Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Uongozi

Utawala wa Jamhuri ya Muungano una Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri wa Mkuu na Baraza la Mawaziri.

Rais wa Jamhuri la Muungano ndiye Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Rais ndiye kiongozi wa Utawala wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais ndiye msaidizi mkuu wa Rais kwa mambo yote ya Jamhuri ya Muungano  kwa ujumla na hasa ana wajibu wa kumsaidia Rais katika;

i. Kufuatilia utelekezaji wa kila siku wa mambo ya Muungano

ii. Kufanya kazi zote atakazopewa na Rais

iii. Kufanya kazi zote na majukumu ya ofisi ya Rais, wakati Rais asipokuwepo au anapokuwa nje  ya nchi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ndiye Kiongozi wa shughuli za Serikali  Bungeni na ana mamlaka ya kudhibitisha, kusimamia na kutelekeza kazi za kila siku na mambo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha anatekeleza jambo lolote ambalo Rais atamwelekeza kuwa lifanywe.

Rais wa Zanzibar ndiye Kiongozi wa Utawala wa Zanzibar, Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar

Baraza la Mawaziri ni pamoja na Waziri Mkuu, anayeteuliwa na Rais kutokana na Wabunge wa Bunge la Taifa. Serikali inatekeleza kazi zake kupitia kwa Wizara zinazoongozwa na Mawaziri. Kila wizara ina dhmana ya kazi na sekta yake.