Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MITAMBO MIPYA YA KISASA YA MATIBABU YA MOYO CATHLAB NA CARTO 3 SYSTEM KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 12 JUNI, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo katika hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.