Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI MKOANI MOROGORO KUANZIA TAREHE 07-08 JULAI, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya siku mbili mkoani Morogoro kuanzia tarehe 07-08 Julai, 2021.  Akiwa njiani kuelekea Morogoro Mhe. rais alisimama na kuwasilimia wananchi wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. 

Aidha, baada ya kuwasili Mkoani Morogoro, Mhe. Rais alisimama na kuwasalimia wananchi wa Mkoa wa Morogoro katika eneo la Msamvu mkoani humo. 

Akiwa Mkaoni humo tarehe 08 Julai, 2021, Mhe. rais Samia Suluhu Hassan alishiriki Mkutano Mkuu wa jumuiya ya Kikristo (CCT). katika Mkutano huo, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba viongozi wa dini kuwahimiza wanaanchi kuheshimu sheria za nchi na kuwaomba kuwakemea watu wanaovunja sheria kwa makusudi na kuhatarisha amani ya nchi.

Mhe. Rais Samia amerejea Jijini Dodoma tarehe 08 Julai, 2021 ambapo alisimama eneo la Dumila na Kongwa na kusalimiana na wananchiwa maeneo hayo wakati akiwa njiani kurejea Dodoma.