ni ya furaha na siku ya kufa ni ya majonzi. Kama tutakubaliana tuikumbuke na siku yake ya kuzaliwa pengine siku hiyo tungeiita Nyerere Day. Tuiadhimishe siku hiyo kusheherekea maisha yake kwa kujadili kazi zake na kufanya shughuli mbalimbali kuenzi mambo mema aliyosimamia na kuifanyia nchi yetu na dunia kwa ujumla.
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013
Ndugu Wananchi;
Kama alivyoeleza Mheshimiwa Waziri kila mwaka Mbio za Mwenge wa Uhuru huwa na ujumbe maalum unaobebwa na kauli mbiu ya mwaka huo. Mwaka huu ujumbe ulikuwa “Watanzania ni Wamoja: Tusigawanywe kwa Msingi wa Tofauti Zetu za Dini, Itikadi, Rangi na Rasilimali”. Ujumbe huu ni muafaka kabisa hasa ukikumbuka misukosuko na majaribu makubwa nchi yetu iliyopitia mwaka huu. Hivyo kutumia Mbio za Mwenge wa Uhuru kukumbushana haja na hoja za kuziba nyufa zilizoanza kujitokeza ni jambo la busara sana. Ni jambo la kuungwa mkono na kila mwananchi na hasa kila mzalendo.
Bahati nzuri upepo huo mbaya umepita na tuombe usirudi tena. Hivi sasa hali ni shwari na Watanzania tunaendelea kushirikiana vizuri bila ya kubaguana kwa dini zetu, vyama vya siasa na kadhalika kama tulivyozoea kuishi miaka yote. Waliotaka kutufarakanisha hawakufanikiwa lakini, lazima tuwe makini kwani wanaweza kujaribu tena kutugawa ama kwa yale yale au mambo mengine.
Ndugu wananchi;
Kwa kweli nafarijika sana kuona Watanzania wakiendelea kukataa ushawishi na uchochezi wa kugawanywa kwa misingi ya dini au mambo mengine. Ndugu zangu naomba tuendelee hivyo na hayo ndiyo mafundisho mema na urithi aliotuachia Baba wa Taifa tunayemkumbuka leo. Tukigawanyika, nchi yetu itavurugika na sote tutakuwa tumeharibikiwa. Dhambi kubwa ya kubaguana kwa misingi yo yote ile ni kupotea kwa amani na utulivu. Bila amani, hatuwezi kuishi kwa furaha katika nchi yetu hii nzuri. Bila amani, jamii haiwezi kujishughulisha kwa ukamilifu na shughuli za kujiletea maendeleo. Amani ikituponyoka nchi yetu itayumba na hakuna atakayebaki salama.
Napenda kuwahakikishia wananchi wenzangu wote, kuwa sisi Serikalini tutaendelea kufanya kila tuwezavyo kujenga, kulinda na kudumisha umoja na mshikamano wetu ambao ndio msingi mkuu wa kuwepo kwa amani na utulivu nchini. Tutaendelea kukemea kwa nguvu zetu na uwezo wetu wote vitendo vinavyosababisha mmomonyoko wa umoja na mshikamano wetu. Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu au kikundi cha watu watakaojihusisha na vitendo vya kuvuruga amani ya nchi yetu. Naomba Watanzania wenzangu mtuelewe hivyo. Napenda kusisitiza na kuwasihi kuwa tuendelee kuaminiana, kuheshimiana na kuvumiliana pamoja na tofauti zetu.
Mapambano Dhidi ya UKIMWI
Ndugu wananchi;
Pamoja na ujumbe huu maridhawa ambao kimsingi ndiyo ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge tangu kuasisiwa kwake, mwaka huu wananchi waliendelea kuhimizwa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, rushwa na dawa za kulevya. Tangu ugonjwa wa UKIMWI uingie nchini kwetu mwaka 1983, inakadiriwa kuwa zaidi ya ndugu zetu milioni 2 wamepoteza maisha kutokana na maradhi haya. Hali kadhalika zaidi ya watoto milioni 1.3 wamekuwa yatima na watu zaidi ya milioni 1.5 wanaishi na VVU hivi sasa. Bahati mbaya karibu asilimia 65 ya hao ni wanawake.
Kitaifa, takwimu zinaonesha kuwa maambukizi ya UKIMWI yanazidi kupungua kutoka asilimia saba mwaka 2005 hadi asilimia 5.7 mwaka 2010 na kufikia asilimia 5.1 mwaka 2012. Hapa Iringa napo maambukizi yamekuwa yanapungua ingawaje bado yapo juu na kwamba ni Mkoa wa pili nchini kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi. Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi Mkoa wa Iringa ni asilimia 9.1, wanaume asilimia 6.9 na wanawake asilimia 10.9. Mkoa wa Njombe ndiyo unaoongoza ukiwa na asilimia 14.8.
Kwa sababu ya maradhi haya idadi ya watoto yatima ni kubwa katika mkoa huu (inakadiriwa kuwa waliopo ni 3400). Inahuzunisha sana kusikia au kuona baadhi ya watoto hawa wamelazimika kukatisha masomo yao baada ya wazazi wao kufariki ili kuwalea wadogo zao. Kwa ajili hiyo, wamelazimika kufanya kazi zisizostahili kufanywa na watu wa umri wao. Wapo pia wazee ambao kwa umri wao wanahitaji kulelewa lakini wamebaki peke yao na wakati mwingine wanalazimika kulea watoto walioachwa na watoto wao.
Ndugu wananchi;
Nilishaagiza viongozi siku za nyuma na leo narudia tena kuwa, tuwatambue watoto yatima kisha tutengeneze mipango thabiti ya kuwasaidia. Lengo letu hapa ni kutaka tuwawezesha kupata fursa ya kukua na kuishi kama watoto wengine. Jambo moja muhimu nililolisisitiza ni kuwa tuhakikishe kuwa vijana hawa wanapata elimu ambayo ndiyo ufunguo wa maisha yao.
Ndugu wananchi;
Tuongeze ari, nguvu na kasi ya kupambana na gonjwa hili hatari. Ni kweli tunapata mafanikio lakini hayatoshi. Kiwango bado ni cha juu mno. Nawaomba viongozi wa Serikali, dini, asasi za kijamii, wanasiasa na wananchi tuendelee kuhamasisha jamii kujiepusha na ugonjwa huu. Tuwahimize watu wajitokeze kupima wajue mustakabali wao, waepuke ngono nzembe na hasa hasa wawe na subira na waaminifu kwa ndoa zao au wapenzi wao. Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu wa kuelimisha na kuhakikisha kuwa dawa za kufubaza vijijidudu vya UKIMWI zinapatikana bure kwa waathirika waliofikia hatua ya kutumia dawa hizo.
Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa kuongeza juhudi maradufu kutokana na ukweli kwamba kiwango cha maambukizi kiko juu mno. Watu waendelee kujitokeza kwa wingi kupima kwa hiari ili kujua afya zao. Katika zoezi la kupima kwa hiari hapa Iringa, watu 388,071 wamejitokeza kupima. Jambo hili ni jema sana. Napenda pia kuchukua fursa hii kuwasihi akina mama wajawazito wawe mstari wa mbele kupima VVU ili wale walioathirika waitumie ipasavyo huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Huduma hii inamfanya mtoto anayezaliwa na mama aliyeathirika kuwa salama. Huduma hii ipo kote nchini na inatolewa katika hospitali zote za Serikali.
Ndugu wananchi;
Ombi langu maalum kwa wanaume, kote nchini ambao bado hawajafanyiwa tohara wajitokeze kwa wingi kufanya hivyo. Madaktari wanasema kuwa mwanaume aliyefanyiwa tohara anapunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuambukizwa VVU wakati wa kujamiiana. Naomba ieleweke kuwa sisemi mtu akifanyiwa tohara hapati UKIMWI. La hasha. Ninachosema ni kwamba ukimlinganisha na yule ambaye hakufanya hivyo, uwezekano wa kuambukizwa unapungua. Wanasema asiye na tohara ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata michubuko ambayo hurahisisha virusi kuingia kwenye mwili wake. Narudia kusisitiza mtu akipata tohara asidhani yuko salama kabisa. Watu wote lazima wachukue tahadhari stahiki.
Ndugu wananchi;
Ombi langu la pili ni kwa watu wanaotumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI wasiache kuzitumia. Wakiacha kwa sababu yo yote ile wanavipa vijidudu nafasi kujiimarisha na hivyo kuhatarisha maisha yao. Ombi langu la tatu ni kwa jamii kuendelea kuwasaidia na kuwahudumia wenzetu ambao wameathirika badala ya kuwanyanyapaa na kuwatenga. Na, muhimu zaidi tuwasaidie watoto yatima na wazee ambao wameachwa bila msaada wowote.
Nawataka viongozi wote katika ngazi mbalimbali washiriki kwa ukamilifu katika mapambano dhidi ya maradhi ya UKIMWI. Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Afya na TACAIDS waendelee kuongoza mapambano hayo bila kuchoka. Mimi bado naamini Tanzania bila UKIMWI inawezekana iwapo tutazingatia masharti ya kuepuka ugonjwa huu na kuwahudumia ipasavyo walioathirika. Ushindi hauko mbali sana.
Mapambano dhidi ya Rushwa
Ndugu wananchi;
Mwaka huu, katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wananchi waliendelea kukumbushwa wajibu wao katika kupambana na rushwa, kwa kauli mbiu isemayo “chukua hatua dhidi ya rushwa sasa”. Ujumbe huu unakwenda sambamba na juhudi za serikali za kupambana na rushwa nchini. Tunafahamu kuwa rushwa ni adui wa haki na kikwazo kikubwa cha maendeleo ya jamii na taifa. Nchi ikiwa imegubikwa na vitendo vya rushwa itakosa maendeleo stahiki na watu watadhulumiwa haki zao.
Hizo ndizo sababu kuu zilizoifanya serikali yetu ichukie rushwa na kuchukua hatua za kupambana na uovu huu, tangu nchi yetu ilipopata uhuru mpaka sasa. Kazi hiyo ngumu na yenye changamoto nyingi inaongozwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Serikali imechukua na itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha chombo hiki ili kiweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. Matokeo yake TAKUKURU sasa ina mtandao mpana zaidi. Ina ofisi kila Mkoa na kila Wilaya, watumishi wameongezeka na vitendea kazi pia.
Nafurahi kuona kuwa mafanikio ya kutia moyo yanaendelea kupatikana ingawaje kazi iliyo mbele yetu bado ni kubwa. Sote tunasoma na kusikia kupitia vyombo vya habari taarifa za watumishi wa serikali, taasisi za umma pamoja na watu wengine wanavyokamatwa na TAKUKURU kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa. Tangu mwaka 2006, kesi 63 zinazohusu rushwa kubwa zimefikishwa Mahakamani. Baadhi zimeisha na wahusika waliopatikana na hatia wameadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Zipo pia tulizoshindwa, ni sawa katika nchi inayoheshimu utawala wa sheria. Nyingine zinaendelea. Vile vile juhudi za TAKUKURU zimeokoa fedha nyingi za umma. Kwa mfano, kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani kati ya 2010 hadi 2013, zaidi ya shilingi bilioni 28 zimeokolewa ambazo zingeweza kunufaisha watu wachache wanaoendeleza vitendo vya rushwa badala ya taifa.
Naomba wananchi waendelee kutoa taarifa zitakazosaidia kuwatambua na kuwakamata watoaji na wapokeaji rushwa. Tukumbuke kuwa mafanikio katika mapambano haya hayategemei Serikali au TAKUKURU peke yake. Ni mapambano ambayo jamii ikijihusisha kwa ukamilifu ushindi mkubwa utapatikana. Yanatuhusu sote kwani tukishinda, matunda yake yatawafaidisha watu wote. Pia, napenda kutumia nafasi hii kutoa wito kwa taasisi na idara zote za serikali zinazohusika moja kwa moja katika vita dhidi ya rushwa zitimize ipasavyo wajibu wake. Aidha pakiwepo na ushirikiano mzuri na mshikamano wa dhati miongoni mwetu kwa hakika ushindi utapatikana. Tukifanya hivyo nina imani tutapata mafanikio makubwa zaidi tena kwa haraka.
Dawa za Kulevya
Ndugu Wananchi;
Tatizo la biashara na matumzi ya dawa za kulevya limeendelea kuwa moja ya changamoto kubwa zinazolikabili taifa letu. Serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa kupambana na changamoto hiyo. Yapo mafanikio yanayopatikana lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya mbele yetu. Ukubwa wa kazi hiyo unaletwa na ule ukweli kwamba watu wanaohusika ni wengi na wanazidi kuongezeka kila kukicha kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka. Isitoshe wakati wote washiriki wake wanabuni mbinu mpya za kusafirisha, kusambaza na kuuza dawa hizo haramu. Pia ni kazi hatari kwani wapambanaji kupoteza maisha si jambo la ajabu.
Pamoja na changamoto hizo, kwa vile matumizi ya dawa za kulevya yana athari mbaya kwa watu wanaotumia na jamii kwa ujumla, Serikali haitachoka kufanya kila tuwezalo kupambana na uhalifu huu mpaka ushindi upatikane. Wakibadili mbinu na sisi tutabadili maarifa ya uchunguzi na utambuzi mpaka tuwapate. Tutawahami ipasavyo watu wanaojitolea muhanga kupambana na uovu huu. Mafanikio yanaendelea kupatikana. Kwa mfano, kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka huu (2013) watu 2000 (wafanya biashara na watumiaji wa dawa za kulevya) wamekamatwa na aina mbalimbali ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kilo 681 za dawa hatari ya heroine, zimekamatwa.
Watu hao kama wasingekamatwa wangeendelea kuuza na kusambaza dawa za kulevya na kuathiri maelfu ya watu na hasa vijana ambao ni nguvu kazi muhimu ya taifa letu na warithi wa jamii na taifa wa kesho. Inatia uchungu sana kuona kuwa tegemeo letu hilo linaangamizwa na watu wachache wenye uroho usio na kifani wa kujipatia utajiri wa haraka, tena kwa gharama yoyote ile.
Ndugu wananchi;
Kwa niaba yenu, napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa viongozi na wafanyakazi wote wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya na vyombo vingine vya dola kwa kazi kubwa na nzuri inayoendelea kufanyika ya kukabiliana na tatizo hili. Katika mapambano yetu tunashirikiana na nchi na taasisi za nchi mbalimbali duniani. Hivyo basi nazipongeza kwa dhati nchi na taasisi hizo rafiki kwa ushirikiano wao ambao umetusaidia kupata mafanikio haya kiasi tunayojivunia leo. Naomba ushirikiano huu uendelee kwani umetusaidia kwa namna nyingi na umekuwa wa manufaa makubwa.
Ndugu wananchi;
Nilishawahi kusema siku za nyuma kuwa ni makusudio yangu na ya serikali kuanzisha chombo chenye uwezo na nguvu kubwa zaidi ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya nchini. Mchakato wa kuunda chombo hicho umeanza na unaendelea vizuri. Hivi sasa tunayo Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya. Chombo hicho kipya kitakuwa na nguvu kubwa zaidi kuliko Tume na hata kuliko kikosi kazi cha vyombo vyote vya dola nilichokiunda kuipa Tume meno.
Ndugu wananchi;
Ili juhudi hizo zifanikiwe na ushindi upatikane itategemea sana msaada, ushirikiano na ushiriki wa wananchi. Nawaomba sana ndugu zangu wananchi wenzangu mshirikiane na vyombo vya dola katika kupambana na usafirishaji, uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya. Baadhi yenu mnawajua watu wanaojihusisha na biashara hii haramu. Watajeni washughulikiwe ipasavyo.
Wiki ya Vijana
Ndugu wananchi;
Kama nilivyosema awali leo pia tunaadhimisha wiki ya vijana. Nimepata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho ya vijana ili kuona shughuli wanazozifanya. Nimefurahi na kufarijika sana na kile nilichokiona. Vijana wanafanya kazi nzuri na kwa kweli ni uamuzi wa busara kuwashirikisha katika sherehe hizi kwani wanapata fursa ya kuonesha kazi wanazozifanya katika kuboresha maisha yao na kuleta maendeleo ya taifa. Hii pia ni nafasi nzuri kwa vijana kukutana, kufahamiana na kubadilishana mawazo, ujuzi na taarifa muhimu zinazohusu maisha na maendeleo yao. Kwa kuzingatia umuhimu na faida ya maonesho haya, ni vyema kuangalia uwezekano wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana yakafanyika katika ngazi ya Mikoa na kuhitimishwa Kitaifa kama tulivyofanya leo.
Ndugu wananchi;
Mimi na wenzangu Serikalini tunatambua na kuthamini sana nafasi na mchango wa vijana katika kuchochea maendeleo ya nchi yetu. Ndio maana Serikali inawekeza sana katika elimu na mafunzo yao. Ndiyo maana pia Serikali imeamua katika mwaka huu wa fedha kuongeza uwezo wa bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili iweze kuwahudumia vijana vizuri zaidi. Tutaendelea kuongeza bajeti hiyo ili Wizara iweze kuwaongezea vijana mitaji ya biashara kupitia Mfuko wa Taifa wa Maendeleo ya Vijana.
Nimefurahi kumsikia Mheshimiwa Waziri akiahidi hapa kwamba baadhi ya vijana walioshiriki katika maonesho niliyoyaona leo watafikiriwa kupewa mikopo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa. Nawasihi vijana watakaopata mikopo kupitia Mfuko huu pamoja na mifuko mingine ya uwezeshaji wahakikishe wanaitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa na kuirejesha kwa wakati ili wengine nao wapate.
Maendeleo ya Mkoa wa Iringa
Ndugu wananchi;
Jana jioni nilipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Iringa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dokta Christine Ishengoma. Natoa pongezi nyingi kwa wananchi wa Iringa kwa juhudi zenu na mafanikio mnayoyapata katika kujiletea maendeleo. Mkoa umeendelea kuwa wa kutegemewa katika kulipatia taifa chakula hasa mahindi na sasa mwelekeo ni mzuri kwa mazao ya chai, mpunga, mboga na matunda. Nawaomba muendelee na juhudi zenu. Ongezeni maarifa na matumizi ya zana za kisasa na pembejeo za kilimo ili tija iongezeke mpate mavuno mengi zaidi. Mtatosheleza mahitaji yenu na mtapata ziada kubwa itakayotumika kwingineko nchini na hata kuuzwa nje ya nchi. Sisi katika Serikali tutaendelea kuwasaidia kwa upande wa upatikanaji wa pembejeo, zana za kilimo, masoko, huduma mbalimbali zikiwemo za ugani, fedha na kadhalika. Mkoa wa Iringa utanufaika kupitia Mpango wetu wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now) na SAGCOT.
Ndugu wananchi;
Serikali itaendelea kununua mahindi ya wakulima kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula. Hata hivyo ni vyema nikaeleza wazi kuwa Hifadhi ya Taifa ya Chakula haitanunua mahindi yote yaliyovunwa nchini. Ukomo wetu kwa sasa ni tani 250,000 lakini tunaendelea kupanua uwezo wa maghala hadi kufikia tani 400,000 ifikapo mwaka 2015. Tayari Hifadhi ya Taifa wameshanunua tani 209,000 hivyo bado tani 41,000. Hivyo nashauri wenzetu wa sekta binafsi nao wajitokeze kununua mahindi ya wakulima.
