Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA SADC NCHINI MSUMBIJI TAREHE 23 JUNI, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Joaquim Chissano uliopo Maputo nchini Msumbiji tarehe 23 Juni, 2021. Mhe. Rais Samia aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula.