Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemwapisha Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemwapisha Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania.

Sherehe za uapisho zimefanyika leo asubuhi katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai na  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mshimiwa Pandu Ameir Kificho, Mawaziri wakuu wastaafu, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wabunge.

Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameapishwa kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na jinalakekupelekwabungeni ambako wabunge wamelithibitisha kwa asilimia 73.5.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jioni (Novemba 20, 2015) anatarajiwa kuhutubia na kulizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano waTanzaniakatika Ukumbi wa Bunge MjiniDodoma.

 

Gerson Msigwa

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

 IKULU.

20 Novemba, 2015