Hotuba

- Mar 17, 2015
HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA WAKUU WA WILAYA TAREHE 16 MACHI, 2015...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Hawa Ghasia (Mb), Waziri wa Nchi OWM – TAMISEMI;
Mheshimiwa Aggrey Mwanry, Naibu Mawaziri, TAMISEMI;
Mheshimiwa Abbas Kandoro – Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa;
Mheshimiwa Chiku Galawa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wetu;
Ndugu Jumanne Sagini, Katibu Mkuu OWM – TAMISEMI;
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Viongozi kutoka Taasisi ya Uongozi na OWM-TAMISEMI;
Watoa Mada na Wawezeshaji wa Mafunzo;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Utangulizi
Namshukuru Waziri Mkuu kwa kunialika na kunishirikisha katika ufunguzi wa Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya Wapya. Nakupongeza Waziri Hawa Ghasia na uongozi wa TAMISEMI kwa kuandaa mafunzo haya muhimu kwa ajili ya viongozi wetu muhimu sana katika safu ya uongozi wa nchi yetu. Nawapongeza pia kwa kuchagua mahala pazuri na tulivu pa kuendeshea mafunzo haya. Hii siyo mara ya kwanza kuwa na mafunzo ya namna hii, tumekuwa tukifanya hivi kila tunapofanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi mbalimbali ili kupata fursa ya kuelekezana kuhusu wajibu na majukumu ya kazi za viongozi wa Serikali katika maeneo yao. Nawapongeza kwa kudumisha utaratibu huu mzuri.
Pongezi kwa Uteuzi
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Napenda kutumia nafasi hii kwa mara nyingine tena kuwapongeza wote kwa kuteuliwa kwenu kuwa Wakuu wa Wilaya. Nimewateua kwa sababu nimeridhika kuwa mmekidhi sifa na vigezo vya kuweza kumudu majukumu niliyowapa ya kuongoza Wilaya. Nendeni mkachape kazi ili mkidhi matarajio yangu kwenu na ya wananchi mtakawaongoza. Nimewaamini, naomba mkalipe imani yangu kwenu kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa uadilifu na uaminifu.
Madhumuni ya Semina
Ndugu Viongozi;
Kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, lengo la mafunzo haya ni kuwapatia stadi na maarifa mahsusi yatakayowawezesha kutekeleza wajibu na majukumu yenu ya Ukuu wa Wilaya kwa ufanisi. Nimeona ratiba yenu na mada 11 zilizoandaliwa na watu waliobobea katika masuala ya uongozi na utawala. Nafurahi kwamba kuna fursa ya majadiliano baada ya kila somo kutolewa. Bila ya shaka mwisho wa mafunzo haya mtakuwa mmepata miongozo mahususi kuhusu majukumu yenu, wajibu wenu na utendaji kazi wenu. Naamini mtarejea vituoni kwenu mkiwa mmeiva vya kutosha na kwamba mkizingatia mlichofundishwa, mkiongeza na uzoefu wenu na mkiwa wabunifu mnaweza kufanya maajabu. Mtatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi wa hali ya juu na kushangaza wengi.
Wajibu wa Mkuu wa Wilaya
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Mkuu wa Wilaya ndiye kiongozi mkuu wa Serikali katika Wilaya. Ndiye mwakilishi wa Rais katika Wilaya. Hakuna mwingine. Ndiye mhimili wa shughuli za Serikali Wilayani. Ni dhamana kubwa hivyo ni lazima mfanane nayo katika utendaji wenu, wa kasi na katika maisha yenu ya kila siku ofisini katika jamii na hata nyumbani. Lazima muwe mfano kwa tabia njema kwa kauli na matendo yenu. Muwe na nidhamu ya hali ya juu na uadilifu usiotiliwa shaka. Wapo wenzenu tuliowaondoa kwa kukosa sifa hizo. Lazima wakati wote mzingatie matakwa ya Katiba, Sheria na taratibu za nchi ndiyo utawala bora.
Kama mjuavyo na kama hamjui naamini katika mafunzo haya mtajua kwamba Serikali ina majukumu ya namna tatu. Kwanza, ina jukumu la utawala, pili, ina jukumu la usalama na tatu, ina jukumu la maendeleo. Hivyo basi, Mkuu wa Wilaya nae kama kiongozi mkuu wa Serikali katika eneo lake wajibu wake nao umegawanyika pande hizo tatu.
Jukumu la kiutawala la Mkuu wa Wilaya ni lile la kuhakikisha kwamba mifumo ya utawala katika wilaya yake inafanya kazi vizuri na kwa ufanisi. Mambo yote yanakwenda vizuri, sheria zinafuatwa kanuni na taratibu zinazingatiwa na haki inatekelezwa katika Wilaya yake. Hakuna jambo ambalo halihusu Serikali: ya Kiserikali yanaihusu Serikali na ya jamii na ya watu binafsi nayo pia yanaihusu Serikali. Ninaposema hivyo sina maana kuwa Mkuu wa Wilaya anafanya kila kitu au anatoa maelekezo kwa kila jambo linalofanywa na kila taasisi na kila mtu katika Wilaya yake. Hapana. Kila jambo lina mtu wake anayehusika nalo na wengi wa watu hao hawawajibiki kumhusisha Mkuu wa Wilaya au Serikali. Ni wajibu wako kujua nani anahusika na lipi, ili uweze kuhakikisha kwamba majukumu hayo yanatekelezwa ipasavyo.
Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa hata mambo binafsi ya jamii na raia yanafanyika vizuri, kwa ufanisi na kwa kufuata sheria. Hii ina maana kuwa zaidi ya kujua vizuri shughuli za Serikali Kuu na Halmashauri ya Wilaya na Serikali za Mitaa, ni lazima pia ajue vizuri mila na desturi za jamii na maisha ya watu waliopo katika Wilaya yake na ahakikishe kuwa mambo yao yanakwenda vizuri. Kuwafanya watu wetu wawe na furaha ni wajibu wa msingi wa Serikali.
Hamna budi kutambua kwamba mfumo wa utawala wa Serikali Kuu unaishia kwenye tarafa. Lakini pia mjue kwamba yapo madaraka ya utawala na ulinzi wa amani yaliyogatuliwa kwa Makatibu Kata. Watumieni viongozi hao katika kutekeleza majukumu yenu. Hata hivyo, hamna budi kuhakikisha kwamba wanayatumia madaraka haya vizuri na kwa ufanisi.
Kwa upande wa jukumu la usalama, Serikali inawajibu wa kuhakikisha kuwa kuna amani na utulivu na kuna usalama wa maisha ya watu, mali zao na rasilimali za taifa. Kwa ajili hiyo Mkuu wa Wilaya anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kama Mkuu wa Mkoa alivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Rais ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa.
Nimeona kuwa mtafundishwa kuhusu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na wajibu wenu. Kamati hiyo ndiyo yenye dhamana ya kumshauri, kumsaidia na kumuwezesha Mkuu wa Wilaya kutimiza ipasavyo majukumu ya kiusalama ya Serikali katika Wilaya. Ni wajibu wa Mkuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa Kamati hii inakutana kwa mujibu wa kanuni zake. Kamati hii ikitimiza ipasavyo wajibu wake matukio yote ya kiusalama yataweza kuyashughulikiwa vizuri. Hali kadhalika, matishio au viashiria vya kuhatarisha usalama vitatambuliwa mapema na hatua zipasazo kuchukuliwa.
Kwa namna hiyo basi Mkuu wa Wilaya anaweza kuhakikisha kuwa Wilaya yake itakuwa salama na watu watapata nafasi ya kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo katika mazingira salama na tulivu. Wakuu wote wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vilivyopo Wilayani ni wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama anayoiongoza Mkuu wa Wilaya. Ni vyema Mkuu wa Wilaya akatambua kwamba vyombo hivyo vina uhuru wake katika kufanya shughuli na haviwajibiki moja kwa moja kwake kwa kila jambo. Vina wajibu kwa wakuu wa vyombo walio juu yao, walioko nje ya Wilaya. Hata taarifa zao huzipeleka huko ingawaje wanaweza kumuambia Mkuu wa Wilaya yale yahusuyo Wilaya yake ambayo wanaona anayowajibika kujua. Naomba mzifahamu vizuri taratibu hizo za vyombo kufanya kazi zake ili muepushe migongano isiyokuwa ya lazima muweze kuvitumia kwa ufanisi mzuri zaidi. Mkiyafahamu vizuri yote haya mtavitumia vyombo hivyo bila kuvunja taratibu zake na bila mikwaruzano. Mtajihakikishia mafanikio makubwa.
Jukumu la tatu la Serikali na hivyo la Mkuu wa Wilaya ni la kuwaletea maendeleo wananchi. Hapa kuna mambo mawili. Upande mmoja Serikali inalo jukumu la moja kwa moja la kupanga mipango ya maendeleo na kuitekeleza. Upande wa pili, Serikali ina wajibu wa kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo kwa kuwapa ushauri au kuwaongezea nguvu kwa yale wafanyayo.
Kwa mujibu wa mfumo wetu wa utawala ulivyo, shughuli za maendeleo zinapangwa na kutekelezwa na Halmashauri za Wilaya na Miji. Hivyo basi, Mkuu wa Wilaya hahusiki moja kwa moja na upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika Wilaya. Namna bora ya kuweza kufanya hivyo ni kuwa na uhusiano wa karibu na viongozi wa Halmashauri na hasa kuwa vikao vya mashauriano. Kupitia vikao hivyo mnaweza kuelewana juu ya mambo ambayo Halmashauri itayaingiza katika mipango na programu zake. Mkuu wa Wilaya anaweza kutumia DCC ingawaje inafanyika mambo yamekwisha kamilika. Hata hivyo, analo jukumu la kusimamia utekelezaji wa mipango hiyo inayofanywa na Halmashauri zake. Mkuu wa Wilaya anategemewa kufanya ziara za mara kwa mara katika Wilaya yake kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli mbalimbali zifanywazo na Serikali Kuu, Halmashauri na wananchi.
Mkuu wa Wilaya anapaswa kuwa mhamasishaji mkuu wa maendeleo katika Wilaya yake. Wakuu wa Wilaya wana jukumu la msingi la kuhakikisha shughuli zote za kiuchumi na miradi ya maendeleo zinatekelezwa ipasavyo kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo. Hivyo basi, mnapaswa pia kuelewa mipango yote ya maendeleo kwenye maeneo yenu pamoja na shughuli zote za kiuchumi zinazofanywa na Serikali Kuu, Halmashauri, taasisi na watu bianafsi kuhakikisha hazikwami. Hali kadhalika, hamna budi kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za umma. Ama kwa kujitolea nguvu zao au kwa kuchangia kwa hiari na kutoa kodi na tozo stahili. Shirikianeni kwa karibu na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri na Madiwani ili kujenga ushirikiano na maelewano katika utendaji wa kazi.
Ili muweze kutekeleza majukumu yenu ya maendeleo ni wajibu wenu kuhakikisha kuwa hamkai ofisini muda wote. Lazima mtoke kwenda kukagua shughuli za maendeleo na kukutana na kuzungumza na wananchi.
Tumewateua mkawatumikie wananchi na si vinginevyo. Hatukuwateua mkakae ofisini tu, wafuateni wananchi waliko, mkasikilize shida na kero zao na mkazitafutie majawabu. Yale yatakayowashinda wapelekeeni viongozi wa juu yenu. Tumewateua mkawe wakombozi wa matatizo yao, tumewateua mkawe daraja la kupita kuelekea kwenye maendeleo. Kafanyeni kazi.
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kwamba: “Kiongozi mzuri katika Taifa letu, ni yule anayekerwa na matatizo ya wananchi”. Maneno haya ya busara bado ni muhimu hata sasa. Jukumu kubwa tunalotakiwa kujishughulisha nalo ni kutatua kero na matatizo ya watu. Mnategemewa muonekane hivyo kwa kauli zenu, mienendo yenu na matendo yenu. Watu lazima wayaone matumaini ya kupata majawabu ya changamoto zao kupitia kwenu. Wanapaswa kuwaona kuwa ninyi ndiyo kimbilio lao. Mnategemewa kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili na katu msiwe sehemu ya matatizo au wanung’unikaji.
Mahusiano ya Mkuu wa Wilaya na Wadau wengine
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Mkuu wa Wilaya pia ni kiungo kati ya Serikali Kuu na wadau wengine katika nyanja mbalimbali za maisha ya Watanzania, kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kiusalama. Ninyi kama viongozi wakuu wilayani mna wajibu wa kujenga mahusiano mazuri na vyama vyote vya siasa vilivyo katika maeneo yenu pamoja na viongozi na taasisi za dini, viongozi wa kijamii na asasi zisizokuwa za kiserikali. Mkijenga uhusiano mwema na makundi hayo itasaidia sana utekelezaji wa mambo mengi muhimu ya maendeleo ya watu na mtaweza kuepuka migogoro ya kisiasa na kijamii inayoweza kujitokeza katika maeneo yenu.
Ni vyema mkatambua kuwa viongozi wa dini na wa kijamii wana mchango muhimu katika ustawi na maendeleo ya maeneo yenu ya uongozi. Wananchi wanawasikiliza, hivyo basi mkiwa na mahusiano mema nao, itakuwa rahisi kwa mambo mengi kutekelezeka hata yale ambayo yanaweza kuonekana kuwa huenda yangekuwa magumu. Pia, viongozi hawa ni tegemeo kubwa katika kudumisha amani na utulivu nchini na kusaidia katika huduma mbalimbali za jamii. Hivyo jengeni uhusiano mzuri na viongozi hawa.
Ndugu Viongozi;
Wakuu wa Wilaya wana uhusiano maalum na chama Tawala kama ilivyo kwangu, kwa Waziri Mkuu na kwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Serikali hii ni ya Chama cha Mapinduzi kilichoshinda uchaguzi. Inatekeleza Ilani ya Uchagui ya CCM, hivyo tunao wajibu wa kutoa tarifa ya mara kwa mara kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa Ilani na majukumu mbalimbali ya Serikali. Mkuu wa Wilaya anao wajibu huo kwa Chama katika Wilaya yake. Ni lazima afanye hivyo katika vikao husika vya Chama vya Wilaya. Si jambo la hiari wala si jambo la muhari unapotakiwa kufanya hivyo.
Majukumu Maalumu ya Kitaifa
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Kila wakati una mambo yake muhimu kitaifa ambayo hamna budi kuyashughulikia. Wakati huu pia una mambo yake. Napenda kuyataja baadhi. Jambo la kwanza, ni ujenzi wa maabara za sayansi katika Sekondari za Kata. Nilitoa agizo Novemba 2012, kuwa kila shule ya sekondari ya kata ambayo haina maabara za masomo ya ya sayansi ziwe nazo ifikapo Novemba, 2014. Kazi kubwa na nzuri imefanyika na takribani kila Wilaya Maabara nyingi zimejengwa. Kwa kutambua kasi iliyokuwa inaendelea niliongeza muda mpaka Juni, 2015 wa kumalizia ujenzi paliposalia. Sitaki maelezo kuwa hukuwepo. Utakuwa umeshindwa kazi.
Jambo la pili, uboreshaji wa daftari la wapiga kura. Kama mjuavyo zoezi la uandikishaji wa wapiga kura limeshaanza katika mkoa wa Njombe na litaendelea katika mikoa mingine kwa mujibu wa ratiba ya Tume. Jihusisheni kwa ukamilifu katika kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Wakumbusheni wananchi kwamba kuwa na kitambulisho cha mpiga kura ndiko kutawawezesha wao kushiriki katika zoezi la upigaji wa Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu baadae Oktoba, 2015. Haipo fursa nyingine.
Jambo la tatu, ni Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanashiriki kwa ukamilifu bila kukosa katika mchakato huo. Ndiyo maana ninawataka muwahimize wananchi wajiandikishe na pia washiriki wakati wa zoezi la kutoa elimu kwa umma na kampeni kabla ya Kura ya Maoni. Hakikisheni wakati wote wa zoezi la upigaji kura kuna amani na utulivu. Tumieni vizuri mamlaka yenu ya ulinzi wa amani katika maeneo yenu ili wananchi waelimishwe, kampeni zifanyike na wananchi wapige kura kwa amani na salama. Tunataka wananchi wapate fursa ya kuamua wanavyoona inafaa kwa uhuru.
Jambo la nne, ni kuhusu Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Kama mjuavyo tunatarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba, 2015. Ninyi kama Viongozi mna wajibu wa kuhakikisha kuwa uchaguzi huu unafanyika katika hali ya utulivu na amani na kila mwananchi anashiriki kwa uhuru katika uchaguzi huo. Hamasisheni wananchi wa maeneo yenu wajiandikishe katika daftari la kudumu la wapiga kura hivi sasa ili waweze kuitumia haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Zipo changamoto kadhaa za kitaifa ambazo hamna budi kuziwekea mikakati maalum ya kuzitafutia uamuzi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Nitazitaja kwa kifupi nikitumaini kuwa baadhi huenda zikazungumzwa katika mafunzo au mtazikuta Wilayani kwenu na waliowatangulia watawasaidia kuwafafanulia. Tunachotegemea kutoka kwenu ni kuwa na mikakati na mipango thabiti ya kutafuta majawabu. Mambo haya ni pamoja na:
(i) Wimbi la Wahamiaji haramu na wavamizi katika misitu ya Hifadhi. Tatizo hilo lipo zaidi katika Mikoa ya Mipakani;
(ii) Lipo tatizo kubwa la biashara na matumizi ya dawa za kulevya, ambalo limesababisha madhara makubwa, hasa kwa Vijana na kuivuruga sifa nzuri ya nchi yetu. Lazima tufanye kila tuwezalo tuzuie na kuikomesha.
(iii) Ipo migogoro ya ardhi katika maeneo mengi nchini ambayo mingi inasababishwa na baadhi ya Watendaji kwa kutozingatia ipasavyo maadili ya kazi zao. Tufanye kila tuwezalo tuitafutie jawabu.
(iv) Kuna migogoro ya wakulima na wafugaji katika sehemu nyingi nchini ambayo tunawajibika kuingilia kati mapema kuzuia isilete maafa. Na lililo muhimu zaidi ni kuipatia ufumbuzi wa kudumu kwa kupanga matumizi bora ya ardhi na kugawa maeneo ya kilimo mbali ya ufugaji na kusimamia mpango huo.
(v) Kuna tatizo kubwa la ujangili wa wanyama pori hasa ndovu, faru, simba na chui ambalo hatuna budi kulikomesha. Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zishirikiane na wadau kupambana na uhalifu huu.
Hayo ni baadhi ya masuala muhimu kitaifa lakini kila Wilaya ina mambo yake. Naomba muende mkashirikiane na viongozi wenzenu na wananchi kubaini matatizo maalum ya maendeleo katika maeneo yenu na kubuni mikakati wa kuyatatua.
Hitimisho
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Naomba nimalize kwa kuwatakia mafunzo mema na utekelezaji mwema wa wajibu na majukumu yenu baada ya mafunzo haya kuhitimishwa. Nendeni mkafanye kazi kwa ubunifu mkubwa, kwa juhudi na maarifa ili muwasaidie wananchi walio katika maeneo yenu kuondokana na umaskini. Hivyo, ni muhimu kila mmoja akatimiza wajibu wake kwa ukamilifu.
Baada ya kusema hayo napenda kutamka kuwa, mafunzo haya ya Wakuu wa Wilaya yamefunguliwa rasmi.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

- Mar 09, 2015
SPEECH BY HIS EXCELLENCY DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AT THE OPENING OF THE 22ND EAST AND SOUTHERN AFRICA ASSOCIATIO...
Soma zaidiHotuba
Hon. Saada Mkuya Salum (MP), Minister for Finance;
Hon. Adam K. Malima (MP), Deputy Minister;
Hon. Mwigulu Nchemba (MP), Deputy Minister;
Dr Servacious Likwelile, Permanent Secretary, Treasury;
Mr. Michael Saas, Chairperson of ESAAG and Accountant General of RSA;
Government Officials Present;
Mrs. Mwanaidi Mtanda, Accountant General of Tanzania;
Members of the Diplomatic Corps and Heads of International Cooperation Organizations;
Members of the Press;
ESAAG Secretariat;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen;
Good morning;
It is a great pleasure, and an honour for me to be accorded this opportunity to officiate at the opening of the 22nd East and Southern Africa Association of Accountants General Annual Conference. Welcome back to Tanzania after 20 years of absence. As you may recall the last time this conference was held in Tanzania was in 1995 in Arusha. In fact, that was the meeting that founded this Association. Tanzanians are immensely delighted to have you in our midst again. We wish you very successful deliberations.
Theme of the Conference
Ladies and Gentlemen;
Let me state at the outset that, I like this year’s Conference theme of ‘’Strengthening Public Financial Management for Socio-Economic Development in the Region”. Indeed, this is the very essence of the establishment of the Office of the Accountant General in all our countries. It is the longstanding wish and demand of everybody in government and the people who own the governments. The demand for sound public financial management, transparency and accountability is everywhere in our societies. It is high time governments in the Eastern and Sothern Africa delivered better on this demand. We look to this conference to provide the best way for governments of the 14 member countries present at this Conference to meet this just demand.
Importance of Public Finance Management
Distinguished participants, Ladies and Gentlemen;
When defining the vision and policy of my new administration on government finance at the opening of new Parliament after my election on December 30th, 2005, I underlined two overarching things. One, that we must strive to increase government revenues with renewed vigour. And, two that we must ensure financial discipline of the highest order possible with regard to expenditure of financial and other government resources. I underlined that the recognition of sound public financial management is what will enable our government to deliver on its promise to the people who elected us into office. Ultimately, sound public financial management is critical for promoting socio-economic development in which lies the very essence of establishment of governments in all nations on this planet.
Public Finance Management Reforms in Tanzania
Distinguished Participants;
In this regard, therefore, reform of Public Finance Management has been one of my Government’s priorities ever since I assumed office in 2005 todate. Fortunately, this has also been the agenda of my predecessors. As a matter of fact, I decided to stay the course of reforms they initiated. A number of initiatives were undertaken with regard to improving operational systems, laws, regulations and institutions responsible for managing public finances. For those who were here during the First ESAAG Conference in 1995 and following developments in Tanzania, would agree with me that a lot of ground has been covered. I can testify that we have lived up to the spirit and purpose of this organization.
Ladies and Gentlemen;
Indeed, public finance reform measures have worked well for the government and the country. Government revenues have been on the increase although not yet enough to meet our requirements; as is always the case. A number of Public Finance Management (PFM) interventions which are parts of the reform programs have helped increase credibility of the budget, financial recording and reporting, and fiscal oversight. There is more transparency and accountability. There is improvement in financial discipline, better allocation of resources to priority areas and improved public service rendered to our people.
The enactment of the Public Procurement Act 2004 (PPA, 2004), its 2005 regulations and the establishment of the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) and the Public Procurement Appeals Authority (PPPA) has increased transparency and predictability with regard to procurement and management of public resources. Much as there may be some challenges, its benefits out weight its challenges. All that is required of us to address those aspects of this important law which require improvement. Over 75 percent of government expenditure is about procurement of goods and services. If this is left unregulated a lot of money will be lost and procurement will be the bedrock of corruption. Improving government accounting system has been a critical component of our public finance reform efforts.
Ladies and Gentlemen;
In the year 2008, the Government adopted the International Public Sector Accounting Standard (IPSAS)-Cash basis of accounting. This has improved the content, credibility and quality of cash flows for revenues and expenditures, good banking arrangement system, and effective utilization and reporting standards. The First Government Financial Reports were produced in 2008 under IPSAS Cash basis. As a result, Audited Certificates have increased from 48 percent in 2008 to 94 percent in 2014 for the Central Government which depicts and underlines our commitment towards better management of public finances. Adoption of IPSAS accrual has improved the content and quality of financial reports, comparability of financial data between Tanzania and other countries. Also, it has improved quality content and accuracy information through training of staff.
Further efforts geared towards strengthening Public Finance Management (PFM) included upgrading the Central Bank (BOT) systems to link them up with Accountant General’s software, thus paving the way for operationalization and roll-out of Electronic Fund Transfer to Ministerial Department Agencies (MDAs) and Local Government Authorities (LGAs).
Ladies and Gentlemen;
As I alluded to earlier, Public Financial Management is not simply a matter of accounting. It is also a matter of accountability. For that matter, the Government has continued to strengthen the national audit office, Controller and Auditor General’s (CAG) Office to enable it perform its functions properly and efficiently in auditing Government expenditures and public finances. The Public Audit Act, enacted in 2008 vested more powers to the CAG giving him greater autonomy to execute his functions. It bestowed greater independent and therefore, more efficient performance.
We also expanded the scope of audit beyond auditing books of accounts, to include forensic audit and value for money audit. The National Audit Office has become more vibrant and better known among the public. Over and above that, we have created the office of the Internal Auditor General to strengthen our internal audit capabilities within the government. The purpose is to improve monitoring and identification of irregularities way before, so that Accounting Officers can take prompt preventive and corrective measures before funds are mismanaged. Auditing should not only be about post mortem, rather it should be a continuous and embedded process of Public Finance Management.
We realized early on that, these reforms needed to be nurtured and backed by legal, institutional framework and political will to make them a succeess. They are inherently susceptible to resistance. Mindful of that, we have introduced systems for assessing these reform initiatives through Public Expenditure and Financial Accountability (PEFA). These actions provide a quantitative and qualitative analysis of the Public Finance Management (PFM) performance which identifies specific strengths and weaknesses in our system.
Challenges
Ladies and Gentlemen;
Despite the fact that, the traditional budget system and the inherent new features introduced in recent years have increased adherence to fiscal discipline and stability, the system’s effectiveness and management of public resources still face challenges. The rapid and dynamic changes in the Public Finance Management as the result of ICT application, pose a challenge to governments to keep up with the ever fast changing innovations.
We are therefore caught up in a cycle of reforms, with one reform informing another. I understand, this has become a toll order to many of you gathered here. Adding to that lot, is the increasing public and stakeholders demand besides the Parliaments that we were used to. Today, we have civil society, media and the public at large who want to know how their taxes are managed and spent. To some of us, it just makes running government more exciting, and our work not boring at all.
Tanzania’s Commitment
Ladies and Gentlemen;
May I reiterate that, Tanzania will continue to uphold and stay the course on Public Finance Management reforms. As you are aware, we are members of Open Government Partnership (OGP) initiative which espouses transparency and government information sharing to the Public. As a matter of fact, our Government Budget, respective Ministry’s budget and Controller and Auditor General’s Report (Audited Financial Reports) are discussed openly by the Parliament of the United Republic of Tanzania. Parliamentary session directly aired on Televisions. They are also open to the public and media. In addition, the Citizen Budget Books are distributed to cater for the normal citizens understanding of the budget in a simplified language. Furthermore, all allocation to all government Ministries, Departments and Agencies are all published in websites and different newspapers. We do so because we believe that, public finance is about public and, therefore it should be made public.
Ladies and Gentlemen;
Tanzania will continue with the Public Finance Management reforms. They have worked for us. They have been useful. We understand that at times these reforms have not been easily accepted by some parties. We are also aware that, reforms can be painful. These shortcomings of the reforms notwithstanding, the best way forward is not to abort them, but rather to improve on them and if need be introduce better reforms.
Conclusion
Ladies and Gentlemen;
I believe, I have said more than enough. I dread the idea of turning my opening remarks becoming a lecture. It is now my singular honour and pleasure to declare the 22nd Eastern and Southern Africa Association of Accountants General (ESAAG) Annual Conference officially open. I wish you good deliberations and a pleasant stay in Dar es Salaam. I urge you also to allocate some time in your busy schedule for sightseeing in Dar es Salaam and elsewhere in Tanzania before you leave.
Thank you for your attention
Asanteni kwa kunisikiliza

