Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMFUNGUA KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA MAISHA YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 07 NOVEMBA, 2021 ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua Kongamano la Kumbukizi ya Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamadi, tarehe 05 Novemba, 2021 na kuwataka Wazanzibari kumuenzi Hayati Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuendeleza mshikamano na umoja wa Kitaifa ili Zanzibar izidi kupata maendeleo makubwa.

Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Mjini Unguja ambapo Mhe Rais. Samia amemtaja Mhe. Maalim Seif kuwa alikuwa daraja la amani na mtu aliyeongozwa na maono ya maslahi mapana ya taifa hivyo hatuwezi kuizungumzia amani ya Zanzibar na Tanzania bila kumtaja Maalim Seif.

Pia Mhe Rais. Samia amebainisha kuwa hata pale wafuasi wake walipokuwa na msimamo tofauti, daima alikuwa na ushupavu katika uongozi na uwezo wa kushawishi kukubalika kwa jambo analoliamini hali iliyopelekea kupunguza jazba ya wafuasi wake.

Mhe Rais. Samia amemuelezea Hayati Maalim Seif kuwa alikuwa kiongozi jasiri aliyekuwa na uwezo wa kwenda kinyume na mawazo ya wafuasi wake hali inayotoa funzo kwa wanasiasa wengine kusimamia wanachokiamini lakini kuweka mbele maslahi ya taifa.