Hotuba
- Sep 19, 2014
KEYNOTE SPEECH BY DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, DURING THE USAID FORUM ON FRONTIERS IN DEVELOPMENT: ENDING EXTREME PO...
Soma zaidiHotuba
Honourable Dr. Rajiv Shah, USAID Administrator;
Honourable Mr. Mark Diop, Vice President of the World Bank;
Distinguished Participants;
Ladies and Gentlemen;
Allow me to begin by thanking you Dr. Rajiv Shah for inviting me to participate in this Forum and for affording me the opportunity to share my thoughts on its very important theme of Ending Extreme Poverty. I commend the USAID for initiating this debate, and I hope participants will come up with pertinent proposals about ways and means to end this human degrading condition of our time. For those of us who live with this reality in our countries, it is heartwarming, indeed, to see that there are friends out here who care about the plight of the poorest and are ready to do what it takes to erase this scourge from the face of this planet.
Distinguished Participants;
Ladies and Gentlemen;
The World Bank Report on End Extreme Poverty and Promote Shared Growth (2013) tells us that globally poverty has declined rapidly over the past three decades since 1990. In this regard, some 700 million people have moved above the US$ 1.25 poverty line but about 1.2 billion still live under conditions of extreme poverty. Out of the 1.2 billion people, more than 750 million live on less than US$ 1.0 a day and nearly 150 million others live on less than US$ 0.50 a day. Similarly, around 800 million are faced with hunger or have inadequate food supply and, 500 million of them, suffer from chronic malnutrition.
Ladies and Gentlemen;
It is good to note that the world has been able to achieve the Millennium Development Goal No.1 of reducing by half the number of people who live under extreme poverty. Indeed, poverty rate in developing countries has been reduced from 43.1 percent in 1990 to 20.6 percent by 2010. This achievement shows that it is possible to eradicate poverty in the world. However, this achievement has not been uniform across the developing world. China and India accounted for most of the success and nearly half of the poor live in 20 countries in South Asia, Sub-Saharan Africa and East Asia and the Pacific.
Ladies and Gentlemen;
The challenge of overcoming extreme poverty is an overwhelming one in Africa. Africa is home to 33 of the 48 world’s least developed countries (LDCs). Moreover, in 2010 more than one-third of Sub-Saharan African countries had an extreme poverty rate of more than 50 percent. Among them, 12 countries had an extreme poverty rate of above 60 percent and 4 countries that are fragile and affected by conflicts were above 80 percent. This condition has not changed much today as we speak.
Ladies and Gentlemen;
Clearly, political stability is an important factor in the fight against extreme poverty. Conflicts worsen the poverty situation. Conflicts disrupt economic activities, scare away investments and cause destruction of property including productive assets as well as social and economic infrastructure. Unfortunately, Africa has had an unfair share of conflicts. Very few African countries have enjoyed uninterrupted peace in the five decades of Africas independence from colonial rule. Of the 33 least developed countries from Africa 25 have gone through some form of conflict. Even the non LDCs in Africa have not been spared. Consequently, lack of peace and stability has been a critical factor in Africa’s slow pace towards poverty reduction.
Paradoxically, even those countries which have had no conflicts have not done very well either. The pace of poverty reduction has been muted. In my view, this is very much a function of the economic policies pursued, in the first two and half, decades since independence. They caused stagnation of economic growth and some economies actually shrank thus aggravating the poverty situation among the people. The turnaround began in the second half of the 1990s after the economic reforms introduced in the mid 1980s began to take effect. The extent of the turnaround depended on the success of the reforms. Likewise, the extent of poverty reduction depended on the success of the reform agenda and the level of poverty the country was in at the beginning of the reforms. It also depended on external environment in particular the global economic architecture which has not been so kind to poor nations and poor people in the developing world.
Ladies and Gentlemen;
My dear country Tanzania is a typical example of a country that enjoyed uninterrupted peace and stability since independence yet we are one of the LDCs from 1971 when LDCs classification started. Besides a hostile global environment, economic policies pursued soon after independence which did not succeed has a big hand in this state of affairs. As a matter of fact, the economy declined to dangerous lows. Things began to change after the introduction of economic reforms from the 1980s. We have stayed the cause of reforms ever since with remarkable success. The country is now enjoying strong macro-economic performance with the last decade being exceptionally successful.
Overall economic growth has increase from an average of 3.5 percent in the 1990s to the average of about 7 percent over the last decade. Despite this growth, poverty reduction has not been correspondingly impressive. In the last two decades income poverty declined from 39 percent in 1990 to 28.2 percent in 2012, a decline of about 11 percent only. This explains why we will not be able to meet the MDG target of halving extreme poverty below the 1990 baseline by 2015. However, we have been successful with regard to reducing by a half the proportion of population living below the national food poverty line. This declined from 21.6 percent in 1990 to 9.7 percent in 2012, a decline of about 12 percent.
Distinguished Participants;
Ladies and Gentlemen;
Our income poverty reduction efforts have not borne the expected results mainly because our growth has not been high enough in sectors that support the majority of the people, especially the poor. The fast growing sectors and their ten-year average growth rates (2004 – 2013) were the following: (1) Services (8.0%) driven by Telecommunication (20.2%), Financial Services (10.8%) and Trade (8.2%); (2) Industry (8.5%) comprising of Construction (9.6%), Manufacturing (8.6%) and Mining (8.2%). Unfortunately, agriculture, which supports about 75 percent of our population in terms of employment and livelihood, grew at an average of only 4.2 percent in the last decade.
Ladies and Gentlemen;
The low growth in agriculture explains why the pace of poverty reduction has not been fast enough as expected. We have been taking action to transform and modernize our agriculture as exemplified by a number of programmes and initiatives being implemented in the country. The Agriculture Sector Development Programme (ASDP), Kilimo Kwanza and SAGCOT are among such initiatives being undertaken. Noticeable progress is being registered and the future of Tanzania’s agriculture looks promising.
Overall, in our quest to promote growth, development and eradicate poverty comprehensively and in focused manner the Tanzania Development Vision 2025 (TDV 2025) was conceived in the late 1990s and unveiled in the year 2000. The Vision, envisages totransform Tanzania from a least developed country in the year 2000 to a middle income country by the year 2025. Tanzania will then be a country characterized by high quality livelihoods, peace, stability, unity and good governance; a well-educated and learning society; and a competitive semi-industrialized economy capable of producing growth and shared benefits.
Ladies and Gentlemen;
After coming into office in December 2005, I undertook to implement the Vision in earnest. The first thing we did was an evaluation of the implementation status of the vision and then plan for its implementation for the remaining period. Subsequently we developed long term perspective plan for the remaining 15 years of the Vision. We decided to divide it in three medium term development plans of five years each.
We are implementing the first Five Year Development Plan (FYDP 2011/12 – 2015/16), whose overarching objective has been implementing measures that are geared at unleashing the growth potentials of Tanzania. Specifically, we are aiming at addressing infrastructural bottlenecks particularly in energy, ports, roads and railways; increasing the pool of skilled labor; advancing science, technology and innovation as well as information and communication technology (ICT); improve the general business environment and enhance productivity in agriculture.
In the second Five Year Development Plan (FYDP 2016/17 – 2020/21) we will focus on nurturing an industrial economy through the development of a vibrant industrial sector. The focus will be on natural gas based industries, agro-processing industries and medium technologies industries. We shall aim at creating jobs by promoting industrial sub-sectors with high potentials for employment creation.
Ladies and Gentlemen;
In the third Five Year Development Plan (FYDP 2021/22 – 2025/26) our focus will be on realizing competitiveness of Tanzania in the regional and the world market place. We will focus on improving competitiveness in all sectors, especially manufacturing and services so as to ensure that manufactured products from our economy are successfully exported. The target of this plan is to transform Tanzania into a manufacturing hub in the region whilst making sure that all the gains made in social services, the business environment, infrastructure development and productivity are consolidated and advanced.
Ladies and Gentlemen;
Apart from high focus on transforming and modernizing agriculture during the implementation of the first Five Year Development Plan, we have accorded high priority to infrastructure development, particularly the transport subsector such as roads, railways, ports, airports and marine transport. The reason for doing this was to deal with one critical constraint to growth and development in the country. It will be easier to facilitate access to inputs and markets, reduce transportation costs and costs of doing business. Significant progress has been made in this regard with roads where 6,500 kilometers are already paved and 11,174 kilometers are under construction. Our objective is to connect all regions in the country with paved roads is being realized. Also, we have been investing heavily in improving rural roads such that over 80 percent are now passable throughout the year.
With regard to electricity priority is on increasing energy generation and distribution. The aim is to catalyze economic activities and improve living standards of our people since energy is key to development and decent life. We intend to increase electricity generation from the current 1,478MW to 2,780MW by 2015. Correspondingly, we are expanding electricity distribution and in doing so, the percentage of households and businesses with access to electricity has increased from 10 percent in 2005 to 36 percent currently.
Ladies and Gentlemen;
In an effort to transform our country’s economy from that of being an exporter of primary products to one that exports value added products. We aim to export more manufactured, processed or semi processed goods from our agricultural products, minerals and other natural resources of which Tanzania is richly endowed. Therefore, we are giving special attention to industrialization. Value addition through industrialization will stimulate more production in raw material source sectors. Also, it will help create jobs and increase employment and incomes thus lifting more people out of poverty.
Ladies and Gentlemen;
To ensure employability of Tanzanians particularly our young people, we have, as a matter of priority, expanded education opportunities at all levels from primary, secondary, vocational to university level. We have more young boys and girls in primary and secondary schools and young men and women in universities than any other time in history. We have increased training and skills development opportunities at various specialized and vocational schools. We have decided to do so because we know the power of education in moving communities out of poverty. It is a game changer.
We have, also, increased investment in health care development which is an important factor in human capital development. It is beginning to pay dividends as evidenced by improved human development situation in the country. More and more Tanzanians have access to health and almost all the major killer diseases are on the decline. Life expectancy has increased from 51 years in 2002 to 61 years in 2012. Due to improvement of health system, our country has also recorded significant gains in child survival rates as measured by reduction of infant and under five mortality rates. Infant Mortality Rate has declined from 115 per 1,000 live births in 1988 to 21 per 1,000 live births over the in 2013. On the other hand, Under Five Mortality rates have improved from 231 per 1,000 live births 1988 to 54 per 1,000 live births in 2013. Definitely, these are significant gains in human development.
With regard to education, after succeeding in increasing access to education at all levels our preoccupation now is on improving the quality of education. Here, also, we have been making significant progress on availability of teachers, text books and other teaching aids. However, we need to do more on teachers housing and science laboratories.
Ladies and Gentlemen;
In our efforts to promote growth and eradicate poverty our experience has taught us a few important lessons which I want to share with you. First, with the right policy mix, appropriate intervention from government and enhanced private sector participation, transformation of the economy is possible. Second, we can win the battle of eradicating income poverty and hunger if we invest in growth enhancing, job creating and poverty reducing interventions. Our efforts in that direction have led to reduction of income poverty by 7.8 percentage points from 36 percent in 2005 to 28.2 percent in 2012 and attainment of MDG target of reducing food poverty by 50 percent. Third, support to vulnerable people or households, through conditional cash transfer or provision of public services, is important if growth and poverty reduction efforts are to be more inclusive.
Distinguished participants;
Invited Guests;
Ladies and Gentlemen;
In conclusion, let me repeat my opening statement that the world is still faced with a daunting task of eliminating extreme poverty and that this task is even more daunting in Africa and LDCs like Tanzania. Political stability and promotion of inclusive and pro-poor economic growth are pre-requisites to poverty eradication. The growth decade in Africa and indeed Tanzania has taught us the lesson that economic growth, while fundamental, is not sufficient. Growth ought to be quality growth for it to be sufficient; meaning it has to be inclusive, create employment and increase people’s incomes.
For this to happen, such growth must take place in pro-poor sectors that ensure inclusivity and accessibility to the growth process by the poor and the marginalized sections of the society. We are encouraged by the World Bank assurance that extreme poverty as measured by spending less than US$ 1.25 a day can be reduced to no more than 3 percent by 2030 by fostering income growth of the bottom 40 percent of the population in every country. We all look with great anticipation to that glorious year, when almost all our people will be living in a prosperous world and living a prosperous life.
It would be remiss of me if I conluded my remarks without acknowledging and thanking the Government and people of the USA for the invaluable support they are extending to developing countries like Tanzania in our endeavours to wrestle our people from object poverty to prosperity. The support is making the difference we all desire. Please continue to do good job.
Thanks for your attention
- Sep 06, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, WAKATI WA MAJUMUISHO YA MKOA WA DODOMA, DODOMA TAREHE 04 SEP...
Soma zaidiHotuba
Utangulizi
Mheshimiwa Dkt. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Miji;
Waheshimwa Madiwani;
Wazee Wangu;
Ndugu wananchi;
Kuna methali ya Kiswahili isemayo hakuna refu lisilokuwa na ncha. Hatimaye ziara yangu ya Mkoa wa Dodoma imefikia mwisho. Ziara hii niliyoianza tarehe 28 Agosti, 2014 imenifikisha kwenye wilaya zote za Mkoa wa Dodoma. Madhumuni ya ziara yangu yalikuwa kuona shughuli za maendeleo. Kuona tulipofanikiwa na pale ambapo pana matatizo tupatafutie ufumbuzi. Nimefarijika sana na hatua kubwa za maendeleo ambazo kila wilaya imezifikia. Nimejionea maendeleo makubwa katika sekta na nyanja mbalimbali za maisha ya wananchi wa mkoa huu. Hongereni sana. Aidha, nimeona au kusimuliwa kuhusu changamoto kubwa na ndogo zinazowakabili, ambazo zikiweza kupatiwa ufumbuzi ufanisi utaongezeka na kasi ya kujiletea maendeleo itakuwa kubwa zaidi.
Elimu
Natoa pongezi nyingi kwa viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma kwa juhudi kubwa mnazofanya na mafanikio mliyopata au mnayoendelea kupata katika kuendeleza elimu Mkoani kwenu. Kwa ajili hiyo basi idadi ya wanafunzi katika ngazi za awali, msingi na sekondari imekuwa kubwa kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu. Hivi sasa Mkoani Dodoma kuna wanafunzi wa Awali 47,427, wa Shule za Msingi 391,475 na wa Sekondari 59,035 ukilinganisha na wanafunzi wa Awali 55,524, wa Shule za Msingi 152,366 na wa Sekondari 24,288 mwaka 2007. Jukumu lililoko mbele yenu na mbele yetu pia ni kutatua matatizo yanayoikabili sekta ya elimu mkoani. Pamoja na kupanda kuliko ilivyokuwa mwaka 2012, kiwango cha ufaulu cha asilimia 38.2 kwa shule za msingi na asilimia 55.4 kwa shule za sekondari kwa mwaka 2013 ni chini ya wastani wa taifa wa asilimia 50.61 kwa shule za msingi na asilimia 58.25 kwa shule za sekondari. Hivyo mnayo kazi kubwa ya kufanya ili kufikia kiwango cha ufaulu cha asilimia 60 mwaka huu na asilimia 80 mwakani. Ongezeni bidii.
Napenda kuwahakikishia kuwa sisi katika Serikali kuu tutaendelea kutimiza wajibu wetu kuhusu elimu. Tutaendelea kuleta walimu, vitabu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Hali kadhalika tutaendelea kutoa pesa zitakazoboresha miundombinu ya shule na nyumba za walimu. Kwa upande wa walimu tumefanikiwa kutosheleza mahitaji ya walimu wa masomo ya sanaa kwa shule zote za sekondari. Kwa baadhi ya Wilaya kuna ziada ya walimu hao. Hii ndiyo hali ilivyo kote nchini. Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi jambo ambalo ni tatizo la kitaifa.
Mkoa wa Dodoma una mahitaji ya walimu 4,076. Waliopo ni walimu 3,250, kati yao walimu 2,482 wa sanaa na 645 wa sayansi. Kuna jumla ya upungufu wa walimu 949 wa sayansi na ziada ya walimu 123 wa sanaa. Walimu wa ziada kwa masomo ya sanaa wapo Wilaya za Mpwapwa (34), Bahi (55), Dodoma Mjini (86) na Kongwa (92). Upungufu wa walimu wa sanaa upo Wilaya za Chamwino (103), Chemba (9), na Kondoa (32). Upungufu wa walimu wa sayansi upo wilaya zote. Hivi sasa kitaifa tuna pengo la walimu 23,500 na uwezo wa vyuo vyetu ni kuzalisha wanafunzi 2,500 kwa mwaka. Tumedhamiria kulikabili tatizo hili kwa nguvu zote na maarifa yetu yote. Sina wasiwasi kwamba tutafanikwia kama ilivyokuwa kwa changamoto nyingine nyinig.
Kuhusu ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari za Kata, narudia kuwakumbusha viongozi wa Wilaya na Mkoa wa Dodoma kwamba muda wa miaka miwili tuliopeana mwaka 2012 unaisha mwezi Novemba, 2014. Na, kupitia kwenu nawakumbusha viongozi wa Mikoa yote na Wilaya zote nchini ifikapo Novemba mwaka huu tutaulizana. Hatutaacha kubanana na kama hapana budi kuwajibishana.
Tunaendelea kuboresha upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Mpaka sasa uwiano wa kitabu kwa wanafunzi umefikia 1:3. Tutaendelea kutenga fedha zaidi ili kila mwanafunzi awe na kitabu chake. Suala la nyumba za walimu nalo ni jambo ambalo tunalipa umuhimu. Tunaendelea kuanzia mwaka wa jana kutekeleza mpango wa kuzipatia shilingi milioni 500 kila Halmashauri kwa ajili ya ujenzi huo. Halmashauri za Wilaya ya Mkoa wa Dodoma zitaingizwa kwenye awamu zinazofuata na fedha pia zitaongezwa.
Nimefurahishwa na utekelezaji wa mpango wa utoaji chakula cha mchana kwa wanafunzi mashuleni katika Wilaya za Chamwino, Bahi, Kondoa, Mpwapwa na Chemba. Huu ni mpango unaofadhiliwa na Shirika la Chakula Duniani (WFP). Hapa nchini Mpango wa Chakula wa WFP za Mikoa 4 ya Dodoma, Singida, Arusha na Manyara. Jumla ya shule 640 za mikoa hiyo zinafaidika na mpango huu upo katika Wilaya 16. Ni mpango mzuri ambao manufaa yake ni kuwaongezea watoto mazingira mazuri ya kufuatilia na kuelewa masomo. Hivyo, tuusimamie vizuri ufanikiwe. Ni vizuri viongozi wa Mkoa na kila Halmashauri mkajipanga vizuri ili mpango huu mzuri uweze kuwepo kila Wilaya na uweze kuendelea punde WFP watakapoacha kugharamia mpango huo. Maana jukumu la kuhakikisha lishe ya watoto wetu ni letu wenyewe.
Mkoa wenu unakabiliwa na tatizo kubwa sana la watoto wanaoanza darasa la kwanza kutomaliza darasa la saba na wanaoanza kidato cha kwanza kutomaliza kidato cha nne. Tatizo hili lipo katika kila Wilaya. Takwimu za Mkoa zinaonesha kuwa kati ya wanafunzi 54,301 waliosajiliwa darasa la kwanza mwaka 2007, ni wanafunzi 39,387 tu ndiyo walifanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2013. Hii ina maana kuwa wanafunzi 14,914 hawakufanya mtihani ambao ni sawa na asilimia 27.5. Na kwa upande wa sekondari, kati ya wanafunzi 16,023 walioandikishwa kidato cha kwanza mwaka 2010, ni wanafunzi 12,693 ndiyo waliofanya mtihani mwaka 2013. Wanafunzi 3,330 hawakufanya mtihani huo, sawa na asilimia 21. Idadi hii ni kubwa mno, haikubaliki. Haiwezi kuachwa kuendelea lazima ikomeshwe.
Narudia kusisitiza agizo langu nililotoa mwezi uliopita kwamba, kuanzia sasa Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule ni lazima watoe taarifa za mahudhurio ya wanafunzi kwa Maafisa Elimu wa Wilaya kila miezi mitatu. Maafisa Elimu wa Wilaya nao watalazimika kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambae nae atawasilisha kwenye vikao vya Baraza la Madiwani la Halmashauri mwezi mmoja baada ya kupokea taarifa hizo. Halmashauri hazina budi kuchukua hatua stahiki, kijamii na kisheria, kuhakikisha kuwa watoro wanarudi shuleni. Wazazi wa watoto hao au mtu ye yote atakayebainika kuhusika na utoro huo abanwe ipasavyo.
Maji
Kama mjuavyo, kuwapatia wananchi wa Tanzania maji safi na salama karibu na wanapoishi ni moja ya malengo ya msingi ya Sera na shughuli za serikali na Chama tawala. Katika ziara yangu nimeshuhudia utekelezaji wake. Nimeweka mawe ya msingi ya ujenzi wa miradi ya maji na nimezindua miradi ya maji iliyokamilika. Jitihada zetu hizo zimetuwezesha kuwapatia maji asilimia 75.4 ya wakazi wa Mijini na asilimia 50.6 ya wakazi wa vijijini mkoani Dodoma. Lengo la kitaifa ni kuwapatia maji asilimia 90 ya wakazi wa mijini na asilimia 65 ya wakazi wa vijijini ifikapo 2015.
Kwa hapa Dodoma kiwango hicho cha upatikanaji maji kina maana ya kufanya kazi ya ziada ili kuweza kufikia lengo. Miradi inayoendelea kutekelezwa sasa mijini na vijijini hapa Mkoani itakapokamilika itawezesha kufikia lengo. Rai yangu kwa viongozi ni kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili wananchi wapate maji safi na salama mapema.
Vile vile, nawaomba kusimamia na kuwaelimisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla wake. Viongozi, waache kulalamika juu ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji. Sheria zipo, mamlaka mnayo chukueni hatua ili kulinusuru taifa letu dhidi ya uharibifu wa mazingira.
Umeme
Tumeongeza, maradufu, juhudi za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme nchini. Shabaha yetu ni kuwawezesha asilimia 30 ya Watanznaia waweze kupata umeme ifikapo mwaka 2015. Tayari tumeshavuka lengo hilo kwa kufikia asilimia 36. Kwa Mkoa wa Dodoma katika mwaka huu wa fedha shilingi bilioni 43.8 zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini. Fedha hizi zitawezesha zaidi ya vijiji 193 kupatiwa umeme katika Mkoa huu. Kila Wilaya niliyoitembelea kuna miradi kadhaa ya umeme inayoendelea kutekelezwa. Ndugu zetu Wilaya ya Bahi walinilalamikia kuwa wao wamepewa vijiji vinne tu. Nikawasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ambae ameahidi kuwa watafanya masahihisho stahiki. Maombi yangu kwa viongozi wenzangu wahimizeni wananchi waunganishe umeme majumbani na kwenye shughuli zao za kiuchumi na kibiashara.
Barabara
Ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari, umeme na simu ni mambo tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Nilisema hivyo katika hotuba yangu ya kwanza tarehe 30 Desemba, 2005 na kurudia katika kupindi chote cha uongozi wangu mpaka sasa. Kwa upande wa barabara lengo letu ni kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami na kuimarisha baraba za mikoa, wilaya na Vijiji ziweze kupitika wakati wote. Katika ziara yangu ya Mkoa wa Dodoma nimeshuhudia mafanikio makubwa ya utekelezaji wa lengo hilo. Nimeweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mayamaya hadi Bonga. Hali kadhalika, nilizindua kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Dodoma hadi Fufu. Nimeambiwa kuwa zimebaki kilometa 25 kwa upande wa Fufu hadi Iringa ili kukamilisha ujenzi wa barabara yote ya Iringa hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 260 kwa kiwango cha lami. Bila ya shaka mtakubaliana name kuwa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Babati unatoa fursa ya iana yake kwa maendeleo ya mji wa Dodoma na Mkoa huu kwa jumla. Jipangeni kuitumia fursa hiyo.
Kule Kongwa niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mbande, Kongwa hadi Mpwapwa na Kibakwe. Napenda kurudia kuwatoa hofu ndugu zangu wa Mpwapwa na Kibakwe kuwa ujenzi wa barabara ile unaendelea na ndiyo maana pale njia panda ya Kongwa tulifanya shughuli za kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Mbande, Kongwa, Mpwapwa na siyo uzinduzi wa barabara ya lami kutoka pale hadi Kongwa.
Nimefarijika sana kuona jinsi barabara za mkoa na Wilaya zikiendelea kuimarishwa. Kwa kweli ilikuwa jambo la faraja kubwa kwangu kusikia kuwa vijiji vyote vya mkoani vinafikika kwa barabara. Ni ushindi mkubwa. Napenda kuwaahidi kuwa tutaendelea kuwapatia fedha kutoka Mfuko wa Barabara ili mzidi kuziimarisha barabara zenu. Bahati nzuri Mfuko huo tumeuongezea sana uwezo wake kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/2006 hadi shilingi bilioni 751.7 hivi sasa.
Tulipokuwa wilayani Mpwapwa niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la Gulwe linalounganisha majimbo ya mpwapwa na Gulwe. Tulipokuwepo pale palijitokeza mawazo mazuri kuhusu namna ya kuikinga reli ya kati ambayo imekuwa inaharibiwa mara kwa mara wakati wa mvua katika maeneo ya Godegode, Gulwe, Msagali na Kilosa. Ulitolewa ushauri kwamba kama yakijengwa mabwawa katika mito inayovuka reli hiyo katika maeneo hayo. Mabwawa hayo yatapunguza wingi na kasi ya maji hivyo kuinusuru reli. Nilivutiwa na mawazo hayo na kuufikisha ujumbe kwa Waziri wa Uchukuzu Mheshimiwa Harrison Mwakyembe ambaye aliniambia kuwa ni jambo linalofanyiwa kazi. Nilizungumza pia na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda asimamie kuhakikisha kuwa jambo hili muhimu linafanyika. Tulikubaliana kuwa Wizara ya Maji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika nao washiriki katika mpango huu kwani ni wadau muhimu wa mabwawa hayo. Hali kadhalika viongozi wa Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Manyara wahusike.
Natambua kuwepo maombi ya kutaka barabara kadhaa za Wilaya ziwe za mkoa ili zisimamiwe na TANROADS. Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John Magufuli amesikia na zipo baadhi ambazo amezitolea majibu ya kukubali na nyingine anaendelea kutafakari nini afanye. Bila ya kuingilia atakachoamua napenda kusisitiza kuwa msingi mkuu unaoifanya barabara kuwa ya mkoa na hivyo kushughulikiwa na TANROADS ni kuunganisha Wilaya moja na nyingine. Barabara inayoanzia na kuishia ndani ya Wilaya haina sifa hiyo hata kama ni ndefu kiasi gani. Nalisema hili kwa sababu umeanza kuzuka mtindo wa Halmashauri kutaka kukwepa wajibu wao. Pale ambapo wamezidiwa ujuzi na uwezo waseme TANROADS itawasaidia lakini wasikwepe majukumu yao.
Kilimo na Mifugo
Masoko ya Mazao ya Kilimo
Viongozi, Wazee wangu na Ndugu Wananchi;
Hongereni kwa mafanikio mliyopata mwaka huu katika kilimo. Mkoa umezalisha tani 687,122 za mazao ya chakula wakati mahitaji yenu ni tani 494,331. Hivyo kuna ziada ya tani 192,791. Hiki ni kielelezo tosha kwamba juhudi zenu za kuleta mageuzi ya kilimo zinafanikiwa. Mkoa wenu una zaidi ya matrekta makubwa na madogo 1,756. Kati ya matrekta hayo Wilaya ya Kongwa ina matrekta 728. Hongereni sana na endeleeni kuongeza matumizi ya zana bora na pembejeo za kisasa za kilimo mpate mafanikio makubwa zaidi.
Nilipoingia mkoa huu kutokea mkoa wa Morogoro kilio kikubwa cha wakulima kilikuwa soko la mahindi kwa maana ya kukosekana mnunuzi anayetoa bei nzuri kwa wakulima. Wapo watu binafsi wanaonunua mahindi ya wakulima kwa bei ndogo sana. Kilio hicho nilikikuta Mkoa wa Morogoro na Tanga kabla ya hapo. Nilizungumza na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa Mhandisi Chiza kuhusu jambo hilo. Akamtuma Katibu Mkuu Mama Sofia Kaduma na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula Ndugu Walwa waje kujiunga na msafara. Ndugu Walwa alieleza kuwa walichelewa kuanza ununuzi katika ukanda wa kati lakini sasa wako tayari kufanya hivyo. Ni matumaini yangu kuwa hatua hiyo italeta nafuu kwa wakulima. Naomba tufanye kazi kwa karibu na NFRA tuwasaidie panapobidi ili wafanikishe jukumu lao. Ni jambo lenye maslahi kwa wakulima, kwa Wakala na Taifa kwa jumla.
Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
Wazee wangu;
Nilipokuwa Kibaigwa, Kongwa nilipokea malalamiko yenye mvumo mkubwa kutoka kwa ndugu zetu wanaofanya shughuli za kilimo katika Wilaya ya Kiteto. Wanalalamikia kufukuzwa, kupigwa, kuuawa, kuchomewa moto nyumba, matreka na kuporwa na kunyang’anywa mali zao na ndugu wa jamii ya wafugaji. Wapo waliokuwa wanadai kuwa walikuwa wanaishi huko kwa zaidi ya miaka thelathini hivyo kujikuta wanaambiwa ondoka, nyumba zinachomwa moto, mali zinaharibiwa ni mambo magumu sana kuelewa. Nilipokuwa Mkoa wa Morogoro nilipokea malalamiko kutoka kwa wakulima dhidi ya wafugaji kwamba mifugo imekuwa mingi mno kupita kiasi na kwamba wanaharibu mazao ya wakulima.
Nilipokuwa Morogoro nilisema mambo ambayo ningependa kuyarudia tena leo. Kwanza, kwamba, ardhi hainongezeki lakini watu wanaongezeka na shughuli zinazohitaji kutumia ardhi zinaongezeka. Kwa sababu hiyo wanadamu hawataweza kufanya kila kitu anachotaka katika ardhi hiyo hiyo aliyonayo. Hivyo analazimika kupanga matumizi bora ya ardhi. Yaani anatakiwa kupanga atafanya nini, wapi katika ardhi yake. Kwa ajili hiyo nimewataka viongozi wa vijiji, Wilaya na Mkoa kuwa na mpango wa matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali katika maeneo yao ya uongozi. Kwa upande wa ardhi inayotengwa kwa ufugaji hawana budi kujua ina uwezo wa kubeba mifugo mingapi na ya aina gani. Mgao huo ukishafanywa lazima usimamiwe kwa dhati. Ikifanyika hivyo mtakuwa na hakika na kila hatua ya maendeleo inayochukuliwa na kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Hapatakuwa na migogoro kwa sababu kila mmoja atakuwa na eneo lake la kutosha kufanyia shughuli zake. Pia hapatakuwa na migogoro kwa vile baada ya ukomo wa uwezo wa mifugo inayoweza kubebwa na ardhi iliyotengwa kujulikana na kuzuia mifugo zaidi isiruhusiwe kuingia.
Najua wakati mwingine wenye mifugo wakiambiwa hivyo wanaona wanabaguliwa na kunyimwa haki yao kama raia. Si hivyo, hawajanyimwa haki ya uraia ya kuishi po pote upendapo. Kilichofanyika ni kuweka utaratibu mzuri wa raia kutumia haki yake hiyo kwa manufaa yake na jamii yote. Inampa fursa za uhakika kustawisha mifugo yake na kumuepusha na ugomvi na wengine.
Jambo la pili, nililolisisitiza kule Morogoro ambalo napenda kulirudia tena hapa leo ni kuwa ndugu zetu wanaofuga wahakikishe kuwa mifugo yao haili mazao ya wakulima. Kwa kweli jambo kubwa linalozua chuki, uadui na ugomvi baina ya wakulima na wafugaji ni mifugo kula mazao ya wakulima shambani. Kama hili halitokei sioni mazingira ya kuwepo mgogoro kati ya wakulima na wafugaji. Kila mmoja ataendelea na shughuli zake na kuwa rafiki wa mwenzake. Nilipokuwa Morogoro niliwaomba wafugaji wapitishe azimio kuwa mwaka huu hakuna hata robo eka ya shamba itakayoliwa na kuteketezwa. Ikiwa hivyo, sidhani kama kutakuwa na mgogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Kuhusu yaliyotokea Kiteto kati ya wakulima na wafugaji nalo ni suala la uhusiano na uongozi. Kama watu wameishi huko na kufanya shughuli zao kwa zaidi ya miaka 30 kuna namna bora zaidi za wao kuondoka au kuwaondoa. Viongozi wanayodhamana kubwa ya kuona kuwa watu wa nchi hii hawafanyiwi vile. Nimezungumza na Waziri Mkuu ili tuangalie uwezekano wa mkutano kati ya viongozi wa Mikoa ya Manyara, Morogoro na Dodoma inayojumuisha Wilaya za Mpakani wakutane na kuzungumza namna ya kuondoa uadui na kuwafanya watu waishi pamoja na kushirikiana.
Afya
Nawapongeza kwa hatua kubwa mliyopiga katika kuboresha sekta ya afya kwa kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi. Mkoa wa Dodoma una mtandao wa hospitali 8, vituo vya afya 41 na zahanati 316. Nafurahishwa pia na jitihada za kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa zahanati na vituo vya afya vipya ili kutimiza azma yetu ya kusogeza huduma za afya ndani ya eneo la mzingo wa kilometa 5 wanapoishi wananchi.
Huko nyuma niliagiza kwamba kila Halmashauri ya Manispaa, Mji na Jiji ambayo iko Makao Makuu ya Mkoa, ijenge hospitali yake ili kuiwezesha hospitali ya Mkoa kufanya shughuli za rufaa za Mkoa. Manispaa ya Dodoma mko nyuma katika kutekeleza agizo langu hili. Tengeni eneo la ujenzi wa hospitali ya Manispaa na wekeni kwenye bajeti yenu ili tuijenge.
Pia upo wajibu wa kisera kuhakikisha kuwa kila Wilaya ina hospitali ya Wilaya. Katika Mkoa wa Dodoma Wilaya za Kongwa, Bahi, Chamwino, Chemba na Dodoma Mjini hazina hospitali za Wilaya. Nimewataka waanze ujenzi wa hospitali hizo. Waweke mahitaji yao kwenye mipango ya maendeleo ili itafutiwe fedha.
Nawapongeza kwa jitihada mnazofanya za kuhamasisha akina mama kujifungua katika zahanati, vituo vya afya na hospitali. Taarifa yenu inaonesha kwamba asilimia 79 ya akina mama wajawazito wanajifungulia katika vituo vya kisasa vya kutoa huduma ya afya na chanjo ya watoto mmefikisha asilimia 96. Msibweteke ongezeni uhamasishaji ili akina mama wote wajifungulie kwenye vituo vya afya na watoto wote wapate chanjo. Kwa ajili hiyo, napenda kushauri kuwa ujenzi wa sehemu ya akina mama wajawazito kusubiria kabla ya kujifungua (maternity waiting homes) ufikirieni kwa uzito unaostahili. Wenzenu wa Morogoro wamelifanya kuwa sehemu ya mipango yao ya kuendeleza afya ya akina mama wajawazito. Inasaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito kunaweza kusaidia Mkoa huu pia na kwingineko nchini.
Aidha, tuendelee kuhimiza mapambano dhidi ya ugonjwa ya UKIMWI katika maeneo yetu. Japo takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya UKIMWI kimkoa yanapungua toka asilimia 3.4 mwaka 2008 hadi asilimia 2.9 mwaka 2012, lengo letu ni kutokuwa na maambukizi mapya kabisa. Ongezeni juhudi ili lengo letu hilo tulifikie.
Nawapongeza pia kwa kuvuka lengo letu la kuhakikisha kwamba asilimia 30 ya Watanzania wanajiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ifikapo 2015. Ninyi mmekwishafikisha asilimia 47.9. Hata hivyo, ziko Wilaya kama za Kondoa, Chemba na Manispaa ya Dodoma ambazo ziko chini sana. Ongezeni jitihada ili wananchi wengi zaidi wapate huduma ya mfuko huo.
Ugonjwa wa Ebola
Ndugu wananchi;
Tangu mwezi Aprili, 2014 nchi za Afrika Magharibi hususan nchi ya Guinea, Siera Leone, Liberia na Nigeria zimekumbwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa hatari wa Ebola. Taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa tayari watu 3,500 wameambukizwa na tayari zaidi ya vifo 1,900 vimetokea. Asilimia 40 ya vifo hivi vimetokea ndani ya wiki tatu hadi kufikia tarehe 3 Septemba, 2014. Ebola ndiyo virusi hatari zaidi duniani kuliko hata UKIMWI. Ndiyo maana Shirika la Afya Duniani limeutangaza ugonjwa huu kuwa ni janga la dunia, na inatarajiwa athari zake zinaweza kuongezeka. Ugonjwa huu husababishwa na virusi vya Ebola na husababisha wagonjwa wengi kufa kwa vile ugonjwa huu hauna tiba maalum wala chanjo.
Wataalam wanatuambia kwamba virusi vya Ebola hubebwa na ndege aina ya popo na wanadamu huupata kupitia kwa wanyama walioambukizwa kwa kuwagusa au kuwala. Wanyama hao ni pamoja na sokwe, nyani na swala. Maambukizi kutoka kwa mgonjwa huenda kwa mtu mwingine kwa kugusa damu au majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo au kwa kugusa maiti ya mtu aliyekufa kutokana na ugonjwa huo. Ugonjwa huu ni hatari sana kiasi kwamba hata watoa huduma za afya kama madaktari na wauguzi kama hawakuchukua tahadhari zinazotakiwa wanaweza kuambukizwa na hata kufa. Mpaka hivi sasa Daktari mmoja aliyekuwa anawahudumia wagonjwa wa Ebola kule Liberia amekufa.
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na mgonjwa kuwa na homa kali ya ghafla, kulegea mwili, kuumwa na kichwa, kuumwa na misuli na kutokwa na vidonda kooni. Dalili hizi zinaweza kuambatana na kutapika, kuharisha, kutokwa na vipele, kutokwa na damu ndani na nje ya mwili na kushindwa kufanya kazi kwa figo na ini. Dalili za ugonjwa huu hujitokeza katika siku 2 hadi 21 baada ya kuambukizwa.
Tunamshukuru Mungu kwani mpaka sasa hapa nchini hajapatikana mtu yeyote mwenye ugonjwa huu. Pamekuwepo na wagonjwa wanne waliohisiwa kuwa na Ebola ambao uchunguzi ulionesha hawakuwa na ugonjwa huo. Watatu kati ya wagonwja hao walikuwa ni wagonjwa wa malaria na mmoja uchunguzi wake bado unaendelea. Wagonjwa wawili ni kutoka Dar es Salaam na wawili ni kutoka Geita na Nkasi. Wagonjwa hawa waliohisiwa walihudumiwa na walifanyiwa uchunguzi kwa kufuata tahadhari zote za ugonjwa wa Ebola. Hii imeonesha utayari wetu wa kukabiliana na janga hili. Pamoja na kutokuwepo kwa mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitika kuwa na ugonjwa huu.
Tumejipanga vizuri kuzuia ugonjwa huu usiingie nchini. Tumechukua tahadhari na kujiandaa vilivyo kukabiliana na janga hili kwa kuchukua hatua zifuatazo:
(i) Tunacho Kikosi Kazi cha Taifa kinachoongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donald Mbando cha kukabiliana na ugonjwa huu katika ngazi ya taifa hadi Wilaya.
(ii) Tumekamilisha mpango wa kitaifa “Ebola Contingency Plan” na tumetenga Shilingi milioni 500 ikiwa ni fedha za awali za utekelezaji wa mkakati huo.
(iii) Tumeshaagiza Timu za Maafa za mikoa na wilaya kutekeleza mpango huo.
(iv) Tumesambaza vifaa “personal protective equipment” kwa watumishi wa afya katika mikoa yote, wilaya zote, hospitali zote za Rufaa na kanda 37, viwanja vya ndege vya Julius Nyerere, Kilimanjaro, Mwanza na Zanzibar. Tumesambaza pia dawa.
(v) Tumetenga kituo maalum tengefu (isolation unit) cha Wilaya ya Temeke na vituo vingine tengefu mikoani.
(vi) Tumechukua tahadhari kubwa kwenye viwanja vya ndege. Tumekwishafunga mitambo maalum ya vipima joto na dalili za wagonjwa wa Ebola katika viwanja vya Mwalimju Nyerere (2), Mwanza (1), Zanzibar (1) na kituo cha Namanga (1). Tumeagiza pia scanners 5 ambazo zimekwishawasili na zitafungwa katika viwanja vyetu.
(vii) Tumetoa mafunzo kwa watumishi wa afya wa mipakani na viwanja vya ndege. Tumetoa mafunzo hayo kwa watumishi 100 wa Dar es Salaam na 45 kutoka mikoa ya Arusha, Kagera, Rukwa, Mwanza, Kilimanjaro, Kigoma na Zanzibar. Tumepeleka watumishi watatu nchini Jamhuri ya Kongo kupata mafunzo maalum.
(viii) Tumeanza maandalizi ya kuboresha maabara zetu ili tuweze kufanya uchunguzi wa sampuli hapa hapa nchini. Kwa sasa, eneo zima la Afrika Mashariki tunategemea na tunatumia maabara ya Nairobi.
Viongozi wa ngazi zote hizi wamepatiwa mwongozo wa utekelezaji. Tunachoomba ni ushirikiano wa wananchi wote katika kuchukua tahadhari na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo mara tu mnapogundua dalili za ugonjwa huu kwa mtu ye yote.
