Wasifu
Mr. BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Rais Mstaafu wa Awamu ya TatuHayati Benjamin William Mkapa aliongoza awamu ya tatu na ni Rais wa kwanza aliyechaguliwa katika uchaguzi ulioshirikisha vyama vingi vya siasa tangu mfumo huo uliporejeshwa mwaka 1992. Aliingia rasmi madarakani Oktoba 1995. Mheshimiwa Mkapa alizaliwa Masasi, Mkoani Mtwara tarehe 12 Novemba, 1938.
Kazi
Mwaka 1962 aliajiriwa kama Ofisa Tawala na hatimaye Ofisa Mambo ya Nje. Kati ya mwaka 1966 na 1976 alifanya kazi katika Taasisi mbalimbali za umma. Mwaka 1976 hadi mwaka Septemba, 1995 alishika nyadhifa zifuatazo: Balozi wa Tanzania nchini Nigeria (1976; Mbunge wa Nanyumbu na Waziri wa Mambo ya Nje (1977 – 1980); Waziri wa Habari na Utamaduni (1980 – 1982); Balozi wa Tanzania nchini Canada (1984 – 1990); Waziri wa Habari na Utangazaji (1990); Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu (1992 – Septemba 1995).
Elimu
Alipata elimu ya msingi na sekondari kati ya mwaka 1945 – 1956 katika shule za Lupaso, Ndanda, Kigonsera na Pugu.
Alipata shahada ya kwanza ya Lugha ya Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda mwaka 1962, na shahada ya Uzamili ya Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Columbia, Marekani mwaka 1963
Nyadhifa nyengine
April 1962: Aliteuliwa Afisa Tawala Dodoma
April 1962: Afisa wa Wilaya
August 1962: Afisa Mambo ya Nje
May 1966:Mhariri Mtendaji, The Nationalist na Uhuru
April 1972: Mhariri Mtendaji, The Daily News
July 1974: Afisa Habari wa Rais
July 1976: Mhariri Mwanzilishi, Shirika la Habari Tanzania
October 1976: Balozi Nigeria
February 1977: Waziri wa Mambo ya Nje
November 1980: Waziri wa Habari na Utamaduni
April 1982: Balozi India
February 1983: Balozi Marekani
AprilL 1984: Waziri wa Mambo ya Nje
1990: Waziri wa Habari na Utangazaji
May 1992: Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu
November 1995: Alichaguliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania