Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri


Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi  za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano ya utawala wake

Uteuzi huo ni kamaifuatavyo;

  1. 1.    Profesa Jumanne Maghembe- Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasilina Utalii.

 

  1. 2.    Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua  kuwa Mbunge).

 

  1. 3.    Mhandisic Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

 

  1. 4.    Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni  baada ya kumteua kuwa Mbunge)

 

  1. 5.    Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi

 

  1. 6.    Prof. Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano

 

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Siku kuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

23  Desemba,  2015