Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VIJANA WA MKOA WA MWANZA KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA NYAMAGANA MKOANI MWANZA TAREHE 15 JUNI, 2021


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na Vijana wa Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya vijana wote nchini ikiwa katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza tarehe 15 Juni, 2021. 

Mhe. Rais Samia amezungumza na vijana hao ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu mkoani Mwanza kuanzia tarehe 13-15 Juni, 2021 ambapo 

amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali.

Mhe. Rais Samia ametaja baadhi ya miradi hiyo ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kuwa ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Magufuli (JPM Bridge) katika eneo la Kigongo – Busisi, ujenzi wa Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere katika mto Rufiji, Reli ya kisasa yaani SGR na  ujenzi na ukarabati wa Viwanja vya ndege.

Mhe. Rais amesema mbali na fursa hizo za miradi ya kimkakati pia vijana hawana budi kutumia fursa zilizopo kwenye kilimo na mifugo ambapo Tanzania ni ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Barani Afrika.

Kwa upande mwingine, Mhe. Rais Samia amewataka vijana wafanyabiasgara ndogo ndogo (wamachinga) kutokutumika na wafanyabiashara wakubwa ambao wanakwepa kulipa kodi.