Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA WILMAR INTERNATIONAL YA SINGAPORE KUOK KHOON HONG, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 18 JUNI, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Juni, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa kampuni ya Wilmar International ya Singapore Bw. Kuok Khoon Hong, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Bw. Hong ameahidi kuwa kampuni hiyo ipo tayari kupanua uwekezaji wake katika uzalishaji wa mchele na mafuta kwa kuwa mchele wa Tanzania ni bora na wenye soko kubwa duniani na mahitaji ya mafuta ni makubwa ndani ya nchi.

Amesema kampuni hiyo imefurahishwa na dhamira ya Mhe. Rais Samia ya kuwavutia zaidi wawekezaji na kwamba tayari imeshawekeza hapa nchini kiasi cha Dola za Marekani Milioni Mia Moja na Hamsini (150,000,000) katika kiwanda cha kusafisha mafuta ya kula, kutengeneza sabuni na tambi ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa takribani Dola za Marekani Bilioni 1 Barani Afrika.