Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Salamu za pongezi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo Mhe. Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu  Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria jana usiku.

Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.

Aidha, Rais Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.

 

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

08 Januari, 2016