Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MISUNGWI MKOANI MWANZA


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan azindua Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Misungwi mkoani Mwanza tarehe 14 Juni, 2021.  Akihutubia wananchi wa Misungwi wakati wa uzinduzi, Mhe. Rais amesema mradi huo unaohusisha miji ya Magu na Lamadi na uliogharimu shilingi bilioni 45. 57 utawahudumia wananchi zaidi ya 64,000.

Aidha, Mhe. Rais Samia ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha miradi yote ya maji inatekelezwa kwa wakati ili kufikia lengo la Serikali la kuwaondolea wananchi adha ya upatikanaji wa maji.