Mchakato wa Katiba
Nilipozungumza na Taifa mwishoni mwa mwezi Julai, nilizungumzia mchakato wa Katiba. Nilielezea utayari wangu wa kufanya kila liwezekanalo kusaidia kufanikisha mchakato wa Katiba unaonndelea sasa. Kwa moyo huo, sikusita, nilipoombwa na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia (Umoja wa Vyama vyenye Uwakilishi Bungeni) Mhe. John Momose Cheyo kukutana nao na kufanya mazungumzo ya mashauriano. Kama mnavyojua tulikutana tarehe 31 Agosti, 2014 Mjini Dodoma. Tumekuwa na mazungumzo mazuri. Tumepeana kazi ya kufanya na tumekubaliana kukutana tena tarehe 08 Septemba, 2014 kuendelea na mazungumzo yetu. Kinachotia moyo ni ule ukweli kwamba kila upande umeonesha kiu na utayari wa kuzungumza. Tuyape nafasi mazungumzo haya yatutoe hapa tulipo na kutusogeza mbele kwa umoja na mshikamano.
CDA
Mwisho, suala la CDA: Wakati wa kuzundia barabara ya Dodoma – Fufu Mbunge wa Dodoma Mheshimiwa Malole alielezea kwa uchungu matatizo ya CDA. Nimewaagiza Wadau wakae tutakutana tarehe 07 Septemba, 2014 tupokee ushauri. Naomba muwe na subira.
Hitimisho
Wazee wangu;
Narudia tena kuwashukuru ndugu zangu wa Dodoma kwa mapokezi mazuri na ratiba nzuri iliyonipa nafasi ya kujifunza mengi kuhusu mkoa wenu. Naondoka nikiwa na kumbukumbu ya mambo mazuri yanayoendelea kufanyika hapa mkoani kuinua hali za maisha ya wananchi. Tafadhali ongezeni bidii. Mimi na wenzangu Serikalini tutaendelea kuwaunga mkono.
- Sep 05, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU KATIKA UFUNGAJI WA ZOEZI LA MEDANI LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA JWTZ ARUSHATAREHE 05 SEPT...
Soma zaidiHotuba
Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
Mhe. Dr Hussein Ally Mwinyi, Waziri wa Ulinzi na JKT;
Jenerali Davis Mwamnyange, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi;
Luteni Jenerali Samueli Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi;
Mhe. Magesa Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha;
Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi;
Maj. Gen. RM Muhuga, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa;
Wakuu wote wa Kamandi mliopo;
Majenerali wote mliopo;
Maafisa Wakuu;
Maafisa wadogo na Askari wote;
Wageni Waalikwa;
Pongezi
Nashukuru kualikwa na kushirikishwa kwenye kilele cha sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya kuzaliwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Natoa pongezi nyingi kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamnyange na viongozi wenzake kwa uamuzi wenu wa busara wa kuadhimisha siku hii muhimu katika historia ya Jeshi letu na nchi yetu kwa zoezi la medani linalohusisha Jeshi zima. Huu ni ubunifu wenye tija ingawaje ndugu zenu wa Dar es Salaam waliojiandaa kuona gwaride la kihistoria wamewa-“miss” sana.
Hongereni kutimiza nusu karne ya uhai wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Imekuwa miaka hamsini ya mafanikio makubwa. Mtu anapoangalia nyuma kwenye kumbukumbu za historia ya Jeshi letu lilivyokuwa Septemba 1, 1964 na lilivyo sasa, hatasita kutambua na kukiri kuwa tumepata mafanikio makubwa ya kujivunia. Kama kuna mtu haoni hivyo basi anatumia miwani ya mbao kusomea.
Historia ya JWTZ
Ndugu Makamanda, Wapiganaji na Wananchi;
Kama tujuavyo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanznia liliundwa kufuatia kuvunjwa kwa jeshi lililokuwepo wakati ule yaani Tanganyika Rifles kufanya uasi. Kwa kweli Tanganyika Rifles lilikuwa Jeshi tulilorithi kutoka kwa wakoloni. Kilichofanyika ni kubadili jina kutoka King African Rifles na kuwa Tanganyika Rifles lakini halikugeuka na kuwa Jeshi la nchi huru na la watu huru. Falsafa yake ilibakia kuwa ile ile ya mkoloni aliyeliunda, ndiyo maana walifanya waliyoyafanya. Kwa namna fulani basi, uasi uliipa nchi yetu fursa ya kuunda jeshi lake lenyewe lililojengwa kwa falsafa ya Uzalendo na kulinda maslahi ya nchi yao huru na watu wake. Iliwezesha kuunda Jeshi linalotokana na wananchi wazalendo na lipo kwa ajili ya ulinzi na maslahi ya wananchi na nchi yao.
Katika kuunda Jeshi jipya na kuvunjwa kwa Tanganyika Rifles, baada ya uasi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mwalimu Julius Nyerere alifanya uamuzi wa kuchukua vijana 1,000 wa TANU Youth League kuwa mbegu ya msingi ya kuunda Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Aidha, aliweka wazi na kuainisha shabaha, malengo na majukumu ya Jeshi letu kuwa ni kufanya mambo yafuatayo:-
i. Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
ii. Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
iii. Kufanya mafunzo na mazoezi ili kujiweka tayari kivita wakati wote;
iv. Kufundisha umma shughuli za ulinzi wa Taifa;
v. Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa;
vi. Kutoa huduma mbalimbali za kijamii;
vii. Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji mali kazi iliyofanywa kupitia Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Kujenga Uchumi; na
viii. Kushiriki ulinzi wa amani na ukombozi.
Tokea kuanzishwa kwake hadi sasa, Jeshi letu halijawahi kuacha misingi, shabaha na malengo ya kuanzishwa kwake. Jeshi jipya limezingatia sifa kuu tatu ambazo zilitofautisha jeshi hili na lile la Tanganyika Rifles. Limebaki kuwa Jeshi la Ulinzi wa nchi na sio la uvamizi. Ni Jeshi linalotokana na wananchi wa Tanzania kwa ajili ya wananchi wa Tanzania na siyo jeshi la kukandamiza wananchi. Na, ni Jeshi la Ukombozi na kulinda amani lilotumika kwenye harakati za ukombozi wa Afrika na kulinda amani duniani.
Mafanikio ya JWTZ
Ndugu Makamanda, Wapiganaji na Wananchi;
Mafanikio mengi makubwa na madogo yamepatikana katika miaka 50 ya uhai wa JWTZ. Tunaweza kusema kwa kujiamini kabisa kuwa, moja ya mafanikio makubwa ya miaka 50 ya nchi yetu ni kuwa na Jeshi imara, lenye uzalendo, weledi, utii na nidhamu ya hali ya juu. Hili ni jambo ambalo mataifa kadhaa hususan ya Afrika yameshindwa kulifanikisha. Tunaweza kusema, amani, utulivu na usalama tulio nao nchini kwetu kwa miaka 50 sasa umechangiwa sana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kutimiza ipasavyo wajibu wake.
Hakika JWTZ limetekeleza vyema majukumu yake ya wakati wa amani na wakati wa vita kwa weledi na ufanisi mkubwa. Mafanikio ni mengi, kwa uchache niruhusuni niyataje yafuatayo:-
i. Kushiriki na kufanikisha harakati za ukombozi barani Afrika kwa kufundisha majeshi ya vyama vya Ukombozi, na ushiriki wa moja kwa moja kwenye vita vya ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika huko Msumbiji, Angola, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini;
ii. Kulinda uhuru na mipaka ya nchi yetu, kwa nyakati mbalimbali limeweza kuzima matishio dhidi ya uhuru na umoja wa nchi yetu. Na mfano mkubwa ni pale Jeshi lilipofanikiwa kuyafukuza majeshi ya uvamizi ya Dikteta Idd Amin na kulisambaratisha kabisa Jeshi hilo;
iii. Kushiriki kwa ukamilifu na kwa mafanikio makubwa kwenye operesheni ya kulinda amani nchini Liberia, Darfur, Lebanon, Ivory Coast, Visiwa vya Shelisheli, Visiwa vya Comoro na hivi majuzi DRC kuyatoa majeshi ya waasi ya M23.
iv. Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika shughuli za uokoaji wakati wa maafa mbalimbali yaliyotokea nchini, yakiwemo mafuriko ya Dar es Salaam, Kilosa, ya kuzama meli kule Zanzibar;
v. Kutoa huduma mbalimbali kwa jamii zikiwemo elimu na afya. Watanzania wengi wanafaidika na huduma za shule na hospitali zinazomilikiwa na jeshi;
vi. Kukuza elimu ya kujitegemea kwa vijana wetu kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).
Changamoto za JWTZ
Ndugu Makamanda, Wapiganaji na Wananchi;
Dunia ya leo inayo changamoto mpya za ulinzi na usalama tofauti na zile zilizokuwepo miaka 50 iliyopita wakati JWTZ lilipoanzishwa. Changamoto mpya za kiusalama zimekuja na matishio mapya ya kiusalama ambayo yamesabishwa na hali ya sasa ya kisiasa na kiuchumi duniani na mapinduzi ya kiteknolojia. Kwa ajili hiyo kuna mabadiliko ya aina ya adui na mbinu zake. Leo hii tunazo changamoto za ugaidi, uharamia, ujangili, na hujuma za kiuchumi. Matishio haya na mengine mengi ya aina hiyo yanahitaji mbinu na utaalam mpya za mapambano. Jeshi letu halina budi kujiandaa na kujiweka tayari wakati wote dhidi ya matishio haya mapya ya kiusalama.
Ahadi ya Serikali
Ndugu Makamanda, Wapiganaji na Wananchi;
Sisi Serikalini tunayo azma ya kuendelea kuliimarisha jeshi letu na kuliweka katika hali ya utayari wakati wote. Dhamira yetu ni kuwa na jeshi la kisasa, lenye uwezo mkubwa wa mapigano. Kwa ajili hiyo tutaendelea kuwekeza fedha zaidi katika kulipatia Jeshi letu silaha na zana za kisasa, vitendea kazi na vyombo vya usafiri, ardhini, majini na angani. Pia tutaendelea kuboresha maslahi na huduma bora kwa wanajeshi wetu. Ninyi ni mashahidi wa kile tulichokifanya na tunachoendelea kufanya. Nawahakikishia tuko tayari kufanya zaidi.
Tunatambua kuwa wakati wa amani ndio wakati wa kuimarisha jeshi. Historia imetufundisha hivyo wakati wa vita yetu dhidi ya majeshi ya Nduli Idd Amin. Tunaitumia vizuri fursa hiyo. Ukweli huu ulisisitizwa pia na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere katika hotuba yake aliyoitoa katika sherehe za Mashujaa tarehe 1 Septemba, 1979, ambapo alipokea wanajeshi wetu waliokuwa wakirejea kutoka vitani. Alisema:
”Vita sasa vimekwisha. Lakini kusema hivyo maana yake si kusema kuwa twaweza kulegeza mikanda. Hatuna wazo lolote la kumvamia mtu yoyote. Lakini ni vyema kuwa tayari wakati wote kwa lolote linaloweza kutokea. Hilo ni funzo moja kubwa tulilolipata kutokana na vita hii”.
Tumekuwa wanafunzi wazuri wa somo hilo. Ndiyo maana katika Awamu yangu ya uongozi, tumewekeza sana katika kuongeza uwezo kimapigano wa jeshi letu katika nyanja zote. Kwa upande wa mafunzo, pamoja na kuimarisha vilivyopo vyuo na shule zilizopo, nyingine mbalimbali zimejengwa katika kipindi hiki. Hii ni pamoja na NDC. Napenda kuwahakikishia kuwa tutajenga Defence Intelligence Colleges, School of Military Police, School of Special Forces, School of Armour na Comprehensive Training Centre, Marines, hali kadhalika Command and Staff College ya Duluti tutaimaliza.
Tumelijengea uwezo mkubwa jeshi letu kwa zana na vitendea kazi kama mlivyojionea wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano na katika zoezi hili la leo. Lakini kazi bado inaendelea. Kwa upande wa huduma ya afya pamoja na kazi iliyofanywa ya kuimarisha hospitali za jeshi, tunakamilisha matayarisho ya ujenzi wa hospitali kubwa ya kijeshi. Ujenzi wa nyumba 6,064 katika Awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 10,000 unaendelea na utakamilika Desemba, 2014. Ujenzi wa nyumba 3,936 zilizobaki utaendelea baada ya awamu ya kwanza.
Matarajio yetu kwa JWTZ
Ndugu Makamanda, Wapiganaji na Wananchi;
Wananchi wa Tanzania wanayo mapenzi makubwa na Jeshi letu, maana ni jeshi lao na linatokana na wao. Wameishi na jeshi hili vizuri na wamefaidika na huduma za kijamii zitolewazo na jeshi lao. Wanayo matumaini makubwa kuwa mtaendelea kutii viapo vyenu, mtailinda Katiba ya nchi na mtaendelea kuwalinda wakati wote na kusaidiana nao wakati wa majanga. Ninyi ni kimbilio la Watanzania wote.
Matarajio haya ya wananchi ndiyo matarajio yangu na wenzangu wote serikalini. Uzoefu wetu wa miaka 50 unatupa kila sababu ya kuziangalia nyakati za mbele yetu kwa matumaini makubwa. Ninapotembelea vikosi na kujionea kazi zenu na utayari wenu kivita, hujisikia vizuri kama Amiri Jeshi Mkuu wenu natembea kifua mbele kote niendako, maana muyafanyayo siyo tu yananipa raha bali yananipa heshima kubwa hapa nchini na nje ya nchi. Nina imani kuwa kwa sasa Jeshi letu lipo katika kiwango cha juu cha utayari kivita kwa vifaa na watu.
Kumbukumbu ya Mashujaa waliotutoka
Ndugu Makamanda, Wapiganaji na Wananchi;
Tunapoadhimisha miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, tunawakumbuka na kuwaenzi wale wanajeshi na viongozi waliotangulia, Marais na CDF na wapiganaji wetu waliolifia Taifa letu wakitekeleza wajibu wao kwa taifa katika mstari wa mbele. Hawa hawakupata bahati ya kuwa nasi siku ya leo tunapoadhimisha miaka 50 ya JWTZ. Leo tunawakumbuka mashujaa wetu hawa kwa fahari. Kamwe hatutasahau mchango wao na kujitoa kwao mhanga ili sisi tuishi maisha ya heshima na tufurahie matunda ya uhuru wetu. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaenzi. Majina yao daima yataandikwa kwa wino wa dhahabu katika historia ya nchi yetu.
Hitimisho
Ndugu Makamanda, Wapiganaji na Wananchi;
Sasa tunaianza safari ya miaka 50 ijayo. Tunaianza tukiwa na matumaini makubwa ya kupata maendeleo makubwa zaidi miaka na miongo ijayo. Sina shaka hata kidogo kwamba Jeshi letu litapata mafanikio makubwa zaidi. Jeshi la Wananchi wa Tanzania halijawahi kushindwa na halitaweza kushindwa na jambo. Daima kumbukeni wosia wa Baba wa Taifa wakati akizindua JWTZ aliposema, “Moyo kwanza kabla ya silaha”.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JWTZ.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
- Aug 27, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWENYE UZINDUZI WA ZOEZI LA UWEKAJI MAWE YA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI, NGARA TAREHE 27 AGOSTI, 2014
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza, Rais wa Jamhuri ya Burundi,
Waheshimiwa Mawaziri kutoka Burundi na Tanzania,
Mheshimiwa Issa Ntambuka, Balozi wa Burundi nchini Tanzania,
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya za Burundi na Tanzania waliopo,
Makatibu Wakuu na Watendaji mbalimbali wa Serikali za nchi zetu mbili,
Ndugu wananchi, Mabibi na Mabwana,
Shukrani
Ni furaha kubwa sana kwangu kukukaribisha Tanzania Mheshimiwa Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi na ujumbe wako kwa ajili ya shughuli hii muhimu na ya kihistoria katika uhusiano wa nchi zetu mbili. Wewe na mimi kuwepo Mugikomero kuzindua zoezi la uwekaji wa mawe ya mpaka baina ya Burundi na Tanzania ni kielelezo tosha cha uhusiano mwema, udugu na urafiki uliopo kati ya nchi zetu mbili na watu wake.
Uhusiano wa Tanzania Burundi
Kama sote tujuavyo nchi zetu tatu za Burundi, Rwanda na Tanganyika sasa Tanzania Bara, kabla ya Vita Kuu ya Kwanza tulikuwa nchi moja chini ya utawala wa Wajerumani na kujulikana kama German East Africa. Ni baada ya Vita Kuu hiyo na Wajerumani kushindwa ndipo tukawa nchi tatu yaani Tanganyika chini ya utawala wa Waingereza na Burundi na Rwanda zikiwa nchi mbili chini ya Wabelgiji.
Umuhimu wa Kuhakiki Mpaka
Ndugu Wananchi,
Mnamo tarehe 5 Agosti 1924, ndipo Mkataba wa Mpaka wa nchi zetu hizi mbili, ulipotiwa saini. Leo miaka 90 baadae tupo kwenye mchakato wa kuhakiki mpaka wetu. Zoezi hili litapelekea nchi zetu kuwa na Mkataba mpya wa Mpaka ambao sasa utakuwa ni wetu wenyewe. Kama zilivyo nchi nyingi za Kiafrika, Tanzania na Burundi zilirithi mpaka uliopo kutoka kwa waliokuwa watawala wetu enzi za ukoloni. Mpaka huu haujafanyiwa mapitio wala kuimarishwa tangu nchi zetu zipate uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita. Katika kipindi hicho kumekuwepo na mabadiliko mbalimbali ikiwemo ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi na kimaendeleo katika maeneo ya mipakani. Aidha katika baadhi ya maeneo hata alama za mipaka zimekuwa vigumu kuzitambua ama kwa sababu ya kuchakaa au mawe kung’olewa. Hali hiyo haiwezi kuachwa kuendelea ilivyo.
Kwa kutambua ukweli kwamba kwa baadhi ya nchi utata kuhusu mipaka kuwa kiini cha migogoro, Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kilichofanyika Accra, Ghana tarehe 27 Juni, 2007 kilizitaka Nchi zote Wanachama wa Umoja wa Afrika kushirikiana katika kuimarisha mipaka yao ifikapo mwaka 2012. Hata hivyo, kipindi hicho kiliongezwa hadi kufikia mwaka 2017. Tumebaki na miaka mitatu kabla ya muda huo kukamilika, hivyo tunafanya zoezi hili ndani ya wakati wake.
Zoezi za Kuimarisha Mpaka
Ndugu Wananchi,
Nchi zetu ziliitikia wito huo wa Umoja wa Afrika (AU) kwa kuunda Kamati ya Pamoja ya Wataalamu ambayo ilikagua mpaka mzima na kubaini mawe yaliyong’olewa, mawe yaliyoharibiwa na kuainisha maeneo ambayo yalikuwa yanastahili kuongezewa mawe ili yaweze kuonekana vizuri miongoni mwa wananchi waishio mpakani.
Zoezi hili ni kubwa na lina changamoto zake. Mpaka wa Tanzania na Burundi una urefu wa Kilometa 450 ambao ni sawa na umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Lindi. Isitoshe mpaka hauko mijini, maeneo mengi yako misituni kwenye mabonde na milima. Ni magumu kuyafikia. Kwa upande wetu mpaka upo katika mikoa miwili ya Kagera na Kigoma na kwenye wilaya tano, kati ya hizo nne ni za Mkoa wa Kigoma (Kigoma, Kasulu, Kibondo na Kakonko) na moja ni hii ya Ngara iliyoko mkoa wa Kagera. Aidha, zoezi hili lina gharama kubwa na hatuna mfadhili hivyo linagharamiwa na nchi zetu mbili. Hali yetu tunaijua lakini tumeamua kufanya wenyewe jambo linaloonyesha utashi mkubwa wa Serikali zetu mbili katika kufanikisha zoezi hili muhimu sana.
Wito kwa Wananchi Waishio Mpakani
Ndugu Wananchi,
Lengo la zoezi hili sio kuwatenganisha wakazi wa mpakani ambao sote tunatambua kwamba shughuli zenu zinaingiliana na wengine mna uhusiano wa kifamilia na kidugu. Tunachokifanya leo ni kuimarisha mpaka na kuwatengenezea mazingira yenu kuwa mazuri zaidi. Kurasimisha mipaka kunafanya kazi za kiutawala mpakani kuwa rahisi baina ya mamlaka za pande zote mbili za mpaka. Kunaweka taratibu nzuri za kurasimisha utoaji wa huduma za umma na kuwezesha maingiliano ya kidugu na kibiashara baina ya watu wa Burundi na Tanzania. Hivyo, kitendo cha kuweka mambo sawa na sio kuwakwaza.
Ndugu wananchi,
Mpaka huu ni wenu. Nawaomba muwe walinzi wa mawe tutakayoweka leo na siku za usoni. Tusiyang’oe au kuyaharibu. Hakuna sababu ya kufanya yote hayo. Maana naambiwa hata baadhi ya sababu hazina maana tena na za kipuuzi. Kwa mfano, ipo dhana potofu kwamba kuna mali za thamani zilizofichwa kwenye mawe hayo. Nafurahi kwamba baadhi ya vijana wenu wanashirikishwa kwenye zoezi hili. Hivyo wao ndiyo mashahidi kwamba mawe haya ni mchanganyiko wa sementi, kokoto na mchanga. Hakuna dhahabu wala vito vingine vya thamani kama ambavyo ilivyokuwa ikidhaniwa miaka ya nyuma na hivyo kupelekea mawe zaidi ya sita kung’olewa. Sisi tuwe ni kizazi cha mwisho kuhujumu mawe ya mpakani kwa sababu yo yote ile. Lazima tutambue kwamba ni jambo baya kufanya hivyo na kwamba ni kujihujumu wenyewe kwani ujenzi wa kurudishia mawe yaliyong’olewa utagharamiwa kwa fedha ambazo zingefanya jambo linguine la manufaa.
Pongezi
Ndugu Wananchi,
Napenda kutumia fursa hii kuipongeza Kamati ya Wataalamu kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya mpaka tumefikia kuwa na hafla hii ya leo ya kihistoria. Wamefanya kazi yao kwa bidii, uaminifu, uadilifu na weledi wa hali ya juu. Wamejali na kuzingatia maslahi ya nchi zetu. Ni wazalendo wa dhati. Daima majina yao yatakuwemo kwenye vitabu vya kumbukumbu na historia ya nchi za Tanzania na Burundi.
Hatma
Baada ya kukamilisha zoezi la kuweka mawe ya Mpaka mzima, utaandaliwa Mkataba wa Mpaka baina ya Nchi zetu ambao utafuta ule wa Kikoloni wa Mwaka 1924. Ni matumaini yangu kwamba wataalamu wetu wataongeza kasi ili zoezi hili likamilike mapema. Kwa ajili hiyo, naziagiza Mamlaka zinazohusika kwa upande wa Tanzania kutimiza wajibu wake ipasavyo ili zisiwe sababu ya kuchelewesha au kukwamisha zoezi hili.
Ndugu wananchi;
Pamoja na zoezi hili linaloendelea, napenda kuwaarifu kuwa tunaendelea na uhakiki wa mipaka yetu na nchi za Msumbiji (kilometa 756), Zambia (kilometa 338), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (kilometa 473) na Kenya (kilometa 769). Baadae, tunakusudia, kufanya hivyo kwa mipaka yetu na Rwanda (kilometa 217), Uganda (kilometa 396) na Malawi (kilometa 475). Nazitaka Mamlaka zinazohusika kuhakikisha kuwa zoezi la kuhakiki Mipaka yote baina ya Tanzania na nchi tunazopakana nazo linafanyika kwa ukamilifu na ufanisi wa hali ya juu.
Hitimisho
Mheshimiwa Rais,
Ndugu Wananchi,
Marafiki huchora mipaka kwa mazungumzo na kalamu, maadui huichora kwa nguvu na kwa wino wa damu za binadamu. Mipaka ya kalamu hudumu kuliko ile itengenezwayo kwa damu. Mipaka ya kalamu hustawisha jamii wakati ile ya damu hufarakanisha, huzua chuki, hujuma na visasi. Kadri tunavyohakiki mipaka yetu kwa njia ya mazungumzo na kalamu, tunaondoa sababu na uwezekano wa nchi kugombana, kufarakana na hata kupigana kwa sababu ya mipaka. Sisi na Burundi ni ndugu, tumechagua njia ya mazungumzo na kalamu. Ni uamuzi sahihi, makini na wa busara na hekima kubwa. Tuzidi kumuomba Mungu atujalie na kutuongoza iwe hivyo kwa nchi zote tunazopakana nazo.
Ndugu wananchi,
Naomba nimalizie kwa kusisitiza mambo makuu matatu;
- Kwanza, narudia wito wangu kwa wakazi wote waishio maeneo ya mipakani kulinda alama za mipaka kwani wao ndio walinzi wa kwanza wa mawe hayo.
- Pili, naitaka Wizara ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa kuhakikisha kuwa Serikali za Mikoa yenye mipaka ya kimataifa zinapanga bajeti kwa ajili ya kulinda alama za mipaka. Hakikisheni eneo la meta 12.5 kutoka mpakani (buffer zone) haliingiliwi kwa shughuli zozote ikiwemo ujenzi na kilimo.
- Tatu na mwisho nazitaka Mamlaka zote zinazohusika zihakikishe kuwa mazoezi ya upimaji wa mpaka huu na mipaka mingine yanakamilika mapema iwezekanavyo.
Mwisho, nakushukuru tena Mheshimiwa Rais kwa upendo na ushirikiano wako. Wewe Mheshimiwa Rais, Serikali na watu wa Burundi ni rafiki wa kweli na ndugu wa Tanzania. Nami nakuhakikishia hapatakuwa na upungufu wa ushirikiano kwa upande wangu na wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Karibu sana.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza!
- Aug 14, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWEE, KATIKA UFUNGUZI WA KONGAMAMO LA KWANZA LA DIASPORA HOMECOMING AND GALA DINN...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu;
Mheshimiwa Bernard Kamilius Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
Waheshimiwa Mawaziri;
Ndugu Emmanuel Mwachulla, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Diaspora Initiative;
Mwakilishi wa International Organization for Migration (IOM);
Wageni Waalikwa;
Wana-Diaspora;
Mabibi na Mabwana;
Leo tunaanza mwanzo mpya katika historia ya uhusiano baina ya Watanzania waishio ughaibuni na Watanzania waishio nchini. Kwa mara ya kwanza tunawakutanisha hapa nchini Watanzania waishio ughaibuni na Watanzania wenzao na taasisi zetu za hapa nchini. Toka tumeanza kampeni hizi za kuhamasisha Watanzania waishio nje kushiriki katika maendeleo hapa nchini, hatujawahi kuwa na mkutano kama huu. Tumefanya mikutano mingi nje ya nchi ya kuwatembelea huko mliko, kuzungumza nanyi na kuwahamasisha kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa. Safari hii, ni kinyume chake. Mmekuja nyumbani kujumuika nasi. Hii ni hatua kubwa na mwanzo mpya.
Nakupongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kuliwezesha jambo hili kuwa. Nawashukuru kwa jitihada mnazochukua kusaidia kusukuma agenda hii ya Diaspora na maendeleo. Matunda haya ya leo ni matokeo ya kazi yenu nzuri. Nakupongeza pia Ndugu Emmanuel Mwachulla na wenzako kwa kubuni wazo hili jema, na kuishirikisha Serikali katika kulifanikisha. Uamuzi wenu wa kulianzisha wazo hili ni mzuri kwani unaondoa ile dhana kuwa suala hili la Diaspora ni suala la sisi viongozi tu na siyo agenda yenu. Kujitokeza kwenu kunatutia nguvu na moyo wa kuendelea kuhamasisha. Ni ukweli usiopingika kuwa sauti yenu katika suala hili la ushirikishaji wa diaspora ina uzito mkubwa zaidi kuliko hata sauti yetu sisi.
Kauli Mbiu ya Mkutano
Mabibi na Mabwana;
Nimevutiwa na kauli mbiu ya mkutano huu “Connect, engage, inform and invest”, yaani unganisha, wasiliana, toa habari na wekeza”. Kuwafikia wana diaspora ilikuwa ni moja ya malengo makuu ya Serikali yetu kwa sababu tunaamini kuwa jukumu la maendeleo ya Tanzania ni la kila Mtanzania po pote pale alipo. Ndugu zetu walioko nje nao kama walivyo waliopo nchini wana wajibu wa kuchangia pia kwa kile wanachokiweza. Nilipokuwa nakutana na Watanzania kote nilikopita nje ya nchi nilifafanua mambo matatu muhimu kwa Watanzania: La kwanza ni kukumbuka nyumbani (East West Home is Best). La pili, wajenge nyumbani na wasaidie ndugu zao, na la tatu wasaidie maendeleo ya nchi kwa kuleta vitega uchumi, kutafuta masoko ya bidhaa, walete teknolojia na walete ujuzi na maarifa.
Umuhimu wa Diaspora kwa Uchumi wa Taifa
Mabibi na Mabwana;
Umuhimu wa Diaspora katika uchumi wa nchi zao za asili ni suala ambalo limepewa mkazo sana katika dunia ya leo. Inakadiriwa kuwa watu wapatao milioni 220 duniani ambao ni asilimia 3 ya watu wote duniani wanaishi nje ya nchi zao za asili. Benki ya Dunia imebaini kuwa, kiasi cha dola za Marekani bilioni 581 zimetumwa na Wana-Diaspora duniani kote kwenda kwenye nchi zao za asili mwaka 2013. Kiasi hiki kinatarajiwa kuongezeka kufikia dola za Marekani bilioni 681 ifikapo mwaka 2016. Nchi zinazoendelea zinatarajiwa kupata ongezeko la asilimia 78, za fedha hizi kutoka dola za Marekani bilioni 404 mwaka 2013 hadi dola bilioni 516 mwaka 2016. Kiasi hiki cha sasa kinakadiriwa kuwa ni mara nne ya fedha ambazo nchi za Afrika zinapokea kama misaada kutoka kwa wafadhili wa nje. Itoshe tu kusema kuwa diaspora ni chanzo muhimu cha kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Pamoja na ukubwa wa mapato hayo, bado Tanzania inavuna kiasi kidogo sana kutoka kwa Watanzania waishio nje. India na China peke yake zinavuna jumla ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 kwa mwaka, na Nigeria kiasi cha dola bilioni 21 katika mwaka 2013. Kwa mujibu wa Ripoti ya UNCTAD ya mwaka 2012 kuhusu ushirikishwaji wa diaspora, inakadiriwa kuwa Tanzania ilipokea kiasi cha dola za Marekani milioni 10.2 tu (sawa na shilingi bilioni 16) mwaka 2011. Kwa ulinganisho wao, kiasi cha dola za Marekani milioni 4.5 zilitoka kwa Watanzania waishio Uingereza, dola milioni 3.2 kwa wale waishio Canada na dola milioni 2.5 kwa wale waishio Kenya, ingawa takwimu hizi hazihusishi fedha zilizorejeshwa nchini kwa njia zisizo rasmi bado. Kiasi hiki ni kidogo sana ikilinganishwa na Kenya iliyopata dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2014.
Changamoto kubwa tuliyonayo nchini ni kutokuwepo na takwimu rasmi za kiasi cha fedha tunachopokea kutoka nje kutokana na fedha nyingi kupita katika mikondo isyo rasmi ya fedha. Naamini kuwa tukiweka mufumo yetu sawa upo uwezekano mkubwa wa kiwango hiki kuongzeka.
Hapana shaka ipo fursa ya Tanzania kuvuna zaidi kutoka kwa Diaspora yake. Hapana shaka pia kwamba ili tuweze kufanikiwa hatuna budi kuwekeza katika kuweka mazingira mazuri ya kisera na kisheria. Hatuna budi kuondoa vikwazo vinavyowazuia Diaspora wetu kushiriki ujenzi wa taifa. Maana uzoefu umeonyesha pale ambapo mazingira ni wezeshi, michango ya Diaspora imekuwa ni mikubwa zaidi. Mfano, Diaspora wa Salvador wanakadiriwa kutuma nyumbani kwao asilimia 16 ya mapato yao binafsi, Bangladesh na Philippines ni asilimia 12 na Senegali ni asilimia 9.
Mabibi na Mabwana;
Sisi katika Serikali tumechukua hatua kubwa katika kurekebisha hali hii ili kujenga mazingira wezeshi. Ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2005 na ile ya 2010 ilitoa maelekezo mahsusi kuhusu kutambua na kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha diaspora kuchangia maendeleo ya nchi yetu. Tumeunda Idara ya kushughulikia Diaspora ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje, tumeunda nafasi ya uratibu ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tumefanya kampeni kubwa ya kuhamasisha wadau wa ndani kutambua na kushirikisha diaspora, na nimetumia kila fursa nilipotembelea nje kukutana nanyi na kuwahamasisha kuchangia maendeleo ya nchi. Aidha, tumewashirikisha diaspora katika mchakato wa Katiba mpya.
Matokeo ya jitihada hizi yameanza kuonekana, ndiyo maana kumekuwepo na ongezeko la fedha zinazotoka Diaspora kama takwimu zinavyoonyesha. Aidha, taasisi za fedha, taasisi za nyumba na mifuko ya jamii nayo imesikia wito huu na wameanza kutoa huduma mahsusi kwa Watanzania walioko nje na watu wenye asili ya Tanzania waishio nje ya nchi. Ni dhamira yetu kuona huduma hizi zikipanuka na kuboreshwa siku hadi siku. Serikali iko katika hatua za kukamilisha sera ya diaspora itakayoshirikisha na kuunganisha juhudi za wadau wote katika kuweka mazingira mazuri kuwezesha ushiriki wenu kwa ukamilifu.
Madai ya Uraia Pacha
Mabibi na Mabwana;
Ninapokutana nanyi huko nje na hivi majuzi nilipokuwa Washington D.C na Houston, Texas, kilio chenu kikubwa ni kupitishwa kwa haki ya Mtanzania wa kuzaliwa kutopoteza uraia wake iwapo atapata uraia wan chi nyingine. Suala hili ni la kikatiba na si la mamlaka ya Rais pekee. Katika Rasimu, suala la Uraia limefafanuliwa katika Sura ya 5 ya Rasimu ya Tume, Ibara ya 59 inazungumzia Hadhi ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania. Yamekuwepo maoni kutoka kwenu kuwa, Ibara hii ilivyowekwa haijakata kiu yenu ya kutaka kuendelea na kuwa na haki ya kutopoteza uraia wa asili wa Tanzania. Mnasema kwamba pamoja na kuwa pendekezo la kupewa “Hadhi” si haba, bado hadhi hiyo sio mbadala wa uraia wa asili.
Mimi nilitimiza ahadi yangu kwenu kwa kuteua Mjumbe mmoja kutoka Diaspora, Bw. Kadari Isingo ili awawakilishe kwenye Bunge la Katiba. Ni juu yenu kumtumia vizuri na pia kuelimisha umma juu ya dai lenu hili. Katika hilo la Uraia, mtumie ushawishi uleule, mpaze sauti vilevile kama mnavyofanya katika mitandao ya jamii kwenye masuala mengine.
Matarajio ya Watanzania Walioko Nchini
Mabibi na Mabwana;
Watanzania walioko hapa nyumbani wanayo matarajio makubwa kutoka kwenu. Wanayo imani kuwa, kwenda kwenu nje kuhemea kutaongeza neema kwenye familia zenu na taifa kwa ujumla. Wanatazamia kuwa maisha yenu huko nje ni bora zaidi na mmekwenda kuvuna ili mjenge na kuendeleza kwenu. Wanategemea mkiwa huko mtawasaidia ndugu zenu kutatua changamoto za maisha. Muonapo fursa za kusaidia maendeleo nchini mtazileta. Mtaleta fedha, mtaleta vitega uchumi, teknolojia za kisasa pamoja na ujuzi na maarifa. Mkiona fursa za ajira mtawasaidia na wenzenu wapate. Kwa wale waliopata bahati ya kupata ujuzi mzuri, tungependa kuwaona mkiutumia ujuzi huo na maarifa yenu kuendeleza kwenu. Kunapotokea nafasi za ajira jitokezeni kuomba. Najua hatuwezi kuwalipa mishahara mikubwa kama ya huko mliko lakini penye utashi wa kuchangia maendeleo kiasi cha mshahara si kigezo pekee.
Ahadi ya Serikali
Mabini na Mabwana;
Sisi katika Serikali hatutarudi nyuma katika azma yetu na kuendelea kuwashirikisha katika maendeleo yetu hapa nchini. Tunayo kila sababu ya kufanya hivyo na tayari tunafanya hivyo. Tutaimarisha sera, mifumo na sheria ili kuweka uwanja wazi wa kuwawezesha kuchangia maendeleo ya hapa nchini. Tunataka mtumie mifumo rasmi na salama ya kutuma fedha, kumiliki mali na kushiriki katika mifumo ya kiuchumi. Hii itawaepusha na hasara mnazoweza kupata pale mnapojaribu kuwekeza nyumbani kwa kutumia fedha kwa njia zisizo rasmi kupitia kwa ndugu, jamaa na marafiki. Nafurahi kwamba katika mkutano huu mtapata nafasi ya kuelezwa yale tuliyopanga kufanya na tunayofanya kwa ajili hiyo. Zitumieni fursa hizo.
Hitimisho
Mbibi na Mabwana;
Nawapongeza tena kwa mwitikio wenu mkubwa na zaidi kwa kufanya mkutano huu nchini. Mmedhihirisha tena ule usemi wetu wa Kiswahili wa “mtu kwao”. Tunafarijika sana mnapotuonyesha kuwa mnakumbuka nyumbani kwenu. Jisikieni kuwa mko nyumbani na muwe huru kuja wakati wote maana “mwenda kwao si mtoro” sisi tunawapokea kwa mikono miwili maana ninyi ni watoto wa nyumbani. Pendeni kwenu, “mkataa kwao mtumwa”.
Asanteni kwa kunisikiliza.
- Jul 31, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI, 2014
Soma zaidiHotuba
Utangulizi
Ndugu wananchi;
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kwa mara nyingine tena kuzungumza na taifa juu ya masuala muhimu yanayohusu nchi yetu. Mwezi wa Saba tunaoumaliza leo ulikuwa na matukio mengi baadhi yakiwa makubwa na kushtusha na mengine yalikuwa matukio ya kawaida.
Mashambulio ya Mabomu
Ndugu Wananchi;
Tarehe 3 Julai, 2014 na tarehe 07 Julai, 2014 kulitokea mashambulizi ya mabomu nyumbani kwa Sheikh Sudi Ally Sudi na katika mgahawa wa Vama kwa mfuatano huo. Kabla ya hapo, kulikuwa na matukio mengine matatu: Kanisa la Olasiti tarehe 5 Mei, 2012, Mkutano wa Kampeni wa CHADEMA tarehe 15 Juni, 2013 na Baa ya Arusha Night Park tarehe 13 Aprili, 2014. Hali kadhalika, tarehe 13 Juni, 2014 kulitokea shambulizi la mabomu katika eneo la Darajani, Zanzibar.
Kila lilipotokea shambulizi uchunguzi ulifanyika na watuhumiwa kukamatwa. Lakini, watuhumiwa waliokamatwa safari hii wanaelekea kutoa sura nzuri zaidi ya mtandao wa watu wanaofanya vitendo hivi vya kikatili pale Arusha na kwingineko nchini. Watu 38 wameishafikishwa Mahakamani, wengine 8 watafikishwa Mahakamani kesho na uchunguzi na msako unaendelea kote nchini kuwapata watuhumiwa wengine.
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri iliyotufikisha hapa tulipo sasa. Tunawaomba waongeze bidii, maarifa na ushirikiano mpaka wote waliohusika wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Aidha, natoa pongezi na shukrani maalum kwa wananchi wema waliotoa taarifa zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa. Napenda kutumia nafasi hii kuwasihi wananchi wenye taarifa kuhusu wanaotafutwa au ye yote anayejihusisha na vitendo hivi viovu watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama ili hatua zipasazo zichukuliwe.
Kutupwa Viungo vya Binadamu
Ndugu Wananchi;
Tarehe 22 Julai, 2014, katika Bonde la Mto Mpiji lililopo eneo la Bunju Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, viligunduliwa viungo vya binadamu na baadhi ya vitendea kazi vya madaktari vikiwemo aprons na gloves. Viungo hivyo vilivyokutwa vimekakamaa na kuhifadhiwa katika mifuko myeusi 85, vilikuwa vimetupwa jana yake tarehe 21 Julai, 2014. Tukio hilo lilileta taharuki na hofu kubwa katika Jiji la Dar es Salaam na nchini kwa ujumla.
Uchunguzi uliofanywa uligundua kuwa viungo hivyo vilikuwa vinatumika kufundishia wanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu cha Tiba kilichoko Mbezi Beach maarufu kwa jina la IMTU. Ni utaratibu wa kawaida kwa vyuo vikuu vya udaktari nchini na kote duniani kutumia miili ya wanadamu waliofariki kufundishia. Hata hivyo, pale viungo hivyo vinapokuwa havihitajiki tena kwa shughuli hiyo, zipo taratibu zake za kuvisitiri ambazo hazikufuatwa. Bahati nzuri mamlaka husika zimeona kasoro hiyo na hatua zimeanza kuchukulikuwa. Tuziachie mamlaka hizo kuchukua hatua zipasazo kwa mujibu wa madaraka yao na kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazotawala shughuli za namna hiyo. Ni matumaini yangu kuwa yaliyofanywa na IMTU hayatafanywa tena na Chuo hicho wala chuo kingine cho chote hapa nchini.
Ziara Yangu Mikoani
Ndugu Wananchi;
Katika mwezi huu wa Julai, nimefanya ziara katika ya mikoa ya Tanga na Ruvuma. Nimefurahishwa sana na hatua kubwa ya maendeleo waliyopiga wananchi wa mikoa hiyo. Pamoja na mchango wa Serikali, ari na mwamko mkubwa wa kujiletea maendeleo walionao viongozi na wananchi wa mikoa hiyo vimechangia sana katika kuongeza kasi ya maendeleo na mafanikio yanayoendelea kupatikana. Katika ziara hizo, nilizindua miradi iliyokamilika na kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile ya barabara, umeme,maji, afya, elimu, majengo ya Serikali, nyumba na kadhalika.