Kwa kuwa hakuna kizuizi cha kuuza nje wanaweza kufanya hivyo wakipenda. Hata hivyo, sisi tungependa kwanza wauze hapa nchini. Naomba ieleweke kuwa hatutawauzia watu akiba yetu ya mahindi katika Hifadhi ya Taifa ya Chakula kwa ajili ya kuuza nje.
Ndugu wananchi;
Pamoja na kuendeleza kilimo katika Mkoa wa Iringa, tutaendelea kuboresha barabara, na huduma za umeme, maji, elimu na afya. Ninyi ni mashahidi kwamba utekelezaji wa ahadi ya kujenga barabara ya lami kutoka Iringa hadi Dodoma unakwenda vizuri na ukarabati wa barabara ya Morogoro – Tunduma kupitia Iringa na Mbeya umekamilika. Tunajipanga kutekeleza ahadi zetu kwa baadhi ya barabara za Mkoa huu.
Kwa upande wa umeme vijijini tunaendelea kuvipatia umeme vijiji 38 vya Mkoa huu na wakati huo huo tunajiandaa kuvipatia umeme vijiji vingine 86. Tutaendelea kuongeza upatikanaji wa maji vijijini na mijini. Aidha, tumeanza kutekeleza mkakati kabambe wa kuboresha elimu kwa shabaha ya kutoa fursa ya elimu kwa vijana wetu wengi na kuongeza kiwango cha ufaulu. Haya yote tunayafanya chini ya mkakati mpya wa kupata Matokeo Makubwa Sasa. Tutaongeza mara dufu juhudi za kuboresha huduma ya afya.
Hitimisho
Ndugu wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu niwakumbushe Watanzania wenzangu kuwa mwaka ujao ni wa aina yake katika nchi yetu. Kwanza tunasherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, pili, tunasherehekea miaka 50 ya Muungano. Na tatu, kama mambo yatakwenda sawa tutapata Katiba Mpya. Niwaombe Watanzania wenzangu tujiandae vyema kufanikisha mambo yetu hayo matatu ya kihistoria. Naomba nimalize kwa kuwashukuru tena wananchi na viongozi wa Mkoa wa Iringa kwa kufanikisha sherehe hii muhimu. Nawashukuru pia wadau mbalimbali ambao wamechangia kwa hali na mali kufanya sherehe hizi zifanikiwe na kufana sana kama hivi. Napenda kutumia nafasi hii pia kuwatakiwa ndugu zetu Waislamu na Watanzania wenzangu wote heri ya Sikukuu ya Idd El Hajj.
Baada ya kusema hayo sasa natamka rasmi kwamba shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana kwa mwaka 2013 zimefikia kilele chake.
Asante sana kwa kunisikiliza.
- Oct 09, 2013
Hotuba ya Rais Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wananchi, Tarehe 4 Oktoba, 2013
Soma zaidiHotuba
Ndugu Wananchi;
Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza mwezi Septemba salama na kuwasiliana kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri. Naomba radhi kuzungumza nanyi siku ya leo kwa sababu nilikuwa safari na nilirejea jioni ya tarehe 30 Septemba, 2013. Awali nilifikiria nisiseme, nisubiri mwisho wa mwezi wa Oktoba. Lakini, baada ya kupata taarifa ya yaliyojiri, nimeshauriwa na nimekubali angalau niyasemee baadhi ya mambo huenda itasaidia. Niwieni radhi nisipoyasemea baadhi ya mambo siyo kwa kuyapuuza, bali kwa kuepuka hotuba kuwa ndefu mno. Nitayatafutia mahali pengine pa kuyasemea.
Uhusiano na Rwanda
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi wa Julai, nilizungumzia hali ya uhusiano wetu na Rwanda kutokuwa mzuri na tatizo la ujambazi na wahamiaji haramu katika Mikoa ya Kigoma, Geita na Kagera. Nafurahi kusema kuwa kwa yote mawili kuna maendeleo ya kutia moyo.
Tarehe 5 Septemba, 2013, nilikutana na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Paul Kagame waRwandamjiniKampala. Tuliitumia fursa ya ushiriki wetu katika Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia uhusiano baina yetu na nchi zetu. Mazungumzo yalikuwa mazuri na sote tulikubaliana kuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Kwa sababu hiyo tulielewana kuwa tutengeneze mazingira yatakayosaidia kutuliza hali na kurudisha nchi zetu katika uhusiano mwema kama ilivyokuwa siku zote. Nawaomba ndugu zangu hususan wanasiasa, watumishi wa umma, wanahabari na wenye mitandao ya kijamii na blog na wananchi kwa ujumla tusaidie kuimarisha uhusiano mwema baina ya Rwanda na Tanzania na watu wake.
Majambazi na Wahamiaji Haramu
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba hiyo pia nilisema kuwa tutachukua hatua thabiti dhidi ya majambazi na wageni wanaoishi nchini bila ya kuzingatia taratibu zinazohusika. Niliwataka majambazi wajisalimishe wao na silaha zao kwa hiari. Wale wanaoishi nchini bila ya kuwa na kibali halali wahalalishe ukaazi wao au warejee makwao. Nilitoa siku 14 kuanzia tarehe 29 Agosti, 2013 wafanye hivyo kwani baada ya hapo tungeanzisha operesheni maalum ya kushughulika na watu wa makundi yote mawili.
Ndugu Wananchi;
Kumekuwepo na mafanikio ya kutia moyo. Kwa upande wa wahamiaji wanaoishi nchini kinyume cha sheria watu wapatao 21,254 waliondoka kwa hiari. Hali kadhalika zaidi ya ng’ombe 8,000 waliondolewa na silaha 102 zilisalimishwa. Baada ya operesheni kuanza tarehe 6 Septemba, 2013 na kumalizika tarehe 20 Septemba, 2013, wahamiaji haramu 12,828 walirejeshwa makwao na watuhumiwa 279 wa unyang’anyi wa kutumia silaha walikamatwa. Aidha, mabomu 10 ya kutupa kwa mkono (offensive hand grenades), silaha 80, risasi 780 na mitambo 2 ya kutengeneza magobole vilikamatwa. Pia, ng’ombe 8,226 walikamatwa wakichungwa katika mapori ya hifadhi. Kwa upande wa mazao ya misitu, mbao 2,105 zilikamatwa pamoja na nyara mbalimbali za Serikali.
Ndugu Wananchi;
Agizo la kuwataka watu wanaoishi nchini isivyo halali wahalalishe ukaazi wao au waondoke kwa hiari au wataondolewa lilipotoshwa hasa na vyombo vya habari vya nje ya Tanzania. Walikuwa wanadai eti Tanzaniailikuwa inafukuza wakimbizi. Madai hayo si ya kweli hata kidogo. Hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2013 wakimbizi 68,711 walikuwepo kwenye Kambi ya Nyarugusu, Mkoani Kigoma. Hakuna mkimbizi ye yote aliyetakiwa kuondoka. Ukweli ni kwamba hakuna mtu ye yote kati ya wale watu walioondoka kwa hiari au kusaidiwa kuondoka wakati wa operesheni ambaye ni mkimbizi. Kama ingekuwa hivyo, wa kwanza kulalamika wangekuwa wenzetu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa. Bahati nzuri jambo hilo halikutokea.
Ndugu Wananchi;
Yalikuwepo pia madai kwamba tunawaonea na kuwatesa watu walioishi nchini miaka mingi. Ati iweje sasa ndiyo waambiwe kuwa siyo raia. Siku zote Serikali ilikuwa wapi? Uraia haupatikani kwa kuishi nchi ya kigeni kwa miaka mingi. Unapatikana kwa kutimiza masharti ya kuomba na kupewa uraia. Kama mtu hakufanya hivyo anabaki kuwa raia wa nchi aliyotoka au walikotoka wazazi wake. Ipo mifano ya watu mashuhuri ambao walilazimika kuachia nyadhifa zao baada ya kugundulika kuwa siyo raia. Hawakuwa wanaonewa, ndiyo matakwa ya Katiba na Sheria za nchi yetu.
Ndugu Wananchi;
Katika kutekeleza operesheni hii niliagiza kuwa wale watu ambao wameishi hapa nchini miaka mingi ambao wana nyumba, mashamba au mali mbalimbali au wameoa au kuolewa na wana watoto au hata wajukuu waelekezwe kuhalalisha ukaazi wao. Iwapo watakataa kufanya hivyo basi wasaidiwe kurejea kwao. Pia niliagiza watu wasiporwe mali zao wala kudhulumiwa. Sijapata taarifa ya kufanyika kinyume na maelekezo yangu. Lakini kama wapo watu waliotendewa tofauti, taarifa itolewe kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa au hata Ofisi ya Rais ili hatua zipasazo zichukuliwe. Hatutaki watu wadhulumiwe au kuonewa.
Napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Waziri wa Ulinzi na JKT, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi kwa uongozi wao mzuri katika zoezi hili. Pia, nawapongeza Makamanda na askari wa JWTZ na Polisi pamoja na maafisa wa Idara ya Uhamiaji, Idara ya Mifugo, Idara ya Wanyamapori, Idara ya Misitu na Idara nyinginezo za Serikali kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya. Najua awamu ya kwanza imeisha tarehe 20 Septemba, 2013 na kama nilivyosema kuwa safari hii operesheni itakuwa endelevu, muda si mrefu awamu ya pili itafuata. Nawaomba waendelee kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na nidhamu ya hali ya juu.
Ziara ya Canada na Marekani
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 17 na 28 Septemba, 2013 nilifanya ziara ya kikazi katika nchi zaCanadana Marekani. Nchini Canada nilitembelea Chuo Kikuu cha Guelph ambapo nilitunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua jitihada zetu tuzifanyazo kujiletea maendeleo na mafanikio ya kutia moyo tunayoendelea kupata licha ya changamoto zinazotukabili. Katika mazungumzo yangu na uongozi wa chuo hicho wamekubali kuwa na ushirikiano wa karibu na Wizara zinazohusika na Elimu, Kilimo na Mifugo pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma. Nimewataka Mawaziri wa Wizara hizo na viongozi wa vyuo hivyo kuchangamkia fursa hiyo bila kuchelewa.
Ndugu Wananchi;
Nchini Marekani nilikutana na kuzungumza na maafisa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya nchi hiyo wakiwemo Rais Barack Obama na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Marekani. Mazungumzo yetu yalilenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zetu na mambo yalienda vizuri. Wote walituhakikishia kuwa mambo tuliyoyazungumza na kukubaliana na Rais Barack Obama wakati wa ziara yake nchini yanaendelea kufanyiwa kazi. Miongoni mwa hayo maombi yetu ya kupatiwa vitabu milioni 2.4 vya sayansi na hisabati yamekubaliwa na utekelezaji umeanza. Upatikanaji wa vitabu hivyo utamwezesha kila mwanafunzi wa sekondari kuwa na kitabu chake.
Ndugu Wananchi;
Jambo lingine kubwa na la faraja kwetu ni kuwa mapendekezo yetu ya miradi ya umeme na barabara za vijijini za kugharamiwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lao la Changamoto za Milenia yamepokelewa vizuri. Kinachosubiriwa ni miradi ipi itakubaliwa na Bodi ya MCC na kiasi gani cha fedha kitatengwa na Bunge la Marekani kwa ajili hiyo.
Tuzo ya Uhifadhi
Jambo lingine muhimu katika safari yangu ya Marekani ni kutunukiwa tuzo na “International Congressional Conservation Foundation” kwa kutambua juhudi zetu katika kuhifadhi wanyamaporina mafanikio tuliyoyapata. Licha ya changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo, tuzo hii imetupa moyo wa kuongeza nguvu katika jitihada tunazozifanya sasa kupambana na ujangili na matatizo mengine ya uhifadhi wa wanyama na misitu.
Ndugu Wananchi;
Kilichotupa moyo zaidi ni kauli za utayari wa kutusaidia katika mapambano hayo zilizotolewa wakati wa kupewa tuzo na katika mkutano wa mfuko wa Maendeleo wa Clinton na katika mkutano maalum wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo duniani.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Ndugu Wananchi;
Shabaha kuu ya safari yangu ya Marekani ilikuwa kuhudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaoendelea jijini New York mpaka Desemba, 2013. Mada kuu ya mkutano wa mwaka huu ni kuandaa agenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 yaani: Post 2015 Development Agenda: Setting the Stage. Kama mtakavyokumbuka Malengo ya Milenia yaliyoamuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2000, yanafikia ukomo wa utekelezaji wake mwaka 2015.
Katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu mjadala umehusu nini kifanyike baada ya mwaka 2015. Hata hivyo, mjadala huo unaanza kwa kufanya tathmini ya utekelezaji wa yale Malengo Manane ya Milenia ya mwaka 2000 umefikia wapi mpaka sasa na utafikia wapi mwaka 2015 kwa kila nchi na kwa dunia kwa ujumla. Tathmini ya jumla inaonesha kuwa kumekuwepo na jitihada kubwa ya kutekeleza malengo haya katika kila nchi. Yapo malengo ambayo utekelezaji wake umefikia shabaha hivi sasa na yapo ambayo upo uwezekano wa shabaha kufikiwa ifikapo mwaka 2015. Vile vile yapo ambayo shabaha haitafikiwa.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wetu, Tanzania, tumefikia shabaha katika mambo yafuatayo:
(1) Lengo la Milenia namba 2 kuhusu uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule ya msingi;
(2) Lengo la Milenia namba 3 hasa kuhusu usawa wa kijinsia katika Shule za Msingi na Sekondari. Ukweli ni kwamba, wasichana wanaanza kuwa wengi kuliko wavulana. Hatujafikia shabaha kwa upande wa usawa wa kijinsia katika elimu ya juu na ni vigumu kulifikia ifikapo 2015. Pia hatujafikia lengo kwa upande wa usawa wa Wabunge wanawake na wanaume. Hata hivyo, kwa kutumia mchakato wa Katiba unaoendelea sasa tunaweza kufikia lengo katika uchaguzi wa 2015 iwapo tutaamua iwe hivyo;
(3) Lengo la Milenia namba 4 kuhusu kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na wale wenye umri chini ya miaka mitano;
(4) Tumefikia shabaha kwa Lengo la Milenia Namba 6 kuhusu kupunguza maambukizi ya UKIMWI; na
(5) Kwa upande wa lengo namba 7 kuhusu mazingira, tumefikia shabaha kwa upande wa upatikanaji wa maji mijini. Bado tuko nyuma kwa maji vijijini ingawaje tunaweza kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 kama tutaendeleza uwekezaji tulioamua kufanya katika bajeti ya mwaka huu. Lakini, hatutaweza kufikia shabaha kwa upande wa usafi wa mazingira mijini na vijijini ifikapo mwaka 2015. Safari bado ndefu sana.
Ndugu Wananchi;
Malengo ya Milenia namba 1 na namba 5 ambayo bado tuko nyuma sana ya shabaha hatutafikia lengo ifikapo 2015. Tumeendelea kutekeleza lengo la Milenia namba 1 kuhusu kupunguza umaskini na njaa kwa zaidi ya nusu kutoka kiwango cha mwaka 2000. Hatua tunazochukua kuleta mageuzi katika kilimo zina lengo la kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza mapato ya wakulima. Mafanikio yanaanza kuonekana lakini si ya kiwango cha kutufikisha kwenye lengo ifikapo mwaka 2015. Tunao, pia, mpango wa kupanua programu ya TASAF ya Conditional Cash Transfer ili tuwafikie watu wengi maskini. Hata kama tutafanikiwa kuutekeleza mapema mpango huu utatusogeza sana mbele lakini bado tutakuwa chini ya lengo kwa upande wa kupunguza umaskini ifikapo 2015.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Lengo la Milenia namba 5, kuhusu afya ya kina mama wajawazito bado tuko nyuma katika kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na kuongeza idadi ya wajawazito wanaojifungua chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya. Hatutaweza kufikia shabaha ifikapo mwaka 2015. Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (2007 – 2017) una nia ya kukabiliana na matatizo haya. Tumeongeza ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali, tumeboresha upatikanaji wa dawa na tumepanua sana mafunzo ya madaktari, wauguzi na wakunga mambo ambayo yamesaidia kutufikisha hatua tuliyopiga mpaka sasa. Naamini juhudi zetu tukiziendeleza zitatusogeza mbele zaidi ingawaje bado tutakuwa chini ya lengo. Miaka michache ijayo, tatizo hili nalo litakuwa historia.
Ndugu Wananchi;
Lengo la Milenia namba 8 linazihusu nchi tajiri kuongeza michango yao kusaidia nchi zinazoendelea kutekeleza Malengo ya Milenia. Bahati mbayasanamataifa tajiri hayajafikia viwango wanavyotarajiwa kutoa na hata vile wanavyoahidi wenyewe kutoa katika majukwaa mbalimbali. Kama wangetimiza ahadi zao, sura ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia ingekuwa tofauti kabisa.
Ndugu Wananchi;
Hiyo ndiyo hali ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia hapa nchini. Hakuna nchi ye yote duniani iliyofanikiwa kutekeleza shabaha za malengo yote kwa ukamilifu. Ushauri wa viongozi wote waliozungumza ulitaka mataifa yaliyoendelea yatimize ahadi zao za kuchangia utekelezaji wa Malengo ya Milenia. Ilionekana suala la upatikanaji wa fedha halina budi kuangaliwa kwa makini sasa na baada ya mwaka 2015. Bila ya hivyo ufanisi utakuwa mdogo katika kuongeza kasi ya utekelezaji kwa pale paliposalia kufikia malengo ya 2015 na hata kwa Malengo ya baada ya mwaka 2015.
Mashambulizi ya Kigaidi ya Westgate, Nairobi
Ndugu Wananchi;
Wakati nikiwa safarini, tarehe 21 Septemba, 2013 kulitokea shambulilizi la kigaidi katika Jengo la Biashara la Westgate, huko Nairobi, Kenya. Watu 67 walipoteza maisha na zaidi ya 200 walijeruhiwa. Nilituma salamu za pole na rambirambi kwa Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wa Kenya na kuwahakikishia kuwa tupo pamoja nao katika wakati huu wa majonzi.
Nafahamu kuwa baada ya tukio hilo watu wengi hapa nchini wameingiwa na hofu kuhusu usalama wetu. Ni hofu ya msingi kwani tarehe 8 Agosti, 1998 Ubalozi wa Marekani hapa nchini ulishambuliwa na magaidi na ndugu zetu 11 wasio na hatia walipoteza maisha.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwafahamisha kuwa tangu shambulio la mwaka 1998, Serikali imekuwa inajenga uwezo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kupambana na ugaidi katika nyanja mbalimbali. Tunaendelea kujiimarisha bila kusita siku hadi siku. JWTZ, Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa ajili hiyo. Juhudi zetu hizo ndizo zinazotufanya tuwe salama hadi sasa.
Baada ya tukio la Kenya, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeimarisha mikakati yao maradufu. Pamoja na kujizatiti kwetu huko hatuwezi kusema kuwa tukio la kigaidi halitaweza kutokea nchini. Uhakika huo hatuna kwani hata mataifa makubwa na tajiri yameshambuliwa. Kilicho muhimu ni kuendelea kuchukua tahadhari na wananchi kusaidia ili vyombo vyetu vifanikiwe zaidi.
Hali kadhalika, tumewataka watu wote wenye shughuli zinazokusanya watu wengi kama vile maduka, maofisi, mahoteli, migahawa n.k. waweke kamera za ulinzi nje na ndani ya maeneo yao. Pia waangalie uwezekano wa kuweka vifaa vya upekuzi (metal detectors and x-rays). Najua watu wanaweza kulalamikia usumbufu au gharama, lakini gharama na hasara ya kushambuliwa ni kubwa zaidi kuliko ya usumbufu huo.
Ndugu Wananchi;
Nawaomba muendelee kufanya shughuli zenu bila ya hofu ingawaje msiache kuwa makini na kuchukua tahadhari. Watu watoe taarifa kwa vyombo vya usalama wanapoona mtu au watu au kitu cha kutilia shaka. Ni muhimu kwa usalama wake, wa kila mtu, jamii na taifa. Maafisa husika wa vyombo vya ulinzi na usalama wataendelea kuelimisha umma kuhusu hatua mbalimbali za tahadhari za kuchukua. Sisi Serikalini tumejipanga kuchukua hatua zaidi kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu na watu wake.
Mchakato wa Katiba Mpya
Ndugu Wananchi;
Kamamtakavyokumbuka, Bunge lilitunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Novemba, 2011. Sheria hii imeweka mchakato mzima wa kupata Katiba hiyo na kuunda taasisi zake. Mwezi Mei, 2012, Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa na imekamilisha hatua tatu muhimu katika mchakato huo. Hatua hizo ni kupokea maoni ya wananchi, kutayarisha rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya na kupokea maoni ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na ya taasisi. Hivi sasa Tume inaandaa mapendekezo ya Rasimu ya Pili ya Katiba itakayopelekwa kwenye Bunge Maalum. Baada ya tafakuri zake, Bunge Maalum litatoa rasimu ya mwisho ya Katiba ambayo itapelekwa kwa wananchi kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kupitia kura ya maoni. Baada ya hatua hiyo, ndipo tutakapokuwa tumepata Katiba Mpya.
Ndugu Wananchi;
Baada ya Bunge la Novemba, 2011 kupitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kulikuwepo na madai ya kutaka sheria hiyo iboreshwe kutoka vyama vyote vya siasa vikiwemo vyama vya upinzani na Chama tawala. Majadiliano yalifanyika baina ya Serikali na vyama hivyo pamoja na shirikisho la asasi za kiraia. Makubaliano yalifikiwa kuwa marekebisho yafanyike kwa awamu. Awamu ya kwanza ihusishe Tume ya Mabadiliko ya Katiba kisha hapo yafanyike marekebisho yanayohusu Bunge Maalum na mwisho Kura ya Maoni.
Kama ilivyokuwa kwa mabadiliko yaliyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba, safari hii nayo vyama vya siasa vilitoa mapendekezo yao. Yalifanyika mazungumzo kati yao na Serikali na maelewano kufikiwa kuhusu maeneo ya kufanyiwa marekebisho. Serikali ilitayarisha rasimu ya Muswada na kuuwasilisha kwa wenzetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ndugu Wananchi;
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitoa mapendekezo yake na ushauri kwenye maeneo mawili. Kwanza kwamba uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum ufanywe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na kuafikiana na Rais wa Zanzibar. Pili walishauri kwamba kamaBunge Maalum litashindwa kufikia maamuzi ndani ya siku 70 zilizopendekezwa, liweze kuongezwa muda hadi kufikia siku 90. Maeneo mengine ya Muswada waliafikiana nayo.
Ndugu Wananchi;
Kwa kuzingatia utaratibu wa kutunga Sheria, Serikali ilifikisha Muswada kwa Spika wa Bunge ambaye nae aliuwasilisha kwenye Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala. Kama ilivyo ada, Kamati hiyo ilifanya vikao na wadau na kupokea maoni yao kuhusu Muswada. Nimeambiwa kulikuwa na mjadala wa kina na mapendekezo mazuri yalitolewa na wadau. Kisha hapo Wajumbe wa Kamati walikaa wenyewe kujadili Muswada walikuwepo pia Wabunge ambao si Wajumbe wa Kamati walioshiriki kwa vile Kanuni zinaruhusu. Nimeambiwa pia kwamba mjadala ulikuwa mpana na wa kina zaidi. Mapendekezo kadhaa yalitolewa na Wajumbe kuhusu vifungu mbalimbali vya Muswada.
Ndugu Wananchi;
Nimefahamishwa kuwa Wabunge wa vyama vyote walichangia na kwamba baadhi ya nyakati mambo yalipokuwa ugumu mawazo mazuri ya baadhi ya Wabunge wa upinzani yalisaidia kupata ufumbuzi. Nimeambiwa pia kwamba Wajumbe wa Kamati na upande wa Serikali walikubaliana kwa maeneo mengi isipokuwa machache ambayo walikubaliana kwa pamoja wayapeleke Bungeni ili Wabunge nao wayajadili na kuyapatia ufumbuzi.
Ndugu Wananchi;
Baada ya Kamati kumaliza kazi yake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Mathias Chikawe aliwasilisha Muswada Bungeni. Akafuatiwa na Mheshimiwa Gosbert Blandes kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kutoa maoni ya Kamati. Baadaye Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Tundu Lissu alitoa maoni yake.
Ndugu Zangu;
Baada ya watu hao watatu kutoa maoni yao ilitarajiwa kuwa Wabunge wangeanza kujadili Muswada. Naambiwa mambo hayakuwa hivyo. Badala yake kukazuka malumbano baina ya Spika na baadhi ya Wabunge wa Upinzani wakitaka Muswada usijadiliwe. Ilifikia wakati hoja hiyo ikabidi iamuliwe kwa kura ambapo ilishindwa. Katika hali isiyotarajiwa, Wabunge wote wa upinzani wakatoka nje ya Bunge isipokuwa wawili. Kitendo hicho kimewanyima Wabunge wengi wa upinzani fursa ya kutetea hoja zao walizozitoa kupitia hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani. Pia wamejinyima nafasi ya kusema mambo mengine wakati wa mjadala na Kamati ya Bunge zima.
Wabunge waliokuwepo waliendelea kuujadili Muswada na kutoa hoja na mapendekezo ya kuuboresha. Walifanya hivyo wakati wa mjadala na wakati wa kupitia kifungu kwa kifungu. Baadhi ya hoja na mapendekezo yalikubaliwa na mengine yalikataliwa. Miongoni mwa yaliyokubaliwa na Wabunge, kwa mfano, ni kuhusu elimu ya mtu atakayekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum na lile la ukomo wa uhai wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Ndugu Wananchi;
Kwa maoni yangu madai ya Kambi ya Upinzani yanazungumzika na hata baadhi yangeweza kukubalika kama Wabunge wake wangekuwepo Bungeni na kushiriki mchakato wote wa kujadili na kupitisha Miswada Bungeni. Bahati mbaya hawakuwepo, hivyo hapakuwepo na mtu wa kusema mawazo yao. Baada ya kupoteza fursa yao halali, kutaka kupata ufumbuzi nje ya Bunge ni jambo lisilowezekana. Haya ni masuala yanayohusu Bunge ambayo hujadiliwa na kuamuliwa Bungeni na si vinginevyo. Kuandamana nchi nzima au kuchukua hatua za kutotii sheria kama Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa Freeman Mbowe anavyotaka, hakutaleta mabadiliko wanayoyataka katika sheria hii. Naamini na wao wanautambua ukweli huo.
Ndugu Wananchi;
Kuna msemo wa wahenga kuwa “historia hujirudia”. Naomba hekima ziwaongoze viongozi wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na zituongoze sote kutumia utaratibu tulioutumia mwaka 2012. Kulipotokea mazingira kama haya pande zote zilikaa pamoja na kuzungumzia hoja moja baada ya nyingine na kukubaliana nini kifanyike na kifanyike vipi. Baada ya kuridhiana hatua zipasazo za kisheria na kanuni zilichukuliwa na kumaliza mzozo.
Ndugu Wananchi;
Kufanya kinyume cha hayo hakutaleta ufumbuzi wa mzozo huu. Tutaliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima. Tukikataa kufanya hayo Watanzania wanayo kila sababu ya kuhoji dhamira zetu na kutilia shaka nia zetu. Watakuwa na haki ya kuuliza nia ni hii yetu sote ya kupata Katiba Mpya kwa kutumia njia za kikatiba na kisheria au tuna dhamira nyingine iliyojifisha?
Kama dhamira yetu ni kutaka kupata Katiba mpya kwa mujibu wa Katiba na Sheria, ushauri wangu na rai kwa ndugu zetu wa CHADEMA, CUF na NCCR-Maguezi ni kuwa waachane na mipango ya maandamano na kufanya ghasia. Badala yake watumie njia halali zinazotambulika kikatiba na kisheria kujenga hoja za kufanya marekebisho wanayoyaona wao yanafaa kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Tukifanya hivyo tutakuwa tunajenga badala ya kubomoa. Tutaliponya taifa. Sisi katika Serikali tuko tayari.
Ndugu Wananchi;
Napenda pia kuzisemea baadhi ya hoja zilizotolewa na Kambi ya Upinzani. Kwanza kabisa nasema kuwa nimesikitishwa sana na madai na tuhuma za uongo eti katika uteuzi wa Tume ya Katiba sikuheshimu mapendekezo ya TEC, CCT na walemavu.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Siyo tu kauli hiyo ya Mheshimiwa Tundu Lissu ni uzushi na uongo mtupu bali pia ni ya unafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu. Nasema hivyo kwa sababu, sipendi kuamini kuwa Mheshimiwa Mbunge amesema yale kwa kutokufahamu ukweli au kwa bahati mbaya. Amesema yale kwa makusudi mazima ya kupotosha ukweli ili pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wale Wajumbe 166 wa Bunge Maalum.
Napenda ieleweke kuwa siishabikii kazi hiyo, lakini kwa kutimiza wajibu na maslahi ya taifa nikiagizwa na Sheria za nchi nitafanya. Nasema hivyo kwa sababu nafahamu ni kazi ngumu. Kama kazi ya uteuzi wa Wajumbe 30 wa Tume haikuwa rahisi hata kidogo, hii ya uteuzi wa watu 166 itakuwa ngumu zaidi. Ile ya Tume ilikuwa ngumu kwa namna mbili. Kwanza, kwamba taasisi zilizoomba na waombaji walikuwa wengi mno kuliko nafasi za kujaza yaani 15 Zanzibar na 15 Bara. Zanzibar ziliomba taasisi zaidi ya 60 na waombaji walikuwa zaidi ya 200 wakati Bara kulikuwa na taasisi zaidi ya 170 zikiwa na waombaji zaidi ya 500. Kupata watu 30 kutoka orodha kubwa kiasi hicho si mtihani mdogo. Pili kwamba tulitakiwa kuunda Tume inayoasili sura ya taifa, yaani watu wa nchi yetu kwa maeneo, vyama vya siasa, dini, wanawake, vijana, walemavu, wafanyakazi, wasomi, Wabunge, Wawakilishi, wanasheria, wafanyabiashara, wakulima, asasi za kiraia n.k.
Ndugu Wananchi;
Pamoja na changamoto hizo, lakini tulifanikiwa kuunda Tume iliyopokelewa vizuri na jamii na kufanya watu wengi hata wale ambao hawakuteuliwa wahisi kuwakilishwa. Tulifanyaje? Kwanza kabisa tulihakikisha kuwa tunapata wawakilishi wa vyama vya siasa vyenye wawakilishi Bungeni na kwenye Baraza la Wawakilishi na tunapata wawakilishi wa mashirika ya dini zetu kubwa yaani, TEC, CCT na BAKWATA. Ndiyo maana nikasema kuwa kwa Mheshimiwa Tundu Lisu kudai kuwa mapendekezo ya TEC na CCT hayakuheshimiwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu.
Baada ya hapo ndipo tukaangalia waombaji wa makundi na taasisi nyingine. Tulijitahidi sana kupata watu ambao wanawakilisha kundi zaidi ya moja. Tulifikiria hivyo kwa sababu ni ukweli ulio wazi kuwa si kila taasisi iliyoomba itapata mwakilishi kwani hata tungependa iwe hivyo nafasi hazikuwepo. Kwa kutumia utaratibu huu makundi mengi yamepata uwakilishi kutokana na watu waliopendekezwa na makundi mengi. Tumefanya kazi kubwa sana ya kuwianisha mambo na makundi ya maslahi mbalimbali nchini.
Ndiyo maana naiona mantiki ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishirikiana na Rais wa Zanzibar wa kuwateua Wajumbe wa Bunge Maalum. Dhana kuwa kila kikundi kiteue chenyewe watu ingefaa sana kama kungekuwepo na nafasi za kutosha kila kundi nchini. Hilo haliwezekani, labda tuwe na Bunge Maalum lisilokuwa na ukomo wa wajumbe.
Ndugu Wananchi;
Mimi na Rais wa Zanzibar tumekuwa tunajiuliza baada ya kazi ngumu na nzuri tuliyoifanya na iliyopongezwa na wengi ya kuteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba nini kilichoharibika sasa hata tuonekane hatuaminiki kuteua hawa 166? Kama ni kwa sababu za Mheshimiwa Tundu Lissu, nimeshasema hazina ukweli wowote. Ninapojiuliza kwa nini aseme uongo nashindwa kupata jibu linaloingia akilini. Wakati mwingine nafikiria kuwa ni hiana. Lakini nadhani ni hila za kisiasa zenye nia ya kutaka kupata watu wa kutetea maslahi ya chama chake. Kama hiyo ndiyo shabaha basi amekosea sana.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Hatutengenezi Katiba ya Chama fulani bali Katiba ya nchi, Katiba ya watu wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama ambao ndiyo wengi kuliko wote. Lazima tuongozwe na ukweli huo na tuwe na msimamo huo wakati wote. Lazima tukumbuke kuwa si watu wote wanaostahili au kuwa na sifa ambao wataomba na kupata nafasi ya kuwa Wajumbe, hivyo wale wachache watakao bahatika lazima wawasemee wote. Wanatakiwa kusikiliza na kuwakilisha mawazo ya wote hata wale wasiokuwa wa Chama chao au kundi lao.
Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri hii ndiyo sifa kubwa iliyooneshwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Wamewasimamia na kuwasemea watu wote bila ya kubagua. Natambua kuwepo kwa baadhi ya watu ambao hawafurahii msimamo huo na matokeo ya kazi yao. Watu hao kuwalaumu Wajumbe wa Tume kwa ajili hiyo ni kuwaonea na kutowatendea haki. Tunataka watakaokuwa Wajumbe wa Bunge Maalum nao waige mfano huu mzuri. Wajali maslahi mapana ya taifa letu na watu wake badala ya kujali yale ya taasisi zao au makundiyao.
Zanzibar Kutokushirikishwa
Ndugu Wanachi;
Nimeambiwa pia kuliwepo madai ya Zanzibar kutokushirikishwa ipasavyo. Nimeeleza kwa kiasi gani Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshirikishwa na kutoa maoni yake yaliyojumuishwa katika Muswada. Hivyo basi napata tabu kuyaelewa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa msingi wake nini! Labda kuna kitu sikuambiwa!
Nimeulizia kuhusu hoja ya Kamati kutokufanya vikao Zanzibar kusikiliza maoni ya wadau wa Zanzibar. Nimeambiwa kuwa Kanuni za Bunge hazina sharti hilo hivyo Kamati haistahili kulaumiwa. Kama hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe Bungeni ili Wabunge walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea kulauminiana isivyostahili. Hivyo basi, kuligeuza jambo hili kuwa ni suala la kukataa Muswada au kususia vikao vya Bunge au kufanya maandamano sidhani kama ni sawa.
Ndugu Wananchi;
Nimeambiwa pia kuwa kulikuwa na hoja ya kutaka idadi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar iwe sawa kama ilivyo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Sababu ya idadi ya Wajumbe wa Tume kuwa sawa inatokana na utaratibu wao wa kufikia uamuzi. Ni kwa maelewano ya wote (consensus) na siyo kwa kupiga kura. Ndiyo maana idadi imewekwa sawa ili sauti za pande zote zisikike sawia. Bunge Maalum lina sharti la kufanya uamuzi kwa theluthi mbili ya kura za kila upande kukubali. Bila ya hivyo hakuna uamuzi.
Hivyo basi, katika Bunge Maalum nguvu si uwingi wa kura ambazo upande fulani unaweza kupata bali ni ulinganifu sawa wa kura za kila upande peke yake. Huu ndiyo msingi unaotumika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi sasa kwa lengo la kulinda maslahi ya Zanzibar. Zanzibar ina Majimbo 50 ya uchaguzi na Tanzania Bara ina Majimbo 189, hivyo ukiamua kwa wingi kila wakati Wazanzibari watashindwa. Lakini, hapajakuwepo madai ya Zanzibar nao kutaka kuwa na idadi sawa ya majimbo kama Bara au kupunguza majimbo ya Bara yawe sawa na ya Zanzibar kwa sababu wingi si hoja. Msingi unaotumika ni kutoa nguvu sawa za uamuzi kwa kila upande wa Muungano wakati wa kuamua masuala ya Katiba. Hakuna mdogo wala mkubwa, wote wako sawa. Hakuna mdogo kumezwa na mkubwa. Ndiyo msingi unaopendekezwa kutumika kwenye Bunge Maalum hivyo hakuna kitakachoharibika kwa idadi ya Wajumbe kutokukulingana. Nadhani inafaa ibaki ilivyo. Lakini kama Wabunge wataamua waongeze idadi itakuwa kwa sababu nyingine siyo hii ya mfano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Ndugu Wananchi;
Katika orodha ya madai ya ndugu zetu wa upinzani lipo suala la uhai wa Tume ya Katiba. Wanataka usiishe wanapokabidhi rasimu ya pili kwa Bunge Maalum bali waendelee kuwepo mpaka mwisho wa mchakato. Nimeulizia ilikuwaje? Nimeelezwa kuwa jambo hili halitokani na mapendekezo ya Serikali wala ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala. Limetokana na pendekezo la Mbunge katika Bunge wakati wa kupitia vifungu na kuungwa mkono na Wabunge wengi. Kwa hiyo kuilaumu Serikali si haki. Serikali inaweza kuwa mshirika katika hoja hii.
Nami naiona hoja ya Wajumbe wa Tume kuwa na wajibu wakati wa Bunge Maalum hasa wa kusaidia kufafanua mapendekezo ya Tume. Je ushiriki huo uwe vipi? Je ni Wajumbe wote au baadhi yao ni jambo linaloweza kujadiliwa.
