Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

taarifa kwa vyombo vya habari
taarifa kwa vyombo vya habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 22 Desemba, 2019 ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Chato Mkoani Geita kusali Dominika ya 4 ya Majilio na ametumia nafasi hiyo kuwatakia heri ya Krismasi na Mwaka Mpya Watanzania wote.

Katika salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli amesema tunapoelekea katika sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya Wakristo na Waumini wa madhehebu mengine mbalimbali wanalo jukumu la kuendelea kuombea amani, upendo na umoja kwa wanadamu wote bila kubaguana.

“Niwaombe ndugu zangu wa Chato na Watanzania kwa ujumla, tusherehekee sikukuu ya Krismasi kwa amani na upendo mkubwa, lakini pia tuukaribishe Mwaka Mpya kwa amani na upendo mkubwa wa Kristo, mwaka unaokuja uwe mwaka wa mafanikio, uwe mwaka wa maendeleo, uwe mwaka wa kujenga umoja wetu kwa Watanzania wote, uwe mwaka wa amani na upendo na uwe mwaka wa kuendeleza Taifa letu katika maendeleo ya kweli” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Waumini wa Parokia ya Bikira Maria Chato kwa kazi kubwa ya upanuzi wa Kanisa wanayoendelea nayo ambayo naye alichangia upanuzi wake mwaka 2016.

Misa Takatifu hiyo imeongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Henry Mulinganisa.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato

22 Desemba 2019