Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

WASILISHO LA MWENYEKITI WA KIKOSI KAZI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN TAREHE 21 OKTOBA, 2022


MAELEZO YA MWENYEKITI WA KIKOSI KAZI KWA MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI ANAWASILISHA RIPOTI YA KIKOSI KAZI

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa George B. Simbachawene (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu

 

Mheshimiwa Balozi Hussein Kattanga, Katibu Mkuu Kiongozi

Mheshimiwa Jaji Fransis Mutungi, Msajili wa vyama vya Siasa

Mheshimiwa Mohamed Ali Ahmed, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa

Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, Makamu Mwenyekiti wa Kikosi Kazi

Waheshimiwa wajumbe wa Kikosi Kazi mliopo

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

SHUKRANI

 

Mheshimiwa Rais, awali ya yote wajumbe wa Kikosi Kazi tunaomba kutumia fursa hii, kukushukuru na kukupongeza kwa juhudi unazofanya za kutuletea Watanzania maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, hususani kuboresha mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa nchini. Mheshimiwa Rais, tunamshukuru na kumpongeza, Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa juhudi anazofanya Zanzibar za kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwemo kuboresha mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa.

 

CHIMBUKO LA KIKOSI KAZI

 

Mheshimiwa Rais, Tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kulifanyika Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Jijini Dodoma ulioitwa “Mkutano wa Wadau wa Kujadili Hali ya Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa nchini Tanzania”. Mkutano huo ulijadili mafanikio na changamoto zilizopo katika suala la demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini. Mkutano huo uliufungua wewe Mheshimiwa Rais na ulifungwa na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

 

Katika mkutano huo, masuala mengi yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa yalijadiliwa na washiriki walitoa maoni na mapendekezo ambayo idadi yake ilifikia tisini na nane (98). Kutokana na wingi wa maoni na mapendekezo yaliyotolewa na kiu ya washiriki wa mkutano huo kuona yanafanyiwa kazi, washiriki wa mkutano huo waliazimia kwamba kiundwe Kikosi Kazi cha kuchambua na kuandaa mapendekezo ya kuwasilishwa Serikalini

 

UUNDWAJI WA KIKOSI KAZI

 

Mheshimiwa Rais, Kikosi Kazi kiliundwa tarehe 23 Desemba 2021 kikiwa na wajumbe ishirini na nne (24), kati ya hao, kumi na sita (16) wanatoka Tanzania Bara na wanane (8) wanatoka Zanzibar. Baada ya Kikosi Kazi kuanza kazi, mjumbe Bibi Christine Solomon Mndeme, Naibu Katibu Mkuu wa CCM alibadilishwa, nafasi yake ilichukuliwa na Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Rais, Uundwaji wa Kikosi Kazi ulizingatia uwakilishi wa wadau waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa uliofanyika tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 Dodoma. Hivyo, muundo wake unajumuisha aina za wadau wafuatao: Wasomi, Wanasiasa, Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Taasisi za Dini, Taasisi za Serikali na Vyama vya Kitaaluma.

 

 

 

 

 

Mheshimiwa Rais, Majina ya wajumbe wa Kikosi Kazi ni haya yafuatayo kwa mpangilio wa alphabeti:-

 

 

Na.

                Jina

   Wadhifa

  1.  

Mhe. Profesa Rwekaza Sympho Mukandala

Mwenyekiti

  1.  

Bw. Hamad Rashid Mohamed

Makamu Mwenyekiti

  1.  

Bw. Slim Said Abdallah

Mjumbe

  1.  

Mhe. Balozi Amina Salum Ali

Mjumbe

  1.  

Bw. Deodatus Mutalemwa Balile

Mjumbe

  1.  

Bibi. Fatma Abdulhabib Fereji

Mjumbe

  1.  

Mchungaji George Paul Fupe

Mjumbe

  1.  

Prof. Edward Gamaya Hoseah

Mjumbe

  1.  

Bibi. Jamila Mahmoud Juma

Mjumbe

  1.  

Bw. Zitto Zuberi Kabwe

Mjumbe

  1.  

Mhe. Juma Ali Khatib

Mjumbe

  1.  

Mhe. Haji Omar Kheri

Mjumbe

  1.  

Dkt. Lucas Luhende Kija

Mjumbe

  1.  

Bibi. Anna Meela Kulaya

Mjumbe

  1.  