Ndugu Wananchi;
Naomba nimalizie kwa kuwasihi viongozi wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kuongozwa na hekima iliyotumika wakati tulipokuwa na tatizo linalofana na hili kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Mimi naamini kama iliwezekana kufanikisha mambo wakati ule inaweza kufanya hivyo hata safari hii. Itatufikisha pale tunapopataka salama salimini bila maandamano, kushupaliana au uvunjifu wa amani. Kupanga ni kuchagua, naomba sote, mmoja mmoja na kwa umoja wetu tuchague njia ya mazungumzo na maelewano kwani itaihakikishia nchi yetu amani, usalama na utulivu. Tukifanya hivyo historia itatuhukumu kwa wema.
Mungu IbarikiTanzania. Nawashukurusanakwa kunisikiliza.
- Sep 28, 2013
Hotuba ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wa 68, New York, Seotemba 27, 2...
Soma zaidiHotuba
Mr. President;
Mr. Secretary-General;
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
Allow me to begin by congratulating you Mr. President on your well-deserved election to steer the affairs of 68th General Assembly of our esteemed organisation. As I congratulate you, I would like to assure you of Tanzania’s support and cooperation in the discharge of your responsibilities. I also wish to acknowledge and commend your predecessor, His Excllency Vuc Jeremic for his outstanding leadership of the 67th General Assembly. A lot was achieved because of his visionary and wise leadership.
In the same vein, I would like to pay glowing tribute to our illustrious Secretary General for the excellent work he is doing for the United Nations and humanity at large.
My delegation and I, find the theme of this year’s General Assembly to be timely and very opportune. Indeed, we should start now to set the stage for the post 2015 development agenda. Hence, for the theme of this 68th General Assembly to be “Post-2015 Development Agenda: Setting the Stage” is the wisest thing to do. It affords us the opportunity to know where we are with regard to the Millennium Development Goals and decide what needs to be done to complete the unfinished business and enable us to make informed decision beyond 2015.
The Status of MDGs
Mr. President;
Millennium Development Goals framework is the best development framework ever developed to address global and national development challenges. The world has never witnessed such a coalescence of concerted efforts into a unified framework. It is heartwarming indeed to note that progress towards attaining MDGs has been made in the last 13 years. However, the progress varies from one goal to another and is highly uneven among nations and continents.
Mr. President;
Although extreme poverty has been halved at the global level, over 1.2 billion people are still trapped in extreme poverty; and an estimated 19,000 children under the age of five and around 800 women die every day mostly from preventable and curable diseases and other causes. This is totally unacceptable in the world of plenty we live in today where there is unprecedented advancement in science and technology which can be leveraged to solve almost all development challenges facing humanity. In a world which has enough food to feed everybody, nobody should go hungry or be undernourished. In a world with so much wealth, there is no reason why poverty, hunger and deprivation should ever continue to inflict pain and cause misery to many people. It is incomprehensible therefore, why the MDG’s could not be attained to the fullest.
This reality must be taken into account when we attempt to find ways to tackle unfinished business of the 2000 MDGs and design the post-2015 development agenda. Mechanism must be put in place to ensure that sources of financing will be adequate and reliable.
Mr. President;
Tanzania made significant progress in implementing the MDGs. We have already achieved the targets in four of the eight MDGs well before the set deadline of 2015. On MDG 2 we have achieved a target on universal primary education enrolment. On MDG 3 we have achieved target of parity of boys and girls in both primary and secondary schools enrolment. This is different from the past when there were more boys than girls. As a matter of fact, the trend appears to be tilting towards getting more girls than boys in the near future. We are yet to meet targets with regard to the ratio of females to males in tertiary education and in position of decision making particularly Parliament. However, it is possible to achieve the target on Parliamentarians by 2015 by taking advantage of the ongoing Constitutional review process.
We are on target with regard to reducing HIV/AIDS infection rate, the requirement of MDG 6. Similarly, we have attained MDG 4 on Child Mortality which is big achievement indeed, compared to where we were in the year 2000. But it is depressing we are not on track with regard to MDG 5 on Maternal Health. We are intensifying efforts to do better in order to improve the maternal health among Tanzania women.
With regard to MDG 7 on Environmental Sustainability we are on target with regard to drinking water for urban population. But, we are lagging behind with respect to rural water supply as well as access to improved sanitation both in rural and urban areas.
That notwithstanding, we have not relented in our pursuit of the targets in the MDGs which we are not likely to achieve by 2015. This will be the unfinished business for which we need to take action probably over and above what we are doing. We are lagging far behind with regard to MDG 1 in its four main indicators. There is not much possibility of achieving the targets despite the efforts we have been making.
We have been intensifying actions to transform and modernise our agriculture. Our aim is to increase productivity and farmers’ incomes as well as ensure food and nutrition security for themselves and the nation. Agriculture employs 75 percent of the Tanzania population and this is where the majority of poor are concentrated. Improved agriculture means less poor and hungry people. Plans are also underway to expand the conditional cash transfer programme under the Tanzania Social Action Fund supported by the World Bank. We want to increase the size of investment to benefit more vulnerable people so as to accelerate the implementation of MDG 1 in the shortest possible time.
Mr. President;
Generally, it remains my firm belief that despite some failures, MDGs have been nothing short of a remarkable success. If the developed countries provided the financing as envisaged under MDG 8 and as per the Monterrey Consensus and their own commitment in different fora of the G8 and G20, we would have implemented all the MDGs to the letter and spirit. It is in this regard we would find unrealistic any approach to the post-2015 Development agenda that does not address the critical issue of ensuring adequate financing. This is also true with regard to accelerating implementation of the MDGs in the remaining period.
We will continue to look at the United Nations for guidance and leadership in steering both processes to their successful conclusion.
The Reform of the United Nations
Mr. President;
The fact that the United Nations needs reform is a matter of little disagreement. Our collective failure to respond to this reality creates scepticism on our common resolve to strengthen an institution that is meant to serve nations and peoples. The reform we demand is long overdue. While we welcome discussions on the reform of the ECOSOC, Africa will not relent in demanding reform of the Security Council so that the continent, with the largest membership of the UN, has a permanent voice.
Global and Regional Conflict Situation
Mr. President;
Regrettably conflicts have continued to interfere in our development endeavours as they linger on in different parts of the world, from the Sahel to eastern DRC, Syria to Afghanistan, and other areas. They have caused enormous loss of innocent lives as populations continue to endure untold sufferings. The recent use of chemical weapons in Syria as confirmed by the United Nations inspections team to kill innocent people is rather distressing. We condemn such flagrant and senseless killing of innocent people including children in Syria. We commend the Secretary General and the UNSC for way they handle the matter. I believe the doors for a peaceful solution to the Syrian problem are not closed and that a military solution should be the last resort.
The Situation in the Great Lakes Region and DRC
Mr. President;
The United Republic of Tanzania regrets to see the suffering of the people of DRC as a consequence of the conflict in Eastern DRC has continued for far too long. We hope this time around the initiative of the Secretary General which resulted in the establishment of the Peace, Security and Cooperation Framework for the Great Lakes Region and DRC signed in February, 2013 will deliver lasting peace, security and development for the DRC and the Great Lakes Region. We highly commend the UN Secretary General for his vision and leadership in this regards. We welcome the choice of Her Excellency Mary Robinson, former President of Ireland as the United Nations’ Special Envoy for the Great Lakes Region. She will surely help advance the cause of peace in the region if supported by all of us in the region and the international community.
Part of the enduring problem facing the DRC is the proliferation of armed groups with varied interests. Bolder action is required to uproot these negative elements. These groups should be neutralized and disarmed. It is in this context that we welcomed MONUSCO’s expanded mandate as per resolution 2098 (2013) of the Security Council that among other things established the Force Intervention Brigade (FIB). Tanzania agreed to contribute troops to the FIB because it can help to deter belligerence and create a conducive environment for a political process to take effect. Of course the panacea to the DRC problem is political rather than military.
Tanzania’s Role in Peacekeeping
Mr. President;
Since 2007 Tanzania has become proactive in contributing troops to the United Nations Peacekeeping Operations. With over 2,500 peace keepers in Lebanon, Darfur and the Democratic Republic of Congo, we are the 6th contributor of military and police peacekeepers in Africa and 12th globally. We are partaking this noble endeavour, as members of the United Nations with the duty of advancing and upholding the ideals of our esteemed organisation.
We are satisfied that our contribution, though modest, is having a broader impact to those who have experienced the horrors of conflict. In this endeavours our peacekeepers have paid the ultimate price as was the case with the loss of we seven brave soldiers in Darfur, Sudan under UNAMID and two in Eastern DRC under MONUSCO. These are our national heroes whose sacrifices are not in vain.
The death of our peacekeepers was a grim reminder of the dangers facing peacekeepers around the world. It is disturbing that, armed groups and peace spoilers are increasingly attacking these servants of peace. We must unreservedly condemn all these attacks as there is no cause or justification for such barbaric attack which constitute a crime under international law. The UN Security Council whose primary role is the maintenance of international peace and security should be in the forefront in condemning such barbaric acts in good time.
Unilateral Sanctions and Embargo
Mr. President;
At this juncture, I wish to reiterate our call for ending unilateral economic, commercial and financial embargo against Cuba which has lasted for more than 50 years. Our call to end this unilateral embargo is not only predicated on its legality but also on humanitarian concerns particularly the negative effects of the quality of life of innocent Cubans.
We are deeply encouraged by recent developments especially of removing restrictions on family travel, cash remittances and telecommunication services. We believe this spirit will culminate into total cessation of the embargo in not to distant a future so that Cubans will be relieved of enormous economic, social and financial hardships they have endured for far too long.
Western Sahara
Mr. President;
The quest to resolve the dispute over the sovereignty of Western Sahara is also long overdue. It is high time that the United Nations took bold actions to give the people of Saharawi the opportunity to decide on their fate. It is incomprehensible why the Security Council which has been able to handle bigger security challenges cannot decide on the matter for nearly forty years now.
International Criminal Court
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
You will agree with me that the Rome Statute establishing the International Criminal Court (ICC) was a major milestone of the international criminal justice system. Indeed, the Court's creation as a machinery for fighting impunity was only possible with the support of Africa.
However, a decade after its entry into force, a rift has grown between the Court and the continent. The court is perceived as irresponsive to what are, in our view, legitimate concerns of African people.
It continues to ignore repeated requests and appeals by the African Union. It was sad to note that legitimate requests regarding the timing of the trials of President Uhuru Kenyatta and Deputy President William Rutto went unanswered. This attitude has become a major handicap that fails to reconcile the Court's secondary and complementary role in fighting impunity. Indeed, the Court's rigidity has proven counterproductive and stands to undermine the support it enjoys in Africa.
Terrorist Attack in Kenya
Tanzania condemns in the strongest terms possible the cowardly terrorist attack that happened last week at the Westgate Mall in Nairobi, Kenya which left at over 60 innocent people dead and hundreds others injured. I spoke and wrote to President Uhuru Kenyatta to express our sadness and dismay. I also reaffirm our solidarity with him and people of Kenya during these difficult moment and the fight against terrorism. This horrendous attack is a heart-breaking reminder of the threat that terrorism poses to humanity. Indeed none of us is completely safe from terrorism as it can happen anywhere, anytime and to anyone.
We must increase vigilance, enhance regional and global cooperation and scale up the fight against terrorism. The challenge ahead of us cannot be understated nor underestimated. The success will depend on our unity of purpose and determination. At this juncture I would like to commend His Excellency Uhuru Kenyatta, President of the Republic of Kenya for his exemplary leadership in the wake of the attack and his unshaken resolve and firm commitment to support the peace building efforts in Somalia and elsewhere. We are with Kenyan people at this time of distress and grief.
Conclusion
Mr. President;
In conclusion, I would like to stress once more that, we are passing through a time of great opportunity despite the many challenges. We must take advantage of the current scientific and technological innovations; information and communication technologies; and knowledge and lessons learned from the implementation of development programmes, including MDGs to build a world without poverty, hunger, diseases and deprivation.
A world that protects its environment and nature. It is possible to have a world without wars, conflicts and acts of terrorism. A world where human rights are respected, rule of law observed, democracy reigns and civil society is regarded as an integral part of the development endeavour. With stronger multilateralism and the United Nations leading the way and, with strong political will on the part of national leaders and the people everything is possible. We can make our world a better place for everyone to live.
I thank you for your kind attention.
- Sep 28, 2013
Hotuba ya Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ya mkutano wa MCC juu ya uchumi wa mpito wa Afrika, New York, Septemba 26, 2...
Soma zaidiHotuba
Ambassador Donald Gips, Chair of the US-South Africa Business Council and Honorary Co-Chairman of the US Chamber’s Africa Business Initiatives;
Excellencies Fellow Presidents;
Mr. Daniel W. Yohannes, CEO of MCC;
Honourable Mr. William Burns, Deputy Secretary of State;
CEOs of Companies;
Ladies and Gentlemen;
I commend you Mr. Daniel Yohannes for organising this important roundtable discussion on Africa’s economic transition. I also thank you for inviting me to participate in this landmark event. Tanzania is one of the beneficiaries of the Millennium Challenge Corporation in Africa. The Government and people of Tanzania highly appreciate the valuable support extended by the Government and the people of the United States.
We shall ever remain grateful because the infrastructure projects in the road, airport, energy and water sectors financed by US$ 698 million MCC grant have made a huge difference in the lives of the people of Tanzania. The Tanzania economy has benefited immensely. Through these funds, we shall have 472.9km of tarmac roads constructed of which 437.9 km will be in Mainland Tanzania and 35km in Pemba Island of Zanzibar. The airport at Mafia Island of Mainland Tanzania will be rehabilitated and upgraded. A submarine electricity cable bringing electricity from Tanzania Mainland to Zanzibar has been constructed. Electricity transmission and distribution projects in 10 regions covering 356 villages in 24 districts have been implemented. In the water sector there are projects to rehabilitate and expand water supply for Dar es Salaam and Morogoro.
Besides improving the living conditions of the people living in the area where these projects were implemented these projects will benefit the Tanzanian economy in a big way. They will open key economic areas for expansion of economic activities in these areas and beyond. These areas are now ripe for investment from elsewhere.
Ladies and Gentlemen;
The Namtumbo – Songea – Mbiga road for example, opens up an important region for corn, tobacco, coffee and cashew nuts production. This region is also rich in minerals such as coal, uranium, gemstones and gold. Similarly, the Tunduma – Sumbawanga road opens up a large corn and tobacco growing belt and gold, copper and gemstones mining areas. The construction of these roads therefore, opens up these regions for taping the huge investment potential which is being underutilized at the moment.
The Mafia Island airport opens up the huge tourism potential of this beautiful island of the coast of Mainland Tanzania. It is renowned for its diversity of marine life including the surviving dinosaur fish silicant and the scuba diving because of its clear waters. It is also near the gas fields discovered and ongoing exploration.
The electricity interconnector between mainland Tanzania and Zanzibar provides Zanzibar with stability of electricity supply as opposed to the current situation where there is only one cable. Rural electrification projects on the mainland open up rural Tanzania for investments big and small. In the villages small industries can be established, but big investors can be attracted because of the availability of electricity.
Mr. Chairman;
Ladies and Gentlemen;
We are now preparing for the second compact with focus on rural roads and electrification. This will further assist Tanzania unlock its development potential and eradicate poverty especially through modernization of agriculture and enhancement of industrialization. It makes the country even more attractive to private investment.
As in the first compact where US companies benefitted in the implementation of the projects and in investing in the areas supported by MCC, we see the same with MCC II. We therefore encourage other US companies to come and work with us and invest in various areas in our economy. We have investment potential in energy including oil and gas, agriculture and agri-business, mining, infrastructure projects including railways and ports, manufacturing and fishing. With the investment climate permissive, I see even bigger potential for more robust FDI flows from the US to Tanzania.
Ladies and Gentlemen;
Let me conclude my remarks by saying that Africa is at a very important juncture where FDI has surpassed ODA and no one would doubt that this is the trend that has to be sustained as African countries have now substantially improved their business and investment climate.
I am looking forward to a continued cooperation between my country and the US Government through MCC and other initiatives that have proved to be useful in complementing our efforts to better lives of our peoples. My Government is fully committed to the process of developing Compact II.
I thank you for your attention
- Aug 23, 2013
Hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwenye Hafla ya Kutunuku Hati Idhini kwa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki nane
Soma zaidiHotuba
Hotuba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati
wa Hafla ya Kutunuku Hati Idhini kwa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki NANE
Tarehe 20 agosti, 2013, IKULU, DAR ES SALAAM
Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania;
Wakuu wa Vyuo Vikuu, Wakuu wa Mabaraza ya Vyuo Vikuu, Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu;
Watendaji Wakuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mliopo Hapa;
Viongozi Mbalimbali wa serikali na taasisi zake mliohudhuria;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri na Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania kwa kunishirikisha kwenye tukio hili adhimu la kutunuku Hati Idhini Nane kwa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki. Natoa pongezi zangu za dhati kwa Wakuu wa Vyuo hivyo ambavyo leo nimevikabidhi Hati Idhini. Mmepewa dhamana kubwa na heshima ya aina yake ambayo mimi nina imani mtailinda.
Natoa pongezi maalum kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania kwa kazi nzuri mliyofanya mpaka kukamilisha zoezi hili la utoaji wa Hati Idhini. Nafahamu siyo kazi rahisi sana, inahitaji umakini na ueledi wa hali ya juu. Ninyi mmeifanya vizuri na mafanikio yake ndiyo haya. Hongereni sana.
Ndugu Wageni Waalikwa;
Leo ni siku ya faraja kubwa kwangu na wenzangu Serikalini kwa vile dhamira yetu ya kupanua fursa za elimu kwa vijana wetu katika ngazi zote inazidi kupata mwelekeo mzuri. Miaka mitatu iliyopita, tulipokutana kufanya kazi kama hii ya leo, nilielezea mafanikio makubwa tuliyokuwa tunaendelea kupata kwa upande wa upanuzi wa elimu nchini. Ni furaha iliyoje kuona kuwa mafanikio hayo yanazidi kuongezeka kadri miaka inavyokwenda. Kwa ulinganifu, idadi ya shule za msingi, sekondari na wanafunzi imeongezeka zaidi kuliko ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita. Kwa mfano, mwaka 2010 idadi ya shule za msingi ilikuwa 15,816 na shule za sekondari 4,266 na idadi ya wanafunzi ilikuwa milioni nane na nusu katika shule za msingi na zaidi ya milioni moja na nusu shule za sekondari. Lakini, mwaka 2012, idadi ya shule hizo imeongezeka kufikia 16,331 kwa shule za msingi na 4,528 kwa sekondari. Kwa upande wa wanafunzi wa elimu ya msingi karibu watoto wote wenye umri wa kwenda shule wameandikishwa na idadi ya wanafunzi wa sekondari imefikia 1,884,272.
Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki imeongezeka kutoka 37 vilivyokuwepo wakati ule hadi kufikia 50. Ongezeko hilo la Vyuo Vikuu nchini limewezesha idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kuongezeka kutoka 117,068 mwaka 2009 hadi 166,484 mwaka 2012. Kwa ujumla nimeridhishwa na mafanikio tuliyopata na utekelezaji wa maagizo yangu niliyoyatoa siku ile.
Mabibi na Mabwana;
Mafanikio tuliyopata hayakuja kwa bahati. Ni matokeo ya sera yetu nzuri ya elimu inayolenga kupanua fursa za elimu ili vijana wengi wa Kitanzania wanufaike. Ndio maana tumekuwa tunaongeza bajeti ya elimu kila mwaka ili tuweze kugharamia upanuzi huo ambao ni lazima tuufanye. Bajeti ya elimu imefikia shilingi trilioni 3.1 mwaka huu wa fedha ukilinganisha na shilingi trilioni 2.1 mwaka 2010/11 au shilingi bilioni 669.5 mwaka 2005/6. Hata ufadhili unaotolewa na Serikali kwa wanafunzi wa elimu ya juu umeongezeka sana kutoka shilingi 243 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi mwaka 2010 hadi shilingi 345 bilioni zilizotengwa mwaka huu wa fedha. Kutokana na ongezeko hili la fedha, zaidi ya wanafunzi 98,000 watanufaika na mikopo ya elimu ya juu ukilinganisha na 72,035 mwaka 2010 au 16,345 mwaka 2005.
Pamoja na sera nzuri na kuongezeka kwa uwekezaji wa Serikali katika elimu, mafanikio tunayoyashuhudia sasa yametokana pia na kuungwa mkono na sekta binafsi, mashirika ya dini na wananchi kwa ujumla. Sekta binafsi na Mashirika ya dini ni wadau muhimu wa Serikali kwenye maendeleo ya elimu nchini. Wamewekeza katika ujenzi wa shule za awali, msingi, na sekondari pamoja na vyuo vya ufundi, ualimu na elimu ya juu. Hatuna budi kuwashukuru kwa mchango wao wenye manufaa makubwa kwa nchi yetu na watu wake.
Ndugu Waziri;
Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe, Naibu wako,Mheshimiwa Philipo Mulugo, Kaimu Katibu Mkuu, Selestine Gesimba, Wakuu wa Idara pamoja na watumishi wote wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa sera yetu ya elimu. Nakupongeza pia kwa uamuzi wa busara wa kuitisha mkutano wa watendaji wakuu wanaosimamia elimu nchini uliofuatiwa na mkutano wa wazi wa wadau wa elimu uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Agosti, 2013. Nawashukuru wananchi na wadau wa elimu kwa ushirikiano wao na michango yao waliyotoa yenye lengo la kuborsha utendaji wa taasisi zinazojihusisha na usimamizi wa sekta ya elimu. Naomba Waziri na timu yako msimamie kwa ukamilifu utekelezaji wa mambo mliyokubaliana kufanya. Hakikisheni kuwa ahadi ya kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa katika Sekta ya Elimu kwa mwaka 2013 – 2015 inatekelezwa ipasavyo. Mkifanya hivyo kasi ya kupata majawabu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu itaongezeka sana.
Nampongeza pia Profesa Mawenya, Profesa Mchome, viongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu pamoja na taasisi na wadau wote wanaoshughulika na maendeleo ya elimu nchini kwa kushirikiana vizuri na Serikali katika kutekeleza jukumu hili zito na muhimu kwa maendeleo na mustakabali wa taifa letu. Kwa namna ya pekee nawashukuru wananchi, sekta binafsi na mashirika ya dini kwa kuitikia vyema wito wa Serikali na kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya elimu. Nawashukuru pia washirika wetu wa maendeleo kwa kuwa nasi bega kwa bega katika kila hatua tunayopiga ya kuendeleza na kukuza elimu nchini. Mchango wao na misaada yao mbalimbali imesaidia sana kutufikisha hapa tulipo.
Ndugu Wageni Waalikwa;
Pamoja na mafanikio hayo ya kutia moyo, hatuwezi kusema kuwa tumefikia pale tunapopataka au tunapopatarajia kufika. Bado tuna safari ndefu mbele yetu na kazi kubwa ya kufanya. Bahati nzuri yale tunayotaka kufanya au yanayotakiwa kufanywa yanafahamika. Kwa upande wa elimu ya juu, lazima tuendelee kuongeza wanafunzi wanaoandikishwa katika vyuo vyetu. Idadi ya wanafunzi 166,484 waliopo katika vyuo vyetu ni ndogo ukilinganisha na nchi kama Kenya ambayo ina wanafunzi wa elimu ya juu takriban 235,000 na Afrika Kusini yenye zaidi ya wanafunzi 800,000.
Maana ya takwimu hizi ni kwamba bado tunayo kazi kubwa mbele yetu katika kuongeza idadi ya Watanzania wenye elimu ya juu. Lengo la Serikali ni kuongeza maradufu idadi ya wahitimu katika vyuo vyetu vya elimu ya juu kutoka 40,000 ya sasa hadi ifikie 80,000 kila mwaka. Hatuwezi kuikwepa kazi hiyo, lazima vijana wetu wengi zaidi wapate elimu ya juu. Jukumu hilo lipo kwenu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, vyuo vikuu, sekta binafsi na wadau wengine wa elimu. Naomba tuifanye kazi hiyo bila kuchelewa.
Mheshimiwa Waziri;
Naomba ikumbukwe kwamba kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi peke yake haitoshi. Ubora pia uzingatiwe sana ili wahitimu wawe na ujuzi na sifa zinazostahili kiwango cha elimu yao. Inatakiwa waweze kutoa mchango unaokusudiwa katika ujenzi wa taifa letu; waweze kuhimili ushindani uliopo katika soko la ajira hasa kwenye nyakati hizi ambapo utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaimarika; na wawe na umahiri wa kukabiliana na changamoto za utandawazi. Kwenye hili pia bado tunayo safari ndefu mbele yetu. Kwanza, kuongeza idadi ya wakufunzi wenye vigezo na sifa stahili. Niliwahi kutoa ushauri huko nyuma kuwa vyuo vyetu vyenye Wahadhiri na Maprofesa wa kutosha katika fani mbalimbali wasaidie kwa kupanua, kuimarisha na kuboresha programu zao za uzamili na uzamivu.
Nafahamu juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanywa kama alivyoeleza Waziri. Lazima tuongeze bidii maradufu. Katika kipindi hiki chenye upungufu mkubwa wa wakufunzi, vyuo visisite kutafuta wakufunzi wenye sifa na vigezo kutoka nchi za nje. Tunaweza kuanza na nchi jirani na za ukanda wetu au kwingine Afrika na duniani kuziba mapengo yaliyopo wakati tunaendelea kujenga uwezo wetu wa ndani. We cannot afford to compromise the quality of our higher education on the excuse that we do not have sufficient qualified lecturers”. Kwa vyo vyote vile, utetezi wa aina hiyo haukubaliki, hausaidii na wala haueleweki. Dunia itatucheka.
Ndugu Mwenyekiti;
Jambo lingine linalokwenda sambamba na ubora wa elimu ya juu ni hali ya miundombinu ya vyuo vikuu nchini. Lazima tuhakikishe kuwa vyuo vyetu vina miundombinu inayotosheleza mahitaji ya kufundishia kwa wakufunzi na kujifunzia kwa wanafunzi. Lazima vyuo viwe na mahitaji yote muhimu ya kutoa elimu iliyo bora. Lazima kuhakikisha kuwa miundombinu hiyo inatunzwa vizuri. Kwa ujumla, uhaba na uchakavu wa miundombinu unachangia sana kuathiri ubora wa elimu inayotolewa vyuoni. Hivyo kuna haja ya vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki kuweka mkazo maalum kwenye kuboresha na kuimarisha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia. Vyuo viwekeze kwenye vifaa na majengo ya madarasa, maabara, maktaba, mabwalo na pia kwenye mabweni na viwanja vya michezo.
Napenda kuvihimiza vyuo vikuu viendelee kushirikiana na vyuo vikuu vya nje kwa kubadilishana ujuzi na uzoefu. Vyuo vipya viendelee kuimarisha ushirikiano na kuiga mifano mizuri ya vyuo vyetu vya zamani. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwao. Aidha, natoa rai kwa vyuo kuendelea kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili viwe na fedha za kutosha kuendesha shughuli zao badala ya kutegemea ada peke yake. Sisi Serikalini tupo tayari kusaidiana nanyi ili kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inakuwa ya ubora unaokubalika na wa hali ya juu.
Naomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tume ya Vyuo Vikuu wachukue hatua thabiti na endelevu za kusimamia na kuimarisha ubora wa elimu ya juu nchini. Kuwe na utaratibu madhubuti wa kufuatilia mwenendo wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki baada ya kutunukiwa Hati Idhini ili viendelee kuzingatia ubora unaokubalika. Vyuo vitavyokuwa na upungufu vioneshe mpango wao wa kurekebisha hali hiyo. Nina imani ukaguzi wa mara kwa mara ukiimarishwa utasaidia sana kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa na vyuo nchini.
Ndugu Wageni Waalikwa;
Mwisho, napenda kuwashukuru wamiliki wote na Wakuu wa Vyuo na Makamu Wakuu wa Vyuo kwa mchango wao mkubwa wanaotoa kwenye maendeleo ya elimu ya juu nchini. Nawapongeza wale waliotunukiwa Hati Idhini siku ya leo, na, nawatakia utendaji wenye tija na ufanisi. Nawaahidi ushirikiano wangu binafsi na wa Serikali ninayoiongoza.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Hotuba
SPEECH BY HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, ON THE OCCASION OF THE TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION (TPSF) BUSINESS DINNER, SERENA HOTEL,
DAR ES SALAAM 15TH AUGUST, 2013
Honourable Dr. Mary Nagu (MP), Minister of State, Prime Minister’s Office; Mama Esther Mkwizu, Chairperson of the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF);
Distinguished Members of the TPSF;
Mr. Godfrey Simbeye, Executive Director, Management and the Entire Staff of TPSF;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen;
I sincerely thank you Mama Esther Mkwizu, Chairperson of the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) and your distinguished leaders of TPSF for being kind enough to invite me to this gala dinner. It is heartwarming indeed to be in the company of such distinguished captain of industry, key partners of government in driving the socio-economic development agenda forward.
I thank you for the kind words you said about me and the government I lead with regard to the efforts we are making to promote growth and development with the private sector in Tanzania being in the forefront. Indeed, it is gratifying to note that through our partnership a lot has been achieved thus far and the spirit of partnership and cooperation between us, the government and the private sector – is taking root and getting stronger with each passing moment.
Ladies and Gentlemen;
We have heard loudly and clearly, the voice of the Chairperson of TPSF narrating the achievements made and the challenges ahead which require our joint attention and action. Fortunately, most of issues are known and work to find suitable and sustainable solutions are on going. My promise to you today is that we will do everything within our powers to help overcome the obstacles. I heard the Executive Director asking me to say something about fiscal measures of this financial year. First and foremost I would like to reaffirm that the participatory nature of the budget process where all stakeholders including private sector are involved will be maintained. As you all know the private sector is an active member of the Task Force on Tax Reforms. This way, the private sector is afforded the opportunity to discuss issues of fiscal policy every time taxes are being conceived. The private sector is part and parcel of the process, it will remain that way. We are ready to listen to advice from the private sector about what more needs to be done to deepen your involvement to ensure an effective participation at all levels.
On particular issues of newly introduced taxes, I would like to inform you that we have heard the feelings of the public and the industry. We have taken note of the valuable suggestions from various stakeholders and, we are working on them. The government is always stands ready to listen and receive views and proposals from individuals, business community and organizations.
Tax measures are the most difficult decision to be taken by government. Let me also state the obvious that taxes are necessary evil, we cannot do away without. Government has to deliver on its duties and responsibilities of the State which are ever expanding as population increases and social and economic functions expand. Every year therefore, there is a need to increase the financial resources over and above what was collected the previous year. Hence, new revenue measures have to be put in place. I don’t need to narrate to you the needs. We all know them.
They are needed to build more schools so that many more children can get formal education; we need resources to increase access to health care so that communities can enjoy higher quality of life. We need additional resources to support infrastructure development and energy projects, to transform agriculture and accelerate industrialization. That is why we need more resources, to ensure social development and overall prosperity. Unfortunately, the traditional sources of revenue are not sufficient to meet those new and emerging needs. As government we have to respond to this reality by exploring new sources of revenue.
Madam Chairperson;
There are two ways of ensure that government gets more revenues. One is strengthening tax administration. This has been done to great success over the last few years with the establishment of the TRA and continuing work of building the institution. It is an ongoing exercise. The second is identifying new sources of revenue that would facilitate widening of the tax base. Tax collection is not an easy task. Sir Winston Churchill, former Prime Minister of United Kingdom, one said: “there is no such thing as a good tax. My humble appeal to you is to please bear with us. We are doing all this for a common good. We need your cooperation and understanding so that together we can build our nation. We do our best to ensure fairness, decency and sense of dignity in the way taxes are collected. It is not in our best interest to suffocate the private sector. We will not kill the golden goose that lays the golden eggs.
Ladies and Gentlemen;
We are ready to work with the private sector. The PPP Act of 2010 is one clear demonstration of our resolve to promote and strengthen the involvement of the private sector in our development endeavors. We want the private sector to be a true engine of growth and partner. In this regard, we have realized that some areas in the PPP Act need further re-enforcement. Indeed, this is exactly what we proposed in the Finance Bill of 2013/2014 which amended some of the aspects. Furthermore, the government has also decided to streamline the coordination of issues related to PPP. We will soon streamline the unit at the Prime Minister’s Office dealing with PPP in order to strengthen the one at the Ministry of Finance. We believe that this will help to expedite decisions on PPP issues.
Another example is the formulation of the Private Sector Development Policy which is at an advanced stage. I am informed that last week the private sector submitted its comments on the first draft of the policy. I want to assure you that the government will take into account your comments and improve the document accordingly. Once it is operational, we will endeavor to implement it by the letter and spirit. Last, but not the least Madam Chairperson, you have rightly said it that the Tanzania Business Council has not met for quite some time. Indeed we will convene TNBC forums, the International and Local Investors Roundtables this coming November. The preparations are well underway as the regional and districts’ business council meetings have started taking place. Now that we have a young and dynamic CEO, I am confident that the affairs of TNBC are in good hands. Indeed, those meetings are important as they provide a platform for exchange of ideas on how to improve the business environment in the country.
Members of the Business Community;
Ladies and Gentlemen;
I would like to take this opportunity to assure you that we value your contributions and the government will continue supporting your efforts. We will continue to undertake reforms and improve economic services particularly transport, power and water to make our country a favorable investment destination. I am happy that we are making a good progress in this regard. Many investors, from all over the world are knocking at our doors. They want to invest in infrastructure, energy, manufacturing, agriculture and in many other areas. They have seen our potential and they are satisfied with the way we are conducting our business.
It is up to you to take advantage of these emerging and potential opportunities. I challenge your apex organizations and indeed the Tanzania Investment Centre, to work together to ensure that adequate information on business opportunities is widely available to local business community. I believe there is a lot to gain out there for all of you.
Madam Chairperson,
Invited Guests,
Ladies and Gentlemen;
The achievements that we have attained so far could not have been possible without the goodwill and support of our development partners. I would therefore like to commend our development partners for their generous support and assistance. We are looking forward to working with them to strengthen further, our private sector. We want to build the capacity of the private sector so that it truly plays its role as our engine of growth. We are not yet far from making this a reality.
In conclusion, I thank you Madam Chairperson for your invitation. I promise to continue working closely with the private sector and the business community through their apex organizations so that we can together realize the aspirations of our people. It is possible if each of us plays higher part effectively. I thank you for your kind attention and enjoy your evening.
Asanteni sana.
- Aug 15, 2013
Hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) (kwa Kiingereza)
Soma zaidiHotuba
Your Excellency Chief Olusegun Obasanjo, Former President of the Federal Republic of Nigeria and IITA Goodwill Ambassador;
His Excellency President Benjamin Mkapa;
Honorable Christopher Chiza, Minister for Agriculture Food Security and Cooperatives;
Hon. Ugandan Agriculture, Animal Industry and Fisheriers Minister;
Governmenent Officials Present;
Professor Bruce Coulman, Chair of the IITA Board of Trustees and Members of the IITA Community;
Director General of IITA,
The IITA Director of Eastern Africa;
Excellencies Ambassadors and Heads of Diplomatic Missions;
Renowned Scientists; Invited Guests;
Ladies and Gentlemen;
I sincerely thank Honorable Christopher Chiza, the Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives and the Board of Trustees of the International Institute of Tropical Agriculture for inviting me to officiate the launching of IITA Science Building located here at Mikocheni, Dar es Salaam. I commend the decision of IITA Board of Trustees to elevate this Station to become the headquarters of the Institute’s regional activities in Eastern Africa.
I welcome all our distinguished guests to Tanzania and to Dar es Salaam in particular. In a very special way, I extend very warm welcome to our senior brother, a longtime friend of Tanzania and an accomplished Pan-Africanist, His Excellency Olusegun Obasanjo, former President of the Federal Republic of Nigeria. He is here today in his capacity as IITA Goodwill Ambassador. We are happy to have you in this capacity. The IITA could not have a better ambassador than you.
Ladies and Gentlemen,
I consider the investment by IITA in this Science Building and the good work being done by IITA, to be very opportune indeed. About 70 to 80 per cent of the people in Africa depend on agriculture for their livelihod. Unfortunately, these are the people who form the bulk of the poor in our dear continent. Also many African countries are food stressed and currently, there is a decline in per capita food production in Africa. All of these are a function of low productivity in our agriculture. This signals an urgent need to revitalize agriculture research and to scale up the application of science and technology as well as agro-processing and agribusiness.
In essence, the economic growth and sustainable development of most African countries depends on agriculture. In this regard, any initiatives that are aimed at improving agriculture productivity in Africa deserve the encouragement and support of all of us. By doing this, we will stand a better chance to attain broad-based economic growth and thereby ensuring food security and poverty reduction.
Ladies and Gentlemen;
I am happy to note that IITA has been an important partner in promoting crop quality and productivity of agriculture in Africa. The Institute has an impressive track record in its research activities and has made tremendous impact in Sub-Sahara Africa notably on key tropical food crops such as banana, maize, cassava, soya beans, cowpea, tree crops, and yam. In Tanzania, we cherish the commendable job the Institute is doing in building the capacity of researchers and agriculture students. We are also thankful for various activities that enabled our farmers to increase production of cassava by developing improved high-quality disease resistant varieties. I would like to assure you that Tanzania will strengthen the working relations with IITA in our pursuit to improve agriculture in the country. We will also contribute more than what we are doing now.
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
We know too well that overcoming the many challenges facing African agriculture is gigantic task. It requires addressing many issues including developing adequate capacities for research in order to develop high yielding and diseases resistant seeds. In this regard, in 2006, the government of Tanzania developed a comprehensive 14-year Agricultural Sector Development Programme to overcome the challenges.
The purpose is to increase agricultural productivity through more application of modern science and technology. We have given more attention to research. Also, we have instituted measures to increase the involvement of the private sector and other stakeholders in agriculture development. In other words, we are including other players as well besides government and development partners as sole agents for agriculture development. I believe when this mix is properly attained other agriculture related sectors such as agro-processing, manufacturing and service industry will come into play and benefit accordingly. In turn, incomes of farmers and many other Tanzanians engaged in these sectors will improve and so will their living standards.
