Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Taarifa kwa vyombo vya habari


Tutaendelea kutumia mashine mpya kukusanya kodi – Rais Kikwete

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Mashine za Electroniki za Ukusanyaji Kodi –EFD ni lazima ziendelee kutumika nchini na ameagiza viongozi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) kukaa chini na wadau na watumiaji wa mashine hizo kuzungumza na kutafuta majawabu yanayolalamikiwa na wadau.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa anajua kuwa yapo maneno mengi kuhusiana na mashine hizo lakini Serikali haitarudi nyuma katika matumizi ya mashine kwa sababu dunia nzima inakwenda huko.

Rais Kikwete ametoa msimamo huo wa Serikali kuhusu EFD asubuhi ya leo, Jumanne, Aprili 22, 2014 wakati alipozunguza kwenye sherehe ya uzinduzi wa Ofisi za TRA mjini Karatu, Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha.

“Najua kuna maneno mengi kuhusu suala hili. Kwa hiyo maelekezo yangu ni kwamba kaeni chini, myajadili matatizo yaliyopo na kupata ufumbuzi. Kama ni suala la bei pia linazungumzika lakini tuhajitaji mfumo huu wa malipo ya kodi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

 

 

“Kwenye hili tusirudi nyuma kwa sababu tukifanya hivyo, tutakuwa

tunarudi nyuma sana kwa sababu dunia nzima inaelekea huko na hata majirani zetu wote ama wameanzisha mfumo huo ama wanajiandaa kuuanzisha.”

Rais Kikwete amesisitiza: “Hatuwezi kurejea kwenye mfumo ule wa kitumia vijirisiti. Mfumo wa sasa unaifanya kazi ya kukusanya kodi kuwa rahisi kwa Serikali yenyewe na kwa walipa kodi. Najua watu hawapendi kulipa kodi lakini hakuna njia ya jinsi ya kuendelea isipokuwa kwa kulipa kodi”.

Rais Kikwete alikuwa katika ziara ya siku moja kukagua shughuli za maendeleo wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha na kesho atafanya ziara kama hiyo ya siku moja katika Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro.    

 

Imetolwa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

22 Aprili,2014