Nimepata faraja kubwa kupata taarifa kuwa ahadi zangu nyingi na zile zilizomo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi zimekamilika na zingine ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Ndoto ya miaka mingi, kabla na baada ya Uhuru, ya wananchi wa Mikoa ya Kusini ya kutaka Mikoa yao ifunguke na kuunganishwa na mikoa mingine kwa barabara za lami sasa kuna uhakika wa kukamilika. Barabara ya kutoka Mbinga, Songea hadi Namtumbo iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Marekani imekamilika na tuliizindua. Tuliweka mawe ya msingi ya kujenga barabara ya lami kutoka Namtumbo, Tunduru, Mangaka hadi Mtambaswala kwenye Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali ya Japan. Barabara ya kutoka Mangaka hadi Masasi iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japan imekamilika na tuliizindua. Katika barabara ya kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay kimebaki kipande cha kilometa 66 kutoka Mbinga kwenda Mbamba Bay ambacho hakikuwa na mpango wo wote wa kuwekewa lami kwa sasa. Bahati nzuri, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Bibi Tonia Kandiero alitangaza pale Namtumbo kuwa Benki yake itafadhili ujenzi wa barabara hiyo. Mambo sasa yamekamilika.
Kule Masasi mkoani Mtwara na Nachingwea mkoani Lindi tulizindua kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Mbwinji unaomaliza tatizo kubwa la maji kwa miji hiyo kwa miaka mingi ijayo.
Nyumba za Bei Nafuu
Ndugu Wananchi;
Nikiwa wilayani Mkinga na katika Manispaa ya Songea nilizindua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirila la Nyumba la Taifa (NHC). Nyumba hizo za vyumba viwili na vitatu zinauzwa kwa bei ya shilingi milioni 31 hadi 42. Wenzetu wa NHC walinieleza utayari wa kujenga nyumba zaidi endapo watapatiwa maeneo na Halmashauri za Wilaya na Miji. Walinilalamikia kuwa hawapati ushirikiano wa kutosha kutoka mamlaka husika. Nilipokuwa Mkinga na Songea niliagiza Halmashauri hizo na nyinginezo nchini kutenga maeneo kwa ajili ya NHC na Mifuko ya Hifadhi za Jamii yote ili waweze kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya wafanyakazi na wananchi kwa ujumla.
Hii ni fursa ya aina yake kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kuweza kujipatia nyumba kwa urahisi. Halmashauri zisiwe kikwazo wakati ardhi imejaa tele na kila wakati wanapima viwanja vipya. Jambo lingine zuri waliloniambia viongozi wa NHC ni kwamba zipo Benki ambazo wanashirikiana nazo kutoa mikopo kwa watu wanaonunua nyumba zao. Ni matarajio yangukwamba uongozi wa Halmashauri zote nchini utaitikia maelekezo yangu na kwamba utatenga maeneo kwa ajili ya mashirika yetu hayo.
Matibabu kwa Wazee
Ndugu Wananchi;
Nilipokuwa wilaya ya Kilindi nilifurahishwa sana na utaratibu wa kuwapatia wazee huduma ya matibabu. Kama mjuavyo Sera ya Afya inataka wazee na watoto wa chini ya miaka mitano watibiwe bure katika hospitali za Serikali. Bahati mbaya vitambulisho wanavyopata wazee vimekuwa havithaminiwi ya kutosha. Kwa sababu hiyo, nafuu wanayostahili kupata imekuwa haipatikani kwa urahisi na wengine huikosa kabisa.
Katika Wilaya ya Kilindi, Halmashauri ya wilaya imeamua kuwakatia wazee hao Bima ya Afya inayotolewa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na hivyo kuondoa kabisa migogoro inayohusiana na vitambulisho vya wazee vilivyokuwepo kabla. Kwa kuzingatia malalamiko ya mara kwa mara ninayoyapata kutoka kwa wazee kuhusu matibabu, nashauri Halmashauri zote nchini ziige mfano wa Wilaya ya Kilindi. Kama Kilindi wameweza kwa nini wengine washindwe.
Ndugu Wananchi;
Katika mikoa hii miwili nilipokea taarifa za kutia moyo kuhusu juhudi za wananchi na Serikali katika kupanua fursa za elimu. Vijana wengi wenye umri wa kujiunga na shule za msingi wanafanya hivyo na wale wote wanaofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata fursa ya kwenda sekondari. Hatuna tena tatizo la fursa. Pamoja na mafanikio hayo mazuri, taarifa za wanafunzi wengi kushindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari, zimenishtua na kunisikitisha sana.
Katika Mkoa wa Tanga kwa mfano, kati ya wanafunzi 50,921 walioanza darasa la kwanza mwaka 2007 , ni wanafunzi 41,017 tu ndiyo waliofanya mtihani mwaka 2013. Hivyo basi, wanafunzi 9,904 ambao ni sawa na asilimia 19.4 hawakumaliza elimu ya msingi. Kwa upande wa sekondari, katika mkoa wa Ruvuma, kwa mfano, kati ya wanafunzi 18,892 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2010 ni wanafunzi 9,968 sawa na asilimia 52.76 ndiyo waliofanya mtihani wa kidato cha nne. Hivyo basi, wanafunzi 8,924 sawa na asilimia 47.2 hawakumaliza elimu ya sekondari. Taarifa za namna hii nilizipata pia katika ziara zangu ya Mikoa ya Kagera, Geita na Simiyu. Nina kila sababu ya kuamini kuwa hali ni hiyo hiyo kwa Mikoa mingine mingi nchini. Kwa kweli kiwango hiki cha wanafunzi wanaoshindwa kumaliza elimu ya msingi na sekondari ni kikubwa mno. Kinanisikitisha sana, hakikubaliki na hakiwezi kuachwa kiendelee.
Ndugu Wananchi;
Kwa maoni yangu wazazi, walimu na viongozi wanao wajibu maalumu wa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanahudhuria masomo shuleni tangu wanapoanza mpaka wanapomaliza masomo yao. Huu ni wajibu wa lazima na siyo hiari. Ni wajibu wa kisheria. Kwa hiyo, nimeagiza kwamba, wazazi, walimu, Maafisa Elimu wa Wilaya wa Msingi na Sekondari na Kamati husika katika Halmashauri zote nchini ziwajibike ipasavyo kuhakikisha kuwa utoro mashuleni unakomeshwa. Ajenda ya mahudhurio shuleni iwe ni ya kudumu katika vikao vyote vya Halmashauri.
Kuanzia sasa Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule ni lazima watoe taarifa za mahudhurio ya wanafunzi kwa Maafisa Elimu wa Wilaya kila miezi mitatu. Maafisa Elimu wa Wilaya nao watalazimika kutoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri mwezi mmoja baada ya kupokea taarifa hizo. Halmashauri hazina budi kuchukua hatua stahiki za kijamii na kisheria kuhakikisha kuwa watoro wanarudi shuleni. Wazazi wa watoto hao au mtu ye yote atakayebainika kuhusika na utoro huo abanwe ipasavyo.
Sheria ya Elimu ya 1978 ipo, itumieni kwa ukamilifu kulitatua tatizo hili. Haipendezi kusubiri mpaka miaka saba kwa wanafunzi wa shule ya msingi au miaka minne kwa wanafunzi wa sekondari ipite ndipo taarifa za utoro kwa wanafunzi zitolewe au zijulikane. Lazima ufuatiliaji wa mahudhurio uwe wa mara kwa mara ili hatua za kuzuia ziweze kuchukuliwa mapema. Ninawataka viongozi wa TAMISEMI, Mikoa na Wilaya kuchukua hatua stahiki kudhibiti tatizo hili la utoro na watoto wengi kutokumaliza masomo. Litarudisha nyuma maendeleo ya taifa.
Umeme Vijijini
Ndugu Wananchi;
Nilipokuwa mkoani Ruvuma nimezindua ujenzi wa miradi mingi ya umeme vijijini. Kwa mujibu wa miradi hiyo vijiji 309 vitapatiwa umeme kati ya vijiji 509 vya Mkoa huo vinavyohitaji umeme. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospiter Muhongo na viongozi wenzake, viongozi na wafanyakazi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) pamoja na TANESCO kwa kazi kubwa na nzuri waifanyayo ya kufikisha umeme vijijini. Kwa kweli ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu suala la umeme vijijini kupewa msukumo mkubwa kiasi hiki, kwani kinachofanyika Ruvuma kipo nchi nzima. Nawaomba wananchi wanaofikishiwa umeme wautumie. Hata gharama za kuunganisha umeme zimepunguzwa makusudi, ili watu wengi waweze kumudu kuingiza umeme majumbani na kwenye shughuli za kichumi na huduma.
Mchakato wa Katiba Mpya
Ndugu Wananchi;
Kama tujuavyo, Bunge Maalum la Katiba lililoahirishwa tarehe 25 Aprili, 2014 kupisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi kushughulikia bajeti za Serikali husika, litakutana tena tarehe 5 Agosti, 2014 kuendelea na kazi yake ya kutunga Katiba Mpya. Kwa vile Bunge Maalumu la Katiba halikuweza kumaliza kazi yake ndani ya siku 70 zilizotengwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, nimeliongezea Bunge hilo siku 60 kwa ajili ya kukamilisha kazi yake. Nimefanya hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na Sheria hiyo hiyo.
Hatua Iliyofikiwa Kabla ya Kuahirishwa kwa Bunge
Ndugu Wananchi;
Itakumbukwa pia kuwa, tarehe 16 Aprili, 2014, baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hasa kutoka vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala uliokuwa unaendelea Bungeni na kutoka nje. Wakati wanatoka Bungeni, kazi kubwa ilikuwa imefanyika. Tayari Kamati zote 12 za Bunge hilo zilikuwa zimekamilisha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Sura hizo zinazungumzia utambulisho wa nchi na muundo wa muungano. Kamati zote zilipiga kura ya kupitisha uamuzi wao kuhusu sura hizo mbili. Kamati kadhaa ziliweza kupata theluthi mbili ya kura kwa Wajumbe wa pande zote mbili za Muungano, jambo lililoonyesha dalili njema kwamba Katiba mpya inaweza kupatikana.
Baada ya hapo, taarifa ya kila Kamati iliwasilishwa kwenye Bunge zima. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, maoni ya wachache nayo yaliwasilishwa. Kazi iliyokuwa inafuatia, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ni kwa Kamati ya Uandishi kukamilisha taarifa yake na kuiwasilisha kwenye Bunge zima kwa ajili ya kujadiliwa. Baada ya Wajumbe kujadili taarifa hiyo itafuatia kupiga kura ili kuamua kuhusu Sura hizo mbili. Kama yalivyo masharti ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uamuzi utafanywa kwa theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano wetu.
Sababu za Baadhi ya Wajumbe Kususia
Bunge Maalumu la Katiba
Ndugu Wananchi;
Sote tumewasikia Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba waliosusia vikao vya Bunge hilo wakielezea sababu zilizowafanya watoke Bungeni. Walitoa matamko kwenye vyombo vya habari na pia katika mikutano ya hadhara waliyoiitisha na kuhutubia sehemu mbalimbali nchini. Sababu walizotoa zimekuwa zikiongezeka na kubadilika kadri siku zinavyosonga mbele na upepo wa kisiasa unavyokwenda.
Hivi sasa wanazungumzia mambo mawili. Kwanza, kwamba Bunge Maalumu halina mamlaka ya kuifanyia mabadiliko yo yote Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa maoni yao, kazi ya Bunge Maalumu la Katiba ni kujadili na kupitisha tu Rasimu ya Katiba ya Tume na siyo kubadili cho chote. Pili, wametoa sharti la wao kurudi Bungeni ni kuhakikishiwa kwamba, kitakachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume. Bila ya sharti hilo kukubaliwa, wamesisitiza kutorudi Bungeni.
Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba
Ndugu Wananchi;
Mimi nimehusika katika kubuni wazo la kuwa na mchakato wa kuandika Katiba Mpya, na katika maandalizi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ya kuongoza na kuendesha mchakato huo. Kwa kweli sikumbuki wakati wo wote katika vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulipozungumzia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho na Bunge Maalumu la Katiba.
Mimi siyo Mwanasheria na hivyo nakiri kwamba naweza kuwa na upungufu katika kuelewa maana ya baadhi ya maneno ya kisheria. Hata hivyo, sikumbuki kuwepo kwa kifungu cho chote katika Sheria kinachosema kuwa Bunge Maalumu la Katiba halina mamlaka hayo. Tangu tulipoyasikia maneno hayo yakisemwa nimeuliza nithibitishiwe ukweli wa madai hayo bado sijaambiwa vinginevyo. Kama ukweli huo upo naomba anisaidie. Badala yake naambiwa kuwa maneno yaliyotumika katika Sheria haiakisi dhana inayotolewa kuwa kazi ya Bunge Maalum la Katiba ni kubariki Rasimu na siyo kufanya vinginevyo. Nimeambiwa kuwa sheria inasemaTume itaanda Rasimu ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba litatunga Katiba iliyopendekezwa.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 30 Desemba, 2010, nilipozungumzia dhamira yangu ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya nilieleza wazi nia ya kuwepo kwa uwakilishi mpana wa Watanzania katika mchakato huo. Ndiyo maana katika Sheria tukaweka ngazi nne katika mchakato wa kutunga Katiba. Ngazi ya kwanza ikiwa ya wananchi kutoa maoni yao juu ya kila wanachotaka kijumuishwe katika Katiba ya nchi yao. Ngazi ya pili, ni ya wananchi kupitia wawakilishi wao katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Kitaasisi kutoa maoni yao kuhusu Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotayarishwa na Tume.
Ngazi ya tatu inajumuisha wawakilishi wa wananchi waliopo kwenye Mabaraza ya Kutunga Sheria ya Sehemu zetu mbili za Muungano, yaani Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi, wakichanganyika na Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii ya Watanzania kutoka pande zote mbili za Muungano. Hawa ndio wanaounda Bunge Maalumu la Katiba, lenye jukumu la kutunga Katiba inayopendekezwa.
Mamlaka ya kutunga Katiba kwa mila na desturi za Mabaraza ya Kutunga Sheria ni uwezo wa kurekebisha, kubadili, kufuta na hata kuongeza kilichopendekezwa. Ingekuwa kilichokusudiwa ni kubariki tu lisingetumiwa neno la kutunga Katiba. Hali kadhalika, lisingewepo sharti la kupiga kura na msisitizo wa kupata theluthi mbili kwa kila upande wa Muungano. Aidha, kama ingekuwa jukumu la Bunge Maalumu ni kubariki tu Rasimu lisingepewa siku 70 za kazi na Rais kupewa mamlaka ya kuongeza siku zaidi kadri aonavyo yeye inafaa.
Ngazi ya nne na ya mwisho, tuliweka kura ya maoni ya wananchi kukubali au kukataa Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba. Kama ingekuwa Rasimu ya Tume haiwezi kubadilishwa hata nukta kwa nini basi tuweke kura ya maoni ya kuwahusisha wananchi wote?
Ndugu Wananchi;
Tulizibuni ngazi hizi nne kwa dhana kwamba kile ambacho hakikuonekana au hakikuwekwa sawa katika ngazi moja kitaonekana na kurekebishwa katika ngazi inayofuata katika ngazi zile tatu za mwanzo. Na, iwapo Katiba iliyotungwa haitawaridhisha wananchi wanayo haki ya kuikataa. Kwa kufanya hivyo, wananchi ndiyo waliopewa turufu ya mwisho.
Ndugu wananchi;
Kwa kweli, napata shida kuelewa mkanganyiko unatoka wapi na hasa wale wanaoongoza kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu kuwa ni wale wale waliotunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tena hatua kwa hatua. Nashangazwa zaidi ninapoona wale wale waliotunga Kanuni za Bunge Maalumu ndiyo wanaoongoza kuhoji uhalali wa kile walichokitunga.
Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Ibara ya 33 (8) inasema: Nanukuu: “Wakati wa mjadala, Mjumbe yoyote anaweza kutoa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliyomo katika Sura za Rasimu ya Katiba zinazojadiliwa kwa utaratibu ufuatao: (a) Ikiwa ni marekebisho, maboresho au mabadiliko yanayobadilisha jambo la msingi, au yanayobadilisha maudhui ya Ibara, mapendekezo ya marekebisho yatapelekwa kwa maandishi kwa Katibu siku moja kabla ya mjadala wa Ibara husika. (b) Ikiwa ni marekebisho madogo, ambayo hayabadili msingi au maana, mapendekezo ya marekebisho yatawasilishwa na mjumbe wakati wa mjadala baada ya kupata ruhusa ya Mwenyekiti”. Mwisho wa kunukuu.
Kanuni hii ilipotungwa, Wajumbe wote wa Bunge Maalumu pamoja na wale ambao baadae walisusia vikao vya Bunge walikuwepo Bungeni na walishiriki kuipitisha. Tena basi, baadhi yao walikuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni iliyopendekeza Kanuni hizo. Unapowaona watu wale wale sasa wanakuwa vinara wa kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba, unajiuliza maswali mengi kuhusu watu hao bila ya kupata majibu yaliyo sahihi na kutosheleza akili na ufahamu wetu.
Ndugu Wananchi;
Unaposoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge Maalumu, hii ni dhahiri kwamba wote walikuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mamlaka ya Bunge Maalumu ya kujadili Rasimu iliyoandaliwa na Tume na kutunga Katiba inayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
Kinachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume
Ndugu Wananchi;
Yapo madai yanayotolewa na kuenezwa na Wajumbe waliosusia Bunge Maalumu la Katiba kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ndiyo maana basi wanaweka sharti la kujadiliwa Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ndipo warudi Bungeni. Madai haya nayo yananipa taabu kuyaelewa. Ndugu zetu hawa walishiriki siku zote 19 za Kamati 12 zilipokutana kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Halikadhalika. walikuwepo na kushiriki kwa ukamilifu wakati taarifa za Kamati, tangu ya Kwanza mpaka ya 12, zilipowasilishwa kwenye Bunge zima. Aidha, na wao walishiriki kutoa maoni ya wachache kwa dakika 20 na kutoa ufafanuzi kwa muda wa dakika 30 kwa kila Kamati. Haya maneno ya sasa kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine kabisa ambayo wanadai eti ni ya CCM yanatoka wapi.
Mimi nadhani kuwa huenda katika Kamati kumefanyika marekebisho kwenye Rasimu ambayo hayakuwapendeza. Kama hivyo ndivyo, wawe wakweli kuhusu jambo hilo kuliko kusema mambo yasiyowakilisha ukweli halisi wa Rasimu inayojadiliwa. Matokeo yake ni kuwafanya wafuasi wao na wapenzi wao na hata watu wengine waamini kuwa kinachojadiliwa siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine tena ni ya CCM. Jambo hilo si kweli na wenyewe wanajua kwamba si kweli ila sijui kwa nini wameamua kupotosha ukweli.
Ndugu Wananchi;
Kinachonishangaza, zaidi ni kwamba, kama hawakuridhishwa na yaliyofanyika, kwa nini wasingetumia mifumo waliyojitengenezea wenyewe kwenye Kanuni kumaliza tofauti zao? Kanuni zinaelekeza kuwa mambo wasiyoridhika nayo yajadiliwe kwenye Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Ukiacha mifumo ya maridhiano ndani ya Bunge ukaenda nje kwa wananchi au vyombo vya habari na mitandao si jawabu la tatizo.
Ndugu Wananchi;
Ndiyo maana nashawishika kuunga mkono wale wote wanaowasihi Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na wengine warejee Bungeni. Watumie mifumo maalum ya Bunge iliyowekwa na Kanuni kutafuta maridhiano. Hali kadhalika, wasichoke kuwa na mawasiliano na vyama vingine vya siasa na hasa CCM kutafuta maelewano. Mimi niko tayari kusaidia pale watakapoona inafaa kufanya hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya ziku za nyuma.
Nililolisema mwanzoni kabisa mwa mchakato na nalirudia tena leo kwamba, ili tuweze kufanikiwa kupata Katiba Mpya ambayo sote tunaitaka, maelewano baina ya wadau wakuu wa kisiasa ni jambo lisilokuwa na badala yake. Vinginevyo kupata theluthi mbili kwa pande zote mbili za Muungano haitawezekana. Ndiyo maana nampongeza sana Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi, kwa uamuzi wa kuvikutanisha vyama vinne vikuu vya siasa kujadili namna ya kuondoa mtihani uliopo sasa katika mchakato wa Katiba.
Ombi langu kwa viongozi wa vyama hivyo ni kuitumia vyema fursa ya majadiliano kuukwamua mchakato kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake. Hali kadhalika nampongeza sana Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Mheshimiwa Samwel Sitta, kwa kuitisha kikao cha Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Bahati mbaya ni kwamba Wajumbe wa vyama vilivyosusia Bunge Maalumu hawakushiriki. Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Sitta hatokata tamaa kuendeleza juhudi za mashauriano na kwamba katika vikao vijavyo na wenzetu hawa watashiriki.
Ndugu Wananchi;
Hivi karibuni kumekuwepo pia madai yanayoelekeza lawama kwangu. Kwanza nalaumiwa eti kuwa mambo yalikuwa yanaenda vizuri mpaka pale nilipotoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Maalumu ndipo yalipoharibika. Pili nalaumiwa kwamba nawezaje kuikana Rasimu ya Katiba ambayo na mimi ni mmoja wa watu waliotia sahihi katika Rasimu hiyo.
Niruhusuni nianze na hili la pili. Nadhani ndugu zetu wanaotoa madai haya yameitafsiri isivyo sahihi yangu katika Gazeti la Serikali lililotangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuandika Rasimu ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano amepewa kazi tatu kufanya. Kwanza, kupokea Rasimu hiyo na Taarifa ya Tume kutoka kwa Mwenyekiti jambo ambalo lilifanywa tarehe 30 Desemba, 2013. Pili, amepewa kazi ya kuitangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume kwa watu wote kuiona na kuisoma ndani ya siku 30. Alipewa sharti la kuitangaza katika Gazeti la Serikali na vyombo vingine vya habari. Hili nalo lilifanywa hivyo tarehe 22 Januari, 2014.
Ndugu Wananchi;
Katika kutangaza katika Gazeti la Serikali sharti linamtaka anayetangaza ajitambulishe kuwa yeye ni nani na atie sahihi yake. Kwa kufanya hivyo, hakumfanyi yeye kuwa naye ni mhusika na maudhui ya kila kinachopendekezwa na Tume. Sahihi zilizomo ndani ya Rasimu na Taarifa ya Tume ni za Wajumbe wa Tume, kamwe sahihi ya Rais haimo hivyo hawezi kulaumiwa kuwa anaikana sahihi yake. Yeye ametimiza wajibu wake wa kutangaza, akaiweka hadharini kwa umma wa Watanzania kuiona na kusoma Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume vilivyotayarishwa na kutiwa sahihi na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kazi ya tatu ni kuitisha Bunge Maalumu ambayo nayo imekamilika tangu tarehe 18 Februari, 2014.
Ndugu Wananchi,
Jambo lingine linalofanana na hilo ni yale madai kwamba nilikuwa napata taarifa ya maendeleo ya mchakato ndani ya Tume mara kwa mara, iweje leo nitoe maoni tofauti kama niliyoyatoa katika hotuba yangu kwenye Bunge Maalumu. Ni kweli kabisa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, Makamu wake, Mheshimiwa Jaji Agustino Ramadhani na Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim wamekutana na mimi kwa nyakati mbalimbali kuzungumzia mwenendo wa mchakato. Lakini, hayakuwa mazungumzo ya kina kuhusu nini kiwe vipi katika maudhui na mapendekezo ya Tume. Ukweli ni kwamba Rasimu zote mbili nilizipata mara ya kwanza nilipokabidhiwa rasmi, tena kwa uwazi. Napenda watu wasijenge dhana kuwa nilipewa Rasimu na kuisoma kabla ya kukamilika na hivyo nilitoa maoni yangu. Tume hii ilikuwa huru na niliiacha iwe hivyo. Sikuiingilia kwa namna yo yote ile kupenyeza mambo ninayotaka yawemo. Kuthibitisha dhamira yangu ya kutaka Tume iwe huru katika kufanya kazi zao hata pale waliponitaka nitoe maoni niliwaomba tusifanye hivyo ili nisiwakwaze katika kufanya kazi zao, wakapata taabu ya kuwianisha wanayofikiria na mawazo yangu.
Ndugu Wananchi;
Kuhusu madai kwamba mambo yalikuwa yanakwenda vizuri na kwamba hotuba yangu iliyavuruga, napenda kusema wazi kuwa lawama hizo hazina ukweli wo wote. Ni madai yasiyokuwa na msingi. Kwani mimi hasa siku ile nilifanya lipi la ajabu. Ukweli ni kwamba nilisema yale yale ambayo Tume yenyewe imeyasema katika Rasimu ya Katiba na Taarifa za Tume. Niliyoyasema kuhusu malalamiko ya watu wa pande zetu za Muungano na uzuri na changamoto za miundo ya Serikali mbili na Serikali tatu ni yale yale yaliyomo kwenye taarifa za Tume. Nimetumia takwimu zile zile za Tume. Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume.
Jambo lingine ambalo nimelifanya ni kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya vipengele vya Rasimu hususan uandishi na dhana mbalimbali zilizokuwamo. Silioni kosa langu kwa kufanya hivyo, kwani Rasimu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Na mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine. Kwa nini nilaumiwe kwa kutumia haki yangu hiyo.
Lakini, pia mimi ndiye Rais wa nchi yetu, ninayo dhamana ya uongozi na ulezi wa taifa letu. Itakuwaje kwa jambo kubwa la hatma ya nchi yetu nilinyamazie kimya. Watanzania wangeshangaa na wangekuwa na haki ya kuhoji Rais wao ana maoni gani. Bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba. Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa namna nilvyotoa maoni yangu sikuwa natoa maagizo wala kushurutisha, ndiyo maana kila wakati niliwakumbusha Wajumbe kuwa mamlaka ya uamuzi ni yao. Yangu yalikuwa maoni tu wanahiyari ya kuyakubali au kuyakataa. Niliwataka Wajumbe wasome na kuielewa vyema Rasimu. Nilisema wasome sura kwa sura, mstari kwa mstari na neno kwa neno. Niliwaomba wajiridhishe kuhusu uandishi na dhana mbalimbali. Nilitoa mifano ya mambo yahusuyo uandishi ambayo ni vyema wayatazame. Pia nilitoa mifano ya dhana ambazo niliwasihi wajiridhishe juu ya kufaa kwake kuwepo.
Kuhusu muundo wa Serikali tatu, nilieleza wazi kuwa sina tatizo nao kama ndiyo matakwa ya Watanzania. Lakini, nilieleza hofu yangu kuhusu mapendekezo ya Tume na kuwataka Wajumbe wafanye kazi ya ziada kuondosha udhaifu iwapo wataukubali muundo unaopendekezwa. Nilieleza nia yangu ya kutaka tuwe na Serikali ya Muungano yenye ukuu unaoonekana, yenye nguvu ya kuweza kusimama yenyewe, inayoweza kuwa tegemeo kwa nchi Washirika, Serikali isiyokuwa tegemezi wala egemezi kwa nchi washirika na ambayo inavyo vyanzo vya uhakika vya mapato. Hivi kwa kutoa ushauri huo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba inageuka kuwa nongwa. Kwa kweli sielewi lawama ni ya nini?.
Naamini sistahili lawama bali pongezi kwa kuwa muwazi na kutoa ushauri wa msingi ambao utasaidia nchi kupata Katiba nzuri inayojali maslahi ya watu wa nchi yetu na ya nchi zetu mbili zilizoungana miaka 50 iliyopita.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Mwisho, ni maoni yangu ya dhati kuwa mgogoro uliopo sasa katika mchakato wa Katiba hauna sababu ya kuendelea kuwepo. Naamini hayo yote ambayo Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wanayalalamikia yanaweza kushughulikiwa kwa ukamilifu katika mifumo ya Bunge Maalumu la Katiba iliyotengenezwa na Wajumbe wote na wao wakiwemo. Nawasihi waitumie. Hali kadhalika, kwa kupitia mazungumzo wanayofanya na wenzao wa Chama cha Mapinduzi wanaweza kutengeneza nguvu ya pamoja kutatua changamoto za sasa na zitakazojitokeza baadaye. Kilicho muhimu ni kwa pande zote kuwa na dhamira ya dhati ya kutoka hapa tulipo sasa. Kama utashi wa kisiasa upo kwa kila mmoja wetu, hilo ni jambo linalowezekana kabisa. Narudia kuahidi utayari wangu wa kusaidia kadri inavyowezekana tusonge mbele.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
- Jul 03, 2014
OPENING SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CAHOSCC COORDINATOR AT THE CAHOSCC MEETING, MALABO, EQU...
Soma zaidiHotuba
Your Excellency, President Mohamed Ould Abdel Aziz,
Chairperson of the African Union;
Excellences Heads of State and Government and members of
the Committee of African Heads of State and Governments
on Climate Change (CAHOSCC);
Your Excellency Dr. Nkosazana Dlamini–Zuma,
Chairperson of the African Union Commission;
Honorable Dr. Binilith Mahenge, President of the AMCEN;
Honorable Rhoda Tumusiime, Commissioner for Agriculture and Rural Economy – African Union Commission;
Distinguished guests;
Ladies and Gentlemen;
It is my great pleasure to welcome you all, Excellencies, to this important meeting, and I thank you for availing your precious time to come to this meeting. As I indicated in my invitation letter, since its establishment, CAHOSCC has been doing a commendable job. It has enabled the AU Member States to cooperate more, forge consensus and speak with one voice on climate change issues since 2009, when this unified system was established. We need to build on this momentum.
At this point in time, the issue before the world is not about why climate change is a threat and who is to blame for it. The most important matter before us now is about how to adapt and how to mitigate climate change effects. The latest report by the Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC) shows that the situation has not gotten better since the last evaluation was done. As a matter of fact, things are getting bad with each passing day. But, the world can combat climate change by the stemming the decline and reversing the trend. What nations are required to do is to muster political will and raise their collective ambition to achieve a carbon neutral world in the second half of the century. Africa, too, has no choice other than join hands to adapt and mitigate the effects of climate change. However, Africa can make a choice on how it can adapt, and mitigate and when it can do so in terms of timeframe and pace.
For Africa, this is both a challenge and an opportunity. If Africa focuses on smart choices, it can win investments in the next few decades in climate resilient and low emission development pathways. Additionally, increased awareness and understanding of climate change politics and negotiation skills at the highest political and diplomatic levels can increase the continent’s competitiveness in trade and international financial flows to address climate change.
Excellencies;
This is why as members of CAHOSCC, we are duty bound to provide vision and guidance on the much needed appropriate actions, within a high level Framework Work Programme on Climate Change Action that will cover all the key areas of our immediate and long-term interests and concerns. I suggest that initially we focus on five areas, namely: Climate Financing and Addressing Technology needs; the Africa-wide Programme on Adaptation; Actions on Mitigation; Cross-cutting actions and Participation; and International Cooperation and Institutional mechanism for follow up. Our experts worked at length to elaborate on these areas in the concept note that I have shared with you in the letter of invitation I sent to you.
Excellencies;
On Climate Financing and Technology needs, we need to underscore the fact that due to past emissions, the impact of climate change on the continent is overwhelming. Addressing it will require massive financial resources and technological support never envisaged before. For example, addressing adaptation alone needs financial resources in the range of USD 7-15 billion per year by 2020. This cost will further increase as temperature rises.
According to the World Bank, as of last year, Africa had received just about US$132 million of adaptation funding. In addition, the cost of putting Africa on a low-carbon growth path can reach USD 22-30 billion per year by next year and USD 52-68 billion per year by 2030. Obviously, African countries are unlikely to generate these huge financial resources from own sources in the short and mid-term period. It is, also, not fair and just for Africa to bear this cost alone. The fact of matter is that our continent bears very little responsibility for causing climate change problems affecting the world today. Africa contributes only less than three percent of total global greenhouse gases that cause climate change. This should be our point of departure and a justification to ask the developed world to contribute more towards bridging the overwhelming funding bill.
Excellencies;
There is an urgent need for African leaders through CAHOSCC to make pressure to bear on the international community to ensure that the resources required for climate change financing are adequate, predictable and easily accessible through the climate change convention processes. In this regard, it is important to note that, The Green Climate Fund operational procedures have been completed. It is, now incumbent upon the developed countries to capitalize it as they have promised and committed to do.
Much as the promise of the 100 billion by 2020 is still far from being realised our right to use this Fund comes with a responsibility on our part. We are supposed to ensure that we put in place right institutions to access these resources. Short of doing this, we will not be able to access these funds. We will lose ground on our just demand for resources. Furthermore, we have to stand out against efforts to account the resources against ODA. At the same time we need to utilize current resources to the fullest.
Excellencies;
To be able to access funding from the Adaptation Fund and the Green Climate Fund, each country has to put in place a National Implementing Entity and a National Designated Authority for each of the two funds respectively. To date there are hardly 10 African countries which have established these institutions. With regard to the Least Developed Countries Fund (LCDF) which provides up to USD 30 million for each African LDC, less than twenty of the 34 Africa’s LDCs have accessed half of the available resources so far. As we appeal for the capitalization of the Green Climate Fund, and call for increased resources in the Adaptation Fund and the LDCF, it will not be of any benefit to Africa if we do not utilize to the fullest the already available resources. This is something that is within our reach. Not doing so is incomprehensible. Let us do it.
Excellencies;
With regard to technology to address climate change in Africa, it is equally important to establish the National Designated Entities (NDEs), for the facilitation of the acquisition and use of the needed technologies for both adaptation and mitigation. The Climate Technology Center and Network which was established in 2012 by the UNEP in Copenhagen, Denmark was a result of the long standing demand by African countries to have a center that can unlock climate related technology transfer barriers. To date, only 19 African countries have put in place these NDEs and there are no sub-regional centers established for the purpose. These NDEs are a pre-requisite for us to get the needed support.
Therefore, Excellencies, it is our duty to remind all African governments to establish these institutions as we prepare for the Secretary General’s Climate Summit this September, and as we move towards the 20th Conference of the Parties in Lima, Peru this December and the 2015 Paris COP 21 and hopefully a binding Climate Change Agreement. This way we shall be able to demonstrate to the world that we are ready to access and make use of any financial and technological resources under the Framework Convention on Climate Change. At the same time we need to see that all LDCs in Africa access the USD 30 million allocated to them by December, 2014. This way we will be able to make the case for additional support.
Excellencies;
The need for an Africa wide programme on adaptation can not be over-emphasized. We need a high level work programme on adaptation that will cover a number of key areas of concern. It is important to remind ourselves that in March, 2014 scientists working under the IPCC, released the Fifth Assessment Report which has re-affirmed that despite a growing number of mitigation policy interventions in various countries, greenhouse gas (GHG) emissions are rising rapidly. Fossil fuel combustion and industrial processes contribute 80 percent of the recent GHG emission growth. The report also noted that about 75 percent of this growth in emissions comes from energy supply and industrial sectors mainly in the developed world and the fastest growing regions of developing countries. With this increase, the world average temperature is now about 0.85Centigrade above the pre-industrial range.
This increase has triggered massive changes in the global natural systems with catastrophic consequences for Africa. For example, Sub-Saharan Africa will face a decrease of 19 percent in maize yields, 68 percent in beans yields and a decrease in crop yields by 18 percent for Southern Africa and up to 22 percent across Sub-Saharan Africa. Africa may brace up for a total annual loss of USD 311 million to regional economy from agriculture. Disease burden is likely to increase especially for malaria and cholera. Climate-induced extreme flooding is likely to impact a good number of African countries by 2020. Ecosystems will be affected by climate-induced longer and more frequent droughts, resulting in deforestation, forest degradation, land-use change, pollution and water scarcity.
The assessment also came with shocking predictions about the impact of climate change on the continent’s urbanization and ecosystems. The global mean sea level rose by about 19 centimeters since the beginning of the last century. This is alarming. These predictions present a serious challenge to our dear continent now and in the future, if the trend is not stammed and reversed. What will Africa look like in 2050, when the population is expected to be 2.4 billion people is a billion dollar question.
We are all witnesses to the many examples of the impact of climate change on Africa, which require urgent and comprehensive programmes for adaptation. This is a matter of our own survival and that of the future generation and countries. We must give climate change adaptation and mitigation the seriousness it deserves. All countries need to put in place National Adaptation Plans and implement them. More importantly, we also need specific adaptation programmes for some key sectors of the economy.
In this context we are proposing an Africa Wide Programme on Climate Resilient Agricultural Development. It is being projected that reductions in yield in some African countries could be as much as 50 percent by 2020, and crop net revenues could fall by as much as 90 percent by 2100. Therefore, we need to ensure that we engage in climate smart agriculture within the changing climate. This way, we would be able to address these challenges and ensure improved food security for ourselves and many generations to come.
Excellencies;
We are also proposing an Africa Wide Program on Mitigation. Africa is not a big emitter of greenhouse gases, but we see a lot of merit and benefit in the continent charting out a environment friendly development path. Indeed Africa’s contribution to climate change from fossil energy and transport sources in the global context is but only worth a footnote. Total Africa’s carbon dioxide emissions, predominantly from the energy and transport industries, amount to approximately 650 million tons per annum. Comparatively, Germany alone emits approximately 800 million tons of carbon dioxide annually. The annual per capita emissions of carbon dioxide in Sub-Saharan Africa is approximately one ton while the US has per capita emission of 16 tons.
With such low carbon dioxide emissions, due to Africa’s low level of industrial development, Africa’s contribution towards a better climate future can predominantly be through the adoption and use of new technologies for enhancing energy security and ensuring economic development within the changing climate. New technologies and financial resources should create opportunities for new jobs, more reliable and affordable energy sources for green growth. Future business ventures and partnerships should be supported to adopt and fairly sail in the green economic growth.
Excellencies;
As part of support to the global mitigation agenda, the forestry sector in Africa as it is elsewhere, has an important role to play. Therefore, a comprehensive programme on Sustainable Forest Management is proposed. African forest resources are under pressure from various “drivers of deforestation and forest degradation”. It is important to underscore the fact that forests play an important part in Africa’s development and the livelihood of its people. The sector is a key contributor to the economic growth of the continent in terms of biomass energy, housing, water, food, and export earnings.
Paradoxically, in terms of climate change mitigation, currently Africa’s contribution towards mitigating climate change is not yet well appreciated by the international community. The stock of carbon dioxide stored by African forests amounts to approximately 60 billion tons, as much as that of all OECD countries put together, including densely wooded members such as Russia and the US. This is a significant contribution. A higher quantity of carbon dioxide is only stored in the forests of the Amazon Basin.
Africa emits only about 1.75 billion tons annually of which 650 million tons are from technical sources and 1.1 billion tones from deforestation. In this respect, effectively Africa is a net sink of all its emissions in addition to emissions from the developed world and other fast developing countries. We need to be appreciated and given the right compensation for this crucial service to humanity and this planet we all call home.
Excellencies;
On cross cutting actions, we need to engage everyone who can make a difference on the continent: governments, business and investors, cities, diplomatic missions, as well as men, women and youths. If the young generation is given the required education, information and guidance they stand a better position to make the needed difference. We will have invested productively in our own future. The same applies to women who are the most vulnerable to the impact. We need also to give clear instructions to our diplomatic missions particularly in Addis Ababa, Geneva, Nairobi, Brussels and New York to understand, uphold and defend Africa’s position and interests in the international climate change discourse. Climate change is presenting a new global order and should become one of our key diplomatic agenda.
Excellencies;
Let me stress also that there is a need to establish mechanisms for follow up on the implementation of decisions, declarations and agreements made between Africa and our partners. This should also include decisions made during the various climate change conferences. This will make Africa effectively benefit from such decisions and agreements.
Excellencies;
I have tried to present to you what I believe should guide Africa’s approach and action on the climate change agenda now and in the near future. Africa needs a clear position and direction as well as a well structured and a focused approach to climate change related issues. Africa cannot afford to lose out on the ongoing debates and negotiations, for we have a big stake, and a lot to lose if we remain unfocused and disenfranchised. Our numbers, put us in a position of strength and our claims are just. All that we need to do and is to be united, coherent and consistent in our appeal, while, remaining honest to our obligations and responsibilities. The concept note I sent to you with invitations to this meeting, elaborates what I have just summarized.
We should and must go to New York, Lima and Paris as one and united continent and people. We must go there with clear vision, mission and one voice. I look forward to fruitful deliberations and I now declare this Meeting of the CAHOSCC officially opened.
I thank you for your attention.
- Jun 26, 2014
HOTUBA YA KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI OMBENI Y. SEFUE, AKIFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA UTAWALA NA RASILIMALIWATU (DAHRMs), MAKATIBU TAWALA WASAI...
Soma zaidiHotuba
Bibi Fatma Salum Ally, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Bw. George D. Yambesi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Bw. HAB Mkwizu, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Bw. Edwin K. Kiliba, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Bibi Rehema S. Madenge, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,
Washiriki wa Mkutano,
Waandishi wa Habari,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana,
Habari za Asubuhi!
Ndugu Washiriki,
Napenda kuanza kwa kukushukuru Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejiementi ya Utumishi wa Umma na wenzako kwa kunialika kufungua Mkutano huu wa Mwaka wa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali na Taasisi za Umma.
Aidha, nachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Watendaji wote wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu. Vilevile, natoa shukrani za dhati kwenu viongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa kukubali kuwa wenyeji wa Mkutano huu na kujumuika nasi siku ya leo. Hali kadhalika, nawakaribisha washiriki wote walioweza kusafiri kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu kuja kuhudhuria mkutano huu muhimu.
Ndugu Viongozi na Washiriki wa Mkutano,
Nimeupa mkutano huu umuhimu mkubwa sana, maana hii ni mara yangu ya kwanza kufungua mkutano kama huu tangu niteuliwe kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma. Mlinialika mwaka jana, lakini nilishindwa kuhudhuria kutokana na majukumu mengine ya Kitaifa. Leo ninafurahi kukutana nanyi mnapojiandaa kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji kwenye Utumishi wa Umma, kubadilishana uzoefu, kujifunza na kufahamiana zaidi.
Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma
Ndugu Washiriki,
Masuala mnayoyasimamia ninyi ni sehemu muhimu sana ya Utumishi wa Umma, yaani masuala yahusuyo utawala na rasilimaliwatu. Masuala haya yasiposimamiwa vizuri, kwa weledi, haki na uadilifu, na kwa kuzingatia misingi iliyowekwa kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu, Utumishi wa Umma utavurugika na tutashindwa kuwahudumia wananchi ipasavyo.
Mojawapo ya kazi za msingi za Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma ni kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma una haiba na sifa nzuri machoni pa wananchi. Ninyi mlio katika ukumbi huu ndio wa kunisaidia kutekeleza wajibu huo kwa kuhakikisha masuala ya utawala na rasilimaliwatu yanaendeshwa na kusimamiwa kwa ukamilifu na weledi, na kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
Ninyi pia ndio washauri wakuu wa Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, kwenye masuala ya utawala na rasilimaliwatu. Mkifanya kazi yenu vizuri hakutakuwa na tuhuma au lawama dhidi ya Utumishi wa Umma kwa ujumla, na hasa dhidi ya ofisi zenu. La sivyo, msipofanya kazi yenu vizuri, hamuwezi kukwepa lawama.
Mkiwa washauri wakuu wa masuala ya utawala na rasilimaliwatu lazima ninyi wenyewe mzifahamu vema Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu zinazohusu utawala na rasilimaliwatu na kisha mzizingatie wakati wote.
Narudia. Jambo la kwanza ni ninyi wenyewe kuzielewa vizuri Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoongoza Utumishi wa Umma. Maana, msipozielewa ninyi, na msipokuwa mfano bora wa kuzisimamia, mtawapotosha sana viongozi wenu wakuu kwenye Wizara, Idara na Taasisi zenu. Na hayo yatakuwa makosa makubwa sana.
Jambo la pili, ni kuhakikisha kuwa Watumishi wa Umma nao wanazielewa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu hizo. Msiifanye miongozo hii ya kuendesha Utumishi wa Umma kuwa ni siri ya wachache. Watumishi nao wanayo haki ya kuijua miongozo hiyo. Nami naamini kuwa mkiwapa haki hiyo, kazi yenu ya kusimamia miongozo hiyo itakuwa nyepesi zaidi.
Na hiyo inanipelekea kwenye jambo la tatu muhimu kwenye eneo hili, nalo ni kuwa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu hazina maana iwapo hazifuatwi, iwapo hazisimamiwi na iwapo zikivunjwa hakuna adhabu stahiki inayotolewa kwa mkosaji. Ieleweke kwamba miongozo hiyo haikuwekwa ili iwe hiari ama kuifuata au kutokuifuata. Miongozo hiyo, kwa maana ya Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu lazima ifuatwe, na wala si jambo la hiari. Na isipofuatwa, lazima hatua zichukuliwe mara moja. There must be consequences!
Na leo yapo maeneo manne muhimu, miongoni mwa mengine, ambayo ningependa kuyazungumzia, kwa vile yana umuhimu wa pekee katika utawala na rasilimaliwatu kwenye Utumishi wa Umma. Hayo ni ajira, maendeleo ya watumishi, upandishwaji vyeo na hatua za kinidhamu. Maeneo haya yana malalamiko mengi miongoni mwa Watumishi wa Umma, na miongoni mwa jamii kwa ujumla.
Ajira
Ndugu Washiriki,
Kwa upande wa ajira, Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu zetu zimeweka wazi miongozo ya kufuatwa kwenye kuajiri watu kwenye Utumishi wa Umma. Miongoni mwa miongozo hiyo ni uwazi katika kutangaza nafasi za ajira, na usawa na haki wakati wa usaili na uajiri. Lakini bado malalamiko yanasikika kuwa ati huwezi kuajiriwa kwenye Utumishi wa Umma isipokuwa kama unajulikana au unatoa rushwa, ama ya fedha au ngono. Jambo hilo linanisononesha sana. Mimi naamini mambo hayo yamepungua sana. Lakini kama yanafanyika, ni kinyume kabisa na Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na lazima tulio katika ukumbi huu tuyapige vita kwa bidii zote, bila kuoneana haya, hadi wananchi waone kuwa kweli hayapo. Tusipuuze hata kidogo malalamiko ya wananchi, bali tujichunguze na tuchunguzane, ili kama mambo hayo bado yapo, kwa pamoja tuazimie kuyakomesha kabisa kwenye Utumishi wa Umma.
Aidha, ningependa mjue kuwa kuanzia sasa tutaweka mkazo mkubwa sana kwenye sifa ya uzalendo kwenye ajira Serikalini. Hatuwezi kuwa na Watumishi wa Umma ambao hawana uzalendo. Hivyo, pale ambapo waombaji kazi kwenye Utumishi wa Umma wana sifa zote sawa, wale waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa watapewa kipaumbele. Lakini, narudia, kipaumbele hicho kitumike pale tu ambapo sifa zingine zote ziko sawa, na si vinginevyo.
Umuhimu wa Mafunzo na Kuendeleza Watumishi
Ndugu Washiriki,
Eneo la pili linahusu umuhimu wa kuwaendeleza Watumishi wa Umma, na kuwajengea weledi, uzoefu na uwezo. Ndio maana nimefarijika kuona kaulimbiu ya Mkutano huu isemayo, “Mafunzo elekezi na yale ya kuwaendeleza watumishi wa umma ni msingi wa tija, ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa umma”. Kauli mbiu hiyo ni sahihi kabisa.
Mafunzo ya kuwaendeleza Watumishi wa Umma huongeza weledi kwenye kazi na hivyo kuwawezesha watumishi kutekeleza kwa ukamilifu majukumu yao. Na lazima yaanze na mafunzo elekezi kwa watumishi wapya ili waelewe majukumu yao mapya, wajibu wao, muundo wa Serikali, taratibu za utendaji bora wa kazi, maadili, nidhamu, uzalendo, uadilifu na ustahimilivu.
Nasikitika sana kuwa tofauti na hali ilivyokuwa wakati mimi naingia kwenye Utumishi wa Umma, siku hizi tumepunguza sana na wakati mwingine hatutoi kabisa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya. Aidha, mafunzo ya kuwaendeleza watumishi walio kazini nayo yanasuasua kwenye baadhi ya ofisi. Nimesikia pia kuwa kwenye baadhi ya ofisi yamezuka mambo yasiyofaa katika kusomesha Watumishi. Miongoni mwa tuhuma ni hizi zifuatazo:
- Kwanza, kuongezeka kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na mali za umma;
- Pili, kuongezeka kwa vitendo vya rushwa ya fedha au ya ngono;
- Tatu, kushuka kwa maadili miongoni mwa baadhi ya Watumishi wa Umma;
- Nne, kutekeleza kazi bila kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu; na
- Tano, kukosekana uzalendo na uadilifu kwa baadhi ya Watumishi wa Umma.
Ndugu Washiriki,
Najua wapo miongoni mwenu mnaofanya kazi vizuri, kwa uadilifu mkubwa, katika kuendeleza Watumishi wa Umma. Nawapongeza sana. Lakini naomba tushirikiane kuwarekebisha wale miongoni mwetu wanaoendekeza aina ya tuhuma nilizozitaja hapa, ambao kwa vitendo vyao wanaharibu sifa nzuri ya Utumishi wa Umma.
Hivyo basi, pamoja na mambo mengine, ningependa Mkutano huu utafakari, ufanye tathmini na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kurejesha utoaji mafunzo elekezi kwa Watumishi wapya wa Umma na mafunzo ya kujiendeleza kwa walio kazini.
Ninazo taarifa kuwa kwa upande wake Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wameanza kufanya uchambuzi wa mtaala wa mafunzo elekezi kwa kuangalia namna bora ya kuendesha mafunzo hayo, muda wa mafunzo, sifa za wakufunzi na taasisi zitakazoendesha mafunzo hayo ili kuwa na mfumo mzuri zaidi wa mafunzo yenyewe.
Napongeza jitihada hizo na ningependa kazi hiyo isiishie tu katika kuwasilisha taarifa bali kuhakikisha mapendekezo yatakayotolewa yanafanyiwa kazi kwa ukamilifu na utekelezaji uanze mapema iwezekanavyo.
Matumizi ya TEHAMA
Ndugu Washiriki,
Kama mjuavyo, tuko katika karne ya matumizi ya TEHAMA, na lazima sasa dhana ya Serikali Mtandao itekelezwe kwa vitendo kama nyenzo muhimu katika kuleta ufanisi, uwazi na uwajibikaji kwenye utendaji kazi na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi. Matumizi ya TEHAMA hayakwepeki katika Karne ya 21. Ukichelewa kutumia TEHAMA unajichelewesha tu, maana dunia haitarudi nyuma kwenye jambo hili.
Ndiyo maana, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kubuni na kuweka mifumo na miundombinu ya Serikali Mtandao ili kurahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa Umma na kwenda na wakati.
Mojawapo ya mifumo ambayo tayari imewekwa ni pamoja na Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (Human Capital Management Information System-HCMIS), Mfumo wa Fedha (IFMS); Tovuti Kuu ya Serikali; Mfumo wa Serikali wa Barua Pepe; Tovuti mbalimbali za Taasisi, pamoja na mfumo wa kuendesha mikutano kwa njia ya mtandao (Video Conference); miongoni mwa mifumo mingine.
Mifumo ya Kimenejimenti
Ndugu Washiriki,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kupitia Programu ya Mabadiliko ya Utendaji Kazi Serikalini, imeweka mifumo mbalimbali ya kimenejimenti katika Taasisi za Serikali. Mifumo hii ni pamoja na Mpango Mkakati; Mikataba ya Huduma kwa Mteja; Mfumo wa Wazi wa Upimaji Utendaji Kazi, Mfumo wa kushughulikia malalamiko na Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini.
Aidha, nimejulishwa kuwa kuanzia Julai mwaka huu, Mfumo wa kupima Utendaji Kazi Kitaasisi (Performance Contracting) nao utaanza kutumika.
Matarajio ni kwamba matumizi sahihi ya mifumo hii yatasaidia kuongeza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na hatimaye kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Hivyo, sikufurahishwa na taarifa niliyopewa kuwa tathmni ya kiwango cha matumizi ya mifumo hii iliyofanyika hivi karibuni katika Taasisi 18 imeonesha kuwa kiwango cha matumizi ya mifumo hii ni asilimia 78 tu. Hivyo, bado jitihada zaidi zinahitajika ili kiwango cha matumizi ya mifumo kifikie asilimia 100 kama ilivyokusudiwa.
Mifumo hii, pamoja na ile inayoendelea kuwekwa, kama ikitumika ipasavyo kulingana na miongozo na mafunzo yaliyokwishatolewa na yanayoendelea kutolewa, itaongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji na hatimaye kuchangia katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini. Muhimu sana kwangu ni kuwa mifumo hii itaimarisha utawala bora na kupiga vita rushwa. Mifumo hii inagharimu Serikali fedha nyingi sana. Hivyo, lazima itumike ipasavyo na tutambue kuwa, kuweka mifumo pekee hakutoshi bila mafunzo ya mara kwa mara kwa Watumishi wa Umma juu ya namna ya kuitunza na kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Upandishaji Vyeo
Ndugu Washiriki,
Eneo lingine muhimu mnalolisimamia ni la upandishaji vyeo. Eneo hili linao uhusiano wa karibu na lile lililopita la kuwaendeleza Watumishi wa Umma. Hakuna faida kwa Taifa kuwapandisha vyeo watu ambao hawajajengewa uwezo na weledi wa kutosha.
Wakati sasa umefika wa kutafakari upya msingi ya kuwapandisha watumishi vyeo, ili uendane sambamba na msingi wa kuwaendeleza watumishi na kunoa weledi wao. Mawazo yangu ya awali, ambayo ningependa myatafakari, ni kuwa tuwe na aina tatu za mafunzo ya msingi ambayo yataunganishwa na upandishwaji vyeo:
- Mafunzo ya kwanza ni mafunzo elekezi kwa Watumishi wapya wa Umma;
- Mafunzo ya pili yafanyike kabla mtumishi hajaingia kwenye ngazi za uandamizi kwenye Utumishi wa Umma. Kwa maneno mengine, mtumishi asipandishwe cheo kuwa Afisa Mwandamizi kama hajafanya mafunzo yoyote tangu aajiriwe.
- Mafunzo ya tatu yafanyike kabla mtumishi hajaingia kwenye ngazi ya ukuu kwenye Utumishi wa Umma. Kwa maneno mengine, Afisa Mwandamizi asipandishwe cheo kuwa Afisa Mkuu mpaka awe amepata mafunzo mengine.
Utaratibu huu, ambao unatumika kwenye nchi nyingi duniani, una faida nyingi ikiwemo kutoa hamasa kwa Watumishi wa Umma kujiendeleza, na kuhakikisha kuwa wakataokuja kushika nafasi za juu kwenye Utumishi wa Umma wameandaliwa vizuri kwa uwezo, weledi, uadilifu na uzalendo.
Najua kwa kuanzia hatuwezi kuutekeleza utaratibu huu nchi nzima, lakini ni muhimu tuanze ili Watumishi wajue kuwa kujiendeleza kimasomo na kwenye taaluma zao ni sifa mojawapo ya ziada ya kupandishwa cheo.
Sifa nyingine muhimu ya kupandishwa cheo lazima iwe rekodi nzuri ya uadilifu, uwezo, uzalendo na utendaji kazi. Muda ambao mtumishi amekaa kwenye ngazi moja ni sifa muhimu katika kumpandisha cheo, lakini haiwezi kuwa ndiyo sifa pekee. Lazima pia mtumishi aoneshe, na aonekane, kuwa amemudu vema majukumu yake kwenye ngazi aliyoko na ana mwelekeo wa kumudu majukumu ya ngazi anayofikiriwa kupandishwa. Ninyi nyote bila shaka mnaijua vema ‘Peter Principle’ isemayo “In a hierarchy, every employee tends to rise to his (or her) level of incompetence”.
Lazima tuwe na mfumo unaotuwezesha kuwatambua wenye vipaji vya uongozi, kuwaendeleza na kuwapandisha cheo kwa kujua watamudu madaraka zaidi. Lakini pia tuwe na mfumo wa kubaini wale ambao kwa uhakika wamefikia kiwango chao cha ‘incompetence’ na hakuna faida kwa Taifa kuendelea kuwapandisha cheo. Jambo hili likifanywa vizuri litasaidia kuweka mfumo bora wa kurithishana madaraka.
OPRAS
Ndugu Washiriki,
Mojawapo ya malengo ya Serikali katika kuanzisha, kwa mujibu wa sheria, utaratibu mpya wa kutathmini utendaji wa kazi wa mtumishi kwa uwazi (OPRAS) ni kusaidia kubaini utendaji na uwezo wao, na pia kujua udhaifu wao, kuwasaidia na kuwaendeleza. Utaratibu huu, kama nilivyosema, upo kwa mujibu wa sheria, na hivyo si jambo la hiari. Lazima mlisimamie vizuri ili lifanyike kwa ukamilifu na kwa haki.
Katika kuhakikisha kwamba mifumo hii inatumika ipasavyo, mwaka 2012 nilitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kwamba kwa kushirikiana na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma wafanye zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa matumizi ya OPRAS katika Utumishi wa Umma. Zoezi hilo lilifanyika ndani ya mwaka wa fedha 2012/13 katika Taasisi za Umma 110 zilizojumuisha Wizara 12, Idara Zinazojitegemea 5, Wakala za Serikali 17, Sekretarieti za Mikoa 11 na Mamlaka za Serikali za Mitaa 65.
Matokeo ya zoezi hilo yalibainisha kuwa katika Taasisi 110 zilizokaguliwa ni Taasisi 29 tu, sawa na asilimia 26.36, zilizotekeleza OPRAS kwa ukamilifu. Taasisi 68, sawa na asilimia 59.36, zilitekeleza kwa kiwango cha chini, na taasisi 13, sawa na asilimia 14.3, zilikuwa hazijaanza kabisa.
Napenda nitumie nafasi hii kuwaagiza Viongozi na Watendaji Wakuu kubadili mtazamo wao kuhusu umuhimu wa OPRAS, kuwaelimisha watumishi na kuwapangia malengo yakinifu yanayopimika. Aidha, ninakuagizeni ninyi washiriki wa Mkutano huu, ambao ndio hasa wasimamizi na waratibu wa OPRAS katika taasisi zenu, kutumia fursa ya mkutano huu kujielimisha zaidi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha mfumo huu ili kujenga Utumishi wa Umma wenye tija na ufanisi.
Nidhamu
Ndugu Washiriki,
Nikiwa Mkuu wa Utumishi wa Umma ninao wajibu wa kuwalinda Watumishi wote wa Umma ili watendewe haki, wasionewe wala kubaguliwa kwa sababu yoyote ile. Lakini pia mimi ninayo mamlaka ya nidhamu kwa Watumishi wote wa Umma. Wa kunisaidia kutekeleza majukumu yote hayo mawili ni ninyi, na ningependa mhakikishe upo mfumo na utaratibu mzuri kwenye ofisi zenu wa kuhakikisha Watumishi wa Umma wote wanatendewa haki, hawaonewi wala kubaguliwa. Lakini pia mhakikishe kuwa upo mfumo na utaratibu mzuri kwenye ofisi zenu wa kuwabaini wote wanaostahili kuchukuliwa hatua za nidhamu, na kwamba hatua hizo zinachukuliwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
Wapo watumishi wengi wanaohamishwa vituo kwa vile ati zipo tuhuma juu yao, ziwe ni tuhuma ya kimaadili au za uzembe au kutotimiza wajibu. Mimi naamini kuwa mtumishi anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu pale pale alipo. Kumhamisha bila kumchukulia hatua ni kukwepa wajibu, na kwa kweli ni kutomtendea haki kwa kumnyima fursa ya kujitetea dhidi ya tuhuma zinazoelekezwa kwake.
Ni kweli yapo mazingira ambapo kumhamisha mtumishi ndilo suluhisho la tatizo, lakini si kila mara. La muhimu ni kwamba uhamisho usitumike kukwepa wajibu wa kuchukua hatua za nidhamu pale kosa lilipotendeka.
Nahisi umezuka woga fulani katika kuchukua hatua za kinidhamu. Ninachosema ni kuwa ukiogopa kuchukua hatua za kinidhamu pale unaporidhika kuwa hatua hizo zinastahili, basi uongozi umekushinda. Na matokeo yake, wakiwepo viongozi wengi waoga namna hiyo, uzembe unaenea kwenye Utumishi wa Umma na sifa yetu mbele ya wananchi inaharibika kwetu sote. Tuache woga, lakini tutende haki!
Lipo pia tatizo la kuchukua hatua za kinidhamu bila kuzingatia kwa ukamilifu Sheria, Kanuni na Taratibu. Nimeona rufaa kadhaa za Watumishi wa Umma ambao wamechukuliwa hatua za nidhamu na wakakata rufaa kwenye Tume ya Utumishi wa Umma, na baadaye kwa Rais iwapo hawakuridhika na uamuzi wa Tume.
Inasikitisha sana pale mtumishi ambaye upo ushahidi wa kutosha wa kutenda kosa, lakini inabidi arejeshwe kazini kwa vile tu mamlaka yake ya nidhamu haikuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Isitoshe, pale ambapo Tume inakubali rufaa ya mtumishi na kuagiza kuwa hatua za kinidhamu zianze upya, wanakasirika na wengine, hasa kwenye Halmashauri, kukataa. Kufanya hivyo ni kumsaidia tu mhalifu maana akienda mahakamani atashinda na itabidi tumlipe. Tusifanye makosa hayo. Tusiwe wakaidi pale tunapoelekezwa na Tume ya Utumishi wa Umma kurudia mchakato wa hatua za kinidhamu, bali tutumie fursa hiyo kujielimisha zaidi ili tusirudie makosa wakati mwingine.
Ajira za Wastaafu
Ndugu Washiriki,
Serikali imekuwa ikiajiri kwa masharti ya mkataba watumishi waliokwishastaafu kazi kwa lazima kwa madhumuni ya kujaza nafasi wazi kwa kada zenye wataalam wachache kama vile madaktari, wafamasia, walimu, wahandisi na kadhalika.
Hata hivyo, baadhi ya waajiri wamekuwa wakiwasilisha kwangu maombi ya ajira za mikataba hata kwa nafasi ambazo zinaweza kujazwa kwa kupandishwa vyeo maafisa waliopo au kwa kuajiri watumishi wapya. Hii inatokana na baadhi ya waajiri kutokuwa na Mpango wa Kurithishana Madaraka (Succession Planning) ambao ungetumika kuwaandaa watumishi mapema kwa kuwapa mafunzo ya kuwaongezea weledi na kuwawezesha kupata sifa za kujaza nafasi zinazoachwa wazi na wastaafu.
Nitaendelea kukataa maombi ya kuwaajiri kwa mkataba watumishi ambao sio adimu kwenye soko la ajira. Aidha, ninawaagiza waajiri wote kuandaa na kutekeleza ipasavyo mipango wa kurithishana madaraka ili wakati wote wawepo watumishi wenye sifa za kujaza nafasi zinazoachwa wazi na watumishi wanaostaafu kwa lazima.
Kuacha kazi na kuomba kuajiriwa tena
Ndugu Washiriki,
Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la watumishi kuacha kazi kwa mwajiri mmoja, na kuomba kazi kwa mwajiri mwingine ndani ya Utumishi wa Umma bila kujua kuwa mwajiri bado ni Serikali hiyo hiyo. Mathalani, katika mwaka 2013 na 2014 wapo zaidi ya watumishi 353 “wapya” ambao Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) ulibainisha kuwa walikwishawahi kuajiriwa Serikalini na sasa wanaomba kuajiriwa kwa mara ya pili. Hali hiyo imesababishwa na watumishi husika ama kutojua utaratibu au kwa kushauriwa vibaya na waajiri.
Kuanzia sasa, watumishi wanapotaka kuomba kazi kwa mwajiri mwingine watakiwe kufuata utaratibu uliowekwa badala ya kuchukua uamuzi wa kuacha kazi.
Uhamisho
Ndugu Washiriki,
Sheria ya Utumishi wa Umma imempa mamlaka Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kufanya uhamisho katika Utumishi wa Umma. Hata hivyo, imeanza kujengeka tabia ya baadhi ya waajiri kukataa kuwapokea watumishi wanaohamishiwa katika taasisi zao au kutowaruhusu watumishi walionao kuhama kwa visingizio mbalimbali. Hali hii ikiachwa kuendelea itaathiri sana utendaji na ufanisi wa kazi. Ninawaelekeza ninyi washiriki wa Mkutano huu kuwashauri ipasavyo Watendaji Wakuu wenye tabia hii waiache mara moja na watekeleze maamuzi yanayotolewa na mamlaka husika.
Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka
Ndugu Washiriki,
Kumbukumbu na nyaraka ni nyenzo muhimu sana katika utendaji wa kazi wa Serikali nzima na wa Taasisi yoyote katika kufikia malengo yaliyokusudiwa. Kwa mfano, kumbukumbu zinasaidia katika:
- Kupanga mipango ya maendeleo;
- Kupima uwajibikaji;
- Kutoa maamuzi sahihi kwa wakati;
- Kugawa na kusimamia rasilimali;
- Kudhibiti matumizi ya fedha;
- Kusimamia utawala wa sheria na uwajibikaji;
- Kuendeleza ushirikiano kati ya nchi na nchi katika sekta mbalimbali; na
- Kushughulikia maslahi ya watumishi wakiwa kazini na wanapostaafu katika Utumishi wa Umma, miongoni mwa faida nyingine.
Ili Serikali iweze kufikia malengo yaliyotajwa hapa juu na kuwawezesha wananchi kujua mwenendo wa Serikali yao, lazima kuwe na kumbukumbu zinazotunzwa vizuri na kupatikana kwa urahisi. Kukosekana kwa taarifa sahihi na kwa wakati kunawafanya watendaji wa Serikali kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kusababisha ucheleweshaji wa maamuzi au kutolewa kwa maamuzi yasiyo sahihi na yasiyokidhi matarajio ya wananchi. Sote tunatakiwa, na ni wajibu wetu, kuzingatia taratibu za utunzaji bora na matumizi ya kumbukumbu na nyaraka za Serikali katika Ofisi zote za Umma.
Vilevile ninyi washiriki wa Mkutano huu mnao wajibu kuhakikisha kuwa siri za Serikali zinabaki kuwa siri na hazivuji, na pale zinapovuja hatua stahiki zinachukuliwa mara moja ili iwe fundisho kwa wengine.
Hitimisho
Ndugu Washiriki,
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu wake, napenda kuwapongeza wote miongoni mwenu mnaotekeleza majukumu yenu kwa haki, uadilifu na weledi mkubwa. Napenda tu kuwakumbusha tena umuhimu wa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.
Aidha, ninaiagiza Tume ya Utumishi wa Umma iendelee kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu kwa kufanya kaguzi za mara kwa mara na kunipatia taarifa za utendaji kazi ipasavyo ili kuniwezesha kuchukua hatua zinazostahili. Kama vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anavyokagua matumizi ya fedha za umma, Tume Utumishi wa Umma nayo lazima ikague utekelezaji wa masuala ya utawala na rasilimaliwatu.
Mwisho kabisa, napenda muelewe uzito na unyeti wa mamlaka yenu katika Utumishi wa Umma na Taifa kwa ujumla. Fanyeni kazi kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, bila kuzipinda wala kuzivunja. Watendeeni haki watumishi wote, na mjali maslahi yao na kuwaendeleza. Mkifanya hivyo heshima ya Utumishi wa Umma mbele ya jamii itaimarika kwa faida yetu sote.
Baada ya kusema hayo, sasa napenda kutamka kwamba mkutano huu umefunguliwa rasmi na ninakutakieni majadiliano mazuri na yenye tija.
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
- Jun 10, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE WAKATI WA UZINDUZI WA CHAPISHO LA TATU LA TAARIFA ZA MSINGI ZA KIDEMOGRAFIA,...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Waziri Mkuu;
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar;
Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi;
Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mawaziri Waliopo;
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
Waheshimiwa Mabalozi;
Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi;
Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu;
Viongozi wa Serikali wa Ngazi Mbalimbali;
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi;
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu;
Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar;
Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Viongozi wa Madhehebu ya Dini;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Shukrani na Pongezi
Ndugu Wananchi;
Awali ya yote, naomba tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo. Napenda pia kuwashukuru waandaaji wa hafla hii kwa kunipa heshima kubwa ya kuzindua Chapisho la Tatu la Taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi Linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.
Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa maelezo yako mazuri ya awali kuhusu Chapisho hili. Nakupongeza wewe, pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa uongozi wenu mzuri wa zoezi la Sensa. Chapisho tunalozindua leo ni matunda ya kazi nzuri mliyoifanya ya kuziongoza Idara za Takwimu za Serikali zetu mbili ambazo ndizo zilizosimamia na kuendesha zoezi lenyewe la sense ya watu na makazi.
Sensa inaendeshwa kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Takwimu (the Statistic Act) sura ya 351. Katika kipindi chote cha miaka 50 ya Muungano wetu tumefanya Sensa mara tano, mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.
Umuhimu wa Chapisho la Tatu
Ndugu Wananchi;
Sensa ni zoezi pana sana. Sensa ni zaidi ya kuhesabu watu. Sensa hujumuisha pia kukusanya na kufanya uchambuzi wa taarifa kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii. Taarifa hizo husaidia Serikali katika utungaji wa sera na kutengeneza mipango na mikakati ya maendeleo nchini. Tangu kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Idara Kuu ya Takwimu ya Taifa na Idara ya Takwimu Zanzibar ambazo ndizo zilizohusika na zoezi hili zimeendelea kutoa matokeo kulingana na kalenda ya utoaji wa matokeo ya Sensa. Matokeo ya mwanzo nilitolewa tarehe 31 Desemba, mwaka 2012 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Siku ile nilitangaza jumla ya idadi ya watu nchini Tanzania. Chapisho la pili lilihusu mgawanyo wa watu kwa umri na jinsi ambalo lilitolewa tarehe 25 Septemba, 2013.
Chapisho la Tatu ninalolizindua leo linatoa taarifa za msingi za kidemografia (mnyumbuliko wa idadi ya watu), kijamii na kiuchumi zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Taarifa za Chapisho la Tatu zina umuhimu wa aina yake. Zinaonesha Tanzania imepiga hatua kiasi gani katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha, upatikanaji wa taarifa katika kipindi hiki utaviwezesha vizazi vijavyo kuifahamu Tanzania ilivyokuwa mwaka 2012.
Muhtasari wa Matokeo ya Chapisho la Tatu
Ndugu Wananchi;
Sensa ya Mwaka 2012 imefanyika katikati ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Miaka 5 (2011-2016). Mpango huu tunaoendelea kuutekeleza una lengo la kutufikisha kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 na ile ya Zanzibar ya mwaka 2020 ambapo tunatarajia kuwa nchi yetu itakuwa imefikia uchumi wa kati. Kwa utaratibu huu wa kufanya Sensa kila baada ya miaka 10, ina maana kuwa Sensa inayofuata itafanyika mwaka 2022 ikiwa ni miaka michache kabla ya kufikia Dira ya Taifa. Hivyo, matokeo haya ni msingi wa kupima mwelekeo wetu kiuchumi na kijamii kufikia lengo letu la kuwa uchumi wa kati ifikapo 2020 kwa upande wa Zanzibar na 2025 nchi nzima.
Chapisho hili lina takwimu nyingi sana kuhusu nyanja mbalimbali za maisha ya Watanzania. Takwimu hizi zinatupa fursa ya kujua maeneo tunayofanya vizuri na yale tunayohitajika kuyaimarisha. Vilevile, zinatuonyesha yale maeneo ambayo tulidhani tunafanya vizuri lakini kumbe siyo, hivyo basi tunatakiwa kuyawekea mkakati maalum. Hali kadhalika, taarifa zinatuamsha kuona yale maeneo mapya ambayo hatukuwahi kuyafikiria lakini sasa tunapaswa kuyaangalia kwa karibu.
Kwa ujumla, kulingana na takwimu za Sensa ya 2012, idadi ya watu Tanzania iliongezeka kutoka watu milioni 34.4 mwaka 2002 hadi watu milioni 44.9 mwaka 2012. Hii ni sawa na kasi ya ongezeko la asilimia 2.7 kwa mwaka. Kwa kasi hii ya ongezeko la watu, Tanzania Bara inatarajiwa kuwa na watu milioni 63.3 mwaka 2025 ambao ndiyo mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2025 kwa Tanzania Bara. Aidha, Zanzibar inatarajiwa kuwa na watu milioni 1.8 ifikapo mwaka 2020 ambao ndiyo mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar. Kwa kasi hii ya ongezeko la idadi ya watu Tanzania inatarajiwa kuwa na watu milioni 125 mwaka 2050.
Ndugu Wananchi;
Ili kufikia dira zetu za maendeleo, yaani ya mwaka 2020 kwa Zanzibar na ya mwaka 2025 kwa nchi nzima ambapo tutakuwa na idadi ya watu takribani milioni 65.1, inatupasa kujitazama tulipotoka na tulipo leo. Kwa mujibu wa Chapisho hili la Tatu, tumepiga hatua kubwa na nzuri katika maeneo mengi, na hivyo kuashiria kuwa tuko katika mstari sahihi kuelekea Tanzania tunayoitamani. Baadhi ya takwimu hizi kwa ufupi ni zifuatazo:
- i. Zaidi ya asilimia 90 ya watu wote Tanzania walizaliwa baada ya Muungano wa mwaka 1964. Tafsiri yake ni kwamba idadi kubwa ya Watanzania ni vijana ambao wamezaliwa, kukua na kufaidika na matunda ya Muungano. Hiki ni kiashiria kikubwa kuwa tumeweza kujenga utaifa mpya, yaani utanzania katika miaka 50 ya Muungano wetu.
- ii. Hii ni Sensa ya tano tangu Muungano wetu mwaka 1964. Sensa ya kwanza ilikuwa mwaka 1967, ya pili mwaka 1978, ya tatu mwaka 1988, ya nne mwaka 2002 na ya tano 2012. Takwimu za Sensa za kati ya mwaka 1967 na mwaka 2012 zinaonesha kuwa idadi ya watu wa Tanzania ambao wanaishi mijini imeongezeka kutoka asilimia 6 mwaka 1967 hadi asilimia 30 mwaka 2012. Ukuaji huu wa miji ni kiashiria muhimu kuwa safari yetu ya kuelekea uchumi wa katini ya uhakika. Hatuna budi sasa, sera na mikakati yetu kuielekeza katika kuhakikisha miji yetu inao uwezo wa kuhimili ongezeko hili la watu kwa maana ya utoaji wa huduma za kijamii na ajira.
- iii. Katika kipindi cha miaka 50 wastani wa umri wa kuishi kwa mtoto wa Kitanzania anayezaliwa umeongezeka kutoka miaka 41 mwaka 1967 hadi kufikia miaka 61 mwaka 2012. Maana yake ni kuwa, huduma za afya zimeimarika, watu sasa wanaishi kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Hata hivyo, bado hatujafikia viwango vya wenzetu wa Asia na Ulaya ambao wastani wao ni miaka 70 na kuendelea.
- iv. Vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka vifo 115 kati ya kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai mwaka 1988 hadi kufikia vifo 45 mwaka 2012. Na, mwaka 2013 tumefikia 21. Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 231 mwaka 1988 hadi 68 mwaka 2012 na 2013 tumefikia vifo 54 kwa 1,000. Pia, idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi imepungua kutoka vifo 578 kwa kila akina mama 100,000 wanaojifungua mwaka 2004/2005 hadi 454 mwaka 2010 na kwa mujibu wa takwimu za Sensa, vifo hivi vimeendelea kupungua hadi 432 mwaka 2012. Hii ni hatua kubwa kuelekea lengo la Milenia ya Mwaka 2015 ya vifo 193.
- v. Asilimia ya kaya zinazopata maji safi ya kunywa imefikia asilimia 57 mwaka 2012. Vile vile, kaya zinazotumia umeme kama nishati ya kuangazia zimeongezeka kutoka asilimia 10 mwaka 2002 hadi asilimia 21 mwaka 2012.
- vi. Kwa upande wa sekta ya elimu, asilimia ya watu wenye umri wa miaka 10 na zaidi wanaojua kusoma na kuandika kwa Tanzania Bara imeongezeka kutoka asilimia 31 mwaka 1967 hadi kufikia asilimia 78 mwaka 2012. Kwa Zanzibar kiwango hiki kimeongezeka kutoka asilimia 39 mwaka 1967 hadi asilimia 86 mwaka 2012.
- vii. Takwimu zinazoonesha kwamba umaskini wa kipato umepungua kutoka asilimia 33.6 mwaka 2007 hadi asilimia 28.2 mwaka 2012.
- viii. Takwimu zinaonesha kwamba makazi ya wananchi wote wa Tanzania yaliyojengwa kwa vifaa vya kisasa (zege, mawe, saruji na vyuma) yameongezeka. Familia zinazoishi kwenye nyumba za bati zimeongezeka kutoka asilimia 46 mwaka 2002 hadi asilimia 65 mwaka 2012.
- ix. Vilevile, umiliki wa simu za kiganjani umeongezeka sana. Mwaka 2012 wastani ulikuwa ni asilimia 64 ikilinganishwa na asilimia 10 mwaka 2005. Kuongezeka kwa simu ni kiashiria cha kuongezeka kwa biashara, idadi ya watu wanaotumia huduma za kifedha kwa njia ya simu na urahisi wa mawasiliano ambao unawezesha usambazaji wa taarifa za kijamii na kibiashara katika maeneo mengi hivi sasa.
Mazingatio Yatokanayo na Chapisho la Tatu la Sensa
Ndugu Wananchi;
Ufupi au urefu wa safari unaweza kuujua tu iwapo unafahamu unapotoka, ulipo na unapokwenda. Taarifa ambazo zimewasilishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu zinaonesha kuwa tumepata mafanikio ya kuridhisha katika maeneo mengi, na kuwa tumekuwa tunasonga mbele mwaka hadi mwaka na siyo kurudi nyuma. Kwa hiyo matokeo haya yanapaswa kuwaongoza Viongozi na Watendaji wa ngazi zote katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kujua maeneo ambayo kasi ya utekelezaji wa programu za maendeleo kwa wananchi ilikuwa ndogo, na hivyo kustahili kupewa msukumo mpya katika utekelezaji wake.
Ndugu Wananchi;
Nimefarijika kusikia kuwa taarifa za Sensa zinaonesha hatua kubwa tuliyopiga katika kuleta usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake. Ingawa viashiria vingi bado vinaonekana bora zaidi kwa wanaume kuliko wanawake, lakini pengo kati yao limepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma. Kwa mfano, asilimia ya wanaume wenye umri wa miaka 10 na zaidi wanaojua kusoma na kuandika ilikuwa asilimia 45 kwa Tanzania Bara na asilimia 55 kwa Zanzibar mwaka 1967. Kwa upande wa wanawake ilikuwa asilimia 19 na asilimia 23 kwa Tanzania Bara na Zanzibar mwaka 1967. Taarifa za Sensa ya Mwaka 2012 zinaonesha kuwa pengo hili limepungua sana. Wanaume wenye umri wa miaka 10 na zaidi wanaojua kusoma na kuandika kwa mwaka 2012 ni asilimia 82 ya wanaume wote kwa Bara ukilinganisha na asilimia 75 kwa wanawake. Kwa upande wa Zanzibar, idadi ya wanaume wanaojua kusoma na kuandika ni asilimia 89 ya wanaume wote kulinganisha na asilimia 83 ya wanawake.
Hatuwezi kupata maendeleo makubwa na endelevu bila kuhakikisha usawa wa kijinsia. Wanawake ni asilimia 51 ya Watanzania wote, hivyo, hatuna namna yoyote tunayoweza kulipuuza kundi hili kubwa, ambalo ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote katika shughuli za maendeleo. Ndiyo maana, tumeelekeza juhudi kubwa kurekebisha kasoro hii ya kihistoria na kimfumo kwa kuwapa wanawake fursa ili nao washiriki sawia katika shughuli za maendeleo katika ngazi ya familia, jamii na hata taifa. Ni vyema ikaeleweka kuwa hatuwapendelei wanawake bali tunawapatia kile wanachostahili kupata kama raia na kama wanadamu. Stahili ambazo wamekuwa wakizikosa kwa miaka mingi.
Serikali itaendelea kuimarisha juhudi za utekelezaji wa Sera ambazo zinalenga kuhakikisha kuwa pengo hili linazibika ili Watanzania wote wafaidike na rasilimali za Taifa bila ya kujali jinsia zao.
Maelekezo kwa Tume ya Taifa ya Takwimu
Ndugu Wananchi;
Nimesema hapo awali kuwa lengo kubwa la kufanya Sensa ni kutoa takwimu ambazo zitachangia katika jitihada za kuboresha maisha ya Watanzania. Taarifa za sensa ambazo zitasaidia kuboresha sera za nchi kwa mambo mbalimbali, kupanga na kutathmini programu za maendeleo na uimarishaji wa utoaji wa huduma za jamii. Lengo hili haliwezi kufikiwa ikiwa taarifa za sensa na nyinginezo kwa ujumla wake hazitawafikia watumiaji wote wanaozihitaji. Ofisi za Takwimu zina jukumu la kutoa takwimu katika mfumo mzuri na lugha rahisi na kuzisambaza na kuhamasisha matumizi yake.
Pamoja na usambazaji wa taarifa za sensa kwa vitabu na machapisho, tumieni tovuti na njia nyingine za kisasa kusambaza taarifa zenu. Ninafarijika kusikia kwamba tayari mmeanza juhudi hizi, kwani uzinduzi wa Chapisho hili la tatu utaenda sambamba na uzinduzi wa usambazaji wa taarifa kwa njia ya mtandao.
Ofisi za Takwimu zimetimiza wajibu wake wa kutoa takwimu na sasa ni jukumu la Wizara, Idara,Taasisi za Serikali na watumiaji wengine wote kuzifanyia kazi. Natoa agizo kwa viongozi ngazi zote za utawala kutafsiri matokeo haya kwa kuoanisha na utekelezaji wa sera na programu za maendeleo ya kisekta katika maeneo yao. Matokeo haya ya Sensa sasa ndiyo rejea yetu ya takwimu katika mipango yetu ya utekelezaji. Kile kisingizio cha kukosekana kwa takwimu mpya sasa kimefikia ukomo. Takwimu ni kitendea kazi, sasa mnazo na mkazifanyie kazi, siyo kuendeleza semina za kujadili matatizo na mapungufu. Takwimu zimetuonyesha mafanikio tuliyoyapata na mapungufu yaliyopo ambayo mkayatatue na siyo kuyajadili.
Wito kwa Wananchi na Wadau
Ndugu Wananchi;
Napenda pia kutoa wito kwa wananchi na wadau wa maendeleo hasa asasi za kiraia kusoma taarifa hizi na kuzitumia vizuri. Kumekuwepo na upotoshaji mkubwa sana wenye kubeza mafanikio yaliyopatikana nchini kutokana na jitihada za Serikali na wananchi kwenye kuleta maendeleo. Taarifa hii inaweka wazi ukweli ulivyo. Zitumieni. Kama upotoshaji ulikuwa ni kwa sababu ya kukosekana kwa rejea ya takwimu sahihi, takwimu ndizo hizo kwa kila mmoja wetu kuziona na kuzitumia. Asiyefanya hivyo ana lake jambo.
