Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali, wadau wa Nishati pamoja na Washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika unaofanyika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amempokea rasmi Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakati alipowasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kushuka kwenye gari Maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya Uchumi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Pamoja na waumini wengine wa dini ya Kiislam katika ibada ya Eid El Fitri Msikiti Mkuu wa Bakwata (Mfalme Mohammed VI wa Morocco), Kinondoni Dar es Salaaam, tarehe 10 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi milioni 500 kwa ajili ya Mashindano yanayohusu Timu za Taifa za Tanzania kutoka kwa Mfanyabiashara Said Naseer Naseer kwa niaba ya Wafanyabiashara wenzake kutoka Zanzibar. Shughuli hii imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpakulia Iftar mtoto Yatima Shuraiya Ramadhan (6) wa Kituo cha Watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Jijjini Dodoma. Rais Samia aliwaandalia Iftar Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wageni wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya walipowasili Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.