Ladies and Gentlemen;
As we all know, research activities in any field require substantial resources and expertise. This is also true for agricultural research and development. It is heartwarming, indeed, to note many governments in Africa are taking research seriously and they are investing resources to that effect. However, African governments are resource constrained as such they cannot allocate adequate resources in view of so many competing priorities. Political will has never been wanting, but the competing needs in our respective countries are overwhelming. It is difficult to choose which activity should get what. In this regard, the support of friends of Africa from the international community is needed to close the financing, technical and technological gap in agriculture research and development needs of Africa.
Excellencies; Ladies and Gentlemen;
Let me express my optimism that Africa is likely to succeed in her quest to transform agriculture and thereby attain food security, poverty reduction and prosperity. Positive signs are emerging for all to see. We should therefore build on the momentum and strengthen our collaboration with all stakeholders towards that end including this, all important International Institute of Tropical Agriculture. I believe this is the time to do it because there is awareness in Africa and growing global consensus to assist and support Africa to achieve this noble objective.
Excellencies; Invited Guests; Ladies and Gentlemen;
It would be remiss of me if I concluded my speech without expressing my heartfelt gratitude to His Excellency Obasanjo, for his commitment and devotion to our dear Continent. He could have decided to rest at his farm and enjoy his retirement but he is right here in our midst taking forward the African agriculture agenda. We really appreciate your efforts.
I also thank Professor Bruce Coulman and the entire leadership of IITA as well as researchers for their hard work and determination to transform African agriculture. I want to assure you that Tanzania, the Eastern African region and Africa as a whole is appreciative of IITA’s efforts to boost agriculture through capacity development with a view to improving the livelihoods of small holder farmers and big farmers alike in Africa. You are giving us a lot of inspiration as we endeavour to overcome the many obstacles. Let us re-dedicate our resolve to ending Africa’s persistent food shortages and poverty by scaling up our efforts and of course, interventions. I am sure we can.
Excellencies; Ladies and Gentlemen;
After these many words, it is now my singular honour and pleasure to declare that the IITA Science Building located in Dar es Salaam, Tanzania is officially opened.
Thank you for your kind attention
- Aug 15, 2013
Hotuba ya Rais Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wananchi, Tarehe 31 Julai, 2013
Soma zaidiHotuba
HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI, 2013
Utangulizi
Ndugu wananchi;
Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kwa mara nyingine tena kutekeleza utaratibu wetu huu mzuri tuliojiwekea wa Rais kuzungumza na taifa kila mwisho wa mwezi.
Ndugu Wananchi;
Mwezi Julai, 2013 ulikuwa wa neema kubwa ya wageni kwa nchi yetu wakiwemo watu na viongozi mashuhuri duniani. Natoa shukrani nyingi kwa Watanzania wenzangu kwa jinsi tulivyowapokea wageni wetu zaidi ya 1,700. Wamefurahi kuwepo kwao nchini na wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu. Wageni wetu wamekuwa wa manufaa makubwa kwa nchi yetu. Wamesaidia kuitangaza Tanzania duniani na kuendeleza fursa za kukuza utalii, biashara na uwekezaji nchini na kwingineko katika Afrika.
Mkutano wa Smart Partnership
Ndugu wananchi;
Wageni wetu wa kwanza ni wale waliokuja kuhudhuria Mkutano wa Global 2013 Smart Partnership Dialogueuliofanyika Dar es Salaam tarehe 28 Juni hadi 1 Julai, 2013. Mkutano huo
ulihudhuriwa na watu zaidi ya 800 kutoka mabara yote duniani wakiwemo Watanzania. Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na wakuu wa nchi na Serikali, viongozi wastaafu, wanadiplomasia, wawakilishi wa mashirika na taasisi za kimataifa, makampuni ya ndani na nje, wafanyabiashara, wasomi, asasi za kijamii na watu wa makundi mbalimbali katika jamii. Makampuni yetu 21nayo yaliungana na makampuni mengine 28 kutoka nje ya nchi kushiriki kwenye maonesho ya matumizi ya sayansi na teknolojia yaliyofanyika sambamba na mkutano huo.
Ndugu Wananchi;
Agenda kuu ya majadiliano ya mwaka huu ilikuwa ni “Matumizi ya teknolojia kama nyenzo ya kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi Barani Afrika(Leveraging Technology for Africa’s Social-Economic Transformation: The Smart Partnership Way). Tuliichagua mada hii kwa kuwa ni ukweli ulio wazi kuwa matumizi ya sayansi na teknolojia ndiyo chachu kubwa iliyoleta mageuzi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi. Ndiyo siri ya mafanikio katika nchi zilizoendelea na zinazopiga kasi kubwa ya maendeleo duniani.
Bahati mbaya sana kumekuwa na maendeleo na matumizi madogo ya sayansi na teknolojia katika Afrika. Ndiyo maana nchi za Afrika ziko nyuma kimaendeleo ukilinganisha na zile zilizoendelea. Katika mkutano huo umuhimu wa kuendeleza na kuongeza matumizi ya sayansi na teknolojia kwa ajili ya maendeleo Barani Afrika ulitambuliwa na kusisitizwa.
Mkutano ulihimiza na kusisitiza kuwa sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya nchi za Afrika zitoe kipaumbele kwa kuendeleza matumizi ya sayansi na teknolojia. Nchi zetu zimehimizwa kuwekeza katika elimu ya sayansi na teknolojia pamoja na kujenga uwezo wetu wa ndani wa uvumbuzi, ubunifu, umiliki na uendelezaji wa sayansi na teknolojia. Aidha, imesisitizwa kwa nchi zetu ziongeze kasi ya kutumia sayansi na teknolojia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii ili kuongeza ufanisi na kasi ya maendeleo.
Ndugu Wananchi;
Jambo la kutia faraja kwetu nchini ni kwamba mambo yote hayo tunayafanya. Tunachotakiwa sasa ni kufanya vizuri zaidi na kuongeza uwekezaji na kasi ya kuendeleza matumizi ya sayansi na teknolojia katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Tutaendelea kuboresha sera, kuboresha mazingira ya uwekezaji na kwa ajili ya maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini.
Ziara ya Rais wa Marekani Nchini Tanzania
Ndugu wananchi;
Mgeni wetu wa pili alikuwa Rais wa Marekani, Mheshimiwa Barack Obama, aliyefanya ziara nchini kwetu kati ya tarehe 1 - 2 Julai, 2013. Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Marekani na Tanzania. Kama mjuavyo, nchi zetu mbili zina uhusiano wa kibalozi tangu Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mwaka 1964.
Uhusiano wetu umepita katika vipindi mbalimbali na kwamba hivi sasa umekuwa mzuri zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi zetu mbili. Kumekuwepo na ongezeko kubwa la misaada ya maendeleo kutoka Marekani na uwekezaji wa vitega uchumi na biashara navyo vinakua. Pia ziara za kiserikali za viongozi wa nchi zetu kutembeleana zimeongezeka. Kama mtakavyokumbuka, mwaka 2008 aliyekuwa Rais wa Marekani Mheshimiwa George W. Bush alifanya ziara ya siku nne nchini. Pia Mawaziri mbalimbali wa Serikali ya Marekani wametembelea Tanzania akiwemo Mheshimiwa Hilary Clinton akiwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliyekuja mwaka 2011.
Ndugu Wananchi;
Nchi ya Marekani imekuwa mshirika wetu muhimu wa maendeleo katika nyanja mbalimbali. Kwa upande wa afya kwa mfano, tunapata msaada mkubwa katika mapambano dhidi ya malaria na UKIMWI. Katika maendeleo ya elimu, nako wanatusaidia katika mafunzo ya wataalamu mbalimbali pamoja na upatikanaji wa vitabu vya sayansi na hisabati kwa ajili ya shule za sekondari. Kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia, Marekani inatusaidia katika kuimarisha miundomuinu ya barabara, umeme na maji. Ujenzi wa barabara za Tanga – Horohoro, Namtumbo – Songea – Mbinga; Tunduma – Sumbawanga na baadhi ya barabara za Pemba, ujenzi wa njia ya pili ya kupeleka umeme Unguja kutoka Dar es Salaam, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia na usambazaji wa umeme katika Mikoa 10 ya Tanzania bara ni miongoni mwa matunda ya msaada wa Mfuko huo. Pamoja na hayo, ipo miradi ya kuongeza maji katika jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Morogoro ambayo inaendelea kutekelezwa.
Ndugu Wananchi;
Wakati wa ziara yake, Rais Obama alielezea na kusisitiza dhamira yake na ya Serikali yake ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu. Alielezea kuridhika na hatua tuliyofikia ya kukuza demokrasia nchini, utawala bora na kuwekeza katika maendeleo ya watu wetu. Aliahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zetu. Katika hili ameahidi kuongeza misaada ya maendeleo na kiufundi katika sekta za afya, elimu, kilimo, barabara, nishati na maendeleo ya vijana. Pia, alithibitisha kwamba nchi yetu itaendelea kunufaika na ufadhili wa Awamu ya Pili ya Mfuko wa Changamoto za Millenia. Katika awamu hii, maeneo yatakayopewa kipaumbele hapa kwetu ni umeme na barabara za vijijini. Mazungumzo ya miradi itakayotekelezwa katika awamu hiyo yanaendelea vizuri.
Power Africa
Ndugu Wananchi;
Rais Obama alitumia fursa ya ziara yake nchini kuzindua mpango wa Serikali yake wa kusaidia maendeleo ya sekta ya umeme katika Bara la Afrika. Mpango huu unaoitwa “Power Africa Initiative” umetengewa kiasi cha dola za Marekani bilioni 7 na Serikali ya Marekani na makampuni binafsi ya nchi hiyo yameahidi kuwekeza dola bilioni 9 katika mpango huo. Kwa kuanzia, nchi sita za Afrika (Ethiopia, Ghana, Nigeria, Tanzania, Liberia na Kenya) ikiwemo Tanzania zitahusishwa.
Bila ya shaka Mpango huo ukikamilika utasaidia sana kuimarisha upatikanaji wa umeme barani Afrika ambayo ni nyenzo muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Ni ukweli ulio wazi kuwa ukosefu wa umeme wa kutosha na wa uhakika ni sababu kubwa inayokwamisha maendeleo ya haraka katika nchi za Afrika. Hivyo basi, msaada huu ni muhimu sana kwetu. Kwa ajili hiyo nimeagiza Wizara ya Nishati na Madini iandae mkakati madhubuti wa namna Tanzania itakavyoshiriki na kufaidika na mpango huo. Nataka mpango huo utakapoanza kutekelezwa utukute sisi tupo tayari kutumia fursa zake.
Vile vile, ndugu wananchi, katika ziara hiyo Rais Obama alielezea nia ya Serikali yake kutaka kuwepo mpango wa kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji baina ya nchi yake na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nimeelekeza Wizara husika yaani Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko nao watengeneze mkakati utakaoonesha jinsi tulivyojipanga kufaidika na mpango huo. Lazima tujiandae vyema na mapema tunufaike saiwa na mpango huo.
Ziara ya Rais Mstaafu wa Marekani Nchini
Ndugu Wananchi;
Sambamba na ziara ya Rais Obama, nchi yetu ilipata bahati ya kutembelewa tena na Rais Mstaafu wa Marekani, Mheshimiwa George W. Bush na mkewe Laura Bush, tarehe 1 hadi 3 Julai, 2013. Kwa udhamini wa asasi ya George W. Bush Foundation waliandaa Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika uliofanyika hapa Dar es Salaam, tarehe 2 na 3 Julai, 2013. Mama Michelle Obama naye alishiriki mkutano huo uliozungumzia kuimarisha maendeleo na afya ya wanawake Barani Afrika.
Katika mkutano huo, pia, Mheshimiwa George W. Bush alizindua mpango wa kuimarisha mapambano dhidi ya kansa ya shingo ya kizazi na matiti barani Afrika. Kufuatia Mpango huo, Serikali ya Marekani imetoa dola milioni 3 na mashine 16 za Cryo Therapy zinazotumia baridi kali kuua chembechembe za kansa. Msaada huo ni muhimu hasa ukizingatia kuwa kila mwaka hapa nchini zaidi ya Watanzania 21,000 wanapata maradhi ya kansa. Kati ya hao asilimia 29.4 ni wanawake wanaopata magonjwa ya kansa ya shingo ya uzazi na asilimia 6.2wanapata kansa ya matiti. Naamini Mpango huu utatusaidia sana katika kuimarisha mapambano dhidi ya maradhi haya yanayowasumbua na kuua kina mama wengi nchini. Nimeitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuweka utaratibu mzuri ili msaada huo utumike ipasavyo na kuwanufaisha walengwa.
Ziara ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Nchini
Ndugu Wananchi;
Tarehe 23 mwezi Julai, 2013 pia tulitembelewa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair. Katika mazungumzo yetu Mheshimiwa Blair aliahidi kuisaidia nchi yetu kupitia taasisi yake ya Africa Governance Initiative kusaidia kusambaza umeme wa jua katika shule zetu za sekondari vijijini, maboresho ya shirika letu la umeme (TANESCO) na kusaidia uanzishaji na uimarishaji wa Kitengo cha Rais cha Ufuatiliaji Utekelezaji wa Programu za Maendeleo (Presidential Delivery Bureau - PDB). Tunamshukuru kwa ahadi yake hiyo itakayochangia katika jitihada za kujiletea maendeleo.
Ziara ya Waziri Mkuu wa Thailand Nchini
Ndugu Wananchi;
Tarehe 30 Julai, 2013 tulimpokea Mheshimiwa Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa Thailand aliyefanya ziara ya siku tatu nchini. Lengo la ziara yake ni kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Thailand na Tanzania. Katika ziara hiyo, tumezindua Jukwaa la Wafanyabiashara wa Thailand na Tanzania (Thai-Tanzania Business Forum) ili kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi zetu. Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra alitumia fursa hiyo kufafanua sera ya Thailand kwa Afrika inayosisitiza kukuza ushirikiano wa karibu wa kiuchumi na kibiashara. Pia amepata nafasi ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujionea mwenyewe jinsi nchi yetu ilivyobarikiwa kwa kuwa na kivutio hicho cha aina yake. Alipokuwa kule nchi zetu zilitiliana saini maelewano ya ushirikiano katika kulinda na kuhifadhi wanyama pori.
Katika mazungumzo yangu na yeye, tumekubaliana kuchukua hatua thabiti kukuza ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Tumetiliana saini mikataba mitano ya ushirikiano kwa mambo yafuatayo: Kukuza na kulinda vitega uchumi; kubadilishana wafungwa; ushirikiano wa kiufundi; na ushirikiano kwa masuala ya madini. Aidha, Waziri Mkuu huyo ameahidi kuwahimiza wawekezaji wa nchini mwake kuja Tanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo kilimo, utalii, viwanda nakadhalika. Pia, Waziri Mkuu wa Thailand ameahidi kuwa Serikali yake itatoa ufadhili kwa vijana 10 kusoma Shahada ya Uzamili nchini humo. Vile vile, nchi hiyo itaanza kuleta wataalamu wa afya wa kujitolea kuja kushirikiana na wataalam wetu kuimarisha huduma ya afya nchini.
Ziara hizi zinaonesha utayari wa dunia kuunga mkono jitihada zetu za kujiletea maendeleo. Naomba Watanzania wenzangu tutumie vizuri utayari huo wa dunia kuongeza kasi ya maendeleo yetu. Tusijikwaze wenyewe.
Ziara ya Kagera
Ndugu wananchi;
Kuanzia tarehe 24 hadi 29 Julai, 2013, nilifanya ziara Mkoani Kagera. Nilishiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa na kuzindua jengo jipya la Mahakama Kuu. Pia niliweka jiwe la msingi la upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Bukoba na kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara za Kigoma – Lusahunga na Kyaka – Kayanga – Bugene. Vile vile nilizindua Wilaya mpya ya Kyerwa na kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuona na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ili kuzitafutia majawabu.
Sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa zilifana sana. Niliwapongeza viongozi wa Jeshi na wa Mkoa kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo. Pia nilirudia kumpongeza Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, kwa uamuzi wake wa busara wa kufanya sherehe za kumbukumbu za mashujaa wetu pale Kaboya badala ya kufanyikia Dar es Salaam tu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Ni uamuzi muafaka na wa busara kwani pale Kaboya ndipo walipolala mashujaa wetu waliopoteza maisha yao kutetea mipaka na uhuru wa nchi yetu dhidi ya Nduli Iddi Amin. Hali kadhalika, kule Naliendele, Mtwara ambapo sherehe za mashujaa zilifanyika mwaka wa juzi, ndipo walipozikwa mashujaa wetu waliopoteza maisha kuisaidia nchi jirani na rafiki ya Msumbuji kutetea Uhuru wake dhidi ya wakoloni, makaburu na vibaraka wao wa ndani ya Msumbiji.
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu pale Kaboya niliwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba katika kuwakumbuka mashujaa wetu wale na wale sisi tulio hai, hatuna budi kutambua wajibu wetu wa kuwa tayari kujitolea muhanga kwa ajili ya kulinda uhuru wa mipaka ya nchi yetu. Nilisisitiza utayari wa nchi yetu kulinda mipaka yake na kwamba mfano wa mashujaa waliolala pale ni fundisho kwa mtu ye yote anayetamani kumega kipande cho chote cha ardhi ya nchi yetu. Atakiona cha mtema kuni kilichomkuta Nduli Iddi Amini au hata zaidi.
Nimesikia kuwa kauli yangu ile imetafsiriwa visivyo na kupotoshwa na baadhi vyombo vya habari na hata majirani zetu. Tafsiri hizo ni potofu. Sikumtaja mtu ye yote au nchi yo yote. Nilikuwa nazungumzia wajibu wa majeshi yetu na raia wa nchi yetu wa kulinda uhuru na mipaka yetu na kwamba hatutamruhusu mtu au nchi yo yote kutupokonya wala kuichezea haki yetu hiyo ya msingi. Tuko tayari kuitetea hata kama gharama yake ni maisha yetu kama walivyofanya mashujaa waliolala Kaboya.
Mahakama Kuu
Ndugu Wananchi;
Katika ufunguzi wa Mahakama Kuu ya Bukoba nilisisitiza dhamira na utayari wa Serikali yetu kuiwezesha Mahakama ya Tanzania kuwa na Mahakama Kuu katika kila Mkoa. Baada ya kukamilika kwa Mahakama Kuu ya Bukoba bado kuna Mikoa 14 hainazo. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14 tumetenga fedha za kujenga Mahakama Kuu katika Mikoa 7 na nilirudia ahadi yangu kuwa katika mwaka ujao wa fedha tutatoa fedha za kumalizia Mikoa 7 iliyosalia. Niliamua tuongeze kasi ya kujenga Mahakama Kuu hizo ili kuiwezesha Mahakama ya Tanzania kutimiza ipasavyo wajibu wake wa kutoa haki nchini.
Maendeleo ya Mkoa wa Kagera
Ndugu Wananchi;
Nilipokuwa Kagera nilifurahishwa na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Taarifa za Mkoa na Wilaya zimefafanua kwa kina mambo mazuri yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika Mkoani. Wameelezea furaha yao kwa mafanikio yaliyopatikana ambayo baadhi nimeyashuhudia au hata kushiriki kuyazindua na kuweka mawe ya msingi. Taarifa hizo pia zimelezea mambo mengi zaidi wanayotaka yafanyike na matatizo mapya na hata ya zamani ambayo wanataka yapatiwe ufumbuzi.
Katika mazungumzo yangu na viongozi na wananchi, yapo mambo ambayo yako kwenye uwezo wao kijijini, Wilayani na Mkoani kuyapatia ufumbuzi. Tulikubaliana na kuelekezana nini kifanyike. Yapo mengine mengine ambayo yanahitaji nguvu ya taifa tumeyachukua kuja kuyafanyia kazi. Kuna baadhi yaliwahusu Mawaziri ambao nilikuwa nao ziarani waliyasemea na kuyafanyia kazi palepale yalipojitokeza.
Ulinzi na Usalama
Ndugu Wananchi;
Kuna mambo matatu yahusuyo usalama ambayo yalizungumzwa na wananchi kwa uchungu mkubwa ambayo niliamua tuyashughulikie kitaifa. Mambo hayo ni ujambazi wa kutumia silaha kuteka magari, kupora mali na watu kuuawa. Jambo la pili ni wahamiaji kutoka nchi jirani wanaoingia, kuishi na kufanya shughuli nchini kinyume cha sheria. Na tatu, mifugo kuingizwa kwa wingi nchini bila kufuata taratibu husika na mingine kuingizwa katika hifadhi za wanyama.
Ndugu wananchi;
Nilitoa maagizo kwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama yaani JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa na Uhamiaji watengeneze mpango kabambe wa kuyashughulikia matatizo hayo. Watayarishe na kutekeleza operesheni maalum itakayo au zitakazokomesha ujambazi, kuondoa wahamiaji wasiokuwa halali na kuondoa mifugo iliyoingizwa nchini kinyume na utaratibu na ile iliyoko kwenye maeneo yasiyo stahili.
Aidha, niliwataka majambazi wajisalimishe na wasalimishe silaha zao ndani ya wiki mbili na siku hizo zinaanzia tarehe 29 Julai, 2013 nilipomaliza ziara yangu Mkoani humo. Kwa wahamiaji wanaoishi nchini kinyume cha sheria nimewataka watumie muda huo kuondoka nchini au kuhalalisha ukaazi wao. Hivyo hivyo kwa mifugo iliyoingizwa nchini kinyume na sheria au ile iliyoko kwenye maeneo yasiyostahili. Ndani ya muda huo watu wote waondoe mifugo yao au wajitokeze kufuata taratibu zilizopo.
Ndugu Wananchi;
Nilisema nilipokuwa Mkoani Kagera na narudia tena leo kuwa baada ya siku 14 kupita, vyombo vya ulinzi na usalama vitaendesha operesheni maalum ya kushughulikia matatizo hayo. Nilisema kuwa operesheni hiyo itafanyika katika Mikoa ya Kigoma, Kagera na Geita kwa wakati mmoja. Napenda kuwahakikishia kuwa hapatakuwa na mahali pa kukimbilia wala kujificha. Nawashauri wale wote wanaohusika na ujambazi, uhamiaji haramu na uingizaji haramu wa mifugo waamue kuchukua hatua muafaka sasa. Wasisubiri operesheni iwakute, wala wasifikirie kuwa hili ni jambo la kupita. Safari hii itakuwa endelevu.
Ndugu Zangu;
Hatuwezi kukubali hali hii niliyoikuta Mkoani Kagera ikaachwa kuendelea. Italeta madhara makubwa zaidi siku za usoni. Haiwezekani raia katika nchi yake, akose uhuru na usalama wa kutembea peke yake mpaka asindikizwe na Polisi. Na, baya zaidi hata Polisi nao wanashambuliwa na kuuawa watakavyo majambazi. Uhalifu huu lazima ukomeshwe, uishe na usijirudie tena.
Pia, haiwezekani hali ya watu kutoka nchi jirani kuingia nchini, kuishi na kufanya shughuli na kutoka watakavyo. Hatuzuii watu kuingia na kuishi Tanzania lakini wafuate sheria na taratibu za kuhamia na kuishi katika nchi yetu. Nchi yetu ina sifa na ukarimu huo. Hakuna uthibitisho mkubwa zaidi ya ule wa mwaka 1982, Rais Julius Nyerere wakati ule alipowaruhusu wakimbizi wanaopenda kuwa raia wa Tanzania wafanye hivyo. Wakimbizi 30,000 tu waliitumia fursa hiyo. Mwaka 2010 tuliwapa uraia wakimbizi 160,000 wa kutoka Burundi. Kwa sababu hiyo hatuoni sababu ya watu kufanya wanayoyafanya sasa kule Mkoani Kagera. Hatuwezi kuacha hali hiyo iendelee ilivyo.
Ndugu Wananchi;
Nilipokuwa Mkoani Kagera nilielezea kusikitishwa kwangu na vitendo vya baadhi ya watendaji na viongozi wa vijiji na wananchi kuwaruhusu watu kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria. Nimewataka waache mtindo huo. Nimeagiza na wao wajumuishwe katika operesheni ijayo. Watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo haramu wachukuliwe hatua zipasazo kisheria. Aidha, niliwataka Maafisa wa Uhamiaji watimize ipasavyo wajibu wao. Ukweli ni kwamba, mambo haya kuendelea kwa muda mrefu kiasi hiki ni kwa sababu ya udhaifu wa mamlaka husika. Vile vile, nimewataka TAKUKURU nao watimize wajibu wao. Hapa kuna uthibitisho tosha wa kuwepo kwa vitendo vya rushwa vinavyohusisha wahamiaji hao na maofisa wa vijiji na idara husika za Serikali. Mimi naamini kama TAKUKURU ikiwabana na Uhamiaji wakichemka vya kutosha tatizo hili lingepungua sana au hata kutokuwepo kabisa.
Uhusiano na Nchi ya Rwanda
Ndugu wananchi;
Katika kipindi cha miezi miwili sasa hususan tangu mwishoni mwa mwezi Mei, 2013, uhusiano baina ya nchi yetu na Rwanda unapitia katika wakati mgumu. Kauli za viongozi wa Rwanda dhidi yangu na nchi yetu ni ushahidi wa kuwepo hali hiyo. Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu na ndugu zetu wa Rwanda kuwa mimi, Serikali ninayoiongoza na wananchi wa Tanzania tunapenda kuwa na uhusiano mzuri na ushirikiano wa karibu na Rwanda kama ilivyo kwa nchi zote jirani. Kama majirani kila mmoja anamuhitaji mwenzake, hivyo lazima tuwe na uhusiano mwema na ushirikiano mzuri.
Napenda kusisitiza kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza tutakuwa wa mwisho kufanya kitendo au vitendo vibaya dhidi ya Rwanda au nchi yo yote jirani au yo yote duniani. Hatuna sababu ya kufanya hivyo kwani ni mambo ambayo hayana tija wala maslahi kwetu.
Ndugu Wananchi;
Ukweli ni kwamba wakati wote tumekuwa tunajihusisha na mambo ya kukuza na kujenga ujirani mwema na kufanya mambo ambayo yatasaidia kuimarisha uhusiano wetu kwa maslahi ya nchi zetu. Hiyo ni moja ya nguzo kuu ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania. Huo ndiyo ukweli kuhusu uhusiano wetu na nchi ya Rwanda kabla na hata baada ya sintofahamu iliyojitokeza sasa. Napenda kuwahakikishia ndugu zetu wa Rwanda kuwa kwa upande wetu hakuna kilichobadilika wala kupungua katika uhusiano na ushirikiano wetu. Mambo yapo vile vile. Kwa upande wangu, binafsi, sijasema lo lote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu. Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha. Sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake. Kwangu mimi sioni kama kuna mgogoro wa aina yo yote. Busara inatuelekeza kuwa tusikuze mgogoro usiokuwepo. Waingereza wanasema “two wrongs do not make a right”.
Ndugu Wananchi;
Kama mjuavyo uhusiano wetu na Rwanda umekuwa mzuri kwa miaka mingi. Tunashirikiana na kusaidiana kwa mambo mengi baina ya nchi zetu kitaifa na katika kanda yetu ya Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu, katika Umoja wa Afrika na hata kimataifa. Uhusiano unaelekea kupata mtikisiko baada ya mimi kutoa ushauri kwa Serikali ya Rwanda kuzungumza na mahasimu wao. Ushauri ule niliutoa kwa nia njema kabisa kwani bado naamini kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia hiyo ni vyema itumike. Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali ya Kongo na kwa Serikali ya Uganda. Katika mkutano ule Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliunga mkono kauli yangu. Rais wa Rwanda hakusema cho chote pale mkutanoni. Baada ya kurudi nyumbani ndipo tukaanza kuyasikia maneno tuliyoyasikia na tunayoendelea kuyasikia.
Kwa kweli nimestaajabu sana na jinsi walivyouchukulia ushauri wangu na wanayoyafanya. Havifanani kabisa, completely out of proportion and out of context. Mimi nilifanya vile kwa kuzingatia mila na desturi zetu za miaka mingi katika ukanda wetu. Tumekuwa tunakutana katika mikutano na vikao mbalimbali tunazungumza na kushauriana kwa uwazi juu ya njia za kushughulikia matatizo na masuala mbalimbali kila yanapotokea. Wakati wote tumeyachukulia kuwa ni mambo yanayotuhusu sote hivyo kupeana ushauri ni wajibu wetu wote. Na mara nyingi ushauri kwa wanaogombana kuzungumza tunautumia sana. Iweje leo mtu kutoa ushauri ule lionekane jambo baya na la ajabu. Jambo la kushutumiwa na kutukanwa! Siyo sawa hata kidogo!! Ushauri si shuruti, ushauri si amri. Una hiyari ya kuukubali au kuukataa. Muungwana hujibu: “Siuafiki ushauri wako”. Hakuna haja ya kutukana wala kusema maneno yasiyostahili wala kusema yasiyokuwepo na ya uongo.
Ndugu Wananchi;
Napenda kurudia kusema kuwa mimi binafsi na Serikali yetu ya Tanzania hatuna ugomvi wala nia yo yote mbaya na Rwanda. Tunapenda tuendelee kuwa na uhusiano mzuri na Rwanda. Labda wenzetu wanalo lao jambo dhidi yetu ambalo sisi hatulijui. Maana na sisi tunasikia mengi yanayozungumzwa na kudaiwa kupangwa kufanywa na Rwanda dhidi yangu na nchi yetu. Hatupendi kuyaamini moja kwa moja tunayoyasikia lakini hatuyapuuzi.
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza, naomba kutumia nafasi hii pia kuwatakia Waislamu wote nchini heri na baraka tele katika kukamilisha ibada muhimu ya kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Naomba tuendelee kuwatakia heri ili wamalize salama na tuweze kusherehekea kwa furaha na bashasha tele siku kuu ya Idd el Fitr pindi itakapowadia.
Mwisho kabisa, nawaomba Watanzania wenzangu wote tuendelee kushirikiana na kuishi kwa upendo, umoja na mshikamano kama ilivyo kawaida yetu.
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Afrika!
Asanteni Sana Kwa Kunisikiliza.
- Aug 14, 2013
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Wazi Kuhusu Mfumo Mpya wa Ufuatiliaji na Tathimini ya U...
Soma zaidiHotuba
Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Seif Shariff Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri;
Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi;
Makatibu Wakuu;
Dkt. Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango;
Washirika na Wadau wa Maendeleo;
Viongozi wa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma;
Viongozi wa Kidini na Sekta Binafsi;
Wataalamu Elekezi kutoka PEMANDU na Mckinsey;
Washiriki wa Maabara;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana:
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wote katika Warsha ya Wazi kuhusu mfumo mpya unaoanzishwa na Serikali wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kitaifa ya kipaumbele. Warsha hii inatoa nafasi ya pekee kwa wananchi kushiriki na kutoa mawazo yao jinsi ya kuboresha mfumo huo unaopendekezwa. Ni Warsha ya kuelimishana, kubadilishana mawazo na kufahamishana mipango na mambo ambayo Serikali inatarajia kuyafanya katika siku za karibuni.
Namshukuru Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, viongozi na watumishi wote wa Tume ya Mipango kwa kuandaa Warsha hii mahsusi. Kwa namna ya pekee nawashukuru pia wataalamu wa PEMANDU na McKinsey kwa kushirikiana vizuri na wataalam wetu katika kila hatua ya safari hii ambayo Serikali yetu imeianza.
Ndugu Wananchi;
Kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo sio jambo geni hapa nchini. Ni jambo ambalo tumelifanya tangu tupate Uhuru na tunaendelea nalo. Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ilianza na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo mwaka 1961 – 1964. Mpango huo uliainisha maadui watatu wa maendeleo ambao ni umaskini, ujinga na maradhi. Mikakati mbalimbali na mipango madhubuti ya maendeleo ilibuniwa ili kupambana na maadui hao. Baada ya hapo ukaja Mpango wa Maendeleo wa Miaka 15 wa mwaka 1964 – 1980, uliokuwa umegawanywa katika vipindi vitatu vya utekelezaji vya miaka mitano mitano.
Baadhi yenu mtakumbuka kuwa utekelezaji wa vipindi viwili vya mwanzo ulikuwa wa kuridhisha. Hata hivyo, utekelezaji wa kipindi cha mwisho cha Mpango ule, yaani kati ya mwaka 1975 – 1980, ulikuwa duni mno. Utekelezaji wake ulivurugwa sana na changamoto za wakati ule kama vile kupanda sana bei ya mafuta, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (1977) na Vita ya Kagera. Mambo haya yalisababisha fedha zetu nyingi kutumika kuagiza mafuta, kujenga taasisi zetu wenyewe na kutetea mipaka ya nchi yetu. Rasilimali kidogo tuliyonayo ikaenda huko badala ya kugharamia miradi ya maendeleo.
Ndugu Wananchi;
Pamoja na changamoto zilizojitokeza, Serikali iliamua kuanzisha mpango mwingine wa maendeleo wa muda mrefu wa mwaka 1981 – 2000. Kwa bahati mbaya mpango huo nao haukutekelezwa kufuatia kuendelea kudorora kwa uchumi. Kati ya mwaka 1981 na miaka ya 90 mwanzoni, Serikali ilianza kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi. Tukawa na National Economic Survival Programme (NESP) mwaka 1981 – 82 na Structural Adjustment Programme (SAP) mwaka 1982 – 1985. Mipango hiyo haikutekelezwa vizuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa rasilimali za kutosha. Kati ya mwaka 1986 – 89, Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ikaanza kutekeleza programu ya kwanza ya kufufua uchumi (ERP – I). Ya pili ikafuatia kati ya mwaka 1989 – 1992.
Mwaka 1994 Serikali ikaanza kuandaa mpango wa maendeleo wa muda mrefu utaowezesha kuzikabili changamoto mpya kufuatia mageuzi ya kiuchumi na kijamii yaliyokuwa yanaendelea nchini na duniani kwa ujumla. Kazi hiyo ilikamilika mwaka 1999 na kuzinduliwa kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025. Malengo ya Dira hiyo ni kuleta maendeleo ya haraka nchini na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Maana yake ni kwamba wananchi wawe na chakula cha kutosha, huduma ya elimu na afya iliyo bora iwafikie watu wengi zaidi, vifo vya watoto na akina mama vipungue, wastani wa kuishi uongezeke, maji safi na salama yapatikane kwa wote, uhalifu upungue na umaskini uliokithiri usiwepo kabisa na pato la wastani la Watanzania liwe zaidi ya dola za Kimarekani 3,000. Vile vile pawe na maendeleo ya viwanda, matumizi ya teknolojia na sayansi yaongezeke, miundombinu ipanuke na uchumi ukue kwa asilimia 8 au zaidi.
Ndugu Wananchi;
Juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali za awamu zote ikiwemo na hii ninayoiongoza mimi zimeleta mafanikio ya kutia moyo. Kwa mfano, uchumi wa nchi umekua kwa wastani wa asilimia 7 kwa miaka kumi iliyopita, mfumuko wa bei upo chini ya asilimia 10, mapato ya ndani yameongezeka, mauzo ya nje yameongezeka na hifadhi ya fedha za kigeni imeongezeka pia. Hata hivyo, idadi ya Watanzania walio maskini bado ni kubwa hususan umaskini wa kipato. Vile vile bado hatujafanikiwa kufikia malengo katika maeneo mengi tuliyojiwekea. Hata tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2025 tuliyofanya mwaka 2000 imethibitisha hivyo. Hatuendi kwa kasi inayotakiwa na utekelezaji wake siyo wa kuridhisha. Matokeo yake tupo nyuma ya hatua tuliyotakiwa kuwa. Kwa mfano, kwa upande wa safari ya kuelekea pato la wastani la watu kuwa dola 3,000 mwaka 2025, tulitakuwa tuwe tumefikia dola 995 mwaka 2010. Lakini ilikuwa tumefikia dola 545 tu. Kwa ukuaji wa uchumi, tulitakiwa tuwe asilimia 8, lakini tulikuwa asilimia 7.
Zipo changamoto nyingi za ndani na nje, zilizofanya tusifikie malengo hayo: Kubwa ni misukosuko ya uchumi wa dunia, uhaba wa rasilimali fedha na ufuatiliaji mdogo katika utekelezaji wa miradi iliyoainishwa kuleta maendeleo. Aidha, mipango na mikakati ya maendeleo ilikuwa na vipaumbele vingi kwa wakati mmoja wakati rasilimali za utekelezaji wake ni kidogo. Hali hii haikutuwezesha kujielekeza ipasavyo kwenye maeneo yenye kuleta matokeo makubwa na kwa haraka.
Ndugu Wananchi;
Baada ya kutafakari yote haya, tukafikiria namna ya kuweza kufikia malengo yetu ya Dira ndani ya muda uliobakia. Hivyo, tukaamua kuja na Mpango ya Maendeleo wa Muda Mrefu wa Miaka 15 ambao utatekelezwa katika awamu tatu za miaka mitano mitano. Katika Mpango wa Kwanza Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16), maeneo yaliyopewa kipaumbele ni Miundombinu, Kilimo, Viwanda, Huduma za jamii na Uendelezaji Rasilimali Watu na Utalii, Biashara na Huduma za Fedha. Changamoto kubwa ikabaki kuimarisha mfumo wetu wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ili kuleta matokeo ya haraka. Kuendelea kufanya vilevile tulivyokuwa tukifanya kusingeweza kuleta mabadiliko tuliyokuwa tunayataka katika utekelezaji wa mipango yetu. Ilibidi tubadilike, ikiwezekana tukimbie pale ambapo wengine wanatembea.