- Mar 01, 2015
HOTUBA YA MWISHO WA MWEZI FEBRUARI, 2015, YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOTOLEWA TAREHE 1 MACHI, 2015
Soma zaidiHotuba
Utangulizi
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuzungumza kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa hotuba za kila mwisho wa mwezi. Kwa mwisho wa mwezi wa Februari nina mambo matano ninayopenda kuyazungumzia.
Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura
Ndugu Wananchi;
Jambo la kwanza ni uandikishaji wa Wapiga Kura. Tarehe 24 Februari, 2015 Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda alizindua rasmi uandikishaji wa wapiga kura ikiwa ni sehemu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchini. Zoezi hili lilizinduliwa Makambako, Mkoani Njombe na litaendelea nchini kote mpaka litakapokamilika kwa mujibu wa ratiba itakayopangwa na Tume ya Uchaguzi. Uandikishaji unatumia teknolojia ya kisasa ya utambuzi wa alama za vidole (BVR) na macho ya mtu anayeandikishwa. Teknolojia hii itatusaidia kuondoa kutoaminiana, manung’uniko na madai kuhusu udanganyifu katika chaguzi zetu kwamba wamepiga kura wasiostahili. Kuanza kutumika kwa teknolojia hii ni kielelezo cha utashi wa Serikali kuwa nchi yetu iwe na chaguzi zilizo huru, wazi na haki.
Ndugu Wananchi;
Mtakumbuka kuwa, kabla ya uzinduzi wa zoezi hili, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya zoezi la majaribio ya uandikishaji wa wapiga kura kwa kutumia mashine za teknolojia hii mpya katika kata 10 katika Halmashauri za Kinondoni, Kilombero na Mlele kati ya tarehe 15 hadi 23 Desemba, 2014.
Habari njema ni kuwa, kwa kutumia mashine za BVR, idadi ya waliojiandikisha ilivuka lengo la uandikishaji kwa kipindi kilichopangwa katika Kata hizo. Katika Halmashauri ya Kilombero walioandikishwa walifikia asilimia 110.9 ya lengo, katika Halmashauri ya Mlele uandikishaji ulifikia asilimia 101 ya lengo na katika Jimbo la Kawe, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni walioandikishwa walikuwa asilimia 105.67 ya lengo. Mafanikio haya ni ya kutia moyo pamoja na changamoto za kiufundi zilizojitokeza na zile zinazotokana na upya wa mfumo wenyewe kwa watumiaji. Changamoto hizo zimefanyiwa kazi na watengenezaji wa vifaa vinavyotumika katika awamu hii ya uandikishaji wa wapiga kura nchi nzima.
Ndugu Wananchi;
Nimefarijika na taarifa kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari na uandikishaji wa wapiga kura limeanza vizuri Makambako. Wananchi wamejitokeza kwa wingi kuliko ilivyotarajiwa. Kati ya tarehe 23 hadi 25 Februari, 2015 kwa mfano, Tume ilitegemea kuandikisha wapiga kura 9,541 lakini kutokana na mwamko wa wananchi kuwa mkubwa wameweza kuandikisha wapiga kura 13,042. Kila kituo kilikuwa kinaandikisha kati ya wapiga kura 80 na 150 kwa siku. Lengo la Tume ni kuandikisha wapiga kura 32,000 katika Halmashauri ya Makambako ambako kwa siku wanatarajia kuandikisha watu 4,320. Naambiwa kuwa hesabu za juzi na jana wameandikisha hadi wapiga kura 6,000 kwa siku. Kwa kasi hii na kama mambo yatakwenda kama inavyotarajiwa, lengo hilo litafikiwa na hata kuvukwa.
Ndugu Wananchi;
Hatuna budi kutoa pongeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa hatua hii ya kutia moyo tuliyofikia katika mchakato huu. Inaondoa hofu iliyoanza kuingia miongoni mwa baadhi ya watu kuwa huenda zoezi hili lisingefanikiwa. Tunachokitaka kwa Tume ni kuona zoezi hili linaendelea na kukamilika kama ilivyopangwa. Napenda kurudia ahadi niliyokwishaitoa kwa Tume kwamba Serikali itafanya kila linalowezekana kuiwezesha kirasilimali ili iweze kutimiza jukumu lake hilo. Nimekwishawakumbusha Hazina kuhusu umuhimu wa zoezi hili kufanikiwa kama ilivyopangwa. Hivyo basi, nimewataka wahakikishe kutoa kipaumbele cha kwanza katika mgao wa fedha. Kama haifanyiki nawaomba Tume waniambie mimi mwenyewe.
Wito wangu kwenu, wananchi wenzangu, ni kujitokeza bila ya kukosa kwenda kujiandikisha kwa mujibu wa ratiba ya uandikishaji katika maeneo yenu kama itakavyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Msifanye ajizi maana hakutakuwepo na fursa nyingine ya kujiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu baada ya fursa hii kupita.
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyoelezwa na Tume na mimi kusisitiza mara kadhaa kuwa watakaojiandikisha wakati huu ndio watakaopiga kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa na ndio watakaopiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu. Vitambulisho vya zamani vya mpiga kura havitatumika, hivyo watu wote ambao ni Watanzania na wana umri wa miaka 18 au zaidi lazima wajitokeze kuandikishwa upya. Watu pekee ambao hawatapaswa kujiandikisha tena ni wale tu walioandikishwa katika zoezi la majaribio lililofanyika katika zile kata 10 za Halmashauri za Kinondoni, Ifakara na Mlele mwezi Desemba, 2014. Vitambulisho walivyopata ndivyo vyenyewe.
Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii pia kuwaomba viongozi wa vyama vya siasa, Serikali, dini na asasi za kiraia kuungana na Serikali na Tume ya Uchaguzi katika kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi wakajiandikishe. Naomba tusiwachanganye wananchi kwa kutoa taarifa zisizokuwa za kweli na kuwafanya wakaacha kujiandikisha. Sisi katika Serikali tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa kila atakayejitokeza kujiandikisha anaandikishwa. Aidha, tutahakikisha kuwa kila panapojitokeza changamoto zinatafutiwa ufumbuzi kwa wakati mwafaka.
Tunatambua kuwa mfumo huu ni mpya hivyo panaweza kujitokeza changamoto zinazosababishwa na upya wake. Nawaomba wahusika kuendelea kuwaelimisha watendaji wanaohusika ili wapate uzoefu unaostahili. Aidha, nawasihi wananchi kuwa wavumilivu na waelewa pale ambapo wakati mwingine watalazimika kukaa kwenye mistari kwa muda mrefu kusubiri kujiandikisha, au wakalazimika kuja siku ya pili.
Ndugu Wananchi;
Kupiga kura kuamua kuhusu Katiba Inayopendekezwa au kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani ni haki na wajibu wa kila raia. Lakini, kuipata haki hiyo na kuweza kutimiza wajibu huo kunategemea kuwa na kitambulisho cha mpiga kura. Bila ya hivyo haiwezekani. Haya shime jitokezeni, mjiandikishe, ili muweze kuitumia haki yenu na kutimiza wajibu wenu wa kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa na kuchagua viongozi mnaowaona wanafaa kuongoza nchi yetu, jimbo lako na kata yako.
Kura ya Maoni
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ninalotaka kulizungumzia ni kuhusu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa. Kama mjuavyo, baada ya Bunge Maalumu la Katiba kutunga Katiba Inayopendekezwa na Rais kuchapisha Katiba hiyo katika Gazeti la Serikali na kutangaza siku ya kupiga kura ya maoni, kinachoendelea sasa ni matayarisho ya kufanyika kwa kura hiyo. Yapo majukumu ya Serikali, yapo majukumu ya Tume ya Uchaguzi, na yapo majukumu ya Serikali na Tume kwa pamoja. Utekelezaji umeishaanza na unaendelea. Miongoni mwa mambo yanayotakiwa kufanyika ni uandikishaji wa wapiga kura ambao umekwishaanza na unaendelea.
Ipo pia kazi ya kuchapisha na kusambaza Katiba Inayopendekezwa ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa kabla ya kupiga kura ya maoni. Tayari Katiba Inayopendekezwa imetangazwa katika tovuti za Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo na katika tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia imechapichwa magazetini.
Hadi tarehe 27 Februari, 2015 vitabu 1,558,805 vilikuwa vimechapishwa na nakala 1,341,300 kusambazwa. Nakala 1,141,300 zimesambazwa kwenye mikoa 25 ya Tanzania Bara na nakala 200,000 zimegawiwa kwa Zanzibar. Kwa upande wa Tanzania Bara kila Kata imepewa vitabu 300. Kwa vile Kata zina wastani wa vijiji vitano (5) hii ina maana kwamba kila kijiji kimepata vitabu 60 kwa kila kijiji ambayo si haba.
Ndugu Wananchi;
Tume ya Uchaguzi itatoa maelekezo kuhusu utaratibu wa kutoa elimu kwa umma. Nimeambiwa tayari asasi za kiraia 420 kwa upande wa Bara na 75 kwa upande wa Zanzibar zimejiandikisha kwa ajili ya zoezi hilo. Halikadhalika, Tume itatoa maelekezo husika kuhusu kampeni ya Kura ya Maoni wakati ukiwadia. Naomba watu wawe na subira na kuzingatia masharti ya Sheria ya Kura ya Maoni na Kanuni zake. Tukifanya hivyo, zoezi hili muhimu na la kihistoria litatekelezwa kwa usalama na utulivu. Watu watafanya uamuzi kwa uhuru, uelewa, amani na usalama.
Hali ya Usalama Nchini
Ndugu wananchi;
Jambo la tatu ninalotaka kulizungumzia ni hali ya usalama nchini. Kwa jumla hali ya usalama ni nzuri, hata hivyo kuna matukio ya kiusalama ambayo ningependa kuyazungumzia. La kwanza ni mashambulizi yenye sifa za ujambazi na mwelekeo wa kigaidi. Na, la pili ni la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Katika kipindi cha miezi 12 hivi kumekuwa na matukio ya watu kuvamia vituo vya Polisi, wengine wanachoma moto au wengine wanapora silaha. Pia kumekuwepo na matukio ya kuwashambulia Polisi walioko kwenye doria na wengine kuporwa silaha. Vituo vya Polisi vilivyovamiwa na silaha kuporwa ni vya Newala Mkoani Mtwara silaha tatu ziliporwa, Ikwiriri katika Wilaya ya Rufiji silaha saba, Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga silaha tano, mbili za polisi na tatu za raia waliokwenda kuzihifadhi pale, na Ushirombo Wilaya ya Bukombe silaha 18. Pugu Machinjioni na Tanga, askari waliokuwa katika shughuli za ulinzi na doria walishambuliwa na kuporwa silaha tatu. Kule Songea kulikuwepo na matukio mawili ya Polisi kushambuliwa lakini silaha hazikuporwa.
Bahati mbaya, vijana wetu saba wa Jeshi la Polisi walipoteza maisha katika matukio hayo. Newala alikufa Polisi mmoja, Kimanzichana mmoja, Ikwiriri wawili, na Ushirombo watatu. Wapo Polisi kadhaa waliopata majeraha ya namna mbalimbali katika mashambulizi haya.
Ndugu Wananchi;
Silaha zote 18 zilizoporwa Ushirombo zimepatikana na watu 10 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo wamekamatwa. Katika tukio la Tanga silaha moja kati ya mbili zilizoporwa imepatikana. Watuhumiwa saba wametiwa mbaroni, wanne kati yao ni wale waliokuwa wamejifisha katika mapango ya Kiomoni katika Kitongoji cha Karasha-mikocheni, kilichoko kijiji cha Mzizima wilayani Tanga. Tayari watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la Ikwiriri wamekamatwa. Polisi wanaendelea na upelelezi kuwapata watu wengine na kuzipata silaha saba zilizoporwa kituoni hapo. Kwa tukio la Newala silaha zote tatu zimepatikana pamoja na bastola moja ya mtuhumiwa aliyehusikaa na watu wawili wametiwa nguvuni. Hali kadhalika, upelelezi unaendelea wa kuzipata silaha zilizoporwa ambazo hazijapatikana mpaka sasa: yaani Kimanzichana moja, Pugu Machinjioni moja na Tanga iliyosalia moja.
Ndugu Wananchi;
Matukio haya yana sura mbili. Yana sura ya ujambazi, lakini pia baadhi yake yana dalili za ugaidi. Vyombo vyetu vya usalama vinaendelea kufanya kazi yake ya uchambuzi wa kila tukio na kulipa nafasi yake stahiki. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa Jeshi la Polisi wakishirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na vyombo vingine vya usalama kwa kazi kubwa na nzuri waifanyayo kupambana na uhalifu nchini. Mafanikio tunayaona, kama nilivyoeleza na kama tulivyosikia kule Tanga hivi karibuni ni matunda ya ushirikiano huo. Hata hivyo, nimewataka waendelee kuwasaka watu hawa waovu po pote walipo ili wafikishwe mahakamani na kuzirejesha mikononi mwa Polisi silaha zote zilizoporwa.
Nawaomba wananchi wenzangu wote kushirikiana kwa karibu na vyombo vya usalama hususan Jeshi la Polisi ili tuweze kupata mafanikio zaidi dhidi ya uhalifu huu na uhalifu mwingineo. Nawaomba mfanye mambo mawili: Kwanza, toeni taarifa Polisi mnapozipata habari za vitendo viovu au nyendo za watu waovu wanavyokusudia kufanya wahalifu au taarifa za wale waliokwishafanya uhalifu.
Pili, naomba watu waache kuwashabikia watu hawa waovu wala kueneza taarifa zao potofu kwenye mitandao ya kijamii. Badala yake tutumie mitandao ya kijamii kuponda fikra zao potofu, fikra zao hasi na vitendo vyao viovu pamoja na kuwafichua wao na mambo yao mabaya wayafanyo. Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wote walioweza kutoa taarifa zilizowezesha kuzuia uhalifu usifanyike au zilizowezesha kutiwa mbaroni kwa wahutumiwa wa vitendo vya ujambazi na ugaidi. Hatuwezi kushinda uhalifu bila ushirikiano baina ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Mauaji ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi
Ndugu wananchi;
Nimesikitishwa sana na taarifa kuwa mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yameibuka upya baada ya hali kuwa tulivu mwaka 2011. Mwaka jana (2014) yalitokea matukio matatu katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Simiyu na mwaka huu limetokea tukio moja mkoani Geita.
Lazima tulaani vikali mauaji ya ndugu zetu albino. Ni vitendo vya kinyama ambavyo havitegemewi kufanywa au kutokea katika jamii yeyote ya watu waliostaarabika, ya watu wanaomuabudu Mungu. Watu wenye ulemavu wa ngozi ni wanadamu wenzetu, wenye haki sawa ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yao kama walivyo wanadamu wengine. Hawastahili kufanyiwa wanayofanyiwa. Hawapaswi kuishi kwa hofu katika kijiji chao, mtaa wao au katika nchi yao. Jamii nzima na sisi sote mmoja mmoja na katika umoja wetu, tunao wajibu wa kuhakikisha usalama wa maisha yao na mali zao kama ilivyo kwa watu wengine wote.
Kwa kweli, mauaji ya albino ni jambo linalofedhehesha na kulidhalilisha taifa letu. Ni vitendo visivyovumilika. Hatuna budi sote kushikamana na kuhakikisha kuwa tunapambana nao kisawasawa na kuwashinda. Tusikubali kamwe wakaturudisha kule kubaya tulikokuwa zamani. Naungana na Chama cha Albino Tanzania kulaani ukatili huu na kutaka watu wote wanaojihusisha na ukatili huu wasakwe, wakamatwe, wafikishwe Mahakamani na kupewa adhabu kali inayowastahili wanapopatikana na hatia.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwahakikishia kuwa wakati wote Serikali imelipa uzito mkubwa suala la kudhibiti na kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au kukatwa baadhi ya viungo vyao wenyewe wakiwa hai. Tumefanya hivyo bila ya kuchoka tangu tukio la kwanza baada ya mimi kuingia madarakani Aprili 17, 2006 na miezi mitatu tu kule Nyahunge, Geita alipouawa Alfa Amon ambapo watuhumiwa wawili waliuawa na raia. Mwaka 2007 kulikuwa na matukio saba. Mwaka 2008 ndio ulikuwa mwaka mbaya sana walipouawa watu 18.
Kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi mauaji yalipungua na kuwa tisa mwaka 2009. Mwaka 2010 kukawa na tukio moja na mwaka 2011 hapakuwepo na tukio lolote. Mwaka 2012 kukawa na tukio moja, mwaka 2013 aliuawa mtu mmoja na wawili kujeruhiwa. Mwaka 2014 waliuawa watu watatu na wawili kujeruhiwa, na Januari, 2015 kumetokea tukio moja kule Geita.
Ndugu Wananchi;
Tangu mwaka 2006 mpaka 2015, watuhumiwa 139 wametiwa nguvuni, miongoni mwao wako watuhumiwa 16 wa matukio ya Desemba na Januari mwaka huu. Mashauri 35 yamefunguliwa mahakamani na kati ya hayo 10 bado yanaendelea na yapo katika hatua mbalimbali. Watuhumiwa 73 wameachiliwa na 15 wamepatikana na hatia. Kati ya hao waliopatikana na hatia 13 wamehukumiwa kifo na wawili wamepata kifungo cha miezi 6. Watuhumiwa kwa matukio sita bado wanasakwa.
Matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yametokea katika mikoa kumi kati ya mikoa 30 hapa nchini. Mikoa hiyo ni hii ifuatayo: Mwanza matukio 13, Kagera sita, Tabora matano, Geita manne, Mara manne, Kigoma manne, Simiyu matatu, Shinyanga mawili, Arusha moja na Mbeya moja. Utaona matukio 41 kati ya 43 yametokea katika ukanda wa ziwa ambapo pia wanaongoza kwa mauaji ya vikongwe na wanawake kwa sababu za ushirikina.
Ndugu Wananchi;
Inawezekana kuwa matukio ya hivi karibuni yanaashiria kuwa uhalifu huu unataka kuibuka upya. Napenda kuwahakikishia ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na Watanzania kwa jumla, kuwa hatutaacha hali iwe mbaya kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Tutatumia mbinu na maarifa tuliyoyatumia kukabili wimbi kubwa la mauaji lililokuwepo mwaka 2007 na 2008 na kwa sababu hiyo tukaweza kupunguza hadi kufikia kutokuwa na tukio lolote la mauaji mwaka 2011.
Tunachokiomba kutoka kwa wananchi ni ushirikiano na msaada wa kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya mauaji na kukata viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi. Pia wasaidie kutoa taarifa kuhusu wanunuzi wa viungo hivyo na waganga wanaochochea mahitaji ya viungo vya albino. Ushirikiano wa wananchi wa wakati ule uliwezesha kupatikana kwa mafanikio niliyaeleza. Naamini safari hii tukifanya hivyo tutafanikiwa pia.
Ndugu Wananchi;
Kutokomeza kabisa matukio ya mauaji na ukataji wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi ni jambo linalowezekana. Hata hivyo, litategemea watu kuacha imani za ushirikina. Imani potofu, ati kuwa mtu akiwa na kiungo cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi atafanikiwa katika shughuli zake za biashara, uvuvi na uchimbaji wa madini ndicho kichocheo cha uovu wote huu unaoendelea. Ni ujinga ulioje kwa mtu kuamini kuwa mafanikio yake hayatategemea juhudi zake na maarifa yake bali kuwa na kiungo cha mwanadamu mwenzake mwenye ulemavu wa ngozi.
Nilisema katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi Machi, 2008 kwamba, kama kuwa na kiungo cha albino ndiko kutakakomfanya mtu kufanikiwa katika shughuli zake za kibiashara na kiuchumi basi ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi wangekuwa ndiyo matajiri wakubwa nchini na duniani. Maana wao sio tu wana viungo bali wana mwili mzima. Kwa sababu ya kuwepo imani hizi za hovyo, juhudi za kuelimisha jamii kuachana na imani hizi potofu ziongezwe. Naomba hili ndilo liwe jambo la msingi katika mapambano haya. Tukifanikiwa katika hili, matatizo yote haya yatakoma. Serikali na jamii haitalazimika kushughulikia mambo haya ambayo siyo tu ni fedheha hata kumsimulia mtu bali yanatisha na kusikitisha.
Ndugu Wananchi;
Wiki ijayo nitakutana na baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi. Nimekubali maombi yao ya kukutana nao ili niweze kusikiliza maoni yao na tubadilishane mawazo juu ya namna bora ya kumaliza tatizo hili. Mimi naamini kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na jamii utatuwezesha kutokomeza mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na kuliondolea taifa letu aibu hii.
Ziara ya Zambia
Ndugu Wananchi;
Tarehe 25 na 26 Februari, 2015 nilifanya ziara ya siku mbili ya kiserikali nchini Zambia kwa mwaliko wa Rais mpya wa nchi hiyo, Mheshimiwa Edgar Lungu. Ziara ilikuwa na mafanikio makubwa. Mimi na ujumbe wangu tulifarijika sana kuona kuwa mawazo ya nchi zetu mbili yanashabihiana sana kuhusu namna ya kuimarisha na kuboresha uhusiano wetu na ushirikiano na uhusiano wa nchi zetu mbili. Kimsingi tumekubaliana katika masuala yote muhimu tuliyoyazungumza.
Kuhusu TAZARA tumekubaliana kuchukua hatua thabiti kutatua matatizo ya kiungozi, kifedha na kiufundi yanayolikabili shirika letu hilo hivi sasa. Tumeelewana kuwa hatuna budi kufanya marekebisho ya kimfumo na kiutendaji ili kutatua matatizo ya kimuundo na kimenejimenti yanayochangia kuzorota kwa ufanisi wa Shirika. Tumekubaliana pia kuwa, Serikali zetu mbili zitekeleze ipasavyo wajibu wake kwa TAZARA ikiwa ni pamoja na kutoa mchango wake wa fedha kwa ajili ya kulifufua Shirika hili muhimu kwa uchumi wa nchi zetu mbili.
Ndugu Wananchi;
Tumekubaliana pia, kwamba, tuangalie uwezekano wa kuruhusu makampuni au mashirika mengine ya reli kutumia reli ya TAZARA kusafirishia mizigo yao kwa kulipa ushuru kwa TAZARA kwa huduma hiyo. Tumeagiza Baraza la Mawaziri kulifanyia kazi wazo hili jema ili litekelezwe mapema iwezekanavyo.
Kwa upande wa sekta ya nishati, tumekubaliana kuwa, nchi zetu mbili ziendelee kushirikiana kuimarisha bomba la mafuta la TAZAMA. Ndugu zetu wa Zambia walitueleza dhamira yao ya kutaka kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia. Wameomba tukubali kuwauzia gesi asilia. Niliwaeleza ni jambo linaowezekana, tumekubaliana nchi zetu zilifanyie kazi ombi hilo.
Serikali ya Zambia, imeahidi kuimarisha njia ya umeme kutoka Kasama hadi Mbala Zambia inakoanzia njia inayoleta umeme Sumbawanga. Kufanya hivyo kutaondoa matatizo ya sasa ambapo umeme unaofika Sumbawanga kutoka Mbala huwa mdogo kiasi kwamba hauna nguvu ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani, maofisini na viwandani. Kwa sababu hiyo, hata mpango wa kuupeleka umeme huo Namanyere, Nkasi na Mpanda haukuweza kutekelezwa kama ilivyokuwa imekusudiwa awali.
Ndugu Wananchi;
Kuhusu kuboresha huduma kwa abiria na mizigo katika mpaka wa Tanzania na Zambia pale Tunduma, tumekubaliana kuwa, Serikali ya Tanzania ikamilishe ujenzi wa jengo litakalowezesha huduma zote muhimu za mpakani kutolewa katika jengo hilo (One Stop Border Post). Wakati tunasubiri kukamilisha ujenzi huo, tumekubaliana tuwe na jengo la muda la kurahisisha taratibu za usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo katika mpaka wetu na Zambia.
Vilevile, tulizungumzia njia za kuimarisha na kuboresha taratibu za forodha kwa mizigo itokayo bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Zambia. Tumekubaliana kuwa, Mamlaka ya Kodi ya Mapato ya Zambia iangalie uwezekano wa kuwaweka maafisa wake katika Bandari ya Dar es Salaam kama inavyofanyika kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hii itarahisisha taratibu za forodha kwa bidhaa za Zambia katika bandari yetu. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeshaanza mchakato wa kupata fursa hiyo. Kwa jumla, ziara ilikuwa ni yenye mafanikio makubwa.
Rambirambi
Ndugu Wananchi;
Wakati tulipokuwa tunajiandaa kurekodi hotuba hii tukapata habari ya huzuni na majonzi makubwa ya kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mheshimiwa Capt. John Damian Komba. Kifo chake kimeliondolea taifa letu mmoja wa viongozi wake wazuri, msanii mahiri, raia mwema na mzalendo wa kweli. Marehemu alitumia muda mwingi wa maisha yake kuelimisha jamii kuhusu mambo mema, amefanya hivyo akiwa mwalimu na baadaye Kiongozi wa Kikundi cha Sanaa cha JWTZ na hapa mwishoni kiongozi wa kikundi cha Tanzania One Theatre cha Chama Cha Mapinduzi. Kwa kutumia kipaji alichojaaliwa na Mola wake ametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu na ustawi wa Chama Tawala. Daima tutamkumbuka kwa mambo mengi mema aliyoifanyia jamii ya nchi yetu na taifa kwa jumla.
Ndugu Wananchi;
Katika salamu zangu za rambirambi kwa Spika wa Bunge na Katibu Mkuu wa CCM niliwaomba kupitia kwao salamu ziwafikie Wabunge wote na viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Hali kadhalika, niliomba kupitia kwao salamu ziwafikie familia ya marehemu Capt. John Komba. Kwa familia ya ndugu yetu mpendwa, napenda kuwahakikishia kuwa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo. Tunawaombea kwa Mola awape moyo wa subira na uvumilivu. Wananchi wa Wilaya ya Nyasa tunawapa pole nyingi kwa msiba mkubwa uliowakuta na pengo kubwa mlilolipata. Nawaomba watambue kuwa namna bora zaidi ya kumlilia Mbunge wao aliyewapenda ni kudumisha mema yote aliyofanya na kukamilisha zile kazi ambazo alikusudia kuzifanya lakini hakuweza kufanya hivyo kwa sababu ya kukutwa na umauti.
Mwisho nawaomba, Watanzania wote tuungane na familia yake kumwombea marehemu Capt. John Damian Komba mapumziko mema. Amin.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibari ki Tanzania!
Asanteni kwa kunisikiliza.

- Feb 22, 2015
REMARKS BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AT THE STATE BANQUET HOSTED IN HIS HONOUR BY H.E. EDGAR CHAGWA LUNGU, PR...
Soma zaidiHotuba
Your Excellency Edgar Lungu and Mrs. Esther Lungu;
Your Excellency Madame Inonge Wina, Vice President;
Honourable Ministers and Members of Parliament;
Your Excellencies, Ambassadors and High Commissioners;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
I thank Your Excellency and dear brother for the kind words you have said about me, my country and the excellent relations which so happily exist between our two sister-republics. I cannot find words good enough to express my profound joy to be able to pay a visit to Zambia, so early into your Presidency. In this regard, I sincerely thank you for your kind invitation and the very warm reception and gracious hospitality. You have made my wife and I and our entire delegation feel very much at home. This is the typical Zambian reception we know. I also thank you so much for the wonderful arrangement which has made my short visit very successful. It speaks a thousand words about the importance you attach to our relations.
I bring with me, very warm and fraternal greetings from the government and your brothers and sisters in Tanzania. They heartily congratulate you on your well deserved election to the highest office of your great country, despite the preceding sad circumstances which necessitated the elections. They wish you well and pray for your success in steering the affairs of your great nation.
The people of Tanzania look to this visit with great enthusiasm and optimism. They do so because, it has been a tradition since the days of the founding fathers of our two sister Republics, His Excellency Kenneth Kaunda and His Excellency Mwalimu Julius Nyerere (now late) that the exchange of such visits not only advance our relations but, also, come up with big things.
The previous meetings between our leaders give birth to the Tanzania – Zambia Highway, the Tanzania – Zambia Railway (TAZARA), the TAZAMA Pipeline and a host of joint endeavours. These symbolic projects have always been the umbilical cord linking our two nations and two peoples. They have been defining and sustaining our bilateral relations. When some of these institutions would be going through difficulties, meetings like ours would help resolve or easy them.
Indeed, our people were right to harbour such expectations. The very fruitful official talks we held, lived up to their wishes and expectations. Let me say that all the pertinent issues obtaining in the Zambia-Tanzania relations and cooperation were discussed in depth and breath. Mutual understanding was reached, particularly on ways and means to tackle the challenges being experienced and develop our bilateral relations and cooperation to the greatest heights possible. This underlines the trust and confidence between our two countries. The cordial nature of the discussions is worth mentioning, for it speaks volumes about the special bonds and friendship between our two countries.
We have discussed ways to revive TAZARA and make it a well functioning railway line for the benefit of our two countries and the region. We discussed the TAZAMA pipelines, the Tanzania - Zambia Highway, the Dar es Salaam Ports, Tunduma/Nakonde border post, as well as movement of people of our two countries. We explored other matters of mutual interest and benefit to our two countries and two peoples. Sincerely, I will go home tomorrow immensely satisfied with the state of our relations. There is a very bright future ahead of us.
Your Excellency;
I am glad we both saw the need of doing more to promote trade and investments between our countries. It is in this regard that I agree with you that we should encourage our Chambers of Commerce and captains of Industries to be more proactive in promoting relations between them. Let them play their rightful role and help grow our economies, create jobs and alleviate poverty. We would like to see them pressurize our two governments to do better with regard to our facilitation role. We also, underscored the role of the Joint Permanent Commission (JPC) as a vehicle to strengthen and advance our bilateral cooperation. Accordingly, we tasked our Ministers responsible for the various cooperation sector to ensure better performance and delivery.
Your Excellency;
I am confident that Tanzanians and Zambians will witness positive things happening in all our areas of cooperation from now on because of this visit. Some will be soon while some will take a while. Honestly, I could not have had a fulfilling visit than this. Once again, I extend my sincere gratitude to you and the people of Zambia for the unmatched friendly welcome, generosity and a very successful short visit. We wish we could stay longer. I hope, you will also find time out of your busy schedule to pay a visit in the near future. It has been a while since we hosted a Zambian President for an official visit in Tanzania. We look forward to welcome you to your second home.
Your Excellency;
Distinguished Guests;
Ladies and gentlemen;
May I now ask all of you present to rise and join me in a toast to the continued good health and success of His Excellency the President and Madame Esther Lungu; to continued friendship and cooperation between our two countries and peoples.
Asanteni sana.
- Feb 20, 2015
SPEECH BY THE CHAIRPERSON OF EAC HEADS OF STATE AT THE 16TH SUMMIT OF EAC HEADS OF STATE AT THE KENYATTA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE, NAIROBI, KENYA ON 20T...
Soma zaidiHotuba
Your Excellency Uhuru Kenyatta, President of the Republic of Kenya,
Immediate Past Chair and Host of This Summit;
Your Excellency Yoweri Museveni, President of the Republic of Uganda;
Your Excellency Paul Kagame, President of the Republic of Rwanda;
Your Excellency Pierre Nkurunziza, President of the Republic of Burundi;
Your Excellency Salva Kiir Myardit, President of the Republic of South Sudan;
The Chairperson of the Council of Ministers, Honourable Dr. Harrison Mwakyembe;
Honourable Ministers;
The Secretary General of the East African Community;
The Honourable Speaker of EALA;
His Lordship Judge President of EACJ;
Members of EALA and National Parliaments;
Members of the Diplomatic Corps;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
Excellencies;
I thank you President Uhuru Kenyatta and the people of Kenya for the warm reception and gracious hospitality. This is befitting Kenyan hospitality that we know. We don’t feel like strangers when in Nairobi. You always make us feel at home away from home. We are gratified, indeed.
I commend the East African Community Secretariat under the able leadership of our illustrious Secretary General, Ambassador Dr. Richard Sezibera for the good preparations and organization of this Summit.
Excellencies;
I thank you for the trust and confidence you have reposed in me and my country. I promise you that I will do my best to live up to your expectation. I will not let you down nor will my government and the people of the United Republic of Tanzania. I commend my predecessor, His Excellency Uhuru Kenyatta, for steering the affairs of our regional economic grouping so well. In the past one year of his leadership a lot has been achieved as it has been very well documented in the Report of the Chairperson of the Council of Ministers. It has been one year of good harvest for our region. I am here to assure you of Tanzania’s commitment to stay the course and propel our integration process to greater heights. Taking over from your good work and strong foundation makes my task ahead to be easy. We will build on your achievements and take our Community to the next level.
Tanzania and EAC
Excellencies;
To us in Tanzania, as it is the case with all East African Community partner states, regional integration is a matter of both principle and policy. We are staunch supporters of the integration process and formidable believers in African Unity and the East African economic and political integration. We strongly believe that, a divided East Africa, will not be able to claim its rightful place and earn respect in the family of nations on the African continent and on this planet. We are aware that fragmented markets, isolated industrial value chains, as well as inadequate cross border infrastructure, have no place in the world that we live in today, and the one ahead of us.
We also, sincerely believe that the best and easiest way to realize continental unity and integration, in Africa, is through regional integration as building blocks. That is why East African integration is very dear and crucial to all of us gathered here. This is why we, in Tanzania wholeheartedly welcome the opportunity to serve as Chairman of the East African Community. Rest assured that the East African Community is in very safe hands.
The State of the EAC
Excellencies;
As we meet here today, and as very elaborately explained by President Kenyatta and Honourable Dr. Mwakyembe, a lot of ground has been covered in the implementation of the East African cooperation and integration agenda. It is heartwarming indeed, to note that trade has increased in a very big way. And, the good thing is, all partner states are realizing the benefits. As we all know very well, trade is the life line of our integration endeavours. In many ways trade drives and holds together any integration process.
Formal intra-East African Community trade for the period from 2010 to 2013 increased from USD 3,722.9 million to USD 5,805.6 million. There was 6.1 percent increase in trade between 2012 and 2013 alone which is quite remarkable. This is not a small achievement at all. It is not merely a matter of numbers, because beneath these numbers lies contacts, relationships and lives touched as well as households transformed. If informal trade statistics were to be captured and included, certainly the volume and value of the trade in the East Africa Community region could be even higher.
It is high time we sought better ways of formalizing the informal sector and informal trade in the integration process. This way important economic statistics and information will be captured. Also, government revenues will be collected. In this regard, we should direct our energy to supporting small and informal businesses by putting in place enabling environment that includes capacity building, provision of technical and financial services. In the meantime, we should do all within our power to take requisite action to eliminate all outstanding non-tariff barriers.
Custom Union
Excellencies;
The East African Community’s flagship integration institution, the Customs Union, is working well. Currently, all goods produced in East Africa which conform to the agreed principle of Rules of Origin, are moving across the borders of the five Partner States duty free. The Customs Union has continued to show positive impact on the economies of East African Community partners states. Government revenues have been increasing year after year. Customs revenue performance for example, was 96.86 percent of the target in 2013 compared to 89.55 percent in 2010. Customs revenues contributed on the average to about 35 percent of total revenues of the Partner States in 2013. This is a momentous achievement.
I believe we could have achieved much more had we succeeded in removing all non tariff barriers. We should do all within our powers to take requisite action to eliminate all outstanding non-tariff barriers. It is in this regard, therefore, I intend to work closely with all of you in ensuring that non-tariff barriers no longer become scourge encumbering the smooth operation of the Customs Union and Common Market in East Africa.
Excellencies;
Work towards full operationalization of the East Africa Single Customs Territory is also progressing well in all countries. So far, so good. It has proven to be useful in reducing non-tariff barriers associated with unnecessary delays in cross border trade and transportation. It also promotes transparency and efficiency in tax and revenue collection. The full realization of Single Customs Territory will be a big leap forward in our resolve to increase flow of trade and efficiency within the Customs Union. It makes implementation of the objectives of the Customs Union easier and faster.
It is encouraging to note the good work being done by East African Community partner states, individually or in collaboration with others, of improving physical infrastructure in the region. There is visible progress in roads, ports, airports, railways and power subsectors and several related sectors and sub-sectors. However, there is need to do a lot more because there is a huge infrastructure deficit in our respective countries and in the region at large. We must seek to do better on mobilization of domestic and external resources for infrastructure development to match with the pace of our fast moving integration.
EAC Common Market
Excellencies;
The ongoing implementation of the Common Market Protocol and the laying of the foundation for the Monetary Union is set to propel our region to become the most advanced regional integration undertaking on the African continent. However, the 2014 East African Common Market Score Card indicated a slow trend and progress by member states in the implementation of some of aspects of the Common Market Protocol. Fortunately, key recommendations have been proposed on increasing the pace of implementation. All of us must ensure full implementation of these recommendations.
With regard to Free Movements of Services, for example, we are told, 63 measures out of 500 key sectoral laws and regulations of partner states were indentified to be inconsistent with the Common Market Protocol. Strangely, professional services accounted for 73 percent of these. In terms of movement of goods, the scorecard appreciates that, a lot has been done, however, non tariff barriers, particularly those related to sanitary and phytosanitary measures remain notorious. Only two out of the 20 capital operations are free of restrictions in all partner states. These are those related to external borrowing by residents and repatriation of proceeds from sale of asset.
We should be grateful that we have with us a tool we can use to measure progress and guide future action. It is important that we undertake to play our part accordingly, based on the findings and recommendations.
EAC Monetary Union
Excellencies;
Let us remain focused on the implementation of the Road Map on the Monetary Union. Specifically, let us make sure that the timelines agreed by all of us are observed. I further, call upon Partner States to fast track the process of attaining the Macro-Economic Convergence Criteria which is a critical factor in the implementation of the objectives of the East African Community Monetary Union.
As we all know, this stage consummates the East African Community economic integration agenda and, it is the last but one step to the ultimate destiny of the East African Federation. For sure, successful implementation of this stage will enable us to move to the political federation with greater confidence. We in Tanzania reaffirm our readiness and commitment to walk in step with the other partner states in ensuring that the East African Community integration process stays the course and succeeds.
Peace and Stability in the EAC
Excellencies;
East Africa is a region that can demonstrate with confidence that development and peace are intertwined. As a matter of fact, we can attribute our success in integration to the peace dividend that we enjoy. Peace, security, and stability are the lifeline to any meaningful integration. It ensures predictability in planning and is fundamental in attracting investments, promoting trade and unobstructed movement of people within the Community.
If we are to realize the fullest potential of our integration, we must continue to nurture the peace and stability we have. We ought to cooperate everywhere and at all levels to secure our region. Fortunately, we are already doing that at the moment, but we should always aspire to do better. I wish to acknowledge and commend the security cooperation that is taking good shape among the defence and security organs of the partner states. Such cooperation compliments the East African Community integration process. It is important that we continue to encourage and strengthen this cooperation to prosper. We should continue to assist other brothers and sisters of South Sudan and Somalia in their just quest for sustainable peace and security in their respective countries. I would like to assure them that we will continue to support them until peace is stored.
Excellencies;
This year will be politically exciting for the region. As President Uhuru Kenyatta has alluded to earlier, we are all aware, the Republic of Burundi will be going to the polls in May 2015 and my own country, the United Republic of Tanzania will be holding the General Elections in October, 2015. For Tanzania, also, in April, 2015 we will hold a referendum on the Proposed New Constitution. Both elections and the Tanzanian Referendum present a great opportunity for the two East African Community partner states to advance democracy, governance and stability which define and distinguish our region. It is, also, an opportunity for our region to demonstrate to the entire world and to our own people, that democracy reigns and democratic values have taken root in our midst.
Conclusion
Excellencies;
As I assume the Chairmanship, I look at the future of our Community with a great sense of optimism, pride, trust and confidence and for even bigger achievements in future. The milestones that we have covered and challenges we have endured, have made us stronger and better prepared to perform even better in future. I reiterate Tanzania’s commitment and readiness to do everything within our power to steer the affairs of the East African Community to greater heights of success during our term of leadership.
The success of our integration depends on all of us: leaders, nations and most importantly, the people who are the main purpose of forming the East African Community. Mine is the humble task of steering our collective efforts. If it is said that it takes the whole village to raise a child, certainly, it takes all of us to nurture a successful East African Community. It can be done, let us all play our part. Tanzania will surely play its part accordingly.
With these many words, I thank you for your kind attention.
ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA!

- Feb 18, 2015
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIKIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014, KATIKA SHULE YA...
Soma zaidiHotuba
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Ghalib Bilal;
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda;
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa;
Waziri wa Nchi OWM- TAMISEMI, Mhe. Hawa A Ghasia;
Naibu Waziri wa Elimu– OWM-TAMISEMI, Mhe. Kasimu Majaliwa;
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Anne Kilango Malecela;
Waheshimiwa Mawaziri wote mlioko hapa,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Said Meck Sadiki;
Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi Ombeni Sefue,
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Naibu Katibu Mkuu –OWM-TAMISEMI;
Katibu Mkuu- OWM-TAMISEMI;
Mabalozi
Wahisani wa Maendeleo;
Wakurugenzi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali;
Walimu, Wanafunzi, Wanahabari,
Mabibi na Mabwana.
Leo ni siku muhimu katika historia ya maendeleo ya elimu nchini. Tunakutanishwa kwa ajili ya kufanya jambo kubwa, la kihistoria na la kimaendeleo la uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014. Uzinduzi wa Sera mpya unaashiria mwanzo wa ngwe mpya katika safari ya kuimarisha, kuendeleza na kuipaisha elimu nchini kufikia viwango vya juu vya kukidhi ubora na mahitaji ya taifa. Ni kielelezo cha utashi na azma yetu ya kuboresha mfumo wetu wa elimu uende na wakati na kuiwezesha jamii kuzikabili ipasavyo changamoto na maendeleo na maisha yao. Maisha bora kwa Mtanzania yanaanzia na kutegemea uwezekano wa kila Mtanzania kupata fursa ya kupata elimu iliyo bora, elimu itakayomuwezesha kutawala mazingira yake na kukabili changamoto za maisha.
Nakupongeza sana Mheshimiwa Waziri, Dkt. Shukuru Kawambwa, Katibu Mkuu, Prof. Sifuni Mchome pamoja na wataalamu wenu na wadau wengine wa elimu kwa kuongoza na kusimamia mchakato huu ulioanza kwa kupitia Sera mbalimbali zilizokuwapo katika sekta ya Elimu na kuzihuisha kwa kuandaa Sera hii. Napenda pia kumtambua Naibu Waziri, Mheshimiwa Anne Malechela Kilango pamoja na upya wake katika Wizara.
Mheshimiwa Waziri;
Nakushukuru pia kwa uamuzi wenu wa kuzindua Sera hii katika eneo la shule. Tunapata fursa maridhawa ya kuoanisha kile kilichopo na kile tunachoazimia kutekeleza kwenye Sera. Nimepata fursa ya kutembelea maabara na kuwaona vijana wetu wanavyopata elimu ya sayansi kwa vitendo. Aidha, mnanipa nafasi ya kusema na walimu na wanafunzi ambao ndiyo wadau wakuu wa Sera hii ya Elimu. Ni jambo la faraja kwangu kuona tulipofikia na mafanikio tuliyoyapata, kama haya niliyoyaona katika shule hii. Inatupa kila aina ya sababu kuongeza bidii na kasi zaidi ya kufikia malengo makubwa zaidi.
Vilevile, nakushukuru, Mheshimiwa Waziri, kwa maneno yako ya utangulizi kuhusu Sera hii. Kama ulivyokwishasema, Sera hii ni matokeo ya mapitio na uhuishaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1966 na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu ya mwaka 1999. Kipindi cha zaidi ya kipindi cha miaka 14 ya utekelezaji wa sera hizo na maamuzi mengine kuhusu elimu kimekuwa cha mabadiliko mengi ya kijamii, kiuchumi na teknolojia ndani na nje ya nchi. Uchumi wetu umekua na kutanuka na kuzua mahitaji mapya ya rasilimali watu na stadi mbalimbali ambazo hazikuhitajika siku za nyuma. Aidha, mipango mitatu ya miaka mitano ya maendeleo kuelekea mwaka 2025 nayo imezaa mahitaji mengine. Yote haya pamoja na maoni ya wadau mbalimbali yamezingatiwa katika Sera hii ya mwaka 2014.
Hali ya Sekta ya Elimu
Mheshimiwa Waziri;
Ndugu Wadau wa Elimu;
Elimu ni kitu kinachomgusa na kumhusu kila mtu hapa Tanzania. Sisi katika Serikali, tunatambua wajibu wetu na nafasi yetu maalum kwa upatikanaji wa elimu nchini. Kwa ajili hiyo, elimu ni jambo la kipaumbele cha juu, ni la kufa na kupona. Ukweli wa usemi wangu huo unajihidhirisha katika uwekezaji mkubwa tunaoufanya katika kuendeleza elimu. Bajeti ya Elimu ndiyo iliyo kubwa kuliko zote kwa miaka mingi na imekuwa ikiongezeka. Kwa mfano, mwaka 2005/2006 zilitengwa shilingi bilioni 669.5 wakati mwaka 2014/2015 zimetengwa shilingi trilioni 3.1. Katika kipindi hicho, bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka kutoka shilingi bilioni 56.1 hadi shilingi bilioni 345. Kwa sababu hiyo idadi ya wanafunzi wanaofaidika imeongezeka kutoka 16,345 mwaka 2005 hadi 98,000 mwaka 2014. Shule za msingi zimeongezeka kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,343 mwaka 2014 na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi nayo kukua kutoka milioni 7.54 hadi milioni 8.23. Kwa upande wa sekondari shule zimeongezeka 531 mwaka 2005 hadi 4,576 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi nayo imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804.056 mwaka 2014.
Upanuzi huu mkubwa na wa kihistoria umetokea pia kwenye vyuo vya elimu ya ufundi stadi ambapo vyuo vimeongezeka kutoka 184 hadi 744 kati ya mwaka 2005 na 2014. Kwa upande wa elimu ya juu, idadi ya vyuo imeongezeka kutoka 26 hadi 50 kati ya mwaka 2005 na 2014 na kufanya idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iongezeke kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 200,986 mwaka 2014. Leo hii tunapokutana hapa, hatuna tena tatizo na fursa ya kupata elimu kwa elimu ya msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.
Mwaka 2005, urari wa wanafunzi kati yetu na wenzetu wa Afrika Mashariki ulikuwa wa chini mno kwa upande wetu. Kenya walikuwa na wanafunzi wa sekondari 925,341 na wa vyuo vikuu 108,407 ikilinganishwa na Tanzania iliyokuwa na wanafunzi 524,325 wa sekondari na 40,719 wa vyuo vikuu. Uganda ilikuwa na wanafunzi 728,393 wa sekondari na 124,313 wa vyuo vikuu. Sasa hali ni tofauti. Kwa mwaka 2013, kwa mfano, Kenya ilikuwa na wanafunzi wa sekondari 2,104,300 na wanafunzi wa vyuo vikuu 324,600. Katika mwaka huohuo, Uganda walikuwa na wanafunzi wa sekondari 1,362,739 na wa vyuo vikuu 140,403. Ongezeko hili linatuweka katika hali nzuri ya ushindani tunapoelekea katika ushindani wa soko la pamoja ndani ya Afrika Mashariki ikilinganishwa na hali ilivyokuwa miaka 10 iliyopita. Jukumu letu ni kuimarisha ubora wa elimu yetu na hasa iwe ni ile inayokidhi mahitaji ya soko la ajira nchini, Afrika Masharini na dunia.
Juhudi zetu hizi za kuendeleza elimu zimetambulika duniani na kutupatia heshima kubwa zikiwemo tuzo mbalimbali. Tumekuwa nchi ya kupigiwa mfano katika kutekeleza Malengo ya Milenia (MDGs) yanayohusu fursa ya watoto kupata elimu ya msingi, na usawa wa kijinsi baina ya watoto wa kiume na wa kike kupata elimu ya msingi na sekondari. Haya na mengine mazuri tuliyofanya ni mambo ya kujivunia. Ni mafanikio yanayotokana na utekelezaji mzuri wa Sera tatu za elimu ya Msingi, Ufundi na Elimu ya Juu zilizokuwepo.
Ndugu Wadau wa Elimu;
Mafanikio hayo makubwa nayo yamezua changamoto mpya mbalimbali. Miongoni mwake ipo ile ya malengo ya Elimu kuwa sawa na goli linalohama kila unapolikaribia. Hali hii haipo hapa nchini kwetu pekee, bali ipo kote duniani. Nimebahatika kutembelea nchi nyingi na kuona yanayofanyika. Hali kadhalika nimesoma yanayoendelea kwenye nchi mbalimbali kuhusu elimu. Ukweli ni kwamba hakuna nchi duniani ambayo imemaliza changamoto zote zihusuzo elimu. Katika kila nchi kuna mjadala unaoendelea kuhusu ubora wa elimu. Na, sababu ni moja, uboreshaji wa elimu ni jambo endelevu. Iko hivyo kwa nchi zinazoendelea kama yetu na hata zile zilizoendelea. Tofauti yetu ipo kwenye aina ya changamoto zilizopo. Nchi zilizoendelea hazina matatizo yanayozikabili nchi zinazoendelea.
Ni jambo la kutia moyo kuwa tangu uhuru mpaka sasa matatizo mbalimbali yanayoisibu elimu yametambuliwa na kushughulikiwa. Katika awamu hii ya uongozi wa nchi yetu tumetoa msukumo maalum tena mkubwa katika kutafuta majawabu ya changamoto zinazokabili sekta ya elimu nchini. Bahati nzuri tumepata mafanikio kwenye nyanja nyingi. Nimekwishaelezea jinsi idadi ya shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vya ufundi na vyuo vikuu vilivyoongezeka. Mambo hayo yameongeza sana fursa za elimu nchini. Hivi leo watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaweza kuwa shule labda wakatae wenyewe au wakatazwe na wazazi au walezi wasioona mbali. Watoto wote wanaofaulu darasa la saba wana hakika ya kwenda sekondari na vyuo vikuu vina nafasi wazi zinazosubiri wanafunzi wenye sifa kuzijaza.
Kimsingi tunaweza kusema kuwa suala la watoto na vijana wetu chini kupata fursa ya kupata elimu inayolingana na umri wao siyo tatizo kubwa tena la kutuumiza vichwa. Hata hivyo, kazi kubwa inayohitajika kuendelea kufanyika ni kuhakikisha kuwa elimu wanayopata watoto na vijana wetu ni bora. Kwa ajili hiyo, hatuna budi kuendelea kuboresha mazingira ya kutolea elimu. Walimu wa kutosha wawepo kwa masomo yote. Tena wawe ni walimu wanaoyamudu vyema masomo wanayofundisha. Hali kadhalika, huduma za msingi kwa maisha na utendaji kazi wa walimu ziboreshwe pamoja na maslahi yao.
Vifaa vya kufundishia na vile vya kusomea na kujifunzia vipatikane kwa uhakika. Majengo ya kufundishia na huduma mbalimbali shuleni na vyuoni yawepo ya kutosha tena yaliyo bora. Pamoja na hayo, mifumo na miundo ya uendeshaji na usimamizi wa elimu nchini iendelee kuboreshwe zaidi na zaidi.
Sera Mpya na Matumaini Mapya
Ndugu Wadau wa Elimu;
Sera Mpya ya Elimu inatupa mwanzo mpya na matumaini mapya ya kututoa hapa tulipo sasa na kutupeleka mbele kwenye neema na mafanikio makubwa zaidi. Mahali ambapo nyingi ya changamoto zinazotukabili sasa zitakuwa hazipo ila zitakuwepo zile za kupeleka elimu yetu mbele zaidi. Sera mpya inatambua umuhimu na nafasi ya elimu kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Sera inatambua kuwa Elimu ni silaha ya ukombozi kwa Watanzania dhidi ya umaskini na madhila yake. Ni nyenzo ya uhakika ya kutupeleka kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Kwa sababu hiyo, Sera inasisitiza umuhimu wa kuendelea kupanua fursa kwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule aende shule. Sera Mpya inatoa dhima kwa taifa kuanza safari ya kumuwezesha kila mtoto anayeanza darasa la kwanza aweze kupata elimu ya sekondari ya mpaka kidato cha nne. Hili ni lengo la muda mrefu kwamba elimu ya msingi iwe mpaka kidato cha nne badala ya darasa la saba kama ilivyo sasa. Hili ni lengo ambalo halitakamilika mara baada ya uzinduzi huu. Yanahitajika maandalizi makubwa. Katika kuanza safari ya kuelekea huko, Serikali imeamua kufuta ada ya elimu ya sekondari kuanzia mwaka 2016 ili wale waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wasishindwe kusoma.
Sera Mpya ya elimu imeweka msisitizo wa pekee kwa kila mtoto kupata elimu ya awali kabla ya kupata elimu ya msingi. Tumedhamiria pia kuwekeza zaidi katika stadi za Kuandika, Kusoma na Kuhesabu (KKK) katika miaka miwili ya elimu ya msingi. Azma yetu ni kujenga msingi imara wa elimu kwa wanafunzi nchini ambao hutegemea sana upatikanaji wa stadi hizo. Watoto wanapoimarishwa vya kutosha kwa upande wa kusoma, kuandika na kuhesabu, aghalabu humudu vyema masomo yao shuleni. Aidha, itasaidia kurekebisha upungufu uliopo sasa.
Ndugu Wadau wa Elimu;
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba ili tuweze kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi lazima tuongeze matumizi ya sayansi na teknolojia nchini. Tunaweza kufanya hivyo tu kwa kuwa na wanasayansi wengi. Sera hii inasisitiza kuimarishwa kwa muundo na utaratibu wa ufundishaji wa masomo ya Hisabati, Sayansi na Teknolojia katika ngazi zote. Kazi hii tayari tumekwishaianza na tunaendelea nayo kwa ari na nguvu. Tumetoa msukumo mkubwa katika ujenzi wa maabara na naamini, Juni, 2015 tutafikia malengo yetu.
Tunapanua mafunzo ya walimu wa sayansi. Tutakapotekeleza mradi wa matumizi ya computer mashuleni tutakuwa tumepiga hatua kubwa muhimu. Sera hii imetoa mwongozo kwa changamoto nyingine nyingi muhimu ambazo zimetolewa maoni na wadau mbalimbali. Kwa mfano, Sera inaelekeza sasa kutumika kwa utaratibu wa kila somo kitabu kimoja kwa shule zote badala ya utaratibu wa awali wa kila shule kuwa na kitabu chake. Sera inatoa msisitizo kuwa elimu ni huduma na inaelekeza kuwekwa kwa utaratibu utakaodhibiti upangaji wa ada katika shule za binafsi kwa utaratibu wa kuweka ada elekezi (indicative fees) kwa msingi wa gharama halisi kwa mwanafunzi (Student Unit Course). Hii itatoa ahueni kwa wazazi na walezi na kuwawezesha kumudu gharama za kusomesha watoto wao katika shule za binafsi.
Suala la ubora wa elimu inayotolewa tumeliwekea mkazo wa kipekee katika sera hii mpya. Tutaimarisha mfumo wetu wa usimamizi na ukaguzi wa shule zetu kwa lengo la kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa. Tutajenga uwezo wa Wizara kwa kutenga fedha za kutosha kwa shughuli za ukaguzi, kuajiri wakaguzi wa kutosha na kuwapatia vitendea kazi vya kuwawezesha wakaguzi kufanya kazi zao kwa ufanisi nchi nzima. Madhali tumeshapata mafanikio ya kutosha kwenye kupanua fursa ya kupata elimu, sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye kusimamia ubora wa elimu inayotolewa.
Wito kwa Wadau
Mheshimiwa Waziri;
Ndugu Wadau wa Elimu;
Mafanikio yote tuliyoyapata katika Sekta ya Elimu yamepatikana kutokana na ushirikiano wa wadau wote wakiwemo walimu, wazazi, wananchi wetu wote na wadau wa maendeleo. Mafanikio haya hayana budi kuenziwa na kuendelezwa. Tunapoanza utekelezaji wa Sera Mpya ya Elimu, hatuna budi kukumbushana tena wajibu wetu na kushirikiana kufikia malengo yetu haya mapya.
Mdau mkubwa wa kwanza katika elimu ni mzazi na mlezi ambao ndiyo viongozi wa kaya wanazotoka wanafunzi wetu. Ninyi mnao wajibu wa kipekee wa kuwahamasisha na kuwahimiza watoto wenu kupenda shule kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kuwawezesha kusoma. Jihusisheni na elimu ya watoto wenu, na jengeni uhusiano na walimu wao katika kufuatilia maendeleo ya watoto wenu. Wakati mwingine inashangaza sana kuona wazazi na walezi kutojali kujua maendeleo ya watoto wao shuleni. Hawakagui maendeleo yao, wala hawajihusishi na kamati za elimu za shule za watoto wao na kata wanazoishi. Njia bora ya kutatua changamoto za elimu za nchi ni kwa kila mmoja wetu kushiriki katika kutatua changamoto zilizoko katika shule iliyoko katika eneo lake analoishi.
Walimu ni wadau wenye wajibu wa kipekee sana. Jukumu lao la kuwafumbua macho na kuwaongezea upeo wa ufahamu wa vijana wetu pamoja na kuwandaa kuwa raia wema halina mfano wake. Halina badala yake. Mnafanya kazi nzuri lakini mnatakiwa kufanya vizuri zaidi leo na siku za usoni. Elimu ni kitu chenye unyumbufu mkubwa na mabadiliko mengi na hasa siku hizi. Lazima muende na wakati. Ni ninyi waalimu, pengine kuliko watu wengi wengine mtakaoumba Tanzania ya kesho iliyo bora kupitia elimu mnayowapa wanafunzi. Ninyi walimu ndiyo wa kutusaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii na nchi yetu. Nawaomba sana muendelee kujizatiti katika kutambua uzito wa majukumu yenu na kuyatekeleza. Sisi Serikalini tutaendelea kufanya kila lililo katika uwezo wetu kuboresha maslahi yenu na mazingira yenu ya kazi.
Nawaomba pia wamiliki wa shule, hususan shule zinazomilikiwa na mashirika ya dini na watu na makampuni binafsi nanyi mtimize ipasavyo wajibu wenu. Tunatambua na kuthamini mchango wenu mkubwa katika utoaji wa elimu. Nawaomba mkumbuke kuwa Elimu ni haki ya mtoto hivyo mjiepushe na upendeleo na ubaguzi. Elimu ni huduma, hivyo mtoze ada zinazohimilika. Aidha, hamna budi kuzingatia mitaala na miongozo inayotolewa na Wizara ya Elimu na Taasisi zake kuhusu elimu. Serikali inawahakikishia kuwa tutaendelea kuweka mazingira rafiki ya kuwawezesha kutimiza wajibu wenu huo wa kutoa huduma ya elimu. Ni kwa sababu hiyo tumewatambua katika Sera hii na mmeshirikishwa kwa ukamilifu katika mchakato wote wa kuitunga. Naomba tuendeleze ushirikiano wetu katika utekelezaji wa Sera hii.
Sina budi kuwashukuru pia wadau wetu wa maendeleo kwa michango yao muhimu iliyotuwezesha kufikia mafanikio makubwa katika Sekta ya Elimu. Tunapowashukuru, tunawaomba waendelee kushirikiana nasi tunapoianza safari yetu hii ya kutekeleza Sera Mpya ya Elimu. Utekelezaji wa Sera hii utahitaji rasilimali nyingi na hivyo tutashukuru kupata mchango wao katika kuongezea nguvu jitihada zetu. Mchango wao utatuwezesha kupata matokeo makubwa kwa haraka.
Hitimisho
Mheshimiwa Waziri;
Ndugu Wadau wa Elimu;
Ni jambo la faraja kubwa kwangu kwamba, katika kipindi changu cha uongozi kwa ushirikiano wetu tumeweza kupata mafanikio makubwa na ya kujivunia katika kuendeleza Elimu nchini. Sera hii tunayoizindua leo ni mojawapo ya mafanikio hayo.
Naamini kuwa tuliyoyafanya yamechangia kwa kiasi kikubwa kuzikomboa kaya nyingi kutokana na kutoa fursa kwa watoto wengi zaidi wa Watanzania kupata elimu ikiwa ni pamoja na watoto wa kike. Bado tunayo kazi kubwa ya kufanya mbele yetu. Bahati nzuri, tunayatambua na tunaendelea kuyafanya. Sera ya Elimu tunayoizindua leo inatoa mwongozo na kutupa mwelekeo mzuri wa namna ya kufanya yanayotakiwa kufanyika sasa na miaka 10 ijayo. Uzinduzi wa Sera hii mpya ya elimu, na yale yaliyomo katika sera hii ni ushahidi tosha wa dhamira yangu na ya wenzetu wote tulioshirikiana kutayarisha sera hii kuona elimu nchini ianzidi kuimarika na kuwa bora zaidi.
Napenda sasa, kwa heshima na taadhima kubwa kutamka kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 imezinduliwa rasmi.
Asanteni sana.