Bw. Ali Omar Makame

Mjumbe

  1.  

Prof. Alexander Boniface Makulilo

Mjumbe

  1.  

Prof. Bernadeta Kilian Mchapwaya

Mjumbe

  1.  

Bw. Abdul Juma Mluya

Mjumbe

  1.  

Bw. Martin Bernard Mung’ong’o

Mjumbe

  1.  

Mhe. Mizengo Kayanza Pinda

Mjumbe

  1.  

Bibi. Saum Hussein Rashid

Mjumbe

  1.  

Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum

Mjumbe

  1.  

Dkt. Ave Maria Emilius Semakafu                     

Mjumbe

  1.  

Kamishna wa Polisi, Benedict Michael Wakulyamba

Mjumbe

  1.  

Bw. Sisty Leonard Nyahoza

Katibu

KAZI ZILIZOFANYWA NA KIKOSI KAZI

Mheshimiwa Rais, baada ya uzinduzi Kikosi Kazi kilianza kazi tarehe 11 Januari 2022. Hadi sasa Kikosi Kazi kimefanya kazi zifuatazo:

  1. kupitia hadidu rejea;
  2. kuchambua hotuba ya kufungua, kufunga, maoni na mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano wa wadau na kuainisha masuala muhimu ya kufanyiwa kazi;
  3. kuandaa Mpango Kazi wenye masuala tisa (9) yaliyoanishwa;
  4. kuchambua na kuandaa maoni na mapendekezo kuhusu suala la mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa;
  5. kuandaa taarifa ya awali ya Kikosi Kazi iliyowasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 12 Machi 2022;
  6. kukaribisha maoni ya wadau;
  7. kutoa maoni kwa Serikali kuhusu utungaji wa Kanuni za kuratibu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa;
  8. kuzungumza na wadau mbalimbali wa demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ili kupata maoni yao; na
  9. kuchambua maoni ya wadau na
  10. kuandaa ripoti ya Kikosi Kazi.

MAENEO YA YALIYOFANYIWA KAZI

Mheshimiwa Rais, baada ya uchambuzi wa kina wa hotuba ya kufungua na kufunga, maoni ya wadau yaliyotolewa katika Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa wa tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021, Kikosi Kazi kiliainisha masuala tisa (9) ya kufanyia kazi yafuatayo:

  1. Mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani ya Vyama vya Siasa;
  2. Masuala yanayohusu Uchaguzi;
  3. Mfumo wa maridhiano ili kudumisha haki, amani, utulivu na Umoja wa kitaifa;
  4. Ushiriki wa Wanawake na Makundi Maalum katika siasa na Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa;
  5. Elimu ya Uraia;
  6. Rushwa na Maadili katika Siasa na Uchaguzi;
  7. Ruzuku ya Serikali kwa Vyama vya Siasa;
  8. Uhusiano wa Siasa na Mawasiliano kwa Umma; na
  9. Katiba Mpya.

 

Mheshimiwa Rais, ili kupata mtazamo mpana kuhusu masuala tisa yanayofanyiwa kazi, tarehe 14 Aprili, 2022 Kikosi Kazi kilitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, kualika watanzania wote kuwasilisha maoni na mapendekezo kuhusu masuala hayo tisa (9), kwa njia mbalimbali ikiwemo, “WhatsApp” kupitia namba ya simu ya Katibu, barua pepe taskforcemaoni@orpp.go.tz, anuani ya posta ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kuzungumza na wajumbe wa Kikosi Kazi ana kwa ana.

 

Mheshimiwa Rais, wakati wa kutekeleza majukumu yake, Kikosi Kazi kimechambua maoni na mapendekezo 98, yaliyotolewa na washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa uliofanyika tarehe 15-17 Desemba 2021 Dodoma. Vilevile, ilichambua maoni ya maandishi na kuzungumza yaliyotolewa na wadau mbalimbali waliowasilisha maoni na mapendekezo kwa Kikosi Kazi. Wadau waliowasilisha maoni kwa Kikosi walitoka katika makundi yafuatayo:

 

  1. Viongozi wa Serikali waliopo madarakani na wastaafu;
  2. Watu Mashuhuri;
  3. Taasisi za Serikali;
  4. Taasisi za Dini;
  5. Vyama vya Siasa;
  6. Makundi ya Kijamii;
  7. Wanataaluma
  8. Asasi za Kiraia
  9. Wafanyabiashara
  10. Wakulima
  11. Watanzania waishio nje -Diaspora

