Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Rais kuzungumza na Wazee wa Dare s Salaam Jumatatu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu, Desemba 22, 2014.

Wakati wa mazungumzo yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita, Novemba 2014.

            Undani zaidi kuhusu mkutano huo kama vile mahali utakapofanyika, saa utakapofanyika na nani wataalikwa utatolewa na mamlaka zinazohusika na maandalizi ya mkutano huo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

19 Desemba, 2014