- Feb 04, 2015
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA SHEREHE YA KUADHIMISHA SIKU YA SHERIA NCHINI, TAREHE 04 FEBRUARI,...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania;
Mheshimiwa Anne Semamba Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Asha-Rose Migiro, Waziri wa Katiba na Sheria;
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani;
Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Mheshimiwa Shabani Ali Lila, Jaji Kiongozi;
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania;
Mheshimiwa George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ;
Waheshimiwa Majaji Wakuu Wastaafu;
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wastaafu;
Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika;
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;
Wasajili, Wakurugenzi na Watendaji wa Mahakama;
Mahakimu na Mawakili;
Mtendaji Mkuu wa Mahakama;
Watumishi wa Mahakama;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana Mheshimiwa Jaji Mkuu kwa kunialika kwa mara nyingine tena kushirikiana nanyi katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania. Hii ni mara yangu ya nane na ya mwisho kuhudhuria sherehe hizi nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sherehe za mwakani zitahudhuriwa na Rais mpya. Natumai mtaendelea kumualika.
Napenda kuwashukuru wale wote tulioshirikiana nao katika utekelezaji wa jukumu zito la kuimarisha mhimili wa Mahakama katika kipindi changu cha uongozi. Napenda kukutambua, wewe mwenyewe Mheshimiwa Mohamed Chande Othman na Majaji Wakuu waliokutangulia, Mheshimiwa Barnabas Samata niliyemkuta na Mheshimiwa Augustino Ramadhani aliyemfuatia. Nawashukuru kwa ushirikiano wenu, umakini, weledi na umadhubuti wa hali ya juu kwa kuwaongoza wenzenu vizuri katika kutoa haki nchini. Nyote mlikuwa kielelezo kizuri cha utoaji haki hapa nchini na kioo cha uongozi bora wa Mahakama yetu. Pamoja nanyi nawashukuru Majaji wote wa Mahakama ya Rufani na wa Mahakama Kuu, Wasajili, Mahakimu Wakazi, Mahakamu wa Mahakama ya Mwanzo ambao wote mmejitoa kusimamia utoaji wa haki katika nchi yetu. Vile vile, namtambua Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Watendaji wa ngazi zote pamoja na watumishi wote wa Mahakama kwa kazi yao nzuri waifanyayo.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu yaani, “Fursa ya Kupata Haki: Wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau” ni muafaka kabisa kwa wakati uliopo. Inatoa fursa kwa mihimili yetu miwili ya dola na wadau wengine kupima jinsi tunavyotimiza wajibu wetu. Naomba tutumie fursa hii tuangalie yale tuliyofanya katika kipindi cha miaka tisa (9) ya uongozi wangu kuhusu kuimarisha utoaji wa fursa ya kupata haki nchini.
Kuboresha utoaji wa haki na utawala wa sheria nchini ilikuwa miongoni mwa mambo tuliyoyapa umuhimu wa juu katika majukumu ya Serikali yetu. Kwa ajili hiyo tumejitahidi kutambua mahitaji na changamoto zilizokuwa zinaikabili Mahakama nchini na kujaribu kutafuta majawabu. Tumechukua hatua na kufanya mambo mbalimbali kwa madhumuni ya kuiwezesha Mahakama kutekeleza wajibu wake wa kutoa haki.
Fursa ya Kupata Haki
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Kama ulivyosema, wewe mwenyewe fursa ya kupata haki imegawanyika katika sehemu mbili. Kwanza, ni fursa ya kuifikia Mahakama, na pili, ni fursa ya kunufaika na huduma za Mahakama yaani kupata haki. Dhana hii inazilazimu Serikali na Mahakama kufanya kazi kwa pamoja, kwani mhimili mmoja pekee hauwezi kufanikisha haya yote mawili. Kimsingi, Serikali inao wajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa Mahakama kuweza kutimiza wajibu wake huo wa kutoa haki kwa wakati.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Ninapoiangalia Mahakama ya leo ninafarijika kuona kwamba hatua zilizochukuliwa na Mahakama yenyewe na nyingine zilizochukuliwa kwa kushirikiana na Serikali zimesaidia kuleta mabadiliko kwenye mifumo na kuboresha utoaji wa haki. Changamoto za kimfumo zilizokuwapo ziliathiri ufanisi katika utoaji haki nchini hususan zilisababisha ucheleweshaji wa mashauri na hukumu.
Hali hii imefanya utatuzi wa migogoro ya mikataba, biashara, ardhi, mahusiano kazini kuchelewa sana (labor matters). Kwa ujumla, jitihada zetu za kukuza uchumi zilipambana na vikwazo vya mifumo yetu ya sheria. Hali kadhalika, kwa upande wa mifumo ya haki jinai, taratibu za kuendesha mashauri hazikuakisi mahitaji ya kutoa haki kwa kuadhibu wakosaji kwa wakati na kutoa fidia na ahueni nyingine inayofaa kwa wahanga wa uhalifu.
Mambo mengi yamefanyika kuboresha Mahakama. Tumetunga Sheria namba 4 ya mwaka 2011 ya uendeshaji Mahakama ambayo pamoja na mambo mengine ilianzisha Mfuko wa Mahakama na kuwezesha Mahakama kuwa na bajeti inayotabirika na ya uhakika. Fedha za Mfuko huu zimekuwa zikiongezeka kutoka bilioni 57.8 mwaka 2012/2013 hadi bilioni 89.6 mwaka 2014/15 sawa na ongezeko la asilimia 54.8. Katika mfumo huu mpya tumeanza sasa kutenga bajeti ya maendeleo inayowezesha uwekezaji katika upatikanaji wa miundombinu ya utoaji haki. Nimesikia mwaka huu bajeti ya maendeleo haijaingia, naomba niwahakikishie kuwa mtaipata. Jana nilizungumza na Waziri wa Fedha aliyenihakikishia kuwa katika nusu ya pili ya mwaka huu wa fedha wataanza kutoa fedha.
Jambo lingine muhimu tulilofanya lilikuwa ni kuongeza rasilimali watu. Tumepunguza uhaba mkubwa uliokuwepo na kuwezesha Mahakama kuboresha kazi yake ya kutoa haki. Hivi sasa kuna Majaji wa Rufani 16 kutoka 9 waliokuwepo mwaka 2005 na kuna Majaji wa Mahakama Kuu 81 kutoka Majaji 35 waliokuwapo 2005. Ninafurahi kuwa kati ya Majaji wote wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu waliopo, Majaji 38 sawa na asilimia 39.2 ni wanawake. Haya ni mageuzi makubwa. Natambua kuwa mahitaji halisi ni kuwa na Majaji 120. Napenda kukuhakikishia Mheshimiwa Jaji Mkuu kuwa mtakapokuwa tayari nileteeni mapendekezo yenu nifanye uteuzi. Kwa upande wa Mahakimu Wakazi, hadi mwaka huu idadi yao ilifikia 677 nchi nzima ukilinganisha na Mahakimu Wakazi 151 mwaka 2005. Mwaka wa jana pekee tulitoa kibali cha kuajiri Mahakimu wapya 300.
Katika kipindi hiki pia tulifanya mambo mawili mengine muhimu kwa utekelezaji mzuri wa majukumu ya Mahakama. Kwanza ni lile la kukamilisha mchakato wa kutenganisha shughuli za upelelezi na uendeshaji wa mashtaka. Imesaidia kupunguza ucheleweshaji wa mashauri na kuimarisha utoaji wa haki.
Jambo la pili ni kuanzishwa kwa nafasi ya Watendaji wa Mahakama iliyo waondolea Majaji majukumu ya utawala na fedha na kuwaaacha washughulike na utoaji wa haki. Jambo hili limeboresha na kuimarisha utendaji na uendeshaji wa shughuli katika Mahakama kwa namna ambayo haijawahi kuwepo huko nyuma.
Huduma ya Msaada wa Kisheria
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Nakubaliana nawe kuwa kukosekana kwa msaada wa kisheria kwa wale wasio na uwezo wa kulipia huduma ya uwakili ni kikwazo kwa watu hao kupata fursa ya kupata haki. Pia inakwaza utoaji wa haki. Nimefurahishwa na pendekezo lako la kuiomba Serikali kuona uwezekano wa kugharamia huduma za uwakili kwa watuhumiwa wasio na uwezo kifedha nje ya watuhumiwa wa makosa ya mauaji. Umeomba sasa tuangalie na wale wenye makosa yenye adhabu kubwa na vifungo virefu. Nakubaliana nawe kuwa wakati sasa umefika wa kuyaangalia mambo hayo kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea nchini ikiwemo kuongezeka kwa aina ya makosa, adhabu na kuwepo kwa Wanasheria wa kutosha wa kuweza kutoa huduma hiyo ni jambo linalowezekana. Sisi katika Serikali tutalifanyia kazi pendekezo hilo na tutawashirikisha mtupe maoni yenu ya namna bora ya kutekeleza wazo hili. Naamini, tukifanya hivyo, tutakuwa tumepanua fursa kwa watu wengi kupata haki ya kisheria.
Wajibu wa Mahakama
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Kama nilivyosema awali, fursa ya kupata haki inategemea pia jinsi Mahakama inavyotelekeza ipasavyo wajibu wake. Nafurahishwa sana na hatua ambazo Jaji Mkuu umechukua ambazo zimewezesha kuboresha fursa ya kupata haki. Taarifa uliyoitoa hapa leo imeonesha wazi mafanikio yaliyopatikana. Kufuatia uamuzi wenu wa kujiwekea ukomo wa muda wa kuendesha kesi na idadi ya kesi kwa kila Jaji na Hakimu, mmeweza kupunguza mashauri ya siku nyingi kwa asilimia 50 kutoka mashauri 6,887 mwaka 2012 hadi 3,632 katika Mahakama Kuu mwaka 2014. Aidha, mmeweza kumaliza mashauri 52 kati ya 59 yanayohusu miradi mikubwa ya serikali iliyoko katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Natoa rai kwa wadau wengine wa sheria yaani waendesha mashtaka na vyombo vya upelelezi kwa upande wa mashauri ya jinai pamoja na Mawakili wa kujitegemea kuunga mkono juhudi zenu hizi. Bila shaka Mahakama itaendelea kuonyesha njia kwa kusimamia mwenendo wa mashauri ya jinai na madai pasipo kuchelewesha. Ni matumaini yangu kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka na vyombo vya upelelezi havitakuwa chanzo cha kuchelewesha mashauri pasipo sababu za msingi.
Kusogeza Huduma ya Mahakama karibu zaidi na Wananchi
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Natoa pongezi nyingi kwamba kwa sababu ya mambo mbalimbali mazuri yaliyofanyika ambayo yamesogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi. Sehemu kubwa ya migogoro inayowagusa moja kwa moja wananchi imeshughulikiwa. Miongoni mwa hiyo ni ile ya ardhi ambapo Mabaraza ya Ardhi yameundwa katika Kata zote nchini chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Jambo hili limepunguza sana mzigo wa mashauri katika Mahakama zetu na kusaidia kuleta usuluhishi katika jamii zetu. Inawezekana utendaji wa vyombo hivi una upungufu mbalimbali kinyume cha matarajio ya wananchi. Dawa yake siyo kuvitelekeza bali kuyatambua matatizo yaliyopo na kuyapatia ufumbuzi.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Halmashauri za Wilaya waendelee kusimamia kwa karibu vyombo hivi muhimu kwa kusogeza huduma ya upatanishi na kushughulikia migogoro midogo ya ardhi. Kuna malalamiko ya kutokuwepo kwa Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya katika Wilaya nyingi nchini. Kwa sababu hiyo watu wamekuwa wanapata usumbufu katika kutafuta haki baada ya kutokuridhishwa na uamuzi wa Mabaraza ya Kata. Wizara iharakishe kuunda Mabaraza hayo na Halmashauri zisaidie upatikanaji wa majengo ya Mabaraza hayo.
Uhusiano wa Mabaraza ya Ardhi na Mahakama Kuu
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Naambiwa kuwa yapo malalamiko ya kukosekana mtiririko mzuri wa majalada kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi. Nia njema ya kuanzisha Mabaraza ya Ardhi imezaa adha. Kilio kilichopo ni kwamba Mabaraza hayo yamekuwa hayataki kutii amri ya Mahakama Kuu ya kupeleka kumbukumbu pindi kunapokuwa na rufaa dhidi ya maamuzi yake ni jambo ambalo sio tu halikutarajiwa bali halikubaliki. Linatia dosari katika utoaji wa haki ya ardhi. Wakati huo huo, Wizara ya Ardhi iwachukulie hatua zipasazo watendaji wa Mabaraza ya Ardhi wanaochelewesha kumbukumbu.
Ni matumaini yangu kuwa wadau wanaohusika yaani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Katiba na Sheria na Mahakama mtakaa pamoja mapema iwezekanavyo kulitafutia ufumbuzi tatizo hili. Kama itahitaji kupitia upya sheria na taratibu ifanyike hivyo ili kuondoa kikwazo hiki na kuondoa malalamiko yanayoendelea kwa muda mrefu sasa kuhusu jambo hili. Ipo rai kwamba Sheria iwawajibishe watendaji wa Mabaraza ya Ardhi kwa Mahakama Kuu moja kwa moja. Busara na hekima ya kufanya hivyo itafakariwe kwa makini. Ni matarajio yangu kwamba hatua hizi zitachukuliwa mapema na pale kwenye mkwamo tuambiane tuone namna ya kusaidia kukwamua.
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Nimefarijika sana kusikia kwamba mkakati uliopo sasa ni kuongeza weledi kwenye Mahakama za Mwanzo kwa kuendelea kuajiri wahitimu wa Shahada ya Sheria kwenye Mahakama hizo. Hili ni jambo zuri ambalo litawawezesha Mawakili kusimamia na kuendesha kesi kwenye Mahakama za Mwanzo. Madhali sasa, hatuna uhaba wa Wanasheria na Mawakili, hili linawezekana. Uamuzi wetu wa kupanua huduma ya Mahakama Kuu kila Mkoa ni mwendelezo wa dhamira yetu ya kuwafanya wananchi waweze kuifikia huduma hiyo karibu na wanapoishi. Bado tunayo dhamira ya kukamilisha ujenzi wa Mahakama Kuu kila mkoa ifikapo mwaka 2016 kama tulivyoagiza. Utekelezaji wa dhamira hii unakwenda sambamba na uteuzi wa Majaji wengi wa Mahakama Kuu kama nilivyoeleza awali.
Mapendekezo yako, Mheshimiwa Jaji Mkuu, ya kupitia upya taratibu zilizopo ili kufanya utatuzi wa migogoro na utoji haki uwe rahisi na unaoeleweka kwa wananchi ni mzuri. Sehemu kubwa ya mashauri ya madai yanahusu usuluhishi. Kinachotakiwa ni kwa wanaosuluhishwa kuelewa na kuridhika na utaratibu uliotumika kusuluhisha migogoro yao. Nakuomba, Mheshimiwa Jaji Mkuu na wenzako myafanyie kazi mapendekezo hayo ili nchi yetu iwe na mfumo rahisi unaoeleweka wa kutatua migogoro kwa haki, wepesi na haraka. Tukiweza kufikia lengo hili, wananchi wataiona Mahakama ni chombo cha kutatua migogoro na siyo mahali pageni pasipofaa kufika hata kama mtu hana budi kufanya hivyo. Hii itaondoa kishawishi kwa wananchi kutafuta njia nyingine zisizofaa kupata haki zao. Tusikubali tufike huko.
Hitimisho
Mheshimiwa Jaji Mkuu;
Napenda kumalizia hotuba yangu kwa kurudia kukushukuru kwa kunialika kuja kujumuika nanyi siku hii adhimu. Katika kipindi hiki tumefanya mambo mengi yaliyoleta mabadiliko madogo na makubwa katika mifumo ya utoaji wa haki nchini na kuongeza ufanisi. Nawashukuru wale wote tulioshirikiana katika kuleta mabadiliko haya. Busara za Majaji Wakuu watatu walioiongoza Mahakama, Majaji wa Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Wasajili, Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama ni hazina kubwa na ya kujivunia. Ushirikiano wa wadau mbalimbali umetusaidia kufikia hapa tulipo sasa. Naamini kama watu wataendelea kuitumikia nchi yetu na watu wake kwa moyo wa uzalendo na kujituma tutapiga hatua kubwa mbele.
Baada ya kusema hayo yote naomba sasa niwatakie siku njema ya Sheria nchini.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!

- Feb 01, 2015
HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 38 YA CCM, KWENYE UWANJA WA MAJIMAJI, SONGEA - RUVUMA, TAR...
Soma zaidiHotuba
Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu na mjumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu;
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM;
Ndugu Mike Mukula, Makamu Mwenyekiti wa NRM ya Uganda na ujumbe wake;
Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Oddo Mwisho, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Waheshimiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa;
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM;
Ndugu Verena Shumbusho, Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Wenyeviti wa Jumuiya za CCM;
Viongozi, wananchama na wapenzi wa CCM;
CCM Oyee!
Naomba nianze kwa kuwashukuru na kuwapongeza wenyeji wetu kwa mapokezi mazuri, hususan napenda kuwatambua wananchi, viongozi na wana-CCM wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mwenyekiti wao ndugu Oddo Mwisho, Katibu wa Mkoa Mama Verena Shumbusho, Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Ndugu Said Mwambungu. Nawapongeza kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizi. Hakika zimefana sana. Hii ni mara ya pili sherehe hizi kuadhimishwa mkoani hapa. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1991 wakati wa kuazimisha miaka 14 ya CCM.
Tunatambua kuwa mmefanya kazi kubwa ya maandalizi mpaka mmeweza kufanikisha shughuli ya leo kwa kiwango cha juu. Waswahili wanasema “Usione vinaelea Vimeundwa”. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi maalum kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana kwa uongozi wake makini uliowezesha mambo kuwa mazuri kiasi hiki. Hongera sana kwa hili na kwa kazi nyingi nzuri unazofanya kwa maslahi ya Chama chetu na nchi yetu.
Leo ni siku ya furaha kwangu na kwa viongozi na wanachama wenzangu wa CCM kote nchini ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Tunastahili kuisherehekea siku hii kwa nderemo na vifijo kwa sababu ya mafanikio makubwa ambayo Chama chetu kimeendelea kupata ndani ya Chama na katika kuliongoza taifa letu. Katika miaka 38 ya uhai wake Chama chetu kimezidi kuimarika na kimeendelea kuliongoza vyema taifa letu: kuna amani, utulivu na maendeleo yanayoonekana.
Tumeeendelea kuaminiwa na kutumainiwa na Watanzania. Kama ilivyothibitika na ushindi wa kishindo katika chaguzi zote tangu mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1995 mpaka sasa. Hata mwaka huu itakuwa hivyo hivyo. Dalili ya mvua ni mawingu: ushindi mnono tulioupata kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni dalili tosha kwamba Oktoba, 2015 watani zetu hawana chao.
Ninaposema hivyo nawaomba wana CCM wenzangu tusibweteke tukadhani kwamba ndiyo tumekwishafika. Bado safari ndiyo kwanza tumeianza na inaweza kuwa na changamoto zake. Lazima tufanye kazi tena kazi kubwa sana ndipo tutakapojihakikishia ushindi. Nguvu ya ushindi inaanzia kwenye Chama. Huu ni mwaka ambao kazi ya Chama ndani ya Chama na kazi ya Chama ndani ya umma inatakiwa ifanyike kwa nguvu zaidi na kwa ari kubwa zaidi. Lazima tuhakikishe tunao umoja wa dhati na kwamba wanachama wetu wanakuwa na mwamko wa hali ya juu wa kukipigania Chama katika kutafuta na kupata ushindi kwa Udiwani, Ubunge, Uwakilishi, Urais wa Zanzibar na Urais wa Muungano.
Huu ni mwaka ambao wanachama na viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakutana mara kwa mara kwa mujibu wa Katiba na hata zaidi kuzungumzia mikakati ya kupata ushindi na kuitekeleza. Huu ni mwaka ambao lazima tuhakikishe kuwa tunazo rasilimali na nyenzo za kutuwezesha kufanya kazi ya Chama ndani ya umma na kuwapatia ushindi wagombea wa Chama chetu.
Huu ni mwaka ambao kazi ya Jumuiya za Chama ya kukiwezesha Chama kuungwa mkono na jamii pana ya Watanzania walio vijana, wanawake na wazazi inafanyika kwa umahiri na ufanisi wa hali ya juu.
Bila ya shaka, ndugu zangu mtayakumbuka maneno niliyoyasema kwa kuyarudia kuwa “Mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine”. Najua baadhi yenu mmezingatia na kuchukua hatua za kufanya maandalizi mapema ya uchaguzi wa mwaka huu mara baada ya kumaliza uchaguzi wa mwaka 2010. Hao nawapongeza. Lakini wapo viongozi na wanachama ambao hawajafanya chochote. Hawa, wananisikitisha kwa athari mbaya na hatari ya kupoteza ushindi wanayokiletea Chama chetu.
Naomba kila mmoja wetu ajipime yupo fungu gani. Kama upo kwenye kundi la kwanza lililokwishaanza maandalizi natoa pongezi nyingi. Nawaomba muendelee kukamilisha ipasavyo. Kwa wale ambao wapo kundi la wale ambao maandalizi yao ni ya kiwango kidogo au hawajaanza kabisa lazima waanze na wakati ni huu. Usikawie, unatakiwa kufanya kazi kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi kama ilivyo kauli mbiu ya CCM. Yapo mambo kadhaa ya kufanya ambayo tulikwishaambiana tufanye. Miongoni mwao ni lile agizo la kutaka kila ngazi ya Chama na hasa Wilaya na Mikoa kuwa na Mfuko wa Uchaguzi. Wakati wake ndio huu sasa wa mfuko huo kufanya kazi iliyokusudiwa. Naomba tujiulize wangapi wanayo mifuko hiyo na wangapi hawana. Kwa wale walionayo wahakikishe ina rasilimali za kutosha. Kama hazitoshi waweke mikakati ya kuitunisha mifuko hiyo. Kwa wale ambao hawajaanzisha wachune bongo kuhusu namna ya kupata fedha za kuendeshea shughuli za uchaguzi. Sina budi kuwatahadharisha kuwa msichukue fedha ambazo zitazua matatizo.
Ndugu viongozi na ndugu wanachama;
Huu ni mwaka wa kutambua ahadi zipi tulizotoa zimetimizwa na zipi bado. Kwa zile ambazo hazijakamilika wajibu wetu ni kuweka mikakati ya kuzikamilisha. Kwa zile ambazo hazitakamilika tutafute maelezo sahihi ya kutoa kwa wadau wa huduma hiyo. Naamini hazitakuwa nyingi za kuchosha. Mwaka huu siyo mzuri kwenda na madeni lukuki ya ahadi. Yanaweza kutupunguzia ushindi wetu.
Huu ni mwaka wa kuongeza ukubwa wa jeshi letu la ushindi kwa kuongeza wananchama wapya. Natambua tatizo la upungufu wa kadi lakini najua mipango thabiti iliyopo ya kuleta kadi nyingi za kutosha wale waliopo nje. Tujiepushe na kuingiza mamluki hivyo taratibu za kuingiza wanachama zizingatiwe ipasavyo.
Ndugu Viongozi;
Ndugu Wananchi;
Jambo lingine kubwa na muhimu sana kufanya mwaka huu ni kuwatembelea wanachama na wananchi na kuzungumza nao. Hatujaifanya vizuri sana kazi hii lakini hatujachelewa. Sina budi kutoa pongezi maalum kwa Katibu Mkuu wa CCM kwa ufanisi mkubwa aliopata kwa jambo hili. Sote hatuna budi kuiga mfano wake mzuri. Tuache kukaa maofisini tutoke kuzungumza na watu kuwashawishi waunge mkono na kuipigia kura CCM katika uchaguzi ujao. Kila Ofisi ya Mkoa na kila Ofisi ya Wilaya inalo gari la kuwawezesha kufanya kazi hiyo. Tafadhali fanyeni hivyo, kwani bila ya kufanya hivyo hakuna uhakika wa kupata ushindi. Kilichobakia kwa upande wetu ni kutafuta vipando kwa Ofisi za Kata na Matawi. Tusaidiane pale inapowezekana.
Uandikishaji wa Wapiga Kura
Ndugu wana CCM na ndugu Wananchi;
Jambo lingine muhimu katika kutafuta ushindi ni kupatikana kwa wapiga kura. Chama chetu kama vilivyo vyama vingine, hatuna budi kuwahimiza wanachama wetu, wapenzi wetu na wananchi wengine wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kupiga kura. Mwaka huu wenye kadi mpya za mpiga kura ndiyo watakaoruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu na katika kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa.
Asiyejiandikisha hatapata fursa ya kushiriki kura ya maoni na uchaguzi mkuu. Kwa sababu hiyo nawaomba viongozi na wanachama wa CCM wawe ndiyo wa kwanza kujitokeza kujiandisha. Pia wawe mstari wa mbele kuwahimiza wananchi wengine kujiandikisha. Nawaomba jambo hili mlipe uzito mkubwa kwani safari ya kutafuta na kupata ushindi inaanzie kwenye kupata wapiga kura hususani wapiga kura wanaounga mkono Chama chetu na wagombea wetu.
Kura ya Maoni
Ndugu wananchi;
Kama mjuavyo, jambo kubwa lililo mbele yetu ni kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendezwa itakayofanyika tarehe 30 Aprili, 2015. Maandalizi yote husika yanaendelea kufanyika ili kuwezesha kura hiyo kutekelezwa kama ilivyopangwa. Kama nilivyokwishaeleza hivi punde uandikishaji wa wapiga kura ni miongoni ma maandalizi hayo. Mengine ni uchapishaji na usambazaji wa Katiba Inayopendekezwa.
Yapo mambo kadhaa ambayo nawasihi viongozi na wanachama wenzangu mfuatilie kwa karibu ili yasiwapite. Yale tunayoyajua tuwaambie. Miongoni mwa mambo muhimu sana ambayo Chama hakina budi kujipanga vizuri ni kuhusu kutoa elimu kwa umma kuhusu Katiba Inayopendekezwa na kampeni ya Kura ya Maoni. Watani zetu watatoa elimu hasi kuhusu Katiba Inayopendekezwa, sisi tutoe elimu chanya. Wenzetu watataka Katiba Inayopendekezwa isipite. Sisi tupige kampeni ikubalike. Nilisema siku ile Dodoma wakati wa kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa na narudia tena leo kwamba Katiba Inayopendekezwa imebeba maslahi mapana ya taifa letu. Hatujawahi kuwa na Katiba kama hii Inayopendekezwa. Misingi ya historia ya nchi yetu yaani kule tulikotoka, tulipo sasa na tuendako imezingatiwa vizuri. Katiba hiyo inatambua maslahi ya makundi yote nchini na kuyawekea utaratibu mzuri wa kutekelezwa. Wakulima, wafugaji, wavuvi, wanawake, vijana, wasanii, wafanyakazi, wazee na watoto wametambuliwa kwa kina na upana zaidi kuliko Katiba ya sasa.
Katiba Inayopendekezwa imeshughulikia kero za Muungano na kujenga mazingira bora zaidi kwa Muungano wetu kuimarika. Yale mambo yaliyokuwa yanaikwaza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuukwaza Muungano yamepatiwa ufumbuzi mwafaka. Sasa Zanzibar itaendesha na kushughulikia mambo yake kwa uhuru mkubwa zaidi.
Ndugu wananchi;
Kwa maoni yangu sioni sababu ya kuikataa Katiba Inayopendekezwa. Hatuna budi kutambua kuwa tukiikataa Katiba Inayopendekezwa, Katiba ya sasa itaendelea kutumika mpaka hapo mchakato mwingine utakapomalizika miaka mingi ijayo. Viongozi wa vyama vinne vya siasa wamesikika wakisema watasusia kushiriki katika kura ya maoni na kuwataka wanachama wao wasishiriki. Kauli hiyo imenisikitisha sana ingawaje haikunishangaza hasa tukikumbuka waliyoyafanya wakati wa Bunge la Katiba. Mimi nawaomba washiriki.
Nawasihi wananchi wasiwasikilize. Wao wakitaka kususia waacheni wasusie lakini nyie jitokezeni kupiga kura. Nawasihi msikubali kupoteza mema mengi yaliyo katika Katiba Inayopendekezwa ati kwa sababu tu hakuna Serikali Tatu walizokuwa wanazitaka. Kama kweli wananchi wa Tanzania wanakereketwa na Serikali Tatu watathibitisha hiyo kwenye kura ya maoni.
Naomba msibabaishwe wala kudanganywa na watu wanaotaka kuturudisha nyuma kutoka katika hatua kubwa muhimu tutakazopiga kwa kuikubali Katiba Inayopendekezwa. Tusikubali kubaki nyuma.
Uchaguzi Mkuu
Ndugu wananchi;
Kama mjuavyo mwezi Oktoba, 2015 nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge, Wawakilishi, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwa nchi yetu kwani tunachagua Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi nataka Rais huyo awe mwana CCM. Sisi sote katika CCM tunataka Rais atoke katika Chama chetu kwa sababu kama alivyousia Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere “Rais wa nchi yetu anaweza kutoka Chama chochote lakini Rais bora atatoka CCM”.
Huu ni usia mzito wenye maono ya mbali. Tusiupuuze wosia huu bali tuuenzi. Sisi katika Chama cha Mapinduzi tuwe mstari wa mbele katika kuuenzi wosia huu kwa kupata mgombea aliye bora wa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi ujao. Mgombea ambaye wananchi wakisikia jina lake likitajwa watasema naam, hapo sawa, hapo barabara. Lakini tukiteua mgombea ambaye watu wataguna na kusema hata huyu? Tutakuwa tumemuangusha Muasisi wa Chama chetu na taifa letu katika wosia wake. Bila shaka laana yake tutaipata. Na hilo likitokea itakuwa hasara kubwa kwa taifa letu na msiba kwa CCM. Nchi itayumba.
Lazima tuhakikishe kuwa hatutafika huko. Watu wazuri wapo wa kutosha katika CCM na naamini tunawajua. Kama hawajajitokeza tuwashawishi wafanye hivyo. Ndugu zangu, tusifanye ajizi katika jambo hili kubwa na la msingi kwa Chama chetu. Kushinda chaguzi za dola katika sehemu zetu mbili za Muungano ndiyo madhumuni makuu ya kuundwa na kuwepo kwa CCM.
Napenda kuwahakikishia wanachama wa CCM na wananchi kuwa, Chama cha Mapinduzi ni Chama kilichokomaa, kilicho makini na imara. Tunao utaratibu unaoeleweka na kutabirika wa kuwapata wagombea. Inazo kanuni na vigezo vya wazi vya kuwapata viongozi walio bora, na tunavyo vikao rasmi vya kuchuja na kuteua wagombea kwa kuzingatia kanuni, taratibu na maadili ya Chama chetu. Hivyo basi, hapataharibika jambo.
Naomba niwahakikishie kwamba CCM itawapatia Watanzania wagombea bora ambao hawatawapa wananchi mashaka wala kigugumizi cha kuwachagua. Tutafanya hivyo kwa nafasi ya Rais wa Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Nawaomba wagombea wazingatie na kuheshimu masharti ya Katiba ya Chama, Kanuni na Madili ya uteuzi kwa wanaotaka kuteuliwa kugombea nafasi katika chaguzi za dola. Asiyezingatia hayo asije akakilaumu Chama bali ajilaumu mwenyewe kwa makosa aliyoyafanya.
Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM
Ndugu wananchi;
Miezi minne iliyopita nilifanya ziara ya mkoa huu wa Ruvuma kukagua shughuli za maendeleo. Nimefurahishwa sana na jitihada za kujiletea maendeleo zinazofanywa na wananchi wa mkoa huu na mafanikio mnayoendelea kuyapata. Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na mipango mbalimbali ya serikali unakwenda vizuri, kiasi cha kuwastajabisha hata wale waliokuwa na mashaka na wasio tutakia mema.
Yako mambo mengi tuliyoahidi kufanya ambayo tumeyakamilisha na mengine utekelezaji wake unaendelea vizuri. Kilio cha miaka mingi cha wananchi wa mkoa huu kuhusu barabara kimefanyiwa kazi vya kutosha. Ujenzi wa barabara ya Namtumbo – Songea na Peramiho - Mbinga kwa kiwango cha lami umekamilika. Tunaendelea na ujenzi wa barabara ya Namtumbo – Tunduru na Tunduru – Mangaka ili kuunganisha mkoa wa Mtwara na Ruvuma kwa barabara za lami. Aidha, mipango ya kujenga barabara ya Mbinga – Mbambabay kwa mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika imefikia mahali pazuri. Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Nyasa hivi sasa mchakato wa ujenzi wa chelezo cha kujengea meli ya ziwa hilo kule kwenye bandari ya Itungi, Kyela unaendelea vizuri. Ujenzi wa chelezo ukishakamilika ujenzi wa meli utaanza.
Kwa upande wa umeme tunaendelea na ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa Kv 220 kutoka Makambako kuja Songea na hadi Mbinga na Namtumbo. Ujenzi wa njia hii ya umeme utakapokamilika utawahakikishia wakazi wa mji wa Songea na mkoa wa Ruvuma umeme wa uhakika. Tumechelewa kidogo kwa sababu ya kubadilisha ukubwa wa njia kutoka msongo wa Kv 132 tuliyotaka kujenga awali hadi Kv 220. Aidha, usambazaji wa umeme vijijini unaendelea kwa kasi katika maeneo yote nchini. Tunataka ifikapo June, 2015 zaidi ya vijiji 5,336 viwe vimepatiwa umeme. Kati ya vijiji hivyo zaidi ya vijiji 300 ni vya mkoa wa Ruvuma. Haya ni mafanikio makubwa na ya kutia moyo.
Kuhusu sekta ya Afya nako pia tumepata mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma ya afya kwa Watanzania. Kwa hapa Songea nimekwishatoa maelekezo kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali mpya ya Mkoa wa Ruvuma na hii iliyopo sasa iwe ni hospitali ya Manispaa ya Mji wa Songea. Halmashauri ya Manispaa ya Songea iharakishe kutenga eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya mkoa ambayo itakuwa ni ya rufaa kwa yale ambayo hospitali za Wilaya zitashindwa kumudu.
Haya ni maeneo machache tu ambayo yanaonyesha hatua kubwa tuliyopiga katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na maendeleo ya mkoa huu. Ukweli ni kwamba Ruvuma ya miaka 10 iliyopita siyo Ruvuma ya leo. Ninyi nyote ni mashahidi wa mambo haya. Mwenye macho haambiwi tazama.
Ndugu wananchi;
Jambo la mwisho ambalo napenda kulizungumzia ambalo nilishalizungumzia kwenye hotuba yangu ya mwaka mpya inahusu ununuzi wa mazao ya wakulima. Nilieleza siku ile kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ilikuwa bado haijalipa shilingi bilioni 89 kwa wakulima kwa mazao yao iliyonunua. Nilielezea kutokufurahishwa kwangu na hali hiyo na kuagiza Wakala kulipa deni hilo.
Nimeambiwa kuwa tayari shilingi bilioni 15 zimeshatolewa na hapa Ruvuma mmepata shilingi bilioni 8. Hivi karibuni shilingi bilioni 36 zitatolewa na kubaki shilingi bilioni 38 ambazo zitalipwa mwezi Machi.
Jambo lingine ambalo tunaendelea nalo kulishughuikia katika Serikali ni kupata masoko mengine kwa mazao ya wakulima. Kama nilivyosema NFRA haiwezi kununua mazao yote ya wakulima nchini. Uwezo wake ni kuhifadhi tani 240,000 wakati uzalishaji wa mahindi hapa Ruvuma ni tani 993,350. Hata kama NFRA ingeamua kununua mahindi yote kutoka mkoa wa Ruvuma peke yake isingeweza kuyamaliza.
Nimewaagiza viongozi wa mkoa wa Ruvuma na mikoa yote nchini washirikiane na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Wizara ya Viwanda na Biashara kutafuta masoko mengi kwa ajili ya mahindi, mpunga na mtama wa wakulima ndani na nje ya nchi.
Tunakokwenda
Ndugu wana CCM;
Mafanikio ya miaka 38 ya Chama chetu yasitufanye tubweteke. Bado tunayo kazi kubwa mbele yetu. Ili tuendelee kuongoza dola hatuna budi tuendelee kuwa tumaini na kimbilio la wananchi wetu. Inatupasa kuwa waaminifu kwa ahadi zetu na watiifu kwa matakwa yao. Kubwa sana, tunatakiwa tuwe tayari wakati wote kubadilika na kwenda na wakati. Tunaweza kufanya hivyo ikiwa tutaendelea kukuza demokrasia ndani ya Chama chetu na kuruhusu na kuvumilia tofauti za mitazamo. Hiyo ndiyo siri ya uhai wa CCM ambayo hatuna budi kuendeleza.
Tunapoanza safari ya kuelekea mwaka wa 39, hatuna budi sasa kuelekeza nguvu zetu kwenye kuondoa utegemezi wa kifedha kutoka kwenye ruzuku na michango ya wafanyabiashara. Kutegemea misaada na michango si mambo endelevu na huo hauwezi kuwa ni mkakati wa kutumainiwa wa kuimarisha Chama chetu. Wakati mwingine michango hii imetugharimu ndani ya Chama chetu. Lazima tuwe wabunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na rasilimali zetu nyingi tulizonazo ili kuwezesha Chama kujitegemea. Tayari yako mawazo yaliyoibuliwa kutokana na kazi nzuri ya Kamati iliyoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mweka Hazina wetu Mheshimiwa Zakhia Meghji tumeagiza yatekelezwe. Naomba mtimize ipasavyo wajibu wenu.
Hitimisho
Ndugu wana CCM;
Leo ni siku ya furaha kwetu sote. Wakati tukisherehekea mafanikio yetu tuwakumbuke pia waasisi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyekuwa Mwenyeti wa TANU na Ndugu Sheikh Aboud Jumbe aliyekuwa Mwenyekiti wa ASP kwa busara, hekima na uamuzi wao uliotukuka uliowezesha kuzaliwa kwa CCM. Tunawakumbuka pia wale wote waliotangulia mbele ya haki ambao walijitoa maisha yao kujenga CCM. Hatuna budi kuwaenzi kwa kutoa mchango mkubwa zaidi mwaka ujao na miaka mingi ijayo. Tuhakikishe kuwa tunaimarisha Chama chetu na kutenda mema kwa ajili ya nchi yetu na watu wake. Hili linawezekana ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake. Kidumu Chama cha Mapinduzi!
Asanteni sana kwa kunisikiliza.