 

Mheshimiwa Rais, Kikosi Kazi kimepata bahati ya kukutana na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara tatu. Tarehe 12 Machi 2022, tarehe 21 Machi 2022 na tarehe 30 Mei, 2022. Vilevile kimekutana na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mara tatu tarehe 10 Januari 2022, tarehe 20 Aprili 2022 na tarehe 15 Agosti 2022. Hivyo, wajumbe wa Kikosi Kazi tunawashukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar kwa fursa mlizotupa za kukutana nanyi pamoja na kuwa na majukumu mengi ya kitaifa. Fursa hizi mlizotupatia ni moja tu kati ya mambo mengi yanayodhihirisha utashi wenu wa kisiasa kwa kazi tunayofanya na maboresho ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa katika nchi yetu.

 

Mheshimiwa Rais, wajumbe wa Kikosi Kazi tunakushukuru kwa usimamizi na mwongozo wako thabiti katika kutekeleza majukumu yetu ya Kikosi Kazi. Tangu tuanze kazi tarehe 10 Januari 2022, hatujawahi kusitisha kazi yetu kwa sababu ya kukosa rasilimali au vitendea kazi, changamoto yoyote ilipotokea umekuwa ukitoa maelekezo ifanyiwe kazi mapema iwezekanavyo, ili kazi isisimame, iendelee kama kauli mbiu ya Taifa letu uliyoiasisi inavyosema.

 

MAPENDEKEZO YA KIKOSI KAZI

 

Mheshimiwa Rais, baada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi kumi (10), sasa tunayo heshima kuwasilisha kwako, matokeo ya kazi uliyotupatia. Ripoti ya Kikosi Kazi tunayowasilisha ina sura kumi na moja ambapo kila sura imeeleza suala husika, maoni ya wadau, uzoefu nchi nyingine, uchambuzi na mapendekezo ya Kikosi Kazi.

 

 

 

 

Mheshimiwa Rais, ili kuokoa mda, ninawasilisha mapendekezo tu. Nayo ni haya yafuatayo:

 

1.    Kuhusu mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

    1. Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa Katiba na Sheria;
    2. Mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote;
    3. yafanyike marekebisho ya Sheria, ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi. Sheria hizo ni pamoja Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi Sura ya 322 na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa za Mwaka 2019.

 

2.    Kuhusu demokrasia ndani ya vyama vya siasa

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho ili:

  1. kulipatia Baraza la Vyama vya Siasa linaloundwa na vyama vyenyewe,  mamlaka ya kushughulikia suala la uvunjifu wa maadili ya Vyama vya Siasa kupitia Kamati yake ya Maadili; yaani self-regulation
  2. Msajili wa Vyama vya Siasa aandae mwongozo wa uchaguzi wa ndani ya Vyama vya Siasa;
  3. kuweka masharti kwamba idadi ya jinsi moja katika vyombo vya maamuzi vya chama cha siasa isipungue asilimia 40; na
  4. kukitaka kila chama cha siasa kuwa na sera ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za chama husika.

 

3.   Kuhusu ruzuku kwa vyama vya siasa inayotolewa na Serikali

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku ya Serikali kwa Vyama vya Siasa uendelee, isipokuwa asilimia 10 ya fedha za ruzuku kwa Vyama vya Siasa zinazotengwa katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha husika, igawiwe sawa kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili kwa mujibu wa vigezo na masharti yafuatayo:
  1. chama kiwe na usajili kamili;
  2. chama kiwe kimefanyiwa uhakiki na Msajili wa Vyama vya Siasa na kuthibitishwa kwamba, kinakidhi vigezo vya usajili kamili;
  3. chama kiwe kimeshiriki Uchaguzi Mkuu angalau mara mbili tangu kupata usajili kamili;
  4. katika mwaka wa fedha uliopita, chama husika kisiwe kimepata Hati Chafu ya Mahesabu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; na
  5. ruzuku itumike kwa shughuli za kuendesha Ofisi ya Makao Makuu, Ofisi Ndogo au Ofisi Kuu ya Makao Makuu ya chama cha siasa husika.
  1. Sheria ya Vyama vya Siasa itamke kuwa, asilimia ishirini (20%) ya fedha za ruzuku kwa Vyama vya Siasa inayotolewa na Serikali katika mwaka wa fedha, igawiwe kwa Vyama vya Siasa vyenye Madiwani wa kuchaguliwa katika kata, kwa mujibu wa uwiano wa idadi ya Madiwani hao ambao kila chama kinao, kwani kwa sasa sheria haijatamka kiwango chochote bali imempa mamlaka Waziri Mwenye dhamana kuamua; na
  2. Serikali iongeze fedha za bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa, ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ikiwemo jukumu linalopendekezwa la kusimamia Maadili ya Vyama vya Siasa.