Hitimisho
Ndugu Viongozi Wenzangu;
Ndugu Wananchi;
Niruhusuni nirudie tena kuwashukuru washirika wetu wa maendeleo waliotusaidia kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi. Kwa namna ya pekee nawashukuru Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Taasisi za Umoja wa Mataifa ikiwemo UNFPA, UNDP na UNICEF. Nawashukuru tena Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda na Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Seif Idd kwa uongozi wenu mzuri uliowezesha zoezi zima la sensa kufanikiwa. Pia, nawapongeza viongozi na watendaji wa Idara zetu mbili za Takwimu kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya. Umakini na umahiri wao ndiyo uliotufikisha hapa. Nawashukuru na kuwapongeza viongozi wote wa Serikali wa ngazi zote za utawala ambao walishiriki kwa ukamilifu katika maandalizi na hatimaye utekelezaji wa Sensa ya Mwaka 2012. Nitoe pia shukrani kwa viongozi wa vyama vya siasa, madhehebu ya dini na mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa ushiriki wenu hasa kwenye hatua ya uhamasishaji wa ushiriki wa umma. Nawashukuru wadau wetu wa maendeleo kwa michango yao muhimu ambayo imesaidia kufanikisha sensa hii.
Shukrani za kipekee ziwaendee Wananchi wote ambao walijitokeza kuhesabiwa na kujibu maswali ya sensa kwa ufahamu mkubwa. Kukubali kwao kushiriki ndiko chanzo kilichowezesha kupatikana taarifa tunazozindua leo na nyingine zitakazofuata. Ni dhahiri kuwa Serikali yetu imetimiza kwa ufanisi jukumu la kufanya Sensa ya Watu na Makazi nchini. Lengo limetimia la kujua hali halisi ya rasilimali watu iliyopo Nchini kama zilivyofanya Awamu zote zilizotangulia.
Ndugu Wananchi;
Baada ya kusema maneno haya ya utangulizi, sasa, kwa heshima na taadhima kubwa, napenda kutamka kwamba Chapisho la Taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Pamoja na Matumizi ya Tovuti katika kupata taarifa mbalimbali za Sensa ya Watu na Makazi limezinduliwa rasmi.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa kunisikiliza!
- Jun 07, 2014
HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA UFUNGUZI WA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NA Y...
Soma zaidiHotuba
Mhe. Mama Salma Kikwete, Mlezi wa MEWATA;
Mhe. Kebwe Steven Kebwe (Mb.), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii;
Mhe Fatma Mwasa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora;
Wakuu wa Wilaya – Tabora, Nzega na Urambo;
Wabunge Wote wa Mkoa wa Tabora Mliopo;
Dkt. Serafina Mkuwa, Mwenyekiti wa MEWATA;
Wawakilishi wa Washirika Wetu wa Maendeleo;
Dkt. Joseph Komwihangiro, Mwakilishi wa Marie Stopes;
Madaktari Wote wa MEWATA na Watumishi wa Sekta ya Afya;
Mwakilishi wa Shirika la Marie Stopes na Wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Waliopo;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Niruhusuni nianze kwa kuwashukuru Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.
Seif Rashid (aliyewakilishwa hapa leo na Naibu Waziri Mhe.Dkt. Stephen Kebwe)
na Mwenyekiti wa Chama cha Madakatari Wanawake Tanzania (MEWATA), Dkt.
Sarafina Mkuwa kwa kunialika kuja kuzindua huduma za uchunguzi wa saratani
ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora. Nawapongeza nyote
kwa maandalizi mazuri kwani ni ukweli usiopingika kuwa shughuli hii imefana sana.
Aidha, nawashukuru wenyeji wetu wa Mkoa wa Tabora wakiongozwa na Mkuu wa
Mkoa, Mheshimiwa Fatma Mwasa, kwa mapokezi mazuri mliyonipatia mimi, mke
wangu na wageni wenzetu. Sikutegemea kupata mapokezi tofauti na haya hapa
Tabora, kwani upendo wenu kwangu na ukarimu wenu tunaujua na unasifika na
wengi.
Ndugu Wananchi;
Nimekubali kuja kujumuika nanyi katika uzinduzi huu, siku ya leo, ili kuongeza
sauti yangu na uzito kuhusu shughuli hii muhimu na adhimu inayofanywa na
Madaktari Wanawake hapa nchini. Ni ukweli ulio wazi kuwa MEWATA imesaidia
kuokoa maisha ya akinamama wengi nchini ambao, vinginevyo, wangepoteza uhai
Shukrani na Pongezi
Madhumuni ya Ziara
kwa saratani hizi mbili zinazowapata wanawake. Hatuna budi kuvunja ukimya na
kuungana na Madaktari Wanawake kuzungumzia maradhi haya na kuelimishana
ili wananchi, wadau na Serikali kwa umoja wetu au mmoja mmoja, tuchukue hatua
stahiki za kukabiliana na maradhi haya.
Aidha, ni nafasi nzuri ya kutoa pongezi zangu kwa wanachama wa MEWATA
kwa kazi kubwa na nzuri waifanyayo na mafanikio yaliyopatikana. Sijui hali ya
maradhi haya ingekuwaje hapa nchini kama Madaktari Wanawake wasingeamua
kufanya kazi hii njema wanayoifanya. Kwa niaba ya wanawake na wanaume wote
wa Tanzania tafadhali pokeeni pongezi zetu za dhati. Endeleeni kufanya kazi hii
njema na Mwenyezi Mungu atawalipa kwa wema wenu na mioyo yenu ya huruma.
Nawaahidi kuendelea kuwaunga mkono kwa hali na mali na kwa kadri ya uwezo
utakavyoniruhusu.
Nimefurahi sana kwamba ndugu zetu wa MEWATA wameweza kufika hapa
Tabora siku ya leo. Mtakumbuka kuwa nilipokuja kwenye Sherehe za Siku ya
Wanawake Duniani tarehe 8 Machi, 2010, niliahidi kwamba nitawaomba MEWATA
waje kufanya uchunguzi wa saratani za mlango wa kizazi na matiti kwa akinamama.
Hayawi hayawi leo yamekuwa. Nawashukuru sana viongozi na wanachama wa
MEWATA kwa kuja kwenu. Mmenitoa kimasomaso. Wahenga walisema: “Ada ya
Mja kunena, muungwana na vitendo”. Ndugu zangu wa Tabora ahadi imetimia, kazi
kwenu. Jitokezeni kwa wingi kupima muokoe maisha yenu.
Ndugu Wananchi,
Tanzania inatambulika kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango kikubwa cha
maradhi ya saratani ya mlango wa kizazi hapa Afrika ya Mashariki. Inakadiriwa
kuwa takriban wanawake 56 katika kila wanawake 100,000 hupata saratani hii.
Inakadiriwa pia kuwa zaidi ya watu 35,000 wanapata saratani hii kila mwaka na zaidi
ya watu 27,000 hupoteza maisha. Mwaka 2010 peke yake, wanawake wapatao 6,000
waligundulika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na wanawake 4,000 kati yao
walifariki dunia.
Wataalamu wanatuambia kuwa, saratani hii huwapata wanawake wa umri wa
miaka 30 na 50. Aidha, wanawake wanaoishi na virusi vya UKIMWI wako katika
hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo kwa asilimia 50. Pamoja na tatizo hili, bado
tunayo changamoto ya saratani ya matiti ambayo ni ya pili kwa kusababisha vifo
vya wanawake wengi nchini. Hivyo basi, hapa nchini wanawake wako kwenye
hatari kubwa ya kufa kwa saratani kuliko wanaume kwa sababu saratani nyinginezo,
hazibagui ukiacha ile ya tezidume inayowapata wanaume pekee.
Hali ya Magonjwa ya Saratani ya Wanawake Nchini
Hatua za Tahadhari za Kuzingatiwa
Bahati nzuri, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti zinaweza kutibika
ikiwa zitagunduliwa mapema. Njia pekee ya kuweza kugundua mapema ni kupima
mara kwa mara. Wataalamu wanashauri kuwa ni vyema wanawake wenye umri
wa kati ya miaka 30 na 50 wakachunguza afya zao walau mara moja katika kila
miaka mitatu. Na, kwa wanawake wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanashauriwa
kuchunguzwa walau mara moja kwa mwaka.
Bahati mbaya sana, uzoefu umeonyesha kuwa wanawake wengi hufika
hospitali wakati ambapo ugonjwa umeshapea na kuenea sehemu nyingine za
mwili. Wanakwenda hospitali wakati maradhi yamefikia hatua isiyoweza kutibika
na hivyo kupoteza maisha. Hivyo basi, kupima na kugundulika mapema kwa
saratani ni hatua muhimu sana ya kuepusha vifo vinavyotokana na maradhi hayo.
Bahati nzuri hivi karibuni kumekuwepo na mwamko na mwitikio mzuri wa kujitokeza
kwa wanawake wengi kupima saratani ya matiti. Haya ni matunda ya kazi nzuri
inayofanywa na MEWATA. Juhudi hizi zinapaswa kuendelezwa. Zinastahili
kuungwa mkono.
Ndugu Wananchi;
Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na saratani ya mlango wa
kizazi. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeanzisha Programu inayoshughulikia
masuala ya Saratani za Uzazi katika Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto mwaka
2008. Kupitia programu hii tuna Mpango Mkakati wa Kukinga na Kudhibiti Saratani
ya Mlango wa Kizazi (2011-2016). Mwongozo wa kutoa huduma umeandaliwa
pamoja na miongozo ya mafunzo kwa watoa huduma na ujumbe wa kuelimisha
jamii kupitia njia mbalimbali. Kupitia programu hii tumeweza kuanzisha vituo zaidi
ya 130 vinavyotoa huduma ya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi katika
Mikoa 17 hapa nchini. Ukilinganisha na mwaka 2008 tulipokuwa na vituo vinne tu
vilivyokuwa vinatoa huduma hii ya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na
tiba ya mabadiliko ya awali, haya ni maendeleo makubwa.
Ndugu Wananchi,
Kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Serikali imeendelea kushirikiana
na wadau mbalimbali wakiwemo MEWATA, Marie Stopes, WAMA na wengineo
kutekeleza mpango wa “Utepe wa Pinki na Utepe Mwekundu” yaani “Pink Ribbon Red
Ribbon”. Kupitia program hiyo, kampeni ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa
kizazi na matiti ilizinduliwa katika mkoa wa Mwanza mwezi Machi mwaka huu katika
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Kupitia mpango huo, tumekabidhi mashine 16 za kutolea huduma za matibabu
ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi (Cryotherapy machine) kwa
Hatua Zinazochukuliwa na Serikali
mikoa ya Mwanza, Mara, Iringa, Njombe na Mbeya. Mipango inaendelea kwa mikoa
iliyosalia pamoja na Tabora kupatiwa mashine hizo kuendeleza juhudi za Serikali
kupanua upatikanaji wa huduma hizi katika mikoa yote nchini.
Lengo letu katika kufanya hivyo ni kutaka kupunguza mzigo mkubwa
unaoielemea Hospitali yetu ya kuu kansa ya Ocean Road. Pia, tunataka
kuwapunguzia wanawake adha na gharama ya kusafiri umbali mrefu hadi Dar es
Salaam kwa ajili ya uchunguzi. Tunatambua umuhimu wa huduma hizi kuwa karibu
zaidi na walipo watu ili ziwafikie wanawake wote bila kujali hali zao za kipato.
Ndugu Wananchi;
Katika jitihada za kutokomeza maradhi haya, Serikali, kupitia Mpango wa Taifa
wa Chanjo, imeanza kutoa chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa Kizazi ya
“Human Papilloma Virus (HPV)”. Chanjo hii hutolewa kwa watoto wa kike wenye
umri wa miaka 9. Chanjo hii hukinga wasipate maambukizi ya virusi ambavyo
husababisha Saratani ya Mlango wa Kizazi. Wizara ya Afya tayari imezindua
mpango huo wa utoaji wa chanjo ya HPV kwa wasichana tarehe 29 Aprili, 2014
wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Duniani na mama Salma Kikwete.
Mpango huo ulizinduliwa kwa Halmashauri tano za Hai, Siha, Moshi Vijijini, Moshi
Mjini na Rombo za Mkoa wa Kilimanjaro, kuashiria kuanza kwa utekelezaji wa azma
ya kutoa chanjo hii nchi nzima ifikapo mwaka 2016.
Ndugu Wananchi;
Napenda kutoa pongezi na shukrani za pekee kwa MEWATA kwa kazi nzuri
na kubwa ya kukuza uelewa wa jamii na kuhamasisha uchunguzi wa saratani
zinazowapata wanawake. Ni dhahiri kwamba ili jambo hili lifanikiwe lazima liwe na
mshika bango wake. Bahati nzuri ndugu zetu wa MEWATA wamejitoa kimasomaso
na wamefanya kazi ya Serikali kuwa rahisi. MEWATA imekuwa inafanya kazi kwa
karibu na Serikali pamoja na wadau wengine katika kuhamasisha jamii kuhusu
masuala ya Saratani ya Matiti na ya Mlango wa Kizazi. Kama nilivyokwisha kusema
awali, juhudi hizo zimewafikia wanawake wengi nchini na kuokoa maisha yao.
Aidha, napenda kuchukua fursa hii kutambua na kutoa shukrani maalum
kwa Shirika la Marie Stopes na wadau wote ambao wanashirikiana na Serikali
katika kupambana na tatizo hili kubwa la Saratani ya Mlango wa Kizazi. Vilevile,
tunawashukuru wale wote wanaotoa huduma ya afya ya uzazi na mtoto nchini.
Napenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia ushirikiano wa Serikali ya CCM
ninayoiongoza kwenu. Ni, dhamira yetu kupunguza na ikiwezekana hata kumaliza
kabisa vifo vitokanavyo na Saratani ya Mlango wa Uzazi na Saratani ya Matiti
ambazo kwa kweli zinaweza kuzuilika.
Shukrani kwa Wadau
Wito kwa Wananchi
Ndugu Wananchi;
Natoa wito kwa wanawake wa Tabora kujitokeza kwa wingi kufanyiwa uchunguzi
wa saratani hizi na wataalamu walioko hapa. Napenda kuwatoa hofu kuwa saratani
ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti siyo magonjwa ya aibu au ya mkosi au
uchawi au laana na wala siyo magonjwa yasiyotibika. Magonjwa haya huweza
kumpata mwanamke ye yote, awe ameolewa au hajaolewa, awe amezaa au
hajazaa, awe tajiri au maskini. Madhali ni mwanamke anaweza kupata. Sharti lake
la kupona ni kugundulika mapema na kuanza tiba mapema. Kuchelewa kugundulika
na kuchelewa kuanza matibabu ndiko kunakosababisha vifo kutokana na maradhi
haya. Waswahili wana msemo usemao, mficha maradhi kifo humuumbua. Hivyo
ndugu zangu kina mama nashauri mfanye uchunguzi mapema, ili kama kuna tatizo
muanze tiba mapema.
Napenda kutumia fursa hii, kuwaasa akina baba na walezi nao kusaidia katika
juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa haya ya saratani ya wanawake. Mwanamke
anayepata magonjwa haya anahitaji matunzo na upendo siyo masimango na
unyanyapaa. Masimango na unyanyapaa huwafanya wanawake waogope
kujitokeza kuchunguza afya zao na kupatiwa tiba kwa kuogopa kubaguliwa au
kuachwa. Magonjwa haya yanatibika. Si kila mwanamke anayepata saratani
hufariki dunia. Kinachotakiwa ni baba na mama kushirikiana kumpeleka mama
kufanyiwa uchunguzi na kupata tiba iwapo atagundulika kuwa na maradhi. Saratani
siyo ugonjwa wa zinaa, hivyo, msiwanyanyapae akina mama bali muwalee na
kuwatunza ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida. Akina baba muwe ndiyo
nguzo ya mafanikio katika mapambano dhidi ya saratani.
Na, kwa wanaume wenzangu, tujenge mazoea ya kupima afya zetu hususan
kuhusu saratani ya tezidume (prostate). Hii ni saratani inayoua wanaume wengi
duniani na hapa nchini. Lakini nayo kama zilivyo saratani za matiti na mlango wa
kizazi zinatibika kama zitagundulika mapema. Kila mkienda kupima afya pimeni afya
ya tezidume mjue mustakabali wenu.
Ndugu Wananchi;
Sote tukiungana pamoja tunaweza kutokomeza saratani ya mlango wa kizazi na
saratani ya matiti. Nia ya kutokomeza maradhi haya tunayo, sababu ya kutokomeza
tunayo na uwezo wa kuyatokomeza tunao. Kinachotakiwa ni kuunganisha nguvu
zetu pamoja. Mimi na mke wangu Mama Salma Kikwete tuko nanyi na tutaendelea
kuwa nanyi bega kwa bega katika vita hii sasa na hata baada ya kuacha Urais
mwakani. Inawezekana, timiza wajibu wako!
Ndugu Wananchi;
Kwa vile niko Tabora ni vyema nikatumia nafasi hii pia, kuyazungumzia baadhi
ya mambo niliyoyazungumzia au kuahidi kufanya safari zilizopita. Kwa upande wa
barabara, napenda kuwahakikishia kuwa barabara kuu zinazoendelea kujengwa
hapa Mkoani Tabora tutazimaliza. Subira yavuta heri. Barabara ya Urambo –Kaliua
ujenzi utaanza mwaka huu wa fedha na Chaya – Nyahua, mchakato wa kutafuta
fedha unaendelea ili nayo ujenzi wake uweze kuanza kabla ya mimi kumaliza kipindi
changu cha uongozi. Kuhusu kupata maji ya Ziwa Victoria, kwa Igunga, Nzega,
Tabora, Urambo na Sikonge hatua za awali zimeanza na kinachofuatia ni kutafuta
fedha kwa ajili ya mradi huo mkubwa. Tunakusudia kuiomba Serikali ya India
ambayo ndiyo iliyogharamia matayarisho ya mradi. Tuna matumaini ya kufanikiwa.
Sote tuzidi kuomba iwe hivyo.
Kwa upande wa tatizo la wakulima wa tumbaku kutokulipwa stahili zao na
vyama vya ushirika nimeelezwa na kulielewa. Kuna tuhuma za wizi na ubadhilifu.
Nimemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi atume watu wake wa upelelezi wa
makosa ya Jinai waje wafanye uchunguzi ili wahusika wakamatwe na kufikishwa
Mahakamani na kupewa adhabu zinazostahili. Ameniahidi kuwa keshokutwa
Jumatatu watu hao watakuja. Wapeni ushirikiano unaostahili ili tukomeshe uhalifu
na dhuluma zinazofanywa na Maofisa wa Vyama vya Ushirika na taasisi za fedha
kwa muda mrefu sasa.
Baada ya kusema hayo, naomba nitangaze sasa zoezi hili la uchunguzi wa
Saratani ya Mlango wa Kizazi na ya Matiti limefunguliwa rasmi.
Nawashukuruni sana.
- May 31, 2014
REMARKS BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, DURING THE MATERNAL, NEWBORN AND CHILD HEALTH COUNTDOWN EVENT AND A...
Soma zaidiHotuba
Deputy Minister for Health and Social Welfare;
Regional Commissioners;
Members of the Diplomatic Corps;
UN Resident Coordinator;
Representatives of the Global Partnership for Maternal, Newborn and Child
Health;
CEO of the Children’s Investment Fund;
Ladies and Gentlemen,
Good morning!
I thank the organizers for associating me with this all important
event convened for the purpose of discussing progress on the health of
women and children in our countries. I welcome all delegates who have
travelled from a far to attend this meeting. It speaks volumes about your
commitment to this noble course. I say welcome to Tanzania and I hope
your hosts are taking good care of you.
Ladies and Gentlemen;
Today, we are 600 days away from the deadline set to achieve
the Millennium Development Goals (MDGs). For some of us who were
privileged to take part in the Millennium Summit in New York in 2000,
the year 2015 was a decade and a half too far away. It was far enough
to allow optimism that, come 2015, the world would achieve all the 8
MDGs. Our optimism overrode the fact that, the task ahead of us was
larger than time. Today, we can say with confidence that a lot has been
achieved, yet a lot more has not or needs to be done.
The Value of Information and Accountability on MDG
Ladies and Gentlemen;
Our experience in implementing MDGs has taught us that without
periodic reviews and clear timelines, goals in themselves do not impose
discipline in execution. It was during the 2010 UN Summit on MDG's
Implementation Review when reality sunk that, the world was lagging
behind in achieving MDGs by many indicators. We took the wise
decision then to accelerate the pace of implementation. This resulted a
number of initiatives, among them, the establishment of the Commission
on Information and Accountability for Women's and Children's Health,
which Honourable Stephen Hamper, Prime Minister of Canada and I had
the privilege to co-chair.
The Commission came out with a number of observations and
10 recommendations that emphasized the need for information for
better results, better tracking of resources and better oversight. The
Commission defined accountability in a circle of act, monitoring and
review. It recommended countries to conduct countdown events, which
involve analysing progress and identifying gaps and key interventions
needed to address them.
Today's countdown event is a result of comprehensive analysis
done by the global countdown team, the Health Sector Strategic Plan III,
and Maternal Newborn and Child Health Road Map, midterm reviews.
It coincides with the launching of the Accelerated Sharpened Plan that
will guide our focus and efforts in the remaining time leading up to 2015.
This plan will also lay a strong foundation for our strategic direction
towards ending preventable maternal and child deaths in post 2015.
Ladies and Gentlemen;
Tanzania has managed to reach its MDG-4 target before 2015,
reaching an under-five mortality rate of 54 per 1,000 live births. The
continuing decline can be attributed to sustained high immunization
coverage, improved malaria control, integrated management of
childhood illnesses, within a supplementation coverage and health
sector reforms.
Tanzania Experience in Implementation of MDG 4 & 5
Despite this achievement, gaps remain in newborn care, nutrition
and care-seeking and management of childhood illnesses in particular
diarrhoea and pneumonia. We constantly remind ourselves that, the
achievements we have attained are not a cause for complacency, but a
reason to encourage us to do more to accelerate the gains.
Ladies and Gentlemen;
We are still grappling with the challenge of reducing maternal
mortality. Much as we have scored a reduction of 45 percent from the
1990 levels, at the current rate of 454 per 100,000 live births, we are still
far from the MDG 5 target of 133 per 100,000. We need to ensure,
essential services reach more families especially the poor and focus on
addressing inequalities. There is need to prioritize the most critical time
which is birth and the first few days of life through linking the community
to facility home based care. In tandem with this we must continue to
strengthen health care systems.
Reviews have shown that, factors that are influencing the slow
progress in reducing maternal mortality include low utilization of family
planning services, low coverage of care at birth by skilled providers and
low postnatal care. Other factors outlined included need for stronger
accountability towards ensuring quality provision of maternal and child
health services at all levels. The review also noted the need to reduce
inefficiencies in mapping and tracking of scope and resources of
implementing partners.
Ladies and Gentlemen;
In 2012 Tanzania signed the commitment to renew our promises
to children to improve child survival. We have never reneged from this
course. Today, we renew our promise to ensure children’s health and
survival. We shall continue to strive for accelerated progress to scale up
key cost effective interventions in the continuum of care to further lower
the neonatal and child mortality as we approach 2015. Beyond 2015 we
shall join with other nations to ensure that we take necessary action to
bend the curve and reduce under-five mortality to less than 20 per 1,000
The Government Commitment
live births per 100 live births by 2030.
Ladies and Gentlemen;
Today I will be launching the Reproductive Maternal Newborn and
Child Health Score card. The scorecard has been developed for
maternal, newborn and child health outcomes. I am told this will be used
to track progress at both national and regional levels. I have directed all
levels to take this scorecard seriously and I will closely follow up. I urge
them to make full use of the scorecard to identify areas of weakness and
take corrective action. They should realize that, they are equally
accountable for the lives of women and children in their areas of
administration. The score card results should be submitted to my office
and to the Prime Minister every four months with explanation of what is
being done to rectify areas of poor progress.
Ladies and Gentlemen;
I task each level to ensure appropriate prioritization of required
interventions. This is important since there exist mixed experiences
within and between districts and regions, as far as maternal, newborn
and child health care is concerned. In Singida region for example,
health facilities are more enabled to provide good services. I am told all
life saving commodities are in place and, there is improved motivation at
the work place. This is happening because there is a committed and
accountable leadership with regard to the provision of the recommended
Reproductive, Maternal, Newborn and Child Health Services. This
region and others which are showing good performance should be
emulated. As I congratulate them, I also implore and encourage them to
do more. For those regions with poor performance, I urge them to learn
from the best practices of their counterparts and improve on their
performance.
Ladies and Gentlemen;
The Government is currently implementing the Big Results Now
(BRN) program which aims at accelerating progress towards achieving
our five year development plan. The first sectors in this programme
include Education, Water, Agriculture, Infrastructure, Energy and
Transport. Because of the critical importance of health and urgency
to do something comprehensive now, I have directed the Presidential
Delivery Bureau to initiate a process to include the health sector in
the BRN initiative. Of course, accelerating progress in women’s and
children’s health will be accorded special attention in this regard. This
means, we will commit more resources in accelerating women and
children’s health.
A Call for Action
Ladies and Gentlemen;
I would now like to take this opportunity to make a passionate
call to all Tanzanians, to play their role responsibly to ensure women
do not die while giving life to other human being and our children
survive the delicate first one month, and first five years as well as
get proper nutrition in the first 1,000 days. While the government and
our development partners continue with efforts to improve access to
information and quality reproductive and child health services, the
community has to play its role accordingly. I call upon the men folk to
ensure that they are involved in reproductive and child health services
and accord the required support to ensure healthy families. Everyone
has a role to play and should be accountable to play their part.
Ladies and Gentlemen;
I am personally committed to see acceleration in interventions, as
well as more accountability and better results with regard to women’s
and children’s health delivery by 2015. My personal involvement in the
United Nations Commission speaks loud on my commitment. I want this
to be a permanent political agenda at all levels of our government. We
must use this opportunity to ensuring that every level takes this matter
seriously. The undertaking made by the Regional Commissioner today
is very reassuring indeed.
It would be remiss of me if I concluded my remarks without
thanking our Development Partners, Non-Governmental Organizations
both local and international, groups and individuals, on your commitment
Conclusion
and support. It has made a huge difference for the better, so far. And,
what was said today by the USAID, UN Resident Representative and
Global Countdown Team is very reassuring indeed that there is a better
future for women and children in Tanzania.
Ladies and Gentlemen;
I thank you for your kind attention!
- May 15, 2014
REMARKS BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, DURING THE MATERNAL, NEWBORN AND CHILD HEALTH COUNTDOWN EVENT AND A PRO...
Soma zaidiHotuba
Deputy Minister for Health and Social Welfare;
Regional Commissioners;
Members of the Diplomatic Corps;
UN Resident Coordinator;
Representatives of the Global Partnership for Maternal, Newborn and Child Health;
CEO of the Children’s Investment Fund;
Ladies and Gentlemen,
Good morning!
I thank the organizers for associating me with this all important event convened for the purpose of discussing progress on the health of women and children in our countries. I welcome all delegates who have travelled from a far to attend this meeting. It speaks volumes about your commitment to this noble course. I say welcome to Tanzania and I hope your hosts are taking good care of you.
Ladies and Gentlemen;
Today, we are 600 days away from the deadline set to achieve the Millennium Development Goals (MDGs). For some of us who were privileged to take part in the Millennium Summit in New York in 2000, the year 2015 was a decade and a half too far away. It was far enough to allow optimism that, come 2015, the world would achieve all the 8 MDGs. Our optimism overrode the fact that, the task ahead of us was larger than time. Today, we can say with confidence that a lot has been achieved, yet a lot more has not or needs to be done.
The Value of Information and Accountability on MDG
Ladies and Gentlemen;
Our experience in implementing MDGs has taught us that without periodic reviews and clear timelines, goals in themselves do not impose discipline in execution. It was during the 2010 UN Summit on MDG's Implementation Review when reality sunk that, the world was lagging behind in achieving MDGs by many indicators. We took the wise decision then to accelerate the pace of implementation. This resulted a number of initiatives, among them, the establishment of the Commission on Information and Accountability for Women's and Children's Health, which Honourable Stephen Hamper, Prime Minister of Canada and I had the privilege to co-chair.
The Commission came out with a number of observations and 10 recommendations that emphasized the need for information for better results, better tracking of resources and better oversight. The Commission defined accountability in a circle of act, monitoring and review. It recommended countries to conduct countdown events, which involve analysing progress and identifying gaps and key interventions needed to address them.
Today's countdown event is a result of comprehensive analysis done by the global countdown team, the Health Sector Strategic Plan III, and Maternal Newborn and Child Health Road Map, midterm reviews. It coincides with the launching of the Accelerated Sharpened Plan that will guide our focus and efforts in the remaining time leading up to 2015. This plan will also lay a strong foundation for our strategic direction towards ending preventable maternal and child deaths in post 2015.
Tanzania Experience in Implementation of MDG 4 & 5
Ladies and Gentlemen;
Tanzania has managed to reach its MDG-4 target before 2015, reaching an under-five mortality rate of 54 per 1,000 live births. The continuing decline can be attributed to sustained high immunization coverage, improved malaria control, integrated management of childhood illnesses, within a supplementation coverage and health sector reforms.
Despite this achievement, gaps remain in newborn care, nutrition and care-seeking and management of childhood illnesses in particular diarrhoea and pneumonia. We constantly remind ourselves that, the achievements we have attained are not a cause for complacency, but a reason to encourage us to do more to accelerate the gains.
Ladies and Gentlemen;
We are still grappling with the challenge of reducing maternal mortality. Much as we have scored a reduction of 45 percent from the 1990 levels, at the current rate of 454 per 100,000 live births, we are still far from the MDG 5 target of 133 per 100,000. We need to ensure, essential services reach more families especially the poor and focus on addressing inequalities. There is need to prioritize the most critical time which is birth and the first few days of life through linking the community to facility home based care. In tandem with this we must continue to strengthen health care systems.
Reviews have shown that, factors that are influencing the slow progress in reducing maternal mortality include low utilization of family planning services, low coverage of care at birth by skilled providers and low postnatal care. Other factors outlined included need for stronger accountability towards ensuring quality provision of maternal and child health services at all levels. The review also noted the need to reduce inefficiencies in mapping and tracking of scope and resources of implementing partners.
The Government Commitment
Ladies and Gentlemen;
In 2012 Tanzania signed the commitment to renew our promises to children to improve child survival. We have never reneged from this course. Today, we renew our promise to ensure children’s health and survival. We shall continue to strive for accelerated progress to scale up key cost effective interventions in the continuum of care to further lower the neonatal and child mortality as we approach 2015. Beyond 2015 we shall join with other nations to ensure that we take necessary action to bend the curve and reduce under-five mortality to less than 20 per 1,000 live births per 100 live births by 2030.
Ladies and Gentlemen;
Today I will be launching the Reproductive Maternal Newborn and Child Health Score card. The scorecard has been developed for maternal, newborn and child health outcomes. I am told this will be used to track progress at both national and regional levels. I have directed all levels to take this scorecard seriously and I will closely follow up. I urge them to make full use of the scorecard to identify areas of weakness and take corrective action. They should realize that, they are equally accountable for the lives of women and children in their areas of administration. The score card results should be submitted to my office and to the Prime Minister every four months with explanation of what is being done to rectify areas of poor progress.
Ladies and Gentlemen;
I task each level to ensure appropriate prioritization of required interventions. This is important since there exist mixed experiences within and between districts and regions, as far as maternal, newborn and child health care is concerned. In Singida region for example, health facilities are more enabled to provide good services. I am told all life saving commodities are in place and, there is improved motivation at the work place. This is happening because there is a committed and accountable leadership with regard to the provision of the recommended Reproductive, Maternal, Newborn and Child Health Services. This region and others which are showing good performance should be emulated. As I congratulate them, I also implore and encourage them to do more. For those regions with poor performance, I urge them to learn from the best practices of their counterparts and improve on their performance.
Ladies and Gentlemen;
The Government is currently implementing the Big Results Now (BRN) program which aims at accelerating progress towards achieving our five year development plan. The first sectors in this programme include Education, Water, Agriculture, Infrastructure, Energy and Transport. Because of the critical importance of health and urgency to do something comprehensive now, I have directed the Presidential Delivery Bureau to initiate a process to include the health sector in the BRN initiative. Of course, accelerating progress in women’s and children’s health will be accorded special attention in this regard. This means, we will commit more resources in accelerating women and children’s health.
A Call for Action
Ladies and Gentlemen;
I would now like to take this opportunity to make a passionate call to all Tanzanians, to play their role responsibly to ensure women do not die while giving life to other human being and our children survive the delicate first one month, and first five years as well as get proper nutrition in the first 1,000 days. While the government and our development partners continue with efforts to improve access to information and quality reproductive and child health services, the community has to play its role accordingly. I call upon the men folk to ensure that they are involved in reproductive and child health services and accord the required support to ensure healthy families. Everyone has a role to play and should be accountable to play their part.
Conclusion
Ladies and Gentlemen;
I am personally committed to see acceleration in interventions, as well as more accountability and better results with regard to women’s and children’s health delivery by 2015. My personal involvement in the United Nations Commission speaks loud on my commitment. I want this to be a permanent political agenda at all levels of our government. We must use this opportunity to ensuring that every level takes this matter seriously. The undertaking made by the Regional Commissioner today is very reassuring indeed.
It would be remiss of me if I concluded my remarks without thanking our Development Partners, Non-Governmental Organizations both local and international, groups and individuals, on your commitment and support. It has made a huge difference for the better, so far. And, what was said today by the USAID, UN Resident Representative and Global Countdown Team is very reassuring indeed that there is a better future for women and children in Tanzania.
Ladies and Gentlemen;
I thank you for your kind attention!
- May 14, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA HAFLA YA UZINDUZI WA HUDUMA YA M-PAWA MLIMANI CITY, MEI 14, 2014,...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia;
Mheshimiwa Balozi Mwanaidi Maajar, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakarugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania;
Ndugu Ndewirwa Kitomari, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Benki ya CBA;
Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa;
Ndugu Isaac Mwuondo – Mkurugenzi Mtendaji CBA;
Ndugu Muhoho Kenyatta, Mkurugenzi wa CBA;
Ndugu Rene Meza, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na viongozi wa Vodacom na CBA kwa kunialika kuja kujumuika nanyi kwenye sherehe hii adhimu ya kuzindua huduma mpya ya fedha kwa njia ya simu nchini ijulikanayo kama M-Pawa. Huduma ambayo itazidi
kurahisisha na kurasimisha malipo ya fedha, kuchochea utamaduni wa kuweka akiba, na kupanua wigo wa wananchi kufikiwa na huduma ya fedha.
Nawapongeza Vodacom na CBA kwa kutudhihirishia jinsi ambavyo huduma za benki na huduma za simu za mkononi zinavyoweza kutegemeana, kuunganishwa na kufanya kazi kwa pamoja. Kwa kufanya hivyo mnaweza kuwafikia Watanzania wengi na kuwapatia huduma za kifedha kwa njia rahisi na nafuu kupitia simu za mkononi. Aidha, wateja wenu watakuwa na akaunti zao benki na kuweza kuzitumia kwa kutumia simu zao za mkononi. Hongereni sana.
Mabibi na Mabwana;
Huduma hii ya M-Pawa ni nyenzo muhimu inayowezesha dhamira ya Serikali ya kutaka Watanzania wengi wafikiwe na kujumuishwa katika huduma rasmi za kifedha (financial inclusion). Lengo la Serikali ni kuona kuwa asilimia 50 ya watu wazima nchini wanatumia huduma za kibenki ifikapo mwaka 2016. Haya ndiyo matakwa ya Tamko la Maya, Mexico mwaka 2011, kuhusu kuwawezesha wananchi kuingia katika mfumo rasmi wa kifedha (Alliance for Financial Inclusion Global Initiative). Kwa ubunifu wa namna hii naamini lengo hilo tutalifikia.
Mabibi na Mabwana;
Taarifa zinaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2012, ni asilimia 17 tu ya Watanzania, ambayo ni sawa na watu wazima milioni 3.7 tu ndiyo waliokuwa na akaunti za benki. Kwa mujibu wa utafiti wa Benki ya Dunia (Global Findex 2012), wakati huo Tanzania ilikuwa nyuma ya wastani wa Afrika ambao ulikuwa asilimia 24. Pia tulikuwa nyuma ya Uganda ambayo ilikuwa imefikia asilimia 20 na Kenya ambayo ilikuwa asilimia 42. Kuanza kwa matumizi ya teknolojia ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu ya mkononi imekuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko. Kumewezesha Watanzania milioni 9.8 ambayo ni sawa na asilimia 43 kuingia kwenye mfumo rasmi wa fedha kwa kuwa na akaunti za fedha kwenye simu ilipofika mwaka 2013. Utafiti wa karibu wa FinScope Tanzania na FinScope Kenya idadi ya sasa ni watu milioni 12 ambayo ni sawa na asilimia 57 ya Watanzania watu wazima kuingia kwenye mfumo rasmi wa fedha kwa kuwa na akaunti za benki au za simu. Haya ni mafanikio makubwa na ya kujivunia. Tutalifikia lengo la asilimia 50 ifikapo 2016.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa bado fursa ni pana sana ya kuwezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na mifumo rasmi ya fedha kwani hivi sasa Watanzania milioni 30 wanatumia simu za mkononi. Utafiti uliofanywa na Wizara ya Viwanda na Biashara wakati wa mapitio ya Sera ya Biashara Ndogo na Kati (SMEs) iliyofanyika mwaka 2013 inaonesha kuwa, kati ya SMEs milioni 3 zinazokadiriwa kuwepo nchini, ni SMEs 620,000 tu, yaani asilimia 20 ndizo zinazotumia mfumo rasmi wa fedha. Asilimia 12 ya SME’s zinatumia mifumo ya kijamii/kienyeji na asilimia 70 hazitumii kabisa mifumo ya fedha. Hii inaonesha kuwa kuna fursa kubwa bado ya kuingiza asilimia 80 waliobakia kwenye huduma rasmi ya fedha. Natoa wito kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha pamoja na makampuni ya simu kuongeza kasi ya kuwahamasisha Watanzania kujiunga na mifumo rasmi ya fedha.
Mheshimiwa Waziri;
Mabibi na Mabwana;
Nawapongeza Vodacom na Benki ya CBA kwa ubunifu wao uliozaa huduma ya M-Pawa tunayoizindua leo. Huduma hii inaboresha zaidi huduma tuliyoizoea ya M-Pesa kwa kuwa sasa inaileta benki mkononi mwa mteja. Inamuwezesha mtu kuweka akiba, kufanya malipo na kwa mara ya kwanza kukopa fedha kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Ni matumaini yangu kuwa M-Pawa na mifumo mingine ya teknolojia ya habari inayofanana nayo itawahamasisha wananchi kuondokana na utamaduni wa kutunza fedha mchagoni na kuziweka katika njia salama zaidi. Kwa njia hii, tutaweza kujenga utamaduni wa kuweka akiba ya fedha ambao baadaye unaweza kuwa chachu katika ukuzaji uwekezaji hapa nchini.
Mabibi na Mabwana;
Huduma ya M-Pawa inajiunga na huduma zingine za fedha zilizopo ambazo tayari zimewanufaisha wananchi wengi. Watanzania zaidi ya milioni 10 sasa wanatumia huduma za fedha kupitia simu ya mkononi, na wanafanya miamala ya wastani wa shilingi trilioni 2 kwa mwezi.
Mabibi na Mabwana;
Ili mpango huu ufanikiwe kusambaa nchini kote tunahitaji kuwa na mifumo rasmi ya utambuzi, uhakiki na uthibiti wa wateja na taarifa muhimu zinazowahusu. Serikali itaendelea kufanya kazi na wadau wote wanaohusika katika sekta ya fedha pamoja na vyombo vya usalama na udhibiti kuhakikisha kwamba watu wetu wanakuwa na namna bora ya kutambulika. Hii itawaondolea ninyi watoa huduma hatari ya kuibiwa fedha na wateja wasio waaminifu. Ni matumaini yangu kuwa mifumo hiyo itakamilika mapema iwezekanavyo. Natambua kwamba kukamilika kwa zoezi la kuwapatia Watanzania vitambulisho kutasaidia sana kufanikisha mifumo ya utambuzi. Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha ndugu zetu wanaotoa vitambulisho vya taifa kuongeza kasi ya utoaji wa vitambulisho kwa Watanzania.
Mheshimiwa Waziri;
Mabibi na Mabwana;
Makampuni ya Vodacom na CBA yana historia nzuri ya ubunifu wa huduma. CBA ni miongoni mwa benki za mwanzo kutoa mikopo ya nyumba kwa utaratibu wa mortgage. Hali kadhalika, Vodacom ni wa kwanza kuleta huduma ya kutumia na kupokea fedha kwa njia ya simu. Mmeonyesha ujasiri mkubwa wa kuthubutu na kuwafikia wananchi hata wale ambao walionekana kuwa hawangestahili huduma hizi. Nina matumaini kuwa ubia wa makampuni yenu mawili utaleta ubunifu mkubwa zaidi siku za usoni.