- Jan 26, 2015
REMARKS BY HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DURING A DINNER EVENT ON THE MARGINS OF GAVI 2ND REPLENISHING CON...
Soma zaidiHotuba
Your Excellency Ibrahim Boubacar Keita, President of the Republic of Mali;
Honourble Dr. Gerd Muller, Federal Minister for Economic Cooperation and Development of Germany;
Honourable Ministers present;
Mr. Bill Gates, Co-Chair of Bill and Melinda Gates Foundation;
Mr. Dagfinn Hoybrated, Chairman GAVI, the Vaccine Alliance;
Dr. Seth Berkley, CEO, GAVI, the Vaccine Alliance;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
Appreciation
Much has been said already, by those who spoke before me at this unique opportunity “making history together”. Mine, therefore, are a few words to amplify the same. Tanzania is proud to be part of this great GAVI family, and part of this historical mission of saving lives of innocent children through vaccine and immunization. This meeting here in Berlin to renew our resolve to scale up our immunization programs to reach more children and save more lives gives us every reason to be hopeful.
I thank Mr. Bill Gates and the Bill and Melinda Gates Foundation for the outstanding contribution they have been making in supporting GAVI and for bringing us together this evening. It takes such a caring and compassionate to do what you are doing for the world, Bill. It is beyond philanthropy, it is beyond service, it is beyond words, it is a reflection of a genuine belief in humanity and the dignity of human beings. This evening we are also celebrating your lives, and accomplishments in life.
Tribute to Late Nelson Mandela
Ladies and Gentlemen;
As we meet this evening, it is befitting that we pay tribute to the legendary leader, the late President Nelson Mandela and the first President of GAVI. Madiba is one of Africa's best sons. We will always applaud him and remember him for his outstanding contribution to this noble course. Words are not good enough to speak about the late Mandela. He is a man of extraordinary accomplishments, lessons and facets.
To many of us, the name Mandela is associated with the fight for equality and justice. His search for equality and justice for both the oppressed and the oppressors distinguished him from many people who otherwise would have searched for one and leave the other. To him, equality and justice was not only meant to be matters of political realm, but of all spheres of life. No wonder, he advocated for equality and justice with regard to the well being of children when he said, " life or death of a young child too often depends on whether he is born in a country where vaccines available or not". Today, his legacy and spirit continue to live with us and they guide our actions. I am gratified that we have dedicated this evening to celebrate his life and renew our commitment to make his spirit immortal.
Achievements of GAVI
Ladies and Gentlemen;
The timing of this meeting is perfect given that it allows us to take stock of the gains and shape the future that is ahead of us. Since 2000, GAVI has made immunization possible to 370 million children, and has helped developing countries to prevent more than 5.5 million future deaths. These would have been caused by preventable diseases such as Hepatitis B, Haemophilus Influenza type B (HiB), Measles, Pertussis, Pneumonic disease, Polio, Rotavirus, Diarrhea and Yellow Fever.
We in Tanzania have made remarkable achievements with regard to vaccine and immunization coverage. Thanks to GAVI we speak about the universality of this program in Tanzania. Every child irrespective of the place they came from, family they belong or gender are granted free access to immunization. These achievements are not small at all. It took a lot of efforts and commitment on the part of a number of players including GAVI, Bill and Melinda Gates Foundation and other partners, to arrive at these hard-won results. I thank each one of those who contributed for making it possible. Each life we have saved, we saved a generation and the next generation.
The challenge ahead of us is daunting one, indeed. One is tempted to say that it is an uphill task which requires timely action. We know fairly well that, securing the gains is one thing and sustaining those gains is another. We must rise to the challenge together.
Conclusive Remarks and Way Forward
Ladies and Gentlemen;
This evening we are walking through the path and footsteps of the great man, the late President Nelson Mandela. As he undertook the long walk to freedom, we are undertaking the long walk to freedom of our children from death caused by preventable diseases. Ours is a long walk for our children’s freedom to access vaccines and immunization, freedom from diseases and preventable deaths, and freedom for our children to pursue their future with hope and as equal. Taking this long walk is the best way to live up to President Mandela's legacy. I thank all of you for your readiness to undertake this long walk and make it bear the desired outcomes. Again, I thank the Bill and Melinda Gates Foundation for leading the walk, and I thank GAVI and all other partners present here for making us walk the talk.
I thank you all for listening.

- Jan 21, 2015
SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CHAIRMAN OF CHAMA CHA MAPINDUZI DURING THE SIGNING CEREMONY OF THE AG...
Soma zaidiHotuba
Your Excellency Yoweri Kaguta Museveni, President of the Republic of Uganda;
Your Excellency Uhuru Kenyatta, President of the Republic of Kenya;
Your Excellency Salva Mayardit Kiir, President of the Republic of South Sudan and Chairman of SPLM;
Your Excellency Cyril Ramaphosa, Deputy President of the Republic of South Africa;
Your Excellency Riek Machar, Former Vice Chairman of SPLM and Former Vice President of South Sudan;
Honourable Deng Alor Kuol, Representative of SPLM Former Leaders Detainees;
Madame Rebecca Nyandeng Garang de Mabior, Mother of the South Sudanese Nation;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
I thank Your Excellencies for accepting my invitation to join our brothers and sisters of South Sudan on this very auspicious occasion of signing an Agreement on the Re-unification of the Sudanese Peoples Liberation Movement.
Today therefore, is a momentous day for the SPLM, its members and all the people of South Sudan. This is the new chapter which they have been anxiously waiting to dawn on their historic party. It is the day when hope for peace and unity for the people of South Sudan is not only being rekindled in earnest but seems to be within reach. As we all know, it is the split in the ranks of the SPLM which landed this youngest nation on this planet into the on going civil war.
All of us gathered here today are deeply touched and elated by the historic event we have just witnessed. We warmly congratulate His Excellency Salva Mayardit Kiir, President of South Sudan and Chairman of SPLM, His Excellency Riek Machar, former Vice Chairman of SPLM and former Vice President of South Sudan and Comrade Deng Alor Kuol of the SPLM’s Former Detainees on this important milestone. We commend and congatulate most sincerely, the negotiating teams from the three factions of the SPLM for the wonderful work. It is a job very well done. Allow me to recognise the SPLM in Government team led by Comrade Daniel Awet Akot, the SPLM in Opposition team led by Comrade Taban deng Gai and the SPLM – Former Detainees team led by Comrade Deng Alor Kuol. At kast their sweat and toil here at the Ngurdoto Montain Lodge since October, 2014 has born the desired fruits. Nothing is impossible. Where there a will, there is a way.
The signing of the agreement today, marks the beginning of a new era and a new beginning in the history of the SPLM. The agreement says it all. It is an era of reconciliation, healing and rebuilding of the party. The signatures apended symbolise the beginning of the end of the dark shadow that has unfortunately shrouded the Party and the nation, causing immense pain and suffering to both members of SPLM and the people of the South Sudan.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
Today’s agreement gives the people of South Sudan and all of us gathered here and beyond, every reason to hope that a successful conclusion of the Addis Ababa peace process is feasible. I believe it will not take long from now to be realized. We hope, from now on the negotiations will move much faster and enable the people of South Sudan to look to the future with even greater hope and antincipation. It is a victory for us all.
Excellencies,
Ladies and Gentlemen;
Allow me to quote a Swahili saying (which goes) “Kuzaa si kazi, kazi kulea”. Translated literary, it means: “giving birth is easy, but bringing up the child is the difficult task”. Senior most SPLM leaders have appended their signatures to this historic agreement on re-unification of their party. The most demanding task begins immediately hereafter. The agreement contains specific commitments and timelines, very well elaborated in the implementation matrix. Please ensure that you keep the promise and stay the course on implementation. Ensure adherence to the timelines.
I know, it is not going to be easy all the time. There may be some difficulties or difficult moments. That should not discourage you. You must never give up. Remain steadfast, maintain dialogue amongst youselves and continue to find amicable solutions to the challenges you may encounter on the way. I would like to assure you that all of us gathered here stand ready, wherever and whenever, to do the needful if you so wish. These include Uganda, Kenya, South Africa and Tanzania. We will not leave you alone. Our presence here today serves as an assurance of our readiness and availability.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
It would be remiss of me if I concluded my speech without expressing words of appreciation to President Salva Kiir, former Vice President, Riek Machar and all leaders and members of the SPLM for the trust you have reposed in Chama Cha Mapinduzi. By that inference you have reposed on Tanzania. It is something we did not expect. I must admit when I received the request from President Salva Mayardit Kiir I had some trepidation. I consider this to be humane. It was the fear of the unknown. I asked myself many question. Can we really, be useful? Can we deliver on their expectations? Are we not creating a parallel initiative to the one of IGAD in Addis Ababa? All that not withstanding we plucked courage and rose to challenge. Here we are, witnessing this momentous achievement by our SPLM comrades. We thank you for your co-operation and understanding for, had it not been for that, we would not have been here, this evening.
Excellencies;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
Allow me to thank my colleagues of Chama Cha Mapinduzi and the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation for the excellent work done. I thank them for agreeing to spare their precious time to undertake this historic mission. Above all I commend their patience and perseverence. I know it has not been easy. I thank the Secretary General of CCM, Comrade Abdulrahman Kinana, Foreign Minister Honourable Bernard Membe, His Excellency John Samuel Malecela, Former Vice Chairman of CCM (the Chairman of process) and his team of cadres for their commitment and had work. You have done Tanzania proud. I also thank in a very special way, the CMI and all friends for the generous support which made undertaking the process possible.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
In conclusion, let me say once again that,reunifying the SPLM is a process whose the success of which requires that today’s agreement be fully and earnestly implemented. It is in your best interest, our SPLM Comrades, and that of the people of Sudan to see that is done. The eyes and ears of all persons in the region, on the continent and in the world are now fixed on you. The whole world wishes to see that South Sudan is restored to normalcy and people live safely, happily and return to their normal and ordinary lives. Personally, I have no doubt in my mind that the people of South Sudan and their leaders will successfully rise to this occasion. You have to prove wrong the doubting Thomases and your detractors. You did so when you joined hands in the liberation struggle and you were crowned with success. After working with you since August, 2014 I know there is a part of the leaders gathered here. You will definitely do it again this time around. You will prevail and overcome the current trials and tribulations. We want you to succeed. Your success is our success. Let me assure you that we in Tanzania, the countries gathered and the whole of Africa shall always be there for the people of South Sudan as we have always been. We will walk with you every step of the way during the process of re-unification of your Party and in the search for sustainable peace and stability in your great nation.
Long live the SPLM! Long live South Sudan! Long Live Africa!
I thank you.

- Jan 09, 2015
SPEECH BY HIS EXCELLENCY DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE NEW YEAR SHERRY PARTY, HOSTED FOR HEADS OF DIPLOMATIC M...
Soma zaidiHotuba
Honourable Bernard Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Cooperation;
Your Excellency Juma Alfan Mpango, Ambassador of the Democratic Republic of Congo and the Dean of the Diplomatic Corps;
Excellencies, Heads of Diplomatic Missions and International Organizations;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen:
Welcome Remarks
I welcome you all to the State House. I thank you for accepting my invitation to attend this traditional event to commemorate the end of 2014 and welcome 2015.
I do hope that, those of you who joined the diplomatic community in Dar es Salaam in 2014, have settled down, and are receiving the necessary cooperation of my government and of your diplomatic colleagues. I extend our very best wishes for the New Year to you all and through you to your Heads of State and Government, Heads if your respective institutions, your people, your spouses and staff,.
Economic and Political Development
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
The year 2014 has been a very eventful year for Tanzania. We are witnesses to important landmark events happening in the social-political and economic landscape of the country. The economy continued to register strong macro-economic performance. GDP growth is expected to be 7.4 percent compared to 7.3 percent in 2013. Inflation rate dropped from 6.0 percent in January 2014 to 4.8 percent in December 2014. This drop is a result of an increase in food production. Last year, we produced a surplus of 3.25 million tonnes of grains which is an increase of 31.4 percent compared to a surplus of 2.23 million tonnes in 2013. The objectives of Kilimo Kwanza and SAGCOT are working and succeeding.
We also registered an increase in export earnings. By 31 October, 2014, Tanzania exported goods and services worth USD 8.539 billion compared to USD billion 8.332 recorded at the same time in 2013. Had it not been for the fall in the world prices of coffee, tea, cashew nuts, cotton and gold, we would have done much better.
Excellencies;
In another development, last year, we concluded the rebasing exercise of our economic statistics. The base year will now be 2007 instead of 2001. Accordingly, therefore, the GDP of Tanzania in 2013 was 70 trillion shillings using 2007 base year compared to 53.7 billion shillings using 2001 base year. Likewise, GDP per capita is 977 USD compared to 742 USD using 2001 figures. Please be informed that this is the 5th time such an exercise was undertaken in Tanzania. Previously it was done in 1966, 1976, 1992 and 2001.
Social Progress
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
We also registered commendable progress in the social-economic services particularly in education, health care, water supply, roads, airports and railways. The New Education and Training Policy was approved by Cabinet. The Policy underlines improving access and quality of education and training as core tenet of the new policy. Everything else is an elaboration of how to see this core policy tenet is realised.
There are two important factors of the new Policy that are worth mentioning. First the renewed emphasis on ensuring that Tanzanians get the type of education that will cater for the needs of the job market in terms of wage employment and self employment. The second is the aspiration of making secondary school education free from next year, 2016. The idea to make primary and secondary school education accessible to every Tanzanian is a major undertaking on our part. That is why we in government have given ourselves the task of ensuring proper preparations are made so that this noble goal can be realised smoothly.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
There are three other landmark developments in education which occurred in 2014 that I would like to share with you today. The first one is with regard to availability of primary and secondary school teachers. With the employment of 36,339 teachers in 2014 we remain with a shortage of 45,233 teachers of which 26,946 are for primary schools and 18,288 are for secondary schools. This is the lowest shortage of teachers we have ever been in the last seven years. Indeed, the cooperative endeavour of some of you and us, to invest in teacher training is paying desired dividends.
The other important highlight worthy mentioning is the fact that there is no more shortage of teachers of arts subjects in secondary schools in Tanzania unlike the situation seven years ago. However, we are still contending with a shortage of 18,277 science teachers in secondary schools. The capacity of our training institutions is to produce 2,500 teachers annually, compounds the problem. In this regard, we welcome the innovative action by the University of Dodoma to design a diploma course for science and mathematics teachers. The plan to enrol 5,602 students annually beginning 2014/2015 academic year should help ease and resolve the shortage of these teachers at the earliest possible time.
Excellencies;
The second thing is the shortage of text books in primary and secondary schools. We have been making steady progress in tackling this problem. In 2005, for example, in primary schools the ratio of book to students was 1:6 while in secondary schools it was 1:5. Through using own budgetary resources and support from development partners, in 2014 the ratio was 1:2 for both. I would like, to use this opportunity to thank our development partners for their support.
Allow me to recognise the United States of America for donating 2.5 million science and mathematics books for secondary school last month. Our overarching ambition is to get to 1:1 ratio by 2016. Your continued cooperation and support will be highly appreciated.
Excellencies;
Through a unique Public People Partnership, close to 3,500 community secondary schools have been built since 2005 todate. Because of serious oversight on the part of leaders, 3,463 of these schools did not construct science laboratories. Two years ago, I launched a major campaign to build laboratories in these schools. Good progress has been made. So far 40.5 percent of the laboratories have been completed, work is at advanced stage for 54.8 percent and 4 percent of the laboratories is at initial stage of construction. I believe in six months time all of these schools will have physics, chemistry and biology laboratories. Any support we can get from your great nations with regard to provision of laboratory equipment and other needs will be highly appreciated.
Excellencies;
After dealing effectively with the issues of shortage of teachers, text books and science laboratories, the next big thing ahead of us will be teacher’s houses. We will launch a major initiative in the next budget to build houses for teachers beginning with rural areas. There is a huge shortage. We will seek your support in this last mile action in primary and secondary school education development in Tanzania. We look forward to your cooperation and support as you have always done in the past.
Health Sector
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
Equally important progress was made in the health sector. This was in terms of building and equipping health delivery centres and dealing with diseases. With regard to employment, in 2014 we employed 8,345 health professionals of whom there were doctors, nurses and other professionals. With regard to training of health personnel, we were able to reach 97 percent of our target of admitting 10,000 students by the year 2017. I am sure, therefore that, we will surpass that target by far by that time.
Infrastructure
Excellencies;
We registered remarkable progress in infrastructure development in 2014. The tarmac road network was extended by 1,459 kilometres with 19 tarmac roads completed in 11 regions. This year we expect 24 roads to be completed in 12 regions. This will add another 1,339.06 kilometres. We also expect work to start on eight new roads in Dar es Salaam, Iringa, Shinyanga, Simiyu, Kilimanjaro, Katavi and Arusha regions. Thousands of kilometres of earth roads have been improved using the Road Fund whose budgetary allocation has been increased to 751.7 billion shillings in 2014 from 504.4 billion shillings in 2013.
Implementation of the rural electrification programme being undertaken by the Rural Energy Agency (REA) has been a tremendous success. 3,836 villages have been electrified by 2014 and we expect another 1,500 will be reached by June, 2015. This means 43 percent of all villages in the country will be covered giving an access to electricity for 38 percent of Tanzanians as compared to 18.4 percent in 2012. This is no small achievement in a short period of two years. A lot has been achieved as well in the railway, ports and water sub sectors. For brevity of time I will not go into details today.
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
It would be remiss of me, if I did not acknowledge, appreciate and thank some of you gathered here for your country’s or institution’s kind support. It has made a huge difference. I appeal for continued support and cooperation in 2015 and other years to come.
50th Anniversary of the Union
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
Another landmark event of last year was the celebration of the Golden Jubilee of the Union between the People’s of Republic of Zanzibar and the Republic of Tanganyika on 26th April, 1964, which gave birth to the United Republic of Tanzania.
The people of Tanzania had every reason to celebrate because it is a momentous achievement. Our Union remain one of the few examples of successful and long surviving mergers of two sovereign republics into one new nation. The secret behind this success has been the continued goodwill of our cooperating states and our readiness to openly discuss challenges facing the union and resolving them.
I initiated Constitutional Review process in the same spirit. There are some issues which require action in the Constitution. I am glad the Constitution Review process went well and if the Proposed Constitution is endorsed in the Referendum a last solution will have been resolved. The Electoral Commission is finalising preparations for the referendum to be held on April 30th, 2015. We are doing everything within our powers to ensure that the problems identified in the pilot registration of voters exercise and others, are addressed speedily.
Excellencies;
It is critically important that the exercise succeeds because the Voters Register being developed for the Constitutional Referendum is the same one that will be used in the General Elections later in October 2015. With regard to support for the General Elections, let me use this opportunity to thank the UNDP and all other partner states and institutions that have expressed readiness to assist our government in the preparations. Please expedite the disbursement of the promised resources. I want to assure you of the readiness of my Government to work with you all.
Local Government Elections
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
On 14th and 20th December 2014, respectively, the country conducted local Government elections. The successful conduct and conclusion of these elections speaks volume about the vibrancy and consolidation of democracy in Tanzania. I commended the Parties and the people who contested the elections. I also congratulated the winners. I commended my Party CCM for the landslide victory and the opposition parties for the stronger performance. I deplored violence by followers of political parties and mistakes committed by some election officials. We took action against both, we are sending a strong message that such action will not be tolerated in the General Elections in October, 2015.
Post 2015 Development Agenda
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
The year 2015 is a special one as far as the global development agenda is concerned. It is the year when the implementation of the Millennium Development Goals (MDGs) comes to a close and the negotiations on the Post 2015 Development Agenda will be concluded.
We in Tanzania would like to see the unfinished business of the MDGs to form part of the post 2015 development agenda. For effective implementation of the post 2015 development agenda Tanzania emphasizes on a clear mechanism to ensure stable, predictable and reliable sources of financing for its implementation. We promise to play our part well in the negotiations of the Post 2015 Development Agenda.
Regional Integration
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
At the regional level, Tanzania will continue to be a committed and proactive member to the EAC, SADC and ICGLR. Last November, Tanzania assumed the Chairmanship of the East African Community (EAC). In our one year tenure of office, we will strive to consolidate the gains made todate and work to advance the East African integration agenda to the greatest heights possible. We shall equally remain committed to the SADC and participate fully in the implementation of the Regional Indicative Development Plan (RIDP), the SADC Strategic Indicative Plan for the Organ (SIPO) and all decisions of the SADC Summit and its Organ on Politics, Defence and Security.
The International Scene
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
At the continental and global scene, Tanzania will remain a faithful member of the African Union and the United Nations. Currently, we have contributed over 3,000 troops to UN peace keeping mission in the DRC, Darfur and Lebanon. Tanzania is the 6th contributor of military and police peacekeepers in Africa and 12th globally. In making this noble contribution, we are advancing both our foreign policy objective and upholding the ideals of the United Nations Organisation. I promise continued contribution to UN peace keeping efforts whenever requested to do so.
Let me use this opportunity to set records straight about Tanzania’s position and role in the evolving security situation in the Eastern DRC and the on going voluntary surrender and disarmament exercise by the FDLR rebels. We have always been supportive and will continue to be supportive of these efforts to ensure the Eastern DRC is free of armed groups that threaten the security of the people of Congo and Congo’s neighbours. Any misrepresentation of Tanzania’s position is done by people who pretend to read Tanzania’s mind and make their thinking the truth. This is preposterous and contemptible. It is done by people who have ill intensions against our country.
Excellencies, Ladies and Gentlemen;
Another development which I would like you to know is about South Sudan. In October, 2014 Tanzania through the ruling party Chama cha Mapinduzi facilitated the Intra – Sudanese People’s Liberation Movement (SPLM) dialogue, in Arusha. This was done following the request of His Excellency President Salva Kiir of South Sudan and the leadership of the SPLM in August, 2014. They requested CCM to help unify the conflicting factions within the SPLM. It is these decisions in SPLM which is actually responsible for the ongoing conflict and war in their dear country.
The first round of the dialogue went very well, and at its conclusion the three factions signed a Framework Document. President Salva Kiir, Former Vice President Riek Machar and I, were present to witness this occasion. The parties are now back, and in accordance with the Framework Document, they will now address the root causes of the conflict within the party and devise the way out.
Excellencies;
I am of the view that, if the negotiating teams maintain the spirit they demonstrated in the first round, this process will be crowned with success. They will be able to reunite their Party and pave the way for ease and success of the IGAD peace negotiations in Addis Ababa. We urge the international community and all other people of good will to spare no effort in assisting the SPLM teams involved in the negotiations in Arusha to reach an amicable solution. Let us help them agree to reunify their Party – the SPLM and end the armed conflict which has caused untold suffering and deaths to innocent people in this youngest nation in the world. The newest member of the African Union and the United Nations.
Bilateral Relations
Your Excellency Dean of the Diplomatic Corps;
Excellencies, Heads of Diplomatic Missions;
Representatives of International Organizations;
Ladies and Gentlemen;
Last but not least in importance, I would like to say a few words about our bilateral relations. I am amply satisfied with the state of relations between Tanzania and the countries and organisations you represent. You have been important contributors to our development endeavours. Some of you have been important partners in regional, and global political-diplomatic arena as well.
On behalf of the government and the people of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, I thank you so much for your friendship, cooperation and support. Let us strive to do more in 2015 and advance our bilateral relations to greater heights. You will always find in Tanzania a trusted and dependable friend and partner.
The year 2015 will be an exciting one, especially on the political front with the Constitutional Referendum and the General Elections. We look forward to your usual cooperation, support and understanding. Please do not do otherwise.
After these many words, I once again thank you for accepting my invitation. I wish you all a happy and prosperous New Year 2015. Thank you for your kind attention.

- Dec 31, 2014
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA, TAREHE 31 DESEMBA, 2014
Soma zaidiHotuba
Utangulizi
Ndugu zangu;
Watanzania Wenzangu;
Kama ilivyo ada imefikia siku ya kuuaga mwaka mmoja na kuukaribisha mwaka mwingine. Leo tunauaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2015. Tunamshukuru Muumba wetu mwingi wa rehema kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuifikia siku ya leo. Kwa ndugu na jamaa zetu ambao hawakujaliwa kuiona siku ya leo tuzidi kuwaombea mapumziko mema. Nasi tumuombe Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema atujaalie umri mrefu, afya njema na mafanikio tele kwa kila tuliombalo katika mwaka 2015 na miaka ijayo.
Ndugu wananchi;
Hizi ni salamu zangu za mwisho za mwaka mpya kutoa nikiwa Rais wa nchi yetu. Mwakani salamu kama hizi zitatolewa na Rais wetu mpya. Mimi wakati huo nitakuwa raia wa kawaida kijijini kwangu Msoga nikifuatilia kwenye TV na radio hotuba ya Rais wa Awamu ya Tano ya uongozi wa nchi yetu akitoa salamu zake za kwanza za mwaka mpya, itakuwa siku ya furaha na faraja kubwa kwangu.
Hali ya Usalama
Ndugu Wananchi;
Tunaumaliza mwaka 2014 kwa salama na amani. Mipaka yetu iko salama na hakuna tishio lolote la kiusalama kutoka ndani au nje ya nchi yetu. Uhusiano wetu na nchi jirani na nyinginezo duniani ni mzuri. Hakuna nchi iliyo adui au tunayoitilia shaka kuwa na njama za kuhatarisha usalama wa Tanzania. Nawapongeza wanadiplomasia wetu pamoja na viongozi na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kuifanya nchi yetu kuwa salama.
Uhalifu Unapungua
Ndugu Wananchi;
Taarifa za Polisi zinaonyesha kuwa, mwaka 2014 vitendo vya uhalifu vimepungua ikilinganishwa na mwaka 2013. Mwaka huu, matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa Polisi yalikuwa 64,088 ikilinganishwa na matukio 66,906 katika mwaka 2013. Haya ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vingine vya usalama pamoja na raia wema. Naomba ushirikiano huu uendelee mwaka ujao na miaka ijayo ili tuweze kupata mafanikio makubwa zaidi.
Ajali za Barabarani
Ndugu Wananchi;
Nimefarijika kusikia pia kuwa matukio ya ajali za barabarani nchini nayo yanaendelea kupungua. Mwaka huu kumetokea ajali 14,048 zilizosababisha vifo vya watu 3,534 na wengine 16,166 kujeruhiwa. Mwaka 2013 kulitokea ajali 22,383 zilizosababisha vifo 3,746 na majeruhi 19,433. Hivyo mwaka huu kulikuwa na ajali 8,335, vifo 212 na majeruhi 3,267 pungufu kuliko mwaka jana. Huu ni mwelekeo mzuri na wa kutia moyo ingawa bado ni nyingi mno. Naomba yale tuliyoyafanya yaliyotuwezesha kupata unafuu huu mwaka huu yaendelezwe maradufu mwaka 2015 na miaka ijayo.
Ugaidi
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tumefanikiwa kutambua mtandao wa viongozi na washirika wao wanaotuhumiwa kupanga na kufanya mashambulizi ya kigaidi kwa kutumia mabomu na kumwagia watu tindikali Tanzania Bara na Zanzibar. Watu 112 wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi wametiwa nguvuni. Tayari watuhumiwa 87 kati yao wameshafikishwa mahakamani na waliosalia watafikishwa wakati wo wote. Uchunguzi unaendelea ili kuwatambua wahusika wengine ambao hawajakamatwa.
Ndugu wananchi;
Kwa niaba ya Watanzania wenzangu wote, natoa pongezi nyingi kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri waliyofanya ya kutambua mtandao wa ugaidi nchini na kuchukua hatua thabiti za kuudhibiti. Hali kadhalika nawashukuru raia wema waliotoa taarifa zilizowezesha haya kufanyika. Hatupaswi kubweteka wala kudhani kuwa mambo yamekwisha. Lazima tuendelee kuchukua tahadhari muda wote kwani hatujui adui anapanga kufanya hujuma gani, lini na wapi.
Dawa za Kulevya
Ndugu Wananchi;
Tumeendelea kupata mafanikio ya kutia moyo katika vita dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini. Mwaka huu watuhumiwa 935 wakiwemo vigogo wa biashara hii haramu duniani wamekamatwa. Jumla ya kesi 19 zimefunguliwa Mahakamani. Aidha, kiasi cha kilo 400 za heroine, kilo 45 za cocaine na kilo 81,318 za bangi zimekamatwa. Narudia kutoa pongezi nyingi kwa Kikosi Kazi Maalum cha Kukabiliana na dawa za kulevya nchini kwa mafanikio yanayoendelea kupatikana. Matunda ya kazi yao tunayaona. Naomba juhudi ziongezwe maradufu mwaka ujao na miaka ijayo. Serikali itaendelea kuwaunga mkono.
Ndugu wananchi;
Kama nilivyoahidi mwaka jana, Muswada wa Sheria ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya umeshasomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Novemba, 2014 wa Bunge letu tukufu. Pamoja na kupendekeza kuongeza adhabu kwa makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya, Muswada huo pia unapendekeza kuanzisha chombo kipya chenye nguvu cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya. Muswada huu ukipitishwa na kuwa Sheria tutakuwa tumeongeza nguvu ya mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Ujangili wa Wanyamapori
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka tunaomaliza leo mapambano dhidi ya ujangili na biashara haramu ya bidhaa zinazotokana na wanyama pori yameimarishwa. Kwa ujumla kasi ya ujangili imeendelea kupungua. Katika mwaka 2014 ndovu 114 waliuawa ikilinganishwa na ndovu 219 waliouawa mwaka 2013 au ndovu 473 mwaka 2012. Aidha, majangili 1,354 wamekamatwa na pembe za ndovu 542 na silaha mbalimbali 184 nazo zilikamatwa. Naamini uamuzi wa kuifanya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa Wakala yaani Tanzania Wildlife Agency (TAWA) kutaongeza nguvu ya kuhifadhi wanyama pori na mapambano dhidi ya ujangili.
Natoa pongezi nyingi kwa askari wa wanyamapori, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Serikali na raia wema kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya na mafanikio yanayoendelea kupatikana. Juhudi za kupambana na ujangili na biashara haramu ya bidhaa zinazotokana na wanyama pori zitaendelezwa kwa nguvu zaidi mwaka ujao 2015 na miaka inayofuatia. Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati marafiki zetu wa maendeleo wanaotuunga mkono kwa hali na mali katika mapambano haya. Naomba waendelee kutusaidia.
Hali ya Uchumi Jumla
Ndugu wananchi;
Mwaka 2014 ulikuwa mzuri kwa uchumi wa taifa. Uzalishaji katika sekta nyingi ulikuwa ni mzuri. Ndiyo maana tunategemea kuwa tutafikia au hata kuvuka lengo tulilojiwekea la pato la taifa kukua kwa asilimia 7.4 mwaka huu. Mwaka 2013 pato la taifa lilikua kwa asilimia 7.3. Mfumuko wa bei uliendelea kushuka na kufikia asilimia 5.8 Novemba, 2014 ukilinganisha na Januari 2014 ulipokuwa asilimia 6.0. Hali nzuri ya upatikanaji wa chakula nchini imesaidia sana kufanya mfumuko wa bei kuendelea kushuka. Ni matumaini yangu kuwa mfumuko wa bei utaendelea kushuka na kufikia asilimia 5 ifikapo Juni, 2015.
Mauzo Nje
Ndugu Wananchi;
Mauzo nje yameendelea kuongezeka. Katika kipindi kilichoishia Oktoba 31, 2014, Tanzania iliuza nje bidhaa na huduma zenye thamani ya dola za Marekani milioni 8,503.9 ukilinganisha na mauzo ya dola milioni 8,332.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2013. Mapato yetu yangekuwa makubwa zaidi kama bei za kahawa, chai, korosho na pamba zisingeanguka au bei ya dhahabu nayo isingepada.
Akiba ya Fedha za Kigeni
Ndugu Wananchi;
Akiba yetu ya fedha za kigeni ilikuwa Dola za Marekani milioni 4,251.8 kwa kipindi kilichoishia Novemba 30, 2014. Kiasi hicho kinatuwezesha kuagiza bidhaa toka nje kwa miezi 4.1. Hii ni chini ya lengo letu la kuwa na akiba ya fedha za kigeni ya kuagiza bidhaa kwa miezi minne na nusu. Hata hivyo, sina wasiwasi kabisa kwamba tofauti hii ndogo tutaweza kuiziba mwaka 2015.
Mapato ya Serikali
Ndugu Wananchi;
Makusanyo ya mapato ya Serikali kwa mwezi, kati ya Julai hadi Novemba, 2014 yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 3,555.5 kipindi kama hicho mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 3,924.1 mwaka huu. Hata hivyo, makusanyo hayo yalikuwa asilimia 90 ya lengo tulilojiwekea la kukusanya shilingi bilioni 4,459.7. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato, zipo sababu mbalimbali zilizosababisha lengo lisifikiwe katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2014/2015. Hatua zipasazo zinaendelea kuchukuliwa kurekebisha mambo hayo ili katika nusu ya pili ya mwaka huu wa fedha makusanyo yafikie lengo na ikiwezekana yazidi ili kufidia pengo la nusu ya kwanza.
Takwimu Mpya za Pato la Taifa
Ndugu wananchi,
Ni utaratibu wa kawaida wa nchi zote duniani kuwa na mwaka unaotumika kuwa kizio (base year) cha kukokotoa takwimu za Pato la Taifa. Ni utaratibu wa kawaida pia kwa kila baada ya muda fulani mwaka wa kizio hubadilishwa. Lengo ni kuboresha takwimu husika. Katika marekebisho hayo pia huingizwa thamani ya bidhaa na huduma mpya katika pato la taifa na kuziondoa zilizotoweka ili kutoa picha halisi ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Katika miaka ya hivi karibuni nchi za Ghana (mwaka 2010), Nigeria (mwaka 2013) na Kenya (mwaka 2014) wamefanya marekebisho ya takwimu zao za pato la taifa. Na sisi Tanzania tumefanya hivyo mwaka huu (2014). Hii ni mara ya tano kwa nchi yetu kurekebisha takwimu za pato la taifa. Mara nne zilizopita ilikuwa mwaka 1966, 1976, 1992 na 2001.
Ndugu wananchi;
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekamilisha marekebisho ya takwimu za pato la taifa na kukokotoa takwimu mpya kwa kutumia mwaka 2007 kama mwaka wa kizio. Kutokana na marekebisho yaliyofanyika, pato la taifa kwa mwaka 2013 ni shilingi trilioni 70 kwa kutumia bei za mwaka 2007. Ukitumia bei za mwaka 2001, pato la taifa kwa mwaka 2013 ni shilingi trilioni 53.17. Kuongezeka kwa pato la taifa kumeongeza pia pato la wastani la kila Mtanzania kutoka shilingi 1,186,200 (sawa na US$ 742) kwa bei za mwaka 2001 hadi shilingi 1,560,050 (sawa na US$ 977) kwa bei za mwaka 2007.
Kilimo na Chakula
Ndugu Wananchi;
Mwaka 2014 ulikuwa mzuri sana kwa uzalishaji wa mazao ya chakula nchini. Uzalishaji ulikuwa tani milioni 16.02 ukilinganisha na uzalishaji wa tani milioni 14.38 mwaka wa jana 2013. Hili ni ongezeko la tani milioni 1.64. Kwa mujibu wa mahitaji yetu ya chakula nchini kuna ziada ya tani milioni 3.25. Katika ziada hiyo, mahindi yanachangia tani milioni 1.55, mchele tani 794,000 na kiasi kinachobakia kinachangiwa na mazao mengine ya chakula.
Ndugu wananchi;
Kuna jambo moja muhimu kuhusu ununuzi wa nafaka ambalo ningependa kulifafanua. Naomba ieleweke kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) sio mnunuzi wa mahindi yote, mpunga wote na mtama wote unaozalishwa na wakulima nchini. Wakala hununua sehemu ndogo tu ya nafaka ya ziada iliyozalishwa na hununua kwa ajili ya kuweka akiba ya taifa ya chakula cha kutumika wakati wa dharura ya watu kupata tatizo la njaa. Aidha, Wakala hununua kiasi kinacholingana na uwezo wa maghala yake kuhifadhi. Kwa sasa uwezo wa maghala yetu ni kuhifadhi tani 246,000 ingawaje tunaendelea kujenga maghala mengine mpaka tufikie uwezo wa kuhifadhi tani 400,000 ifikapo 2015. Hivyo basi kwa Wakala kununua tani 292,415.41 mwaka huu ina maana kwamba kiasi cha karibu tani 50,000 zinahifadhiwa nje ya maghala kwa kutumia maturubai. Huu siyo utaratibu mzuri na haifai kuendelea nao kwani kuna hatari ya nafaka hiyo kuharibika na kuzua mgogoro mkubwa siku moja.
Ndugu wananchi;
Baada ya NFRA kununua tani 292,415.41 kuna takribani tani milioni 2.96 za nafaka ya ziada ambayo iliyobaki mikononi mwa wakulima. Mategemeo yetu ni kuwa wafanyabiashara wetu watanunua nafaka hiyo kwa ajili ya kuuza mijini na kwingineko inakohitajika. Bahati mbaya mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka wa jana, wafanyabiashara wetu hawakuweza kununua nafaka yote ya ziada ambayo Serikali haikuweza kununua kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula. Hali hii imezua tatizo ambalo Serikali kwa kushirikiana na wafanyabiashara nchini hatuna budi kulitafutia majawabu. Tunalazimika kutafuta masoko mengine ndani na hata nje ya nchi ya kuuza mahindi, mpunga na mtama wa ziada. Nimeagiza Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Wizara ya Viwanda na Biashara kukaa chini na kushirikiana na wafanyabiashara kulitafutia ufumbuzi suala hili lenye maslahi makubwa kwa wakulima na nchi yetu kwa jumla.
Ndugu Wananchi;
Katika mazingira haya, ninapopata taarifa ya kuwepo watu wanaotaka kuuza mahindi nje ya nchi lakini wanawekewa vikwazo na maafisa wa Serikali inanishangaza na kunisikitisha. Nawataka wale wote wanaofanya hivyo waache mara moja na badala yake wawasaidie wafanyabiashara hao kufanikisha azma yao. Hali kadhalika, tuwashawishi watu wengine nao wajitokeze kufanya biashara hiyo. Jambo muhimu ninalopenda kulisisitiza ni kwamba pawepo na utaratibu mzuri ili biashara hiyo ifanywe kwa kutumia njia halali na zilizo wazi. Kutumia njia za panya hakukubaliki na wala hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Miradi ya Kimkakati
Ndugu wananchi;
Katika mwaka 2014 utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) umeendelea vizuri. Tunayo matumaini makubwa kwamba katika mwaka 2015 miradi mingi itakamilika.
Tuanze na Mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam. Mradi huu unategemewa kukamilika Januari, 2015. Utakapokamilika utatuwezesha kutimiza lengo letu la kuzalisha MW 2,780 za umeme ifikapo 2016. Mipango ya kupata ardhi ya ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi asili kuwa ya kumiminika (LNG) ili iweze kusafirishwa kwenda kwenye masoko, inakwenda vizuri.
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati wa kusambaza umeme vijijini umeendelea vizuri na tumepata mafanikio makubwa yasiyokuwa na mfano wake katika historia ya nchi yetu. Hadi kufikia Novemba, 2014, jumla ya vijiji 3,836 vimepatiwa umeme na vingine 1,500 vinategemewa kupatiwa umeme ifikapo Juni, 2015. Hivyo basi, vijiji 5,336 kati ya vijiji 12,423 vya Tanzania Bara vitakuwa vimepatiwa umeme. Hii ni sawa na asilimia 43 ya vijiji vyote nchini vitavyokuwa vimepata umeme. Hivi sasa wananchi milioni 17.3 nchi nzima sawa asilimia 36 wamefikiwa na huduma ya umeme ikilinganishwa na watu milioni 8.1 sawa na asilimia 18.4 waliokuwa wamefikiwa na huduma hiyo mwaka 2012. Mwaka 2015 tunatarajia watu milioni 18.2 sawa na asilimia 38 watafikiwa na umeme. Kwa upande wa vijijini mwaka 2012 watu milioni 2.3 sawa na asilimia 7 walikuwa na umeme. Ifikapo Juni 2015, idadi hiyo itaongezeka na kuwa milioni 7.4 sawa na asilimia 21. Haya ni mafanikio makubwa kwa wananchi wengi vijijini na mijini kupata umeme katika kipindi kifupi kiasi hiki. Ni mageuzi ya aina yake yatokayotoa mchango muhimu katika kuinua hali za maisha ya Watanzania.
Ndugu Wananchi;
Tunaanza kuiona nuru ya matumaini kwamba siku si nyingi kutoka sasa, makaa ya mawe ya Mchuchuma na madini ya chuma ya Liganga yataweza kutumika kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wa Ludewa. Maandalizi yote muhimu yamekamilika kwa ajili ya Januari, 2015 kuanza ujenzi wa mgodi wa makaa ya mawe kule Mchuchuma, mtambo wa kufua umeme, ujenzi wa mgodi wa chuma kisichoyeyushwa pale Liganga na ujenzi wa kiwanda cha kuyeyusha chuma.
Natoa pongezi maalum kwa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na wabia wenzao, Kampuni ya Sichuan Hongda ya China kwa hatua iliyofikiwa. Inakadiriwa kuwa miradi hii ikikamilika itatoa ajira 33,000 za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja.
Ndugu Wananchi;
Mradi mwingine mkubwa wa kimkakati ni ule wa kujenga Eneo Maalumu la Kiuchumi (Special Economic Zone) la Mbegani, Bagamoyo. Kwa mujibu wa mpango kazi wa wabia wa mradi huo yaani Mamlaka ya Kuendeleza Maeneo huru ya Uwekezaji (EPZA), Kampuni ya China Merchants Holdings International na Mfuko wa Uhifadhi wa Akiba ya Mali za Serikali ya Oman (Oman State General Reserve Fund), ujenzi wa bandari na miundombinu mingine itakayowezesha viwanda kujengwa imepangwa kuanza Julai 2015.
Miundombinu ya Usafiri na Uchukuzi
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka huu wa 2014 kazi ya kujenga barabara za lami na kuimarisha barabara za udongo ili ziweze kupitika wakati wote ziliendelea kote nchini. Huu nao ni mradi mkubwa wa kimkakati. Barabara za lami 19 zenye urefu wa kilometa 1,459 zimekamilika kujengwa mwaka huu katika Mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Kagera, Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Morogoro, Arusha, Tabora na Shinyanga. Ujenzi unaendelea kwa barabara nyingine 24 katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Rukwa, Simiyu, Katavi, Tabora, Mwanza, Dar es Salaam, Kagera na Pwani ambazo wakati wo wote mwaka 2015 zitakamilika. Maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara nyingine nane yanaendelea vizuri sehemu mbalimbali nchini.
Kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara, tumeendelea kufanya kazi ya ujenzi na ukarabati wa barabara za udongo kote nchini. Mwaka huu Mfuko huo umetengewa shilingi bilioni 751.7 ukilinganisha na shilingi bilioni 504.4 mwaka jana. Aidha, mwaka huu tumeweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero. Matumini yetu ni kuwa ujenzi wa daraja hilo na Daraja la Kigamboni utakamilika mwaka 2015. Ujenzi wa Daraja la Malagarasi ulishakamilika mwaka jana, kinachosubiriwa ni sherehe ya uzinduzi.
Kwa upande wa jiji la Dar es Salaam, tunategemea kukamilisha ujenzi wa Awamu ya Kwanza ya barabara za mabasi yaendayo kasi. Ni matarajio yetu pia kwamba mabasi yataanza kusafirisha abiria katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2015. Halikadhalika, tunategemea katika mwaka 2015 ujenzi utaanza wa barabara zinazozunguka jiji la Dar es Salaam (ring roads), barabara ya Mwenge - Morocco na ile ipitayo juu ya nyingine (flyovers) eneo la TAZARA. Vile vile, daraja jipya la Salenda litaanza kujengwa. Aidha, kivuko cha abiria 300 cha MV Dar es Salaam kitaanza kusafirisha abiria kati ya Dar es Salaam Kaskazini na Ferry mapema mwakani. Hatua zote hizi zinalenga kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Usafiri wa Anga na Reli
Ndugu wananchi;
Jitihada za kuboresha huduma ya usafiri katika Reli ya Kati zimeendelea kwa mafanikio. Mwaka huu vichwa vinane vya treni vimekarabatiwa, mabehewa mapya 22 ya abiria na mabehewa 274 ya mzigo yamenunuliwa. Mabehewa hayo yameanza kuwasili nchini kati ya Novemba na Desemba mwaka huu. Kati ya Januari na Mei, 2015 tunatarajia kupokea vichwa vipya vya treni 13. Uboreshaji huu wa huduma za treni unakwenda sambamba na ukarabati wa reli yenyewe, ujenzi wa madaraja na kuimarisha maeneo yaliyo korofi katika reli hiyo.
Kuhusu ujenzi wa reli iliyo pana zaidi (standard guage), yenye uwezo wa kubeba mabehewa mengi na kuwezesha treni kwenda kwa mwendo wa kasi zaidi, juhudi za kutafuta fedha za ujenzi au wabia wa kushirikiana nasi kujenga zinaendelea. Wakati huo huo, tunaendelea na juhudi za kutafuta ufumbuzi kwa matatizo ya reli ya TAZARA ili mambo yaende vizuri. Tutashirikiana kwa karibu na wabia wenzetu wa Zambia. Bahati nzuri Serikali ya China iko tayari kuunga mkono juhudi zetu za kufufua reli ya TAZARA.
Usafiri wa Anga
Ndugu Wananchi;
Sekta ya usafiri wa anga imeendelea kukua katika mwaka 2014. Idadi ya abiria wanaowasili na kutoka katika viwanja vyetu vya ndege nchini imeongezeka kutoka abiria milioni 2.5 mwaka 2013 hadi abiria milioni 3.5 kufikia Septemba, 2014. Safari za ndege kati ya Tanzania na nchi za nje zimeongezeka kutoka 274 Januari, 2013 hadi 295 kufikia Septemba, 2014. Hili ni ongezeko la asilimia 8. Safari za ndege ndani ya nchi nazo zimeongezeka kutoka safari 230,458 mwaka 2013 hadi safari 241,922 mwaka 2014. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 39. Maongezeko haya ni kielelezo na ushahidi kuwa shughuli za utalii na biashara nchini zimeendelea kukua.
Ndugu Wananchi;
Ujenzi wa Jengo la 3 (Terminal 3) la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unaendelea vizuri. Jengo hilo litakapokamilika mwakani, litakuwa na uwezo wa kuhudumia wastani wa abiria milioni 8 kwa mwaka. Aidha, ukarabati wa Jengo la 2 (Terminal 2) utafanyika ili liweze kutoa huduma iliyo bora zaidi. Sambamba na ujenzi huo, Wakala wa Viwanja vya Ndege wameendelea kukarabati na kuboresha viwanja vya ndege vya KIA, Mwanza, Songwe, Bukoba, Tabora na Kigoma. Tunatarajia ukarabati wa viwanja vya ndege vya Shinyanga na Sumbawanga kuanza mapema mwaka 2015.
Elimu
Ndugu wananchi;
Tumeendelea kupiga hatua za kuridhisha katika kuboresha elimu nchini. Tumefanikiwa kupunguza tatizo la upungufu wa maabara, vitabu na walimu wa shule za msingi na sekondari. Mwaka huu tumeajiri walimu 36,339 kati ya 81,562 wanaohitajika. Tumebakiwa na upungufu wa walimu 45,223 yaani 26,946 wa shule za msingi na 18,277 wa shule za sekondari hususan wa masomo ya sayansi. Hivi sasa hatuna tatizo la walimu wa masomo ya sanaa katika shule za sekondari.
Mwaka huu tumeanza mpango maalumu wa kutoa mafunzo ya Diploma ya Ualimu kwa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambapo jumla ya wanafunzi 5,602 wa masomo hayo wamedahiliwa. Mpango huu utatuwezesha kupunguza pengo kubwa tulilonalo la walimu wa sayansi katika muda mfupi zaidi.
Ujenzi wa Maabara
Ndugu wananchi;
Ujenzi wa maabara za Fizikia, Kemia na Baiolojia katika shule za sekondari za Kata 3,463 umekwenda vizuri kiasi. Kwa idadi hiyo ya shule inatakiwa zijengwe maabara 10,389 ilipofika Novemba, 2014. Taarifa kutoka TAMISEMI zinaonyesha kuwa hadi kufikia Desemba 29, 2014, maabara 4,207 sawa na asilimia 40.5 zilikuwa zimekamilika, maabara 5,688 sawa na asilimia 54.8 zilikuwa katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji, na maabara 494 sawa na asilimia 4. zilikuwa katika hatua za awali za ujenzi.
Ndugu Wananchi;
Natoa pongezi nyingi kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Miji nchini pamoja na wananchi, kwa jitihada kubwa iliyofanyika. Kwa kutambua jitihada hizo, nimeongeza miezi sita zaidi kwa wale ambao hawajakamilisha ujenzi wa maabara hizo wafanye hivyo. Sikusudii kuongeza tena muda baada ya hapo. Naomba watumie kipindi hicho kitumike kutafuta vifaa vya maabara. Serikali itasaidia upatikanaji wa watunza maabara (laboratory technicians) ambao tumeanza programu kubwa ya mafunzo yao na mahitaji mengine ya maabara.
Ununuzi wa Vitabu
Ndugu Wananchi;
Tumeendelea kupunguza tatizo la uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia katika shule za msingi na sekondari. Tumekuwa tunanunua vitabu kwa kutumia Bajeti ya Serikali na misaada kutoka kwa marafiki zetu wa maendeleo. Kwa mfano, Serikali ya Marekani imetupatia vitabu milioni 2.5 vya masomo ya sayansi na hisabati kwa shule za sekondari. Ongezeko hili la vitabu linashusha uwiano uliopo sasa wa kitabu kimoja kwa wanafunzi wanne na kufikia kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili. Lengo letu ni kila mtoto kuwa na kitabu chake kwa kila somo ifikapo mwaka 2016.
Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Ndugu wananchi;
Mafanikio mengine tuliyopata mwaka huu ni kukamilika kwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014. Hii ni hatua muhimu sana katika maendeleo ya elimu nchini hakuna badala yake. Sera mpya inalenga kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha Watanzania wengi zaidi kupata fursa za elimu iliyo bora na inayolinga na wakati tulionao. Jambo jipya sana na la kihistoria katika Sera mpya ya Elimu ni dhamira ya Serikali ya kuondoa ada katika elimu ya sekondari kuanzia mwaka 2016. Mpaka sasa hatuna ada kwenye shule za msingi, sasa wakati umefika kufanya hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kwa mujibu wa maelezo hayo ya Sera, nimekwishatoa maagizo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Fedha na Tume ya Mipango kuanza kutafakari namna jambo hilo litakavyotekelezwa.
Afya
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2014 jitihada za kuboresha huduma ya afya kwa Watanzania ziliendelea. Tulipambana kwa mafanikio na mlipuko wa homa ya dengue iliyowapata watu 1,039 na kusababisha vifo vya watu 3 kati yao. Kwa upande wa maradhi ya ebola tumejiandaa vya kutosha kutambua watu wenye maradhi hayo wanapoingia nchini kupitia viwanja vya ndege vya kimataifa na vituo vyote vya mpakani. Aidha, tumejipanga vyema kuwahudumia wagonjwa wa maradhi hayo iwapo watatokea.
Mwaka huu pia, Madaktari wetu watano wamekwenda Liberia kusaidiana na ndugu zetu wa huko katika kukabiliana na ugonjwa wa ebola. Madaktari wetu hao wako salama na wanaendelea vizuri kutoa huduma. Madaktari hao watakaporejea nchini watakuwa hazina kubwa ya taifa katika kupanga mipango ya kukabiliana na ugonjwa huu hatari. Hali kadhalika, watakuwa viongozi wa wengine katika kutibu wagonjwa wa maradhi ya ebola iwapo watatokea nchini.
Ndugu Wananchi;
Katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2014, tumeweza kuajiri watumishi wa sekta ya afya 8,345 ambao kati yao kuna madaktari 244, madaktari bingwa 75, wauguzi 2,555 na wataalamu wa kada nyingine za afya 5,471. Mwaka huu pia tumefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 7,956 katika mwaka 2012/2013 hadi wanafunzi 9,730. Kwa ongezeko hilo, sasa tumefikia asilimia 97 ya lengo letu la kudahili wanafunzi 10,000 ifikapo mwaka 2017.
Jitihada zetu za kuongeza fursa za mafunzo kwa Madaktari, Wauguzi na wataalamu wengine wa afya zina muelekeo mzuri. Ujenzi wa hospitali ya kufundishia pale Mloganzila unaendelea vizuri na hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Dodoma umekamilika. Ni matarajio yangu kuwa wakati wo wote mwakani ujenzi wa kampasi mpya ya Chuo Kikuu cha Muhimbili pale Mloganzila utaanza. Ujenzi huo ukikamilika Chuo kikuu cha Muhimbili kitaweza kudahili wanafunzi 12,000 kutoka wanafunzi 2,500 wa sasa jambo ambalo litafanya upungufu wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Afya kupata jawabu la uhakika. Tumeendelea kufanya mambo mengine ikiwemo ujenzi wa jengo la tiba za ubongo na mishipa ambalo limekamilika pale Muhimbili, sasa tunahangaikia kupata vifaa.
Maji
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka huu wa 2014 tumeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kuwapatia wananchi maji safi na salama mijini na vijijini. Kwa ajili hiyo miradi 498 ya maji vijijini imekamilika na miradi 740 ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Miradi mingine 378 ipo katika maandalizi ya ujenzi kuanza. Ni matarajio yetu kwamba katika mwaka ujao wa 2015, miradi mingine 731 itatekelezwa na vituo 25,790 vya kuchota maji vitajengwa. Miradi hii ikikamilika tutaweza kuwafikia asilimia 71 ya wananchi wanaopata maji safi na salama vijijini kutoka asilimia 58 ya sasa. Kwa ajili hiyo, tutakuwa tumevuka lengo tulilojiwekea la kuwapatia watu maji asilimia 65 ya Watanzania waishio vijijini ifikapo 2015. Ombi langu kwa ndugu zetu wa Hazina waiangalie sekta hii ya maji kwa ukaribu zaidi na wawapatie fedha kwa wakati.
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa mradi wa kuipatia maji miji ya Mwanga – Same – Mkomazi pamoja na miji na vijiji vyote vya njiani, utaanza Februari, 2015. Fedha zimekwishapatikana na Mkandarasi wa Awamu ya Kwanza ameshapatikana. Makandarasi wa Awamu ya Pili na Tatu watapatikana muda si mrefu kutoka sasa. Hii pia itahusu kupata Mkandarasi wa mradi wa maji wa mji wa Orkesment.
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu miradi ya kuipatia maji miji kadhaa nchini ilikamilika na tatizo la upungufu wa maji litakuwa limepatiwa ufumbuzi. Ipo miji kadhaa ambayo miradi imefikia hatua ya juu na kwamba wakati wowote mwakani itakamilika. Jiji la Dar es Salaam lipo katika kundi hili. Kazi ya upanuzi wa miradi ya maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kwa msaada wa Serikali ya Marekani na mkopo kutoka Serikali ya India imefikia hatua nzuri. Inatarajiwa kukamilika katika nusu ya kwanza ya mwaka 2015. Mwaka ujao pia visima virefu vya Kimbiji na Kipera vitachimbwa na Bwawa la Kidunda litaanza kujengwa.
Serikali ya India pia imekubali kutupatia mkopo wa Dola za Marekani milioni 268.2 kwa ajili ya kugharamia mradi wa kuipatia maji miji ya Tabora, Nzega na Igunga kutoka Ziwa Victoria. Uwezekano wa kujumuisha miji ya Sikonge na Urambo katika mradi huo utaangaliwa.
Bunge na Mahakama
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2014, mihimili ya Bunge na Mahakama iliendelea kutekeleza vyema majukumu yao. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeweza kuendesha shughuli zake kama ilivyopangwa pamoja na kulazimika kugawana Ukumbi ule wa Bunge na Bunge Maalum la Katiba. Bunge limefanya mikutano mitatu, Miswada 17 ya Sheria ilisomwa kwa mara ya kwanza, Sheria tano na maazimio saba yalipitishwa. Maswali ya msingi 569 na ya nyongeza 1,541yaliulizwa na kujibiwa. Aidha, sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow nalo lilijadiliwa na kutolewa maazimio. Tumeshaanza kuchukua hatua kuhusu maazimio hayo na bado tunaendelea.
Napenda kuitumia nafasi hii kutoa pongezi nyingi kwa Wabunge wetu kwa kutekeleza vizuri wajibu wao wa Kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Nawasihi waendelee na msimamo huo mwema na chanya kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Mahakama napenda kutambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa ya kupunguza mrundikano wa mashauri katika Mahakama za ngazi zote. Wahenga wamesema “mcheza kwao hutunzwa”. Hatuna budi kutoa pongezi maalum kwa Jaji Mkuu, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kwa uongozi wake mahiri. Chini ya uongozi wake Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wamejiwekea malengo ya kusikiliza na kutoa hukumu kwa mashauri yasiyopungua 200 kwa mwaka kila mmoja wao.
Habari njema na ya kuleta faraja ni kwamba utekelezaji unaendelea vizuri. Mashauri 870 yalisikilizwa na kuamuliwa kwenye Mahakama ya Rufani, mashauri 11,334 kwenye Mahakama Kuu, mashauri 8,715 kwenye Mahakama ya Mahakimu Wakazi na Mashauri 25,683 katika Mahakama za Wilaya. Aidha, mkakati wa kupeleka timu ya Majaji wa Mahakama Kuu kwa wakati mmoja kwenye maeneo yenye mashauri mengi kama ilivyofanyika Kigoma, Shinyanga na Tabora umesaidia sana kupunguza mrundikano wa mashauri ya siku nyingi. Haijawahi kutokea mashauri mengi kiasi hicho kusikilizwa na kumalizwa katika historia ya Mahakama nchini.
Ndugu Wananchi;
Mkakati huu mpya umeleta matumaini mapya kwamba tatizo la kuchelewesha kwa mashauri ambalo lilidhaniwa kuwa ni tatizo sugu sasa limeanza kupatiwa ufumbuzi. Kwa niaba ya Watanzania wenzangu wote natoa shukrani na pongezi nyingi kwa Jaji Mkuu, Majaji wa Rufani, Jaji Kiongozi, Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakimu wa ngazi zote kwa kazi nzuri waifanyayo.
Hali kadhalika, nampongeza Mtendaji Mkuu wa Mahakama na watendaji wote wa Mahakama kwa kazi nzuri waifanyayo ya kuwawezesha Majaji na Mahakimu kutimiza ipasavyo majukumu yao. Hakika utendaji Mahakamani umebadilika na kuwa bora zaidi. Mimi naahidi kuendelea kusaidia Mahakama kwa kuwahimiza ndugu zetu wa Hazina kutoa kwa wakati pesa zilizotengwa katika bajeti.
Mapambano Dhidi ya Rushwa
Ndugu Wananchi;
Mapambano dhidi ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka yameendelea bila ya ajizi. Katika mwaka huu wa 2014 TAKUKURU wamepokea taarifa 237 na wamekamilisha uchunguzi wa mashauri 545. Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani ni 428. Mashauri yaliyomalizika ni 205, kati ya hayo 125 watuhumiwa waliachiliwa na 80 walipatikana na hatia na kuhukumiwa. Mwaka huu wa 2014 mali na fedha taslimu zenye thamani ya shilingi bilioni 38.96 zimeokolewa. Katika kuimarisha Taasisi hiyo kiutendaji, maafisa wapya 394 wameajiriwa.
Sherehe za Miaka 50 ya Muungano
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu wa 2014 tuliadhimisha miaka 50 ya Muungano wa nchi zetu mbili yaani Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika kwa heshima inayostahili. Maadhimisho yalifikia kilele tarehe 26 Aprili, 2014 na zilifanyika sherehe nchini kote na sherehe hizo zilifana sana. Ni ukweli usiopingika kuwa kwa Muungano wetu kuweza kudumu kwa nusu karne ukiwa bado imara na unazidi kustawi ni mafanikio makubwa. Matumaini kwa siku za usoni ni mazuri. Naamini Muungano wetu utaimarika zaidi iwapo Katiba Inayopendekezwa itapitishwa kwani yale mambo yenye kuleta matatizo hivi sasa yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.
Miaka 50 ya JWTZ
Ndugu Wananchi;
Wakati nchi inasherehekea miaka 50 ya Muungano, baadhi ya vyombo na taasisi muhimu kitaifa zilifanya hivyo hivyo. Miongoni mwa walioadhimisha nusu karne ya kuundwa kwake ni Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kama mjuavyo JWTZ ilizaliwa tarehe 1 Septemba, 1964. Jeshi letu liliadhimisha siku yao hiyo kwa kufanya zoezi kubwa la kivita lililoanza Kibaha mkoani Pwani na kumalizikia Monduli Mkoani Arusha.
Nilibahatika kushuhudia siku ya mwisho ya zoezi hilo. Nilifurahishwa sana na kiwango cha utayari kivita cha Jeshi letu. Wanajeshi wetu walionesha weledi wa hali ya juu, umahiri mkubwa, ujasiri, ukakamavu na uvumilivu wa aina yake wakati wa kutekeleza majukumu yao katika mazingira magumu ya uwanja wa medani za vita. Niliwapongeza siku ile na narudia tena leo kuwapongeza. Niliyoyaona yamenihakikishia mimi na Watanzania wote kuwa Jeshi letu la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania liko imara kulinda mipaka ya nchi yetu na kuhakikisha usalama wa taifa letu na watu wake. Jeshi letu bado ni lile tunalolijua sisi sote, lakini limezidi lile lililomng’oa mvamizi Dikteta Iddi Amin wa Uganda, tena limezidi kwa mbali.
Mchakato wa Katiba Mpya
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu pia tumeshuhudia kukamilika kwa zoezi muhimu la kuandika Katiba Inayopendekezwa. Kama tujuavyo sote, mchakato uliozaa Katiba Inayopendekezwa ulikuwa na changamoto nyingi ndani na nje ya Bunge Maalum la Katiba. Pamoja na hayo, Bunge hilo lilikamilisha kazi yake kwa salama siku mbili kabla ya tarehe 4 Oktoba, 2014 ambayo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho. Mimi na Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein tulikabidhiwa nakala za Katiba Inayopendekezwa tarehe 8 Oktoba, 2014. Nimeshatimiza wajibu wangu wa kuchapisha katika Gazeti la Serikali na kutangaza siku ya kupiga kura ya maoni kuwa tarehe 30 Aprili, 2015. Nimeshatoa maagizo kwa Tume ya Uchaguzi kufanya matayarisho husika ya kuwezesha Kura ya Maoni kufanyika.
Ndugu Wananchi;
Moja ya mambo muhimu ambayo Tume ya Uchaguzi inafanya kwa sasa ni kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Mpiga Kura. Tume imeamua kutumia mfumo mpya wa Biometric Voters Register. Uandikishaji wa majaribio umefanyika katika baadhi ya Kata katika Majimbo ya Mlele, Kawe na Kilombero. Matatizo yaliyojitokeza yatasaidia kuboresha mfumo huo kabla ya uandikishaji wa watu wote wenye sifa stahiki kuanza.
Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kuwafahamisha Watanzania wenzangu wote kuwa mfumo mpya unatengeneza Daftari Jipya la Mpiga Kura ingawaje lugha inayotumika ni uboreshaji wa Daftari la sasa. Uboreshaji huu wa Daftari la Mpiga Kura ni tofauti na ule tuliouzoea ambapo walikuwa wanaandikishwa wapiga kura wapya na wale waliopoteza vitambulisho vyao. Safari hii wanaandikishwa wote wapya na wa zamani na wote watapata vitambulisho vipya. Hivyo basi, sisi wenye vitambulisho vya kupiga kura vya zamani tusifanye ajizi, tujitokeze kujiandikisha wakati ukifika.
Jambo la pili ni kwamba, Daftari la Mpiga Kura linalotayarishwa siyo kwa ajili ya Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa peke yake, daftari hilo hilo litatumika pia kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015. Hivyo basi, kujiandikisha ni jambo muhimu sana. Usipofanya hivyo siyo tu utajinyima fursa ya kushiriki kuamua kuhusu Katiba Inayopendekezwa bali pia utakosa fursa ya kuchagua Rais wako, Mbunge wako na Diwani wako. Katu usikubali yakukose hayo.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Ndugu Wananchi;
Kama mjuavyo tarehe 14 Desemba, 2014 na 20 Desemba, 2014 ulifanyika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa. Uchaguzi umekwisha na viongozi wamekwishapatikana. Sasa ni wajibu wa viongozi hao kufanya kazi waliyoiomba. Kwa walioendesha uchaguzi ni wakati mzuri wa kufanya tathmini ili wapate mafunzo yatokanayo na uchaguzi huo. Kwa TAMISEMI na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, lengo liwe ni kuona namna ya kuimarisha mazuri na kusahihisha makosa na matatizo yaliyojitokeza. Kwa walinzi wa amani watambue matatizo ya kiusalama yaliyotokea na kuona namna ya kutengeneza mikakati ya kuzuia matatizo ya namna hiyo yasijitokeze tena. Hatma ya yote, shabaha yetu ni kutaka kufanya vizuri zaidi katika chaguzi zijazo za Serikali za Mitaa na kufanya vizuri zaidi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu Tanzania imechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ni zamu yetu kwa mujibu wa mzunguko wa uongozi wa Jumuiya yetu kati ya nchi wanachama. Ni dhamana kubwa na kwamba wenzetu wa Afrika Mashariki wanatutegemea tuwaongoze katika kutekeleza malengo na madhumuni ya Jumuiya kama yalivyoainishwa katika Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hali kadhalika, tunategemewa kuongoza katika utekelezaji wa maamuzi mbalimbali ya vikao vya Jumuiya. Hii inahusu maamuzi yaliyokwishafanywa kabla yetu ambayo utekelezaji wake unaendelea na uamuzi mpya utakaofanywa katika kipindi cha uongozi wetu.
Kwa niaba ya Watanzania wote napenda kuwashukuru ndugu zetu wa Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda kwa kutuamini. Napenda kuahidi kuwa hatutawaangusha. Sisi Watanzania tutafanya kila tuwezalo kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa manufaa ya Jumuiya yenyewe, nchi zetu na wananchi wa Afrika Mashariki. Tutajitahidi kuwa wabunifu kwa nia ya kuona utangamano unakua na kustawi kwa kasi na kuzaa matunda ya maendeleo tunayoyatarajia sote. Matunda tuliyoyatarajia tulipoamua kuanzisha Jumuiya hii na matunda tuliyoyapata tulipoamua kwa hiari yetu kujiunga nayo kuwa wanachama.
SADC, AU NA UN
Ndugu Wananchi;
Kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, tunaahidi kuendelea kuwa wanachama waaminifu na kushiriki kwa ukamilifu katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mashirika haya ya kikanda na kimataifa. Kwa upande wa SADC tutaendelea kushiriki katika utekelezaji wa mikakati na mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ile ya kisiasa na kiusalama kama ilivyoainishwa katika RISDP (Regional Indicative Strategic Development Plan) na SIPO (SADC Strategic Indicative Plan for the Organ). Kwa ajili hiyo Tanzania, itaendelea kutoa mchango wake katika kukuza utangamano wa kiuchumi katika SADC na kusaidia kuimarisha uhusiano mwema na usalama miongoni mwa nchi wanachama wa SADC. Hii ni pamoja na kusaidia katika kutatua migogoro ya kisiasa na kusalama kati ya nchi wanachama.
Kwa upande wa Umoja wa Afrika tutaendelea kutekeleza maamuzi ya vikao na taasisi mbalimbali za Umoja huo. Daima tutakuwa wanachama waaminifu wa Umoja wa Afrika na kuchangia katika uimarishaji wake. Kuhusu Umoja wa Mataifa tutaendelea kutimiza wajibu wetu kama wanachama wa Umoja huo wa kimataifa ulio adhimu na muhimu kwetu na dunia nzima. Tutaendelea kushiriki katika shughuli za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa. Hivi sasa tunao wanajeshi wetu katika majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Sudan na Lebanon. Tuko tayari wakati wote kuchangia zaidi iwapo Umoja wa Mataifa watatutaka tufanye hivyo.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Namaliza hotuba yangu hii ndefu kwa kuwashukuru Watanzania wote kwa kuiunga mkono Serikali yetu na kwa mchango wenu uliowezesha nchi yetu kupata mafanikio haya makubwa tunayojivunia katika mwaka 2014. Tumeweza kuvuka mitihani na nyakati zenye majaribu mengi. Umoja wetu na mshikamano wetu ndivyo vilivyotuwezesha kufika hapa. Tunauanza mwaka 2015 kwa matumaini makubwa. Mwaka 2015 unatupa fursa kubwa ya kuendelea kuliimarisha zaidi taifa letu. Mwaka ujao ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, hivyo huenda ukawa na changamoto na majaribu magumu zaidi kuliko mwaka huu. Uelewa wetu, umoja wetu, mshikamano wetu na moyo wetu wa uzalendo ndivyo vitakavyotuvusha kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma. Mimi nina imani kubwa kwa uwezo na utayari wa Watanzania wenzangu kuidumisha sifa nzuri ya nchi yetu ya umoja na mshikamano wa watu wake uliozaa amani na utulivu. Tumeweza mwaka huu na miaka ya nyuma, tutaweza tena mwakani na miaka ijayo. Inawezekana, Timiza Wajibu Wako! Nawatakia heri ya mwaka mpya.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa kunisikiliza.

- Dec 22, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DAR ES SALAAM, TAREHE 22 DESEMBA, 2014
Soma zaidiHotuba
Shukrani
Mheshimiwa Makamu wa Rais;
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
Viongozi wa CCM Mkoa;
Viongozi Wenzangu;
Viongozi wa Dini;
Wazee Wangu;
Wananchi Wenzangu;
Nawashukuru sana wazee wangu wa Dar es Salaam, kwa kukubali mwaliko wangu na kuja kuzungumza nami siku ya leo. Natambua kuwa taarifa ilikuwa ya muda mfupi lakini mmeweza kuja kwa wingi kiasi hiki. Naomba radhi kwamba ilikuwa tukutane Ijumaa lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu tukaahirisha mpaka leo. Asanteni sana kwa uvumilivu wenu.
Kama mjuavyo, kila ninapoomba kukutana nanyi ninalo jambo au mambo muhimu kitaifa ambayo napenda kuzungumza nanyi, na, kwa kupitia kwenu taifa zima linapata habari. Leo nina mambo mawili.
Wazee Wangu;
Kwanza kabisa, nataka kurudia kuwashukuru Watanzania wenzangu kwa moyo wenu wa upendo mliouonyesha kwangu katika kipindi chote cha matibabu yangu nikiwa nje na hata baada ya kurejea nchini. Kwa kweli nina deni kubwa kwenu. Lazima nikiri kuwa, salamu zenu na taarifa kwamba watu wamekuwa wananiombea uponaji wa haraka na uzima zinanipa faraja kubwa na kunitia moyo. Nadhani zimechangia sana kuifanya afya yangu kuendelea kuimarika kila kukicha. Bado sijawa “fit” kabisa lakini naendelea vizuri. Hali yangu ilivyo sasa sivyo ilivyokuwa wiki iliyopita au siku niliporejea nchini.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Ndugu Wananchi;
Jambo la kwanza ninalotaka kulizungumzia leo ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Jumapili iliyopita tarehe 14 Desemba, 2014 na jana tarehe 21 Desemba, 2014 katika maeneo ambayo uchaguzi huo uliahirishwa. Bila ya shaka sote tumesikia taarifa ya awali ya zoezi la upigaji kura iliyotolewa na Mheshimiwa Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tarehe 17 Desemba, 2014. Katika taarifa yake hiyo, Mheshimiwa Waziri alieleza kwamba kwa jumla zoezi limeenda vizuri kwenye maeneo mengi nchini. Uchaguzi ulifanyika kwa ukamilifu katika Halmashauri 141 kati ya 162. Katika Halmashauri 21 uchaguzi wake uliahirishwa na umefanyika jana tarehe 21 Desemba, 2014.
Kwa jumla, katika maeneo mengi uchaguzi ulifanyika kwa salama na amani na hivyo kuwapa wananchi fursa ya kuchagua viongozi wanaowapenda kuongoza vijiji vyao, vitongoji vyao na mitaa yao. Kufanyika kwa uchaguzi huu ni uthibitisho mwingine wa kuendelea kukomaa kwa demokrasia nchini. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa wale wote walioshiriki katika uchaguzi huu kwa maana ya vyama vya siasa na wagombea. Natoa pongezi maalum kwa walioshinda. Nawaomba sasa wakae chini kutengeneza mikakati na mipango ya kuwaongoza wananchi wa maeneo yao katika kupata ufumbuzi wa changamoto za maendeleo na za maisha, zinazowakabili.
Ndugu wananchi;
Katika taarifa yake hiyo pia, Waziri Hawa Ghasia alielezea masikitiko yake kuhusu kasoro za uendeshaji wa zoezi zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali. Aidha, aliahidi kuchukua hatua stahiki za kinidhamu dhidi ya watendaji na viongozi wa Serikali waliosababisha kasoro hizo. Alifafanua kuwa miongoni mwa hatua zinazoweza kuchukuliwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, kusimamishwa kazi, kushushwa cheo, kukatwa mshahara au kupewa onyo.
Napenda kuelezea kufurahishwa kwangu na msimamo huo wa Waziri wa TAMISEMI na nampongeza kwa hatua alizochukua. Namuunga mkono na namtaka aendelee na msimamo huo katika kukabili vitendo vya utovu wa nidhamu wa watumishi wa umma. Lazima kila mtumishi wa umma ajue kuwa asipotimiza ipasavyo majukumu yake kuna adhabu inayolingana na kosa alilofanya. Isitoshe, watu hao ndio watakaoendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwakani wakiwa mawakala na wasaidizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hivyo basi, kuwajibishwa wale waliozembea katika uchaguzi, itakuwa fundisho kwao na kwa wengine katika uchaguzi wa mwaka 2015 na chaguzi nyingine zijazo.
Ndugu wananchi;
Kwa upande wa ghasia, fujo na ugomvi uliotokea wakati wa zoezi la uchaguzi, nimezungumza na viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi na kuwataka kuhakikisha kuwa wale wote waliofanya vitendo vya kuvunja sheria wanatiwa nguvuni na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Nimewataka wasifanye ajizi na watu wa aina hiyo. Hawa ni watu hatari ambao hawana budi kuchukuliwa hatua thabiti za kuwadhibiti na kuwaadabisha. Tusipofanya hivyo tunawakatisha tamaa raia wema na watiifu wa sheria. Aidha, watu wakikamatwa na kuachiliwa muda mfupi baadae, wakati mwingine hata bila dhamana ya namna yo yote inawachanganya sana watu wema. Isitoshe tutakuwa tunalea maradhi ya watu wabaya na kuwafanya waendelee kusumbua jamii. Nimewakumbusha kuwa wasipokuwa wakali sasa tunaweka mazingira ya hatari ya kuja kutokea mambo mabaya zaidi mwaka ujao kwenye uchaguzi mkuu.
Sakata la Akaunti ya Tegeta ESCROW
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ninalotaka kulizungumzia si geni masikioni kwenu, nalo ni sakata la Akaunti ya Escrow ya Tegeta. Bila ya shaka mtakumbuka kuwa wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti mwezi Juni, 2014, kulitolewa madai kuwa fedha zilizokuwemo katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta iliyoko Benki Kuu zimechotwa kinyemela na mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power Solution (PAP) akishirikiana na Maafisa wa Serikali.
Serikali iliahidi kufanya mambo mawili. Kwanza, kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi wa Akaunti hiyo na kwamba taarifa yake itawasilishwa Bungeni. Na, pili, kumuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa mwenendo mzima wa miamala katika Akaunti hiyo na kama kuna uhalifu wo wote uliopo kwenye mamlaka yake achukue hatua zipasazo kwa mujibu wa mamlaka na madaraka aliyonayo.
Ndugu Wananchi;
Yote mawili tuliyoahidi tumefanya. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefanya ukaguzi wa miamala katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta iliyoko Benki Kuu na taarifa yake ilishawasilishwa Bungeni. Pia niliagiza taarifa hiyo ichapishwe kwenye magazeti na tovuti ya Serikali ili watu waweze kuisoma. Agizo hilo nalo limetekelezwa. TAKUKURU wameendelea na uchunguzi wao na watakapomaliza na kuridhika kuhusu makosa yaliyofanywa watawafikisha wahusika Mahakamani. Mkurugenzi Mkuu wa PCCB alifika kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali na kutoa baadhi ya mambo kuhusu suala hili aliyoyaona ni muhimu Kamati iyajue.
Mambo Manne Makuu
Ndugu Wananchi;
Tarehe 8 Desemba, 2014 nilipoanza kazi baada ya mapumziko ya ugonjwa nilikabidhiwa taarifa mbalimbali kuhusu sakata hili. Tangu wakati huo nimekuwa nazisoma pamoja na kuzungumza na watu mbalimbali na kuagiza nipatiwe ufafanuzi wa mambo mbalimbali kutoka kwa wahusika. Shabaha yangu ni kuyaelewa vizuri mambo hayo ili niweze kufanya uamuzi ulio sahihi na wa uhakika. Nimebaini kuwa yapo mambo makuu manne:-
(a) Akaunti ya ESCROW
(b)Miliki ya PAP kwa IPTL
(c) Kodi za Serikali, na
(d)Tuhuma za Rushwa
Akaunti ya ESCROW
Ndugu Wananchi;
Katika Mikataba ya Kununua Umeme (Power Purchase Agreements) ambayo TANESCO imetiliana sahihi na kampuni binafsi za kuzalisha umeme za IPTL, SONGAS, SYMBION POWER na AGGRECO, kuna malipo ya namna mbili yanayofanywa na TANESCO. Kwanza, hulipia umeme ilionunua kutoka kwa kampuni hizo yaani tozo ya umeme (energy charges). Na, pili hulipia gharama za uwekezaji uliofanywa na kampuni hizo, yaani tozo ya uwekezaji (capacity charges). Katika mikataba yote hiyo imekubaliwa kuwa iwapo kutatokea kutofautiana, au mzozo unaohusu uwekezaji, upo utaratibu wa usuluhishi. Utaratibu huo unataka kwanza kufanyike mazungumzo, wakishindwa kuelewana watafute mtu wa kuwashauri na kuwasuluhisha; wakishindwa kukubaliana wapeleke shauri lao kwenye Kituo (Mahakama) cha Kimataifa cha Usuluhisi wa Migogoro ya Uwekezaji, (International Centre for Settlement of Investment Disputes – ICSID) kilichopo London, Uingereza
Ndugu Wananchi;
Mwaka 1998 TANESCO walifikisha kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji, London, malalamiko kwamba gharama za uwekezaji za IPTL ni kubwa mno kuliko kiasi halisi walichowekeza. Mwaka 2001 Kituo cha Usuluhisi kilifanya uamuzi wa shauri hilo. Madai ya TANESCO yalikubaliwa kuwa uwekezaji halisi uliofanyika ni Dola za Marekani 127 na siyo Dola milioni 163.17 walizodai IPTL. Kutokana na kupungua huko kwa gharama za uwekezaji, tozo ya uwekezaji (capacity charges) nayo ilipunguzwa kutoka Dola za Marekani milioni 3.6 kwa mwezi mpaka Dola za Marekani milioni 2.6 kwa mwezi. Kituo pia, kilitoa mwongozo kuhusu ukokotoaji wa tozo hiyo.
Ndugu Wananchi;
Miaka minne baadaye TANESCO ilianza vuguvugu la kutaka kupata nafuu zaidi. Waliamua kugomea kulipa tozo ya uwekezaji kwa mkokotoo wa mwaka 2001. Nimeambiwa kuwa wanasheria wa TANESCO walishauri Shirika hilo lidai ukokotoaji kiwango cha tozo ya uwekezaji wa IPTL ufanyike kwa kuzingatia thamani ya hisa walizolipia wawekezaji ambayo ni shilingi 50,000 badala ya kutumia msingi wa mtaji uliotokana na mkopo wa Dola za Marekani milioni 38.16 wa wanahisa uliotumiwa na usuluhisho wa kwanza ICSID-1.
Wakati wakisubiri mchakato wa usuluhishi wa mzozo huu mpya kuanza, pande zote mbili zilikubaliana kuanzisha Akaunti ya Escrow ya Tegeta. Tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ikaanzishwa kwa mkataba uliyotiwa sahihi na IPTL upande mmoja na Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya TANESCO upande mwingine. Aidha, Benki Kuu iliteuliwa kuwa wakala wa kutunza akaunti hiyo nayo ilitia sahihi.
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa mkataba huo, Kampuni ya IPTL iliendelea kupeleka madai ya tozo ya uwekezaji kwa TANESCO ambayo nayo iliwajibika kulipa madai hayo. Malipo hayo yalitakiwa kupelekwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta tofauti na ilivyokuwa kabla ambapo yalipelekwa IPTL moja kwa moja. Utaratibu huu mpya ulikubaliwa kutumika hadi pande mbili zitakapofikia mwafaka kuhusu kiwango cha ukokotoaji. Kwa upande wa malipo ya gharama ya umeme (energy charges) TANESCO imeendelea kulipa moja kwa moja kwa IPTL bila kupitia Akaunti ya Tegeta ESCROW maana hizo hazikuwa na mgogoro.
Ndugu Wananchi;
Kwa miaka saba tangu tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ilipoanzishwa mpaka tarehe 5 Septemba, 2013, wakati Mahakama Kuu ilipokabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP, hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa tozo ya uwekezaji baina ya ITPL na TANESCO. Pande mbili husika hazikuwahi kukaa kuzungumza na wala hakuna shauri lililofikishwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mogogoro ya Uwekezaji kama ilivyofanyika mwaka 1998.
Wakati wote huo, TANESCO iliendelea kulipa madai ya tozo ya uwekezaji ya IPTL na kupeleka malipo hayo kwenye Akaunti ya Escrow. Ulipaji ulisimama katika kipindi kifupi wakati kampuni ya IPTL ilipowekwa kwenye ufilisi. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG, wakati akaunti hiyo inafungwa tarehe 20 Novemba, 2013, kulikuwa na fedha taslimu shilingi 8,020,522,330.37; Hatifungani zenye thamani ya shilingi 159,231,370,000 na Dola za Marekani 22,198,544. Fedha zote hizo ni sawa na shilingi bilioni 202.9.
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kama TANESCO ingelipa tozo ya uwekezaji ipasavyo, wakati huo Akaunti hii ingekuwa na shilingi bilioni 306.7. Kwa sababu ya kutolipa fedha zote ipasavyo, wakati Akaunti inafungwa TANESCO walikuwa wanadaiwa na IPTL shilingi bilioni 103.8. Kwa mujibu wa Mkataba wa Mauzo ya Umeme (PPA) malipo yaliyocheleweshwa, yanatozwa riba ya asilimia mbili ya fedha zote ambazo hazikulipwa kwa wakati. Hivyo basi, riba iliyotokana na TANESCO kuchelewesha malipo ilikuwa Dola za Marekani milioni 33.6.
Ni matumaini yangu kuwa ufafanuzi uliotolewa katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali unasaidia kuweka kumbukumbu sawa na sahihi kuhusu kiasi gani kilichokuwepo kwenye Akaunti ya ESCROW siku uamuzi wa Mahakama ulipofanya akaunti hiyo ifungwe. Kwa kifupi Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaeleza kuwa Akaunti hiyo ilikuwa na shilingi bilioni 202.9 na siyo shilingi bilioni 306.7 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Fedha za Nani
Ndugu Wananchi;
Ni matumaini yangu pia kwamba maelezo haya kwa kiasi fulani yamesaidia kutoa jibu kwa swali maarufu la fedha za kwenye akaunti hii ni za nani? Je ni za umma au za IPTL? Pengine nianze kwa kuelezea Akaunti ya ESCROW ni nini? Akaunti ya ESCROW ni tofauti na akaunti nyingine tunazozijua katika Benki zetu ambazo mtu anaweka fedha zake. Kama tujuavyo, katika Benki zipo Akaunti za aina tatu ambazo wengi tunazifahamu na kuzitumia yaani Akaunti ya Akiba (Savings Account), Akaunti ya Hundi (Current Account) na Akaunti ya Muda Maalum (Fixed Deposit Account). Akaunti ya Escrow ni akaunti maalum inayoanzishwa kwa ajili ya kufanya kazi maalum, kwa masharti maalum na kazi hiyo ikiisha akaunti yenyewe hufungwa. Akaunti hiyo husimamiwa na wakala aliyeteuliwa kwa makubaliano ya wale wanaofungua akaunti hiyo. Wakala ndiye mwenye jukumu la kusimamia akaunti na kumlipa mwenye fedha wakati ukifika. Kwa akaunti ya Escrow ya Tegeta pande mbili husika zilikubaliana kuwa Benki Kuu ndiyo iwe Wakala. Ni muhimu kujua kuwa akaunti hiyo ingeweza kufunguliwa kwenye Benki yoyote siyo lazima BoT.
Akaunti ya Tegeta ESCROW ilifunguliwa BoT mwaka 2006 kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya uwekezaji (capacity charges) zilizokuwa zinalipwa na TANESCO kabla hazijakabidhiwa kwa anayelipwa ambaye ni IPTL. Kabla ya hapo TANESCO ilikuwa inalipa moja kwa moja kwa IPTL. Kama nilivyokwishasema, awali ilifanyika hivyo ili kutoa nafasi kwa pande hizo mbili husika kumaliza tofauti zao kuhusu kiwango cha tozo ya uwekezaji ya IPTL.
Kimsingi basi, fedha hizi ni za IPTL kwani ndiye mlipwaji na ni malipo yanatokana na madai ya IPTL kwa TANESCO kuhusu tozo ya uwekezaji. Hata hivyo, kwa mujibu wa CAG, inawezekana katika fedha hizo kuna fedha za umma. Hi ni kwa namna mbili.
Kwanza, kama mgogoro baina ya TANESCO na IPTL ungetatuliwa na kiwango cha tozo ya uwekezaji kupungua kama ilivyofanyika mwaka 2001 katika ICSID-1 na kama pande mbili husika zingekubaliana au kuagizwa kuwa punguzo hilo lianze kuhesabiwa tangu tarehe ilipofunguliwa Akaunti hiyo (tarehe 5 Julai, 2006), basi kungekuwepo pesa za kurejeshwa TANESCO. Maadamu hili halikufanyika mpaka Mahakama ilipofanya uamuzi uliosababisha akaunti hiyo kufungwa. Katika mazingira hayo fedha zote zinakuwa ni za IPTL maana hakuna madai ya TANESCO.
Ndugu Wananchi;
Namna ya pili ni ile ambapo katika fedha hizi kunaweza kuwepo fedha za umma na iwapo kuna kodi za Serikali ambazo hazijalipwa. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuthibitishwa na TRA ni kwamba kulikuwa na kodi ya VAT ambayo haikulipwa. Nimeambiwa kuwa TANESCO ndiyo ilikuwa na wajibu wa kukata kodi hizo kabla ya kulipa madai ya IPTL lakini kwa baadhi ya malipo haikufanyika hivyo. Hivi IPTL inastahili kudaiwa kodi ya Serikali? Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa, kodi inayotakiwa kulipwa na IPTL ni shilingi bilioni 21.7. IPTL wameshapelekewa madai na TRA, na IPTL wamekubali kulipa.
Katika ukaguzi wa Hesabu za TANESCO za mwaka 2012, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu fedha zilizopo kwenye Akaunti ya ESCROW kama ni fedha zao. CAG aliwaambia TANESCO kwamba fedha hizo si zao.
Maagizo hayo ya CAG yanasomeka kama ifuatavyo:
“As a result, the deposit balance in Escrow account does not meet the definition of an asset of the Company and therefore an adjustment has been made to de-recognize the asset and related liability to the tune of the amounts available in the Escrow account”
Kwa tafsiri yake ni kuwa: “Hivyo basi, fedha zilizowekwa kwenye akaunti ya Escrow hazina sifa ya kutafsiriwa kama ni mali ya kampuni (TANESCO) hivyo, marekebisho yamefanywa ili kutotambua mali na madeni yanayohusu fedha hizo kwa kiasi cha fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow.”
Kutokana na maelezo haya ni dhahiri kwamba, fedha zilizokuwa kwenye Escrow siyo za TANESCO na hazikupaswa kuingizwa kwenye vitabu vya TANESCO kama mali yake.
Chimbuko la Sakata
Wazee Wangu;
Chimbuko la kadhia yote hii Bungeni na kwenye jamii ni uamuzi wa tarehe 5 Septemba, 2013, wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuitambua PAP kuwa mmiliki halali wa IPTL na kuagiza Mfilisi akabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP. Katika utekelezaji wa uamuzi huo wa Mahakama Kuu ukazuka mjadala mkali kuhusu fedha zilizomo kwenye akaunti ya ESCROW kukabidhiwa kwa PAP. Kwanza kabisa mjadala ulikuwa ndani ya Serikali miongoni mwa viongozi na watendaji wa Wizara na Taasisi zinazohusika moja kwa moja na akaunti hiyo. Hizi ni Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO na Benki Kuu. Viongozi na Watendaji husika walikuwa wanajiuliza na kuuliza kama walipe au wasilipe. Walipotaka ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakaelekezwa watekeleze uamuzi wa Mahakama Kuu. Alisema uko sawa na hauna matatizo. Halikadhalika, Benki Kuu walipoulizia kuhusu kodi za Serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza kuwa hakuna kodi ya kulipwa.
Kwa kuzingatia ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, malipo yakafanyika kwa IPTL tena bila ya kodi kulipwa. Baada ya malipo kufanywa ndipo mjadala huo ukahamia katika jamii na Bunge na kugeuka kuwa kadhia kubwa iliyochukua sura ya kashfa yenye dalili za rushwa na wizi.
Uamuzi Unaotiliwa Shaka
Wazee Wangu na Ndugu Wananchi;
Kwa jumla uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu akaunti ya Escrow, ushauri wa Mwanasheria Mkuu kwa Serikali wa kuelekeza uamuzi huo utekelezwe na viongozi wa Serikali kutekeleza ushauri huo vimetiliwa shaka. Umeonekana kuwa haukuwa uamuzi sahihi na kwamba umeitia hasara nchi. Isitoshe uamuzi huo umeibua hisia za kuwepo harufu na vitendo vya rushwa. Wapo waliosema si bure iko namna! Wapo waliotaja majina na watu wanaodai wamepata mgao wa Escrow tena wengine wamechukua fedha kwa viroba, sandarusi na rumbesa. Bahati mbaya sana katika mjadala ilijengeka dhana isiyokuwa sahihi kwamba jambo hili lilianzishwa na Maafisa hao wa Serikali kwa nia ya kujinufaisha wao binafsi. Ukweli ni kwamba uamuzi ulifanywa na Mahakama Kuu na kwenye Serikali ilikuwa utekelezaji wa amri hiyo.
Wazee Wangu;
Nilipokutana na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupata maoni yake kuhusu kadhia hii ameendelea kusema alichosema Bungeni kuwa hakukosea katika ushauri wake na wala Mahakama haikufanya makosa. Hivyo basi, hakuona sababu ya kwenda Mahakamani kuomba marekebisho ya uamuzi wa Mahakama kuhusu fedha zilizokuwepo kwenye akaunti ya Escrow ya Tegeta kukabidhiwa kampuni ya PAP mmiliki wa IPTL. Vilevile haoni kama kuna hasara yo yote ambayo nchi imepata kwa sababu fedha zile ni za IPTL na imelipwa IPTL.
Akifafanua, alisema kuwa akaunti ya Escrow ilianzishwa kwa ajili ya kutunza fedha za malipo ya tozo ya uwekezaji kwa IPTL yaliyokuwa yanafanywa na TANESCO. Kabla ya mzozo kuhusu ukokotoaji wa tozo hiyo na kuanzishwa kwa akaunti ya Escrow ya Tegeta, TANESCO ilikuwa inalipa tozo ya uwekezaji moja kwa moja kwa IPTL. Baada ya kutokea mzozo na akaunti kuanzishwa mambo mawili hayakubadilika. Kwanza kwamba IPTL haikuacha kupeleka madai ya tozo ya uwekezaji kwa TANESCO. Na, pili, kwamba TANESCO haikuacha kulipa madai hayo. Mdai na mdaiwa hawakubadilika. Kuwepo kwa akaunti ya Escrow hakubadili mwenye fedha zake. Akaunti hiyo iliundwa kuhifadhi fedha za IPTL wakati suluhu inatafutwa kuhusu kiwango cha tozo. Matumaini ni kwamba kama kiwango kitapunguzwa, TANESCO inaweza kupata nafuu ya malipo.
Kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu kuruhusu IPTL ilipwe fedha za akaunti ya Escrow, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema ni uamuzi sahihi na wala taifa halikupata hasara kwa sababu pesa zimelipwa IPTL na siyo mtu mwingine. Isitoshe anaona uamuzi wa Mahakama umeisaidia TANESCO kutua mzigo mkubwa iliyokuwa nao kwa miaka saba.
Kama mjuavyo, akaunti ya Escrow ilianzishwa kuhifadhi pesa za malipo ya tozo ya uwekezaji ya IPTL. Ilianzishwa kwa matumaini kuwa TANESCO watapata nafuu ya tozo ya uwekezaji. Lakini, hapakuwahi kufanyika mazungumzo baina ya TANESCO na IPTL kuhusu jambo hilo na wala suala hilo halijafikishwa ICSID. Haikuweza kufanyika hivyo kwa sababu washauri wa kisheria wa TANESCO hawajafanya hivyo. Wapo wanaodai kuwa hawafanyi hivyo kwa sababu hakuna sababu mpya zinazoweza kupatikana kuifanya ICSID ibadili uamuzi wake wa 2001 kuhusu kiasi cha tozo na namna ya ukokotoaji wake.
Matokeo yake ni TANESCO kuwa na akaunti ya Escrow ambayo mwisho wake haujulikani. TANESCO inaendelea kudaiwa na IPTL tozo ya uwekezaji na kulazimika kulipa kwenye akaunti hiyo. Kwa masharti ya akaunti ya Escrow wanaposhindwa kulipa wanatozwa riba. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG mpaka tarehe 20 Novemba, 2013, TANESCO ilikuwa inadaiwa shilingi bilioni 103.8 ambazo hawajalipa kwenye akaunti ya Escrow na riba ya Dola za Marekani milioni 33. Kwa sababu hiyo basi uamuzi wa kufunga Akaunti ya Tegeta Escrow unalipatia unafuu TANESCO dhidi ya kulimbikiza madeni na riba.
Kwa upande wa kodi za Serikali ambazo hazikulipwa, Mheshimiwa Jaji Werema alisema yeye alitoa ushauri tu. Hata hivyo, kama mamlaka husika inaona zipo kodi zinazostahili kulipwa izidai. Hakuna kilichopotea kwa sababu anayedai, yaani TRA yupo, na mdaiwa yupo, IPTL.
Uamuzi wa ICSID II Kuhusu Tozo ya Uwekezaji
Wazee Wangu;
Yalitolewa mawazo kuwa kama fedha za akaunti ya Tegeta Escrow zingelipwa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji (ICSID II) kutoa uamuzi wake, TANESCO ingepata nafuu ya kupungua kwa tozo ya uwekezaji. Kuhusu jambo hilo nimeambiwa kwamba kuna mambo mawili ya msingi. Kwanza kwamba Mahakama hiyo haikutoa viwango vipya vya tozo kama ilivyofanya mwaka 2001 kwenye ICSID–I. Haikubadili mwongozo wa ukokotoaji wa tozo. Imesema madai yanaweza kuzungumzwa na kusisitiza kuwa katika mazungumzo hayo TANESCO watambue kwamba wanahisa waliwekeza mtaji wao binafsi wakati wa kununua mtambo na pia walikopa madeni, na kwamba kiasi cha fedha walichowekeza kilitakiwa kiwe na kiwango cha juu zaidi cha faida.
Jambo la pili ni kwamba, shauri hili la pili la ICSIDI II halikuihusisha kampuni ya IPTL mwenye Mkataba wa Kuuza Umeme na TANESCO na siyo Benki ya Standard Charterd. IPTL wameweka pingamizi la utekelezaji wa uamuzi wa shauri hilo hapa nchini, hivyo inakuwa vigumu kwa TANESCO kufanya mazungumzo kwa msingi wa shauri hilo.
Kinga Dhidi ya Madai
Wakati wa kufunga akaunti ya Escrow, upande wa Serikali ulielezea hofu yake ya uwezekano wa siku za usoni mtu kudai tena kulipwa fedha hizi hizi ilizolipwa PAP. Nimeambiwa kuwa suala hilo haliwezi kutokea kwani limetengenezewa wigo imara wa kimkataba kuzuia. PAP imetiliana sahihi na Serikali kwamba iwapo kutatokea mdai yo yote PAP itawajibika kulipa.
Mashaka ya Miliki ya PAP kwa IPTL
Ndugu Wananchi;
Hofu nyingine kuhusu uwezekano wa Serikali kupata hasara ni yale madai kuwa huenda miliki ya PAP kwa asilimia 70 za hisa za IPTL zilizokuwa za kampuni ya Mechmar Berhard ya Malaysia siyo halali. Pale mwanzoni ilidaiwa kuwa kampuni ya Mechmar ilipouza hisa zake kwa kampuni ya Piper Link ya British Virgin Islands ilikuwa chini ya mchakato wa ufilisi kule Malaysia. Kama ingekuwa hivyo, kisheria mtu hawezi kuuza hisa zake akiwa kwenye mazingira hayo. Katika uchunguzi wa CAG alieleza kuwa amethibitisha kwamba madai hayo si kweli, Mechmar walipouza hisa zao tarehe 9 Septemba, 2010 kampuni haikuwa kwenye ufilisi. Iliingia kwenye mchakato wa ufilisi mwaka 2012.
Lakini kwa upande wa kampuni ya Piper Link ya Uingereza inasemekana iliuza hisa hizo baada ya kuwa wamepokea amri ya Mahakama ya Malkia ya BVI kuizuia isiuze hisa hizo. Je ni kweli? Imefanyika hivyo? Kama ni kweli je PAP waliponunua hisa hizo walijua kama kuna zuio au hapana? Kama walijua basi na wao ni sehemu ya njama za kufanya udanganyifu. Kama hawakuwa wamejua basi wametapeliwa. Nimeagiza uchunguzi wa kina ufanyike kupata ukweli. Natambua hivi sasa Mahakamani zipo kesi zinazohoji uhalali wa PAP kumiliki asilimia 70 za hisa za Mechmar Berhad. Uchunguzi wetu hautaingilia mchakato huo lakini unaipa Serikali fursa nzuri ya kuchukua hatua zipasazo kuhusu suala hili lenye mjadala mkubwa. Jambo lingine muhimu ambalo limeleta matatizo kwa Mahakama zetu nchini na BRELA ni uuzaji wa hisa za IPTL au kuwekwa rehani hisa hizo bila ya uamuzi huo kusajiliwa BRELA na kwenye Mahakama zetu. Sheria zetu ambazo ndizo za nchi ya Jumuiya ya Madola kama ilivyo kwa Hong Kong, Malaysia, na BVI, inaitaka kampuni ya Piper Link ya BVI iliponunua hisa za Mechmar katika IPTL kusajili BRELA ununuzi huo. Hali kadhalika, inaitaka SCB ya Hong Kong na kupata amri ya Mahakama kuzuia deni la Mechmar na kuwekwa dhamana ya hisa za Mechmar katika IPTL. Piper Link isiuze hisa 70 za Mechmar katika IPTL. Walitakiwa wasajili na BRELA na Mahakama yetu. Kutokufanya hivyo ndiko kunazua maneno mengi na mzozo kuhusu uuzaji wa hisa hizo kwa PAP. Kwa SCB wanapata usumbufu wa kudai madeni yao IPTL kwa sababu hiyo hiyo. Uchunguzi utakaofanyika utapata ukweli wa yote kwa uhakika.
Ndugu Wananchi;
Taarifa niliyopewa wakati najiandaa kuzungumza nanyi ni kuwa katika Mahakama zetu nchini kuna mashauri yahusuyo miliki ya PAP ya hisa 70 zilizokuwa za Mechmar katika IPTL na yapo mashauri yahusuyo PAP kupewa fedha za akaunti ya Escrow. Zipo pia nyingine za masuala mbalimbali yakiwemo mashauri yaliyofunguliwa na PAP dhidi ya watu, na makampuni binafsi na vyombo vya Serikali. Naamini uamuzi wa Mahakama zetu utatoa majibu kwa masuala yote hayo.
Pamoja na hayo yatakayokuwa yanaendelea Mahakamani, Serikali itaendelea kufanya uchunguzi wake na kuamua namna ya kushughulikia taarifa zitakazopatikana ili nayo iweze kwenda Mahakamani itakapolazimu kufanya hivyo.
Jambo lingine muhimu nataka uchunguzi wa kina ufanyike ni kujua nani ni nani katika uuzaji na ununuzi wa hisa za Mechmar. Hususan nataka tujue kwa ukweli na uhakika hisa hizo zimeuzwa kwa bei gani. Je, ni kweli gharama zinazosemwa ndizo zenyewe? Nataka kuthibitisha ukweli huo ili tujue kodi yetu ya ongezeko la mtaji (Capital Gains Tax) inayostahili kulipwa Tanzania ni kiasi gani? Je kiasi gani kimelipwa na kipi hakijalipwa ili kidaiwe?
Tuhuma za Kuwepo kwa Harufu ya Rushwa
Wazee Wangu;
Kumekuwepo na tuhuma za vitendo vya rushwa katika mchakato mzima wa kufunga akaunti ya Escrow na kukabidhi fedha hizo kwa kampuni ya PAP. Halikadhalika, kumekuwepo na hisia hizo hizo kwa upande wa jinsi kampuni ya VIP Engineering and Marketing ilivyotumia pesa zake zilizoko kwenye Benki ya Mkombozi. Yamesemwa mengi sana na mmeyasikia na kuyasoma.
Rushwa ni kosa la kijinai ambalo kwa Serikali yetu ni kosa ambalo ni vigumu kulivumilia wala kulifumbia macho. Mara baada ya kupata fununu za uwezekano wa vitendo hivyo kufuatia taarifa ya awali ya CAG ya kwenda kukagua miamala, niliagiza taarifa husika zifikishwe kwenye Taasisi ya Kupamba na Kuzuia Rushwa (PCCB) kwa uchunguzi zaidi. Naambiwa taarifa hizo zimefika na kazi ya uchunguzi inaendelea. Tayari watu kadhaa wamehojiwa na wengine wanaendelea kuhojiwa. Wakati nawasihi wananchi kuvuta subira ili tuwape nafasi PCCB wakamilishe kwa ufanisi wa hali ya juu kazi yao waliyokwishaianza, nawaomba PCCB waongeze kasi ya uchunguzi. Napenda kufafanua kwamba kwa upande wa miamala iliyotoka katika akaunti ya kampuni ya VIP Engineering and Marketing ya Ndugu James Rugemalila, Serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa kuzingatia Sheria ya Maadili ya Utumishi wa Umma, maana suala lao ni la kimaadili. Hatuwahoji wasiokuwa watumishi wa umma.
Maazimio ya Bunge
Ndugu Viongozi;
Wazee Wangu;
Ndugu Wananchi;
Niliona nianze kwa kutoa maelezo hayo ya utangulizi kabla ya kuyazungumzia maazimio ya Bunge. Serikali imepokea maazimio hayo ya Bunge na kuyafanyia kazi kwa ajili ya utekelezaji wake. Nawapongeza Wabunge wetu kwa moyo waliouonesha wa kuchukia maovu na kutaka yashughulikiwe ipasavyo. Napenda kuwahakikishia kuwa niko pamoja nao. Nampongeza Mheshimiwa Anna Makinda, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, Naibu Spika na Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Mussa Zungu kwa uongozi wao mahiri. Hakika haikuwa kazi rahisi, lakini chini ya uongozi wao mambo yameisha salama na tumepata maazimio nane yanayozungumzika na kutekelezeka. Nawashukuru na kuwapongeza sana Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya uongozi wa Mheshimiwa Zitto Kabwe na Mheshimiwa Deo Filikunjombe na pia Wajumbe waliounda Kamati ya Mapendekezo kwa kufikia mwafaka wa mapendekezo haya 8 ambayo yaliazimiwa na Bunge.
Mwisho lakini si ya mwisho kwa umuhimu, nawapongeza Wabunge wote kwa michango yao mizuri. Jambo lililonifurahisha sana ni ushirikiano wa Wabunge wa kambi zote katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili muhimu,. Hivi ndivyo inavyotakiwa Bunge liwe. Kwa kweli lazima nieleze mshangao wangu niliposikia kambi ya upinzani ikijaribu kufanya maamuzi yale ni yao wao na wenzao hawamo. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ina Wajumbe 19 wa CCM na wa Upinzani 5. Bunge lina Wabunge wa CCM asilimia 74 na wa upinzani asilimia 26. Hivi kama ni yao wao pekee na wa upande wa CCM wangepinga yangekuwa? Yasingefika po pote, yangefia kwenye Kamati. Huku ni kutafuta umaarufu kwa mgongo wa wengine. Na, Wabunge wengi wa CCM na nyie semeni msikike kwa uamuzi mliyofanya wote.
Napenda kuwahakikishia kuwa mimi na wenzangu Serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kutekeleza yale maazimio yanayoangukia katika dhamana yetu. Napenda kuainisha mtazamo na mwelekeo wa Serikali katika utekelezaji wa maazimio hayo manane kama ifuatavyo:-
Azimio la kwanza: Serikali iangalie uwezekano wa kuchukua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa mujibu wa Sheria za nchi.
Pendekezo tumelipokea, ni jambo linalowezekana kufanya. Hata hivyo, tunapopima ujumbe tunaoupeleka kwa jumuiya ya wawekezaji tunachelea kuwa inaweza kuleta hofu na kuwatisha wawekezaji waliopo na wajao. Nalisema hivyo kwa sababu sisi tuna historia ya kutaifisha mali za kamapuni binafsi. Hofu hiyo bado ipo. Tukichukua mitambo hii tunaweza kurudisha hofu za kurudi tulikokuwa na kukimbiza mitaji tunayohitaji kwa uchumi kukua na nchi kupata maendeleo. Nashauri tuendelee kuyapatia ufumbuzi matatizo ya IPTL kila tunapoyabaini. Aidha, Mahakama imetusaidia sana kwa kuamuru mitambo ya IPTL ibadilishwe ili itumie gesi asilia na kutoza bei ya umeme isiyozidi senti nane za Marekani. Tuyafuatiliye haya kwanza.
Azimio la Pili: Azimio hilo linazungumzia kuhusu uwazi wa Mikataba linasomeka ifuatavyo: “Bunge limeazimia kwamba Serikali itekeleze Azimio husika la Bunge mapema iwezekavyo na kwa vyovyote vile kabla ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti. Serikali iwasilishe taarifa ya utekelezaji wa mapitio ya mikataba ya umeme”.
Azimio hili tumelipokea na tunaangalia namna bora ya kulitekeleza ili kuweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kwanza, kuitikia kilio cha muda mrefu kuhusu uwazi katika mikataba ambayo Serikali inaingia na wawekezaji; na pili kuhakikisha usiri wa mikataba hiyo ambayo ni haki ya wawekezaji hao dhidi ya washindani wao inazingatiwa. Serikali na Bunge tutakaa chini hivi punde kutafuta namna bora ya kisheria na tutafanya hivyo kwa kujifunza pia kutokana na uzoefu wa nchi ambazo zina utaratibu wa aina hii.
Azimio la Tatu: Linasomeka; “Bunge linaazimia kwamba TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama vichukue hatua stahili kwa mujibu wa sheria za nchi yetu dhidi ya watu waliotajwa kwenye taarifa maalum ya Kamati husika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya ESCROW, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusu kuhusika kwao katika vitendo hivyo vya jinai”
Vyombo husika vimekwishaagizwa kufanya hivyo na kazi imeanza na inaendelea. Ikiwa wapo watu wenye makosa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Azimio la nne: Linasomeka, “Kamati za Bunge kuwavua nyadhifa zao wenyeviti wa Kamati za Bunge waliotajwa kupewa fedha na kampuni ya VIP Engineering kabla ya kikao kijacho cha Bunge”
Azimio hilo liko chini ya mamlaka ya Bunge lenyewe. Nawaachia wao waamue.
Azimio la Tano: Linasomeka; “Bunge linaazimia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania”
Azimio hili nimelipokea, tumelijadili hata hivyo, itabidi tufuate utaratibu wa kikatiba na kisheria wa kushughulikia masuala ya namna hiyo. Inatakiwa suala kama hili lianzie kwenye Mhimili wa Mahakama yenyewe na siyo kwa Rais au Bunge. Tume ya Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumtaka Rais aunde Tume ya Kijaji ya kumchukulia hatua Jaji yeyote pale inaporidhika kuwa amepoteza sifa za kuendelea kufanya kazi hiyo. Nashauri suala hili tumuachie Jaji Mkuu wa Tanzania alishughulikie atakavyoona inafaa.
Azimio la Sita: “Bunge linaazimia kwamba mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi kuitaja Stanbic Bank Ltd. na benki yeyote itakayogundulika kufuatia uchunguzi wa mamlaka ya uchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika akaunti ya ESCROW kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu (Institutions of money laundering concerns).
Pendekezo la Bunge ni zuri kwamba mamlaka husika na udhibiti wa vitendo vya utakatishaji fedha vifanye uchunguzi kwa mujibu wa Sheria. Serikali imelipokea na mamlaka husika yaani Financial Intelligence Units kulishughulikia. Naamini wameshaaza, tuwape muda watimize wajibu wao kwa mujibu wa sheria.
Azimio la Saba: “Bunge liliazimia kwamba Serikali iandae, na kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria iliyounda TAKUKURU kwa lengo la kuanzishwa Taasisi mahsusi itakayoshughulikia kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Kazi ya kufanya mageuzi katika TAKUKURU inaendelea. Tayari Sheria mbalimbali zimetungwa ikiwa ni pamoja na Sheria Mpya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2008, Sheria ya Kudhibiti Matumizi ya Fedha Haramu ya mwaka 1991 ambazo zote zinaweka utaratibu wa kushughulikia vitendo vya rushwa. Tutaendelea kuziboresha sheria hizo kwa kadri itakavyohitajika. Kazi iliyopo mbele yetu ni kuimarisha usimamizi wa sheria hizo. Jambo hilo nalo litazingatiwa katika maboresho hayo. Ni dhamira yangu na ya Serikali ninayoiongoza kupambana na kushinda vita dhidi ya rushwa. Kwa hiyo tuko tayari kulifanyia kazi pendekezo lolote linaloimarisha dhamira yetu hii njema.
Azimio la nane: “Bunge linaazimia kwamba Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi na Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.
Azimio hili ndilo Azimio ambalo limevuta hisia za watu wengi, na pengine ndilo ambalo utekelezaji wake unasubiriwa kwa hamu. Utekeelzaji wake umeanza. Kwanza, ni kuhusu Bodi ya TANESCO, tumeanza mchakato wa kuunda Bodi mpya kwani iliyopo imemaliza muda wake. Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni mtumishi wa umma anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshajiuzulu. Tumelitafakari suala la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi la kupokea fedha kutoka VIP Engineering and Marketing ambazo kwa maelezo yake ni kwa ajili ya shule anayoimiliki na kuiendesha. Mwenyewe ameeleza wazi kupitia vyombo vya habari. Pamoja na hayo yapo mambo ya msingi kimaadili ambayo hayakuzingatiwa, hivyo tumemwomba atupishe tuteue mwingine. Kuhusu Prof. Muhongo nimemuweka kiporo, kuna uchunguzi niliagiza ufanywe na vyombo vyetu bado nasubiri taarifa hiyo ili nifanye uamuzi ndani ya siku chache zijazo.
Hitimisho
Wazee Wangu;
Nawashukuruni kwa kunisikiliza.

- Nov 04, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA DODOMA, UKUMBI WA KILIMANI, DODOMA, 4 NOVEMBA, 201...
Soma zaidiHotuba
Ndugu Wananchi;
Nakushukuru sana Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Dodoma, Mheshimiwa Balozi Job Lusinde kwa kuandaa mkutano huu. Wakati nilipofanya ziara ya Mkoa wa Dodoma tulipanga tukutane lakini kwa vile ratiba yangu iliingiliwa na mambo mengi, hivyo haikuwezekana, lakini leo imewezekana. Pengine hii ndiyo siku ambayo Mwenyezi Mungu alipanga tukutane. Tumshukuru Muumba wetu kwa rehema zake, na tumuombe ajaalie mkutano wetu uanze salama na uishe salama. Nawashukuru kwa Risala yenu na maudhui yake. Nawaahidi nitayafuatilia na majibu mtapata. Pamoja na yaliyomo kwenye risala yenu mimi nina mambo manne ambayo ni yatokanayo na ziara yangu nchini China na Vietnam, maradhi ya Ebola, uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hatua zinazofuata kwenye Mchakato wa Katiba.
Ziara ya China na Vietnam
Ndugu Wananchi;
Kuanzia tarehe 21 Oktoba, 2014 hadi tarehe 28 Oktoba, 2014 nilikuwa katika ziara rasmi ya kutembelea nchi za China na Vietnam. Nilitembelea China tarehe 21 hadi 26 Oktoba, 2014 na Vietnam tarehe 26 hadi 28 Oktoba, 2014. Ziara hizo nilizifanya kufuatia mwaliko wa Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping na mwaliko wa Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tan Sang. Ziara katika nchi hizo zilikuwa za mafanikio makubwa sana hata kuliko nilivyotarajia. Nchini China tulipokelewa kwa namna hawajafanya kwa miaka mingi.
Ziara ya China
Ndugu Wananchi;
Nchini China, kwa makubaliano na wenyeji wetu tulifanya hafla maalum ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China. Katika hafla hii upande wa China uliwakilishwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Li Yuanchao. Pande zetu mbili ziliitumia fursa hiyo kuzungumzia tulipotoka, tulipo sasa na mbele tuendako.
Kwa jumla wote tumeridhika kuwa tumekuwa na nusu karne ya uhusiano wenye mafanikio makubwa. Katika kipindi hiki nchi zetu zimekuwa marafiki wa kweli, wa kuaminiana na kusaidiana kwa mambo mengi. Katika medani za kimataifa nchi zetu zimekuwa zikielewana kwa mambo mengi na kusaidiana. China ilikuwa ngome kuu katika kusaidia kwa hali na mali harakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika.
Wakati ule Tanzania ilikuwa ikiongoza nchi za mstari wa mbele. Wenzetu bado wanakumbuka sana jinsi nchi yetu ilivyokuwa mstari wa mbele kuipigania nchi ya China kurejeshewa haki yao hususan ya kuketi kiti chao katika Umoja wa Mataifa, baada ya Chama cha Kikomunisti chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mao Tse Tung kufanikiwa kukishinda Chama cha Kuomintang na kiongozi wake Chian Kai Sheki na kulazimika kukimbilia Taiwan. Mataifa makubwa ya Magharibi yalikataa kuitambua China mpya na kuitenga. Katika kufanya hivyo, waliitambua Taiwan na kuifanya kuwa ndiyo wawakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa.
Baada ya hapo Jamhuri ya Watu wa China ilipinga uamuzi ule na kuanzisha kampeni ya kudai haki yake stahiki. Madai yao hayo yalipata nguvu pale Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alipoamua kuwa Tanzania ishiriki katika kampeni hiyo kwa nguvu zake zote. Kwa kushirikiana na nchi nyingine rafiki, jitihada hizo za pamoja zilizaa matunda na mwaka 1971, China ilipokubaliwa kuchukua nafasi yake stahiki katika Umoja wa Mataifa na Taiwan kuondolewa. Ndugu zetu wa China hawasahau msaada wetu huo na hawaoni haya kulisemea waziwazi jambo hilo na vizazi vyote vya China vinafundishwa kuhusu wema ambao Tanzania imewafanyia. Kwa sababu hiyo, Tanzania ina nafasi maalum nchini China. Wao wenyewe wana msemo maalumu kuhusu Tanzania kwamba ni “all weather friends”. Yaani marafiki wa majira yote.
Katika ziara yangu nilifuatana na kaka yangu Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye ndiye alikuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakati ule. Rafiki zetu wa China walifurahi sana kumwona Dkt. Salim kwani yeye hasa ndiye aliyefanya kazi ya kushawishi nchi nyingine kuiunga mkono Jamhuri ya Watu wa China. Pia nilifuatana na Mheshimiwa Balozi Mstaafu Jenerali Mrisho Sarakikya aliyekuwa Mkuu wa Majeshi wa kwanza wa Tanzania. Yeye ndiye alihusika sana kujenga uhusiano wa mambo ya kijeshi baina ya nchi yetu na China. Pia, nilikwenda na Balozi Mstaafu, Mzee Waziri Juma aliyewahi kuwa Balozi wa Pili wa Tanzania nchini China.
Kama mjuavyo nchi ya China imetusaidia mambo mengi kwa maendeleo yetu. Misaada mingine ilihusu vitu vikubwa ambavyo katika hali ya kawaida isingewezekana kusaidiwa na nchi nyingine zinazotoa misaada ya maendeleo na mikopo. Miongoni mwa hayo ni ujenzi wa Reli ya Uhuru (TAZARA), misaada ya zana, vifaa na mafunzo vilivyosaidia kujenga Jeshi letu jipya yaani JWTZ baada ya kuvunjwa kwa lile tulilorithi kutoka kwa Wakoloni kuaasi Januari 20, 1964. Msaada wao mkubwa ndiyo uliotuwezesha mpaka kuweza kulinda na kukomboa nchi yetu dhidi ya uvamizi na kutekwa eneo la Misenyi, Kagera na majeshi ya dikteta Iddi Amin wa Uganda.
Hata sasa China imeendelea kuwa mshirika wetu mkubwa kuliko wote katika kuimarisha na kuendeleza Jeshi letu. Msaada mwingine mkubwa ni ule mkopo wa dola za Marekani bilioni 1.2 wa kujenga bomba jipya la gesi kutoka Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam. Isingekuwa rahisi kupata mkopo mkubwa kiasi kile kutoka nchi nyingine au Shirika lolote la fedha duniani. Mkopo ule unalimaliza tatizo la upungufu wa umeme kutokea sasa mpaka mwaka 2020 inapokadiriwa kuwa nchi yetu itahitaji megawati 10,000. Hata wakati huo bomba hili ni muundombinu wa msingi utakaorahisisha upanuzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme kutosheleza mahitaji hayo kama itaamuliwa gesi iendelee kuwa chanzo kikuu cha nishati ya umeme nchini.
Katika mazungumzo yangu na Waziri Mkuu Li Keqiang na Rais Xi Jinping wote wawili wameelezea kuridhika kwao na uhusiano baina ya nchi zetu tangu siku za nyuma mpaka hapa tulipo sasa. Hali kadhalika walielezea kuwa wangependa kuona uhusiano wetu na ushirikiano wetu unaimarika na kukua mpaka kufikia hatua bora na ya juu kabisa. Niliwahakikishia kuwa hiyo ndiyo fikra yangu na Watanzania kuhusu uhusiano baina ya nchi zetu mbili rafiki.
Kwa nyakati tofauti viongozi wote wakuu wa China walinihakikishia utayari wao wa kuendelea kuchangia maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiusalama ya Tanzania. Jambo lililonipa faraja kubwa mimi na wenzangu ni kuwa mambo yote tuliyoomba ndugu zetu wa China watusaidie wamekubali. Hakika Wachina wameendelea kuwa marafiki wa kweli wa nchi yetu na watu wake.
Tuliwaomba waendelee kushirikiana nasi na wabia wenzetu wa Zambia kulijenga upya Shirika la Reli ya TAZARA na wamekubali. Tuliwaomba pia tuendelee kushirikiana kukuza uwekezaji na biashara baina ya nchi zetu mbili rafiki. Walilipokea jambo hilo kwa furaha. Ni ukweli ulio wazi kwamba biashara na uwekezaji umekua sana kiasi cha kuifanya China kuwa nchi inayoongoza kwa mambo yote mawili. Hata hivyo, sote tumekubaliana kuwa biashara ya dola za Marekani bilioni 3.7 na uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 2.5 ni kidogo mno hivyo tuongeze juhudi tufanye vizuri zaidi katika kipindi kifupi kijacho.
Ndugu Wananchi;
Kulikuwa na mkutano mkubwa wa uwekezaji uliohudhuriwa na makampuni ya kichina yapatayo 500 yaliyokuwa tayari kuwekeza na kufanya biashara na Watanzania. Kwa upande wetu miradi kadhaa tuliyopeleka imepata wabia. Miongoni mwa waliofaninikiwa sana ni Shirika la Nyumba la Taifa waliopata wabia watakaowekeza dola za Marekani bilioni 1.7 kwenye ujenzi wa nyumba.
Aidha, kuhusu ujenzi wa Ukanda wa Kiuchumi wa Mbegani ambao tuliwaomba watusaidie kusukuma utekelezaji wake, viongozi wa China walielezea utayari wao kusaidia mradi huo ufanikiwe. Tulipokuwa Shenzhen, tulipata nafasi ya kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya China Merchants Ltd., na kuzungumza na viongozi wake. Walitembezwa kuangalia shughuli za kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na jinsi Kampuni hiyo ilivyoshiriki katika ujenzi wa mji wa Shenzhen kutoka kijiji cha uvuvi na kuwa jiji kubwa la kisasa, lenye maendeleo ya kiuchumi, teknolojia na biashara. Waliahidi kutumia ujuzi wao, maarifa yao na uwezo wao wa kifedha kujenga Mbegani kama ilivyotokea Shenzhen.
Siku ile pia tulishuhudia Mfuko wa Akiba wa Oman wakitiliana saini na China Merchants na Mamlaka yetu ya Uendeshaji wa Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) hati ya makubaliano kujiunga rasmi katika kuwekeza na kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo. Kilichonifurahisha sana siku ile ni kule kuwepo kwa mpango kazi unaotarajia ujenzi wa bandari na ukanda wa maendeleo ya kiuchumi wa Mbegani kuanza tarehe 1 Julai, 2015. Hali kadhalika, nilipokuwa Shenzhen nilipata nafasi ya kutembelea kampuni za teknolojia ya habari na mawasiliano za Huawei na ZTE. Nilifika mjini Jinan, Jimbo la Shandong na kutembelea kampuni nyingine kubwa ya aina hiyo iitwayo INSPUR. Bahati nzuri kampuni zote zimewekeza Tanzania na wanataka kupanua uwekezaji wao.
Nilipokuwa Jinan nilitembelea Hospitali Kuu ya Jimbo la Shandgon, Mjini Jinan, ambayo imetoa madakatari wengi na kupata nafasi ya kuwashakuru viongozi wa Jinan na Jimbo la Shandong kwa kutuletea madakatari na wataalamu wengine wa afya kuja kufanya kazi nchini Tanzania. Vile vile, nimewashukuru kwa mchango wao muhimu uliotuwezesha kupata hospitali ya moyo katika Hospitali ya Muhimbili. Pamoja na kuwashukuru niliomba idadi iongezwe kwani mahitaji yapo na watu wanawapenda Madaktari wa China. Yapo mambo mengi mazuri yaliyofanyika katika ziara yangu nchini China ambayo tutakesha kama tutahitaji kuyafafanua moja baada ya jingine. Hata hivyo, napenda kuyazungumzia mambo mawili. Kwanza ni taarifa aliyonipa Rais Xi Jinping kwamba wanaongeza ufadhili wa masomo kwa kutupa nafasi 100 zaidi kwa vijana wa Tanzania kusoma China kwa kipindi cha miaka mitano. Pia wamekubali kutusaidia ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA) cha Mkoa wa Kagera. Aidha, wamekubali ombi langu la kuongeza idadi ya madaktari na wataalamu wa afya kutoka China kuja kufanya kazi nchini.
Ziara Vietnam
Ndugu Wananchi;
Baada ya kumaliza ziara yangu China nilitembelea Vietnam kwa siku mbili. Huko nako nilikwenda kuimarisha na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu, na kujifunza zaidi kutoka kwa wenzetu ambao wamepata mafanikio makubwa kiuchumi katika kilimo na viwanda kwa kipindi kifupi. Hii ni nchi ambayo tulianza nayo mageuzi ya kiuchumi wakati mmoja mwaka 1986. Wenzetu wameweza kupata mafanikio makubwa katika kilimo, viwanda, ufugaji wa samaki na mengine mengi. Kwa upande wa teknolojia ya mawasiliano ya simu, wanayo kampuni ya Viettel ambayo imekuwa kubwa duniani na inakusudia kuwekeza nchini.
Kwa kweli mafanikio ambayo Vietnam imepata tangu mwaka 1986 yanatupa matumaini kwamba na sisi Tanzania tunaweza kufanikiwa kama wao. Hatuna budi kujipanga vizuri. Tumekubaliana kushirikiana zaidi hasa kubadilishana uzoefu na maarifa katika kilimo na viwanda.
Ugonjwa wa Ebola
Ndugu Wananchi;
Jambo la pili ninalotaka kulizungumzia, si mara yangu ya kwanza kufanya hivyo. Hili si jingine bali ni tahadhari juu ya maradhi ya Ebola yaliyoanzia huko Afrika Magharibi katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea. Baadae yalifika Nigeria, Senegal, Mali, Marekani, Spain na Uingereza. Inakadiriwa kuwa ugonjwa huu hatari umekwishaua watu 4,960 na wengine 13,567 wameambukizwa toka ulipoanza hadi sasa. Ugonjwa huu umeendelea kuwa tishio la dunia kutokana na kasi kubwa ya kuenea kwake. Lakini hasa kwamba asilimia 70 mpaka 90 wanaoupata ugonjwa huu hupoteza maisha. Bahati mbaya hauna dawa wala kinga. Bado wataalamu wa dawa wanachuna bongo.
Taarifa njema ni kuwa ugonjwa huu haujaingia nchini Tanzania. Hata hivyo, hii haiondoi ukweli kuwa unaweza kufika kwani watu wanatembea kutoka nchi zenye maradhi haya na kuja nchini kwetu. Hapa jirani na sisi upo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Sitashangaa pia kwamba wapo Watanzania wanaokwenda nchi zenye maambukizi makubwa hata wakati huu. Watu hao wana hatari kubwa ya kupata maambukizi.
Narudia kukumbusha umuhimu wa kuchukua tahadhari kitaifa na kila mtu anayeishi hapa nchini. Sisi Serikalini tunaendelea kuchukua hatua stahiki na kuimarisha jitihada na hatua za kuwachunguza wageni katika mipaka yetu ya usafiri wa nchi kavu na usafiri wa anga. Tumejiandaa vya kutosha kutambua watu wenye joto kubwa zaidi ya joto la kawaida la mwili wa mwanadamu. Hali kadhalika, tumewataka watu wanaoingia nchini kueleza kama katika wiki tatu zilizopita wametembelea nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia. Nia ya kutaka waseme siyo kuwazuia wasiingie nchini bali kuwapa ushauri juu ya dalili za ugonjwa wa Ebola na nini wafanye iwapo dalili hizo zitawatokea. Pia tunapenda kujua mahala watakapofikia ili tuweze kuwafuatilia.
Ndugu Wananchi;
Ninawaomba ushirikiano wa kila mmoja wenu kutoa taarifa kwa wakati mara mtakapoona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo ambazo ni homa kali ya ghafla, kutokwa na damu mwilini, kutapika na kuharisha kwa wakati mmoja. Toeni taarifa ili wataalamu wenye ujuzi na vifaa stahili vya kujikinga waweze kuja kuwahudumia ipasavyo wagonjwa wenye dalili hizo. Jiepusheni na kumsogelea au kugusana na mtu wa aina hiyo. Na, maiti aliyekufa kutokana na ugonjwa wenye dalili hizo pia asiguswe. Kufanya hivyo ni kujiweka kwenye hatari ya moja kwa moja ya kuambukizwa kwani huenda mtu huyo ni muathirika wa Ebola. Toa taarifa upate maelekezo ya kitaalamu.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Ndugu Wananchi;
Kama mnavyofahamu tarehe 14 Desemba, 2014 tutafanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ngazi ya vitongoji, mitaa na vijiji. Tumelazimika kufanya Uchaguzi huo mwezi Desemba, 2014 badala ya mwezi Oktoba kama ilivyostahili kutokana na shughuli za Bunge Maalum la Katiba kuendelea hadi tarehe 4 Oktoba, 2014 kwa kupitisha Katiba Inayopendekezwa. Kutokana na Taifa kuwa katika jambo lile kubwa ilionekana ni busara kuacha kwanza mchakato ule ukamilike kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Nimeambiwa na TAMISEMI kwamba maandalizi ya uchaguzi huo yanakwenda vizuri na kwamba ratiba imekwishatolewa, na majina ya mitaa, vijiji na vitongoji vipya nayo yamekwishatolewa. Kazi ya kuandikisha wapiga kura itafanyika kuanzia tarehe 23 Novemba, 2014 na itamalizika kwa orodha ya wapiga kura kubandikwa mahali pa wazi hasa kwenye mbao za matangazo katika vitongoji, mitaa, na vijiji husika ifikapo tarehe 30 Novemba, 2014. Kufanya hivyo kutawezesha wananchi kukagua orodha hiyo kuona kama majina yao yapo, na kujiridhisha kuwa majina ya wale walioandikishwa kwenye daftari hilo ni wapiga kura wenye sifa stahiki za kupiga kura katika uchaguzi huo katika eneo husika. Nawasihi wananchi wote mjitokeze kwa wingi kujiandikisha na kukagua orodha ya wapiga kura itakapobandikwa ili kufanikisha zoezi hilo.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi vyama vya siasa vinapaswa kuwasilisha fomu za wagombea wao kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuanzia tarehe 20 hadi 22 Novemba, 2014. Kwa maana hiyo, wale wenye shauku, nia na sifa za kugombea uongozi katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa, wanapaswa kutega sikio ili kujua ratiba za uchaguzi na uteuzi ndani ya vyama vyao ili wapate fursa ya kuteuliwa kugombea. Napenda kuchukua fursa hii kuwahimiza wananchi wote wakiwa pia vijana na wanawake wasibakie nyuma, wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizo na nyingine katika Uchaguzi Mkuu ujao. Ratiba ya uchaguzi huo iliyotolewa na TAMISEMI inaonyesha kwamba mikutano ya kampeni ya kuwanadi wagombea itafanyika kwa siku 14 kuanzia tarehe 30 Novemba, 2014 hadi tarehe 13 Desemba, 2014 siku moja kabla ya siku ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Ndugu Wananchi;
Mfumo wa utawala wa nchi yetu huanzia katika ngazi ya kitongoji na mtaa kisha kijiji, kata na hatimaye taifa. Kwa hiyo uchaguzi wa vitongoji, mitaa na vijiji ndiyo msingi wa uongozi na utawala wa nchi yetu. Tukipata viongozi wazuri katika ngazi hii ya msingi, tutakuwa tumefanikiwa sana katika kuimarisha utawala bora na kuongeza kasi ya maendeleo yetu. Rai yangu kwenu, wananchi wenzangu ni kuwa mjitokeze kwa wingi wakati wa kampeni kuwasikiliza wagombea wetu wakijieleza, kisha tuwachague wale watu ambao sisi tunaona wanatufaa. Lazima tutambue kuwa ngazi ya vitongoji, mitaa na vijiji ndiyo msingi wa uongozi wa nchi yetu. Tukipata watu wazuri tutakuwa tumejenga msingi imara wa uongozi katika taifa letu.
Watu wote watakaojitokeza kugombea katika ngazi ya vitongoji, mitaa na vijiji vyetu ni watu tunaoishi nao na kwamba tunawafahamu vizuri sana. Hatuna budi kuvitendea haki vijiji, mitaa na vitongoji vyetu kwa kuwachagua viongozi wazuri watakaokuwa chachu ya maendeleo katika maeneo yetu. Tukifanya makosa ya kuchagua watu wasiofaa tuelewe kwamba tutakuwa tumejinyima fursa ya kuwa na viongozi bora kwa kipindi cha miaka 5 ijayo. Pia tunaweza kuzua migogoro na kupunguza kasi ya maendeleo katika maeneo yetu. Tusione haya kuwashawishi watu wazuri wajitokeze kugombea.
Mchakato wa Katiba na Kura ya Maoni
Ndugu wananchi,
Bunge la Katiba lilikamilisha kazi yake ya kutunga Katiba mpya ilipofika tarehe 2 Oktoba, 2014 ambayo ilikuwa siku mbili kabla ya muda uliopangwa wa tarehe 4 Oktoba, 2014. Tarehe 8 Oktoba, 2014, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba aliikabidhi Katiba hiyo kwangu na kwa Rais wa Zanzibar kama yalivyo matakwa ya Kifungu cha 28A(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mara nyingine tena nawapongeza kwa dhati aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel John Sitta, Makamu wake Mhe. Samia Suluhu na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa kazi kubwa na nzuri. Wametupatia Katiba Inayopendekezwa inayojitosheleza kwa kila hali. Nawapongeza pia Makatibu wa Bunge, Sekretarieti yao na wafanya kazi wote. Bunge Maalum la Katiba linastahili pongezi nyingi kwa kazi nzuri waliyofanya na hasa kwa kuikamilisha ndani ya muda wa uliopangwa wa siku 130 tu. Baadhi ya nchi duniani jukumu hili limechukua muda mrefu zaidi ya uliokusudiwa au hata kushindikana.
Tutakuwa wachoyo wa fadhila tusipoipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba na Makamu wake Mheshimiwa Jaji Augustino Ramadhani pamoja na Wajumbe wote wa Tume hiyo. Tunawapongeza kwa kutayarisha Rasimu nzuri ya Katiba ambayo ndiyo iliyoliongoza Bunge Maalum la Katiba kupata Katiba Inayopendekezwa iliyo bora. Kilichobakia ni kuwaachia wananchi kuamua kama wanaitaka Katiba Inayopendekezwa au hapana. Watafanya hivyo kwenye kura ya maoni itakayofanyika kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Sheria ya Kura ya Maoni iliyotungwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Ndugu wananchi,
Miaka ya nyuma kulikuwa na tangazo la sabuni ya Omo lililokuwa likisema “Uzuri wa Ngoma Sharti Uicheze”. Uzuri wa Katiba Inayopendekezwa siyo wa kuambiwa. Unahitaji uione, uisome na uielewe. Imeandikwa kwa Kiswahili rahisi na fasaha. Inasomeka na kueleweka kwa urahisi sana. Ni rai yangu kwamba wananchi wote muipate nakala ya Katiba Inayopendekezwa na mjisomee. Sheria imeniagiza kuichapisha Katiba hiyo kwenye gazeti la Serikali ndani ya siku saba baada ya kukabidhiwa. Nimekwisha kufanya hivyo. Aidha, Sheria inaeleza kwamba Katiba Inayopendekezwa isambazwe kwenye magazeti ya kawaida ndani ya siku 14. Zoezi hili ni endelevu. Usambazaji wa Katiba Inayopendekezwa unaendelea na utaendelea mpaka Kura ya Maoni itakapopigwa.
Wito wangu kwenu Watanzania wenzangu ni kwamba msikubali kulaghaiwa na maneno ya wale wachache wanaotaka kuturudisha nyuma na kutunyima fursa ya kupata Katiba iliyo bora zaidi. Maana hapajawahi kutokea ushiriki mpana kama huu katika kutengeneza Katiba katika nchi yetu. Pengine, hata kwingineko duniani si wengi wametoa fursa kama tulivyofanya sisi.
Kura ya Maoni
Ndugu wananchi,
Sheria ya Kura ya Maoni iliniagiza kutangaza tarehe ya Kura ya Maoni katika Gazeti la Serikali ndani ya siku 14 baada ya kupokea Katiba Inayopendekezwa. Nimefanya hivyo. Awali Sheria hiyo iliagiza Kura ya Maoni ifanyike na matokeo yake yajulikane ndani ya siku 70. Waziri mwenye dhamana ya Uchaguzi alipowauliza viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuhusu utekelezaji wa matakwa hayo ya Sheria, Tume ilisema isingweza kuendesha Kura ya Maoni ndani ya muda huo. Mambo yanayojitajika ni mengi mno ambayo hayawezi kukamilika katika muda huo. Wakaomba wapewe muda zaidi. Bahati nzuri Kifungu 51 cha Sheria ya Kura ya Maoni kimetoa mamlaka kwa Waziri mwenye dhamana ya Uchaguzi baada ya kushauriana na Waziri anayehusika na Uchaguzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kubadilisha masharti haya kama kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.
Baada ya mashauriano hayo, Mawaziri wenye dhamana ya uchaguzi wa pande zetu mbili za Muungano waliridhika kuwa upo umuhimu wa kusogeza mbele muda ili kutoa fursa kwa Tume kukamilisha taratibu inazowajibika kufanya. Hayo ni pamoja na kuboresha Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, matayarisho ya upigaji wa Kura ya Maoni na mambo mengine kadhaa. Hivyo basi, tarehe 03 Oktoba, 2014, Waziri mwenye dhamana ambaye ni Waziri Mkuu kwa kutumia mamlaka aliyopewa ya Kifungu cha 51 cha Sheria ya Kura ya Maoni, alitangaza kupitia gazeti la Serikali kubadilisha sharti la siku 70 na kuacha Rais aamue siku ya kupiga kura. Kwa sababu ya mabadilikio hayo, tarehe 10 Oktoba, 2014 nilitangaza kupitia Gazeti la Serikali kuwa Kura ya Maoni itakuwa tarehe 30 Aprili, 2015 ili kutoa fursa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kukamilisha taratibu zake. Katika tangazo hilo pia, nilielekeza kuwa kampeni zitaanza tarehe 30 Machi na kuisha tarehe 29 Aprili, 2014 siku moja kabla ya siku ya kupiga kura, kama ilivyo desturi yetu katika upigaji kura hapa nchini.
Ndugu Wananchi;
Natambua kuwepo dhana kuwa siku za kampeni ni 60. La hasha! Siku za Kampeni zinaamuliwa na Rais, kufuatia Kifungu cha 4 (2) b kisemacho: “Amri kwa ajili ya kura ya maoni itakuwa kama ilivyo kwenye fomu iliyotajwa kwenye jedwali la Sheria hii, na itaainisha:
(a) Katiba Inayopendekezwa kuandikwa;
(b) Kipindi ambacho kampeni kwa ajili ya Kura ya Maoni itafanyika;
(c) Kipindi ambacho Kura ya Maoni itafanyika”
Tume ya Uchaguzi ina mamlaka ya kuruhusu vyama vya kijamii na vya kiraia kutoa elimu ya umma ndani ya siku 60 kabla ya siku ya Kura ya Maoni. Tume imepewa mamlaka hayo na Kifungu cha 5 (4) cha Sheria ya Kura ya Maoni. Kwa sababu hiyo, nawaomba Watanzania wenzangu tuzingatie matakwa ya Sheria ya Maoni ambayo imeelekeza vizuri kuhusu lini Kura ya Maoni itafanyika na lini wadau watoe elimu kwa umma. Naomba tuwe na subira mpaka hapo Tume ya Uchaguzi itakapotoa maelekezo ya utekelezaji wa fursa husika kwa wadau.
Ndugu wananchi,
Ni matarajio yangu kwamba wananchi wote mtajitokeza kwa wingi kwenda kuboresha taarifa zenu kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kama itakavyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na hatimaye itakapofika tarehe 30 Aprili, 2015 mtakwenda kwa wingi kupiga kura ya kuamua kuhusu hatma ya Katiba Inayopendekezwa. Naomba mfanye uamuzi mzuri. Fursa hii ni adhimu na ya kihistoria ambayo tukiipoteza huenda itachukua miaka mingi kuipata tena. Mtakapokuwa mnakwenda kupiga kura zingatieni maslahi yenu pamoja na ya watoto na wajukuu zenu, maana Katiba ndiyo inayoweka misingi na mstakabali wa taifa letu sasa na karne nyingine zijazo.
Hitimisho
Ndugu Watanzania wenzangu,
Naomba nimalizie kwa kuwasihi mjitokeze kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 14 Desemba, 2014. Endeleeni kusoma Katiba Inayopendekezwa ili muda utakapofika kila mtu atoe uamuzi stahiki na wenye maslahi kwa nchi yetu. Nimezitaka Wizara na Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa makubaliano yetu na Serikali ya China na Vietnam kuchukua hatua za ufuataliaji na wanipe taarifa. Narudia kutoa wito tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola. Nawaomba muendelee kuiunga mkono Serikali yetu katika jitihada zake za kuiletea maendeleo nchi yetu na watu wake.
Mwisho, ingawa siyo kwa umuhimu, vijana wetu 297,488 wameanza mtihani wa taifa wa kidato cha nne jana tarehe 3 Novemba, 2014. Tuna imani wamejiandaa vya kutosha na wameandaliwa vyema na walimu, wazazi na walezi wao kwa ajili ya mtihani huo. Naungana na walimu, wazazi, walezi na Watanzania wote kuwatakia kila la heri katika mtihani wao huo.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Ahsanteni Sana kwa kunisikiliza!

- Nov 03, 2014
SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DURING THE OPENING OF THE 12TH SAFAC ANNUAL GENERAL MEETING, MALAIKA BEAC...
Soma zaidiHotuba
Hon. George Mkuchika, Minister of State President’s Office (Good Governance);
Hon. Engineer Evarist Ndikillo, Regional Commissioner – Mwanza;
Dr. Edward Hoseah, Director General of PCCB and Chairperson of SAFAC;
Mr. Ekwabi Mujungu, Secretary General of SAFAC;
Heads of Anti Corruption Agencies from the SADC Region;
Distinguished Participants;
Hon. William Ngeleja, Chairman of the Parliamentary Standing
Committee on Constitutional Affairs, Justice and Administration;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen;
Good Morning,
It is a pleasure for me to welcome you all to Tanzania and to Mwanza in particular. I thank Dr. Edward Hoseah, the Director General of Tanzania’s Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) and Chairman of Southern Africa Forum for Anti-Corruption (SAFAC) together with the SAFAC Secretariat for inviting me to officiate at the opening ceremony of your 12th Annual General Meeting. I also thank you for choosing Tanzania to play host to this year’s meeting. Thank you for the honour you have reposed in us.
I am informed that this meeting has been convened to address two overarching issues in the fight against corruption as enshrined in the theme of this meeting: “Strengthening Asset Recovery, Forfeiture and Corruption Prevention Mechanisms in the SADC Region”. I commend this initiative whose time has come, and whose realization will go a long way towards reduction of corrupt practices in our respective countries and in the region as a whole. You have also intimated the need for hastening formation of SADC Anti-Corruption Committee as part of your agenda. This is highly welcome and let me assure you of my personal support and that of our country. Certainly, SADC needs such a Committee.
Defining the Problem and Action
Ladies and Gentlemen;
Fighting corruption is the right thing for us to do. Also, it is the kind of fight that we must win. Losing is not an option. Its consequences are too ghastly to contemplate. Simply, it is an imperative to fight this war and win. Left unchecked corruption has dire consequences.
Corruption can erode the moral fabric of politics and public service resulting into people losing confidence and trust in politicians, civil servants and the government at large. Corruption, therefore, puts the legitimacy of governments at stake. This is something awful. Corruption undermines the administration of justice and delivery of government services. It erodes the moral fabric of society where people with the money can buy their way on anything even what they are not supposed to get. In a society bedeviled by corruption the poor get hurt disproportionately. Their basic rights as citizens and human beings are denied or trampled upon simply because they cannot afford to make illicit payment. It divides society and people into categories of the have and the have-nots which is not healthy and terribly dangerous.
Corruption undermines economic growth and development. It causes investments and trade to shy away from the country. Development assistance becomes difficult to get because of the fear that the money they contribute will not benefit the intended persons but line the pockets and fill the pot bellies of corrupt government officials and corrupt elements in the private sector. There may be no value for money on work done or service delivered. Something substandard or even nothing at all would be done and money would be paid, because of connivance between corrupt officials and corrupt contractors. Corruption makes many people live a life of misery and depravation while a small group of corrupt individuals live a life of plenty, splendor and luxury at their expense. This has to be stopped. It cannot be left to go for long, for it will create social strife. Nobody should be left to suffer because of some corrupt people. In the same vein, nobody should be allowed to live a life of luxury and splendor through corrupt practices. Nobody should be left to tarnish the image of the government, its institutions or the good name of the country because of his or her greed and corrupt practices.
The scourge of corruption must be stopped. This can happen through first and foremost getting public and private officials who are of high integrity. People who whatever the circumstances they will not indulge in corrupt practices. We need to put in place mechanisms and measures which will discourage and prevent the weak hearted from indulging in corrupt practices or being tempted to do so. We must also sensitize the general public to hate corruption and the people who perpetrate this heinous crime. They should refuse to pay corrupt officials even when coerced to do so. They should refuse to pay bribes and refuse to keep silent about it. They should go further and be ready to name them to the responsible authorities for action to be taken. Over and above that there should be laws that will be effective enough to plug the loopholes and severely publish the offenders. Laws that will prevent corruption from happening, and met out punishment discourage those who have been punished to do it again and others fear joining the fray.
The fight against corruption needs champions to spearhead and lead the fight against it. We need strong institutions of the state to undertake this task. We need strong anti-corruption institutions to lead the fight. But these institutions must have adequate investigative capacity and sufficient mandate to apprehend and take to courts of law the suspected offenders. Equally, important there must be people who are ready to volunteer information about corrupt practices they know and the people involved. The anti-corruption institutions must have officers with integrity and moral authority to enable them deal with corruption cases without any inhibitions. To compliment these efforts there is need for the justice system to be corruption free.
Where and when all these elements are available it is possible to fight the war on corruption successfully. However, it should be noted that, it is not possible to have a society that is completely free of corruption. The practice has been there from time immemorial even the Holy Scriptures have talked about this scourge. There is corruption in big and small nations and in rich and poor nations alike. However, developing nations suffer comparatively more because of weak polities and weak institutions of governance including those involved in the fight against corruption. Therefore, developing nations need to do more to make up for their inherent weaknesses.
Action is Being Taken
Ladies and Gentlemen;
It is encouraging to note that, in the whole of the SADC region, there is awareness about the evils of corruption and serious efforts are being made to fight the scourge. Each country has an anti-corruption law and an anti-corruption institution as evidenced by this gathering today. Progress is being registered although it differs from one country to another.
As we acknowledge and commend the actions being taken, we must be cognizant of the work ahead of us. In all our nations corruption remains a big problem which calls for more robust action. It also needs cooperation among countries, particularly the anti-corruption institutions. They need to share intelligence and information and develop modalities of cooperation, for example, on matters like training and joint action especially with regard to cross boarder corruption crimes.
The formation of the Southern African Anti-Corruption Forum is the right thing to do and habit of holding annual meeting serves the purpose very well. At this juncture, let me re-state that I fully support the proposal of establishing a SADC Anti-Corruption Committee. It will certainly go a long way towards complementing your efforts and strengthening the fight against corruption in our region.
The Global Challenge
Ladies and Gentlemen;
The transnational nature of Corruption is not a problem limited to the SADC region alone. Not at all. As a matter of fact, it is one of the biggest challenges facing Africa and the world we live in. We are told that Africa alone, politically exposed persons (PEPs) sustain the continent a loss of between 20 – 40 billion USD, which are starched abroad by corrupt means. This is not good news at all. That amount of resources can make an enormous impact to the economic wellbeing of our people if invested in the continent. The international frameworks of cooperation such as the SADC protocol Against Corruption, the Africa Union Convention on Prevention and Combating Corruption and the United Nations Convention Against Corruption (UNCAC) are key instruments in ensuring cooperation among states to address this problem.
The theme of this meeting is therefore timely in ensuring that we set up mechanisms and processes for ensuring that the economic loss to our region and the continent in particular is checked. As much as we have moved from reactionary mechanisms of apprehending and punishing the corrupt to a more proactive role of “Prevention and Combating” corruption, there is also need for being proactive in the otherwise equally important role of prevention of economic losses that are caused by corruption.
In this score let me underline the importance of taking stock of legal processes for plugging holes in order to mitigate the economic losses that are sustained through corruption. Efficient oversight measures in public procurement and payment systems are such means, which if properly managed can be very effective in addressing the economic losses. Diligent execution of Anti Money Laundering Mechanisms is yet another instrument to be used. These mechanisms alone may go a long way towards instilling perfection and tidiness in our financial systems. Furthermore, assurance of level playing field in all our economic spheres will add a lot of value. I am one of those staunch believers in the efficacy of leveraging information and communication technology in conducting government business. E-Government will minimize people’s contact with public officials, hence reducing the temptation of asking and paying bribes. Similarly, e-finance instills law help in the fight against theft and corruption. It transparency a big disincentive to stealing and bribery. Erstwhile, people effecting financial transactions using cash from their pockets are susceptible to bribery and create a favourable ground for corruption. We need, therefore, to put our houses in order, with a view to scaring away corrupt conduct.
The Tanzanian Experience
Ladies and Gentlemen;
The history of Tanzania’s fight against corruption has come a long way. The existence of the problem of corruption was acknowledged very early on before and after independence. It is for this reason that the fight against corruption was one of the key elements in the creed of the independence movement and it has remained an important guide to it this day: It says I quote: “Corruption is an enemy of justice, I shall not give or receive a bribe”. It is the spirit of this creed which has guided our anti-corruption efforts since independence to this day.
Solid legal frameworks for preventing, apprehending and punishing the corrupt were put in place from time to time depending on the needs of the time. But, more serious action was taken in 1971 the Prevention of Corruption Act of 1971 was enacted. This legislation was the first attempt to introduce more robust measures to fight corruption in the country after previous measures proved inadequate. As a result an institutional framework for the fight against corruption was established. Hence the Prevention of Corruption Bureau (PCB) was established. Amendments were made in 1991 to the Law which increased the mandate of the institution from that of apprehending and punishing the corrupt to the prevention of corruption.
Eventually, beginning year 2006 efforts were put in place with the aim of undertaking a comprehensive overhaul of the whole legal regime. This was done in order to have a legislation which will usher in holistic approach to the problem. Subsequently, in 2008 we enacted a new legislation which was comprehensive and gave birth to the PCCB in its present force, is a much stronger institution with more powers and greater operational certitude. Thanks to the architects of the process, some of whom are with you today.
The new legislation on Prevention and Combating of Corruption (PCCA), the Anti Money Laundering and the Proceeds of Crime Act, 1991 provide answers to many challenges in the fight against corruption. The legislations and actions taken to implement them speaks volumes about the resolve of the Government to intensify the fight and ensure that the corrupt are punished and no one is left to enjoy the ill-gotten proceeds of criminal activities.
I am aware that many of the countries represented here have taken more or less a similar path, because we are parties to international instruments on corruption. Some of you are members of the Commonwealth fraternity, which in recent years has taken a number of initiatives in combating corruption in particular, and transnational crime in general. Yet, we ought to do more so that we can achieve more. I believe through local action and regional collaboration and sharing of experience, information and intelligence on combating corruption, we shall do better and achieve more. I say so, knowing that at times, the corrupt or their actions transcend national boundaries and their proceeds are kept or invested in other countries in the region and beyond.
Ethics as a drive on the war against corruption:
Ladies and Gentlemen;
In addressing corruption, we need to put in place solid institutional frameworks for championing ethics, since corruption is more or less a consequence of a weak ethics foundation. The PCCB’s success is grounded not only on a strong legislative framework and its National Anti Corruption Strategic Plan, but also on a strong national policy framework and legislations on ethics. In fact the ethics oversight mechanisms such as the law establishing the National Ethics Committee and the Election Expenses Act, 2010 feed into the anti-corruption drive spearheaded by the PCCB. The legislations and mechanisms are so intertwined that they are inseparable. Recently Constituent Assembly saw the merit and wisdom of bolstering Anti-corruption endeavours and recognizing the need of creating stronger institutions to fight corruption and enforce national ethics. We hope the proposed Constitution will be passed because the PCCB will enjoy a Constitutional clout and muscle to fight corruption.
As alluded to earlier, the success of the PCCB in fulfilling its mandate is related to work of other institutions such as the National Audit Office, the Public Procurement Authority, the Tanzania Revenue Authority, the National Ethics Committee, the Commission of Human Rights and Good Governance, the National Elections Bodies and the Judiciary. In their own ways, depending on each institution’s mandate, they are the eyes, ears, nose and the hand in the fight against corruption. Each one of them has a role to play in ensuring that our society does not let loose the scourge of corruption to reign.
Conclusion
Ladies and Gentlemen;
I am confident that, by the end of the three day meeting, you will have shared experiences on how to improve your efforts in the fight against corruption in our region especially in the area of Asset Tracing and Recovery. We are putting a lot of hope and expectations on the outcome of this meeting. Your deliberations will provide us with yet another opportunity to gain more mileage in our noble fight and just war against corruption.
That being said, it is now my singular honor and pleasure to declare that the 12th SAFAC Annual General Meeting opened. I thank you for you kind attention. KARIBU MWANZA and KARIBU TANZANIA.