 

4.    Kuhusu uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. tume ya Taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya Serikali, maoni ya chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote; na
  2. utendaji wa Tume ya Uchaguzi uruhusiwe kuhojiwa kwenye Mahakama ya Juu pale itakapoanzishwa ili kuongeza uwajibikaji wa Tume.

 

5.    Kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa utaratibu ufuatao utumike kuwapata wajumbe wa tume ya Taifa ya Uchaguzi:

  1. kuwe na Kamati ya Uteuzi ya Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakayokuwa na wajumbe wafuatao:
  1. Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
  2. Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti;
  3. Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Tanzania Bara;
  4.  Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Zanzibar;
  5.  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu; na
  6.  wajumbe wengine wawili watakaoteuliwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupendekezwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika na Chama cha Wanasheria Zanzibar.
  1. angalau wajumbe wawili wa Kamati ya Uteuzi wawe wanawake;
  2. sifa za mtu kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ziainishwe;
  3. nafasi ya mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itangazwe na Mtanzania yeyote mwenye sifa aruhusiwe kuwasilisha maombi kwa Kamati ya Uteuzi ya kuwa mjumbe wa Tume;
  4. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili wa watu waliowasilisha maombi ya kuwa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaostahili kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
  5. Kamati ya Uteuzi itawasilisha kwa Rais majina manne (4) zaidi ya idadi ya nafasi zinazohitajika kujazwa; na
  6. Rais ateue wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi miongoni mwa majina yaliyowasilishwa kwake na Kamati ya Uteuzi.

 

6.   Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutohojiwa Mahakamani

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa, matokeo ya uchaguzi wa Rais yahojiwe kwenye Mahakama ya Juu mara itakapoanzishwa.

 

7.    Kuhusu watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria, weledi, maadili, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wakati wa kufanya kazi zao; na
  2. wasimamizi wa uchaguzi watakaokiuka sheria na utaratibu wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria.

 

8.    Kuhusu bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipewe fedha zilizotengwa katika bajeti kwa wakati, hata baada ya uchaguzi, ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wote.

9.    Kuhusu sheria zinazosimamia masuala ya uchaguzi Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. itungwe sheria ya kusimamia shughuli za Tume ya Taifa Uchaguzi;
  2.  kuwepo na sheria moja ya uchaguzi itakayotumika kusimamia uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani, badala ya kuwa na sheria mbili ambazo ni Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343 na Sheria ya Uchaguzi wa Madiwani Sura 292; na
  3. maafisa wa Tume ya Uchaguzi watakaowaengua wagombea kushiriki katika uchaguzi bila kuzingatia sheria na weledi  uchaguzi wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

10.  Kuhusu matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. matumizi ya TEHAMA katika mchakato wa uchaguzi yahamasishwe na kiwango chake kiongezwe; 
  2. zitayarishwe Kanuni mahsusi za kuratibu matumizi ya TEHAMA kwenye mchakato wa uchaguzi; na
  3. kuwepo na uwekezaji wa kutosha kwenye miundombinu ya TEHAMA na usalama wake wakati wa uchaguzi.

 

11.  Kuhusu ushiriki wa Wanawake katika Siasa, Demokrasia na Uongozi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. Sheria ya Vyama vya Siasa irekebishwe ili:
  1. kuweka sharti la kila chama cha siasa kuwa na sera ya jinsia na ujumuishi wa makundi maalum katika jamii;
  2. kuweka sharti la kisheria kwamba idadi ya jinsi moja katika vyombo vya maamuzi ndani ya chama cha siasa isipungue asilimia 40;
  3. Kanuni za Usajili na Ufuatiliaji wa Vyama vya Siasa za Mwaka 2019 ziwe na vigezo vya ufuatiliaji ili kupima utekelezaji wa Sheria, katiba na kanuni za vyama vya siasa, kuhusu masuala ya jinsia na ujumuishaji wa makundi maalum ya jamii katika chama na uchaguzi; na
  1. katiba za vyama ziwe na Ibara zinazoshughulikia masuala ya ukatili wa jinsia ikiwemo udhalilishaji wa wanawake;
  2. kila chama cha siasa kiwe na programu maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake kugombea ubunge, uwakilishi na udiwani, ikiwemo kuwa na mipango na mikakati ya kufikia usawa wa kijinsia;
  3. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kila chama cha siasa kiwe na dawati la jinsia litakalofanyia kazi masuala ya jinsia ndani ya vyama vya siasa;
  4. utaratibu wa kuwa na viti maalum vya Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wanawake uendelee, isipokuwa sheria ziboreshwe kuweka ukomo wa miaka kumi kwa mtu kuwa Mbunge, Mwakilishi au Diwani wa viti maalum vya wanawake. Uwakilishi huu uwe ni njia ya kupata uzoefu na kisha kupisha wanawake wengine wenye nia ya kuongeza ujuzi wa masuala ya siasa na uongozi.
  5. kuwepo na mwongozo wa kisheria wa uteuzi wa wagombea na uchaguzi wa viongozi ndani ya Vyama vya Siasa, ikiwemo wabunge wa viti maalum ili kusaidia uteuzi na uchaguzi huo kuwa wa haki, uwazi na huru;
  6. kila chama cha Siasa kiweke mkakati wa kuongeza idadi ya wanawake wanaogombea katika majimbo na kata za uchaguzi; na
  7. kwa kuwa idadi ya wanawake ni ndogo katika Baraza la Vyama vya Siasa aongezwe mjumbe mmoja mwanamke kutoka kila chama cha siasa kuwa mjumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa; na
  8. Wabunge wa Viti Maalum vya Wanawake waitwe Wabunge wa Taifa na Madiwani, waitwe Madiwani wa Wilaya, kwa sababu wabunge hao wanatokana na kura za nchi nzima na Madiwani wanatokana na kura za Wilaya. Aidha, Sheria ya Mfuko wa Jimbo ifanyiwe marekebisho ili itambue Wabunge wa Taifa kuwa miongoni mwa Wabunge wanaofaidika na fedha za Mfuko huo.

 

12. Kuhusu ushiriki wa Watu Wenye Ulemavu katika Siasa, Demokrasia na Uongozi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. sheria zisizozingatia ujumuishwaji wa Watu Wenye Ulemavu na zile zinazokwamisha ushiriki wao katika siasa, demokrasia na uongozi ndani ya vyama siasa zifanyiwe maboresho;
  2. Vyama vya Siasa viweke mazingira rafiki yatakayowawezesha Watu Wenye Ulemavu kufanya shughuli za kisiasa bila vikwazo;
  3. kila chama cha siasa kianzishe dawati la kushughulikia masuala ya Watu Wenye Ulemavu;
  4. kuwepo na nafasi maalum kwa Watu Wenye Ulemavu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Madiwani. Viti vya uwakilishi wa Watu Wenye Ulemavu Bungeni viwe katika uwiano utakaozingatia jinsi. Sula hili lifanyiwe kazi katika mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ili lifanyike kwa ufanisi. Hata hivyo, kwa kuanzia kila chama cha siasa kitumie utaratibu wa sasa wa viti maalum vya Wanawake kujumuisha Watu Wenye Ulemavu;
  5. Sheria ya Vyama vya Siasa irekebishwe ili:
  1. iweke sharti kwamba chama cha siasa kiwe na nakala ya Katiba na Kanuni zilizo katika maandishi ya breli (nukta nundu). Aidha, katika mkutano mkuu wa chama taifa, awepo mkalimani wa lugha za alama;
  2. katazo la ubaguzi kwa Watu Wenye Ulemavu katika vyama vya siasa lililopo katika kifungu cha 9(1)(c) cha sheria ya vyama vya siasa liwahusu pia viongozi wa vyama vya siasa; na
  3. katiba ya chama cha siasa iwe na ibara inayokitaka chama husika kiwe na programu za kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika michakato ya kisiasa, demokrasia na uongozi ndani na nje ya chama.
  1. zitungwe Kanuni za utekelezaji wa Kifungu cha 6A (2) cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinachoelekeza chama cha siasa kuzingatia suala la ujumuishwaji wa Watu Wenye Ulemavu katika masuala ya vyama vya siasa na demokrasia; na
  2. vyombo vya habari viandae vipindi maalum vya elimu ya uraia vinavyoeleza haki na mahitaji ya Watu Wenye Ulemavu.

