Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan azungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu siku 100 tangu kuingia Madarakani tarehe 28 Juni, 2021, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu siku 100 tangu kuingia kwake madarakani Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Juni, 2021 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake aliojiwekea wa kukutana na makundi mbalimbali ili kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya mustakabali wa taifa.