Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI NCHINI RWANDA KUANZIA TAREHE 02-03 AGOSTI, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya siku mbili nchini Rwanda kuanzia tarehe 02-03 Agosti, 2021. Katika ziara hiyo Mhe. rais Samia alipokelewa na mwenyeji wake Mhe. Rais Paul Kagame katika Ikulu ya Kigali nchini humo na kufanya mazungumzo na baadae Rais Samia alizungumza na vyombo vya habari. Aidha, Marais hao wawili walishuhudia utiaji saini wa hati nne (4) za makubaliano ambazo zinahusu ushirikiano katika masuala ya Uhamiaji, Elimu, Teknolojia ya Habari na Mawasilinao, na  Sheria ya Bidhaa za Dawa. 

Katika siku ya kwanza ya ziara yake Mhe. Rais Samia pia alitembelea Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo alisaini kitabu cha kumbukumbu na kuweka shada la maua katika kaburi lililopo katika makumbusho hayo na baadae usiku kisha kuhudhuria dhifa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. rais Paul Kagame.

Tarehe 03 Agosti, 2021 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alihitimisha ziara yake kwa kutembelea eneo la uwekezaji nchini humo ambapo alizuru Kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini Kigali kinachozalisha Juisi, Maziwa na Maji ya kunywa; Kiwanda cha kutengeneza magari cha CFAO motors kinachozalisha magari aina ya Volkswagen pamoja na kiwanda cha kutengeneza simu cha Mara Phones. 

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliagana na mwenyeji wake Mhe. Rais Paul Kagame Katika Uwanja wa Ndege wa Kigali na Kisha kurejea Jijini Dar es Salaam, Tanzania.