Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Wasifu

Mhe. Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
Mhe. Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
Rais wa Awamu ya Tano

Hayati Dkt. John P. Magufuli alizaliwa  Oktoba 29, 1959 Wilayani Chato Mkoa wa Kagera ambayo hivi sasa ipo Mkoa wa Geita. Dkt. Magufuli amemuoa Mwalimu Janet na wamejaliwa kupata watoto.

 

kazi

Harakati zake za kisiasa zilianza mwaka 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi. Mwaka 2000 Dkt. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.

Aidha, katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010. Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

 

Elimu

Dkt. Magufuli pia alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria akianzia Makutupora, Dodoma (Julai - Desemba 1983), kisha akaenda kambi ya Makuyuni, Arusha (Januari hadi Machi 1984) na akamalizia katika kambi ya Mpwapwa mkoani Dodoma (Machi – Juni 1984). Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988.

Kati ya mwaka 1991 na 1994 alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza na baadaye mwaka 2006-2009 alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamivu ya Kemia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kutokana na taaluma yake  Dkt. Magufuli ameandika vitabu na machapisho mbalimbali.

 

Nyadhifa nyengine

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa