Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, APOKEA TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM KUTOKA KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) BW. CHARLES KICHERE JIJINI DODOMA LEO TAREHE 01 JULAI, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amepokea Taarifa ya Ukaguzi Maalum inayohusu matumizi ya Fedha zilizotolewa Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  kati ya mwezi Januari na Machi mwaka 2021, kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Charles Kichere leo tarehe 01 Julai, 2021 Jijini Dodoma.

Aidha, Taarifa hiyo inatokana na agizo alilolitoa Mhe. Rais Samia tarehe 28 Machi 2021, wakati akipokea Taarifa ya CAG kwa mwaka 2019/ 2020.

Katika taarifa ya ukaguzi maalum, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Charles Kichere amesema katika ukaguzi uliofanyika imebainika kuwa fedha  zilizotolewa BOT katika kipindi hicho zilifuata taratibu zote, isipokuwa baadhi ya malipo yaliyokuwa yanatoka Hazina Kuu kwenda katika Taasisi mbalimbali za Serikali yalibainika kuwa na mapungufu ikiwemo baadhi ya taasisi kama vile Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kufanya malipo mara mbili kwa kazi moja au kuchelewa kutumia fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya malipo ya kazi husika.