Mheshimiwa Waziri,
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kama mjuavyo Dira ya Maendeleo ya Tanzania inalenga nchi yetu kuwa taifa la uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Lengo hilo litawezekana tu iwapo tutaweza kuwajumuisha Watanzania wengi zaidi katika sekta iliyo rasmi badala ya ilivyo sasa ambako wengi wapo sekta isiyo rasmi. Kupitia ubunifu wa aina hii ya M-Pawa kwa upande wa huduma ya fedha Watanzania wengi wataweza kupata fursa na uwezo wa kushiriki katika uchumi rasmi. Inaongeza uwezo wa taifa kufikia Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025. Naomba muendeleze ubunifu na sisi kwa upande wa Serikali tutaendelea kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Moja ya hatua ambazo Serikali imechukua kuboresha mazingira ya biashara kwa upande wa mawasiliano ni kujenga mkongo wa taifa. Mkongo huo wenye urefu wa kilometa 7,560 ndiyo muundombinu msingi uliowezesha mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano na fedha, mapinduzi yaliyozaa M-Pesa na sasa M-Pawa. Mkongo umewezesha kushuka kwa gharama za simu kwa asilimia 57 na gharama za intaneti kwa asilimia 75 katika kipindi kifupi cha tangu 2009 hadi 2013. Kushuka huku kwa gharama kulisababisha watumiaji wa intaneti kuongezeka kutoka wateja milioni 2.8 mwaka 2011 hadi milioni 9 mwishoni mwa mwaka 2013, na watumiaji wa simu kuongezeka kutoka milioni 3.6 mwaka 2005 hadi milioni 28 mwaka 2013. Lengo la Serikali ni kufikisha mkongo huu katika Wilaya zote nchini. Tutakapofanya hivyo tutakuwa na uwezo wa kuwafikia watu wengi zaidi na kuwezesha makampuni yanayotoa huduma za simu na intaneti kupata watumiaji wengi zaidi.
Mheshimiwa Waziri;
Mabibi na Mabwana;
Hakika mambo yetu ni mazuri. Mwenye macho haambiwi tazama. Na leo Vodacom na CBA wanafanya kuwa mazuri zaidi. Narudia tena kuwashukuru kwa kunishirikisha kwenye tukio hili la kihistoria. Narudia kuwapongeza ndugu zetu wa Vodacom na CBA kwa hatua hii kubwa ya maendeleo mliyopiga. Pia ni hatua muhimu ya maendeleo kwa taifa. Nawatakia mafanikio mema.
Kwa heshima na taadhima kubwa, sasa natangaza kuwa huduma mpya ya M-Pawa imezinduliwa rasmi Tanzania.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
- May 13, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa, Gaudentia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira;
Mheshimiwa Daktari Makongoro Mahanga, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira;
Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Naibu Waziri – TAMISEMI;
Mheshimiwa Magesa Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha;
Waheshimiwa Wabunge;
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Ndg, Abubakar S. Rajabu;
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ndugu Crecentius Magori;
Menejimenti ya NSSF;
Wageni waalikwa wenzangu;
Ndugu Wadau wa Hifadhi ya Jamii;
Mabibi na Mabwana;
Shukrani na Pongezi
Nakushukuru Mheshimiwa Waziri na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF kwa kunikaribisha kufungua mkutano wa nne wa wadau wa Hifadhi ya Jamii unaoanza leo hii hapa jijini Arusha. Mkutano wa mwaka huu una umuhimu wa kipekee kwani ni fursa ya kujipongeza kwa NSSF kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964. Wakati ule ikijulikana kama Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (NPF).
Nakupongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wajumbe wako, Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti ya shirika pamoja na wafanyakazi wote wa NSSF kwa kazi nzuri mnayoifanya na mafanikio yaliyopatikana. Kazi yenu inaonekana na inapimika. Kutokana na kazi yenu nzuri, mnawatia moyo wanachama wenu na kuwapa imani kuwa amana zao walizowekeza kwenu ziko salama, na kwamba mko tayari kukabiliana na changamoto za leo, na za miaka 50 ijayo.
Umuhimu wa Mikutano ya Wadau
Mheshimiwa Waziri na Wadau;
Nimefurahishwa na utamaduni wenu wa kuwa na mikutano hii ya wadau kila mwaka. Ni utamaduni mzuri kwani unatoa fursa ya wadau kushiriki katika kufanya tathmini ya mwaka hadi mwaka na kupeana mrejesho wa hali ilivyo miongoni mwa wadau. Utaratibu huu unasaidia kuamsha ari ya kutekeleza malengo. Ni fursa nzuri pia ya kuhuisha malengo yenu kuendana na mabadiliko ya mazingira, maana tofauti na zamani, mabadiliko katika dunia ya sasa yanakwenda kwa kasi kubwa. Huu ni utamaduni ambao hamna budi kuudumisha na kuuendeleza.
Umuhimu wa Hifadhi ya Jamii
Mheshimiwa Waziri na wadau wa hifadhi ya jamii,
Hifadhi ya Jamii ni haki ya msingi na asili ya kila mwanadamu. Msingi wa haki yenyewe ni kulinda thamani ya utu wa binadamu. Haki hii inazingatia kuwa binadamu kwa asili ni mwanajamii, anastawi tu akiwa miongoni mwa jamii na anachangia katika maendeleo ya jamii yake, hivyo, anayo haki ya kusitiriwa na kupata hifadhi kutoka kwa jamii pale uwezo wake wa kuchangia unapokoma kutokana na uzee, ulemavu au janga lisilotazamiwa.
Hifadhi ya jamii ina faida kwa mwanajamii na jamii yenyewe. Kwa upande mmoja inamkinga mwanajamii dhidi ya kupoteza utu na thamani katika jamii, na upande wa pili inaikinga na kuinusuru jamii dhidi ya madhara ya kiuchumi na kiusalama yanayoweza kusababishwa na kuwa na jamii iliyokata tamaa.
Upo uhusiano mkubwa kati ya ustawi wa jamii na hifadhi ya jamii. Ndio maana, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu wa mwaka 1948 umetambua haki ya binadamu kupata hifadhi na Katiba ya nchi yetu ya mwaka 1977, nayo imetambua haki ya kupata hifadhi ya jamii. Katika Ibara ya 11, ibara ndogo (i). Katiba inatamka kuwa “Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kupata elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi...” Huu ni wajibu wetu kikatiba na tutaendelea kuutekeleza.
Hali ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini
Ndugu Wadau;
Shughuli za Hifadhi ya Jamii nchini imeanza miaka 50 iliyopita na hatua kubwa imepigwa katika kipindi hicho. Sisi sote ni mashahidi wa mapinduzi makubwa yaliyofanyika katika Sekta hii. Idadi ya mifuko, wigo wa wanachama na idadi ya mafao.
Tulianza na Mfuko mmoja tu wa akiba ya wafanyakazi maaarufu kwa jina la NPF mwaka 1964. Leo tuna mifuko 6 ya NSSF, PPF, LAPF, GEPF, PSPF na NHIF. Wigo wa wanachama wa mifuko hii nao umetanuka. Mwanzoni ilihusu watumishi walioajiriwa, tena walichaguliwa mfuko wa kujiunga nao kutokana na sekta zao lakini leo tunao wanachama kutoka sekta binafsi waliojiajiri, na wako huru kuchagua mfuko wanaoupenda kujiunga nao. Hali kadhalika, mafao yaliyokuwa yakitolewa wakati ule yalikuwa ni mafao ya pensheni tu, tena kwa mkupuo mmoja, hivi sasa kuna mafao mengi na malipo ni kwa mwezi katika uhai wote wa mwanachama. Mafao mengine hufaidisha hata wategemezi wa mwanachama.
Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Hifadhi ya Jamii yamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa letu. Sekta hii ilichangia wastani wa asilimia 11 ya pato la taifa kwa mwaka 2011/2012. Mtaji wa mifuko hii sasa umefikia shilingi trilioni 5,242 kutoka trilioni 1.36 mwaka 2005/2006. Kutokana na hali nzuri ya ukwasi tayari mifuko hii imewekeza kiasi cha shilingi trilioni 4.4 mwaka 2012 ambapo asilimia 19 imewekezwa kwenye sekta ya ujenzi na makazi, asilimia 18 kwenye hisa na asilimia 63 kwenye amana za serikali na mikopo.
Miaka 50 kutoka Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (NPF) hadi Mifuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Ndugu Wadau wa Hifadhi ya Jamii;
Serikali, kupitia Sheria Na. 28 ya mwaka 1997, ilianzisha Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii – NSSF, kwa kuboresha Shirika la Akiba ya Wafanyakazi (NPF) lililoanzishwa mwaka 1964. Maboresho hayo yalilenga kuongeza ubora na idadi ya mafao, kupanua wigo wa wanachama na kuisaidia Serikali katika kutoa huduma za hifadhi ya jamii. Mabadiliko haya yaliliwezesha Shirika la NSSF kutoa mafao ya pensheni ya uzeeni, urithi na ulemavu kwa wanachama wake pamoja na mafao mengine kama vile matibabu, uzazi, fidia ya kuumia kazini na gharama za mazishi.
NSSF imeendelea kukua na kuimarika mwaka hadi mwaka. Thamani ya mfuko imeongezeka kutoka shilingi trilioni 1.97 katika mwaka 2011/2012 hadi kufikia shilingi trilioni 2.24 mwaka 2012/2013. Kuongezeka huko kwa thamani ya mfuko kumeambatana na kuongezeka kwa mafao yanayolipwa na NSSF kutoka shilingi bilioni 178 mwaka 2011/2012 hadi shilingi bilioni 228 mwaka 2012/2013.
NSSF imekuwa mchangiaji muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu kwa kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo inayochochea ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa ajira. Tumeona manufaa ya uwekezaji wa NSSF katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, daraja la Kigamboni, ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela na miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma na nyumba za wafanyakazi.
Inafurahisha kusikia kuwa shirika limetunukiwa cheti cha kimataifa cha utoaji wa huduma bora (ISO 9001:2008 CERTIFICATION), na hivi karibuni, kutunukiwa cheti cha utawala bora kwa kufuata kanuni bora za manunuzi na ugavi (PPRA Award). Kwa haya mawili nawapongeza sana na kuwaomba muendelee na viwango hivi vya ueledi. Maana shirika lenu ni nyeti katika uchumi wa taifa, kwa kuwa mmeaminiwa kuhifadhi na kuwekeza kwa fedha za akiba za wanachama. Umakini mkubwa unahitajika katika kuwekeza. Hamna budi kuwekeza vizuri ili mfuko uendelee kustawi na wanachama wake waendelee kupata hifadhi kutoka kwenu.
Wajibu wa Serikali: Usimamizi na Uendeshaji wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Ndugu Wadau wa Hifadhi ya Jamii;
Sisi katika Serikali tunao wajibu wa msingi wa kulea mifuko hii ili iweze kustawi na kuwa endelevu. Katika kutekeleza wajibu wetu huo, na kwa kuzingatia ukuaji wa sekta yenyewe, Serikali ilianzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) mwaka 2010. Lengo kuu la kuanzishwa kwa SSRA ni kusimamia na kuratibu shughuli zote katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho katika nyanja za uwekezaji na mafao yanayotolewa kwa wanachama.
Naipongeza Wizara ya Kazi na Ajira pamoja na Msimamizi na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kusimamia mageuzi ya kiutendaji na ya uendeshaji wa Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii. Naiomba SSRA iendelee kuboresha mazingira ya ushindani katika mifuko kwani ushindani hatimaye huleta unafuu kwa wanachama. Tumeona namna ambavyo ushindani umechochea kila Mfuko kuongeza ubunifu katika utoaji wa huduma na aina ya mafao yanayotolewa. Kazi kubwa waliyonayo sasa, ni kubuni mkokotoo mpya utakaosaidia kuoanisha mafao yatolewayo na mifuko hiyo.
Wito kwa NSSF na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Ndugu wadau wa hifadhi ya jamii,
Pamoja na mchango mkubwa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika uchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla, bado ni sehemu ndogo sana ya Watanzania wanapata kinga dhidi ya majanga kupitia Mifuko hii. Takwimu zinaonyesha kwamba kati ya Watanzania milioni 22.4 wenye uwezo wa kuzalisha kipato, waliomo katika Mifuko yote 6 si zaidi ya asilimia 6 tu. Idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya Watanzania ambao wanafanya kazi zenye kipato. Aidha idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na wastani wa asilimia 10 kwa nchi za Afrika na Kusini mwa Asia.
Kwa mujibu wa tathmini ya Sekta ya Viwanda na Biashara Ndogondogo (SMEs) ya mwaka 2013, sekta isiyo rasmi ilichangia asilimia 39.7 ya pato la taifa kwa mwaka 2010. Vile vile, ilikadiriwa kuwa zipo SMEs milioni 3 zinazoajiri wananchi milioni 5.2. Wito wangu kwenu ni mifuko ya hifadhi ya jamii kutoka maofisini kwenda kuhamasisha wananchi wengi wajiunge na mifuko hii. Waelezeni manufaa yake, na watoeni hofu zao juu ya fikra potofu walizonazo kuhusu hifadhi ya jamii. Wengi wanaamini hifadhi ya jamii ni stahili ya wafanyakazi wajiriwa tu, tena wafanyakazi wa kipato kikubwa. Wajulisheni kuwa hivi sasa hifadhi ya jamii ni fursa huru kwa wote, wale walioajiriwa na wale waliojiajiri. Wafafanulieni wale walio kwenye sekta isiyo rasmi kuwa, utaratibu wa wao kujiunga, kuchangia na kunufaika. Waonyesheni mifano hai ya wale wakulima na wajasiriamali namna wanavyochangia na wanavyofaidika.
Natoa rai hii nikitambua kuwa wako wananchi wengi katika sekta ya kilimo na sekta isiyo rasmi ambao kwa vipato vyao wangeweza kujiunga na hifadhi ya jamii. Nawapongeza NSSF kwa mpango wake wa kuwafikia wakulima na wachimbaji wa madini ambapo hadi sasa wakulima 29,000 wachimbaji madini 7000 wamejiunga na NSSF na wanafaidika na mafao yanayotolewa.
Uzoefu wa NSSF unatuonyesha kwamba wananchi wengi wamekosa tu uelewa na taarifa sahihi. Wakumbusheni kuwa hifadhi ya jamii si jambo jipya au la kigeni, hata katika jamii zetu kabla ya kuja kwa mifumo hii rasmi, kumekuwepo na utaratibu wa jamii kujiwekea mifumo ya hifadhi ya jamii. Katika jamii zetu kumekuwa na utaratibu wa kuwahudumia wazee, wasiojiweza na watoto. Mtu hakupoteza heshima na thamani yake katika jamii kwa kuwa amepoteza uwezo wake wa kuchangia katika jamii, ama kwa kustaafu, kwa ajali au kwa kutojaaliwa uwezo wa kuchangia.
Mabadiliko ya kidunia yameifanya mifumo hiyo sasa isiweze kuhimili jukumu hilo. Hivyo, mifuko ya hifadhi ya jamii ndio mbadala na salama ya ustawi wa mtu katika dunia ya leo. Wakumbusheni kuwa shida na majanga huwafika watu wakati ambao hawajajiandaa. Hivyo, ni vyema kujisitiri kabla hujasitiriwa.
Ndugu wadau wa hifadhi ya jamii,
Ni vizuri kukumbushana pia kwamba, uhai wa mifuko ya hifadhi ya jamii unategemeana pia na uendelevu wa michango ya wanachama. Hivyo, hatuna budi pia kutoa kipaumbele katika kuelimishana juu ya umuhimu na wajibu wa waajiri kuwasilisha michango ya wanachama kwa wakati. Mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuhakikisha inakusanya michango ya wanachama wake bila ajizi. Wahamasisheni wanachama wa mifuko juu ya umuhimu wa kuhakikisha michango yao inawasilishwa, na inabaki katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili iwafae wakati wa matatizo na maisha ya uzeeni. Waelemisheni juu ya athari ya tabia ya sasa ya baadhi ya watumishi kuamua kushirikiana na waajiri wasio waaminifu kutopeleka michango hiyo, au baadhi ya wanachama kujitoa katika mifuko ya awali pale inapotokea amebadilisha ajira kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwingine.
Mchango wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuelekea Dira ya 2025
Ndugu Wadau wa Hifadhi ya Jamii;
Mifuko ya hifadhi ya jamii ina wajibu mkubwa wa kuchangia juhudi za Serikali katika kufikia dira yetu ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Mifuko hii imeonyesha uwezo wa kuwekeza katika sekta na miradi ya uwekezaji wa muda mrefu ambayo sekta binafsi imekuwa ikikwepa. Miradi ya aina hii kama miundombinu msingi na nishati ndio inayoweza kukwamua nchi katika umasikini, na kuleta mapinduzi kimaendeleo.
Uzoefu huu unashawishi kuwa mifuko hii sasa itazame katika sekta ya Kilimo. Kilimo ndio sekta mama ya uchumi wetu na inaajiri zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wetu, lakini ukuaji wake ni asilimia 4.4 ambayo ni chini ya kiwango kinachotakiwa cha asilimia 6 kwa mwaka kutokana na kukosa uwekezaji wa kutosha. Ndio sababu, pamoja na kasi nzuri ya ukuaji wa uchumi ya wastani wa asilimia 7, umasikini umepungua kwa asilimia 2 tu.
Umasikini huzuia pia kasi ya ukuaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Hivyo, uwekezaji wenu katika sekta itakayosaidia kuondoa umasikini, ni kujitengenezea pia fursa kwa mifuko yenu kupata wanachama wengi zaidi siku za usoni. Tumeshuhudia namna ambavyo uwekezaji wa pamoja wa NSSF, PPF na PSPF wa kiasi cha asilimia 45 katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera kumezalisha ajira 3,500. Mbali na ajira, wataalam wanasema pia kuwa katika kila shilingi moja inayowekezwa vizuri kwenye kilimo, huzalisha faida ya hadi shilingi 3.2. Nawatia shime muangalie uwezekano wa kuwekeza katika kilimo hususan kwenye viwanda vya pembejeo za kilimo na vya kusindika na kuongeza thamani ya mazao. Tukiweza kuongeza thamani na kuepuka kuuza nje mazao ghafi, tutakuwa tumewatoa Watanzania wengi kutoka kwenye umasikini na mifuko yetu itapata wanachama wengi zaidi na wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuchangia mifuko hiyo.
Hitimisho
Ndugu wadau wa hifadhi ya jamii,
Kwa kumalizia napenda kwa mara nyingine tena kukushukuru Mheshimiwa Waziri kunialika na nikupongeze kwa namna unavyilea vizuri mifuko yetu ya hifadhi ya jamii. Nakupongeza Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF kwa uongozi wenu mzuri. Natoa pongezi nyingi kwa Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Ramadhani Dau kwa kazi nzuri unayoifanya, na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika NSSF chini ya uongozi wako. Nifikishie pongezi hizi pia menejimenti na wafanyakazi wote wa NSSF. Kazi mnayoifanya inaonekana na tuna matarajio ya kuona mengi na makubwa zaidi miaka hamsini ijayo.
Baada ya kusema hayo, napenda kutangaza kwamba mkutano huu wa nne wa wadau wa Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umefunguliwa rasmi. Nawatakia mkutano mwema.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza
- May 12, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI, TAREHE 12 MEI, 20...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Dkt. Kebwe Stephen Kebwe(Mb) – Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii;
Mheshimiwa Stanslaus Magesa Mulongo - Mkuu wa mkoa wa Arusha;
Ndugu Paul Magesa - Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania;
Ndugu Clavery Mpandana – Muuguzi Mkuu wa Serikali;
Daktari Khadija Malima, Mwenyekiti wa Baraza la Wauuguzi Tanaznia na Chama cha Wauguzi Tanzania;
Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana Ndugu Rais na viongozi wenzako wa Chama cha Wauguzi na Wakunga (TANNA) kwa heshima kubwa mliyonipa ya kuja kujumuika nanyi katika maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Wauguzi Duniani. Nakupongeza pia Mheshimiwa Magesa Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na wananchi wote wa Arusha kwa kutupokea vizuri na kwa kukubali kuwa wenyeji wa sherehe hii na kushiriki kwa ukamilifu katika kufanikisha maandalizi yake.
Nawapongeza nyote kwa maandalizi mazuri ya maadhimisho haya. Hakika yamefana sana. Nimefurahishwa na maonesho kuhusu baadhi ya shughuli zinazofanywa na wauguzi katika kuwahudumia Watanzania. Maonesho ya aina hii husaidia sana kukuza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu yenu, wajibu wenu na mchango wenu katika kuimarisha afya za Watanzania. Pamoja na kutembelea mabanda ya maonyesho, nimeshuhudia maandamano yenu na kusoma ujumbe kwenye mabango ya washiriki. Pia nimesikiliza Risala yenu iliyosomwa kwa ufasaha na utulivu mkubwa na Rais wa Chama cha Wauguzi Ndugu Paul Magesa. Kwa ujumla, maadhimisho haya yanadhihirisha kuwa wauguzi ni kiungo muhimu sana katika utoaji na maendeleo ya huduma ya afya nchini na ni nguvu thabiti ya mabadiliko.
Kauli Mbiu
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi na ndugu wananchi;
Nilipopata mwaliko kutoka kwenu sikusita kukubali kuja kujumuika nanyi siku ya leo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, kwamba wauguzi ni kada muhimu sana katika utoaji na maendeleo ya huduma ya afya nchini. Bila ya kuwepo wauguzi huduma ya afya itayumba. Natambua kuwa Wauguzi ni zaidi ya asilimia 60 ya watumishi wote wa sekta ya afya na hutekeleza asilimia 80 ya shughuli zote za afya. Aidha, Muuguzi ndiye mwenye kuandaa mazingira mazuri kwa daktari kutekeleza majukumu yake. Daktari anapomaliza kumuona mgonjwa, na kutoa maelekezo yake, Muuguzi husimamia utekelezaji wa maelekezo hayo pamoja na tiba yenyewe. Muuguzi ndiye anayefanya kazi ya kuuguza mgonjwa. Sote ni mashahidi kuwa wagonjwa wanatumia wakati mwingi zaidi mikononi mwa wauguzi kuliko muda wanaoutumia mikononi mwa wahudumu wengine wa afya.
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi;
Sababu ya pili ni kwamba nimevutiwa na kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo; “Wauguzi ni Nguvu ya Mabadiliko na Rasilimali Muhimu ya Afya”. Ni kauli mbiu sahihi na mwafaka kabisa. Ni ukweli ulio wazi kuwa wauguzi wanayo nafasi maalum katika maendeleo ya huduma ya afya na sekta yenyewe kwa jumla. Ni chachu muhimu ya mabadiliko katika sekta ya afya, na ndiyo rasilimali ya kuwezesha mabadiliko hayo kutokea na kufanikiwa.
Huwezi kuzungumzia mabadiliko katika sekta hii bila kutambua mchango wa Wauguzi na kuwahusisha. Ujenzi wa miundombinu ya vituo vya kutoa huduma ya afya, ununuzi na usambazaji wa madawa, ununuzi wa vitendea kazi vya kisasa katika hospitali zetu vitakuwa na maana tu pale ambapo wauguzi wapo na wanatimiza wajibu wao ipasavyo. Tunaweza kusema kwa uhakika kabisa kuwa hakuna mbadala wa wauguzi.
Ndugu Wananchi;
Uangalizi unaotolewa na wauguzi, upendo na huruma yao husaidia sana kurejesha matumaini ya wagonjwa na watu wengine wanaojishughulisha na maendeleo ya huduma ya afya. Huongeza ari ya mapambano dhidi ya maradhi na kuleta matumaini kwamba ushindi utapatikana. Ninyi ndiyo kioo cha huduma ya afya. Ndiyo watu wa kwanza mnaokutana na wagonjwa wanapofika hospitali, na ni watu wa mwisho kuwaona wanapotoka baada ya matibabu.
Mheshimiwa Naibu Waziri;
Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi na ndugu Wananchi;
Kuboresha huduma ya afya ni moja ya vipaumbele vya juu vya Serikali ninayoiongoza na ndiyo maagizo ya Ilani ya Uchanguzi ya Chama Tawala – CCM. Kwa sababu hiyo tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulitoa umuhimu wa pekee kwa zoezi la kupitia upya Sera ya Afya ya mwaka 1997 kwa lengo la kuihuisha. Matokeo yake ni kupatikana kwa Sera Mpya ya Afya ya mwaka 2007 na Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi wa mwaka 2007 uliotengenezwa maalum kuongoza utekelezaji wa Sera hiyo.
Kama mjuavyo huu ni mpango wa miaka kumi mpaka mwaka 2017 unaolenga kuleta mageuzi na maendeleo makubwa katika sekta ya afya. Kwa muhtasari tumepanga kufanya mambo makuu mawili. Kwanza, kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi wananchi kwa kujenga na kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya. Pili, kuimarisha ubora wa huduma ya afya inayotolewa kwa wananchi kwa kuvipatia vituo hivyo vifaa vya uchunguzi na tiba vilivyo bora pamoja na dawa za kutosha. Pia kuvipatia rasilimali watu, kwa maana ya Madaktari, Waganga, Wauguzi, Wakunga na Wataalamu wengine wa afya.
Ndugu Wauguzi na Ndugu Wanannchi;
Leo miaka karibu saba baadae ninyi ndiyo mashahidi wa mafanikio tuliyoyapata katika utekelezaji wa Mpango huu. Tumefanikiwa kwa kiasi cha kutia moyo ingawaje bado tunayo kazi kubwa mbele yetu. Kwanza kabisa tumeongeza sana bajeti ya afya kutoka shilingi bilioni 271 mwaka 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.4 mwaka 2013/2014. Imekuwa bajeti ya tatu kwa ukubwa baada ya elimu na miundombinu kutoka ya sita. Kwa sababu ya ongezeko hilo tumeshuhudia mambo mengi mazuri yakifanyika katika kuboresha huduma ya afya nchini. Kwa mfano, zahanati ziko 5,960 ukilinganisha na 4,930 zilizokuwepo mwaka 2007. Vituo vya afya viko 716 ukilinganisha na 565 na hospitali ziko 249 ukilinganisha na 230 wakati ule.
Kazi kubwa imefanyika kuimarisha hospitali za Wilaya, Mikoa, Kanda na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kazi bado inaendelea na tunaweza kusema ndiyo kwanza imechanganya. Miundombinu imeongezwa na majengo mengine yanaendelea kujengwa. Huduma zinaendelea kuboreshwa na nyingine ambazo hazikuwepo zimeanzishwa. Hali kadhalika vifaa tiba na uchunguzi vya kisasa vimeendelea kuwekwa na uwezo wa hospitali kuchunguza na kutibu maradhi umekuwa mkubwa.
Tumeendelea kupanua fursa za mafunzo na ajira kwa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wengine wa afya. Kwa upande wa mafunzo kwa mfano Madaktari waliojiunga na mafunzo wameongezeka kutoka 520 mwaka 2005 hadi 1,057 hivi sasa. Kwa Wauguzi na Wakunga wameongezeka kutoka 1,586 mwaka 2005 hadi 3,569 hivi sasa, kwa jumla kila kada imeongezeka. Ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili pale Mloganzila itaongeza sana uwezo wetu wa kufundisha Madaktari na Wauguzi kutoka Chuo hicho kutoka 3,000 mpaka 15,000. Ukiongeza na wanafunzi 5,000 wa Chuo cha Tiba katika Chuo Kikuu cha Dodoma tatizo la rasilimali watu nchini litapatiwa ufumbuzi miaka michache ijayo. Tayari ujenzi wa Hospitali ya Kufundishia ya vitanda 600 umeanza pale Mloganzila. Hospitali hiyo nayo itaimarisha ubora wa huduma ya uchunguzi na tiba ya maradhi kwa namna yake hapa nchini. Hali kadhalika ujenzi wa Hospitali ya Kufundishia pale UDOM unatarajiwa kukamilika mwaka huu.
Hivyo hivyo, kwa upande wa ajira nako kumekuwa na ongezeko. Idadi ya Madaktari waliosajiliwa imeongezeka kutoka 1,339 mwaka 2006 hadi 3,133 na Wauguzi kutoka 20,115 mwaka 2007 hadi 34,740 hivi sasa. Aidha, katika kipindi cha miaka 3 iliyopita, tumeajiri wauguzi 8,659 na tunatarajia kuajiri wengine 1,152 kabla ya Julai, 2014. Tutaendelea kufanya hivyo mwaka ujao wa fedha na miaka inayofuatia. Hii itasaidia kupunguza mzigo wa kazi mlio nao sasa hivi ambao mmeutaja kwenye risala yenu.
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi;
Kwa upande wa maslahi nako, tumejitahidi kuboresha, najua bado tunayo kazi kubwa ya kufanya mbele yetu. Bado mishahara ni midogo lakini hatujafika mwisho, tunaendelea kuboresha. Tumekuwa tunaongeza kila mwaka na tutaendelea kufanya hivyo mwaka huu na miaka ijayo.
Risala ya Wauguzi
Ndugu Wauguzi,
Nimesikiliza kwa makini risala yenu iliyowasilishwa vizuri na Ndugu Paul Magesa, Rais wa Chama cha Wauguzi na Wakunga. Namna ambavyo ameiwasilisha, lugha aliyotumia kuiwasilisha na jinsi mlivyoishangilia inathibitisha kuwa risala hii ni shirikishi, na yaliyosemwa ni mambo muhimu kwa wauguzi kwa ujumla wenu. Ni risala iliyosheheni ukweli kuhusu mafanikio tuliyoyapata na mambo yanayowatatiza mnayotaka yapatiwe ufumbuzi. Kuna ushauri mzuri uliotolewa kuhusu nini kifanyike kuboresha mazingira ya kazi ya Wauguzi na huduma ya afya nchini. Lazima nikiri kuwa nimeguswa sana na ahadi yenu ya kuendelea kufanya kazi kwa mujibu wa viapo vyenu, licha ya changamoto zilizopo.
Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inaelewa mchango wenu muhimu na inauthamini sana hivyo basi, sisi tutakuwa watu wa mwisho kupuuza mambo ya wauguzi. Kama kuna jambo halijafanyika haitokani na kupuuza au ukosefu wa dhamira ya kuyashughulikia bali kuna sababu fulani fulani za msingi zinazotukwaza katika utekelezaji wake.
Nimefurahishwa sana na dhamira yenu njema ya kutaka kuona mabadiliko yanafanyika katika sekta ya afya na ninyi kuwa sehemu kamili ya mabadiliko hayo. Ndiyo maana sehemu kubwa ya risala yenu ina mapendekezo ya mambo ya kubadilisha ili kuboresha utoaji wa huduma ya afya. Nawaunga mkono kwa msimamo wenu huo. Nimefarijika sana kusikia kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Wizara nyingine za Serikali kuwa mambo mengine yametekelezwa na yapo ambayo tunaendelea kuyatekeleza. Hata hivyo, bado yapo mambo ambayo tunayavutia pumzi kwa maana ya kujenga uwezo wa kuyatekeleza.
Ndugu Wauguzi;
Hii ni mara ya tatu napata nafasi ya kukutana na kuzungumza na viongozi wa Wauguzi. Mara ya kwanza ilikuwa Mnazi Mmoja mwaka jana, mara ya pili Ikulu tarehe 29 Aprili, 2014 na leo ndiyo mara ya tatu hapa Arusha. Jambo mojawapo muhimu nililojifunza ni kuwa mambo mengi yanayowatatiza wauguzi, ambayo pia yameainishwa katika risala yenu leo, yanaweza kumalizwa kwa kuboresha mawasiliano na mahusiano kati yenu na Wizara zinazohusika na kati yenu (wauguzi) na kada nyingine katika sekta ya afya. Naamini kama hayo yakifanyika mambo mengi yatapatiwa ufumbuzi na kwamba yatabaki machache yanayohitaji msaada wa ngazi za juu. Hii itasaidia kuondoa kutiliana mashaka, kutokuaminiana na hisia za kupuuzwa kwa wauguzi. Nimeona nitumie fursa ya maadhimisho haya ya leo kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya masuala tuliyozungumza siku zilizopita na yaliyoibuliwa hapa leo kwenye mabango na risala.
Madai ya Wauguzi
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi,
Katika risala yenu mmezungumzia mambo yahusuyo muundo wa utumishi, mafunzo, posho, huduma ya makazi na mambo mengineyo muhimu. Mambo yote haya ni ya msingi na napenda kuwahakikishia kuwa tutayachukulia kwa uzito unaostahili na tutayafanyia kazi ipasavyo ili tuwatengenezee mazingira mazuri ya kufanya kazi zenu.
Muundo wa Utumishi wa Uuguzi
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
NduguWauguzi;
Kwanza kabisa nawapongeza kwa kukamilisha mapendekezo ya Muundo wa Utumishi. Nitawasaidia kufuatilia kwa mamlaka husika ili uamuzi ufanyike mapema iwezekanavyo. Kukamilika kwa zoezi hilo kutatoa ufumbuzi kwa mambo mengi yanayowatatiza hivi sasa. Itayaweka sawa masuala ya upandishaji wa vyeo. Itawezesha kutambuliwa ipasayo kwa wauguzi wanaomaliza shahada za uzamili na uzamivu. Kwa kweli nashangaa kwa nini watu waliojiendeleza kiasi hicho wapate taabu ya kutambuliwa inavyostahili katika utumishi wa uuguzi.
Hivyo hivyo nashangaa tena napata taabu kuamini kuwa mtumishi akienda masomoni kuongeza ujuzi anasimama kupanda cheo au hata kushushwa cheo. Haya ni ya kustaajabisha mambo ambayo hayastahili kufanyika. Naomba Wizara na mamlaka husika zihakikishe kuwa uonevu huu hauendelei kufanyika. Iweje leo kujiendeleza iwe ni balaa kwa mfanyakazi na mwajiri badala ya kuwa jambo jema kwa wote.
Ndugu Wauguzi;
Nadhani suala la uanzishwaji wa Kurugenzi ya Uuguzi ndani ya Wizara ya Afya limefikia hatua nzuri. Nimeambiwa kuwa Wizara iliridhia maombi yenu na kuyawasilisha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Wataalamu wa Mifumo katika Idara Kuu ya Utumishi walichoshauri ni kuwa Sehemu ya Uuguzi sasa ipandishwe hadhi na kuwa Kitengo cha Uuguzi kitakachoongozwa na Mkurugenzi. Nimeambiwa pia kwamba Wizara ya Afya imekubali na tayari imefanya marekebisho na kuwasilisha upya pendekezo hilo. Nimesikia kuwa jambo hili litakamilishwa muda si mrefu na huenda muundo huo ukaanza tarehe 1 Julai, 2014 hivyo kuhitimisha maombi yenu. Niruhusuni niwapongeze kwa hatua iliyofikiwa mpaka sasa.
Maslahi ya Watumishi
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi;
Kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma, hususan mishahara na posho mbalimbali ni mambo ambayo Serikali imeyapa kipaumbele. Tumekuwa yunafanya hivyo kila mwaka na tutaendelea kufanya hivyo. Maombi yenu tumeyapokea na tutayafanyia kazi. Napenda kusema hata katika Bajeti ya mwaka ujao wa fedha hatua kiasi fulani zitachukuliwa.
Nimesikia kilio chenu kuhusu posho zilizoamuliwa kutokutekelezwa na ile ya sare za kazi ambayo imeahidiwa na kuongezwa kutoka shilingi 150,000 na kuwa Shilingi 300,000 kutokamilishwa mpaka sasa. Nitatoa maagizo kwa mamlaka husika katika Serikali kufuatilia na kuwabana, watakaokaidi. Hivyo hivyo, kwa posho ya kufanya kazi usiku, kama ilishaamuliwa ilipwe, mamlaka husika zitatakiwa kutekeleza bila ajizi.
Nyumba za Wauguzi
Serikali inatambua umuhimu wa wauguzi kuwa na makazi karibu na maeneo yao ya kazi. Kwa kutambua umuhimu huo Serikali imekuwa inatenga fedha za kujenga nyumba za madaktari na wauguzi kila mwaka. Hata hivyo kasi ya ujenzi ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa mahitaji kwa sababu ya ufinyu wa bajeti. Tutatafuta njia nyingine za kuharakisha ujenzi wa nyumba hizo. Mipango hiyo ikikamilika mtaona matokeo yake. Kwa sasa tutaendelea na kazi ya ujenzi wa nyumba katika mikoa ya Mtwara, Rukwa, Tabora na Mara.
Nimelipokea pendekezo lenu la kutaka msaidiwe kupata viwanja vya kujenga nyumba. Nitaagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wawasaidie. Miaka miwili iliiyopita niliagiza utengenezwe mpango maalum wa mikopo ya nyumba kwa watumishi wa umma. Matayarisho yanaendelea, ukikamilika utasaidia wafanyakazi wa umma wakiwemo Wauguzi kujipatia nyumba za kuishi.
Udhamini wa Mafunzo
Ndugu Rais wa Wauguzi;
Ndugu Wauguzi,
Nimesikia rai yenu ya kutaka Serikali itoe udhamini kwa wanafunzi wanaosomea shahada ya kwanza ya uuguzi kama tunavyofanya kwa wale wanaosomea udaktari. Nakubali maombi yenu, nitaagiza mamlaka husika walifanyie kazi. Kama hivi sasa wanafunzi hao siyo wengi tunaweza kuanza hata bajeti ijayo lakini kama ni wengi itabidi tuanze mwaka wa fedha wa 2015/16 lazima tujipange vizuri kwani inahusu pesa.
Naamini uamuzi huu utahamasisha wauguzi kujitokeza kwa wingi kujiendeleza kitaaluma. Wauguzi wasiishie kwenye Cheti na Diploma bali waende zaidi ya hapo. Napenda kuwahakikishia pia kwamba pamoja na uamuzi huu, Serikali bado itaendelea kudhamini wauguzi wanaosomea shahada ya uzamili na uzamivu kama tufanyavyo sasa. Nimesikia utayari wenu wa kupewa nafasi za uongozi katika Wizara ya Afya na kwingineko kama tulivyofanya kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Wito kwa Wauguzi
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi,
Tunapoadhimisha siku ya wauguzi, tunakumbuka pia siku ya kuzaliwa kwa Bi. Frorence Nightlingale, mwanzilishi wa taaluma na fani hii adhimu ya uuguzi. Mama Nightlingale aliyeishi kati ya mwaka 1820 hadi 1910 ndiye aliyeanzisha shule ya kwanza ya wauguzi huko London katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas. Alianzisha huduma hii baada ya uzoefu wake katika kuwashughulikia majeruhi wa kivita, na wanajeshi wagonjwa wakati wa vita.
Sifa yake kubwa ilikuwa ni wito na moyo wa kujitolea na huruma vitu ambavyo aliamini ndio misingi ya kuwa muuguzi. Alipata kunukuliwa akisema, “Kama muuguzi atakacha kutoa huduma kwa sababu yoyote ile au kusema haimuhusu, basi uuguzi kwake sio wito”. Kutokana na maisha yake ya kuwaangazia nuru wagonjwa na kuwatembelea usiku akiwa na taa ya kandili kuwafariji na kuwahudumia, alipewa jina la “Mwanamke Mwenye Kutembea na Nuru”.
Ndugu Wauguzi;
Ninyi ni watu wenye dhamana kubwa juu ya maisha ya watu na mnategemewa sana. Nawapongeza kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo. Kwa sababu yenu mmeokoa maisha ya watu wengi na kuwapunguzia maumivu wagonjwa. Wakati mwingine moyo wenu kuonyesha kujali, upendo na huruma hutoa matumaini kwa mgonjwa na kumrejeshea siha yake. Hivyo, nawaomba muendelee kuwa na kauli nzuri na nyuso zenye tabasamu na nyoyo za huruma na upendo kwa wagonjwa. Tabia hiyo ni tiba ya aina yake.
Nimeona niikumbushe hadithi ya muasisi Mama Florence Nightngale ili kuwaomba wakati wote iwaongoze na muendelee kukumbushana kuizingatia. Minong’ono kuwa mienendo ya baadhi yenu inalalamikiwa na wagonjwa kuwa hailingani na mafundisho ya muasisi wa kazi hii adhimu inanisumbua sana. Kama nilivyosema awali, ninyi ndiyo watu wa kwanza mnaokutana na mgonjwa akifika hospitali na ni watu wa mwisho anapotoka hospitali baada ya matibabu. Ikiwa mtakuwa na nyuso za ukatili na ulimi mkali au wa kebehi, mtakuwa mnawakwaza wagonjwa na hata kuongeza ukali wa maumivu yao. Wengine wanaweza kukata tamaa na hata kupoteza uhai. Msifanye watu wajutie kufika zahanati au hospitali. Narudia kuwasihi mzingatie kiapo chenu na maudhui ya kauli mbiu yenu ya kutaka mabadiliko. Kwa maana nyingine naomba mtambue kuwa kauli mbiu yenu ya mabadiliko inawahusu na nyie pia kama inavyotuhusu sote. Lazima mabadiliko yaanze na ninyi wenyewe.
Homa ya Dengue
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nizungumzie ugonjwa mpya wa Homa ya Dengue uliojitokeza katika jiji la Dar es Salaam hivi karibuni. Huu si ugonjwa asili kwetu. Ni ugonjwa wa huko Asia na Bara la Amerika lakini ndiyo umeshafika. Kwa mara ya kwanza ugonjwa huu ulijitokeza Jijini Dar es Salaam mwaka 2010 na kuathiri watu 40 ambao walipatiwa matibabu na kupona. Ugonjwa huu ulitoweka lakini ukaibuka tena Mei na Juni, 2013 ulipojitokeza tena na kuwakumba watu 172. Mwaka huu ugonjwa huo umerudia tena kwa kasi kubwa zaidi. Kati ya Januari na Aprili 6, mwaka huu wagonjwa 399 wamethibitika kuugua katika Jiji la Dar es Salaam. Kati ya wagonjwa hao 322 walitoka Wilaya ya Kinondoni, 61 Wilaya ya Ilala na 16 Wilaya ya Temeke. Kwa bahati mbaya wawili kati yao walipoteza maisha.
