Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, APOKEA TAARIFA YA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI INAYOTARAJIWA KUFANYIKA AGOSTI 2022 LEO TAREHE 01 JULAI 2021 JIJINI DODOMA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amepokea Taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi, inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2022, kutoka kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa, leo tarehe 01 Julai, 2021 Jijini Dodoma.

Dkt. Chuwa amesema Sensa ya mwaka 2022 itatumia teknolojia ya kisasa ya Kidijitali chini ya mfumo uliopo wa Serikali katika ngazi zote za Utawala kwa pande zote za Muungano.

Aidha, amesema Sensa ya majaribio itafanyika mwezi Agosti mwaka huu (2021)  katika mikoa saba kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.