Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

UTEUZI KATIKA TUME YA UTUMISHI WA UMMA NA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

 

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe. DKT. STEPHEN JAMES BWANA, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na BWANA EDRISSA R. MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Mavura ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.

 

            Sambamba na uteuzi huu, Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo, ambapo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ni:

 

(i)

Bwana George D. YAMBESI, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.  

(ii)

Alhaj Y. F. MBILA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.

                

(iii)

Bwana Mgeni Mwalimu ALLY, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma iliyomaliza muda wake.

 

(iv)

Bibi Adieu H. NYONDO, Mkurugenzi wa Maadili mstaafu.     

 

(v)

Bibi Salome S. MOLLEL, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu mstaafu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali    

 

(vi)

Bibi Evelyne ITANISA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.

 

Aidha Makamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ni:

 

(i)

Bwana Paul Herbert Kinemela, Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi na Ajira  

(ii)

Bwana Mathias Bazi Kabunduguru, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

                

(iii)

Bwana Njaa Ramadhani Kibwana, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU).

 

(iv)

Bwana Jones Kyaruzi Majura, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Sekta ya Biashara na Viwanda – (TUICO).

 

(v)

Bwana Jaffari Ally Omari, Mwanasheria Kiwanda cha Sukari – TPC, na Kamishna wa Tume iliyomaliza muda wake.

 

(vi)

Bibi Suzane Charles Ndomba, Afisa Sheria wa ATE na Wakili wa Mahakama Kuu.

 

Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2015.