Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

Taarifa kwa vyombo vya habari
Taarifa kwa vyombo vya habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11 Julai, 2018 ameagana na Mabalozi watatu waliomaliza muda wa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania.

Mabalozi walioagana na Mhe. Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Mhe. Hawa Olga Ndilowe – Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Katarina Rangnitt – Balozi wa Sweden nchini Tanzania na Mhe. Hanne-Marie Kaarstad – Balozi wa Norway nchini Tanzania.

Mabalozi hao wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Serikali anayoiongoza kwa ushirikiano mzuri walioupata kwa muda wote ambao walikuwa wakiziwakilisha nchi zao hapa nchini na wameeleza kuwa katika kipindi hicho ushirikiano wa nchi zao na Tanzania umekua na kuimarika zaidi.

Wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa, kusimamia rasilimali za Taifa, kutekeleza miradi mikubwa ya kukuza uchumi na kuvutia uwekezaji kupitia kupitia mwongozo wa uwekezaji (Blue Print) ambao umelenga kuondoa kero zinazowakabili wawekezaji.

Mabalozi hao wamemuahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuinadi Tanzania katika nchi zao ili kukuza uwekezaji, biashara, utalii na ushirikiano utakaokuwa chachu ya manufaa kwa Tanzania nan chi hizo.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Mabalozi hao kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kipindi walichoziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewaomba kufikisha salamu zake kwa viongozi wakuu katika nchi zao na kuwakaribisha kuitembelea Tanzania.

Mhe. Rais Magufuli amesema anatambua mchango mkubwa ambao nchi hizo zinautoa kwa maendeleo ya Tanzania, na amewasihi wawaeleze Mabalozi watakaokuja kuchukua nafasi zao kuendeleza ushirikiano huu mzuri uliopo kati ya nchi hizo na Tanzania na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha uhusiano huo unakuzwa kwa kujikita zaidi katika diplomasia ya uchumi.

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

11 Julai, 2018