Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) Abebe Aemro Selassie Ikulu Jijini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 29 Juni, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bw.Abebe Aemro Selassie kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi Shirika hilo litakavyosaidia Tanzania kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu, Jijini Dodoma.

 

Katika mazungumzo yao, Bw. Selassie ametoa salamu kutoka kwa Mkurugenzi wa IMF Bi. Kristalina Georgieva ambaye amemuhakikishia Mhe. Rais Samia kuwa IMF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufikia maendeleo yanayokusudiwa.

Akizungumzia kuhusu kukabiliana na ugonjwa Corona  (Covid 19), Bw. Selassie amesema IMF ipo tayari kuendelea kufanya kazi na Wataalam wa Tanzania kuandaa andiko litakalowezesha kupata msaada wa fedha kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na Uviko.