Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI KATIKA KILELE CHA TAMASHA LA KIZIMKAZI KATIKA KIJIJI CHA KIZIMKAZI KUSINI UNGUJA DAR ES SALAAM TAREHE 28 AGOSTI, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitaka jamii nchini kulinda na kuendeleza mila, tamaduni na desturi zilizo nzuri na kuwarithisha vizazi vya sasa na vijazvyo.

Mhe. Rais Samia amesema hayo tarehe 28 Agosti, 2021 wakati akihutubia kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi katika Kijiji cha Kizimkazi kusini Unguja Zanzibar.

Amesema kwa sasa dunia ipo kwenye zama za utandawazi hivyo mikakati thabiti inahitajika kuhakikisha jamii inalinda mila, tamaduni na desturi zilizo nzuri ili zisipotee na kuachana na zile mbaya kama ndoa za utotoni na ukeketaji.

Pamoja na mambo mengine, Tamasha la Kizimkazi linahamasisha miradi ya maendeleo kufanyika ikiwemo ujenzi na ukarabati wa shule za awali, Msingi na Sekondari, nyumba za walimu pamoja na nyumba za watumishi wa afya pamoja na kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo kwenye eneo hilo hususan kilimo, utalii, uchumi wa bahari ama uchumi wa buluu na utalii wa pomboo (Dolphin) ambao hupatikana katika eneo hilo la Kizimkazi.

Vilevile, Mhe. Rais Samia amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2022, kwa kuwa Sensa ni muhimu katika kuwezesha Serikali kufahamu idadi ya watu itakayosadia kupanga mipango ya maendeleo.

Sambamba na hilo,  pia amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO 19 na kujitokeza kupata chanjo katika kukabiliana na maradhi hayo.