Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Uteuzi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Moses Mpogole Kusiluka (42) kuwa Kamishna Ardhi nchini.

Uteuzi huo ulianza Jumanne ya Desemba 23, mwaka huu, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Kusiluka alikuwa Mkuu wa Idara ya Real Estate Finance and Investment katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar Es Salaam, ambako amekuwa mhadhiri kwa miaka minane iliyopita, tokea 2006.

Dkt. Kusiluka ana Shahada ya Kwanza ya BSC (Land Management and Valuation) kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Shahada ya Uzamili ya MSC (Land Management) kutoka pia Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Shahada ya Uzamivu ya PhD (Real Estate Investment) kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.

 Katika kumteua Dkt. Kusiluka kuwa Kamishna wa Ardhi, Rais Kikwete ana matumaini makubwa kuwa ataleta nguvu mpya na mtazamo mpya katika kushughulikia kero na changamoto mbali mbali za umiliki na uendelezaji wa ardhi nchini.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

29 Desemba,2014