Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

Kuhusu Marais wa zamani wa Tanzania
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka 2011-12-30 hadi 2015-11-05

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa tarehe 7 Oktoba mwaka 1950 Msoga, mkoa wa Pwani, mtoto wa sita katika familia ya watoto tisa. Amemuoa mama Salma Kikwete na wamebarikiwa watoto nane.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka 1995-11-23 hadi 2005-12-21

Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa aliongoza awamu ya tatu na ni Rais wa kwanza aliyechaguliwa katika uchaguzi ulioshirikisha vyama  vingi vya siasa tangu mfumo huo uliporejeshwa mwaka 1992. Aliingia rasmi madarakani Oktoba 1995. Mheshimiwa Mkapa alizaliwa Masasi, Mkoani Mtwara tarehe 12 Novemba, 1938. 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka 1985-11-05 hadi 1995-11-23

Mheshimiwa Alhaj  Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza serekali ya awamu ya pili aliingia madarakani rasmi tarehe 5 Novemba 1985. Mheshimiwa Alhaj Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Kivule, Mkuranga,  mkoa wa Pwani  tarehe 5 mei, 1925. 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka 1964-10-29 hadi 1985-11-05

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alizaliwa tarehe 13 Aprili, mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma katika Mkoa wa Mara. Alikuwa mtoto wa Chifu Nyerere Burito na Bibi Christina Mugaya Wanyang’ombe. 

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wa awamu ya kwanza walielekeza juhudi zao katika kuwaunganisha Watanzania na kuweka misingi imara ya kuijenga taifa; kudumisha uhuru na amani na kuweka itikadi na sera za kukabili ujinga, umaskini na maradhi. Aidha, awamu hii iliweka