Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

taarifa kwa vyombo vya habari
taarifa kwa vyombo vya habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanzia tarehe 17 Aprili, 2018.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mhe. Rais Magufuli amewateua Makamishna wa Tume ya Madini kama ifuatavyo:

  1. Bw. Doto James – Katibu Mkuu, Fedha na Mipango.
  2. Bi. Dorothy Mwanyika – Katibu Mkuu, Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
  3. Dkt. Florens Turuka – Katibu Mkuu, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  4. Mhandisi Musa Iyombe – Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  5. Bw. Haroun Athuman Kinega – Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini (FEMATA).
  6. Dkt. Evaristo Emmanuel Longopa – Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  7. Prof. Abdulkarim Hamis Mruma – Mkurugenzi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafutaji Madini Tanzania (GST).
  8. Dkt. Athanas Simon Macheyeki – Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Uteuzi wa Balozi Mstaafu Njoolay umeanza tarehe 17 Aprili, 2018.

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

18 Aprili, 2018