Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

Taarifa kwa vyombo vya Habari
Taarifa kwa vyombo vya Habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 03 Novemba, 2019 amemuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kufanya mabadiliko kwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, zilizopo katika Mkoa wa Morogoro kama ifuatavyo;

  1. Halmashauri ya Mji wa Ifakara iongezwe idadi ya Kata, kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

 

Makao Makuu yawe Ifakara Mjini.

 

  1.  Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ibadilishwe jina, na iitwe Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba.

 

Makao Makuu yawe Mngeta kama ilivyoamuliwa na Baraza la Madiwani.

Mhe. Rais Magufuli amewasisitiza viongozi wa halmashauri kutowayumbisha wananchi na watumishi kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo.

Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mhe. Waziri Jafo kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo kwa mujibu wa sheria

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

03 Novemba, 2019