Ndugu wananchi;
Wataalamu wa afya wanasema kuna aina tatu za ugonjwa wa dengue. Aina ya kwanza ni Homa ya Dengue, aina ya pili ni Dengue ya Damu na aina ya tatu ni Dengue ya Kupoteza Fahamu. Hapa kwetu Homa ya Dengue ndiyo ugonjwa uliothibitika kuathiri wagonjwa wote. Homa hii ina dalili kubwa tatu: homa kali ya ghafla, kuumwa kichwa, na maumivu ya viungo au uchovu. Kwa vile dalili za ugonjwa huu zinafanana sana na dalili za ugonjwa wa malaria, ipo hatari kwa watu waliozoea kutumia dawa bila kupima kumeza dawa za malaria wakati wanaugua Homa ya Dengue. Wakifanya hivyo watahatarisha maisha yao. Natoa wito kwa mtu yeyote anayejisikia dalili hizi aende hospitali akapimwe; asinywe dawa bila kupima kama baadhi yetu tulivyozoea. Ni hatari kwa maisha yetu.
Ndugu Wananchi;
Ugonjwa huu unaambukizwa na mbu aina ya Aedes akishamuuma binadamu. Tena huuma mchana. Hatua za kupambana na mbu huyu ni sawa na zile zinazochulikuwa kupambana na mbu wa Anopheles anayeambukiza malaria. Watu waendelee kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa, kupaka dawa za kuzuia kuumwa na mbu na kuharibu maeneo ya mazalia ya mbu.
Nimetoa maelekezo kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha kuwa Bohari Kuu ya Madawa ya Serikali (MSD) wanaleta kits za kupimia maradhi haya (Dengue Rapid Test Kits) za kutosha na kuzisambaza kwenye hospitali na vituo vya afya. Nimeambiwa hivi sasa vipimo hivi havipo vya kutosha. Hii ni dharura ya kitaifa ambayo lazima ipewe uzito na uharaka unaostahili na Wizara ya Afya na Hazina.
Hitimisho
Ndugu Rais wa Chama cha Wauguzi;
Ndugu Wauguzi;
Niruhusuni nimalize hotuba yangu kwa kurudia kuwashukuru kwa kunialika na kwa risala yenu nzuri. Nimejifunza mengi na kama nilivyosema, nakwenda kuifanyia kazi risala yenu na yote niliyosikia na kuona yanayohitaji kuchukuliwa hatua. Yale masuala ya kimuundo na mengineyo nitakwenda kuyakwamua huko yalikokwama, ili utekelezaji uanze. Yale yahusuyo posho, kama nilivyoeleza, baadhi yake yatashughulikiwa katika bajeti ijayo na mengine tutaendelea kuyashughulikia kadri uwezo utakavyoruhusu.
Ninachoweza kusema kwa uhakika kabisa ni kuwa tunawapenda, tunatambua umuhimu wenu na tunawathamini sana. Katu hakuna upungufu wa dhamira bali tunakwazwa na uwezo mdogo wa mapato ya Serikali kuweza kutosheleza mahitaji yote ya kuboresha huduma ya afya na maslahi kwa watumishi wa afya nchini. Narudia kusisitiza kuwa kamwe sio kutokana na kukosekana kwa utayari wa kutatua changamoto zinazowakabili wauguzi au watumishi wengine wa umma.
Upo ushahidi wa wazi wa juhudi za Serikali ninayoiongoza ya kufanya mambo mengi makubwa na madogo ya kuboresha mazingira ya kazi kwa kila kada na sekta kadiri uwezo unavyoruhusu. Mtakubaliana nami kuwa hali ya kada ya wauguzi ilivyo leo, si sawa na ilivyokuwa miaka 10 iliyopita. Tumepiga hatua kiasi chake lakini bado tuna safari ndefu na tutaendelea kufanya zaidi. Ni dhahiri kwamba tumesogea kutoka pale tulipokuwa, ingawa hatujafika tunapodhamiria kwenda. Kwa vile msimamo na muelekeo wetu ni sahihi, naamini baada ya muda si mrefu tutafika. Penye nia pana njia. Inawezekana Timiza Wajibu wako.
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
- May 05, 2014
SPEECH BY HIS EXCELLENCY DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE OPENING OF THE INTERNATIONAL ASSOCIATION OF WOMEN J...
Soma zaidiHotuba
Hon. Mohamed Othman Chande, Chief Justice of the United Republic of Tanzania,
Hon. Madame Aloma Mariam Mukhtar, Chief Justice of the Federal Republic of Nigeria,
Hon. Dr. Asha-Rose Migiro, Minister for Constitutional and Legal Affairs;
Hon. Eusebia Munuo, President of the International Association of Women Judges, (IAWJ);
Hon. Engera Kileo, Chairperson of Tanzania Women Judges Association,
Hon. Presidents of various Courts and Tribunals Present
Hon. Judges and Magistrates;
Madame Joan Winship, Executive Director of International Association of Women Judges (IAWJ),
Members of the Diplomatic Corp;
Distinguished Guests,
Ladies and Gentlemen;
I thank your Lordship Mr. Chief Justice Mohamed Chande Othman and Madam Justice Eusebia Munuo for inviting me to join you at this auspicious occasion of gracing the 9th Biannual Conference of International Association of Women Judges. I thank the organisers for affording my dear country, Tanzania the rare opportunity of hosting this all important biennial conference for the first time. On a personal note, I sincerely appreciate the honour and priviledge of being associated with the two conferences.
Allow me at the outset, to welcome to Tanzania, all distinguished delegates who have travelled from afar. I thank you for coming, you have done us proud. As I wish you successful deliberations, I implore you to visit some of the tourist sites near Arusha. As you know this is the hub of Tanzania northern tourist circuit which is home to Mount Kilimanjaro and world renown sanctuaries like the Serengeti National Park and the Ngorongoro Crater which is the cradle of humanity. The spice Islands of Zanzibar, the ultimate paradise on the Indian Ocean is only half an hour away by plane.
I am sure you will enjoy the experience of visiting these leisure places and be enticed to come back for a longer safari and holiday experience.
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen;
This distinguished gathering of women legal luminaries from all over the world presents a perfect occasion to reflect upon important issues relating to administration of justice. I understand that, this gathering of experts from across the globe blends knowledge and experience, which is a perfect recipe for an enriched thinking and discussion. I trust that the coming five days of this Conference will generate useful discussions and ideas for the improvement of our respective legal sectors and systems, as well as the profession at large.
The Conference Topic
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen;
I have been informed that this conference has chosen to deliberate on a theme “Justice for All”. This is laudable, for, a gathering of Women Judges would definitely be concerned with matters relating to human equality in terms of equal access to justice than anybody else. This is for obvious reasons. The current social dispensation cries very loud for enhanced equality in our societies and the dispensation of justice is one such area that calls for that. It is unfortunate that, in this 21st century, we are still grappling with matters that are a hindrance to equality in accessing justice.
I am constrained to note that my country, with more than 50 years of independence is also still grappling with such matters. Let us together reflect on these issues, the efforts we have made in addressing them and the way forward. We shall definitely find that they resemble in most jurisdictions, where the majority of the delegates present here come from.
Distinguished Delegates,
Ladies and Gentlemen;
A discussion of the theme “Equal Access to Justice” will require to address issues like adequacy of laws, rules and regulations that govern administration of justice, sufficiency of manpower, infrastructure and resources to dispense justice as well as ethics and attitude of the legal staff as well as the society towards justice. Unfortunately, most of our societies have found themselves in situations which all the above matters are serious challenges for their resolve to ensure equal access to justice. To cap it all, poverty is the biggest hindrance to any effort to address the shortcomings that come across the efforts to unlock these problems.
Inadequacy of Laws
Ladies and Gentlemen;
When it comes to laws, rules and regulations, except for the developed world and countries which in one way or the other laws are home grown, which are few, the majority of our countries which emerged from colonialism have found ourselves inheriting foreign laws, rules and regulations that had to be administered in dispensing justice. Unfortunately, these laws alien as they are, are incomprehensible to the majority of the people. To make matters worse, the vexing procedural aspect born out of them has resulted in making the process of dispensing justice inordinately very slow, hence not effective to the desired standards. This has made most of our legal regimes to be seen as methods of coercing our respective societies rather than a desired tool of regulating our good lives.
To the poor, these laws are perceived as expensive tools best used by the affluent in society to oppress them, and to expropriate their properties, freedom and dignity. Unfortunately, even our customary laws which are homegrown came to be interpreted in the same way. Concerted efforts are, therefore, required to ensure that our legal system is reformed enough in order to guarantee equal access to justice.
Insufficiency Infrastructure, Manpower and Resources
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen;
To add to the inadequacy of laws, rules and regulations, there is an inherent problem of insufficiency of infrastructure, manpower and resources. Most jurisdictions emerged from colonialism with a despicable state of poverty. Hence in scaling up priorities, economic development was ruled rather higher than anything else. Second to it ranked the provision of social amenities particularly health and education. Administration of justice trailed far behind.
For quite a while the legal sector was not accorded the requisite investment. The transition from colonialism was very slow in this regard. It is not gainsaying therefore that, our respective legal machineries are characteristic of shortage in infrastructure in terms of buildings equipment, manpower and resources. Thanks to the awakening realization which came to catch up a few decades later that, economic development has a lot to do with justice in our societies. Two good examples can be made out. First, societal stability has a close relationship with the capacity to punish criminals, as this creates a stable society for a vibrant economic growth. Second, the realization that capacity to enforce contracts is necessary in order to provide a regulated and orderly interpersonal economic relationship and trust, which provide a solid basis for economic growth.
Adequate infrastructure alone without competent manpower may not bring about the desired results. Investment in manpower of all cadres in the administration of justice is critical for ensuring quality justice. I am told, the quality of justice is reflected first in professionalism in terms of excellent knowledge of the law by all players; Judges, Magistrates and other Judicial Staff on the one hand and a vibrant bar; Attorneys, Prosecutors and Advocates. Second is discipline and a sense of responsibility. Without these attributes the very root of professionalism will be defeated.
Efforts to Unlock the Shortfalls
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen;
The realization of the need to unlock bottlenecks that has befallen the legal sector, made my country, and many of our jurisdictions embark on Legal Reform Programmes aimed at ensuring efficiency in dispensation of justice taking into account the ability to access justice by the majority of the citizens from all walks in life. Through a number of programmes, country’s have embarked on reforms of the legal sector for the purpose of making our justice system accessible by the majority of the people. In my country for example, thanks to the formidable work by our old Jurist Judge Bomani and his team who between 1993 and 1996 produced the legal sector report, which formed the basis for the more ambitious legal reform strategy, that addresses among other things, challenges relating to access to justice.
Through the Law Reform Commission and BEST Project among others, a number of our legislation have been reviewed with a view to putting in place a speedy and effective civil justice system. The Commercial Court which specializes in resolution of commercial disputes has been established and has shown good progress in resolution of commercial disputes. The Labour Court has also been reformed in line with a revamped Labour Legislation. We now have a more effective labour disputes resolution system, compared to the hitherto semi executive system which was ineffective. The Land Courts and tribunals which have been established across the country from the village level to the High Court provide better access to litigants than was the case before they were established.
The criminal justice system has gone through an evolution of reform in line with the enhancement of Human Rights. I must admit though, that a lot more remains to be done in order to ensure effective penal, corrective and rehabilitative services are rendered to the society. It is my wish that forum like this one tackles difficult issues of this nature and provides practical solutions.
Institutional Rehabilitation
Ladies and Gentlemen;
Access to justice requires institutional rehabilitation of our justice system in order to instill efficiency. Our resolve to bring justice close to our people entails assurance that justice services are made available as close to the people as possible. We have resolved to build High Court Centres in every region, establish Courts of Resident Magistrates in every district and we have embarked on a momentous resolve to assign graduate lawyers at Primary Courts level. So far we have employed 300 graduate lawyers to serve in Primary Courts. The end result of this will be to ensure that eventually quality justice is accessed right from the Primary Court level to the highest level. One endeavour we have set to accomplish while in office is the building of High Court buildings in every region. We have managed to built High Court buildings in 17 regions, this year we have committed funds to build four High Courts and the remaining four will be built in the next financial year.
The institutional rehabilitation of our justice system includes reshaping of our administrative structures of the judiciary by adding up expertise in the management of the judiciary. In so doing, a legal as well as administrative framework of deploying a court administrator in the judiciary has been completed. This has added a lot of improvement, by unlocking the judicial staff and making them available for Judicial work, while Court administrators have been left to deal with administrative matters.
To ensure budgetary independence of the judiciary, the establishment of the Judiciary Fund has proved extremely useful. Now the judiciary has been more independent in the management of their finances.
Judiciary Manpower
Distinguished Participants;
Whatever investment in the justice system will only yield the desired success with deployment of adequate competent manpower. We have increased the establishment of Judges in the High Court and Court of Appeal. When we came into office in 2005 there were 45 Judges, out of whom, women were 10. Currently we have 78 Judges and 30 of them are women. I am one of those leaders who have a strong conviction in gender balance if not equality. Hence during our tenure in office we have been able to appoint the highest number of the Women Judges both of the Court of Appeal and the High Court. We have also directed those who employ judicial staff in the Lower Courts to do the same. I believe, with a good number of women judges in our high judicial offices our justice system is in good hands. Fortunately, they have not let me down. I am aware that a good number of our Regional and Zonal Registries which are manned by women judges are exemplary demonstration of dedication, hard work and output. I commend them all for the work very well done.
Legal Representation
Distinguished Delegates,
Ladies and Gentlemen;
Effective access to justice has a lot to do with legal representation. In our case, until very recently the number of advocates never exceeded a thousand. Thanks to the efforts and initiatives of the present leadership in the Judiciary, which has taken advantage of the expanded training of the legal professionals to increase enrollment of new advocates from 1,060 Advocates in 2006 to 4,184 advocates in 2013, an increase of 3,124. Still even with this number, the ratio of an advocate to the population remains to be very low. The demands for legal services in our society is very high. Many people are denied of their rights simply because of lack of legal representation, which invariably is perceived as an expensive luxury for the affluent in the society. Pro-bono schemes which are meant to assist the disadvantaged groups in society are mostly confined in urban areas leaving the majority in the rural areas unable to access such services. Unfortunately, the most vulnerable are the silent majority in the rural areas.
I am told even the legal practice in the urban areas require to be further defined in terms of specialization and organization. Until such time when retraining and organization in terms of specialization will be achieved, access to specialized justice system will remain an expensive affair for the few. Unless efforts are made to ensure that provision of legal services pro-bono to the disadvantaged majority, access to justice by all may not be achieved.
We in government have realized that these are challenges. The decision to staff courts of all ladders with graduate magistrates is meant to ensure that legal representation becomes possible in all Courts. We want to overcome the present situation which do not allow legal representation in primary courts because they are manned by non graduate judicial staff, yet they attend to the majority of our citizenry in a manner that does not accord effective access to justice.
Multisectoral Approval to Justice Dispensation
Distinguished Delegates;
Ladies and Gentlemen;
The reforms of our Justice System will not bear the desired results without involving the whole legal sector. The Criminal Justice System for example, requires that the whole system to be made effective to address not only new challenges and emerging crimes but also is compliant to human rights standards. The hounds of justice, prosecutors and prisons must be brought to the chain in order to make the system effective and accountable. This way deterrence to crime will be achieved. We are doing everything within our disposal to achieve that. There are conspicuous achievements on this score.
The modernization of Civil Justice System entails review of a number of legislation in order to weed out archaic rules and procedures that impede access to justice. The unwanted laws which are discriminatory to women and children have to be corrected and work for the accomplishment of this task is underway. It is our desire to see that our legal system is an effective and perfect tool for making all our citizen access justice notwithstanding their differences on their status in life.
Conclusion
Distinguished Participants;
Accessing justice by every person is a precious right that has to be embodied in every sphere of life. This endeavor has to progress in tandem with growth in the economic as well as social spheres. We do no longer wish to see our countries ranked down in parameters like cost of doing business indices, simply because our justice systems are dysfunctional that they cannot enforce Contracts. We do not wish to see our societies are so segmented that the rich can buy their way and the poor are driven for a ride. We need to see that every person who happen to be in this universe has guaranteed rights without regard to the status in life he or she may happen to live. We want to see that our women are respected and are held to the highest esteem they deserve. We need to groom our children to become justice minded in a society that respects justice.
Ladies and Gentlemen;
This conference is best placed to address all the overarching issues in respect of inclusion of all persons in society in addressing challenges on equal access to justice. I wish you all the best in the days you will stay here and that you spend your good time to participate in the Conference. You will, as I said earlier, find that Arusha is a very pleasant place where you can do both work and relaxation. Make use of this unique opportunity. I know you need it.
Madam President,
Distinguished Delegates,
Ladies and Gentlemen;
It is now my singular honour and pleasure to declare that this 9th Biennial of Conference International Association of Women Judges is officially opened. I wish you fruitful deliberations.
I thank you for your kind attention!
Asanteni sana.
honourable duty of our Women Judges in their efforts to reconstruct our society into an equitable one, the efforts which accord women their deserving equitable position in the society. I would be the very last person not to join my hands in adding my contribution to their efforts.
- May 02, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWENYE KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI, MEI MOSI 2014, DAR ES...
Soma zaidiHotuba
Kaimu Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania;
Bibi Northburga Maskini;
Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Gaudensia Mugosi Kabaka(MB);
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi,
Mh. Regina Rweyemamu;
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Sadiki
Meck Sadiki;
Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge;
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Dunia (ILO), Kanda ya
Afrika Mashariki, Ndugu Alexio Msindo;
Viongozi mbalimbali wa Serikali mliopo hapa;
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi,
Ndugu Nicholaus Mgaya;
Ndugu Almas Maige, Mwenyekiti wa ATE;
Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),
Dr. Aggrey Mlimuka;
Mheshimiwa Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mliopo;
Waheshimiwa Mabalozi;
Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri, Ndugu Doroth Uiso;
Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Wafanyakazi;
Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Ndugu Wafanyakazi wenzangu;
Mabibi na Mabwana;
Shukrani
Awali ya yote naomba tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uhai na kutuwezesha kukutana leo katika sherehe za mwaka huu za kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani. Aidha, natoa shukrani nyingi kwa Kaimu Rais wa TUCTA Mama Northburga Maskini na viongozi wenzako kwa heshima kubwa mliyonipa ya kuja kuungana na wafanyakazi wa Tanzania katika kuadhimisha siku hii adhimu.
Napenda kutumia fursa hii kupitia kwako Kaimu Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania, kutoa salamu nyingi za pongezi na mkono wa heri kwa wanachama na Viongozi wa Vyama Vyote vya Wafanyakazi katika kuadhimisha siku hii kubwa na adhimu. Nawapongeza sana Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti (RAAWU) kwa kuratibu vizuri maadhimisho ya mwaka huu. Nimefurahi kusikia kuwa maadhimisho ya mwaka huu yamehusisha wiki ya wafanyakazi ambako kumekuwa na maonyesho ya waajiri na wafanyakazi. Huu ni utaratibu mzuri ambao licha ya kuongeza hamasa kwa maadhimisho haya lakini pia umetoa fursa kwa wananchi wengi kujionea wenyewe mambo muhimu mnayoyafanya wafanyakazi.
Nitakuwa mwizi wa fadhila nisipowapongeza na kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Saidi Meck Sadiki kwa kukubali kuwa wenyeji wa sherehe hii. Si kazi rahisi hata kidogo, hivyo wanastahili pongezi zetu kwa kufanikisha vyema shughuli hii. Tumeona jinsi uwanja ulivyofurika na maandamano yalivyofana. Usione vinaelea vimeundwa. Tafadhali pokeeni pongezi zetu sote.
Pongezi kwa Wafanyakazi Bora
Wafanyakazi Wenzangu,
Kwa mara nyingine tena katika sherehe hizi wafanyakazi bora wametambuliwa na kupewa tuzo. Mnastahili pongezi zetu sote kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na nidhamu na kutambuliwa. Wahenga walisema, ”Chanda chema huvishwa pete”. Nawapongeza TUCTA na waajiri kwa kutambua umuhimu wa kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora. Inaongeza ari ya kufanya kazi na tija kazini. Tafadhali udumisheni utaratibu huu. Kwa wale ambao hawakupata safari hii wasikate tamaa na wao siku yao yaja waongeze bidii, maarifa na nidhamu kazini ili mwakani, siku kama ya leo iwe zamu yao kupongezwa.
Risala ya Wafanyakazi
Ndugu Kaimu Rais wa TUCTA,
Wafanyakazi Wenzangu,
Nimeisikiliza kwa makini sana risala yenu iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa TUCTA Ndugu Nicholas Mgaya ambaye anastahili pongezi kwa kuwasilisha vizuri na kueleweka. Ni risala nzuri iliyosheheni mawazo mazuri ya kujenga. Ndani yake inayo maombi, lakini pia mapendekezo. Napenda kuwahakikishia kuwa mapendekezo yote nimeyachukua na tutakwenda kuyafanyia kazi. Baadhi ya maombi si mapya, yamerudiwa ili kuweka msisitizo. Mengine majawabu yake tunayo, nitayatolea maelezo katika hotuba yangu.
Kauli Mbiu
Wafanyakazi Wenzangu,
Nawapongeza kwa Kauli mbiu yenu isemayo, ”Utawala Bora Utumike Kuondoa Kero za Wafanyakazi”. Kauli mbiu hii ni muafaka na maridhawa kabisa. Ni ukweli usiopingika kuwa utawala bora ni jambo muhimu sana na pale ambapo upo si tu kwamba husaidia kutatua kero za wafanyakazi, bali pia huepusha mikwaruzano na migogoro kati ya wafanyakazi na waajiri.
Wafanyakazi Wenzangu,
Uzoefu unaonyesha kuwa migogoro ya wafanyakazi na waajiri hujitokeza zaidi pale ambapo kanuni za utawala bora za ushirikishwaji, uwajibikaji na uwazi hazifuatwi. Usiri usiyo wa lazima katika uamuzi, hufanya hata uamuzi mzuri kutiliwa shaka na kujenga hofu isiyostahili kuwepo. Wakati mwingine inaweza kusababisha hata uamuzi mzuri kukataliwa. Pia, ukosefu wa taarifa sahihi unaweza kusababisha wafanyakazi kutoa madai yasiyotekelezeka kwa sababu ya kuwa na matarajio makubwa mno kuliko uwezo wa mwajiri kumudu.
Tumejifunza, vilevile, kuwa utawala bora hauishii kwenye kutunga sheria na kuunda taasisi na vyombo vya usimamiaji na utekelezaji wa Sheria. Utawala bora hauna budi kuwa sehemu kamili ya utamaduni wa kazi na uhusiano ambao unapaswa kuzingatiwa na waajiri na waajiriwa. Wakati mwajiri anawajibika kuwa muwazi kwa wafanyakazi wake na kuwatimizia stahili zao kama inavyopasika, waajiriwa nao wanawajibika kumtendea haki mwajiri kwa kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu taratibu za kazi ikiwa ni pamoja na zile zihusuzo namna ya kuwasilisha madai yao.
Waajiri na waajiriwa kudai haki zao hakuwaondolei wajibu wao kwa kila mmoja wao. Hivyo basi, kudumisha utawala bora kunawataka waajiri na wafanyakazi kuheshimu Sheria za nchi zikiwemo zile zinazotawala uhusiano na ajira sehemu za kazi. Hapa nazungumzia, Sheria ya Majadiliano katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2003 na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004.
Ndugu Zangu;
Lazima tutambue na kukubali kuwa ufanisi sehemu za kazi hutegemea uhusiano uliopo baina ya wafanyakazi na waajiri. Kama umejengwa juu ya misingi ya kuheshimu sheria na majadiliano, mambo huwa mazuri. Vitisho vya mwajiri na migomo ya wafanyakazi si suluhisho la kuondoa kero za wafanyakazi. Kwa jumla hupunguza ufanisi. Hivyo basi, lazima tufanye kila tuwezalo kujenga uhusiano mwema kati ya waajiri na waajiriwa. Ni kichocheo kikubwa cha watu kufanya kazi kwa bidii, kuongeza tija na uzalishaji sehemu za kazi hivyo kumwongezea mwajiri kipato na uwezo wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
Hali ya Uchumi
Ndugu Viongozi na Ndugu Wafanyakazi;
Mwenendo wa uchumi wetu katika mwaka 2013/2014 ni mzuri. Uchumi umeendelea kuimarika ikilinganishwa na mwaka uliopita. Ukuaji wa uchumi unategemewa kuongezeka kutoka asilimia 7.0 ya mwaka 2013 hadi asilimia 7.2 mwaka huu. Haya ni matunda ya kazi nzuri ya wafanyakazi, wakulima na wadau wengine nchini. Tunayo kila sababu ya kujipongeza kwa mafanikio haya.
Habari nyingine njema kwa wafanyakazi ni kwamba mfumuko wa bei umeteremka kutoka asilimia 9 tulipokutana mwaka jana hadi asilimia 6.3 tunapokutana leo. Azma yetu ni kutaka ubaki chini ya asilimia 10 na hasa uwe asilimia 5 au chini ya hapo ifikapo Juni, 2015. Tunahangaikia sana kushuka kwa mfumuko wa bei kwa vile unapokua juu, unasababisha hali ngumu ya maisha kwa wafanyakazi. Tukidhibiti mfumuko wa bei uongezaji wa viwango vya mishahara utakuwa na tija. Aidha, inamuwezesha hata yule mwenye mshahara mdogo kuweza kukidhi baadhi ya mahitaji yake muhimu, hivyo kumpunguzia ukali wa maisha. Kwa sababu hiyo, hatuna budi kuongeza bidii katika kukuza uchumi na kushusha mfumuko wa bei. Kwa vile hapa tulipofika sio ukomo wa uwezo wetu, naamini tunaweza kupata mafanikio makubwa zaidi tukiongeza utawala bora mahala pa kazi. Kiwango cha ukuaji wa uchumi kinaweza kuwa kikubwa zaidi na kutunufaisha sote.
Mabaraza ya Wafanyakazi
Ndugu Wafanyakazi;
Hatuwezi kuzungumzia utawala bora mahala pa kazi bila ya kuwa na ushirikishwaji wa wafanyakazi. Ushirikishwaji wa wafanyakazi, unawezekana tu pale ambapo yapo mabaraza ya kazi na yanafanya kazi. Mabaraza ya kazi ni fursa kwa wafanyakazi kuwakilisha na kujenga madaraja kati ya menejimenti na wafanyakazi. Madaraja haya hujenga mazingira ya kuwezesha madai ya wafanyakazi kufika katika menejimenti, na uamuzi kufanywa na mrejesho wa menejimenti kuwafikia wafanyakazi.
Nimepata taarifa isiyofurahisha kuwa bado zipo taasisi chache za Serikali ambazo hazijaunda mabaraza hayo. Nimeambiwa pia kwamba baadhi ya yale mabaraza yaliyoundwa hayakutani kama inavyopasa. Hata hawakutani kujadili bajeti za taasisi zao, jambo ambalo ni sharti la msingi kutekelezwa kwa kisingizio cha kukosa fedha. Madai haya hayaingii akilini hata kidogo. Mbona semina na vikao vya menejimenti vyenye posho nono hatuoni vikiachwa kufanyika?.
Napenda kuwakumbusha wakuu wa taasisi zote za umma kuwa uundwaji mabaraza ya wafanyakazi na ushirikishwaji wa mabaraza hayo katika mchakato wa Bajeti sio jambo la hiari bali ni matakwa ya kisheria. Wasiounda mabaraza na wale wasioitisha vikao vya mabaraza kujadili bajeti za taasisi zao wanavunja sheria. Hili ni jambo lisilovumilika. Nimewaagiza Waziri wa Kazi na Ajira na Katibu Mkuu Kiongozi wahakikishe kuwa Wizara zote na taasisi zote za umma zinazingatia Agizo la Rais Na. 1 la Mwaka 1970 pamoja na matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6 ya Mwaka 2004. Lazima wahakikishe kuwa mabaraza yanaundwa mapema iwezekanavyo, na zile Wizara, Idara na Taasisi zisizoitisha mabaraza yao zibanwe kufanya hivyo bila ajizi.
Umuhimu wa Vyama vya Wafanyakazi Mahali pa Kazi
Ndugu Wafanyakazi;
Jambo lingine ambalo limenisikitisha sana ni taarifa kuwa bado wapo waajiri hasa katika sekta binafsi ambao wanakaidi matakwa ya kisheria ya kuwepo kwa matawi ya vyama vya wafanyakazi mahala pa kazi. Naambiwa hata pale wafanyakazi wanapoanzisha mabaraza hayo, wale wafanyakazi wanaokuwa mstari wa mbele kudai kuwepo matawi hayo au kutetea haki za wafanyakazi wamekuwa wanapata wakati mgumu. Huishia kuhamishwa au hata kufukuzwa kazi. Aidha, wapo baadhi ya waajiri ambao wameanzisha mifumo mbadala ambayo haiko kisheria katika kukwepa kushughulikia maslahi ya wafanyakazi.
Napenda kurudia na kusisitiza kuwa kuwepo kwa matawi ya vyama vya wafanyakazi mahala pa kazi si suala la hiyari bali ni matakwa ya kisheria. Hivyo, hakuna sekta, kampuni wala mwekezaji ambaye yuko juu ya sheria hii. Ni vizui ukaeleweka kuwa hii si tu ni sheria ya nchi yetu peke yake, bali ni matokeo ya mikataba ya kimataifa na ni haki ya msingi ya wafanyakazi na utawala bora.
Ndugu Viongozi na Ndugu Wafanyakazi;
Sisi katika Serikali ni mashahidi wa manufaa ya kuwepo kwa matawi ya wafanyakazi mahala pa kazi. Uzoefu wetu umetuthibitishia kuwa pale ambapo kuna matawi ya vyama vya wafanyakazi ambayo yanatimiza majukumu yake vizuri na menejimenti inatimiza wajibu wake ipasavyo uhusiano wa kikazi huwa mzuri. Inasaidia kupunguza migogoro, kuepusha migomo na huongeza tija na ufanisi. Matawi hayo hutoa fursa ya majadiliano na mazungumzo kati ya wafanyakazi na waajiri. Si kweli hata kidogo kuwa, kuwepo kwa matawi haya hukwamisha ufanisi mahala pa kazi.
Nimemwagiza Waziri wa Kazi kuhakikisha kuwa matawi ya vyama vya wafanyakazi yanakuwepo mahala pa kazi. Pia, ahakikishe kuwa wakaguzi wanapita sehemu za kazi na kukagua utekelezaji wa sheria kuhusu kuwepo kwa matawi hayo. Wale waajiri wanaokaidi wachukuliwe hatua za kisheria bila kuoneana muhali. Aidha, nimemtaka asisite kuwachukulia hatua zipasazo za kinidhamu, wakaguzi wanaoshirikiana na waajiri kudhoofisha haki za wafanyakazi. Hawa ni watu walioshindwa kutimiza majukumu yao hivyo wasivumiliwe. Wanaipaka matope Serikali.
Wapo Wakaguzi ambao wanakwazwa na kukaa kituo kimoja kwa muda mrefu, wamezoeleka mno na wamejenga mazoea yasiyofaa kati yao na waajiri na wanashirikiana kuwakandamiza wafanyakazi. Wahamishwe. Wakati huohuo wakumbusheni kuwa kazi yao ni kusimamia sheria, kutetea haki za wafanyakazi na waajiri na kamwe sio kuwa mawakala wa kuwasaidia waajiri kukiuka sheria.
Hatua za Serikali dhidi ya Uwakala wa Ajira
Ndugu Wafanyakazi;
Nimefurahishwa sana na uamuzi wa Mheshimiwa Gaudensia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira na viongozi wenzake Wizarani wa kufuta mfumo mpya ulioanzishwa wa makampuni kuajiri kupitia uwakala wa ajira. Naunga mkono uamuzi wenu wa kupiga marufuku utaratibu unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini wa kukodisha wafanyakazi katika Makampuni. Utaratibu huu ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya 1999. Sheria ya Huduma ya Ajira inaelezea majukumu ya msingi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira kuwa ni kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri na siyo wao kuwa waajiri na kukodisha wafanyakazi kwa makampuni.
Wakala wa Ajira kufanya mambo kinyume na matakwa ya sheria haikubaliki. Anawakosesha wafanyakazi haki zao za msingi kama vile mishahara, huduma za hifadhi ya jamii, likizo ya uzazi, matibabu, mafunzo na mengineyo. Inaondoa uwajibikaji wa moja kwa moja wa waajiri kwa wafanyakazi wao. Hili ni jambo ambalo hatuwezi kuliacha liendelee. Nimempa Waziri wa Kazi na Ajira baraka zangu zote kulishughulikia kwa nguvu zake zote na kwa umakini na ufanisi mkubwa ili tuweze kukomesha kabisa dhulma hii.
Uimarishaji wa Vyombo vya Mashauriano
Wafanyakazi wenzangu;
Jambo lingine ambalo linahitaji kupatiwa ufumbuzi katika kuimarisha uhusiano kati ya wafanyakazi na waajiri ni ufanisi wa vyombo vya mashauriano. Serikali imefanya kazi nzuri ya kuunda vyombo hivi ikiwemo Baraza la Mashauriano (LESCO). Lengo la kuunda mabaraza hayo ni kutoa fursa ya usuluhishi wa migogoro ya kikazi na maslahi ya wafanyakazi kabla ya kuiwasilisha katika mifumo ya kimahakama.
Pamoja na nia njema ya Serikali, chombo hiki kimeendelea kulalamikiwa kwamba hakitekelezi wajibu wake kwa ukamilifu. Mashauri yanayowasilishwa hayatatuliwi kwa wakati kutokana na Baraza hili kutoitisha vikao, kwa madai ya ufinyu wa bajeti. Matokeo yake, wafanyakazi aidha wanaamua kufikisha migogoro yao kwa Waziri wa Kazi, au kwenda mahakamani au kuchukua sheria mkononi. Hatua zote hizi nje ya matumizi ya Baraza la LESCO, si endelevu na hazijengi mazingira ya maridhiano kati ya waajiri na wafanyakazi. Kwa jumla zinadhoofisha utawala bora.
Nimeelekeza, kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015, Wizara ihakikishe inatenga fedha za kutosha za kuwezesha Baraza la LESCO kufanya vikao vyake. Aidha, bajeti hiyo ilindwe ili kuhakikisha kuwa pesa hizo zinatumika kwa ajili ya kazi za Baraza la Mashauriano. Ni jambo linalowezekana. Nataka tuone kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha Baraza hili linafanya kazi yake ipasavyo. Sote tunakubaliana kuhusu umuhimu wake kuwa ni mkubwa na ipo mifano ya nchi nyingine ambazo Baraza hili hufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Naamini kwamba, kwa kuwa changamoto yetu si udhaifu wa Sheria yenyewe iliyounda LESCO bali ufanisi katika utendaji tu, upatikanaji wa fedha za kutosha utawezesha Baraza hili kufanya kazi kwa ufanisi. Mwisho wa yote tutaepusha migogoro isiyo ya lazima, lakini pia tutaimarisha utawala bora kwa kujenga madaraja kati ya watumishi na waajiri pale panapojitokeza mikwaruzano.
Ushiriki wa Wafanyakazi kwenye Bodi za Mashirika
Wafanyakazi Wenzangu,
Sambamba na kulihuisha Baraza la LESCO, Serikali inalifanyia kazi suala la kushirikisha wafanyakazi katika Bodi za Mashirika ya Umma. Tunafanya hivyo kwa kutambua kuwa, Bodi za Mashirika ni vyombo muhimu vinavyofanya uamuzi wa kisera na kiuendeshaji wa mashirika. Uamuzi wake hugusa moja kwa moja maslahi ya wafanyakazi hivyo uwakilishi wao ni muhimu.
Natambua kuwa tayari yapo mashirika ambayo kwa mujibu wa Sheria ya kuanzishwa kwake, yametambua uwakilishi wa wafanyakazi katika Bodi zake. Lakini yapo mashirika mengine hayana sharti hilo katika Sheria zilizounda mashirika hayo. Manufaa na umuhimu wa kuwashirikisha wafanyakazi si mambo yanahotaji mjadala. Yapo wazi. Katika yale mashirika ambayo Bodi zake zina wajumbe kutoka vyama vya wafanyakazi, tumeona namna ambavyo mchango wa wafanyakazi umekuwa wa msaada mkubwa.
Nimeelekeza Wizara husika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuchukua hatua za haraka kuandaa na kuwasilisha muswada wa Sheria Bungeni wa kulirasimisha jambo hili kwa mashirika yote ya umma. Lengo letu ni kutaka kuhakikisha kuwa, jambo hili muhimu haliwi suala la utashi tu wa Shirika husika, bali ni utaratibu rasmi wa kisheria. Naamini ushiriki wa wafanyakazi katika Bodi za Mashirika utaimarisha utawala bora na kupunguza kero za wafanyakazi mahala pa kazi.
Maslahi ya Wafanyakazi
Ndugu Kaimu Rais, Ndugu Viongozi na Ndugu Wafanyakazi;
Nafahamu kuwa hotuba yangu haitakuwa imekamilika bila kuzungumzia maslahi ya wafanyakazi. Na, wengi hasa wanasubiri kusikia nasema nini kuhusu nyongeza ya kima cha chini cha mshahara na kupungua kwa kodi ya mapato, yaani Paye As You Earn (P.A.Y.E).
Napenda kurudia kuwahakikishia kuwa mimi na wenzangu Serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo. Tumethibitisha hivyo miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo. Leo nitapenda kuzungumzia mambo matatu: La kwanza ni kuhusu Kima cha Chini cha Mshahara. Kama tulivyoahidi mwaka jana, Serikali ilipandisha kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa Umma kwa asilimia 41. Kwa ongezeko hilo, kima cha chini cha watumishi wa umma kiliongezeka kutoka shilingi 170,000 hadi shilingi 240,000. Na mwaka huu nawaahidi tena kuwa tutaongeza. Najua kwamba nyongeza hii si kubwa kuliko vile ambavyo wafanyakazi na hata mimi ningependelea iwe. Kwa kweli kinachotukwaza ni mapato ya Serikali kutokuwa makubwa kumudu nyongeza kubwa ya mshahara kwa wakati. Nyongeza hii peke yake inaifanya Serikali kutumia asilimia 44.9 ya bajeti ya Serikali kulipa mishahara na asilimia 10 ya pato la taifa (GDP). Kwa vigezo vyo vyote vile kiwango hiki ni kikubwa mno hivyo ni kielelezo thabiti cha dhamira yetu njema na kujali.
Isitoshe naomba mkumbuke kuwa mwaka 2005 kima cha chini cha mshahara kilikuwa shilingi 65,000.00. Hivyo ndani ya miaka saba tumeongeza kima cha chini karibu mara nne ya ilivyokuwa na kufikia kima cha chini cha sasa. Nawaahidi mwaka huu tutaongeza tena. Kama nilivyogusia, hatuwezi kutoa nyongeza kubwa mara moja lakini, kidogo kidogo tunaweza. Na tumeweza. Naamini, miaka mitano ijayo mambo yatakuwa mazuri zaidi wakati mapato ya Serikali yatakapoongezeka sana mauzo ya gesi asilia yatakapoanza.
La pili ni Kima cha Mishahara Katika Sekta Binafsi: Kima cha chini cha mishahara katika sekta binafsi bado hakinifurahishi. Kwa upande wa sekta binafsi, mfumo wa upangaji wa kima cha chini cha mshahara unatawaliwa na Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya Mwaka 2004. Sheria hii inaanzisha Bodi za Mishahara za kisekta ambazo zina wajibu wa kutoa mapendekezo kwa Waziri wa Kazi na Ajira kuhusu kima cha chini cha mshahara katika sekta husika. Naambiwa kuwa Bodi hizi zinapata changamoto katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kuwa waajiri hawatoi ushirikiano wa kutosha.
Mnamo mwezi Juni, 2013, Mhe. Waziri wa Kazi na Ajira alitangaza mishahara ya kima cha chini kisekta kupitia Gazeti la Serikali Na. 196/2013 kwa sekta 12 za Madini, Afya, Kilimo, Nishati, Usafirishaji, Viwanda, Ujenzi, Ulinzi binafsi, Shule binafsi, Hoteli, Huduma za Majumbani na Mawasiliano. Taarifa ninayopata ni kuwa, sehemu kubwa ya waajiri wa sekta binafsi hawazingatii viwango hivyo. Nimemuelekeza Waziri wa Kazi awabane wsiotekeleza watekeleze Tuzo alizotoa.
Naguswa sana na kilio cha wafanyakazi katika sekta binafsi. Sisi kama Serikali hatuwezi kukwepa wajibu wa kuwasaidia. Nimeelekeza kuwepo na mkakati maalum kushughulikia jambo hili. Katika mkakati huo, nashauri utaratibu wa Utatu yaani Wafanyakazi, Waajiri na Serikali utumike kufanya tathmini na kubaini matatizo yaliyopo na kupendekeza namna bora ya kuhakikisha wafanyakazi wa sekta binafsi wanapata mishahara wanayostahili. Katika mkakati wa muda mrefu, tumekubaliana na viongozi wenu kuimarisha vyombo vya mashauriano, usimamizi na bodi za kisekta ili huko mbele ya safari visimamie kwa ukamilifu jambo hili.
Jambo la tatu ni Kodi ya Mapato kwa wafanyakazi yaani PAYE: Kumekuwepo pia na ombi la muda mrefu la kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara ya wafanyakazi kuwa chini ya asilimia 10. Kama nilivyoahidi mwaka jana, hili tutaendelea kulishughulikia kadri uwezo wa Serikali utakaporuhusu. Tumeshafanya hivyo kabla, na hatuna sababu ya kutofanya hivyo huko tuendako. Tayari tumepunguza kutoka asilimia 18.5 mwaka 2007 hadi asilimia 13 hivi sasa. Maombi yenu tumeyapokea, tuachieni, tuangalie nini tunachoweza kufanya kama miaka iliyopita. Kwa jumla ni nia yetu kuendelea kufanya hivyo mwaka hadi mwaka, tunakwazwa na uwezo mdogo wa mapato ya Serikali.
