Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AELEKEZA KUPUNGUZWA KWA TOZO KWENYE MAFUTA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kupunguzwa kwa tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali katika bidhaa za mafuta  hapa nchini zenye thamani ya shilingi Bilioni 102 kwa mwaka, kwa lengo la kupunguza bei za mafuta ili kuwapa unafuu wananchi.

Mhe. Rais Samia ametoa maagizo hayo  wakati akipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Nishati, Mhe. January Y. Makamba kuhusu utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Wizara hiyo kupitia mwenendo wa biashara ya mafuta na bei zake hapa nchini tarehe 05 Oktoba, 202, Chamwino, Mkoani Dodoma.

Utekelezaji wa maagizo hayo umeenda sambamba na marekebisho ya Kanuni mbalimbali zinazohusiana na tozo na yatachapishwa katika Gazeti la Serikali tarehe 05 Oktoba, 2021.

Mhe. Rais  Samia amechukua hatua hiyo ili kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika soko la dunia ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikipanda kwa kiwango kikubwa na kuathiri watumiaji wa bidhaa hiyo hapa nchini.