Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

Taarifa kwa vyombo vya Habari
Taarifa kwa vyombo vya Habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Januari, 2019 amefanya uteuzi wa Majaji 6 wa Mahakama ya Rufani, Majaji 15 wa Mahakama Kuu, Wakuu wa Wilaya 2 na Wakurugenzi 10 wa Halmashauri za Wilaya hapa nchini.

Uteuzi wa viongozi hao umetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni;

 1. Mhe. Jaji Sahel Barke
 2. Mhe. Jaji Dkt. Mary Levira
 3. Mhe. Jaji Rehema Kerefu Sameji
 4. Mhe. Jaji Winnie Korosso
 5. Mhe. Jaji Ignus Kitusi
 6. Mhe. Jaji Lugano Samson Mwandambo

Walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ni;

 1. Cyprian Phocas Mkeha
 2. Dunstan Beda Ndunguru
 3. Seif Mwinshehe Kulita
 4. Dkt. Ntemi Nimilwa Kilikamajenga
 5. Zepherine Nyalugenda Galeba
 6. Dkt. Juliana Laurent Masabo
 7. Mustapha Kambona Ismail
 8. Upendo Elly Madeha
 9. Willbard Richard Mashauri
 10.  Yohane Bokobora Masara
 11.  Dkt. Lilian Mihayo Mongella
 12.  Fahamu H. Mtulya
 13.  John Rugalema Kahyoza
 14.  Athumani Matuma Kirati
 15.  Susan Bernard Mkapa

Wakuu wa Wilaya.

 1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Charles Francis Kabeho kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime.

Bw. Kabeho anachukua nafasi ya Bw. Glorious Luoga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

 1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Thomas Cornel Apson kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga.

Bw. Apson anachukua nafasi ya Bw. Aaron Mbogho ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya walioteuliwa kujaza nafasi zilizokuwa wazi ni.

 1. Isaya M. Mbenje - Pangani
 2. Dkt. Fatuma Ramadhani Mganga - Bahi
 3. Regina Bieda – Tunduma
 4. Jonas Emmanuel Mallosa – Ulanga
 5. Ally Juma Ally – Njombe
 6. Misana Kalela Kwangura - Nkasi
 7. Diodes M. Rutema – Kibondo
 8. Netho Ndilito - Mufindi
 9. Elizabeth Mathias Gumbo – Itilima
 10.  Stephen Mhoja Mashauri Ndaki – Kishapu

Uteuzi wa viongozi hawa unaanza leo tarehe 27 Januari, 2019.

Majaji Wateule wa Mahakama ya Rufani na Majaji Wateule wa Mahakama Kuu wataapishwa Jumanne tarehe 29 Januari, 2019 kuanzia saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Wakuu wa Wilaya 2 na Wakurugenzi 10 wa Halmashauri za Wilaya walioteuliwa leo, wanatakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Januari, 2019 saa 3:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maelekezo ya kikazi na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

27 Januari, 2019