Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU MBILI NCHINI BURUNDI KUANZIA TAREHE 16-17 JULAI, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameanza rasmi ziara ya Kitaifa ya siku mbili Nchini Burundi kwa mwaliko wa Rais Mhe. Evariste Ndayishimiye.

Mhe. rais Samia aliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mechior Ndadaye Jijini Bujumbura na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Prosper Bazombanza.

Rais Samia amefanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Rais Evariste Ndayishimiye yaliyolenga kukuza zaidi uhusiano kati ya mataifa haya mawili hususan katika kukuza biashara na uwekezaji.

Katika siku ya kwanza ya ziara yake, Mhe. Rais Samia ametembelea Benki ya CRDB iliyopo Jijini Bunjumbura na kuzungumza na wafanyakazi wa benki hiyo ambapo amewataka kuendelea kuchapa kazi zaidi mbali na mafanikio wanayoyapata.

Pia Mhe. Rais ametembelea kiwanda cha kuzalisha Mbolea Asili cha Fertilizer Organo Mineral Industries (FOMI),  na kumshukuru Mhe. Rais Ndayishimiye kwa mapokezi makubwa tangu alipoingia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mechior Ndadaye na katika maeneo mbalimbali aliyotembelea.

Mhe. Rais Samia ameendelea na ziara yake nchini Burundi ambapo tarehe 17 Julai, 2021  amezungumza na Jukwaa la Wafanyabiashara wa Burundi na Tanzania pamoja na kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Burundi