Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA TAREHE 25 JUNI, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,  tarehe 25 Juni, 2021 amezungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu  Katoliki Tanzania na kueleza kuwa Taaisisi za Dini nchini ni muhimu kwa kuwa zina mchango mkubwa katika kudumisha amani, kustawisha maisha ya wananchi  na kupambana na umasikini. Mhe. Rais Samia amewasihi Watanzania kuendelea kuvumiliana kwenye tofauti za kidini zinazojitokeza ili kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewaomba Maaskofu na viongozi wengine wa Dini kuwakumbusha waumini wao kuhusu umuhimu wa kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa mipango ya Serikali ya miaka mitano kuwa ni pamoja na kudumisha mema yote ya Awamu zilizotangulia na kubuni mengine mapya. Amesema Serikali imejipanga kuendeleza kukuza uchumi ili kupambana na umasikini na tatizo la ajira kwa kuboresha mazingira ya biashara.