Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Wasifu

Mr. ALI HASSAN MWINYI
Mr. ALI HASSAN MWINYI
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili

Mheshimiwa Alhaj  Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza Serekali ya Awamu ya Pili aliingia madarakani rasmi tarehe 5 Novemba 1985. Mheshimiwa Alhaj Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Kivule, Mkuranga,  mkoa wa Pwani  tarehe 5 mei, 1925. 

 

Kazi

Alikuwa mwalimu wa shule za msingi za Mangapwani na Bumbwini, Zanzibar.Kisiasa, mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alijiunga na chama cha Afro Shiraz(ASP) mwaka 1964 na kushika nyadhifa mbali mbali za serekali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile katibu mkuu, Wizara ya Elimu Zanzibar 1963, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970 na kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Afya, Wizara ya Mambo ya Ndani, Maliasili na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Misri. Mwaka 1984 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 

Elimu

Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi pia ana cheti cha umahiri wa lugha ya kiingereza, alichohitimu katika taasisi ya Regent, Uingereza mwaka 1960 na cheti cha umahiri wa lugha ya kiarabu alichohitimu, Cairo, Misri, mwaka 1972-74.