- Oct 30, 2014
HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA TUME YA UTUMISHI WA...
Soma zaidiHotuba
Mhe. Celina Kombani (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma;
Waheshimiwa Mawaziri;
Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi;
Bibi Claudia Mpangala, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma;
Makatibu Wakuu wa Wizara;
Mhe. Dkt. Didas Massaburi, Meya wa Jiji la Da r es Salaam;
Makatibu Tawala wa Mikoa;
Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Idara Zinazojitegemea na Wakala wa Serikali;
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nimefurahi kualikwa kuja kushiriki katika ufunguzi wa Kongamano la kuadhimisha miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma tangu ilipoanzishwa tarehe 7 Januari, 2004. Imekuwa ni miaka 10 ya mafanikio na mafunzo mengi ambayo tunajivunia hii leo. Hivyo basi leo ni siku ya kujipongeza kwa mafanikio tuliyoyapata, kujifunza kutokana na uzoefu tulioupitia, na kujiandaa kufanya vizuri zaidi na hivyo kupata mafanikio makubwa zaidi miaka 10 na zaidi ijayo mbele yetu.
Nawapongeza Tume ya Utumishi kwa maandalizi mazuri ya kongamano hili. Maadhimisho haya yanatoa fursa kwa wananchi na watumishi wa umma kupata kufahamu kazi zenu mnazofanya, na muhimu zaidi mchango wenu katika kuboresha utumishi wa umma, ambao ndio nyenzo ya serikali ya utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria na kisera. Kwa kweli hatuwezi kuzungumzia maendeleo au uboreshaji wa huduma za jamii bila ya kuwa na utumishi wa umma unaozingatia weledi, uwajibikaji, nidhamu na uadilifu. Yote haya manne, yanasimamiwa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Ndugu Washiriki;
Nimeambiwa katika Kongamano hili mada tatu zitatolewa. Mada ya kwanza itahusu Chimbuko la Tume ya Utumishi wa Umma (kuanzia mwaka 1955 hadi 2004), mada ya pili itahusu uzoefu, mafanikio na changamoto katika kipindi cha miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma (kuanzia mwaka 2004 hadi 2014) na mada ya tatu, itahusu matarajio ya Tume katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Ndugu Washiriki;
Kongamano hili linafanyika wakati ambako kumekuwepo na mafanikio yanayoonekana katika utumishi wa umma. Hata hivyo yapo pia, manung’uniko kuhusu watumishi wa umma kutoka kwa wananchi, vyombo vya habari, sekta binafsi na hata viongozi wa kisiasa. Wengi wa hawa wameonesha kukwazika na vitendo vya baadhi ya watumishi wa umma wachache wenye mienendo isiyoendana na matarajio yetu juu ya sifa na hadhi ya mtumishi wa umma. Wapo wanaotuhumiwa kutumia vibaya nyadhifa zao, kudai na kupokea rushwa, uzembe na kauli na wajihi usioridhisha. Vitendo hivi vya wachache vinatia dosari taswira na imani ya wananchi na wadau kwa utumishi wa umma.
Wakati mwingine inashangaza na kushtua zaidi kuwa hata watumishi wa umma wenyewe nao huulalamikia utumishi wa umma, ambao wao wenyewe ni sehemu yake. Watumishi wa umma wa ngazi za chini wananung’unikia viongozi wao na wakuu wa sehemu zao za kazi kwa kutowatendea haki. Wamekuwa wanapindisha taratibu, kanuni na sheria za utumishi wa umma. Yapo malalamiko kuhusu kutopandishwa vyeo kwa wakati, kutotolewa kwa fursa za mafunzo, au kuwepo kwa upendeleo, unyanyasaji wa kijinsia, na kutolewa kwa adhabu zisizofuata kanuni za adhabu. Wapo wakubwa ambao kauli zao, matakwa yao na mapenzi yao huwa ni sheria, tena juu ya zile zilizoainishwa kwenye kanuni za utumishi (standing orders). Mengi ya malalamiko hayo hunifikia kwa njia ya rufaa za watumishi kupitia Tume hii.
Ndugu Washiriki;
Manung’uniko haya na minong’ono hii siyo ya kupuuza hata kidogo, kwani kuendelea kwake kunapunguza imani na taswira ya utumishi wa umma katika jamii. Jambo hili ni baya. Hatutarajii watumishi wa umma, na hasa viongozi kuwa malaika. La hasha! Hata hivyo, hatutazamii wawe ni watu ambao jamii haina imani nao. Kwa sababu hiyo ni matarajio ya wananchi na wadau ni kuwa pale watumishi wa umma wanapokosea, hatua ziwe zinachukuliwa na mamlaka zao za nidhamu. Kwa yale makosa yenye kustahili adhabu za kiutawala, na pale inapoonekana inabidi, hatua za kisheria zichukuliwe ifanyike hivyo. Ni vyema pia adhabu zizingatie sheria, kanuni na taratibu na si utashi wa kiongozi. Kufanya hivyo kutaepusha si tu manung’uniko bali pia itaokoa fedha za serikali tunazolazimika kuwalipa kama fidia kwa wale wanaoathirika na maamuzi yasiyozingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Kwa minajili hiyo, Serikali ikaunda Tume ya Utumishi wa Umma kupitia Sheria Namba 8 ya mwaka 2002 na kuipa majukumu ya:-
(a) Kupokea na kushughulikia rufaa na malalamiko ya watumishi wa umma;
(b) Kufanya ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu katika usimamizi wa rasilimali watu;
(c) Kushughulikia masuala ya nidhamu kwa walimu kupitia Idara yake ya Utumsihi wa Walimu.
Aidha, kwa kutambua unyeti na umuhimu wake, Tume ikapewa uhuru wa utekelezaji wa majukumu yake ikiongozwa na Mwenyekiti na Makamishna ambao wanateuliwa na Rais, miongoni mwa watumishi wa umma wastaafu wenye uzoefu wa kutosha na uadilifu usiotiliwa shaka.
Ndugu Washiriki;
Katika miaka 10 ya uhai wake, Serikali imeonyesha dhamira ya dhati ya kuimarisha Tume na kuiwezesha kibajeti, vitendea kazi na rasilimali watu ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Tumeongeza bajeti ya Tume kutoka shilingi bilioni 4.88 Mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 118 mwaka 2014/2015. Aidha, Tume imepokea na kusikiliza rufaa 926 za watumishi na malalamiko 108 katika kipindi cha miaka 10. Imefanya ziara za ukaguzi kwenye taasisi 257 kati ya 425, kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi 4,284 ambapo 1,933 sawa na asilimia 45 walifukuzwa kazi. Mafanikio hayo yamefanya nchi nyingine za Afrika kuja hapa nchini kujifunza kutoka kwetu.
Changamoto kwa Tume
Ndugu washiriki;
Tume imekabidhiwa jukumu zito na dhima kubwa sana ya ulezi wa utumishi wa umma. Wananchi na wadau wengine wakiwemo watumishi wa umma wanayo matarajio makubwa sana juu yenu. Wananchi na wadau wanatarajia mtasimamia vizuri utumishi wa umma ili wahusika watimize ipasavyo majukumu yao na kuboresha huduma kwa wananchi. Katika kipindi cha miaka 10 tumeshuhudia mlivyojitahidi kutekeleza wajibu wenu huo kwa moyo wenu wote na uadilifu mkubwa. Kumekuwepo na changamoto na ugumu mbalimbali ambao Tume ilikabiliana nayo katika utekelezaji wa majukumu yake. Mmekabiliana nayo vyema kiasi cha kujenga imani kwa watu kuwa mnaweza kufanya vizuri zaidi ya mnavyofanya sasa siku zijazo. Miaka 10 iliyopita imeipatia Tume uzoefu wa kutosha kuiwezesha kufanya vizuri zaidi miaka 10 ijayo.
Matarajio hayo yanakuja na changamoto zake kwa Tume. Ili muendelee kuaminiwa na kutumainiwa, hamna budi kujipanga vizuri ili muweze kuboresha zaidi ufanisi wenu. Mnatarajiwa muendelee kusimamia na kutenda haki tena kwa wakati, maana “haki inayocheleweshwa ni haki inayopokonywa” Jitahidini kushughulikia mashauri yanayoletwa kwenu kwa wakati maana kutokufanya hivyo ni kuwaletea madhila makubwa wale wanaotumikia adhabu wasizostahili huku wakisubiria rufaa zao.
Katika kutenda haki huko, hali kadhalika msichelee kufanya hivyo hata pale ambapo Serikali au kiongozi ndiye mwenye haki dhidi ya mwajiriwa. Wajibu wenu ni kutenda haki kwa pande zote. Aidha, msisite kuchukua hatua na kupendekeza hatua kuchukuliwa dhidi ya wakuu wa kazi wenye kutumia madaraka vibaya kunyanyasa walio chini yao ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia. Leteni kwangu yale mashauri yaliyowazidi kimo, ikiwemo wale wanaokaidi maelekezo ya Tume ili nichukue hatua stahili kwa wale ambao mamlaka yao ya nidhamu inaangukia kwangu.
Utumishi wa umma umepanuka sana katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kutokana na serikali kuajiri wafanyakazi wengi wapya kufidia lile pengo la kutokuajiri kwa miaka 10 wakati wa mageuzi ya kiuchumi. Matokeo yake, leo hii tunao watumishi wengi vijana ndani ya utumishi wa umma. Wengi wa hawa hawafahamu vizuri kazi za Tume, jambo ambalo limesababisha watumishi wengi kutojua njia sahihi ya kushughulikia mashauri yao. Wengine kwa kutofahamu, wamekuwa wakiniandikia mimi moja kwa moja na wengine kuwasilisha malalamiko yao kwenye vyombo vya habari, na hata Bungeni.
Nawatia shime muanze sasa kufikiria mkakati wa kuwafikia watumishi wa umma na kuwaelimisha kuhusu majukumu ya Tume na taratibu rasmi za kuwasilisha mashauri yao. Hii itaepusha tabia inayojengeka sasa ya kupitisha malalamiko ya kiutumishi kwenye njia na mamlaka zisizo sahihi na wakati mwingine kuzaa migogoro isiyokuwa ya lazima.
Tume Miaka 10 Ijayo
Ndugu Washiriki;
Sisi katika Serikali tunayo matumaini na matarajio makubwa kwa Tume ya Utumishi wa Umma katika miaka 10 ijayo. Kama mjuavyo miaka 10 ijayo nchi yetu inatakiwa iwe imepanda daraja kutoka kuwa nchi maskini na kuwa nchi ya uchumi wa kati (ifikapo mwaka 2025). Ili kufikia lengo letu hilo ambalo linaashiria kuwa nchi ya uchumi wa kisasa wa viwanda na sekta ya huduma iliyokubwa na kutoa mchango mkubwa katika katika kuchangia pato la taifa, sekta ndogo ya utumishi wa umma ina mchango maalum. Tena mkubwa na muhimu katika kuwezesha sekta nyingine za uchumi kutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kutekeleza malengo ya Tanzania Development Vision 2025. Hivyo, basi Tume inapaswa kujipanga vyema kuwawezesha watumishi wa umma kutimiza ipasavyo wajibu wao.
Tume ya Utumishi wa Umma iendelee kuhimiza na kusimamia nidhamu, weledi na uadilifu kuliko ambavyo imefanya miaka ya nyuma. Kinachonipa matumaini makubwa ni kuwa wananchi, Tume ya Marekebisho ya Katiba na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba nao wameuona umuhimu huo, kwa kupendekeza Tume ya Utumishi wa Umma sasa kuwemo kwenye Katiba Inayopendekezwa. Nina imani maboresho hayo iwapo yataungwa mkono na wananchi kwa kupitisha Katiba Inayopendekezwa katika kura ya maoni, tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kuwa na utumishi wa umma unaokwenda na wakati.
Sisi katika Serikali tunaahidi kuendelea kuiwezesha Tume kwa fedha, rasilimali watu na vitendea kazi ili iweze kutekeleza kwa ukamilifu, majukumu yake kama inavyotarajiwa na kwa mujibu wa Sheria iliyoiunda.
Hitimisho
Ndugu washiriki;
Mwisho, napenda kuipongeza tena, Tume ya Utumishi wa Umma kwa kazi kubwa na nzuri inayofanya. Pongezi za kipekee ziwaendee Makamishna wa Tume waliopo na wale waliopita katika kuwezesha Tume kupata tunayojivunia leo. Nawapongeza na kuwashukuru Katibu wa Tume na watumishi wote wa Tume kwa kufanya kazi zao kwa moyo umakini na weledi mkubwa. Tunawaomba waendeleze rekodi hii nzuri ya miaka 10 iliyopita katika miaka 10 ijayo. Baada ya kusema hayo, sasa ninayo furaha kutangaza kuwa Kongamano la miaka 10 la Maadhimisho ya Tume ya Utumishi wa Umma limefunguliwa rasmi.
Asanteni kwa kunikiliza!

- Oct 23, 2014
ACCEPTANCE SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, UPON RECEIVING AN HONORARY PROFESSORSHIP FROM THE CHINA AGR...
Soma zaidiHotuba
Excellency Comrade Jiang Peimin, Chairman of the
China Agricultural University Council;
Hon. Comrade Ke Bingsheng, President of China Agricultural University;
Distinguished Council Members;
Distinguished Members of the Convocation;
Distinguished Students;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen;
Introduction
I thank you Comrade Chairman, Comrade President and Members of the Council of the China Agricultural University for having me here and for awarding me Honorary Professorship of this prestigious University. I must admit it was a big surprise when I got the news of the award. I am used to getting Honorary PhD never expected such a big award. All the same, I am very happy and grateful for the recognition and honour. I will always cherish it.
Ladies and Gentlemen;
I accept this award on behalf of the people of the United Republic of Tanzania. Through me, this great University has recognized their collective efforts to transform their country and their lives from underdevelopment to prosperity. This award gives them a sense of satisfaction and optimism that their sweat and toil is being noticed and appreciated. More importantly, they are getting another important partner to buttress their efforts in addressing the challenges of transforming their agriculture and livelihood.
Ladies and Gentlemen;
As it is customary at such occasions, the awardee is expected to say something in accepting the award. I have chosen to speak about agriculture, a subject of particular interest to this University, to the faculty and to students. Specifically, I have decided to share my views on the essence and essentials for transforming agriculture in Africa and Tanzania, in particular.
The Importance of Agriculture
Mr. Chairman;
Ladies and Gentlemen;
Let me hasten to say that one cannot talk of development in Africa without talking about agriculture. For many African countries, agriculture is the lifeline of their economies. The livelihood of two out of every three Africans depends on agriculture. Besides being the source of food, agriculture is the leading foreign exchange earner and a source of raw materials and employment.
In Tanzania, for example, agriculture contributes about 25 percent of GDP; 34 percent of foreign exchange earnings and about 95 percent of food requirements. Agriculture employs 75 percent of the labour force, and is an important source of raw materials for the manufacturing sector.
Given the important role that agriculture plays, particularly that of being source of livelihood to the majority of the people of Africa, no serious discourse about transformation of African economies or poverty reduction can be complete without talking about agriculture.
Indeed, we look to China for good examples and inspiration in agricultural transformation. It is an open secret that China is a success story in increasing economic growth and substantially reducing poverty, with transfromation of agriculture being an important factor. China succeeded to increase agricultural productivity and overall output under the Green Revolution. The success with agriculture have had a multiplier effect in other sectors of the economy, particularly with industrial development.
Problems Facing Agriculture in Africa
Ladies and Gentlemen;
Despite its central role, African agriculture is underdeveloped and characterized by low productivity and low production. For example, maize production in Africa averages 1.8 tons per hectare while in China it is 5.7 tons per hectare. Low productivity is a result of limited application of modern science and technology in crop production and animal husbandry.
This is exemplified by low mechanization and the hand hoe being the dominant farming implement. As a result farm sizes are small and so is the volume of production. The situation is compounded by little use of irrigation and insufficient use of high yielding seeds, fertilizers and other farm inputs. Extension service is inadequate and so are financial services. Rural infrastructure is not well developed and crop marketing is plagued with a lot of inadequencies. Invariably, the buyers and prices they offer to farmers’ produce are not certain.
African agriculture, therefore, needs radical transformation to turn it from backwardness to modernity, from low productivity to high productivity and from subsistence to being commercial. In other words, Africa needs a Green Revolution.
China’s experience has taught us that there is no substitute to the Green Revolution in tackling the problems and challenges constraining the development and advancement of agriculture. I know it is not easy and quite expensive but, there is no better option than this. It confirms the historical path of development of human society that no country has leaped forward without transforming its agriculture.
Boosting Agricultural Production: Transforming Small Scale Farmers
Ladies and Gentlemen;
In pursuit of the desire to transform our agriculture, our government in 2006 launched the Agricultural Sector Development Programme. This is a comprehensive seven year programme designed to tackle the main constraints that impede growth and development of agriculture in our dear country.
Under the ASDP, deliberate efforts are being made to reduce the predominance of rain-fed agriculture and increase irrigation in agriculture. Currently, the proportion of irrigated agriculture in Africa is very minimal. At 5 percent, Africa has the lowest irrigated agriculture on this planet. Asia is at 37 percent and Latin America is at 14 percent of their cultivated area. Tanzania, has 29 million hectares of arable land that can be irrigated of which only 450,000 hectares are being utilized for that purpose.
Indeed, high priority has been given to irrigation. About 60 percent of the financial resources for implementation of the Agricultural Sector Development Programme is set aside for irrigation. The biggest problem has always been the inability of our government to get all the money both from local and external sources. Because of that not all budgeted money is being disbursed by government hence complicating the implementation processes and causing low performance in irrigation.
Comrade Chairman;
It is one of the cardinal objectives of the Agricultural Development Programme to reduce the dominance of and the use of rudimentary farm implements like the hand hoe. The aim is to adopt modern technology and equipment: mechanize our agriculture. Currently, 70 percent of farmers are using the hand hoe, 20 percent are using oxen ploughs and only 10 percent are using tractors. As a result farm sizes are small and, coupled with little use of irrigation, high yielding seeds and fertilizers, productivity and production is low.
To address this problem, mechanization of our agriculture is one of the main objectives of the ASDP. In this regard, the Local Government Authorities and the National Service have been importing tractors and selling them to farmers on credit. We have, also, taken action to remove import duty for most agricultural implements and equipment to encourage the private sector to deal in these important tools. This has turned out to be a good incentive to both the public and private sectors. It has enabled the tripling of the importation and use of tractors in the country, from 5,308 tractors in 2005/06 to 14,668 in 2012/13.
Ladies and Gentlemen;
For the last seven years we have employed more than 4,295 extension workers. They are important cadres to educate farmers on application of new farming methods and techniques as well as on the use of modern inputs and implements. The Government has been working with other stakeholders and on its own to invest in improving agriculture related infrastructure such as big irrigation canals, rural roads, electricity, telecommunications and water supply.
Ladies and Gentlemen;
We have increased the budget to subsidize inputs for small holder farmers’ from TShs. 8.5 billion (5 million USD) in 2005/06 to TShs. 157.8 billion (92.8 million USD) in 2013/14. Close to one million farmers are beneffiting with fertilisers, seeds and pesticides provided under this programme. This way our farmers have been able to increase fertilizer usage from 8.5 kg per hectare in 2005 to 13kg per hectare in 2013. The average for Africa is 8kg per hectare. We want our farmers to use at least 50kg per hectare as per the target set by the Abuja Declaration on Fertilizer for the African Green Revolution. As you know very well even that amount would still be too low by world standards.
Lack of reliable sources and avenues of agricultural financing remains one of the major constrains and a setback to transformation of agriculture in Tanzania and Africa as a whole. Farmers cannot easily access credit to enable them buy farm implements, agricultural inputs and machinery. If we cannot overcome this challenge the Green Revolution will take a long time to happen in Africa. Our experience has taught us that agriculture needs special if not peculiar financing mechanisms or arrangements.
Commercial banks have shown indifference in lending to farmers. They also find it difficult to lend money to buyers of farmer’s crops. That is why it deemed necessary to us to introduce input subsidies to small holder farmers. Because of problems of sustainability we consider the input subsidy programme as an interim measure. For the long term we have decided to establish the Tanzania Agricultural Development Bank, which will exclusively finance agricultural activities. We have been talking to major financial houses in China to explore the possibility of assisting us in this endeavour. We are also encouraging the private sector to establish financing facility to in the country.
Modernizing Agriculture
Ladies and Gentlemen;
The implementation of the ASDP and two other initiatives: the Kilimo Kwanza and SAGCOT which compliment it, has very much improved matters in agriculture.
With Kilimo Kwanza (Agriculture First) initiative we took deliberate measure to involve the private sector in the agriculture value chain. With SAGCOT we also involved both local and international private sector in collaboration with small holder farmers to develop the agricultural potentials of the Southern Agricultural Growth Corridor. There is also the participation of the development partners and civil society. It is worth noting that these initiatives have had positive results. Agriculture productivity and output has been increasing substantially. In 2012/13 food self-sufficiency in the country was at 118 percent and in 2013/14 it is close to 130 percent. Interestingly, we are now facing the challenges related to our successes. There is the problem of market for farmers’ produce and that of inadequate storage facilities.
Indeed, the assumption that the invisible hand called “market” will solve these problems has not worked very well for us. The private sector buyers have not been able to buy all farmers produce at favourable prices. As a result the prices offered are low and not the whole crop is bought. This sad state of affairs demoralizes farmers and keeps them and us under pressure about how to overcome these new challenges. We are now looking for new and innovative ways of addressing crop marketing problems. This compels us to expedite and hasten the process of establishing a Commodity Market Exchange. We are also working on building more warehouse facilities for storing crop. It is important to do so in order to help farmers overcome the problem of post harvest losses.
Research and Development
Ladies and Gentlemen;
Agricultural research is an important factor in the transformation of agriculture. Unfortunately, this is a matter we have not been doing well. In this regard, we have been taking measures to correct past inadequacies and improve the matters. The deliberate action I took to provide funding for research has been a game changer of its own kind. It has enabled our scientists to do research work. The funds have enabled our research institutions to buy new equipment as well as repair and upgrade existing equipment. Many scientists are getting the money to do Masters and PhD studies. I know USD 30 million is not enough but I have set a target of allocating one percent of the national budget to research purposes. We have not been able to meet this objective yet but we are on course to get there. However, as alluded to earlier even at the current levels of funding noticeable progress has been made. The unfreezing of employment has also been useful to our research institutions and future research work. The employment of young scientists is giving new hope and life to agriculture research in Tanzania. With more money being spent on seed multiplication, by government and the private sector researchers are getting motivated even more.
Comrade Chairman;
Let me at this juncture, applaud China University of Agriculture for its determination to support agricultural research in Tanzania through scholarship and research. I understand that you have offered to the Ministry of Education and Vocational Training seven scholarships beginning next academic year. I sincerely thank you for this generous support. The partnership you have entered with the Sokoine University of Agriculture will surely enable researchers from our two institutions of higher learning to work together for our mutual benefits. Your plan to establish demonstration centres in villages around Morogoro will go a long way towards helping the dissemination of your research findings to farmers. This is exactly what we need. This is why universities are there for. I want to assure you that my government is very supportive of this initiative.
Support from China
Ladies and Gentlemen;
We are building a new Agricultural University in Butiama, the birth place of Mwalimu Julius Nyerere to compliment the work done by the Sokoine University of Agriculture. We are looking for partners in this important endeavour. We will highly appreciate your readiness to support and work with us to the full realisation of this noble dream.
Let me conclude by once again thanking you for the honour you have given me and for the support that you are giving to our country in our historic mission and duty to transform Tanzania’s agriculture.
I thank you for your attention!

- Oct 23, 2014
KEYNOTE ADDRESS BY HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE THIRD TANZANIA CHINA INVESTMENT FORUM IN BEIJING,...
Soma zaidiHotuba
Mr. Luo Jun, Deputy Director of Foreign Affairs Office, Guangdong Province;
Your Excellency Mr. Lu Youqing, Ambassador of the Peoples Republic of China in Tanzania;
Mr. Xu Zhiming, Vice Chairman, China Africa Business Council (CABC);
Mr. Wang Xiaoyong, Secretary General, China Africa Business Council (CABC);
Mr. Bai Xiaofeng, Director for International Communications, China; Africa Business Council (CABC);
Members of my delegation from Tanzania;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
Introduction
I am in China for official visit at the invitation of His Excellency President Xi Jinping. The objective is to strengthen the excellent bilateral relations that so happily exist between our countries. It is also an opportunity to promote and deepen our investment and trade relations. This Forum demonstrates our commitment in that respect.
Ladies and Gentlemen;
50 years ago, Tanzania and China did not have such an opportunity to bring together our private sectors in Tanzania-China Business and Investment Forum. At that time, such an undertaking could only be achieved through government to government arrangement. The Forum today speaks for its self about the progress we have made and the transformation that has taken place in both China and Tanzania. It denotes growing relations beyond governments, to relations between private sectors.
Doing Business in Tanzania
Ladies and Gentlemen;
We are gathered here to share views and experiences in terms of investment and business opportunities. Some of you are already involved in various businesses in Tanzania and in China are new comers and would like to explore available investment and trade opportunities in both Tanzania and China. I am here to tell our Chinese friends what Tanzania has to offer and why you should choose Tanzania as the destination for their trade and investment.
Ladies and Gentlemen;
There are eight key attributes which make Tanzania an investment destination of choice for our Chinese friends. First, China and Tanzania have enjoyed warm and friendly bilateral relations for half a century now. Surely, this presents the confidence and assurance that your investments operates in a favourable and friendly environment. Second, Tanzania pursues sound economic policies which have engendered strong macro-economic performance and stability for over two decades now. Tanzania’s economy grew by an annual average of 7 percent in the last decade and is among the 7 fastest growing economies in Africa. Tanzania is the leading FDI’s destination in the East African Community. Inflation is at 6.6 percent and headed to 5 percent by June, 2015.
Third, Tanzania is a peaceful and stable country. Fourth, Tanzania has a friendly business environment underwritten by good investment policy and legislation. We continue to take measure to improve investment climate as and when need arises. Tanzania’s investment environment continues to offer predictable, transparent and strong long-term proposition to investors. Investment is safe against expropriation and one is allowed to repatriate profits and dividends. In terms of investment facilitation, the Tanzania Investment Centre (TIC), Zanzibar Investment Promotion Agency (ZIPA) and Export Processing Zone (EPZA) promote, coordinate and facilitate all investments in Tanzania. These are premier ports of call for investors coming to Tanzania. In particular, TIC is a one stop centre for all investors’ needs. The CEOs of these Institutions are in our midst today. Make a full use of them.
Fifth, Tanzania’s geographic location position makes her as a natural regional business hub. Tanzania borders 8 countries, 6 out of which namely Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi, Zambia and Eastern part of the Democratic Republic of Congo, uses the Dar es Salaam port and Tanzania’s railways and roads for their sea freight. This presents good opportunities for investment in infrastructure development, trade, transport and logistics.
Sixth, Tanzania provides a sizeable market of 48 million people. Being a member of two regional economic groupings, namely the East African Community (EAC) and the Southern African Development Community (SADC), Tanzania provides a market access of close to 400 million people for her investors. Our country also enjoys duty free and quota free access to the US market through AGOA, the European market through the EBA facility as well as with China through FOCAC arrangements, India through Indo-Africa Partnership and Japan through TICAD.
Seventh, is the availability of semi skilled and skilled labour force. As a developing country, Tanzania’s population of about 48 million people is predominantly young, which is a pool of labour seeking for jobs. The country has invested heavily in education at all levels and in training of the skilled labour force.
Eighth and last is the fact that in Tanzania, offers plenty of investment opportunities. There include oil and gas, mining, agribusiness, infrastructure development, manufacturing, health care, tourism, housing, ICT and other services. So far among all TIC registered projects, 31 percent are in manufacturing, 25 percent in tourism, 14 percent real estate and 30 percent are in other sectors including oil and gas exploration.
Ladies and Gentlemen;
The detailed account of available opportunities in oil and gas, mining, agriculture and agribusiness, manufacturing, information and communication technology, power, ports, railways and tourism will be presented by the respective members of my delegation who are here with me.
Ladies and Gentlemen;
It is worth stating here that the seven attributes that I have mentioned, have worked well for us and our investors. Our country has, in recent years, witnessed a phenomenon increase in the flow of FDIs. Investment projects and value of those investments have been on the increase. For example, FDI inflows increased from US$ 150 million in 1995 to US$ 1.8 billion in 2013. Overall investment projects registered by Tanzania Investment Centre (TIC) increased from 178 projects worth US$ 874 million in 2000 to 826 projects worth US$ 7.1 billion in 2011 to 869 projects worth US$ 11.4 billion in 2012.
Confidence in Tanzania’s business environment has further been strengthened by the fact that Tanzania has emerged as the leading East African country in attracting investments and inflows of FDI in recent years. In 2013, for example, Tanzania received US$ 1,872 million, Uganda US$ 1,146 million, Kenya US$ 514 million, Rwanda US$ 111 million and Burundi US$ 7 million. Importantly, in Tanzania FDI inflows were almost fully financed by equity and retained earnings, which signals the confidence of foreign investors in the country's economic prospects.
Chinese Investments in Tanzania
Ladies and Gentlemen;
The Government of Tanzania is pleased that Chinese companies are amongst the top five investors, in terms of value of investments, in Tanzania. Up to the end of December 2013, Tanzania Investment Centre had registered more than 522 Chinese projects worth more than US$ 2,490.21 million. These investments are scheduled to create more than 77,335.28 jobs once all are fully operational. Large inflows were recorded in the manufacturing sector which accounted for 354 out of the 522 projects registered. Although oil and gas projects are the largest source of FDI, manufacturing projects are just as valuable to the country if not more as they have the propensity to generate more jobs.
Ladies and Gentlemen;
I am told that following the 2nd Tanzania-China Business Forum held in Dar es Salaam from 23rd - 25th June 2014 during the visit by His Excellency Li Yuanchao, Chinese Vice President, many business interests were registered by various investors, including 100 Chinese Investors and Businessmen delegates who accompanied the Vice President. This is witnessed by the increase in value of registered projects by Chinese investors from July-September 2014, which reached US$ 533.9 million compared to US$ 124.14 million recorded in July-September 2013. It is my sincere hope that this 3rd Tanzania-China Business Forum will generate even more investment deals.
Ladies and Gentlemen;
It is through increased investments that we can promote more trade between our two countries. Trade volume has been on the increase but we can do more. For example, in 2012/2013, the total trade volume between China and Tanzania was only US$ 3.7 billion of which China's exports to Tanzania were worth US$ 3.1 billion and imports from Tanzania were worth US$ 600 million. We both can do more.
Conclusion
Ladies and Gentlemen;
In conclusion, I would like to emphasize that Tanzania has many investment and trade opportunities and political – economic environment is permissive for Chinese companies to come and invest. I am glad that some Chinese companies have already seen this opportunity and are already doing business with us. I expect more companies to come and join. With the existing cordial relations between our countries, I am sure, working together with Chinese business, we can increase many times the size of investment and the volume of trade. Please, Come one, Come all.
Thank you very much, asanteni sana.

- Oct 22, 2014
OPENING REMARKS BY HIS EXCELLENCY, DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE CNN MULTICHOICE AFRICAN JOURNALIST OF THE YE...
Soma zaidiHotuba
Dr. Fenella Mukangara, Minister for Information, Youth, Culture and Sports,
Ms. Deborah Rayner, CNN SVP International News Gathering,
Mr. Nick Meyer, CEO of the MultiChoice Africa,
Ms. Julieth Kairuki, Executive Director, Tanzania Investment Centre,
Distinguished Judges of the Panel
Award Finalist and Nominees,
Distinguished Guests,
Ladies and Gentlemen
I can’t find words good enough to express our gratitude to CNN and MultiChoice Africa for the honour they have bestowed on our dear country Tanzania of hosting this prestigious event is no small matter. It puts our country on the spotlight in a manner that is in incorporable with a lot of benefits to reap in future. I hope my fellow countrymen and women will take advantage of this event and make full use of it.
2014 CNN Journalist Awards
Ladies and Gentlemen,
I commend CNN and MultiChoice for conceiving the idea of presenting Awards to African journalists who have excelled in perfoming their duties ad functions. In many ways these Awards act as a major incentive for our journalist to observe professionalism, diligence, honesty and integrity. Sometimes these important attributes remain wanting among the practioners of this important profession in respective countries. In many ways these awards encourage our journalists to do better. I am particularly pleased to note that one of our own Mr. Dickson Ng'hilly, from the Guardian Newspaper is among those who have been nominated. I pray that it ends well for Dickson, and if otherwise it still remain a sense of pride for us for him to have come this for.
CNN and Africa
Ladies and Gentlemen,
I commend CNN for the wonderful work they are doing of providing news and information in Africa and the world. By all standards CNN is a global media power house with a big stake in Africa According to the EMS Africa Survey 2014, CNN is the undisputed number one international news brand in Africa and the Middle East reaching larger audience than all direct news competitors in every lucky across the region on TV, Digital and cross platform. The statistics show that, CNN reaches 59 percent of Africa's upscale population every month, 71 percent of key business decision makers in Africa, 79 percent of Opinion Leaders and 10 percent of all the continent’s affluent people who use CNN mobile services every month. I hope these statistics will encourage CNN to consider having Swahili Service program.
Africa and Freedom of Press
Ladies and Gentlemen;
Undoubtedly, there has been a lot of improvement in the state of journalism and freedom of the press across Africa. In many ways this is very much a function and measure of the progress being made in democracy and good governance. I know, there are still countries where press freedom remains a challenge but overall the future looks prospective in Africa as democracy, good governance, rule of law, and respect for human rights are taking roots.
Freedom of Press in Tanzania
Ladies and Gentlemen,
Tanzania takes the freedom of press very dearly. I for one, have done a lot to promote press freedom in the country. I am happy to note that freedom of press continues to take roots in Tanzania as days pass by. Today, we have 29 television stations, 94 radio stations , 825 newspaper and publications compared to one television station, three radio stations, and three newspapers in year 1992. Mind you, the state owns only, one TV station, two newspapers and one radio. For one to read all the daily newspapers, he or she must be required to spend at least between 20 and 30 US dollars per day.
We are committed to do more to enhance freedom in the country. We are going to table before the parliament a Bill on Freedom of Information which will go a long way towards guaranteing access to information by general public and journalists. The purpose is to foster transparency and accountability on the part of government. Challenges notwithstanding, freedom of press and information remains important building block for a healthy democratic society. We will never waver nor renage in pursuit of the same.
A Call to Africa Journalists
Ladies and Gentlemen,
My brothers and sisters in the media please continue to do the good work. My humble appeal to you, be responsible journalists, be ethical, be professional and have integrity. Use the power of the media judiciously to promote unity and harmony. Shy away from promoting disorder and social tensions above all be free of corruption so that you can have the moral authority to point fingers at others.
Once again I thank and commend CNN and Multichoice for affording Tanzania this prestigeous honour. We will always cherish and remember this day.
Thank you for your kind attention.

- Oct 22, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA UFUNGUZI WA KIJIJI CHA SANAA ZA AFRIKA KILICHOPO WILAYA YA SONGZH...
Soma zaidiHotuba
Waheshimiwa Mawaziri…
Professa Li Songshan na Dokta Han Rong, Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika;
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa nchi za Afrika hapa China;
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana;
Shukrani na Pongezi
Ninayo furaha isiyo kifani kuwepo hapa kwenye kijiji cha Sanaa za Afrika. Napenda kuwashukuru Professa Li Songshan na Dokta Han Rong, waanzilishi wa Kijiji hiki kwa kunialika kuja kushiriki katika uzinduzi wake rasmi. Napenda pia kutumia nafasi hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa Profesa Li na Dkt. Han kwa kufanikisha ujenzi wa Kijiji hiki maalum kwa ajili ya Afrika. Mandhari yake nzuri, yenye maudhui na hisia za Kiafrika ni mambo yanayovutia sana.
Napenda vile vile kuwashukuru waheshimiwa Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini China kwa kujumuika nasi hapa siku ya leo katika ufunguzi rasmi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika.
Kuenzi Miaka 50 ya Ushirikiano wa Tanzania na China
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Tukio hili la kufungua kijiji cha Sanaa za Afrika lina umuhimu wa kipekee kwa Tanzania. Kwanza, kwa kuwa muanzilishi wake Profesa Li. Songshan na Dokta Han Rong wageni wakubwa wa Afrika na wameishi muda mrefu Tanzania. Pili, sherehe hizi zinafanyika wakati ambapo Tanzania na China zinasherehekea miaka hamsini (50) tangu kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia. Tunaiona kama ni namna nzuri ya kusherehekea mafanikio haya makubwa.
Katika nusu karne ya uhusiano wa nchi zetu mbili rafiki mambo mengi yanayoonekana na yasiyoonekana yamefanyika. Kati ya yale yatakayokumbukwa milele ni Reli ya TAZARA. Reli hii ambayo ilikuwa ikiitwa ´Reli ya Uhuru´ ilitumika sio tu kuinua uchumi wa nchi za Zambia na Tanzania, lakini ilitumika pia katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika. TAZARA ni kielelezo cha dhamira ya ukweli ya urafiki baina ya China na Afrika. Miradi mingine muhimu ni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kituo cha Tiba ya Maradhi ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, bomba la gesi kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es Salaam. Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema, “…katika dunia hii, tuna marafiki wengi , lakini tuna rafiki mmoja wa kweli, ambaye ni Jamhuri ya Watu wa China…."
Ukweli huu unaendelea kujidhihirisha hadi hii leo ambapo kiuchumi, takwimu za 2013 zinaonesha kuwa, China ni nchi iliyoongoza kuwekeza mitaji na kufanya biashara na Tanzania. Serikali ya Watu wa China imeendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jitihada zetu za kujiletea maendeleo nchini Tanzania.
Mahusiano ya Watu wa China na Tanzania
Wageni waalikwa;
Uhusiano wa Tanzania na China hauonekani tu kwenye vitu bali pia kwa watu wetu. Katika kipindi cha miaka 50 tunajivunia kukua kwa uhusiano wa watu-kwa-watu kati ya nchi hizi mbili. Watu wetu wanashirikiana katika shida na raha, masika na kiangazi, neema na dhiki.
Takwimu zinajieleza vizuri zaidi. Tangu 1968 mpaka 2014, Tanzania imepokea madaktari 1,705 kutoka China (1,055 wakiwa Tanzania Bara, na 650 wakiwa Zanzibar). Kadhalika, katika kipindi cha mwaka 2011 - 2013, zaidi ya wanafunzi 1,600 Wakitanzania wamepata mafunzo katika fani mbalimbali nchini China. Aidha, tunao ushirikiano wa damu kwani kuna Wachina 69 waliofia Tanzania wakati wa kujenga Reli ya TAZARA. Vile vile wapo Wachina wengi wanaoishi na kufanya shughuli za uchumi na biashara nchini Tanzania. Hali kadhalika,wapo Watanzania wengi wanaoishi na kufanya shughuli zao za kujipatia riziki nchini China. Kwetu sisi Tanzania, Wachina sio wageni bali ndugu zetu na sehemu yetu. Tunafurahi kuona kuwa, uhusiano huu wa watu-kwa-watu unaendelea kukua siku hadi siku.
Prof. Li na mke wako Dokta Han;
Kuishi kwenu Tanzania kwa miaka 26 tangu mwaka 1978 na kuamua kurudi nyumbani China na kuanzisha mradi huu wa Kijiji cha Sanaa za Afrika ni ishara ya matunda ya urafiki wa kweli, wa kidugu na wa muda mrefu kati ya watu wa Tanzania na watu wa China. Wewe Profesa Li pamoja na mke wako Dkt. Han ni mfano dhahiri wa Marafiki wa Kweli wa Tanzania. Tunashukuru sana!
Umuhimu wa Kijiji cha Sanaa za Afrika
Wageni waalikwa;
Umuhimu wa Kijiji hiki kwa Tanzania na Afrika ni wa aina yake. Kijiji kinatoa nafasi ya kutangaza sanaa na utamaduni wa watu wa Afrika kama vile lugha, sanaa za mikono na ngoma. Kadhalika kinalenga kutangaza vivutio vya utalii vya Afrika kama fursa za biashara na uwekezaji vya Bara letu. Vile vile kituo hiki kitatumika kufanya majadiliano ya maendeleo kati ya wanazuoni wa Afrika na China. Kijiji hiki sio tu kinatoa nafasi ya kuitangaza Afrika nchini China, lakini pia kinaileta Afrika karibu sana na nchi ya China na watu wake.
Kwa kutambua umuhimu wa kijiji hiki, ningependa kuwahakikishia kwamba, Serikali ya Tanzania inayo dhamira ya dhati ya kushirikiana kwa karibu na uongozi wa kijiji hiki katika kutimiza malengo yake ya kutangaza na kukuza sanaa na utamaduni wa Afrika pamoja na fursa za biashara, uwekezaji na utalii zilizopo Afrika na Tanzania. Vilevile, Serikali yetu iko tayari kushirikiana na Kituo hiki kupata waalimu watakaofundisha lugha ya Kiswahili katika Kijiji hiki.
Tunafurahi kuona kizazi cha sasa na vizazi vijavyo vinaendeleza kijiji hiki ili kikue na kuwa jiji la Afrika ili kuzidi kuenzi na kukuza uhusiano mzuri uliopo baina ya China, Tanzania na Afrika kwa ujumla wake katika nyanja za uchumi, utamaduni na kijamii.
Hitimisho
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nimalizie kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Profesa Li na Dkt. Han pamoja na wadhamini wote kwa ujenzi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika kilichogharimu zaidi dola za Kimarekani milioni 20. Majengo tunayozindua leo ni sita (6) yakijumuisha jengo la ghorofa la makazi lenye nyumba 13 (apartments), makumbusho, ukumbi wa kisasa wa mikutano na mihadhara, ofisi, maduka na mgahawa.
Natoa rai kwa nchi za Afrika kukitumia kijiji hiki muhimu katika kukuza uelewa na udugu baina ya China na Afrika. Kupitia uhusiano wa kiutamaduni na uhusiano wa watu wetu tutaweza kuendeleza na kuudumisha uhusiano wetu na China na kurithisha kizazi hata kizazi. Kama wahenga wa Kichina wanavyosema; “ukitaka kuvuna ndani ya mwaka mmoja panda ngano, ukitaka kuvuna baada ya miaka mitano panda mti, na ukitaka kuvuna kwa muda mrefu, pandikiza watu”. Kijiji hiki ni ushahidi wa dhahiri wa dhamira yetu hiyo.
Baada ya kusema hayo machache, napenda kutamka kuwa sasa majengo ya Kijiji cha Sanaa za Afrika Songzhuang yamefunguliwa rasmi!
Asanteni sana kwa kunisikiliza.