Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Taarifa kwa vyombo vya habari


Kesho Ijumaa 01 Januari, 2016 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wataapishwa rasmi katika Ukumbi wa Ikulu, uliopo lango kuu litazamalo baharini kuanzia saa nne asubuhi.

Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao wataapishwa na wale ambao walishaapishwa wanapaswa kuhudhuria katika tukio hili, ili mara baada ya kiapo kukamilika washiriki zoezi la kutia saini Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma (Integrity Pledge).  

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema zoezi la kutia saini hizo, litafanyika kwa uwazi mbele ya vyombo vya habari.

Aidha, Balozi Sefue amefafanua kuwa hata kama wapo baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu ambao walishasaini Hati hizo, watapaswa kusaini upya mbele ya vyombo vya habari.

Tukio hili pia litarushwa ‘live’ kupitia luninga.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU

31 Desemba, 2015