Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Habari

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASASAN AZUNGUMZA KWA NJIA YA SIMU NA RAIS WA CHINA XI JINPING TAREHE 21 JUNI, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping tarehe 21 Juni, 2021.

Katika mazungumnzo hayo Tanzania na China zimekubaliana kukuza ushirikiano katika nyanja za uchumi, utamaduni na ushirikiano wa Kimataifa ambapo China imeahidi kufungua zaidi soko lake kwa bidhaa za Tanzania pamoja na kuongeza uwekezaji hususan katika sekta ya viwanda.

Aidha, kupitia mazungumzo hayo, China imeahidi kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali.