Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA CHELEZO KATIKA BANDARI YA MWANZA SOUTH MKOANI MWANZA


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan azindua Chelezo katika Bandari ya Mwanza South mkoani Mwanza tarehe 15 Juni, 2021 wakati wa ziara yake ya siku 3 ya kikazi mkoani humo. 

Mhe. Rais amesema kuwa Chelezo hicho kitakapokamilika kujengwa kitagharimu shilingi Bilioni 36.4. Chelezo hicho kwa sasa kinatumika kutengeneza Meli mpya ya Mv. Mwanza pia kitatumika kutengeneza na kukarabati Meli nyingine hapa nchini na hata kutoka nje ya nchi.

Sambamba na hilo, Mhe. Rais Samia pia amezindua Meli mbili za New Butiama (Hapa Kazi Tu) na New Victoria (Hapa Kazi Tu) ambazo zimefanyiwa ukarabati mkubwa na kwa hivi sasa zinatoa huduma kama awali kwa kusafiri kati ya Mwanza na Bukoba na Nansio Ukerewe.

Katika siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Mwanza, Mhe. Rais pia ameshuhudia utiaji saini wa Mikataba mitano ya ujenzi na ukarabati wa Meli ambazo baadhi yake zitatumika kutoa huduma katika Ziwa Tanganyika na bahari ya Hindi, zitakazogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 438.