Ndugu Wananchi;
Tukiwa katika hali hiyo ya kutafakari cha kufanya, mwezi Mei, 2011 ikawa bahati mimi kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa “Langkawi International Dialogue” uliofanyika mjini Kuala Lumpur, Malaysia. Katika mkutano huo, Serikali ya Malaysia iliwasilisha mada jinsi inavyoendesha na kusimamia utendaji wake ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na huduma kwa jamii. Mimi na viongozi wenzangu tuliohudhuria mkutano huo tulivutiwa sana na mfumo wa utendaji wa Malaysia na tukadhamiria kujifunza zaidi kutoka kwao. Tukaomba watusaidie. Bahati nzuri Serikali ya Malaysia ikakubali ombi letu na kuandaa warsha maalum mwezi Novemba, 2011. Ujumbe wa Tanzania kwenye warsha hiyo ya aina yake uliongozwa na Dkt. Philip Mpango. Waliporudi, tukaamua kuwa na sisi tuanze kutumia utaratibu wa Malaysia wa “Matokeo Makubwa Sasa” ama kwa Kiingereza “Big Results Now”.
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa mfumo wa “Big Results Now” hapa nchini ulianza kwa kuainisha maeneo sita yenye uwezo wa kutupatia matokeo makubwa kwa haraka. Maeneo hayo ni nishati, elimu, maji, miundombinu, kilimo na utafutaji fedha. Kazi ya kuchagua maeneo sita ya kwanza nayo haikuwa rahisi. Tulibishana sana katika kuchagua vipaumbele vichache lakini vyenye kuleta matokeo makubwa. Hatimaye tukafanikiwa. Vipaumbele hivi vinabeba msingi wa kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa Tanzania kwa ujumla na kuchochea ustawi wa maisha bora kwa wananchi.
Hatua ya pili ikawa ni kufanya uchambuzi wa kina kupitia awamu ya kwanza ya maabara (lab) kama alivyoeleza Katibu Mkuu Kiongozi. Kazi hiyo ilitekelezwa kwa wiki sita mfululizo na wataalam wetu zaidi ya 300 kutokanyanja na sekta mbalimbali na kukamilika tarehe 05 Aprili, 2013. Nawapongeza sana kwa kazi hiyo kubwa na moyo wao wa kujitolea. Tumeandaa ratiba ya utekelezaji kwa kila mradi na programu ikionyesha kazi zilizopangwa kufanywa, mtekelezaji-husika na muda na kukamilisha kazi.
Katika mfumo huu, Mawaziri na Watendaji katika Wizara na Idara watapimwa kwa vigezo vilivyo wazi na ninyi wananchi mtapata fursa ya kuvijua vigezo hivi pamoja na matokeo ya upimaji. Hapatakuwa na siri. Hii itarahisisha usimamizi wa utendaji kwa maana Waziri au Katibu Mkuu atajifunga yeye mwenyewe kimaandishi na ataweka saini yake kwenye vigezo ambavyo atapimwa navyo na wananchi mtashuhudia matokeo ya upimaji huo.
Ndugu Wananchi;
Ili kuweza kuratibu vyema shughuli za ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mfumo huu mpya, nimeunda chombo maalum kitakachokuwa chini ya Ofisi yangu ambacho kitajulikana kama President’s Delivery Bureau (PDB). Kazi zake za msingi zitakuwa ni pamoja na: kupanga na kuendesha shughuli za uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs); kuandaa mikataba ya kupima utendaji kazi wa Mawaziri kwenye miradi na programu za maendeleo katika wizara zao; kwa kushirikiana na Tume ya Mipango kuishauri Serikali kuhusu maeneo machache ya kipaumbele yenye kuleta matokeo ya haraka (National Key Results Areas); kusaidia sekta binafsi kuwekeza kwenye maeneo hayo; na kufanya tathmini huru ya utendaji kwa viongozi wote hususan Mawaziri katika utekelezaji wa maeneo muhimu ya kitaifa.
Ndugu Wananchi;
Tumefanya kazi kubwa sana ya kuandaa na kuainisha maeneo ya kimkakati na kuyaandalia programu za kina kwa ajili ya utekelezaji. Lakini tumeona ni vyema kuwashirikisha wadau na wananchi katika jambo hili kubwa. Ndio maana tupo hapa kuhakikisha kuwa wananchi kwa ujumla wenu mnapata fursa ya kuchangia katika miradi na programu hizo kwa maendeleo ya taifa letu na watu wake.
Ndugu Zangu;
Sitapenda kuongea sana hivyo basi nataka niwape nafasi wananchi na wadau wengine mliofika hapa kupita katika eneo la kila maabara na kupata maelezo ya kina kutoka kwa wataalam. Muwe huru kuuliza maswali, kujenga hoja, kutoa maoni na kukosoa na kuboresha katika kila maabara. Baada ya kupata maoni yenu ndipo tutaboresha na kwenda kuyafanyia kazi maoni na ushauri wenu.
Ndugu Wananchi;
Baada ya kusema hayo, napenda kutamka kuwa Warsha ya Wazi imefunguliwa rasmi. Ninawatakia majadiliano mazuri na uchangiaji mzuri.
Asanteni kwa kunisikiliza
- Aug 14, 2013
Hotuba ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kwenye Ufunguzi Rasmi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre , Dar es Salaam, Machi...
Soma zaidiHotuba
Your Excellency, Comrade President Xi Jinping and Madame Peng Liyuan;
Excellencies;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
Once again I heartily welcome you, and First Lady Madam Peng Liyuan, to Tanzania. Congratulations on your well deserved election to the highest offices of your great Country: Secretary General of the Communist Party of China and most recently President of the Peoples Republic of China. We are very pleased and, in fact humbled that you included Tanzania in your first visit to Africa since you assumed the Presidency in your great country.
We in Africa highly appreciate this gesture of friendship and solidarity that in your first foreign trip, Africa is in your itinerary. And, more importantly we are anxious and excited that you will seize the opportunity of your visit to Tanzania to speak about China-Africa relations.
Mr. President;
Your visit to Tanzania will further consolidate and advance the long-standing friendship and cooperation between Tanzania and China, built on a very solid foundation by the founding fathers of our two nations, (who unfortunately all are late) President Mwalimu Julius Nyerere on the Tanzanian side, Chairman Mao Zedong and Premier Zhou en Lai on the Chinese side. The relationship we are witnessing today was further nurtured, consolidated and advanced by the successive generations of leaders in our respective countries. Fortunately for Tanzania two of my Predecessors, His Excellency Ali Hassan Mwinyi, the Second President and His Excellency Benjamin Mkapa the Third President are here with us.
Sino -Tanzania relationship has endured a lot and withstood the test of time. It is the steadfastness of our leaders and peoples of our two countries which sustained it and enabled it to grow from strength to strength. Now, we have become all weather friends. The words of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere in a speech, delivered at the Peking Square in Beijing, during his state visit to China in February 1965 attests to underline this fact. He said:
“We shall see for ourselves what are China's intentions towards us. We shall not be told by others.... the fears of others will not affect Tanzania's friendship with China, any more than our friendship with other countries would be affected by what their opponents say of them".
Mr. President; Ladies and Gentlemen;
When President Julius Nyerere established diplomatic relations with China in 1964, visited China in February, 1965, Premier Zhou En Lai visited Tanzania in June 1965 and Tanzania supported China to take her rightful seat at the United Nations, it was at the height and intense heat of the cold war. Today, forty eight years later the fear of China by others still remains, despite the cold war having ended. Those words of wisdom by the founding father of our nation still resonate in my mind and the minds of all of us in government. They informed and guided Tanzania’s - China policy for the past five decades. The fact of the matter is that: “We will always be guided by our own judgment based on Tanzania’s best interests”. I say this to assure you that Tanzania will continue to work closely with China at bilateral and multilateral settings in pursuit of national and global development goals of mutual interest.
Mr. President;
Next year our two countries will be celebrating 50 years of the establishment of our diplomatic relations, friendship and cooperation. Our relationship is excellent and China and Tanzania see eye to eye on many bilateral, regional and global issues. Trade and investments have been increasing. Tanzania has received invaluable support and assistance in our development endeavours as it has been the case with many African countries. These have made a huge difference in the livelihood of our nations and peoples. We will always be grateful and pray for continued support and assistance both at bilateral level and under FOCAC, which has proved to be a very useful initiative to support Africa’s development. In this regard we look forward to expansion of areas of cooperation and resource.
Your Excellency; Ladies and Gentlemen;
We are gathered here this morning for official handover and inauguration of the Julius Nyerere Convention Centre built by the support and assistance from the Government and people of China. This is another important milestone in the cooperation and solidarity between our two nations and peoples. Indeed, it is quite befitting that this monumental building bears the name of the founding father of the Tanzanian nation and of China-Afri-Tanzania relationship. We could not have chosen a better name.
The Convention Centre joins the long list of other symbols of Sino-Tanzania friendship and co-operation. These include, among others, the Tanzania-Zambia Railway, URAFIKI Textiles Mills, the National Stadium and several others which for brevity of time I will not mention all of them.
The Julius Nyerere Convention Centre will provide another modern conference facility for Tanzania and will be the first of its kind in Dar es Salaam. It will now be easy for Dar es Salaam to host local and international conferences which require facilities like the ones available at this Convention Centre. I am sure it will also be a source of promoting conference tourism for the City of Dar es Salaam.
Allow me, at this juncture to acknowledge and pay homage to your predecessor, His Excellency President Hu Jintao, for accepting my request and making it possible for this magnificent Julius Nyerere Convention Centre to be built. The people of Tanzania will forever cherish this symbol of true friendship.
Your Excellency;
Before I conclude let me express my profound gratitude to the China’s policy towards Africa. It has worked well and we have no doubt that the people of China will continue to walk with the people of Africa. So far China has been a dependable supporter and ally of African countries and other Third World countries, in their quest for support in their development efforts and plea for a just and equitable world economic order. We are eagerly waiting to hear from you on the policy of your administration towards Africa. It is now my singular honour and pleasure to welcome you to address this audience.
Long live China-Tanzania friendship! Long live China - Africa friendship! Please welcome.
I thank you for your kind attention.
Hotuba
STATEMENT BY HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, ON THE OCCASION OF HANDING OVER THE CHAIR OF SADC ORGAN ON POLITICS, DEFENSE AND SECURITY COOPERATION, 17TH AUGUST, 2013, LILONGWE, MALAWI
Your Excellency Joyce Banda, President of the Republic of Malawi, Chairperson of SADC and our host;
Your Excellency Armando Emilio Guebuza, President of Mozambique and outgoing Chairperson of SADC;
Excellencies Heads of State and Government;
Heads of Delegations;
Honourable Ministers;
Your Excellency, Dr. Tomaz Augusto Salomao, SADC Executive Secretary;
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen;
Allow me to begin by thanking Her Excellency Joyce Banda, President of the friendly Republic of Malawi and the great people of Malawi for the warm reception and gracious hospitality accorded to me and my delegation since our arrival in this beautiful city of Lilongwe. I congratulate you Madam President on the well deserved election to the Chairmanship of SADC. We trust that under your able hands our regional cooperation institution will continue to make progress and attain greater heights.
I also thank Your Excellencies for the honour you reposed on me last year to Chair the Organ on Politics, Defence and Security Cooperation. I have the pleasure to present to you the report of the work of the Troika of the Organ in the past twelve months. Let me hasten to say that it was a very eventful year. The Troika met a record seven times, probably unprecedented in the history of our organization. We were obliged to do so because of the demand for action in view of what was happening in the DRC, Madagascar and Zimbabwe.
Excellencies;
On the Democratic Republic of Congo, the Troika was preoccupied with ending the fighting between the Government of the D.R. Congo and the rebels of the M23. In this regard the Troika, the SADC Chairperson and the SADC Secretariat worked closely with International Conference on the Great Lakes Region. As a result of this cooperation our two organizations agreed on a number of things to do together including the creation of the Neutral International Force. Later this force became the Force Intervention Brigade under the United Nation’s – MONUSCO. Several SADC countries volunteered to contribute troops to the Brigade. Ultimately, three countries South Africa, Malawi and Tanzania were chosen by the UN to deploy. South Africa and Tanzania have already deployed Malawi is in the process of doing so.
The decision to establish and deploy this Force has not been without its own challenges. There were voices which did not favour the idea and worked to oppose it. After establishment and deployment there are efforts to discredit the Force probably for the purpose of influencing its dissolution or recall of some countries who have deployed or break the morale of the soldiers. This calls for continued support on the part of SADC and vigilance on the part of the nations which have deployed. And, the officers and men of the Force Intervention Brigade must beware of these unusual circumstances. This means, besides discharging their duties with highest levels of professionalism they must exercise and take extra caution because one would not know what is up their sleeves of those who are not happy with their very presence.
You will recall, Excellencies, that at the August 2012 Summit we also agreed on a number of things to do to help our brothers and sisters in the DRC build capacity in various fields. The idea was to assist them address the challenges they are facing. I must admit that, the security situation in the Eastern part of this country exhausted most of our energy at the expense of these other important matters. I appeal to incoming Chair to give due attention to these outstanding issues. They are equally and critically important for the future of stable peaceful and prosperous DRC.
Ladies and Gentlemen;
With regard to Madagascar and Zimbabwe, the Troika of Organ worked in close collaboration with SADC’s very able Mediators. His Excellency Jacob Zuma President of the Republic of South Africa with regard to Zimbabwe and His Excellency Joachim Chissano, former President of Republic of Mozambique with regard to Madagascar. We tirelessly engaged the political stakeholders in both countries and it is encouraging to note that these efforts did not go in vain. A host of challenges were overcome and visible progress has been made.
In Zimbabwe, for example, the constitution making process was successfully concluded. The referendum on the draft Constitution was held on 16th March, 2013 and a new constitution has been put in place thereafter. This paved the way for the harmonized elections of 31 July, 2013 despite the brevity of preparatory time. SADC was able to deploy observers for both the constitutional referendum and elections. Unlike the last election, this time around the election was peaceful so people had the opportunity to vote freely.
The SADC Electoral Observer Mission issued its preliminary report to that effect. They deemed the election free and peaceful. We are anxiously awaiting the final report where they will pronounce themselves on the other aspects of the elections in accordance with the SADC Electoral Observation Guidelines.
Excellencies;
We commend the people of Zimbabwe on the peaceful elections. We congratulate President Robert Mugabe on his re-election and the ZANU-PF on convincing victory in Parliamentary seats. We commend Prime Minister Morgan Tsvangirai, Professor Welshman Ncube and their respective Parties for participating in the elections and on the hard fought campaign and for what they were able to achieve.
We humbly appeal to all parties to remain civil and where there are grievances, legal and constitutional means should be invoked. We advice against resorting to violence. It is not in their best interest neither is it in the best interest of the people of Zimbabwe and their great country. Overall as we congratulate the people of Zimbabwe on the peaceful and orderly elections, we wish them every success going forward.
Excellencies;
On behalf of the Troika, I would like to call upon this August Assembly to commend the sterling job done by our facilitator on Zimbabwe, His Excellency Jacob Zuma, President of the Republic of South Africa and officials of this esteemed government who helped him deliver on our promise. Indeed, the road has not been easy. It has many challenges, it needed the patience and diplomatic skills of the facilitator and his team to achieve what we have been able to achieve thus far. We owe them a vote of thanks and big applause.
Excellencies;
Madagascar has been very tricky and quite a challenge. However through concerted efforts of the Troika and the SADC Mediator, Former President Joacquim Chissano of Mozambique commendable progress in the implementation of the Roadmap has been made. All institutions of transition have been established and the Amnesty Law was enacted. Preparations for the elections were made, the implementation process was initiated but got stalled because of the problems which had arisen.
Perhaps the most intriguing challenge we faced was that of leaders and other stakeholders reneging on promises and commitments they make. This has been the cause of reversals as well as delays and slow pace in implementation of the Road Map. It is very much the reason behind the unreliability of the many decisions being made.
Excellencies;
Among such examples is the way President Andry Rajoelina and Former President Mark Ravalomanana chose not to honour their promise not to contest. The other is lack of respect for rule of law and the Constitution as was exemplified by the candidature of President Andry Rajoelina, Mrs. Lalao Ravalomanana and former President Didier Tatsiraka. Both these candidates and the Special Electoral Court decided not to respect the law.
The list of things not done as agreed is long. In short, the issue of Madagascar is unfinished business, hence the Troika and the SADC has to remain seized with the matter. We must ensure that the parties stick to the Roadmap and implement decisions of SADC, AU, UN and International Contact Group on Madagascar. We should also push for the reconciliation particularly of the main protagonists for the sake of durable peace and stability in Madagascar.
Another important milestone that we achieved was the launch of the Second Edition of the Strategic Indicative Plan for the Organ (SIPO II) in November last year. Your Excellencies agree with me that SIPO remains one of the key frameworks for the SADC regional integration agenda. It provides SADC with a consistent and comprehensive programme of longterm political, economic, social and security policies. At the same time it provides SADC Secretariat with a strategic direction and sets priorities for Member States.
SIPO II has been structured to respond to existing and emerging challenges facing our Region including climate change, unconstitutional change of government, illegal immigration, increase in organized transnational crime, drug and human trafficking, money laundering, illicit mining and maritime piracy. The good thing about SIPO II is that it has a strong monitoring and evaluation mechanism. I therefore, appeal to all Member States to support the implementation of this important policy document as it provides SADC with an opportunity to move forward with unity of purpose and renewed strength. Let me underscore the obvious fact that its success will depend on each one of us playing his or her part accordingly. It can be done, play your part.
Excellencies;
During the last twelve months we also undertook various activities aimed at achieving the broad objectives of the Protocol on Politics, Defense and Security Cooperation of the Southern African Development Community. I am pleased to announce that during this Summit we will witness the launch of the Hashim Mbita Research Publication following the conclusion of Member States’ Chapter.
I had also the rare opportunity and privilege to work very closely with various institutions established under the Organ. I was thrilled and encouraged to learn that we have a formidable institutional set up and highly motivated staff. However, we need to do more to build the capacity of these institutions to make them more effective in responding to regional challenges. In this regard, sufficient funding should be made available to these institutions if we are to achieve the outcomes we all desire.
Excellencies;
It is clear that a lot of ground has been covered over the past twelve months but several challenges still remain ahead of us. I am confident that with concerted efforts, close cooperation and commitment of all the SADC Member States, our Region will eventually overcome the challenges. As I am handing over the baton to able hands of my brother, His Excellency Hifikepunye Pohamba, President of the Republic of Namibia, I have no doubt that our organization will effectively rise to challenges. I pledge unqualified support to our new chair in discharging his new responsibilities. He can count on me and my other colleagues in the government I lead. I wish President Hifikepunye Pohamba and the people of Namibia every success.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
It would be remiss of me if I did not thank our illustrious Executive Secretary, His Excellency Tomaz Augusto Salomao his Deputies and the entire team at the SADC Secretariat and indeed our development partners for the support and cooperation rendered to me and my country during our tenure of office. We are truly indebted to you all.
And now it is now my singular honour and pleasure to officially present the Report of the work of the Organ on Politics, Defense and Security Cooperation for the period of August, 2012 to August, 2013 to the 33rd Summit of SADC Heads of State and Government for your consideration.
Thank you for your kind attention. Mercy beaucoup, Muite obligado, Asanteni sana.