TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi 3 kama ifuatavyo;
Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Dkt. Shein anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas A. Samatta ambaye anamaliza muda wake.
Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Dkt. Mwakyembe anachukua nafasi ya Bi. Mariam Joy Mwaffisi ambaye amemaliza muda wake.
Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudentia Mugosi Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Bi. Gaudensia Mugosi Kabaka anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 24 Novemba, 2020.
Hatimiliki ©2015 Ikulu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha | Kanusho|
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Inaendeshwa na Ofisi ya Rais Ikulu