13. Kuhusu ushiriki wa vijana katika Siasa, Demokrasia na Uongozi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa, juhudi zinazofanywa na Serikali kuhusu ushiriki wa vijana katika siasa, demokrasia, uongozi, uchumi, ulinzi na usalama wa nchi yetu ziendelee na mikakati mipya ibuniwe ili kuongeza ufanisi na tija.

 

14.  Kuhusu elimu ya uraia

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

  1. Serikali iandae mwongozo wa kitaifa, mpango kazi na mikakati ya utoaji elimu ya uraia, ili utoaji wa elimu hiyo uzingatie vipaumbele vya taifa na kuwa na uelewa wa pamoja wa walengwa;
  2. elimu ya uraia ikiwemo elimu ya mpiga kura ifundishwe katika ngazi zote za mfumo wa elimu kuanzia shule za awali mpaka katika vyuo vya elimu ya juu. Aidha, mtaala wa elimu ujumuishe masuala ya elimu ya uraia;
  3. Serikali na wadau wengine waongeze kiwango cha ufadhili katika kutoa elimu ya uraia ikiwemo elimu ya mpiga kura, ili kukabiliana na upungufu wa rasilimali fedha, watu na vifaa katika kutoa elimu hiyo;
  4. elimu ya mpiga kura itolewe kipindi chote siyo cha uchaguzi pekee, ili kuongeza muda wa kutoa elimu hiyo kuwezesha kuwafikia walengwa wengi zaidi; na
  5. uratibu na ufuatiliaji wa elimu ya uraia unaofanywa na taasisi mbalimbali kwa mujibu wa sheria uendelee, isipokuwa ufanywe katika hali isiyokwamisha juhudi za kuwafikia watanzania wengi kupata elimu hiyo.

 

15. Kuhusu suala la kuzuia na kupambana na Rushwa katika Siasa na Uchaguzi

Kikosi Kazi kinapendekeza kuwa:

      1. suala la rushwa litamkwe katika Katiba, ili wananchi watambue kuwa vitendo vya rushwa havitavumiliwa wala kuonewa muhali. Pendekezo hili lifanyiwe kazi katika mchakato wa kupata Katiba Mpya ili lifanyike kwa ufanisi;
      2. Sheria ya vyama vya Siasa Sura 258 irekebishwe ili:
  1. kuweka sharti kwamba, katiba ya chama cha siasa iwe na adhabu ya kumwondoa katika mchakato wa uchaguzi, mtia nia au mgombea aliyedhaminiwa na chama, endapo atathibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa;
  2. Msajili wa Vyama vya Siasa apewe mamlaka ya kuandaa mwongozo wa kufuatilia mchakato wa uteuzi wa wagombea na uchaguzi wa viongozi, ndani ya Vyama vya Siasa; na
  3. kukitaka kila chama cha siasa kuwa na Kanuni za Maadili, zitakazodhibiti ukiukwaji wa maadili ndani ya chama, ikiwemo mwanachama kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kanuni hizo ziweke utaratibu wa kushughulikia ukiukwaji wa maadili na adhabu, ikiwemo onyo, karipio, faini, kuvuliwa ujumbe wa kikao husika, kutoruhusiwa kugombea uongozi ndani ya miaka kumi tangu alipopatikana na hatia, kusimamishwa au kufukuzwa uanachama.
      1. Sheria ya Gharama za Uchaguzi irekebishwe ili:
  1. kutoa adhabu kwa mgombea atakayeshindwa kufanya marejesho ya gharama za uchaguzi badala ya kukiadhibu chama cha siasa;
  2. vitendo vinavyokatazwa katika sheria hiyo kuwa na sifa ya kuwa kosa la jinai;
  3. nyaraka za uthibitisho wa matumizi ya gharama za uchaguzi zibaki katika chama cha siasa husika badala ya kuwasilishwa kwa Msajili wa vyama vya siasa; na
  4.