Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA JPM (KIGONGO - BUSISI) MKOANI MWANZA TAREHE 14 JUNI, 2021


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan atembelea na kukagua Daraja la JP Magufuli lenye Urefu wa Km 3.2 (Kigongo -Busisi) mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo tangu tarehe 13-15 Juni, 2021.

Akizungumza na wananchi mara baada ya ukaguzi wa daraja la JPM linalojengwa katika eneo la Kigongo–Busisi, Mhe.Rais Samia amesema ujenzi wa daraja hilo ni sehemu ya mipango ya Serikali ya kulifanya Jiji la Mwanza kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za Maziwa Makuu.

 

Mhe. Rais Samia amesema daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3.2 ambalo litagharimu shilingi Bilioni 716 litakapokamilika litafungua fursa zaidi za  kiuchumi kwa kuwawezesha wananchi hususani wafanyabiashara kuvuka kwa muda mfupi tofauti na ilivyo sasa ambapo hutumia muda mwingi kusubiri kivuko kwa ajili ya kuvusha bidhaa zao.