Mageuzi katika Mifuko ya Kijamii
Wafanyakazi wenzangu;
Kama nilivyosema wakati wa sherehe za Mei Mosi zilizofanyika mkoani Mbeya mwaka jana, Serikali ina dhamira ya dhati ya kupanua wigo wa hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi na kwa wananchi wote kwa ujumla. Hatua kwa hatua tutaendelea kufanya marekebisho katika Hifadhi ya Jamii nchini ili iweze kukidhi haja hiyo.
Eneo moja ambalo tumejiandaa kulitekeleza kuanzia Julai, 2014 ni kuhusu fidia kwa wafanyakazi wanaoumia au kuathirika wakiwa kazini. Wote tunafahamu kwamba tangu mwaka 2008 Serikali ilipitisha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ambayo inaunda Mfuko wa Fidia utakaoshughulikia malipo yaliyo bora zaidi ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia au kufariki au kupata maradhi yatokanayo na kazi kuliko ilivyo sasa. Mfuko huu utahudumia wafanyakazi wa sekta zote yaani sekta binafsi na ya umma na utatoa mafao bora zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
Tunafanya hivyo kutokana na uzoefu tulioupata wa wafanyakazi wengi hasa katika sekta binafsi kushindwa kupata fidia stahili, wakati mwingine kutokana na uchanga wa waajiri wao. Kwa kuwa na mfuko huu kutawapunguzia waajiri mzigo wa kuwalipa fidia wafanyakazi wao hasa wakati ambao hawana uwezo wa kufanya hivyo. Mfuko utawapa wafanyakazi uhakika wa kulipwa fidia yao pale watakapopata madhara mahala pa kazi. Serikali itachangia asilimia moja ya jumla ya mishahara ya wafanyakazi kila mwezi kuanzia mwezi Julai, 2014. Waajiri binafsi nao watachangia asilimia 0.5 ya jumla ya mishahara ya wafanyakazi wao.
Wafanyakazi Wenzangu;
Eneo jingine ambalo tuliahidi kulifanyia kazi ni kuhusu kuainisha mafao ya pensheni. Mchakato huu unaendelea vizuri na nafahamu kuwa Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Wadau yaani Vyama vya Wafanyakazi wanatarajiwa kukutana tarehe 5 Mei, 2014 kwa majadiliano zaidi. Kikao hicho kitajadili ulingano wa mafao yanayotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kuweka vikokotoo bora vya Mafao ya Pensheni.
Ni vizuri kukumbushana kwamba, kuwa na vikokotoo vizuri ni jambo moja, na kuhakikisha uendelevu wa mifuko ya hifadhi ya jamii ni suala lingine. Hivyo, wakati tunaendelea na majadiliano hayo, hatuna budi pia kutoa umuhimu katika kuelimishana juu ya umuhimu na wajibu wa waajiri kuwasilisha michango ya wanachama. Mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa inakusanya michango ya wanachama wake na kuwekeza kwa umakini mkubwa. Wanachama wao wanatakiwa kuhakikisha kuwa michango yao inabaki katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili ije kuwafaa wakati wa shida na maisha ya uzeeni, badala ya tabia ya sasa ya watumishi kuamua kushirikiana na waajiri kutokatwa michango hiyo, au kujitoa katika mifuko hiyo kila wanapobadilisha ajira kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwajiri mwingine.
Madai ya Waalimu
Wafanyakazi Wenzangu,
Serikali pia imeendelea kushughulikia madai mbalimbali ya watumishi wa umma hususan madeni ya mishahara na yasiyokuwa ya mishahara. Tumekamilisha uhakiki wa madeni kwa wafanyakazi wasiokuwa walimu. Hazina wameniarifu kuwa yatalipwa kabla ya mwaka ujao wa fedha. Kwa upande wa walimu, Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Walimu (CWT) tumekuwa tunafanya uhakiki wa madeni ya walimu katika Halmashauri zote 147 za Tanzania Bara. Kazi imekamilika kwa Halmashauri 96 na inaendelea kwa Halmashauri 51 zilizosalia. Nimeambiwa kuwa madeni yaliyohakikiwa yameanza kulipwa. Na, kama nilivyosema kwa wafanyakazi wasiokuwa walimu ni makusudio ya Hazina kuwa madeni hayo yalipwe katika mwaka huu wa fedha.
Ni jambo la kutia faraja kwamba, katika kufanya kazi ya uhakiki wa madeni ya walimu. Serikali na Chama cha Walimu tumeweza kubaini mzizi wa fitina. Tumekubaliana kuutafutia dawa ya kuung’oa ili tatizo hili lisijirudie.
Kwa ajili hiyo, nimeelekeza Wizara na Taasisi zinazohusika hasa Wizara ya Fedha, Wizara ya Elimu na Mafunzo na Ufundi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu maofisa wa Serikali, wanaohusika na udanganyifu huu. Halikadhaika, wafanyakazi walioghushi stakabadhi nao wachukuliwe hatua za kisheria. Kwa muda mrefu, udanganyifu na hila za watumishi hawa zimechochea kutokuelewana na kutokuaminiana kati ya walimu na Serikali.
Ifike mahala sasa, walimu na Serikali tupate suluhu ya kudumu baada ya kumpata mchawi wetu. Tumekubaliana kuendelea na mfumo huu wa uhakiki wa pamoja kama msingi wa kutatua tatizo hili la muda mrefu. Huu ni mfano mzuri wa namna utawala bora unavyoweza kutatua kero za wafanyakazi kupitia ushirikishaji na uwazi.
Kuhusu muundo mpya wa Utumishi wa Walimu, habari njema ni kuwa muundo huo umekwishapitishwa na unatarajiwa kuanza kutumika tarehe 1 Julai, 2014. Suala la upandishaji wa madaraja ya walimu nalo linakwenda vizuri ambapo hadi kufikia Aprili 2014, walimu 30,236 walikuwa wamepandishwa vyeo.
Kuhusu wimbo wenu, Shemeji mshahara mdogo. Nimefuatilia nimebaini ni kweli kumekuwa na ucheleweshaji. Nimefuatilia Benki Kuu wanasema walitoa pesa mapema, lakini kumekuwepo na mkwamo mahali ambapo tutapatafuta.
Utoaji Holela wa Vibali vya Ajira kwa Wageni
Ndugu Kaimu Rais wa TUCTA;
Wafanyakazi wenzangu,
Yamekuwepo malalamiko kuwa kumekuwepo na utoaji holela wa vibali vya kazi kwa wageni kufanya kazi nchini. Naambiwa siku hizi hata zile ajira ambazo Watanzania wana ujuzi nazo hujazwa na wageni. Serikali imeyafanyia kazi malalamiko haya na kugundua kuwa udhaifu upo kwenye kuwepo kwa taasisi zaidi ya moja inayoshughulika na utoaji wa vibali kwa wageni kuishi na kufanya kazi nchini. Hali hii inatoa mwanya kwa watu wasiokuwa waaminifu kutoa vibali kwa watu wasiostahili.
Serikali imeamua kuzifanyia marekebisho sheria husika na iko mbioni kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Vibali vya Ajira. Nimeelekeza kuwa jitihada zifanyike ili Muswada huo uwasilishe kwenye kikao cha Bunge la Oktoba, 2014. Sheria hii sasa italiweka suala la vibali vya kazi kushughuhulikiwa na taasisi moja na hivyo kuweka udhibiti katika utoaji wa vibali hivyo.
Ndugu Wafanyakazi;
Niruhusuni nichukue fursa hii, pia, kukumbusha kuhusu umuhimu wa wafanyakazi kuheshimu na kuthamini kazi. Waswahili wana msemo “Usichezee kazi, chezea mshahara”. Yapo madai yanayojirudia kutoka kwa waajiri kuwa wafanyakazi wa Kitanzania hawathamini na kuheshimu kazi zao. Wanatuhumiwa kwa uvivu, udokozi na nidhamu ndogo. Napata taabu kukubali madai haya kuwa hii ndio sifa ya wafanyakazi wote wa Kitanzania. Leo nimetunuku tuzo kwa wafanyakazi bora na tumekuwa tunafanya hivyo kila mwaka. Kitendo hiki ni ushahidi kuwa wafanyakazi hodari wapo. Hata hivyo, siwezi kusema wavivu, wezi na watovu wa nidhamu hawapo. Lakini, sina uhakika na ukweli wa madai yanayotoa sifa mbaya na kutia doa baya kwa Wafanyakazi wa Kitanzania.
Sifa hizo hasi ndizo zinazowashawishi waajiri na hasa wawekezaji kutafuta wafanyakazi nje. Ninawaomba viongozi na wanachama wa vyama vya wafanyakazi mlitafakari suala hili kwa uzito unaostahili kwani linaelekea kuaminika. Kulikataa tatizo peke yake hakutoshi kwani hakutatui tatizo lililopo, zaidi ya kutupa faraja ya muda tu. Natoa rai kwa vyama vya wafanyakazi na Wizara ya Kazi na Ajira kulifanyia kazi jambo hili haraka.
Mchakato wa Katiba
Wafanyakazi Wenzangu,
Katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika mwaka jana kule Mbeya, mlitoa rai ya wafanyakazi kushirikishwa katika mchakato wa kutunga Katiba Mpya. Niliwaahidi kuwa mtashirikishwa kwa vile wafanyakazi ni sehemu kubwa sana ya jamii yetu na kundi muhimu sana katika taifa. Nimetimiza ahadi yangu wakati wa kuteua Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba. Kuna uwakilishi mkubwa wa wafanyakazi na kumfanya Ndugu Maige, Mwenyekiti wa ATE alalamikie uwakilishi mdogo wa waajiri. Kazi yangu nimemaliza, sasa iko kwa wawakilishi wenu kutumia vizuri fursa waliyopata kupigania haki na maslahi ya wafanyakazi bila ya kusahau maslahi ya Watanzania wengine. Bahati nzuri wajumbe wengi ni wafanyakazi hata kama hawakuingia Bungeni wakiwa moja kwa moja wanawakilisha wafanyakazi. Kwa hiyo ni rahisi kwa masuala ya wafanyakazi kutetewa. Hamna budi kuwasiliana nao.
Jambo muhimu kwenu kufanya ni kujipanga vizuri kwa hoja za kuwapa wawakilishi wenu kuzipigania. Msipofanya hivyo mtakuja kujikuta wawakilishi wenu wakatekwa na makundi yenye agenda na misimamo isiyoendeleza maslahi yenu. Sisemi wasijihusishe na mambo mengine yenye maslahi kwa taifa, la hasha!. Ninachosema wasifanye hayo na kuacha kusemea yenye maslahi ya wafanyakazi. Wanaweza kukosekana watu wa kuyasemea mkajutia fursa hii.
Naungana nanyi kusikitika kutokana na mienendo na kauli zisizoridhisha za baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Naungana nanyi pia kuwasihi watumie lugha ya staha na wazo la kutafuta majawabu kwa njia ya mashauriano itatuwezesha kumaliza tofauti za kambi. Nawasihi waliotoka Bungeni warejee pale Bunge Maalum la Katiba litakapoanza upya baada ya mapumziko ya kupisha Bunge la Jamhuri na Baraza la Wawakilishi kufanya shughuli za lazima hususan bajeti za Serikali zetu mbili.
Hitimisho
Ndugu Kaimu Rais wa TUCTA, Katibu Mkuu na Wafanyakazi Wenzangu;
Naomba nimalize kwa kurudia kuwashukuru tena kwa kunipa nafasi hii adhimu ya kujumuika nanyi tena katika sherehe za mwaka huu. Napenda kuwahakikishia, kwa mara nyingine tena, kwamba dhamira yangu binafsi, na ile ya Serikali ninayoiongoza ya kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi iko palepale. Kilio chenu ni kilio changu. Tumejitahidi katika kipindi hiki kutatua matatizo ya wafanyakazi na mafanikio yake mnayaona. Nina imani kuwa tukishirikiana katika mwaka mmoja uliobakia tutaweza kutatua kero nyingi zaidi.
Mwisho, napenda kuwakumbusha kuwa, maslahi mazuri kwa wafanyakazi yana uhusiano wa moja kwa moja na kuongezeka kwa tija, uzalishaji, na pato la waajiri katika sekta binafsi na sekta za umma. Shime nawasihi muongeze juhudi ili nanyi mnufaike zaidi. Kwa upande wangu naamini kwamba neema haiko mbali sana. Tumefanikiwa kuweka misingi mizuri ya kiuchumi, tumeunda taasisi na kuweka mazingira mazuri ya kisheria na kisera. Bahati nzuri Mwenyezi Mungu ametushushia neema ya rasilimali ikiwemo gesi asilia. Vyote hivi kwa pamoja, vinatupa matumaini kuwa ndoto yetu ya kufikia nchi ya uchumi wa kati mwaka 2025 itatimia. Inawezekana Timiza Wajibu Wako.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni sana kwa kunisikiliza. Nawatakia sherehe njema.
- Apr 28, 2014
HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA HOSPITALI YA CHUO KIKUU CH...
Soma zaidiHotuba
Mheshimiwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini;
Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
Waheshimiwa Mabalozi;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam,
Professa Ephata Kaaya, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili.
Viongozi na Watendaji wa Serikali,
Viongozi na Wanajumuia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana;
Shukrani
Awali ya yote, napenda kukushukuru Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kunialika kuja kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya kisasa ya kufundishia na kutolea huduma katika eneo hili la Kampasi mpya ya Chuo Kikuu cha Afya Sayansi Shirikishi Muhimbili, Mloganzila. Leo ni siku ya aina yake katika historia ya Chuo Kikuu cha Muhimbili na taifa kwa jumla. Kitendo hiki cha leo kinaashiria kuanza rasmi kwa kazi ya ujenzi wa Kampasi mpya ya Mloganzila ya MUHAS na ni kubwa katika uboreshaji wa huduma ya afya nchini. Shughuli hii kufanyika leo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wetu ni jambo stahiki kabisa. Ujenzi huu ni moja ya kielelezo thabiti cha juhudi na mafanikio ya Serikali yetu, katika kuwapatia Watanzania huduma bora zaidi za afya.
Hali ya Sekta ya Afya Wakati Tunaungana
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana;
Utoaji wa huduma bora za afya ni wajibu wa msingi wa Serikali yetu na uhai wa taifa letu. Wakati tulipoungana tarehe 26 Aprili, 1964, hali ya huduma ya afya ilikuwa duni na afya ya wananchi wetu haikuwa ya kuridhisha. Kulikuwa na hospitali chache mno, halikadhalika, vituo vya afya na zahanati zilikuwa chache sana. Iliwalazimu wananchi kutembea umbali mrefu sana kutafuta huduma za afya. Katika vituo hivyo vya kutolea huduma za afya vifaa vya uchunguzi na vifaa tiba vilikuwa haba na duni. Wataalamu wa fani mbalimbali za afya walikuwa wachache sana. Watu walikuwa wanakufa siku si zao kwa maradhi yanayoweza kuzuilika na kutibika. Umri wa wastani wa kuishi ulikuwa miaka 35. Kwa ajili hiyo, Serikali zetu zilitangaza maradhi kuwa moja ya maadui watatu wakubwa, wengine wakiwemo umaskini na ujinga.
Katika kipindi cha miaka 50 ya muungano, Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimepambana na adui maradhi kwa nguvu kubwa. Tumetoa kipaumbele cha juu katika kupanua na kuboresha huduma za afya. Hii imejidhihirisha kwa sera na mikakati mbalimbali ya afya inayotekelezwa, ukubwa wa bajeti za afya zinazotengwa, idadi ya miradi inayotekelezwa na matokeo mazuri yanayopatikana kutokana na juhudi hizo za Serikali.
Mafanikio ya Miaka 50 ya Muungano katika Sekta ya Afya
Ndugu Wananchi;
Jitihada zilizofanyika katika miaka 50 iliyopita zimewezesha kuongezeka kwa zahanati, vituo vya afya na hospitali, vifaa vya uchunguzi, vifaa tiba na wataalamu wa kada mbalimbali za afya. Kutokana na juhudi hizo, idadi ya Watanzania wanaopata huduma bora za afya katika ngazi zote imeongezeka sana na ushindi dhidi ya maradhi mengi unaonekana. Uwezo wetu wa kupambana magonjwa yanayoua watu wengi nchini umefikia mahali pazuri, na ule wa kuchunguza na kutibu maradhi yanayotulazimu kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi unaendelea kuimarika. Kwa mfano, maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa watoto na akina mama wajawazito yamepungua kwa asilimia 50, na kule Zanzibar maambukizi ya malaria ni asilimia 0.3. Maambukizi ya UKIMWI yamepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1986 hadi kufikia asilimia 5.1 hivi sasa.
Tunaendelea kuimarisha vituo vya kutoa huduma ya afya kuanzia zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, mikoa, kanda na taifa kwa majengo, vifaa tiba, vifaa vya uchunguzi na wataalamu. Katika ngazi ya taifa kwa mfano, tumepiga hatua ya kutia moyo kwa maradhi ya moyo, figo, saratani, mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu. Kwa upande wa maradhi ya moyo tumejenga kituo cha tiba na mafunzo ya magonjwa ya moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili yenye vitanda 100. Kituo hiki kinawezesha wagonjwa wa moyo wengi kupata matibabu hapa hapa nchini badala ya kupelekwa nje. Katika kipindi cha mwaka mmoja cha ufanyaji kazi wake, kituo hiki kimeweza kufanyia upasuaji wagonjwa 347, kuwawekea mashine za kuongeza nguvu kwenye moyo (pacemaker) wagonjwa 3 na mwaka huu wameanza uwekaji wa vyuma vidogo (stent) katika mishipa ya damu ya moyo ambayo imebana. Haya ni mafanikio makubwa na ya kutia moyo.
Kwa upande wa figo, hivi sasa tunatoa huduma za magonjwa ya figo katika Hospitali ya Muhimbili, Hospitali ya Kanda, Mbeya na Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Pale Chuo kikuu cha Dodoma pia tunajenga kituo kikubwa kitakachobobea kwenye maradhi ya figo. Lengo letu ni kwamba, kitakapokamilika chuo hiki kiweze kufanya matibabu ya kubadilisha figo (kidney transplant).
Aidha, tumeboresha taasisi ya saratani ya Ocean Road kwa mejengo, vifaa na wataalamu. Tumeongeza maradufu uwezo wa taasisi hiyo kulaza wagonjwa kutoka wagonjwa 120 mwaka 2011 hadi wagonjwa 290 hivi sasa. Halikadhalika, tumenunua mashine mpya kwa ajili ya uchunguzi na tumeongeza wataalamu waliobobea wa magonjwa ya saratani. Vilevile, tunakamilisha ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mifupa, Ubongo na Mishipa ya Fahamu. Litakapokamilika tutaliwekea vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba ili kuongeza uwezo wetu wa kukabiliana na maradhi haya.
Ujenzi wa Hospitali ya Kufundishia ya Kampasi ya Mlonganzila
Ndugu Wananchi;
Jiwe la msingi tunaloweka leo, ni mwendelezo wa juhudi hizi za Serikali za kupambana na adui maradhi. Hospitali hii itakuwa na vitanda 600, itakuwa na vifaa tiba vya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mishipa ya fahamu. Ujenzi wa Hospitali ya Kampasi hii utasaidia sana kupunguza msongamano kwenye hospitali ya rufaa ya Taifa ya Muhimbili na za rufaa zilizopo nchini, ambazo hutoa huduma za utaalamu wa juu. Aidha, itasaidia kupunguza ulazima wa kupeleka wagonjwa nchi za nje kwa ajili ya matibabu. Matibabu nje ya nchi ni gharama kubwa kwa Serikali, lakini pia fursa zenyewe ni chache na wengi wengi hawapati nafasi ya kupelekwa nje kwa matibabu. Hivyo ujenzi wa hospitali hii ya Chuo Kikuu cha Muhimbili ni ishara ya wazi ya dhamira ya serikali katika kukabiliana na tatizo hili.
Hatua Zilizochukuliwa na Serikali Katika Ujenzi wa Kampasi na Hospitali ya Kufundishia
Ndugu Wananchi;
Baada ya Chuo Kikuu cha Muhimbili kutafuta eneo la kupanua huduma zake, mwaka 2006 nilifanya uamuzi wa kuwapatia eneo hili lenye ukubwa wa ekari 3,800 kwa ajili ya kujenga Kampasi mpya na hospitali ya kisasa ya kufundishia na kutolea huduma. Tulianza kutafuta fedha za ujenzi wa hospitali ya kufundishia, tukafanikiwa kupata mkopo wa riba nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini wenye thamani ya dola za Marekani milioni 76.5. Mkopo huo ungetosheleza kujenga jengo la hospitali hiyo pamoja na vifaa vya kisasa vya kutosheleza mahitaji ya hospitali.
Ujenzi haukuweza kuanza kwa wakati kutokana na mgogoro wa ardhi uliokuwepo katika eneo hili. Matokeo ya ucheleweshaji huo umepandisha gharama za ujenzi kwa dola za Marekani milioni 18. Maana yake ni kuwa fedha za mkopo tulizopata hazitoshi tena kukamilisha jengo hilo na kununulia vifaa kama ilivyokusudiwa. Viongozi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili waliponijia nilikubali bila kusita kwamba Serikali itaongeza hizo dola milioni 18 zinazohitajika. Niwahakikishie kuwa tutatoa fedha hizo ili ujenzi ukamilika kwa kiwango kilichotarajiwa.
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana;
Ni mategeneo ya Serikali kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kampasi hii, Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili kitakuwa na uwezo wa kuongeza udahili wa wanafunzi wa fani mbalimbali za afya kutoka takribani wanafunzi 3,000 na kufikia wanafunzi 15,000. Hii itapunguza kwa kaisi kikubwa, kama si kumaliza kabisa uhaba mkubwa wa wataalam wa fani za afya ulioko nchini kwa sasa. Aidha, ni mategemeo yangu pia kuwa wakati ujenzi utakapokamilika idadi ya wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu itaongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo kuongeza idadi ya wataalamu waliobobea wa fani mbalimbali za afya.
Hitimisho
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana;
Kwa kumalizia, napenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini kwa kutupatia mkopo wa ujenzi na vifaa vya hospitali hii. Mkopo uliotolewa ni mkopo wenye riba nafuu ambao kama usingepatikana ingebidi tutumie fedha iliyopangwa kwa ajili ya miradi mingine kwenye ujenzi wa hospitali hii. Napenda kuwashukuru wananchi wa maeneo ya Kwembe na Mloganzila kwa kutoa ushirikiano katika mradi huu. Mradi huu ni moja ya kielelezo cha mafanikio ya Muungano wetu wa Miaka 50, tuutunze utakapokamilika ili utufae kwa miaka 50 mingine. Nawatakieni kila la heri katika kusherehekea miaka 50 ya Muungano wetu.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
- Apr 28, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWENYE UFUNGUZI WA KITUO CHA UPASUAJI WA MOYO NA MAFUNZO CHA HOSPITALI YA TAI...
Soma zaidiHotuba
Mwakilishi wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Chen Changzhi,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Seif S. Rashid (Mb),
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Charles Pallangyo,
Mhe. Balozi wa Serikali ya Watu wa China,
Waheshimiwa Mabalozi waliopo hapa,
Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Viongozi Wenzangu;
Wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili;
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana,
Shukrani
Nakushukuru Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa kunialika kuja kushiriki nanyi katika ufunguzi wa kituo hiki muhimu cha upasuaji wa moyo na mafunzo. Nafurahi kuwa Mheshimiwa Chen Changzhi, Naibu Spika wa Bunge la China amejumuika nasi katika hafla hii. Alikuja hapa kwa sherehe za miaka 50 ya Muungano akimwakilisha Rais wa China. Tukaona tutumie fursa hiyo pia tuzindue kituo hiki muhimu kilichojengwa kwa msaada wa Serikali ya China kugharamia sehemu kubwa ya gharama. Kituo hiki kimegharimu shilingi bilioni 26.6 kati ya hizo China imetoa shilingi bilioni 16.6 na Tanzania imetoa shilingi bilioni 10.
Kituo tunachokizindua leo ni kituo cha kisasa kabisa, chenye vifaa vya hali ya juu, vinavyotumia teknolojia ya kisasa katika uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo. Kupatikana kwa kituo hiki, Tanzania inapiga hatua nyingine muhimu katika kuendeleza huduma ya afya nchini. Ni ukweli usiofichika kwamba maradhi ya moyo duniani yanaongezeka. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa kwa mwaka takribani watu milioni 12 wanakufa duniani kwa maradhi haya. Hapa nchini inasemekana wagonjwa wa maradhi haya wamekuwa wanaongezeka kwa asilimia 26 kwa mwaka. Maradhi haya yameanza kuwa tatizo kubwa hapa kwetu, hivyo hatuna budi kuchukua hatua thabiti kukabiliana nayo.
Kwa sababu ya kukosa uwezo wetu wa ndani, haswa kwa wagonjwa wanaohitaji upasuaji kuwekewa wa moyo, pacemakers au stents, tumelazimika kuwapeleka nje ya nchi kwa matibabu. Ni gharama kubwa, hivyo hatuwezi kuwapeleka watu wengi wanaohitaji tiba hiyo. Matokeo yake ni wagonjwa wengi kuishi kwa mateso na hata kupoteza maisha.
Kwa nia ya kutaka kuokoa maisha ya Watanzania waliopata maradhi ya moyo, ndipo tulipowaomba ndugu zetu wa China. Wakati ule Rais wa China, Mheshimiwa Hu Jintao alitukubalia. Jimbo la Shandong ambalo ndilo limekuwa linatoa madaktari wengi kutoka China, lilikabilidhiwa jukumu la ujenzi wa kituo hiki. Kama nilivyosema, kwa ushirikiiano wa pamoja wa nchi zetu, kituo kimekamilika na kimekwishaanza kutoa huduma.
Tunapofanya uzinduzi wa kituo hiki leo, ni fursa nzuri kuwashukuru marafiki zetu wa China. Tunawashukuru kwa msaada mkubwa waliotupatia na tunawashukuru kwa heshima ya Mjumbe mzito kwenye sherehe hii. Tunashukuru pia kwamba mgeni huyu pia amekuja kumwakilisha Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping na watu wa China katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
Mheshimiwa Waziri;
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
Mkuu wa Taasisi Hii;
Kituo kimekamilika sasa kazi kwetu. Tunaomba muhakikishe kuwa kituo hiki kinatimiza majukumu yake kama ilivyokusudiwa. Kwa ajili hiyo, naomba mfanye yafuatayo:
- Hakikisheni vifaa na mahitaji ya upasuaji yanapatikana wakati wote. Itakuwa haina maana kujenga jengo zuri kama hili na kufundisha mabingwa wa upasuaji wa moyo kisha wasifanye kazi waliyosomea kufanya.
- MSD ielekezwe kuhakikisha kuwa vifaa na mahitaji hayo yanapatikana wakati wote.
- Wizara, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mkuu wa Kituo hiki hakikisheni kuwa mnatoa kipaumbele cha kwanza kwa shughuli za upasuaji katika kituo hiki. Hii ina maana ya mgao wa fedha na mipango ya kazi ya kituo.
- Waziri na Mkurugenzi Mkuu anzeni kufikiria utaratibu bora wa uandeshaji wa kituo hiki. Angalieni uwezekano wa kufanya kituo hiki kuwa taasisi inayojiendesha chini ya Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Nazungumzia mfumo unaokaribia kufanana na Taasisi ya Mifupa. Hii itaihakikishia kituo hiki ustawi na uhai endelevu.
- Jiepusheni na kishawishi cha kugeuza wodi za taasisi hii kuwa ni wodi za wagonjwa ambao ni watu mashuhuri na wenye uwezo. Ninachoshauri, tengenezeni mpango wa kujenga jengo kama hili kwa watu hao. Nachelea tusije kujikuta, wamejaa watu wengine, wagonjwa wa moyo wakakosa nafasi.
- Naomba uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, uongozi wa kituo na wafanyakazi kukitunza kituo hiki kwa kiwango cha juu ili kidumu na kilifae taifa letu na watu wake kwa miaka mingi ijayo. Hakikisheni kunafanyika matengenezo kwa wakati. Msifanye ajizi kwani ukarabati husababishwa na kuchelewa kufanya matengenezo. Ukifanya matengenezo kwa wakati huhitaji ukarabati. “Rehabilitation is deferred maintenance”.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Nimalize kwa kutoa tena shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Rais mstaafu Mheshimiwa Hu Jintao na Rais Xi Jinping, Serikali ya Jimbo la Shandong na Kampuni ya Uhusiano wa Kiuchumi na Kiufundi ya Kimataifa ya Shandong kwa mchango wao uliowezesha ujenzi wa Kituo hiki. Wananchi wa Tanzania wanathamini na kuienzi zawadi hii kutoka kwa wananchi wa China kwa ajili yetu. Serikali ya Tanzania itahakikisha kwamba Kituo hiki kinaendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa kama inavyotarajiwa.
Baada ya kusema haya sasa naomba kutamka kuwa Kituo cha Upasuaji, Tiba na Mafunzo ya Moyo kimefunguliwa rasmi.
- Apr 15, 2014
SPEECH BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, DURING THE WORLD ECONOMIC FORUMS ALIGNMENT MEETING ON DEVELOPMENT OF CENT...
Soma zaidiHotuba
Hon. Dr. Harrison Mwakyembe, Minister for Transport, United Republic of Tanzania;
Hon. Prof. Silas Lwakabamba, Minister for Infrastructure, Republic of Rwanda;
Hon. Eng. Virginie CIZA, Minister for Transport, Public Works and Equipment, Republic of Burundi;
Hon. Justin Kalumba MWANA NGONGO, Minister for Transport and Water Ways, Democratic Republic of Congo;
Hon. Eng. Abraham Byandala, Minister for Transport and Works, Republic of Uganda;
Dr. Donald Kaberuka, President of the African Development Bank;
Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the East African Community;
Dr. Stogomena Tax, Executive Secretary of SADC;
Dr. Ibrahim A. Mayaki, President, NEPAD Agency;
Mr. Philippe Dongier, World Bank Country Director for Tanzania, Uganda and Burundi;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
It is a pleasure for me to welcome you all to Tanzania and Dar es Salaam. I thank the organizers for affording this rare opportunity to speak at this all important World Economic Forum Alignment Meeting on Development of the Central Corridor.
This meeting could not have been organized at a better time, than this. As a matter of fact such people of this region have been waiting for this type of action for a long time. Besides that, this meeting is part of the preparations for the World Economic Forum for Africa meeting scheduled for 7th to 9th May, 2014. The work of this meeting will therefore have a special significance to the implementation of the Priority Action Plan of Programme for Infrastructure Development in Africa (PIDA) which has its roots from the World Economic Forum in Africa held in Addis-Ababa, from 9th to 11th May, 2012.
It is gratifying to see high level participation of four important institutions among us: the EAC, SADC the AfDB, the NEPAD Agency and the World Bank. It is heartwarming indeed, to have you with us because you are critical factor on the success of the agenda at hand. We look forward to your continued involvement until we reach the objectives of this initiative.
From WEF Addis Ababa to WEF Abuja: Private Sector and
African Infrastructure Development
Distinguished Delegates;
The 2012 World Economic Forum for Africa was a turning point with regard to how we approach the question of development of infrastructure in Africa. It came to our awareness and realization that we need to bring in Private Sector in infrastructure development in Africa. Such a perspective had not been embraced before by governments in Africa, with each one trying to shoulder the cost alone.
I commend the joint-initiative of the WEF, the AfDB, the AU Commission and NEPAD (New Partnership for Africa's Development) for taking forward the agenda. As a follow up, an African Strategic Infrastructure Initiative (ASII) was formally launched in Johannesburg on the 9th of July, 2012, with the formation of the Business Working Group (BWG), a platform for African infrastructure development strategies and initiatives.
I am pleased with the work of the Business Working Group for identifying projects with high potential for short-term acceleration. I am particularly delighted with the choice of the Central Corridor in this regard. I also thank you for affording my country the honour of preparing a Wider Concept Note on the development of the Central Corridor.
Importance of the Transport Corridors
Distinguished Delegates;
The importance of transport corridors as game changers for regional growth and development need not be over-emphasized. Studies after studies have concluded that many landlocked developing countries are among the poorest in the world. It is said, out of 31 such countries, 16 are classified as least developed and half of these are in Africa.
These countries are said to be penalized annually by 1.5 percent reduction in average growth compared to coastal states by simply being landlocked. It goes without saying that: growth of landlocked countries depends on the growth of the coastal countries. That implies the ability of the coastal countries to put in place infrastructure for trade facilitation, as a pre-requisite for development of the land locked countries.
Distinguished Delegates;
The coastal states have never fallen short of good will in facilitating the landlocked countries. They have been putting in place supportive infrastructure because they too, are primary and secondary beneficiaries of such infrastructure. It is the difficulties of raising financing of these infrastructures that has been holding back coastal states particularly the Least Developed Countries, from rising to challenge effectively.
Efforts to exploit joint regional financing mechanisms has also proven unsuccessful. Experience has shown that it is easier to arrange investment for national infrastructure than for regional ones. Our experience on the ongoing construction of 11,174 kilometers of road to tarmac level serves as a good lesson. It is for this reason that, we welcome this approach of partnering with the private sector for regional infrastructure development.
Status of Central Corridors
Distinguished Delegates;
The Central Corridor is located at the strategic geographical position which makes it a natural choice as a major trade route for countries of the Eastern and Central African regions. Indeed, for many decades the Dar-es-Salaam Port, Tanzania’s roads and railways have served the neighboring countries of Uganda, Rwanda, Burundi and the Democratic Republic of Congo (DRC).
Economies of countries served by this corridor have shown strong GDP growth rates of between 4 and 8 percent. Transit demand is forecasted to increase from 2.7 million to 9.8 million tons by 2030. The Dar es Salaam port captures 14 percent of imports and exports of these countries. As a result the throughput at the port has increased from 7.4 million tons in 2007 to 13 million tons by December 2013.
The Central Corridor also enjoys one of the best roads in East Africa. The Dar es Salaam-Rusumo/Kabanga and Dar es Salaam-Mutukula (at the borders of Rwanda/Burundi and Uganda respectively) are fully paved. The presence of these routes makes the Central Corridor a competitive option for cross border trade through the Port of Dar es Salaam.
Distinguished Delegates;
Rwanda and Burundi are connected to the Port of Dar es Salaam by the Central Corridor that consists of several routes. These routes include an all-road unimodal option from Dar es Salaam to Bujumbura and Kigali. Alternatively, cargo flows along the intermodal routes made up of rail from Dar es Salaam to Isaka then trans-shipped to Kigali and Bujumbura. Rwanda and Burundi are now working together with Tanzania to extend the central railway line from Isaka to Kigali on wards to Keza – Musongati in Burundi.
The Republic of Burundi has discovered enormous deposits of nickel. The corridor is about to transport more volumes of heavy minerals within the coming two to three years. Our neighbor Burundi may in the coming 2 or 3 years start exporting between 1.5 million tons to 3 million tons of nickel concentrates a year. In the same development, we expect two nickel mines in Tanzania (Kabanga and Dutwa) to be operational in the same time span. It is likely that nickel processing would require importation of huge volumes of sulphur per annum. All these volumes are expected to pass through the Central Corridor.
Challenges Facing Central Corridor
Distinguished Delegates;
Despite the great potentials and opportunities presented by the Central Corridor, all is not rosy in terms of both effectiveness and efficiency. Transport inefficiencies in this region, have contributed to prohibitively high transport costs, and impede the region's ambition to realize its overall vision for socio-economic development.
The design capacity of the Tanzania Railway Limited (TRL) line is to move traffic of about 5million tons per year. Unfortunately, this capacity has never been achieved as the maximum capacity reached so far is only 1.4 million tons of cargo moved by train as the performance record in 2002. While there are prospects of transit cargo to double up within the coming few years, as the region braces itself to start exporting millions of tons of copper and nickel a year, the existing 2,707 kilometers Central railway, cannot in its present condition cope with the growing volume of cargo along the central corridor.
Distinguished Delegates;
It suffices to say, both our roads and the central railway line lead to the Port of Dar es salaam needs a turn around. It needs refurbishing. We still need to expand our berth capacity, modernize our cargo handling facilities as well as procedure to cope with the growing volume of throughput. We have indeed embarked on the exercise, but in a limited way by using our yearly budgetary allocations and development partners' support. Thanks to the World Bank, the AfDB and JICA. Apart from the measures we have so far taken to enhance port efficiency, reliability and security. We thank to Trade Mark East Africa, DFID and the World Bank for the continued support to improve port efficiency.
Efforts Undertaken by Tanzania to Improve the
Central Corridors
Distinguished Delegates;
Tanzania has continued to fulfill her regional responsibility to our landlocked neighbors, and international obligations under the Almaty Programme of Action. There are number of efforts we have put in place which are short and long-term plans. Our short-term plan is to rehabilitate the railway line by reinforcing its formation, strengthening its bridges, removing lighter, old, worn out rails, fasteners, sleepers and installing new heavier rails, sleepers and ballast. We have so far done almost 600 kilometers. Thanks to the World Bank and JICA.
We have continued to make available our Dar es Salaam Port as an export and import gateway for the landlocked countries of Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia, Malawi and the DRC. Some of the initiatives which are underway includes;
a) Dredging of the Dar es Salaam port entrance channel;
b) Construction of Berths 13 and 14;
c) Strengthening and deepening of Berths 1-7;
d) Development of the Roll on – Roll off (RO-RO) Berth at the Dar port;
e) Plan to develop Kisarawe Freight Station with intention to decongest container traffic at the Dar port and development of new port at Bagamoyo among others.
The government decided to give due weight to these initiatives through mainstreaming them in the Big Results Now (BRN) Port Initiatives, with the aim to ensure their timely implementation. We have earmarked to increase throughput of the Dar es Salaam Port from the current 13 million tons per annum to about 18 million tons annually by end of 2015. Furthermore, it is targeted to reduce time taken by a truck to transport a transit container from the Dar es Salaam Port to the borders of Burundi and Rwanda to 2½ days from the current 3½ days by the end of 2015.
Distinguished Delegates;
But these short-term measures will not enable us to service a growing regional economy effectively and efficiently. The Dar es Salaam Port for example, currently handles 13 million tons of freight per year but hardly 2 percent of the freight is carried on rails, the rest is transported by trucks, drastically shortening the lifespan of most of our paved roads.
It is against this background that we came up with a long-term plan or strategy to upgrade the central line to standard gauge. Part of the line i.e. Dar es Salaam – Isaka – Keza – Kigali/Gitega – Musongati (1,591 kilometers long), is a joint project by Tanzania, Rwanda and Burundi. It is estimated to cost us a minimum of USD 4.13 billion. We have jointly done all the preliminary studies. With the completion of the detailed study recently, we are now on procurement of Transaction Advisor. Thanks to the AfDB for its support.
Tanzania and Burundi have also a bilateral arrangement to construct a 200 kilometers standard gauge railway between Uvinza in Tanzania and Musongati in Burundi expected to cost us USD 550 million.
Private Sector and Central Corridor
Distinguished delegates;
The central corridor projects I have briefly narrated cannot be successfully implemented within the context of the traditional method of financing infrastructure development. Government financing alone may not easily raise all the money required. We do not have the money nor can we easily get someone to lend us so much money. We have tried this option over the years without much success.
It is time we encouraged further private sector participation. It remains an alternative and viable option to minimize the public financing gap in infrastructure development. I have vested my hopes in this meeting which I believe will take us to the next level in terms of unlocking private sector funding, identifying cross-border regulation gaps and building private-public sector confidence.
Distinguished Delegates;
It is befitting that this alignment meeting is taking place at this point in time. We have undertaken to put in place conducive environment to facilitate private sector to join our efforts. The government has put in place the National Public-Private Partnership (PPP) Policy in 2009, in 2010 we enacted the Public-Private Partnership Act, Cap 403 and Regulations in 2011. In addition, feasibility studies have been undertaken while various identified PPP projects have been advertized for private sector to show interest. We will continue to work together with our Central Corridor member states in soliciting funds to invest in the key transport infrastructure projects along the corridor.
The Government, in partnership with the OECD and NEPAD, undertook a review of its investment policies to support the national strategy for economic reform and improve the business climate to attract more investment in key sectors, such as infrastructure and agriculture. The review was launched on 31st January, 2014 and will be used to update all investment policies; and continue with implementation of Government Roadmap on the Improvement of the Investment Climate by undertaking administrative measures with very limited cost implications while reducing hurdles of significant costs to local and foreign investors. These measures go along with automated and electronic payment systems that minimize human interference and discretionary powers.
Way Forward
Distinguished Delegates;
I am optimistic that the groundwork we have undertaken as a region for the implementation of the Central Corridor Infrastructure projects through public private sector cooperation have caught the attention of the international business community. I thank the WEF in collaboration with the AfDB, the AU Commission and NEPAD for championing this noble cause for Africa's economic development. As corridor member states with a lot to gain from improved inter and intra-regional trade, let us continue to plan, discuss, decide and implement together our infrastructure development projects. Our numbers would always attract the attention of serious investors.
Conclusion
Distinguished Delegates;
I am optimistic that our regional efforts to implement the Central Corridor Infrastructure projects through public private partnership is now at a point of take-off and definitely will bear good results in the very near future. We believe that WEF strategies under this new model of Central Corridor to be the African pilot project for accelerating investments will support the current potential infrastructure projects along the corridor to secure strategic investors soon. What I wish to share with our colleagues from the Corridor member states is to continue working together under these efforts so as to achieve the expected regional investment goals. Everything is possible if we plan, discuss, decide and implement together.
This is the opportunity for our governments to interact with other stakeholders including the private sector, with a view to coming up with a programme of action for the development of the central transport corridor.
To conclude my remarks, I have taken note of the fact that you have a rather long and demanding agenda in front of you and, for that reason, I wouldn't like to keep you any longer than necessary. It is therefore my singular honour and pleasure to wish you a very fruitful meeting and to declare that the Alignment meeting on the Central Corridor is now opened.